NIACHE NILIE ---5 😓😓😓😓

6 days ago

Ilipoishia...

Wengine wakasema haya uenda mama yake mwenyewe anamuuwa mwanae kila mmoja alitamka analoweza kutamka na kwa walio mzarau Mungu walisema Mtu gani huyu ambae anaombewa na watu wote hao lakini haponi alafu eti ni walokole, walokole si wanasemaga, wanaponya mbona huyo haponi ni maneno yaliyoendelea kutolewa na binadamu ambao hawakuwa na hofu ya Mungu ndani yao Nilizidi kuumia zaidi kwa maneno makali na yasiyokuwa na uzima ndani yake.



SONGA NAYO...



Maombi yaliendelea kila kona bila ya watu wa Mungu kukata tamaa. Mchungaji Kabese wa kanisa la E.A.G.T Chemchem alizidi kujitolea kwa ajili yangu na kwa ajili ya uhai wangu alifunga usiku na mchana kwa ajili yangu, na yote hayo nikumlilia Mungu kwa ajili ya hali yangu. Maombi yaliendelea na watumishi waliendelea kunitia moyo, mawasiliano ya babu yangu, yaliendelea kai yake na mtumishi wa Mungu Mwakasege kwa ajili ya kuiponya afya yangu. 

Babu yangu Mwakalinga alijitaidi kwa nguvu zake zote na uku maombi yakiendelea kwa kila mmoja, mchungaji Haule bila kukata tama aliendelea na maombi pia. Mungu aliyasikia maombi yaliyekuwa akiomba na kulia kwa ajili yangu hali yangu ilianza kujirudi polepole na kujikuta naendelea vizuri kabisa na ile hali ya kutokwa na damu ilipotea. Niliendelea kwenda shule kama kawaida niliendelea vizuri kabisa. 

Nilisoma kwa muda mrefu bila kuugua nikiwa nakaribia kufanya mtihani wangu wa kidato cha pili hali yangu ilianza kuwa mbaya tena na iyo ilitokana na mwalimu kuingia darasani na kuanza kuadhibu wanafunzi ambao hawakufanya kazi aliyoiacha darasani yaani ambao hawakuandika kazi aliyoiacha ubaoni. Nilimueleza mwalimu kuwa sikuwepo shuleni ile siku aliyoacha kazi hiyo, alinijibu ungewauliza mwenzako nikamwambia mwalimu nitaandika lakini mwalimu hakuelewa ingawa wanafunzi wenzangu walinitetea lakini mwalimu hakuelewa baada yake alichukua uwamuzi wakuniadhibu, alinichapa fimbo moja tu lakini baada ya kunichapa fimbo ili hali ilibadilika, nakuwa mbaya tena. Tumbo lilianza kuniuma kichwa na kujisikia vibaya mwili mzima baada ya muda nilianza kutoka damu puani na baada ya muda tena nilianza kutapika damu kutokana na maumivu makali ya tumbo. 

Baada ya muda waalimu wangu waliamua kunipeleka hospitali ya Mount Meru na ndipo nilipo lazwa. Madaktari waliangaika na mimi bila mafanikio yoyote kwani walijaribu kupima vipimo vyote lakini hakuna kilichoonekana na kila walipojaribu kupima damu ilikuwa ikiganda walijaribu kuchukua damu kila mara lakin ilikuwa ikifika maabara inaganda haifai tena kupima madaktari walijaribu kuchukua tena damu lakini ilishindikana kutokana na mishipa kutoonekana, hivyo waliamua kuchukua damu pembezoni mwa sehemu za siri ili kupata damu kwa ajili ya vipimo. Hivyo ilibidi wafanya hivyo na baadae walifanikiwa na damu iipatikana na waliamua damu ikafanyiwe uchunguzi Nairobi. Waliamua kuwashirikisha wazazi wangu. 

Damu ilisafirishwa na kupelekwa Nairobi lakini cha kushangaza na cha kustabisha damu ilipofika kwenye vipimo iliganda tena na hivyo haikuwezekana na kupima ulishindikana. Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi na damu zilizidi kutoka kila sehemu yenye uwazi katika mwili wangu. Mtihani wa kuingia kidato cha tatu ulifanyika, uku mimi nikiwa bado hospitalini hivyo sikuweza, kabisa kufanya mtihani wa kidato cha pili. Hali yangu ilizidi kuwa mbaya zaidi na nidpo nikiwa hospitali nilipoteza fahamu na madaktari kunizania kuwa nimekufa ni baada ya kupoteza fahamu siku 4 na kunitaka kupelekwa mochwari kutokana na maombi ya watakatifu wengi na mmoja wao akiwa ni mama yangu mzazi RUTH MWAKALINGA. 

Hivyo mama yangu pamoja na baba yangu mlezi STEPHEN NGOME ambae kwa sasa ni marehemu walichukuwa uwamuzi wakwenda, kumkamata baba yangu mzazi Ernest na kumpeleka, kituoni na walipofika kituoni na kuadhibiwa ndipo alipotamka kauli kali na ya kuumiza watu Alisema hivi:-

Ernest Kuna kanisa mke wangu alinipeleka na nilipofika waliniamia kama nataka kuwa tajiri nimtoe mtoto wangu wa kwanza kafara ndipo, nitakuwa tajiri kama ndugu zangu.

Nikiwa hospitali, baada ya baba yangu huyo kutamka hayo ndipo nilipata ufahamu na kuamka na baada ya kuamka tu ilibidi mama yangu kwa kusaidiana na wauguzi kunitoa katika sehemu ile na kumwambia mama anipeleke nyumbani kwani wanaogopa, kutokana na kuandika kwenye faili kuwa nimefariki na hiyo itawasababishia kufukuzwa kazi mama yangu aliamua kufanya hivyo na kabla kufanya hivyo nilitolewa kwanza zile pamba kwani nilikuwa nimeshawekewa kabisa pamba kama mfu hivyo waliniondoa, kila walichokiweka kwenye mwili wangu na kuondoka. Tuliendelea kukaa nyumbani nikiendelea na maombezi:. 

Mama yangu mzazi na mama zangu wadogo ambao ni wadogo zake na mama yangu mzazi pamoja na baba yangu mlezi waliendelea kunitia moyo na kunijenga kwa hali ya kumwamini Mungu na kuomba na kuamini na kukiri uponyaji pia. 

Moyo uliniuma sana kwani mtihani sikufanya na niliendelea kujiuliza moyoni kwa nini mimi tu? Niliona kama dunia nzima hakuna anayeteseka kama mimi. Nilizidi kujiona sina thamani yoyote hapa duniani na hiyo ilinifanya nizidi kuumia zaidi kutokana na kuwa na ndugu wengi lakini hawana msaada wowote kwangu. Kwanza kwa baba yangu mzazi wako kumi wasichana watano na wavulana watano lakini hakuna aliyekuwa anaiyona thamani ya maisha yangu na zaidi niliumia kutokana na wao kuwa na uwezo mkubwa mali lakini hawatoi msaada wowote kwangu, zaidi ya shangazi mmoja kuangaika kuiangalia hali yangu na kunitia moyo, nitumuombea Mungu azidi kumbariki shangazi yangu huyo kwa jina la Yuster. Niliendelea kuishi kwa maswali mengi na yaliyoniumiza moyo, akili na ufahamu wangu na niliumia kutokana na matendo, machafu yasiyo na huruma na makali aliyonitendea baba yangu pamoja na mkwewe ambae ni mama wa kambo kwangu. 

Niliumia kwa kuwa aliyetenda hayo ni baba yangu mzazi, mzazi asiyekuwa na huruma, mzazi asiyekuwa na hofu ndani ya moyo, mzazi aliyekuwa hana staahata ya kuona huyu ni mtoto wangu. Niliumia sana na kuzidi kumchukia zaidi na kumuona labla si baba yangu mzazi kwani angekuwa ni baba yangu aliyejua thamani, uchungu asingefanya hayo aliyoamua kunifanyia. Wameuzalilisha mwili wangu wameukumu mwili wangu wameharibu afya yangu bila huruma yoyote ile. 

Mungu aliyasirika maombi ya watakatifu wake na hali yangu ilianza kuwa nzuri tena. Baada ya muda hali ikawa nzuri kabisa. Na hali yangu ilibadilika zaidi pale mtu alipojaribu kunikemea, kunigombeza kunifokea na hata kunishtua ndipo hali ilijirudia kwa matukio haya mtu yeyote kuyafanya.

Baada ya muda na hali yangu ilikuwa sawa nilienda Moshi kwa bibi yangu nikiwa na mama yangu mzazi tulielekea Moshi Marangu ambapo aliishi bibi na babu mzazi wa baba. Ambao ni wazazi wa baba yangu mzazi Ernest. Tulipofika tuliwaelezea yote na kuwaambia yote yaliyonikuta nay ale ambayo mtoto wao amenitendea waliuzunika sana waliumia sana na waliamua hivi:-

- Maana mmechukua uwamuzi mzuri wakuja kusema mbele yetu nyie nendeni tutawasiliana naye na tutakapo wasiliana nae tutamwita na akija tutawaambia ili kuweze kukaa kikao. Baba Martine Tairo ndiye aliyetamka haya na alizidi kusema haya.

- Namuacha aendelee na huo upumbafu wake hadi mwisho kwani siku izi amebadilika sana hata mimi niliye mlezi, wake nimeshajaribu kumwita hapa lakini hataki kuja.



Alisema Nendeni tutawasiliana. Tuliondoka na kurudi jijini Arusha ambapo tunaishi. Baada ya muda tulirudi moshi tena Marangu na ndipo tulienda kwenye kikao ambacho babu yangu alikisema tangu mwanzoni. Tulifika moshi nikiwa mimi, mama yangu na baba yangu mlezi na tulipofika tuliwakuta. Niliwaona ndugu wa baba ambao ni baba zangu wakubwa na shangazi wakubwa na shangazi zangu na baadhi ya watu wa ukoo. Tulikusanyika na kupata chakula cha mchana. 

Na baada ya hapo tulianza kutambulishana na tulipomaliza matambulishano, mazungumzo yalianza na yalikuwa kama ifuatavyo:-

Babu Karibu sana wanangu

Tuliokuwepo - Asante sana baba

Babu Ningependa kikao hiki kiwe cha amani bila magombano yoyote.

Kwa kuwa sisi kwa upande wetu tulienda na mchungaji, basi mchungaji alisema haya.

Mchungaji Baba pamoja na ndugu mliopo katika kikao hiki ningefurahi zaidi kama tungeomba, na ndipo tufungue kikao chetu.

Baba Ndiyo vizuri zaidi ili Mungu awe pamoja na sisi na atuongoze tuanze salama tumalize salama.

Basi mchungaji alifanya maombi kwa ujumla na alipomaliza maongezi yaliendelea kama walivyokuwa wameanza na yaliendelea hivi:-

Babu Ernest mwanangu umeanza lini ukatili na unyama mkali na waajabu kama huu 

Ernest Kwani nimefanya nini baba?

Babu Kwani haujui ulichokifanya?

Ernest Sijui

Babu Eli mwali wewe na mwenzako mmeanza lini mambo yakishetani kama haya?

Mwali Mambo yapi baba?

Babu Kwani hamjui mlichokifanya?

Mwali Hatujui baba

Yalikuwa ni majibishano ya baba yangu mzazi na baba yake mzazi. Martini Tairo pamoja na mama yangu wa kambo. Niliendelea kujisikia vibaya zaidi kwani niliwaona mbeya na hasira zilizidi kuwa kali ndani yangu machozi yaliendelea kunitoka na nilizidi kuumia kutokana na maswali wanayoulizwa kujifanya hawaelewi nilitamani kuwarukia.



****



Waliendelea hivi:-

Babu Ernest nakuuliza tena umefanya nini?

Ernest Nimefanya nini, nini?

Babu Nitakupiga

Ernest Mimi sikuelewi mzee

Baba wa baba yangu alikasirika sana na kutaka kumpiga mwanae na ndipo ndugu na watu waliokuwepo katika kikao kile waliamua na kumwambia baba yako huyu.

Ernest hakuna laana kama baba mzee kama huyu na wewe ukiwa kama mwanae kutaka kupigana unataka kupigana na babayako mbona unajitafutia laana na huyu ni mzee anajua unachofanya na anapokuuliza anajua anachokifanya sawa. Muelewe baba yako na umjibu kile anacho kuuliza kwa usahihi zaidi na umuelewe. Ni baadhi ya ndugu zake waliojaribu kumuweka sawa.

Ugomvi ulipungua na tulikaa chini kuendelea na maongezi yaliyotupeleka kijijini pale.

Babu aliyasema haya:-

Babu kwa kuwa Ernest na mkewe hawaelewi walichokifanya basi naomba mjukuu wangu aeleze mbele yenu yale aliyofanyiwa na huyu mwanamke pamoja na baba yake ndipo mtakapoelewa sawa.

Nilipewa nafasi yakuanza kuyaeleza yale yote ambayo yalitendwa na mama wa kambo. Na ndipo nilip0anza kuelezea kwa uchungu na moyo uliugua zaidi kwani ninayotaka kuyaelezea yalishaniumiza na yataendelea kuniumiza zaidi pale nitakapo endelea kuyaongea zaidi nilianza mazungumzo na kusema kama iliyvokuwa na kuyasema yule yote waliyokuwa wakinitendea nilivyokuwa naishi nao. Ndipo watu waliokuwa kwenye kikao kile walipoanza kutia na kuanza kumgombeza baba na Yule mama na wengine walibaki kushangaa niliumia sana na nilibaki kulia zaidi kwani wahusika walikuwa karibu nami niliwachukia siutaka kuwaona katika machoyangu. Nilipomaliza maongezi hayo babu yangu aliendela hivi:-

Babu Nadhani mmeyasikia 

Waliopo Ndiyo baba ni makubwa na yakutisha.

Waliendela hivi.: yaani kaka yetu umeamua kumzalisha mwanao kwa sababu ya mwanamke? Mbona hauna uchungu wewe, kama ni ushetani kweli umeamua kuufanya kwani utajiri utakaa nao milele? Umetuaibisha ndugu zako kwa nini haukumtoa kafara huyo mtoto wa kwanza wa huyo mwanamke? Wauwaji nyinyi.

Walishambuliwa kwa maongezi hayo na wengine, walitamani kumpiga na shangazi yangu yule mwalimu ambae niliishi nae alilia kwa uchungu na kusema haya.

Shangazi Kama kumbe ulikuja kumchukuwa mtoto kwangu kwa kujua unachoenda kukifanya? Kweli umetuabisha ndugu zako.

Basi baada ya hayo babu aliamua hayana kuongea haya.

Babu Ernest ni kweli umefanya hayo.

Ernest Kimya

Babu Mwali hayo mtoto ambayo ameyasema ni ya kweli?

Mwali Kimya

Baadhi yawaliokuwepo walisema haya ebu jaribuni kuwa wawazi ili tujue tufanye nini? Lakin walizidi kuwa kimya hakuna aliyejibu chochote kati ya wazazi wale.

Basi babu aliamua haya:-

Tunapeana kiapo kama hayomambo mmemtendea mtoto kweli yawarudi wenyewe na kama ni wao basi yanirudi mimi.

Baba zangu wakubwa na shangazi zangu alisema ndiyo, fanya hivyo baba.

Lakini hata kabla ya kitendo ambacho baba wa baba yangu alichoamua kukifanya hata kabla hajakifanya baba yangu mzazi na huyu mama wa kambo walikimbia kwenye kikao kile ingawa watu waliokuwepo, upenyo wakuwakimbia. Walikimbia wote wawili na hawakuonekana tena na ndipo kikao kilipoisha. Babu yangu aliniambia haya.

Mjukuu wangu ingawa baba yako ameamua kujiingiza kwenye mambo ya ushetani lakini bado mimi niko pamoja nawe mjukuu wangu. Nitakuombea mjukuu wangu na utapona. Nikamwambia sawa babu. Kikao kiliisha bila kupata mafanikio yoyote na suluhu ya yale mambo yaliyotupeleka Moshi Marangu. 

Tulifunga kikao kwa maombi na babu yangu kutupa Baraka na ndipo tuliondoka na kabla hatujaondoka tukiwa kwenye kikao nilimwambia baba yangu mzazi, wewe si baba yangu. Baba yangu ni Mungu kwa hiyo mama yangu alipata mimba yangu kwa uwezo war oho mtakatifu kwa hiyo wewe si baba yangu. 

Niliongea hayo kutokana na baba yangu mzazi kunitamkia kuwa hajazaa na mama yangu kwa hiyo mimi nikae na mama yangu nimuulize baba yangu ni nani lakini yeye si baba yangu ndivyo alivyonitamkia na ndiyo sababu iliyonipelekea mimi kumwambia maneno kama hayo ingawa yaliwaliza shangazi zangu na waliokuwa kwenye kikao kile. Mama yangu mzazi alilia sana na kumsababishia kuongea maneno mengi na yakuumiza mkusanyiko wa watu waliokuwa katika mazungumzo yale. Tulimaliza mazungumzo na kuondoka kurudi. Arusha tulipokuwa tukiishi.

 Tulifika salama nyumbani na hali yangu kwa ujumla ilizidi kuwa mbaya zaidi. Maombi yaliendelea kwa watumishi wa Mungu mbalimbali. Sikumoja nikiwa nyumbani hatujui kinachoendelea tulipewa taharifa kuwa mama yangu mdogo amekamatwa na askari: mama yangu alifanya mpango na kuwasiliana na ndugu zake wengine na walifika nyumbani na kuelekea moja kwa moja hadi kituoni. Na walipofika mama yangu nae aliwekwa chini ya ulinzi na walimwambia haya.

Tumemkamata mdogo wako kwa kukutafuta wewe. Punde si punde baba alifika kituoni na alipofika alitoa maelezo na baadae mama yangu mdogo alitolewa. Kesi iliendelea katika kanisa la katoliki kwa father babu na ndipo ilipoishia. Mchungaji wangu kabese pamoja na waumini wote walifunga kwa ajili yangu na uku wakiendelea na maombi ya kufunga. Mungu wetu hana upendeleo umasikini kila aombae, Mungu aliyesikia maombi ya watu wake na hali yangu iliendelea kubadilika na kujikuta nakuwa katika ile hali yangu nya mwanzo, nilianza, kubadilika na kuwa tofauti zile hali zikiendelea, kupotea nilibadilika na kuwa mzima kabisa uku nikiendelea na maombi. 

Niliendelea vizuri kabisa na baada ya muda mama alichukua uwamuzi wa kunipekea kwa mjombas wake moshi ambae ni kaka wa bibi yangu mzaaa mama ambae mimi nitamwita babu. Mama alinieleza na nikamuelewa na hivyo nilianza kujiandaa kwa ajili ya safari ya kuelekea Moshi tena kwani ndiko nilipotokea mara ya kwanza. Nilijiandaa na muda ulifika na safari iliwadia ya kuelekea Moshi niliondoka na kwenda kwa babu nikiwa pamoja na mama yangu tulipokelewa na kuelezwa kuwa kuanzia muda ule mimi nitakuwa naishi pale na likizo nitakuwa naenda kumsalimia mama yangu. 

Ingawa iliniuma sana lakini sikuwa na jinsi kwani nilisha wazoea sana wazazi wangu hivyo maisha ya kurandaranda kwa watu tena siku ya penda kwani nimekuwa nikirandaranda mikononi mwa watu nimekuwas sina makao maalumu ya kuishi kwani nimeishi na mama yangu mzazi kwa miaka mitatu tu. Na ndipo nilipoondoka na kuelekwa Moshi tena.



Maisha yalikuwa hivi baada ya kufariki bibi yangu, ambae ni mama wa mama yangu. 

- Baada ya kufariki bibi yangu niliendela kuishi na kaka yake ambae nitamwita babu. Na baadae:-

- Nilipoondoka kwa babu nikiwa natarajia kwenda kuishi na baba nilienda kuishi na shangazi yangu ambae ni dada wa baba yangu na niliishi nae kwa miaka mitano na miezi minne ambapo nilipata likizo ya mwezi wa 4 na kuelekea Arusha kwa baba. 



Na baada ya hapo:-

- Nilikaa kwa baba miezi mitatu tu nandipo nilipofanyiwa vitendo vya kikatili kama hivyo na ndipo nilipoamua kuondoka na kuelekea kwa mama yangu mzazi. Kwa mama napo palikuwa hivi:

- Niliishi na mama tangu miezi kadhaa nikiwa darasa la sita na kuanza mwaka mpya nikiwa darasa la saba ambpo ndipo nilipoanza kuhesasbu maisha niliyoishi na mama yangu ambayo ni miaka mitatu na miezi kadhaa ile ya darasa la sita ambayo ndiyo nilivyoanza kuishi na mama yangu huyu. Nampenda sana mama yangu Ruth Mwakalinga kwa kuyajali maisha yangu.



Na nikiwa na ishi na mama yangu ilikuwa hivi:

- Niliishi na mama yangu na baadae nilienda kuishi na mdogo wake Judith na baada ya kutoka kwake nilirejea kwa mama na baada ya muda niliendelea kuishi kwa shangazi ya ngu, Yuster na baadae nilirudi tena nyumbani na ndipo mama alichukuwa uwamuzi wakunipeleka tena Moshi kule nilipokuwa nikiishi mara ya kwanza na bibi yangu ambapo nilikuwa nakaa bibi yangu ambae ni mama wa mama yangu.

Hivyo sikuwahi kuishi maisha ya utulivu na yenye amani leo huku kesho huku na ndipo sasa nimerejea kule nilipotoka kwa mara ya kwanza na kuanza makao tena. Nao pia maisha yaliendelea kuwa kama ifuatavyo.

Nilifika moshi salama nikiwa nimeongozwa na mama yangu na alinikabidhi kwa mjomba wake nae akaondoka nakumbuka ilikuwa mwaka 2008. Niliendelea kuishi na babu yangu huku mjomba ambae ni mtoto wa babu yangu akiendelea kunitafutia shule wakiwa wanasaidiana na mama yangu mzazi.

Baada ya muda mama yangu aliekea katika shule ya Secondary, Kisarikas Secondary alipofika alikutana na mkuu wa shule na katika maongeziyao ilikuwa hivi. Baada ya kupeana salamu.

Mama Mwalimu nimetafuta nafasi kwa ajili ya mtoto wangu lakini nimekosa.

Mwalimu Umeeda wapi na wapi mama?

Mama Nimeenda Uru Secondary lakini nimekosa nafasi, na pia ile ni privet hivyo mkuu wa hiyo shule ameniambia kama nikumpeleka katika shule yake aanze form 1.

Nakumbuka mama alivyoniambia habari ya kurudia form 1 nilikataa kwani nilishafika kidato cha pili na nimesoma kwa mateso makali hivyo sikuwa na budi kukataa kurudia shule.

Waliendelea 

Mwalimu Sasa nikusaidieje mama?

Mama Naomba unisaidia mwalimu 

Mwalimu Niwakidato cha ngapi?

Mama Cha pili mwalimu naomba msaada nafasi za kidato cha pili zimejaa mama sijui nifanye nini ili niweze kukusaidia mama lakini ukweli nafasi zimejaa.

Walimalizana na mwalimu na baadae mama aliondoka Mama aliendelea kuangaika huku na huko kuendelea kutafuta nafasi?



Alifanikiwa tena katika shule ya Sekondari Mawela Secondary nako pia ilikuwa hivi:-

Baada ya salamu na maojiano.

Mama Mwalimu natafuta nafasi ya mwanafunzi wakidato cha pili. Naomba unisaidie.

Mwalimu Ametokea wapi?

Mama Ametokea Arusha.

Mwalimu Kwani mama umeshatafuta nafasi katika shule nyingine?

Mama Hapana 

Mwalimu Na ni kwa nini umuamishe mtoto kutoka Arusha umlete Moshi?

Mama Kuna matatizo mwalimu.

Mama alijaribu kumueleza historia yangu kwa ufupi na akamwambia mwalimu kutokana na hayo ndiyo maana nimeamua kumwamisha mtoto. Mwalimu naomba msaada wako wa hali na mali sina msaada mwingine naomba unisaidie mwalimu.

Mwalimu mkuu aliongea haya Mama kwanini mwanao awe na matatizo makubwa kama hayo. Na hapa hamna nafasi Mama aliendelea kumwambia nisaidie mwalimu kwani mtoto wangu ni wako pia.

Mwalimu alijibu:-

Siwezi kupokea mwanafunzi mwenye matatizo na inawezekana mwanao ameondolewa huko shuleni Arusha kwa sababu ya uhuni. Inawezekana alikuwa anatoa mimba alafu unasema eti ana matatizo. Hamna nafasi mama. 

Mama aliumizwa sana na maneno makali na yakuzalilishwa aliyo yatoa mwalimu mkuu wa shule ya Mawela Secondary iliyopo Moshi maeneo ya KCMC kwa jina la mkuu huyo ni GOSADI. 

Mama alifika nyumbani kwa mjomba ake akiwa na huzuni na machozi pia. Nilimpokea na kumpa pole na ndipo alipoanza kunielezea yaliyomkuta huko.

Nililia sana kwani nimezalilishwa na kupewa sifa chafu tena na mwalimu niliendelea kujiona sina maana katika dunia hii nilitamani kufa killa nilipojaribu kuyawaza maisha ninayopitia nitazidi kukosa amani zaidi raha ya maisha siku hiyo na tena niliendelea kujiona binti mwenye mikosi kila kukicha nilijiona si kustahili kuendelea kuishi tena duniani.

 Namshukuru sana mama yangu mpenzi Ruth Mwakalinga kwa kuendelea kunijenga kiimani na kunitia moyo pale mabaya yalipozidi kunilemea. Nakupenda sana mama. Niliendelea kuishi kwa kuyawaza maneno ya Yule mwalimu na yalizidi kuniweka katika hali ya ugonjwa kila nilipowaza niliumia kwani hata mwanaume siku wahi kumjua na wala matendo machafu kama, hayo siku wahi kuyafanya. 

Mama hakukata tamaa aliendelea kutafuta nafasi ya shule tena. Na ndipo alipofanikiwa kupata nafasi katika shule ya Sekondari Mangi Sabas Secondary na alipoonana na mkuu wa shule ambae ni Deodath yalikuwa haya. 

Mama alianza kwa kumpa history ya maisha halisi niliyoishi na hadi kufikia uwamuzi wakuniamisha shule katika mkoa wa Arusha. 

INAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post