SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA: 21

Presha ilianza kushuka ghafla nikaanza kujisikia vibaya shangazi alivyoona hivyo walinyanyuka wakaondoka wakaniacha nahangaika naona kabisa pumzi inakata sijui nini kiliendelea nilikuja kushtuka nipo hospitali na francy yuko pembeni,,,nikamuuliza imekuaje niko hapa,,akaniambia ulipoteza fahamu nilivyorudi nilikukuta haujitambui,,,nikakumbua mara ya mwisho nilikua na shangazi nikamuuliza ulionana na shangazi akasema acha kuongelea habari za shangazi usinikwaze sasa hivi,,mmh nikakaa kimya sikuendelea,,,nilipata nafuu nikaruhusiwa tukarudi nyumbani,,usiku tukiwa tumelala akaniambia winie inabidi uende kwenu kwanza ukapumzike nami nitulize akili alafu utarudi,, nikamuuliza kuna usalama?? Akaniambia ulichokifanya sijakifurahia hauwezi kumtukana shangazi yangu kiasi kile,,unajua wale ni wazazi wangu hapa dar esaalam unapowakosea heshima siwezi kukuelewa hata kidogo,,,nikashangaa muda gani nilimtukana shangazi,,nikamwambia mimi sikumtukana shangazi yako ila yeye ndo aliniambia habari ambazo sikujua kama alizifikiria mara mbili,, ebu acha kuongea uongo shangazi kaniambia kila kitu,,hivi unajua mimi navumilia mangapi kua nawe? Nachekwa na kusemwa lakini navumilia tu alafu wewe unaanza kuleta mambo ya ajabu,,,kiukweli maneno yake yaliniuma sana nikamuuliza kesho ntaondoka saa ngapi? Akajibu,muda wowote utakaojisikia nauli ntakuachia mimi nitaenda kufungua duka,,nikamwambia sawa,,,nikageuka nikalala kwa mara ya kwanza tulilala bila kunigusa huku nikiwa sipo period...asubuhi niliamka saa kumi na mbili nikaenda nikaoga yeye bado kalala,,nikajiandaa nikapaki nguo zangu nikamuamsha nikamwambia mimi naondoka njoo ufunge mlango,,kisha nikatoka nikaenda kituoni hakukua mbali na tulipokua tunakaa,,,moja kwa moja ubungo nikapanda basi safari morogoro,,,njiani niliwaza sanaa nikamuachia tu mungu,,,nilivyofika msamvu nikachukua bodaboda hadi mjini lakini nikamuomba boda anipeleke kanisani kwanza, alinifikisha akaniacha nikaingia ndani nilipiga magoti nikamlilia mungu,, nililia mpaka nikahisi kukaukiwa nikamuuliz mungu hiki kikombe mbona kinanishinda,,,najua nimekosea kutoa mimba hapo awali lakini wewe ni baba wa huruma na husamehe mbona unaniadhibu kiasi hiki baba,,,nipunguzie hii adhabu ni kubwa sana 😭😭😭😭 niliomba masaa matatu kisha nikatoka nikaita boda nikaelekea nyumbani nafika mama sikumkuta alikua kazini niliwakuta tu wengine...nikapitiliza chumbani nikaweka mizigo nikalala...nakuja kushtuka jioni mama ananiamsha,,hapo sijala kitu toka nilivyokula jana,, mama akaniuliza mwanangu kuna usalama? Mbona umeisha hivi unaumwa?? Nikaamwambia siumwi mama ila nimerudishwa nyumbani,,,akaniuliza kwanini? Nikamuelezea kila kitu ilivyokua,, kama mzazi aliumia sanaa akaniambia usijali maadam umefika nyumbani pumzika kua na amani si kakurudisha mwenyew basi usijali,,punde francy akampigia mama akamwambia mama shikamoo,, mama akaitika marhaba habari za huko? Nzuri mama,,samahani naomba jumamosi nije tuzungumze na naomba winie akae huko kwanza mpaka nikija,,mama akamwambia sawa karibu kisha akakata simu,,,
   Nilikaa nyumbani karibia mwezi mzima hakutokea na wala hatukumpigia kumuulizia,, kwa upande wangu niliona hafadhari nipumzike kuchezea 🍆🍆 maana ingeniua,,,kuna kaka yangu ambae kaniachia ziwa huyo ndo ilikua shidah alikua anapatana sana na francy,,francy akamzaja mameno kaka yangu maana walikua wanawasiliana sana na kaka nae akaanza kumjaza maneno mama nikaonekana mimi ninadharau simuheshim francy namjibiza kila anachokiongea ndo maana nikaridishwa,,,baada ya mwezi na nusu francy alikuja kikawekwa kikao,,mwanaume alijua kujielezea yule yaani nilionekana mie ndo mkorofi kutokana na hasira niliyokua nayo nikawa nashindwa kuongea nalia tu,,mwisho wa siku nikaambiwa nimuombe msamaha na nirudi kwa mmewangu,,hapo miaka yote hiyo hatukufunga ndoa na nashukuru kwa hilo maana sijui ingekuaje,, niliomba msamaha kuepusha shari akataka tuondoke wote nikakataa nikamwambia we nenda nitakuja,,,baada ya siku mbili nikarudi tena dar esaalam,,ile kufika tu baada ya kusalimiana nae simu ya shangazi yake ikaingia,waliongea kwa muda kisha akanipa simu,,hello shikamoo shangazi,,marhaba hujambo?? Sijambo?? Akanambia siku nyingine ukigombana na mwenzio usikimbilie kuondoka uje tuongee maana unaondoka alafu unarudi ndo nini sasa,mwanaume atakudharau namna hiyo,,,nikamjibu tu sawa shangazi nimekuelewa,,,akakata simu,,, 
   Yaani baada ya kurudi mambo ndo yalizidi kua mabaya,,tunacheka siku moja baada ya wiki,,kufanywa kukarudi kulekule hapo wifi yangu anatafuta kila njia anamkutanisha rafiki yake na kaka yake,,akawa anapeleka maneno ya uchonganishi kijijini kwa wakwe zangu nashukuru mungu wakwe zangu walinipenda sana nikapata taarifa zoote,,,aisee siku hiyo sikumbakisha nikamfata nyumbani kwake tena nilimkuta na mumewe na wote walikua lao moja niliwachamba kisawasawa nikawatukana matusi ya kila rangi kisha nikaondoka zangu,maana niliwavumilia nikachoka,, tangia hapo mmawasiliano nao yakaishia hapo
ITAENDELEA.... 

Post a Comment

Previous Post Next Post