Viungo 5 Murwaaa katika Ndoa !


Ili pilau la sikukuu linoge halina budi lipikwe kwa ufundi na maujuzi mengi,bila hivyo pamoja na hamu ambayo wanafamilia watakuwa nayo ujue fika hakuna atakaye thubutu kulisogelea pilau hilo ikiwa halijawekewa nakishi nakishi za kupendeza.

Katika hali hiyo hiyo wanandoa hawana budi kufahamu wajibu wao wawapo katika ndoa.

Nakupendekezea viungo muhimu sana katika ndoa yako ambavyo kupitia hivyo waweza kuponya ndoa yako.

Viungo hivyo ambavyo nakupendekezea ndugu msomaji ni ;


ASANTE MPENZI WANGU

Hivi utapungukiwa nini kama utamwambia mpenzi wako asante kwa hicho kidogo alicho kupatia?
Ujue wakati mwingine ni ujinga wetu tu....hata tunajikuta katika majanga.Kuna watu ili washukuru wanataka wapewe magari kama Rambo guene ndipo waseme asante.
Je unajua kuwa zawadi ya ua ina maana kubwa kuliko vile unavyo Dhani? Jifunze kushukuru kikubwa hata kidogo pia.

POLE MPENZI WANGU

Mpe pole mpenzi wako kwa kazi na shughuli za kutwa.Usiu nyime haja yake moyo wako.
Jisikie amani na furaha kushiriki mbaraka wa upendo na mwenzi wako.
Kwa mlioko katika mahusiano neno pole lisiondoke katika safari yenu ya maisha ya Mapenzi.

NAKUPENDA MPENZI WANGU

Kuna baadhi ya wapenzi ambao nahisi kabisa wanaishi katika ndoa lakini,toka waingie kwenye ndoa hakuna ambye amewahi kumwambia mwenzake nakupenda mpenzi wangu.
Kosa hawa wapenzi wapate watoto ,hapo huwa ndio mwisho wa haya yote.
Hata iweje ! Wapenzi hawana budi kuishi kama wachumba daima mpaka kifo .
Picha ya mapenzi yenu ya ujanani iwe ndio ngao pekee kuwapeleka mbele.

UMEPENDEZA MPENZI WANGU.

Wanaume wengi tunaongoza kwa kuchukulia mambo kirahisi,hii naona Ndiyo sababu kubwa ya mahusiano mengi kuwa katika migogoro.
Inashangaza unatoka nyumbani kwako,unashindwa kumpongeza mwenzi wako kwamba amependeza ,ati unakutana na kibinti njiani au ofisini unaanza kukisifia ,hivi kweli unachokifanya unadhani kinaweza kuwa na manufaa katika mahusiano yako?
Pengezi zote anapaswa apewe mwenzi wako maana hiyo ni stahiki yake.

SAMAHANI MPENZI WANGU.

Ukikosea usione haya kushuka na kuomba msamaha.
Ukiomba msamaha hutapungukiwa na chochote zaidi ya kubalikiwa zaidi.
Ukikosea kubali kushuka na kukiri kosa.
Hivi unajaua kuwa miongoni mwa ndoa zenye furaha ni zile ambazo wapenzi wamejifunza kuombana msamaha?
Najua hakuna ndoa ambayo wapenzi wanaishi ,murwaaa kabisa pasipo misuguano.
Misuguano midogo modogo ipo lakini kuimaliza misuguano hiyo ni mmoja kujishusha.
Kuna mtu mmoja amewahi kusema ndoa yenye furaha ni ile ambayo imefungwa kati ya mwanaume kipofu na mwanamke kiziwi.

Mungu akupatie ujasiri namna ya kuyadumisha mahusiano yako.



BARIKIWA.



MUNGU NI PENDO.

Post a Comment

Previous Post Next Post