SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA: 22

Baada ya kuwachamba wifi yangu na mmewe mawasiliano nao yakaishia hapo tutakawa hatuongei wala hatusalimiani,,,bahati mbaya mjomba alianza kuugua kansa ya koo,,mjomba ake na francy,,aliugua sana karibia mwaka mmoja ikafika hatua akawa anapigwa mionzi,akawa anakula kwa kutumia mirija,,wanasaga chakula chake kisha wanamlisha kwa kutumia sindano maalum...hapo shangazi sina mawasiliano nae vizuri ila nilikua nampigia mara mojamoja,, siku hiyo nikamwambia francy nataka kwenda kumuona mjomba hospitali,,alikua amelazwa muhimbili,,,akanipa nauli 4000 nikawaza hii hela ntaifanjaje maana siwezi kwenda mikono mitupu na hapo sikua na hela nyingine maana nilivyorudi nilikuta duka limemshinda vitu vimeisha dukani na hela ya kununulia hamna hivyo kukawa na magepu dukani kiufupi palifirisika na kazi alikua hataki nitafute yaani hakutaka niajiriwe,,,basi nikasema ngoja nikanunue matunda wanaweza hata kusaga juice akanywa, maana aliwekwa chumba cha private cha peke yake na shangazi ndo alikua anamuuguza,,,nilienda huku nikijishtukia maana sikua na kitu cha maana ila nikasema ni bora kwenda kuliko kutokwenda kabisaa,,,,nikafika hadi wodini nilikuta watu kama woote kiufupi walikua wengi,, nikamsalimia shangazi kisha nikawanaenda kuweka matunda kwenya meza shangazi akaniwahi juu yuu nini hiyo unaweka nikamwambia matunda akaniambia yatoe hapo yatoe haraka hatumii hayoo,,,nilijisikia vibaya jamaniii watu wote waliniangalia mimi nikatoka nayo nnje nikakaa kwenya bench nikasema hivi hawa watu wananichukuliaje kwani,,,hata kama mgonjwa hali lakini muuguzi si anaweza kula maana alikua anashinda huko sila siku na mgonjwa alikua haruhusiwi kunywa vitu vyakusindika na chakula chake kinapikwa special lazima ujue kukupika na niliogopa pia kupika maana shangazi anamdomo nisije kupika tofauti ikawa shida...nilikaa sana nnje kisha nikaona acha tu niondoke,nikatoka nikaenda kumuaga kua naenda hakunijibu mi nikaondoka zangu sikutaka kuendelea kukaa sehem ambayo sihitajiki,,,
   Nilipofika nyumbani nikamuadithia francy kila kitu akajibu achana nae,,akili ikaniijia hapa lazima nitafute kazi ya kufanya maana la sivyo mambo yatazidi kua machungu,, kweli nilihangaika sana kutafuta kazi na mungu akasaidia nikaipata,, ilikua kazi nzuri sana ni shirika binafsi lilikua chini ya wazungu kutoka brazil,,,walikua wanasaidia watu wasiojiweza ila kwa makundi yaani lazima wawe kwenye kikundi,hivyo kazi yetu kubwa ilikua kutembelea hivyo vikundi na kuwasilikiza matatizo yao na kujua msaada wanaoutaka alafu tulikua tunawapa semina ya biashara na kisha tunawafungulia biashara waliokua wanahitaji, ila tulikua hatuwapi hela bali tunawapa vifaa vyote vinavyohitajika na bidhaa za kuanzia kulingana na aina ya kitu wanachotaka kufanya,,,ilikua ni kazi nzuri maana kila tukienda kutoa semina ukirudi ulaipwa posho ya siku nzima,,,nikamtaarifu francy kua nimepata kazi,,,yaani baada ya kufurahi ndo kwanza akaniambia ukitoa mguu wako hapa kwenda kwenye hiyo kazi usirudi hapa tena,,nikaona huyu ananichezea nikawa napambana naenda kazini hivyo hivyo,,hapo naenda kwa kulazimisha sana si kwa kukubariwa,,akaona simsikilizi kazini naenda akaamua kwenda kuniharibia offisin na kama mnavyojua wazungu hawapendagi drama kwenye kazi nikasimamishwa kazi hapo ndo alinivuruga kupitiliza nikasema sasa hapa nimefikia mwisho huyu si wakuvumilia na wala hawezi kubadirika ,,nikampigia simu mama nikamueleza kila kitu akaniambia maamuzi unayo wewe maana ndo unaishi naye nikasema asante nikakata simu...baada ya kuniharibia kazi nilikaa kama mwezi nipo tu nyumbani ila niliona ni ujinga nikaamua kwenda offisini nikamkuta boss wangu nikaongea nae kiutu uzima nikaomba sana msamaha na kuomba kurudishwa kazini,,mungu bado alikua upande wangu nikakubariwa na nikapangiwa kwenda zanziba kuna tawi lao wamefungua halina msimamizi na hapo nilimwambia boss kua nimeachana na mmewangu ili wasiweke kikwazo maana mwanzo aliniambia nikamalizane na mme wangu kwanza ili aniruhusu,lakini nilivyomwambia kua tumeachana ndo akanipanga kwenda zanzibar...nilimshukuru sana boss wangu na niliambiwa kesho yake natakiwa kureport,,,nilirudi nikiwa na furaha sana na nikasema leo ndo mwisho wa mateso yangu yoote...nilipofika nyumbani nikapika chakula kizuri nikawa namsubiri kitunguu maji kirudi nikiwashie moto,,,usiku alivyorudi nikapakua chakula tukala hapo nimechangamka hatari hadi akawa anashangaa akaniuliza kuna nini leo mbona umechangamka hivyo?nikamwambia kuna kitu kizuri nataka kukwambia akaniambia okay niambie basi maana so kwa furaha hiyo uliyokua nayo,,,nikamwaambia ukimaliza kula ntakwambia akasema sawa...tulivyomaliza kula nikaenda kuoga nikapanda kitandani nae akafanya hivyohivyo kisha nikamwambia,,,francy asante sana kwa maisha tuliyoishi,,asante kwa kunipenda tangu siku ya kwanza na kuniomba niishi nawe, asante kwa kunipa heshima kwetu maana ulikua mwanaume wa kwanza kwenda kujitambulisha......
ITAENDELEA..... 

Post a Comment

Previous Post Next Post