Mwalimu Mama nafasi umepata wewe fanya taratibu zote mtoto aanze masomo.
Mama Asante mwalimu lakini naomba unisaidie.
Mwalimu- Nikusaidie nini tena mama? Kama ni mtoto nimeshamkubali nini kingine?
Mama- Mwalimu mtoto amekaa nyumbani kwa muda mrefu hivyo naomba aendelee kuja shule kati naendelea kushughulikia uwamisho na mengineyo. Ni saidie mwalimu tafadhali.
Mwalimu Kama ni hilo hakuna wasiwasi wewe ni mzazi mwenzangu na mtoto akisha zaliwa niwawote na majukumu ni ya wote pia mama. Lazima tusaidiane kwani leo kwangu kesho kwako na leo ni kwao hauenda kesho kwangu nitakusaidia mama.
Mama alipata furaha iliyopotea kwa muda na amani ilianza kurudi tena. Alirudi nyumbani kwa furaha, nakuanza kumwambia mjomba wake kwa furaha na amani na baadae alikuja kuniambia mimi mwenyewe . nilifurahi sana na amani iliyopotea kwa muda mrefu ilianza kurejea tena.
Nilimwambia mama nashukuru kwa kuangaika na mimi, mama nilipokukwaza naomba unisamehe, nilikuwa mwepesi sana kuomba msamaha pale nilipomkwanza mama yangu na si mama tu kila ninayemkwaza au kuhisi kuwa nimemkwanza mtu huwa naanza kujikomba kwake na hiyo yote ni ili nipate ukweli kama nitakuwa nimekosea na hivyo kujirudi haraka na kuomba msamaha mapema kwani sipendi mtu anikwaze na mimi pia sipendi kumkwaza mtu katika maisha yangu kwani hali yangu ni lihifahamu hivyo sikupenda kukwazika bila sababu na hiyo ndiyo tabia yangu haddi sasa.
Siku iliwadia na nilianza kwenda tena shule. Na mama nae alirejea Arusha kumalizia baadhi ya vitu vya shule. Nilianza kuingia darasani mwaka 2008. Nilirudia kidato cha pili kwani nilipokuwa Arusha sikuweza kabisa kufanya mtihani wa kidato cha pili kulingana na hali yangu ilivyokuwa na hivyo sikuwa nabudi nilirudia kidato cha pili. Niliendelea na masomo yangu chini ya uwangalizi wa mkuu wa shule Deodath na msaidizi wake Helena pamoja na akademiki wangu Mwandinda pamoja na baadhi ya walimu nilianza masomo yangu salama bila matatizo na baada ya wiki kama tatu hali ilianza kubadilika na kuwa mbaya nilianza kutapika tena damu nikiwa shuleni na baadae nilipelekwa hospitali ya rufaa KCMC na nilipofika waliniagalia na baadae walinipeleka wodini na kunilaza ICU gorofa namba 2 nikiwa chini ya dokta Moleli na wengine pamoja na nesi mmoja kwa jina ambalo nilikuwa nikilisikia akitajwa ni mama Inno pamoja na wengine ambao kwa sasa siwakumbuka tena. Niliendelea na matibabu na nilipoenda kwenye vipimo waliniambia navidonda vya tumbo lakini katika vidonda hivyo havina uwezo wa kutoa, damu lakini hata wao wanaishangaa hiyo hali. Niliendelea na matibabu hayo kwa muda wa wiki 1 na baadae nilirudi nyumbani.
Ilinilazimu kurudi nyumbani kuendelea na matibabu kwani hospitali hawakuweza kujua hali yangu halisi hivyo waliniambia nikaendelea na matibabu nyumbani. Hali halisi nyumbani haikuwa mbaya niliporudi nyumbani nikawa mzima kabisa. Wengi walistaajabu kuona nikiwa mzima kabisa lakini nilipewa dawa za vidonda vya tumbo, hivyo niliendelea kumeza hizo dawa kwani madaktari waliniambia nisiache kumeza hizo dawa kila siku. Dawa zilikuwa nyingi kupita uwezo wangu kwani nakumbuka yalikuwa mabox 32 ya dawa pamoja na zile sindano nilizokuwa nikichoma pia zilikuwa ni nyingi kwangu. Mwili ulichoka na afya yangu ikawa ya maajabu nilipata afya nzuri nikawa kama si mgonjwa tena. Na kila aliyeniangalia hakuamini kama, mimi ni mgonjwa siku.
***
Siku zilizidi kwenda na haliyangu ikawa nzuri na niliendelea kwenda shule kama kawaida. Siku moja nikiwa shuleni hali ilibadilika na baada ya muda nilitoka nje. Mwalimu wa zamu alinikuta nikiwa nje na kuniambia Emiliana kwa nini wenzako wako darasani alafu wewe uko nje ni kamwambia mwalimu sijisikii vizuri naomba nipate japo upepo kidogo alafu nitarudi darasani, mwalimu Muungano hakuweza kunielewa alinichapa fimbo na kuniambia nenda darasani wewe pumbavu nilienda darasani wakati napanda, ngazi kuingia darasani hali ilibadilika na nikaanza kutapika tena damu, hali yangu ilikuwa mbaya zaidi.
Na damu zilianza kutoka tena puani kwa ujumla hali yangu ikawa mbaya tena na hivyo ilinilazimu kurudishwa tena hospitali na nililazwa wodi ile ile ya mara ya kwanza na madaktari waliniambia wewe si umetoka hapa juzi juzi tu? Kwa kuwa nilikuwa katika hali ya tofauti sikuweza kujibu lakini daktari mmoja alikuja na kusema huyu si yule wa juzi yaani mmesahau? Nililazwa tena na kuwekewa hoksijeni na baadae waliniwekea mipira ya kuvuta damu tumboni, hali yangu ilikuwa mbaya kupita ile ya mara ya kwanza lakini cha ajabu hakika dawa nilizopewa zaidi ya kutundikiwa dripu na mama yangu aliposikia kuwa niko hospitali alikuja Moshi na kuwaomba wanitoe hospitali: madaktari wakamwambia mama yangu hatuwezi kumtoa mtoto hospitali hadi hali yake itakapo turidhisha. Mama alizidi kuwaomba na baadae walikubali na mimi nilitoka hospitali na tulirejea nyumbani: cha kushangaza siku iliyofuatia ni liamka nikiwa mzima kabisa ingawa nilikuwa nikisikia uchovu mwingi: mama alimwambia mjomba wake Emmy akiumwa msiwe mnampeleka hospitali huyu ni wa maombi tu.
Mjomba wake ambae mimi ni babu yangu hakuweza kumuelewa kwa haraka waliendelea na maojiano na baadae babu alimuelewa. Mama yangu alichukuwa uwamuzi wa kwenda shule na alipofika waliongea kwa marefu zaidi na ilikuwa hivi:
Mama Pole sana mwalimu kwa kazi ngumu nilivyokupa.
Mwalimu - Ni yakawaida ingawa yanatisha kwa ni sikuwahi kuona mtu anatapika damu kiasi kikubwa hivi.
Mama- Hiyo ndiyo hali halisi ya mwanafunzi wake.
Mwalimu Pole sana mama sasa tufanye nini?
Mama Mwalimu huyu siyo wa hospitali anatakiwa maombi tu kwani hali yake naifahamu kama ni hospitali tutazidi kupoteza ela bure kwani huyu akiumwa ukimplekea nyumbani nimzima kabisa.
Mwalimu- lakini hii ni hali ya ajabu
Mwalimu alimuelewa mama na baadae waliachana. Siku inayofuatia nilienda shule na mama yangu, na tulipofika tuliachana na kuagana na mama kwani yeye alikuwa anarejea Arusha niliendelea na masomo uku nikiwa naendelea kumeza dawa za vidonda vya tumbo. Niliendelea kuombewa na mchungaji Justine katika kanisa la E.A.G.T niliendelea kuombewa na watumishi mbalimbali akiwemo Paster Siksi Betri wa kanisa la Victor lililopo karibu, na kanisa la kristo Mfalme chini ya idara ya maji na Mchungaji huyo nilimfahamu kupitia mwalimu wangu aliyejaili afya yangu na kuyahurumia, maisha yangu alijaribu kuyaokoa sana maisha yangu. Mwalimu Rose Mery alinipeleka hadi katika kanisa lao hilo la Victoria na kukutana na Pastor huyo na kuniombea. Namshukuru Mungu kwa ajili ya Paster Siksi Betri kwa kuyaokoa maisha yangu aliniombea na hali yangu ilianza kurejea kuwa katika hali yangu ya mwanzo. Namshukru sana kwani nilienda nikiwa natapika sana damu na nyingine zilikuwa zikitoka katika masikio. Hali iliendelea vizuri kabisa na shule nilienda bila matatizo yoyote.
Maisha yaliendelea na nyumbani nilipoishi waliendelea kuangaika huku na huko wa ufumbuzi wa kunitafutia dawa ambayo itaweza kuniweka hali yangu iwe sawa kabisa na ikiwezekana kupona kabisa. Bibi yangu ambae ni mke wa mjomba wake mama ambae ni babu yangu aliendelea pia kutafuta shuluhu ya ugonjwa kwa kwenda hata kwa waganga wa kienyeji. Siku moja nikiwa nimetoka shuleni bibi yangu huyo aliniita na kuniambia:-
Bibi ambae anaitwa Mery Hendry Chua alianza kwa kuniambia:-
Nimeenda kwa mtaalam mmoja na nilipofika nilimueleza hali yako halisi na baade mtaalamu huyo aliniambia kuwa aliyefanya yote hayo na kukufanya wewe kuwa katika hali hiyo ni baba yako kwa hiyo ameniambia kesho nikupeleke ili akakupe dawa.
- Nilimwambia bibi kama nikawa waganga mimi siendi kama nakufa acha nife lakini kwa waganga siendi.
- Aliniambia kama hautaki ukiumwa hamna mtu yeyote yule atakae angaika na wewe.
- Ni kamwambia sawa.
- Bibi yangu alienda kumwambia muwewe Hendry kuwa mjukuu wako nimemwambia kuwa kuna mahali nampeleka akapewe dawa asiumwe tena lakini amekataa katakata.
- Babu alikuja na kuanza kuniambia haya
- Je unataka kupona ? nikajibu ndiyo.
- Je unapenda kuumwa ?- nikamwambia hapana
- Au unafurahia hiyo hali ya kuanguka anguka na kutapika damu!
- Nikamwambia hapana babu hata mimi hali hii nimeshaichoka.
Alinijibu haya:-
Hiyo hali unaipenda na tena inawezekana unaifurahia sana kwa sababu ungekuwa haupendi, kuifurahiya hali hiyo yale ambayo bibi yako amekwambia ungeya fuatilia na kushirikiana nae kuitetea hali yako. Nilimjibu, babu najua kuwa mnanipenda na tena hampendi kuona nikiishi katika hali ya mateso kiasi hichi na furahi sana kwa hayo, lakini swala la kwa waganga siko nalo sawa kama nikwa waganga siendi kabisa. Kwa hilo naomba mnisamehe. Alijibu utajua peke yako lakini kakaeni , ufikirie vizuri ukiwa tayari utuambie.
Siku ziliendelea kwenda na hali yangu ikawa imekaa sawa. Siku moja ya jumapili mjomba yangu Paul Hendry Chua alikuja nyumbani kwa baba yake ambae, ndiye babu yangu, kwani makao yake yeye anaishi KCMC na sisi tuishi Uru Kitandu.
Alikuja nyumbani na kuniambia leo nataka kutoka na wewe. Nikamwambia twende wapi tena mjomba? Akaniambia leo ni jumapili twende ukanywe hata soda moja turudi nyumbani nikamwambia sawa mjomba tuliondoka na kuelekea dukani na duka hilo lilijulikana kijijini pale kama kwa TENGIO SHOP lilikuwa ni duka kubwa lenye kila kitu tulifika na kuudumiwa.
Tuliendelea kupata vinywaji ukutukiendelea na stori za hapa na pale. Tukiwa tunaendelea na stori alitokea kijana mmoja kwa jina la Deodath Joseph Kimaro, tulijumuika naye lakini yeye alikuwa akinywa maziwa mtindi. Alinikaribisha na nikamwambia asante lakini siwezi kuchanganya maziwa na soda.
Stori ziliendelea na baadae mimi nilinyanyuka na kuelekea chooni: na choo hicho hakikuwa mbali sana na pale dukani: nilienda na nilipokuwa natoka chooni nilimkuta kijana Yule nje kwa haraka haraka nilishtuka na nilipishana nae lakini alinisimamisha kwa kunizuiya. Nilisimama na kuanza kumsikiliza . alianza hivi:-
Deodath Mambo
Emmy Powa
Deodath Samahani unaitwa nani?
Emmy Naitwa Emmy au Ester.
Kwani unashida gani hadi unanizuiya nisipate?
Deodath Naomba niongee na wewe kidogo.
Emmy Kuna nini?
Deodath Pauli ni nani wako?
Emmy Ni mjomba angu.
Deodath Emmy, nisikusumbue sana nataka kukwambia nakupenda.
Emmy Kwa leo siwezi kuyazungumzia hayo kwani hapa, si mahali pake na mwanaume anayempenda msichana hamsimamishi barabarani anamfuata kwao. Na anakaribishwa kwa hiyo naomba tuongee kesho kwa leo siko tayari.
Tuliachana na mimi nilielekea nilipokuwa nimekaa na mjomba na baada ya muda mfupi tuliondoka, na kuelekea nyumbani. Siku ya jumatatu iliwadia nilielekea shule na baada ya kurudi nilikuja kuitwa kuambiwa kuwa kuna mtu anakuita pale dukani ulipokuwa na mjomba wako jana. Nilienda na wazi wazi nilijua kuwa ni Deodath ndiye ananiita kwani nilimwambia tutaonana tena. Nilienda na akanikaribisha na kunipa kiti kisha tulianza mazungumzo.
Alianza na kusema pole na shule, nikamwambia asante,. Akaanza kama nilivyo kwambia jana jumapili kuwa nakupenda sana, nilianza kumjibu kuwa mimi bado ni mwanafunzi tena ni wakidato cha pili kwa hiyo niache shule? Alisema hapana Emmy siyo uwache shule, nilimwambia kama siyo acha shule unaniambia nini hicho? Alinijibu nitakusubiria hadi umalize shule, nilishangaa na kumwambia siyo wanaume. Alinijibu naomba uniamini Emmy. Nilianza kwa kumwambia haya, kaka yangu hata kama umenipenda kweli kuwa na mimi hautaweza aliniulizia kwa nini unasema kuwa na mimi hautaweza? Nilimwambia usinione hivi wengine wananikimbia wengine wananiogopa wengine hawanipendi pia.
Akauliza kwa nini unasema hivyo? Nilimwambia mimi ni msichana mwenye matatizo na hali yangu si nzuri hata kidogo. Akaniambia matatizo gani. Nilianza kumwadithia historia yangu yote ya maisha na baadae alinielewa na kuniambia Emmy hizo stori nimesha zisikia sikia kumbe ni kweli. Nilimjibu ni kweli na kwa kupitia hilo hauta niweza kwa hiyo tafuta msichana mwingine kwa mimi hapana.
alimjibu haya Emmy sijakupenda kwa sababu eti mzuri au nikuaribu au kukuchezea hapana nimekupenda kama ulivyo na nimekupenda pamoja na hayo matatizo uliyonayo. Naomba unielewe na baada ya hapo tuliachana na pale pale ndipo hali ya urafiki ilianza.
*******
BONYEZA HAPA KUSOMA MAKALA ZA MAFANIKIO
INAENDELEA
Tags:
RIWAYA