SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA: 20

Siku hiyo sikulala yaani nikipitiwa tu na usingizi kidogo anakushikashika nashtuka namtoa mkono,,kazi ilikua ni hiyo usiku kucha nilikuja kulala asubuhi alipoondoka kwenda kazini na sikumpa hiyo siku aliondoka amenuna balaa,,nikasema potelea pote we nuna,,,kumwambia mama nashindwa huyu ni mkwewe nilihisi nitamvunjia heshima na ukizingatia mama alitulea mazingira ya kutokua na ukaribu wa kumshirikisha mambo ya ndani sana,hivyo ilikua ngumu kwangu namna ya kuanza kumuelezea,,,ilifika kipindi UTI na Fangazi zikawa haziniachi nikipumzika ni wiki tu lakini kila siku kuumwa na hapo hata ukiumwa hakuachi nikimwambia subiri nipone anakwamvbia si unatumia dawa haina shidah yaani nilijuta mimi,, radha ya mapenzi ikaondoka kabisaa nikawa napata maumivu makali kila tunapokutana,,,nilikua naonekana kama bibi ama mdada ambae ameugua ugonjwa muda mrefuuu hata nikivaa nguo sivutiii,,,,akaanza tabia ya wivu hataki kuona naongea na mtu yoyote yule,,kiufupi mimi sikua na marafiki ila Mungu amenijalia ucheshi,,sasa kuna kipindi umeme unakatika na ndani hakukaliki inabidi nitoke nnje kama mnavyojua joto la dar likianza,,,basi natoka nakaa nnje mlangoni kwangu na chumba cha jirani nae akatoka nnje kiufupi hiyo ni kawaida na walitoka wengine tukawa tunapiga story,,muda huo francy akanikuta nnje alikua amefika kutoka kazini,,,aliwasalimia wengine mi akanipita akaingia ndani, nami nikaingia ili kumsalimia jamani nilikutana na maneno ya shomboo,,,hivi wew mwanamke mbona unapenda kujirahishisha hivyo unakaa na wanaume nje mnaongea kitu gani?,,,nikashangaa nikamwambia lakini mimi nilikua napunga tu upepo ndani joto na mbona tupo wengi tu nnje,,,akajibu kwa ukari,,kama unataka mtu wa kuongea nae si uende kwa wifi yako kuliko kuongea na hao wanaume wanakusaidia nini,,,uwiii nikamwambia wifi gani unaemsemea huyo mnafki au mwingine?? nikaona huyu atanikausha damu nikatoka nnje nikamuacha ndani kavuta mdomo hatariii,,,hapo wifi yangu na shangazi yake kutwa kuniongelea hovyo mara sizai na sitokaa kuzaa,,,wakadiriki kusema nilikua najiuza kimboka kwa mliokua dar nadhani mnapajua na aliyekua akiongea hayo maneno ni shangazi yake,wakati hiyo kimboka yenyew nimekuja kuisikia miaka ya hivi karibuni kipindi chote hicho sikuwahi isikia wala kuijua maana dar kwanza nilikua mgeni na sikua mzurulaji,,nikasema hawa watu wananitaka nini mimi jamani mbona shidah,, ndani gubu haliishi kila kukicha ni kero...
   Siku zilizidi kusonga alipokua anafanya kazi akaachishwa, waliamua tu kupunguza wafanyakazi hivyo alivyopata pesa yake ya NSSF akanifungulia duka la mangi,,,lakuuza vyakula na vitu vidogovidogo yeye akawa anahangaika kutafuta kazi sehemu nyingine, hilo duka likazidi kunikondesha,,,nilikua napenda nikienda dukani nakua smart navaa vizuri lakini kwake ilikua ugomvi anasema navaa napendeza nampendezea nani kwenda dukani tu navaa kama naenda mjini,,,yaani kiufupi alikua anataka niende nimefunga khanga chini nyingine nijifunike juu kama naenda msibani,,,,nikashindwa niishije na huyu mtu,,,kuna siku alipita muuza miwani,,kuna miwani ilinivutia nikanunua nikasema siku mojamoja nitakua navaa,,jamani jamani alivyorudi nyumbani akaikuta ugomvi ukaanza..tuligombana usiku kucha kisa tu miwani,,kwamba nikivaa naonekana si hadhi yake 😳😳😳....
   Tuliendelea kuishi kwa tabu hivyo hivyo tukamaliza miaka mitatu,,mimba sijafanikiwa kupata,,kwenye suala hilo hakuwahi kuninyanyasa kwakweli ila wifi yangu na shangazi mlijua kunikosesha raha nawashukuru kwa hilo,,,siku hiyo alikuja shangazi na mwanae wa kike nikawapokea vizuri sana nikawapikia chakula wakala hapo francy hakuwepo,,,baada ya kumaliza akaniambia nimekuja kuongea na wewe jambo moja,,,nikamwambia sawa shangazi nakusikiliza,,,akaendelea,,hivi mmefikia wapi swala la mtoto?? Nikamwambia bado tunahangaika hatujakata tamaaa,,,shangazi akasema kama unaona hutaweza kuzaa ongea na mwenzio atafute mtu amzalishe alafu akuletee mtoto ulee,, 😳😳😳 presha ilishuka ghafla nikaanza kujisikia vibaya....
ITAENDELEA..... 

Post a Comment

Previous Post Next Post