Simulizi: Kaka Utatuua Sehemu Ya Nne (04) FINAL


 “Haustahili kufa, unatakiwa kuishi kwa mateso mpaka ujutie siku ulipomuua mtoto wangu.” Yule Kaka alionge, ile risasi hakumlenga kaka yangu, aliipiga juu na baada ya kuipiga alichukua ile Bastoa na kumkabidhi Baba.

“Chukua kaihifadhi sehemu nzuri, nina uhakika kuna siku utaihitaji!” Aliondoka na kutuacha pale, kwa zaidi ya nusu saa tulikua tumesimama kila mmoja akimuangalia mwenzake, wote tulijawa na uoga hata Kaka ambaye alikua ni mwanajeshi, alikua anajiamini sana alikua anaogopa mpaka anatetemeka kabisa.

Baada ya yule Kaka kuondoka hakuna mtu aliongea kitu, kila mmoja alitoka kivyake, ni kama alikua ametuwekea dawa kwani hata Baba alifuata maelekezo yake na kwenda kuiweka ile Bastola hakumrudishia Kaka. Hali ya ukimya iliendelea katika familia yetu, tulianza kuishi kwa kuogopana, kila mmoja akimuona mwenzake kama adui, hakukua na maongezi tena. Nyumba haikua na amani tena, mimi niliondoka nyumbani na kwenda kuishi kwa rafiki yangu wa kiume, kusema kweli hali ya pale ilinitisha, sijui yule Kaka alitufanyia nini lakini mimi baada ya lile tukio nilijawa na hofu sana.

Usiku mmoja nilipigiwa simu, Baba alikua katika hali mbaya, nilishangaa kwani siku mbili kabla Baba alimpigia Mama simu kuwa anasafri, kuna rmzigo anaenda kuchukua Morogoro, alikaa kwa siku moja na kurudi. Lakini aliporudi nyumbani hali yake haikua sawa kabisa, alikua anatetemeka kama mtu mwenye baridi kali, alikua kama kachanganyikiwa, haongei kitu yaani ilikua ni hofu tu. Pamoja na yote yaliyotokea lakini nilikua nampenda sana Bba yangu, kama mtoto pekee wakike nyumbani wketu Baba yangu alikua ndiyo kila kitu. Niliongozana na mchumba wangu mpaka nyumbani, nilifika wakati wanajiandaa kumpeleka hopspitalini.

Lakini Baba alikua anagoma kupelekwa hospitalini, alikua haongei vitu vingine lakini likija suala la hospitalini absi anakataa aktakata, anaongea na hata kutaka kupigana. Kaka alipigiwa simu na kuja, alimuona vile na kuanza kumbembeleza Baba kukubali, baada ya kuongea naye alikubali, wakati huo tulikua sebuleni, akaomba kuingia ndani kubadilisha nguo ndiyo twende. Mama alitoka na kwenda jikoni, siju alikua anaangalia nini lakini haikupita hata dakika mbili, tulisikia mlio wa risasi “Paaaa!”

Kila mtu aliogiopa, Kaka alinyanyuka harakaharaka kuingia chumbani lakini alikuta Baba ameshafariki dunia. Baba alikua kachukua Bastola ya Kaka na kuiweka mdomoni kama alivyoelekezwa na yule Kaka na kujilipua, ubongo wopte ulikua chini, damu zilitapakaa chini kiasi kwamba hata kumuangalia ilikua ni shida. Mimi nilishindwa kuangalia, nilirudi sebuleni lakini kabla hata ya kukaa chini nilidondoka na kupotea fahamu.

Nilikuja kuzinduka masaa mawili baadaye nikiwa niko hospitalini, kumbe wakati nandondoka niliumia kichwa, kitu cha kwanza nilimuulizia Baba lakini watu waliniangalia tu, nilijua kuwa ameshakufa lakini nilitaka mtu kuniambia kuwa nilikua naota Bbaa alikua hai. Niliambiwa nikazimia tena, nikawa mtu wa kuzimia na kuzindika, nazimia nazinduka mpaka kesho yake ndiyo nilitolewa hospitalini.

Nilitoka hospitalini ambapo maandalizi ya mazishi ya Baba yalikua yanafantyika, hakuna mtu aliyekua anajua sabbau za Baba kujiua lakini akili yangu nilihisi kuwa kuna kitu ambcho yule kaka aalikifanya mpaka Bbaa kufikia hatua ya kujiua. Ilikua ni huzuni kubwa, kila mtu alikua anaumia kivyake kwani hakuna mtu aliyekua anaongea na mwenzake, Kaka ndiyo alikua kachanganyikiwa kabisa, kila wakati alijiona kuwa yeye ndiyo alikua ni sababu ya kifo cha Bbaa.

Maandalizi ya mazishi yalifanyika, siku ya mazishi yule Kaka alikuja kwenye mazishi ya Baba. Hakuishi kuja tu kanisani au makaburini bali alikuja mpaka kutusalmia na kutupa pole baada ya mazishi ya Baba. Yaani baada ya watu kutoka makaburini alikuja na kutusalimia sisi tena kwa kutushika mkono na kutupa pole. Nilikua na hasira sana lakini nilijikaza, alimfuata Kaka yangu na kumpa mkono, kaka alikataa kumshika mkono, alimshika Begani na kumuambia.

“Afadhali wewe umezika Baba ni mtu mzima kayachoka maisha mimi nimezika mke na mtoto kwa siku moja, inauma sana uchungu nilioupata hata nusu haujaupata.” Kaka alikasirika na kurusha kofi kutaka kumpiga lakini yule Kijana alilidaka lile kofi na kuurudisha mkono wake chini. Wakati hicho kitu kinatokea kuna Baba mmoja ambaye ni Bosi wake na Kaka yangu alikuja pale. Alimsihi kaka yangu kuacha vurugu na kisha kuanza kumuomb a msamaha yule kaka mwingine, akiomba msamaha kwa niaba ya Kaka tena kwa heshima, alimuomba waondoke akamuondoa pale.

Baada ya kama dakika kumi hivi yule Bosi wake na Kaka alimfuata Kaka na kumuuliza.

“Unamjua yule mtu uliyekua uantaka kumpiga?” Kaka alitingisha kich3wa kusema hamjui.

“Hata sijali, yule mbwa ndiyo kamuua Baba yangu!” 

“Kivpi wakati unasema alijipiga risasi na wewe ulikuepo?” Bosi wake alimuuliza kwa mashaaka.

“Sijui lakini najua tu, hata kama hajampiga yeye ila ni yeye kasababisha, nina uhakika kuna kitu kamfanyia Baba yangu na nitajua tu undani wake!” Kaka aliongea kwa hasira.

“Basi nikuambie tu, hata kama ni kweli kakuumiza lakini achana na hayo mambo, yatakupotezea kazi, achana na huyo mtusi mtu mzuri usipambane naye! Hiyo ni amri na si ombi!”

Kaka alitaka kubisha alimuuliza huyo ni nani ndipo bosi wake alimuinamia na kumnong’oneza, hatukusikia chcochote lakini baada tu ya kuambiwa Kaka alinyong’onyea hakuongea kitu, alibaki kimya, mpaka Bosi wake anaondoka Kaka hakuongea kitu hata tulipomuuliza hakusema kitu. Maisha yaliendelea kila mtu akiwa kivyakae. Lakini haikuisha hata mwezi Kaka alisimamishwa kazi, akaanza kunyw apombea, akawa ni mtu wa vurugu kupiga watu mtaani mpaka akaja kugukuzwa kazi.

Mpaka wakati huo hakuna mtu aliyekua anajua sababu za Baba kujiua, hali ya Mama ilikua mbaya kwani alikua na presha na sukari lakini figo zake zilianza kufeli, maisha yalikua magumu, mimi nilikua nimemaliza chuo sina kazi, mdogo wangu anasoma chuo hana mkopo Kaka aliyekua anamlipia ada alishakua mlevi na hakua na kazi.

Ilifikia hatua hata chakula nyumbani ilikua ni shida, Kaka aliuza nyumba yake na pes ayote ikaishia kwenye pombe, Matibabu ya Mama yalikua ni ghali sana, huwezi amini niliamua kujiingiza kwenye Biashara ya kuuza mwili ili kuweza kumhudumia Mama kwani mdogo wangu wa kiume baada ya kusimamishwa chuo kutokana na ada aliondoka nyumbani akaw2a anaishi na mwanamke Mama mtu mzima ambaye alikua anamlea.

Nilihasngaika ili kuhakikisha angalau nyumbani wanakula, Kaka alitaka kuuza nyumba tuliyokua tunaishi lakini niligoma kwani hata nilikua nayo, ikawa ni ugomvi, kila sikua anrudi nyumbani, anataka chakula na akikosa ni kunipiga, alikua ananipiga sana, Mama alikua mdhaifu akiongea basi anamtukana matusi mpaka ya nguoni. Siku moja nilikua kwenye misha miehse zangu, nilikua na mwanaume ambaye alininunua.

Wakati natoka nataka kuingia kwenye gari na huyo mwanaume Kaka aliniona, alinifuata na kuanza kunipiga, alinipiga Mimisana na yule kaka alipoingilia alianza kumpiga, alimpiga sana mpaka watu wakaingilia, akakamatwa na kupelekwa polisi. Alikaa mahabusu kwa wiki mbili, hakukua na mtu wa kumuewekea dhamana, Mama alipojua aliniambia nimsamehe lakini sikua tayari kwa hilo. Lakini siku moja tu nilishangaa Kaka katoka, alirudi nyumbani na kujifanya kuomba msamaha kwani amejifunza.

Nilimuuliza ni nani kamuwekea dhamana akaniambia hajui ila kesi imefutwa, aliniambia huyo mwanaume niliyekua naye kaamua asinisitaki tena. Niliamua kumtafuta huyo mwanaume kwakua nilikua na namba zake, tukaonana nikamuuliza kwanini kafuta kesi basi alishangaa, akaniambia kuwa Kaka yangu mwingine alimfuata na kumpa milioni mbili ili asiendelee na kesi.

“Aliniambia nichukue milioni mbili nifute kesi au niache milioni mbili iende mahakamani akamazlizane na hakimu. Mimi nikaona kuwa Kaka yako hawezi kunilipa chochote, hata akifungwa basi hawezi siwezi kufaidika chochote. Nilichukua milioni mbili na kufuta kesi!”

Nilishangaa ni Kaka yangu gani ambaye anaweza kutoa milioni mbili, nilimuulizia aliponielezea ndipo niligundua kuwa alikua ni yule yule Kaka ambaye alikua ni mchumba wa wifi yangu. nilizidi kuchanganyikiwa kwani nilijua kuwa kama kamtoa Kaka absi ana malengo yake, kweli baada ya siku mbili alikuja nyumbani, akaja kutusalimia, alinikuta Mimi na Mama, Mama alikua kitandni hali yake mbaya, hata hakua anaweza kumtambua kwani kumbukumbu zake zilianza kupokea.

Alimuulizia Kaka yangu niakamuambia katoka, aliniangalia kwa dharau na kuniambia.

“Nashukuru, ndiyo nilichotaka….” Nilimuuliza anamaanisha nini.

“Kaka yako angefungwa angerudi ni mtu mzima, lakini sasa hivi na hizo pombe nina uhakika kama ambavyo mimi sina amani basi yeye hana amani na nyie hamna amani!” Aliongea kwa hasira, alionekana kuwa na chuko sana. Nilijikuta nakasirika na kumuuliza.

“Kwahiyo Bdo hujamsamehe Kaka yangu, unajua mke wako angekuepo angetaka umsamehe!”

“Najua, kwakua alikua ni mwanamke mzuri lakini Kaka yako na familia yenu mlimharibu, sasa hayupo kusamehe, nipo mimi na klazi yangu ni mpaka kuhakikisha kuwa mnaishi kwa mateso mpaka mtamani kufa!”

“Huoni kama na wewe unajitesa, kwanini usisamehe na kuwa na mania tu,”

“Najua najitesa lakini ndiyo hivyo, siwezi kusamehe, nataka Kaka yako ateseke mpaka siku moja atamani kujichoma kisu afe, tofauti na hapo nitaendelea kuhakikisha kuwa hawi na amani kwani mimi sina amani!” Aliongea huku analia, kusema kweli alikua na kisasi lakini alionekana yeye kuumia zaidi.

“Ulimfanya nini Baba yangu?” Niliamua kumuuliza, nilikua namuogopa lakini suala la kifo cha Baba liliniumiza sana, ni kitu amcbho nilishindwa kukisahau, kwa nilivyokua namfahamu Baba yangu nilijua kabisa asingeweza kujiua kizembe namna ile.

“Sikumfanya kitu, nilimuonyesha tu ushenzio wa mtoto wake ndipo akaamua kujiua…” Alianza kunielezea. Alipozichukua zile flash na memory za Kaka alitaka kuzichoma moto, lakini alibaki nazo, siku hiyo Baba anaaga anaenda Morogoro alikua hajaenda, alimchukua yeye mpaka nyumbani kwake, walikua wawili tu. Akamuonyesha Baba zile video zote, namna Kaka alivyokua anampaka mke mchumba wake, namna alivyokua anampiga na kumtukana.

Baada ya kumaliza kumuonyesha alimvua Baba nguo zote, kisha akamuambia.

“Unaona, mimi ni tofauti na mtoto wako, uko uchi mbele yangu, ningeweza kukuiga, kukubaka, kuwaita watu wakufanyie ushenzi na usingeweza kunifanya chochote lakini nimeamua kuacha kwakua mimi ni mwema. Sasa vaa nguo zako na ondoka, ninachotaka kukuambia kuwa mwanao hatakua na amani tena, alifanya makosa sana kuniulia mtoto wangu, alifanya makosa sana!”

“Inamaana hukumgusa Baba yangu?”

“Hapana, ningemgusa nisingekua na tofauti na Kaka yako, nilitaka kumuonyesha tu kuwa mimi ni mshenzi kama nikiamua kuwa mshenzi na mwanae ni chkoko tu kwangu.”

“Lakini ulijua kuwa atajiua?”

“Nijue kwani mimi ni Mungu!” Aliongea kwa hasira na kuondoka, aliniacha nikiwa nimeduwaaa.

Nilipata amani kidogo kujua kuwa Baba hakufanyiw akitu kibaya sana lakini niliumia kuwa ushenzi wa Kaka yangu ndiyo ulimuua Baba yangu. Hali ya Mama ilizidi kuwa mbaya, ilifikia hatua hata chakula kikawa ni cha shida mpaka mwaka jana mwishoni ndiyo Mama yangu alifariki dunia. Ingaw ani Mama yangu lakini nilishukuru Mungu kuwa angalau anaenda kupumzika, kusema kweli Mama yangu aliteseka sana. Kaka alilazimishai mpaka tukauza nyumba tukagawana kila mtu kibyake, kipindi hicho hocho ndiyo nilianza kukusoma Kaka Iddi.

Niliamua kuchukua pesa yangu nikanunua kitabu chako cha Biashara, nikafungua Biashara ya kuuza vyombo. Kaka yeye pes ayake iliishia Baa, alianza kuja dukani kwangu kunisumbua,a nataka pesa nikimnyima ananipiga, kuna siku alinipiga mpaka nikalazwa hospitalini, nikamuuliza amemuua Baba na sasa anayaka kuniua na mimi. Niliripoti Polisi na kufungua kesi lakini nahsii yule Kaka aliingilia kati Kaka ayangu katoka.

Ni Kaka yangu wa damu lakini natamani kumfunga, natamani asiwepo mtaani, yaani sina amani, nikiwa wkenye mahusiano atatafuta namna ya kuyavunja. Baada ya mambo kuwa magumu sana niliamua kumtafute yule Kaka na kumuomba msamaha, nilimuambia kama ni kujifunza tushajifunza atusamehe kwani familia yetu imeshasambaratika, aliniuliza unataka nifanye nini. Nilijikuta namjibu.

“Nataka sasa hivi nikim[peleka Kaka yangu Polisi umauche huko huko, muache aoende jela labda atajifunza.”

Yule Kaka aliniangalia kwa huruma na kuniambia.

“Sitaingilia tena mambo yenu, wewe mpeleke tu!” kusema kweli alikua anazungumzia mimi kumfunga Kaka yangu lakini jibu lake limenipa amani sana. Najua ni suala la mdua tu Kaka yangu ataharibu na mimi nitalazimika kumpeleka Polisi, ni ndugu yangu lakini nimechoka, Kaka yangu kamuua Baba, Mama na sasa anataka kutuuana sisi, hapana, na mimi nina msiha bora akaozee tu jela na sisi tupumue!

BONYEZA HAPA UPATE MAKALA ZA MAFANIKIO

MWISHO




1 Comments

  1. Je! unataka kununua figo, viungo vya mwili au unataka kuuza yako
    figo au viungo vya mwili? Je, unatafuta fursa ya kuuza
    figo yako kwa pesa kutokana na kuharibika kwa kifedha na hujui la kufanya, basi wasiliana nasi leo na tutakupa kiasi kizuri cha pesa $500,000 dola kwa Figo yako. Jina langu ni Daktari Patricia Marie na mimi ni Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu katika MAX HEALTH CARE Hospitali yetu ina utaalam wa Upasuaji wa Figo na pia tunashughulika na ununuzi na upandikizaji wa figo na wafadhili anayeishi na sambamba. Tunapatikana India, USA, Malaysia, Singapore. Japani.

    Tafadhali tujulishe ikiwa una nia ya kuuza au kununua figo au
    Organs tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa na kupitia barua pepe.

    Barua pepe: maxhealthcare406@gmail.com

    Kila la heri
    MKURUGENZI MKUU WA TIBA

    ReplyDelete
Previous Post Next Post