Ilipoishia...
alimjibu haya Emmy sijakupenda kwa sababu eti mzuri au nikuaribu au kukuchezea hapana nimekupenda kama ulivyo na nimekupenda pamoja na hayo matatizo uliyonayo. Naomba unielewe na baada ya hapo tuliachana na pale pale ndipo hali ya urafiki ilianza.
SONGA NAYO...
Nilimueleza mjomba kuhusu ilo na pia sikuweza kumficha mama yangu niliwaweka wazi kuhusu hilo na nyumbani wakawa wameshamjua na ndivyo nilipenda kwani, sikupenda iwe siri hata kidogo kwani yule ni mwanaume mimi ni msichana na tena bado ni mwanafunzi na nilifanya hivyo kuepuka kama kunatatizo lolote litajitokeza kwangu. Basi tuliendelea na kwao walinifahamu.
Siku ziliendelea kwenda na hatimaye siku za kufanya mtihani wa kidato cha pili ulitimia. Nikiwa najiandaa na mtihani hali yangu ilibadilika tena na kuwa mbaya zaidi nilianza tena kutoka damu puani na kutapika na hali hiyo ilipoanza kuwa nazimia hali yangu ilikuwa mbaya nilianza tena kuangaika na bibi yangu alianza tena kuniambia unaona sasa utafanyaje na mtihani ndiyo huo umekaribia? Twende nikupeleke kule niliko kwambia.
Nilimwambia bibi sintaenda sehemu yoyote ile na zaidi endapo nikwa mganga. Aliwaambia baadhi ya watu kuhusu ilo ili waje kunishauri na mmoja wao alikuwa ni mama wa Deodath ambae ni rafiki yangu. Alikuja nyumbani na kuniambia kuhusu wataalamu wa kienyeji lakini nilikataa. Nanilizidi kukataa kwa kila ambae aliniambia mambo kama hayo.
Na nilimchukia kila ambaye alinishauri kwenda kwa waganga wa kienyeji siku ya mtihani ilifika hali yangu ikiwa bado ni mbaya nilienda shule nikiwa katika hali ile ile na nilipofika shule hali ilikuwa mbaya zaidi lakini waalimu walinisaidia na baadae niliingia darasani na kuanza mtihani na wenzangu hali ilibadilika tena na kuanza kutoka nje.
Nilifanya mtihani ule kwa mateso makali na uku nikiendelea kuombewa na mama mmoja aliyekuwa amejenga karibu na shuleni kwetu kwa jina la mama Kimambo. Niliombewa na mama huyo lakini bado hali iliendelea kuwa ile ile. Hivyo hali hiyo iliendelea hadi nilipomaliza kufanya mtihani wa kidato cha pili. Hali ya nyumbani ilikuwa mbaya kwani nilichukiwa baada ya kukataa kwenda kule walikotoka kunipeleka na hali ile ilifanya hadi waanze kuniambia walokole ni waongo unajifanya umeokoka na wakati hao hao ndio waliokuloga.
Niliendelea kuumia na kulia na nilianza kumchukia sana bibi yangu kwani ndiye aliyeanza kunisema sema vibaya na katika kijiji nilichokuwa naishi hakuna ambae hakufahamu na kujua hali halisi niliyokuwa nayo. Walinisema vibaya wengine walisema ni babu ninayeishi nae ni mchawi wengine walisema ni mama yangu mzazi kila aliyeweza kusema aliloweza alisema niliendelea kufarijiwa na rafiki yangu ambae ni Deodath alinitia moyo na alikuwa karibu nami kila nilipokuwa mgonjwa.
Tulifunga shule na niliondoka na kwenda Arusha kwa mama yangu mzazi Ruth Mwakalinga nilikaa hadi likizo ilipoisha: baada ya likizo kupita nilirudi Moshi kwa babu ili kwenda kuendelea na masomo. Tulifungua shule na kuingia kidato cha tatu.
Hali ilianza tena kuwa mbaya nilipoenda shule. Na siku moja hali ilibadilika tena darasani na kuwa mbaya zaidi na baadae waalimu waliamua kunipeleka hospitalini. Walinipeleka hospitali ya rufaa ya KCMC na nilipofika nilikuwa katika hali mbaya nilikuwa nimezimia na nilipozinduka nilijikuta katika wodi ile ile ambayo nimekuwa nikilazwa mara zote ICU.
Nilikuwa pale kwa muda wa wiki tatu hali ilikuwa mbaya zaidi kwani nilianza kupoa tena mwili ulianza kuwa wa baridi na baada ya muda madaktari walinipeleka kwenye vipimo na kumezeshwa mpira wa vipimo na baadae waliniambia navidonda vya tumbo lakini havina uwezo wa kutoa damu lakini damu niliyokuwa nikitapika ni nyingi mno.
Nilirudishwa wodini na kuingiziwa mirija puani ambayo ilielekea moja kwa moja hadi tumboni na madaktari walinishauri kutoitoa mirija hiyo kwani wameniwekea ili kuvuta ile damu ili yopo tumboni kweli nilipata maumivu makali mno na pale nilipojaribu kumeza mate nilipata maumivu makali mno.
Nilipoteza fahamu baada ya muda mfupi baada ya kuwekewa mirija ile na nilipopata fahamu nilikuta nimewekewa oksijeni na taa mbili ambapo taa moja ilikuwa kichwani na nyingine miguuni nilijisikia vibaya sana kwani mwili ulikuwa na baridi kali na mirija ilinifanya kuzidi kujisikia vibaya zaidi pale nilipotaka kumeza mate.
Hali iliendelea kuwa hivyo na baada ya wiki tatu nilirudi nyumbani nakuendelea na mauguzi . nilichoka nilitamani hata kunywa sumu na haswa nilipomwangalia mama yangu kwani nilimwonea huruma na alikuwa akilia kila alipokuwa akiniangalia hali hiyo ilinifanya niwe katika hali mbaya zaidi.
Mama aliendelea kunifanyia maombi na ndugu zangu pia waliendelea na maombi pia. Baadae hali ilibadilika na kuwa nzuri mama alikuwa amekuja Moshi kwa ajili ya kuniuguza aliondoka na kurudi Arusha. Nilianza tena kwenda shule na
niliendelea vizuri na kila nilipokuwa nikiwaangalia wenzangu niliumia kwani wao wanasoma kwa raha kwa amani lakini mimi tu ndivyo hivyo hali yangu si kama za wenzangu. Na pia sikuwa nafanya chochote kile shuleni zaidi ya kusoma na muda wa kutoka shule ufike niende nyumbani. Siku wahi hata kufagia siku wahi hata kuchapwa na hali ile iliwafanya baadhi ya wanafunzi kujisikia vibaya.
Kwani pale walipo kuwa wakiadhibiwa walitamani na mimi ni hadhibiwe lakini kwa wengi wao zaidi walinionea huruma na kulia pale walipoona ile hali walinihurumia na kunisadia.
Nilipendwa sana na wanafunzi wenzangu na hali hile ilinifanya kujisikia kuwa napendwa ingawa ndugu zangu hawakunipenda na nilifarijika sana pale nilipokuwa na wanafunzi wenzangu kwani walinibadilisha mawazo na kuniweka sawa.
Walinitia moyo na kuwa karibu nami zaidi kuliko wanandugu zangu na waalimu pia walinijali na kunipenda zaidi. Nasema ndugu zangu hawanipendi na sitaogopa kusema kuwa hawakunipenda kwani nilipokuwa naugua siku muona hata mmoja ingawa ndugu zangu hao wanauwezo na wanaweza kunisaidia na kunipa chochote kile nilichoitaji lakini siku waona na nili umia sana kwani kwa baba yangu mzazi Ernest Martin Tairo wako kumi, wasichana watano na wanaume watano lakini hakuna ambae alikuja kuniangalia zaidi nitamshukuru shangazi yangu mmoja ambae ni Yuster Martin Tairo ambae ni mdogo wa baba yangu Ernest ambae shangazi huyo nilipokuwa Arusha alinifuatilia na kujua hali yangu na nilipoamia Moshi aliendelea kunifuatilia kwa njia ya kuniulizia kwenye simu.
Niliishi kwa kujiona sina ndugu, zaidi ya ndugu wa mama yangu Ruth Mwakalinga ambao wako karibu na mimi hadi leo. Nampenda sana mama yangu pamoja na baba yangu mlezi, Stephen Ngome pamoja na wadogo zangu ambao ni watoto wa babu mlezi.
Basi niliendelea kwenda shule na baada ya muda nilianza tena kutokuwa na ile hali lakini waalimu hawakunipeleka tena hospitali nilikuwa nikirudishwa nyumbani na nilipokuwa ni kirudi na kufika nyumbani huwa nakuwa mzima kabisa lakini nikienda shule hali iliendelea kuwa mbaya. Mkuu wa shule ya Sekondari Mangi Saba ambae ni Deodath aliamua kunipalikizo ya kukaa nyumbani hadi hali yangu itakapokuwa sawa. Nilikuwa nyumbani kwa kuwa hali ile ilifanya kutowafanya wanafunzi wenzangu kutokusoma kwa amani na kila ile hali iliponianza ilinilazimu kunitoa nje na kuwafanya kupitwa na masomo.
Na pia wanafunzi hao walileta vurugu pale ambapo waalimu walipokataa kunipeleka hospitali kila hali pale ilipobadilika na waalimu walisita kuendelea kunipeleka hospitali kwa kuwa hakuna kilicho kuwa kinaonekana zaidi ya kuendelea kuongezewa maumivu zaidi, kwani nilipokuwa nikifika hospitalini nilitundikiwa dripu na kuchomwa sindano, hali ambayo ilizidi kuwa umiza wazazi na waalimu wangu pamoja na wanafunzi mwenzangu.
****
Siku moja nikiwa nyumbani nilitembelewa na marafiki zangu na walilia zaidi kwani hali yangu ikiwa ni mbaya mmoja wa wanafunzi alijitolea kuniombea kila siku na alifunga na kuomba kwa ajili yangu. Blandina dada mkuu wa shule ya Sekondari Mangi Sabas ambae ni Renalda aliendelea kutoa ripoti ya hali yangu kwa wanafunzi wenzangu na kila kukicha niliwaona wanafunzi wenzangu nyumbani. Walikuwa wakija na kuniombea na kulia zaidi pale walipokuwa wakiniangalia kuiyona ile hali nilivyokuwa nayo. Waliniaga na baadae waliondoka na baada ya kuondoka nilianza kujiona mpweke.
Sikujali baada ya mda mfupi mvua ilianza, kunyesha. Nilikaa barazani nikiwa na babu yangu na baada ya muda mfupi alikuja mchumba wangu Deodath na nilianza kumuona ni rafiki wa kweli kwani kila nilipo pata matatizo nilimuona karibu na hali hiyo ilinifanya kuondoa neno la urafiki kinywa ni mwangu na kumuona yeye ni mchumba kwangu.
Tulimkaribisha vizuri na mazungumzo yaliendelea baada ya muda mfupi babu yangu aliamka na kuondoka na kuniacha nikiwa na Deodath. Tulianza mazungumzo na yalikuwa hivi:-
Emmy Vipi mbona umekuja na mvua?
Deodath Kwani kunatatizo gani?
Emmy Ungesubiri mvua ipite ndiyo uje.
Deodath Emmy ngoja ni kwambie, mahali penye tatizo ni lazima upaangalie kwa moyo mmoja kwani ingekuwa ni sherehe nisinge kwenda?
Emmy Ndiyo ungeenda lakini ungesubiri hii ni mvua.
Deodath Tuachane na hayo unaendeleaje?
Emmy Kama unavyo niona, namshukuru Mungu Deodath.
Deodath Jitahidi kufuata unayo shauriwa na madaktari pia.
Emmy Sawa.
Baada ya hapo nilianza kumfikiria akilini na kumuona ni kijana mwenye busara na anayemjali mtu katika hali zote kwani ninapokuwa mgonjwa namwona na ninapokuwa mzima na muona pia na kwahali ile ilinifanya kumuona ni wa muhimu sana na nilisha anza kumzoea pia kwa ajili ya ule ukaribu wake. Muda uliwaacha na alitaka kuondoka lakini nilimbana na kumwambia bado na mazungumzo na wewe na nilifanya hivyo kwa kuwa nilikuwa nataka kujua, kitu kwa kumuoji maswali na kumpima zaidi na kuendelea kumchunguza kwani vijana wa sasa wengi wao ni waongo huja kwa kila aina ya unyenyekevu lakini inakuwa sivyo. Nilijaribu kumwambia naomba hatanikuwekee chai ingawa mara ya kwanza unekataa, lakini alinijibu hapana Emmy nimesha kunywa.
Nilianza kumuoji kwa namna hii:
Emmy Deodath kwa nini siku ya jumapili ya tarehe 5/2/2008 uliniona na ilikuwa ni
siku ya kwanza na ulinitamkia unanipenda
Deodath Emmy siyo siku moja nilikuona
Emmy Uliniona lini tena?
Deodath Tangu nilipotoka Dar es Salaam
Emmy Dar es Salaam?
Deodath Ndiyo
Emmy Kwani ulikuwa unakaa Dar
Deodath Ndiyo Emmy, nimetokea Dar.
Emmy Sasa kwania umetoka Dar una muda?
Deodath Yapata mwezi na wiki kadhaa sasa.
Emmy Sasa ni nini kimekuleta Moshi?
Alianza kwa mazungumzo haya:-
Emmy siyo kwamba nimependa kuja Moshi kuna mambo ambayo hayako sawa na ndiyo sababu kubwa ya mimi kuwepo Moshi. Nilimuuliza mambo gani? Aliniambia ni Mungu tu kwani ungekuta nimekufa. Nikamwambia ungekufa? Akajibu ndiyo. Nikamwambia kwa nini?
Alianza na kuniambia haya:-
Nilipata matatizo makubwa sana kwani nilikuwa nafanya kazi Dar es Salaam lakini ilinibidi niache. Nilimkalisha mazungumzo kidogo na kumuuliza ulikuwa unafanya kazi gani? Akamwambia yeye nifundi magari na katika ufundi huo ndiyo matatizo yalipo anza aliendelea kwa kusema haya:-
Nilikuwa nikifanya kazi katika gereji moja ambayo inajulikana kwa jina la MAKI GEREJI. Baada ya muda nilichukua uwamuzi wa kwenda kujiendeleza kimasomo ambapo nilienda chuo cha VETA CHANG’OMBE na nilitumia muda wangu vizuri. Kwani asubuhi na mapema niliingia kazini na ilipofika saa 2:30 mchana nilitoka kazini na kurudi nyumbani ambapo nilikuwa nimepangisha na nilipofika nilikuwa Napata maji na baada ya hapo napumzika kidogo na ikifika saa 3:15 naanza safari kuelekea chuoni ambapo tuliingia darasani 4:00 mchana. Nilijaribu kumwambia sasa kama ni hivyo unakula saa ngapi? Alinijibu muda wa kula kiukweli mara nyingi huwa mdogo mara nyingi naenda chuoni hata sijala. Lakini kama muda unatosha nikitoka kazini naenda kula kwenye vioteli vyetu hivi vidogo vidogo alafu naenda kujiandaa.
Nilimuuliza vioteli vidogo vidogo ndiyo vipi?
Alijibu kwa mama ntilie. Na baada ya hayo tu niliendelea hivi. Baada ya muda kama wa miaka 8 mambo yalianza kubadilika na kuwa mabaya kwa upande wangu nikamwambia yalikuwaje? Nilkuwa nikiingia chooni huwa nadondoka na hiyo ilitokea kila nilipoingia chooni.
Nikamwambia nikila choo au nikwa hapo ulipokuwa unaishi tu? Aliendelea hivi: kiukweli ni kwa hapo nilipokuwa nikiishi tu na hali hiyo ilizidi kuendelea na kukosa amani sana na pia hali ile ilinitisha na kuniweka katika wakati mgumu sana na kunifanya kujiuliza maswali yasiyo kuwa na majibu na hali hiyo ilinipelekea na kujikuta sikumoja Napata majeraha makali katika mwili wangu na sehemu za mwilini kama vile kichwani: baada ya hapo alinionyesha kovu lililopo kichwani mwake.
Na baadae ilinibidi niondoke na kurudi nyumbani Moshi ambapo wazazi wangu walikuwa wakiishi na hata nilipotoka Dar es Salaam siku muaga mtu hata mmoja zaidi ya kijana niliyekuwa naishi nae na kumfanya kama mdogo wangu na ndugu yangu kwa jina la MAX kwa jina lingine lililofahamika kwa jina la Judika Kitomari:
Nilipofika Moshi niliwaelezea wazazi wangu, hali halisi niliyokuwa nikiishi nayo Dar es Salaam na baada ya kuwaelezea walinikataza kurudi tena Daa.
Siku ziliendelea kusonga mbele na ndipo siku moja nikiwa nimekaa dukani kwangu nilikuona ukipita ingawa sikujua unaelekwa wapi lakini niliwauliza baadhi ya vijina wenzangu huyo binti anaishi wapi na nilipoambiwa unapoishi na ni mjukuu wa Hendry ambae anafuhamika sana kijijini kwetu ndipo hapo nilipoanza kukufuatilia kwa ukaribu zaidi na pia nilifurahi kwani mjomba wako ambae ni Paul Yule uliyekuja nae pale dukani ni rafiki yangu na nilikuwa na ukaribu nae zaidi na baada ya muda tuliachana na mimi kuelekea Dar.
Na ndiyo hapo safari yangu ya kukufuatilia ilianza na hadi kufanikiwa kuonana na wewe ingawa vijana wengi waliniambia wewe hauongei na vijana ovyo na hiyo yote inatokana na wao kukutongoza tangu ulipokuja Moshi kimasomo na kuona haueleweki.
Kwa lugha nyingine unawakataa na kuwatukana pia kwa kupitia hayo waliniambia hautamuweza huyo msichana kwani huwa hapendi mazoea na vijana. Nilimwambia ni kweli ndivyo nilivyo lakini kwako sijui nini kimetokea na kukubali mi mwenyewe nashangaa.
Baada ya hayo nikamwambia kwa hiyo lile duka ni la kwako? Alinijibu ndiyo nila kwangu lakini nilipolifungua nilimuweka mtu maalum nimerudi nitaendelea peke yangu kuliuza. Binafsi nilifurahi kupata mtu aliyepitia majaribu na hapo ndipo nilijua kuwa yeye ndiye rafiki na mchumba bora kwangu kwani anayajua majaribu na ndiyo maana anaikubali hali yangu na kuwa mfariji wa karibu sana kwangu baada ya hapo aliniaga kwa lengo la kutaka kuondoka nilimwita babu aliagana nae na kuondoka urafiki uliendelea kuwa mkubwa na wakusaidia.
Siku ziliendelea kwenda na baada ya muda niliendelea kwenda shule kama kawaida na hali yangu ilikuwa sawa kabisa niliendelea na kuwa na amani kwani sikupata matatizo tena kwa muda mrefu hivyo kupelekea kuanza kusahau ile hali taratibu.
Lakini siku moja nikiwa naenda shule nikiwa njiani kichwa kilianza kuniuma ghafla na baadae nilipata kizunguzungu baada ya muda mfupi nikaanza kutapika damu na nyingine zilitoka puani na sikuwa na msaada wowote kwani nilikuwa peke yangu. Niliondoka na kila kilichoendelea siku kifahamu nilipata fahamu na nilipoamka nilijikuta hospitalini KCMC wodi ile ile ICU nikiwa nimewekewa oksjeni na mirija kama wanavyo niwekeaga.
Nilijaribu kuwauliza manesi kuhusu hali ya mimi kuwa pale alianza kwa kuniambia kuna wasamaria wamekuleta na tulipowahoji walisema wamekuta umedondoka barabarani ukiwa unaelekea shuleni na hivyo wakakunyanyua na kukuleta kwani ulikuwa unatoka damu nyingi puani na mdomoni lakini walipitia shuleni kwako na kuwaeleza waalimu wako na wengine walikuja kutokana na wewe kuchelewa kuzinduka imebidi warudi shuleni lakini watarudi baadae sawa. Niliridhika na kuendelea kupumzika.
Baada ya mida ya saa 2:00 mchana alikuja mkuu wa shule Deodath Mushi alifika hospitalini aliniambia:-
Mwalimu Hujambo Emiliana
Emmy Sijambo mwalimu
Mwalimu Unaendeleaje.
Emmy Mwalimu najisikia nimechoka sana.
Mwalimu Utapona endelea kumwomba Mungu sawa.
Emmy Sawa mwalimu asante.
Mwalimu aliniaga na kuondoka, lakini kabla hajaondoka aliniagizia chakula na maji na kuniambia wanafunzi wenzako wakitoka shule watakuja kukuona. Baada ya hayo aliondoka. Nilimshukuru Mungu kwa upendo ambao niliuwona kwa waalimu wangu pamoja na wanafunzi pia. Haikuishia hapo. Muda wa wanafunzi wa kutoka shule ulifika na kweli walikuja kunisalimia walilia waliponiangalia hali ambayo ilinipelekea mimi kujisikia vibaya na kuanza kulia pia.
Walinibembeleza lakini ndani nilizidi kuumia zaidi nilizidi kuwaangalia kwa uchungu na nilitamani sana muda ule ule nipone. Waliniahidi kuendelea kuniombea ili nipone na kuweza kuendelea na masomo kama kawaida niliwashukuru sana na nilifurahi kwa ujio wa wanafunzi wale. Ingawa nilipata uchungu ndani yangu lakini sikufa moyo niliridhika kwa ujio wao na kuweza kunitia moyo.
Baada ya muda mfupi waliniaga na kuomba manesi ruhusa ya kuniombea. Walikubaliwa wakafanya maombi na walipo maliza waliniaga na wakaondoka. Nilianza kujisikia mpweke walipoondoka nilianza kujiuliza maswali ambayo hayakuwa na wakumjibu zaidi yangu mi mwenyewe. Nilihisi ni mimi tu mwenye mikosi duniani na niliona hakuna wazazi ambao wanaweza kufanya kitendo ambacho baba yangu alinifanyia.
Niliendelea kuivuta sura yake machoni mwangu nilianza kumchukia zaidi ingawa watumishi wengi wanao niombea na mabo walishawahi kuniombea waliniambia ni msamehe ni baba yangu ili niweze kupokea uponyaji. Lakini msamaha kwangu ulikuwa mgumu nilizidi kuendelea kumuona ni mbaya zaidi kutokana na hali yangu kwa ujumla.
Na ambacho kilinifanya nisimsahau baba ni kutokana na ndugu zake pia kuwa kimya kwangu kwa maana nyingine niliona fika kuwa hawanipendi na hata kama hawanipendi basi wangenisaidia hata kutetea ile hali yangu. Niliumia sana na sikuwa na njia ya kufanya nilitamani mauti inifike kwani hata thamani yangu siku io na niliona kama mzigo kwa watu nilijiona mimi ni mtu wakuharibu fedha za watu kwani kila nilipoumwa nilipelekwa hospitalini hali ambayo niliona watu wanapoteza fedha kwa ajili yangu na ugonjwa nao nisumbua haujulikani.
Baaada ya muda daktari alikuja katika kitanda nilichokuwa nimelala na kuniambia Emiliana nisikilize kwa makini na uyaelewe haya nitakayo kwambia na ukiyazingatia hautakuwa wa kulazwa kila siku na huu ugonjwa hautakuwa unakusumbua tena mara kwa mara.
Ugonjwa hautakuwa unakusumbua tena mara kwa mara. Nilimwambia dokta kwani kuna nini maana hata mimi mwenyewe nashindwa kujielewa na hii hali alianza kwa kuniambia haya:
Dokta Emiliana naomba ni kuulize maswali kidogo
Emmy Sawa dokta mi niko tayari
Dokta Emiliana unaishi na nani?
Emmy Naishi na babu na bibi
Dokta Kwani wazazi wako wanaishi wapi?
Emmy Wanaishi Arusha.
Dokta Kwa nini usiishi nao?
Emmy Dokta nimekuja Moshi kimasomo nikimaliza nitaenda kwa wazazi wangu.
Dokta Kwa nini usiendelee na masomo yako ukiwa unaishi na wazazi wako?
Emmy Mm mm,mm.
Nilishindwa kumjibu kwanza uchungu uliniingia ni kaanza kulia kwa kuyawaza yale ambayo yalishatokea na niambayo baba yangu aliyatenda alafu dokta nae anasema kuishi na wazazi, niliona ananichanganya. Aliniambia tuachane na hayo sasa nisikilize vizuri na uyazingatie nitakayo kwambia. Hapo ulipo una presha na presha hiyo ni mbaya kwako, kwani niyakushuka na ndiyo maana unaanguka na kuzimia.
Hali ambayo kwa wewe na udogo ulionao ni mbaya sana nakwambia ni mbaya kwa sababu hata kwa mtu mzima ni mbaya sasa wewe bado ni binti mdogo taifa bado linakuitaji ebu jitaidi kupunguza mambo unayo yawaza kwani utakufa ukiwa bado ni mdogo.
Nilimwambia dokta mbona hakuna ninachowaza? Alinijibu hali kama hii haiwezi kutokea tu, lazima kuna tatizo. Sasa nakushauri kupunguza hayo mawazo uliyonayo na ikiwezekana uishi na wazazi wako pia itasaidia. Sawa nilimjibu sawa dokta nimekuelewa.
Kingine una vidonda vya tumbo lakini na hivyo pia vinachangia pia kuwa na mawazo na kushinda na njaa kwa muda mrefu. Sasa jitahidi kwa haya nitakayo kwambia na uyazingatie sawa.
Alianza
i. Punguza mawazo unayo yawaza
ii. Punguza kula vyakula vyenye mafuta mengi
iii. Punguza kula vyakula vyenye nyanya
iv. Punguza hasira mtu anapokukwaza ebu jaribu kumsamehe na kusahau.
Tags:
RIWAYA