Zingatia sana:-
i. Kula matunda
ii. Kunywa maji mengi
iii. Kunywa chai ya kahawa
iv. Pata muda wa mapumziko zaidi
v. Kunywa maziwa fresh hata mara tatu kwa siku
vi. Epuka sana kukaa na njaa n.k
Zingatia hayo machache na ukiyafuata kama ilivyo, na kwambia baadhi ya matatizo yatapungua kwako na utakuwa kama wengine sawa. Pia usisahau kumuomba Mungu pia sawa. Nilijibu sawa daktari nitajitaidi.
***
Niliruhusiwa kwenda nyumbani kuendelea na dawa zile zile walizonipa mara ya kwanza. Dawa za vidonda vya tumbo. Nikiwa nyumbani niliendelea kujihoji maswali zaidi sasa Mungu mimi natatizo gani? Kama ni vipimo mbona havieleweki? Na kama ni damu mbona natapika tu. Lakini nikifanyiwa vipimo naambiwa damu imepungua, lakini wakitaka kuniongezea damu naambiwa damu imezidi sana mwilini mbona sielewi mimi. Mungu kama mimi niwakufa sinife tu kuliko yote haya.
Yaani hata mimi sasa nimechoka na hali hii na pia najiogopa mwenyewe maana hata mimi hii hali inanitisha niliendelea kujioji haya maswali na huku nikimuuliza Mungu. Vile vile niliongea peke yangu kwa kumwona Mungu kama vile nikonae ana kwa ana niliuliza:
Hivi Mungu mimi unioni au? Na ninavyokuomba unamaana unisikii au? Na hao ambao unawaponya alafu mimi unaniacha unakuwa na maana gani. Eeee kama mimi niwakufa niuwe sasa mbona unaniacha tu nateseka na magonjwa ambayo hayaonekani zaidi ya kunitesa tu eeee. Nilijiona kama vile nakuwa kichaa kwani kwa wakati mwingi niliongea peke yangu na nilika mahali hata kanisani sitaki tena kwani naona kama huyo Mungu ninayemuomba hayupo.
Baada ya muda kidogo nikamwambia Mungu nisamehe bure maana hii hali ni mwenyewe imenichosha na ndio inayonisababishia kuongea maneno ya ajabu. Nisamehe Mungu wangu siku ziliendelea kwenda maswali hayakuisha akilini mwangu. Shule mwalimu aliniambia ni pumzike hadi nitakapo kuwa sawa, hali ambayo bado ilinichanganya kwani hata maendeleo yangu ya kielimu yalikuwa ni mabaya, sana na hayaridhishi hata kidogo. Sasa ninapoendelea kukaa, nyumbani ndiyo nazidi kuwa mjinga kabisa.
Muda uliendelea kwenda nikaanza kwenda shule hali yangu ikaanza kuwa nzuri na hali yangu ikaanza kuridhisha. Niliendelea kwenda kama kawaida nilimshukuru Mungu kwani niliendelea vizuri hadi ule mwaka ukaisha.
Mungu alisaidia. Lakini nilipewa taarifa kuwa babu yangu amefariki babu mzaa mama ambae aliyatetea maisha yangu kwa kadri alivyoweza kwa kunipa dawa za majani aliyoyajua na kuhakikisha naishi na kuyazingatia masharti niliyokuwa nikipewa na madaktari niliugua, sana lakini sikuwa na jinsi nilienda kwenye msiba na nilifanikiwa kuuwona mwili wake na baadae walimpeleka Mbeya kwa ajili ya maziko lakini mimi siku bahatika kwenda.
Kifo chake kiliendelea kuwa jeraha kwangu kwani nilikumbuka mengi mema aliyoyatenda kwangu nilikumbuka ile siku ambayo nilikuwa nimelazwa Mount Meru hali yangu ikiwa mbaya zaidi, alikwenda kuongea na mtumishi wa Mungu Mwakasege kwa ajili ya maombi. Nilikumbuka mengi na niliumia sana. Mungu amlaze mahali pema. Ameni.
Mwaka ulikatika na kuingia kidato cha 4 nilianza vizuri na nilisoma kwa amani kabisa bila matatizo yoyote yale. Baada ya muda mfupi sana mama yangu alinipigia simu na kuniambia kuwa babu yangu amefariki nilihisi kuchanganyikiwa kwani ni muda mfupi sana tangu, kufariki kwa babu yangu mzaa mama alafu tena, naambiwa babu yako mzaa baba amefariki ambae ni baba wa baba yangu mzazi Ernest ambae alifanya ule uchafu wake kwa ajili yangu.
Roho na moyo viliugua kwa kuwa na alikuwa sana upande wangu na hakusita kumchukia mwanae kwa kitendo cha kikatili alichonifanyia. Na nilikumbuka alivyoyatetea maisha yangu pia.
Nilikumbuka siku ya kikao alivyotaka kutulambisha damu ya kiapo kwa kusema, tunalamba damu ya kiapo kama Ernest utakuwa umemfanyia mjukuu wangu ubaya yatakurudia.
Lakini hata kabla ya kutoa kiapo, kile baba yangu Ernest na mkewe Matlida walikimbia katika kusanyiko lile. Hakika babu yangu alinipigania kwa kadri ya uwezo wake. Daima nitamkumbuka, daima nitamuenzi. Alijali na kupenda watu wote. Mungu alimpenda zaidi nilivyompenda Mungu amlaze mahali pema Ameni.
Taharifa hizi ziliendele kuniweka katika wakati mgumu sana, kwani zile zilikuwa ni nguzo kwangu. Sikuwa na jinsi maalumu baba mlezi alikuwepo na ndiye aliyenitunza kwa muda mrefu na ananijali na kunipenda kama wanae.
Na hakuna nilicho hitaji na kumpenda kama wanae. Na hakuna nilichohitaji akaacha kunitimizia kama mtoto mwingine nilizidi kumwomba Mungu kwa ajili yake pia. Siku ziliendelea kwenda, miezi na miezi iliendelea kusogea. Na mimi niliendelea vizuri katika masomo yangu ingawa maendeleo yalikuwa hayarizishi.
Siku moja nikiwa nimetoka shule nikiwa nyumbani mama yangu Ruth Mwakalinga alinipigia simu na kunieleza kuwa baba yangu ni mgonjwa nilimwambia mama unasema baba yangu ni mgonjwa akajibu ndiyo. Sikuwa na wasiwasi na wala sikushtuka niliona ni sawa kabisa na niliona hivyo kwa kujisemea mwenyewe bora kwani yeye alivyonitendea anafikiri mimi nakaa kwa amani eeee sasa zamu yake na ataipata.
Aumwe hadi ashike adabu na ajue kuwa aliyoyafanya siyo mazuri alaaa. Safi sana tena safi sana na hapo bado ataipata freshi nilifurahi sana na kujiambia ndani ya moyo, ndivyo inatakiwa. Baada ya hapo niliendelea na mawasiliano na mama na kuendelea kumuoji mama maswali zaidi kwani mama wewe nani amekwambia hayo?
Mama Alinipigia simu na kunieleza kuwa hajisikii vizuri sana.
Emmy Imekuaje hadi baba yangu akupige simu .
Mama Ester mbona unanichekesha?
Emmy Kwa nini mama?
Mama Si mume wangu? Kwa nini asiniambie pale anapokuwa mgonjwa? Au wewe una maanisha nini?
Emmy Yaani mimi na kwambia tangu lini Ernest akakupigia simu mbona maajabu.
Mama Ester unaongea nini wewe? Mimi tangu lini nikawa na mazungumzo na Ernest.
Emmy Sasa wew unamaanisha ni nini?
Emmy Au nimefanya vibaya kukuuliza?
Mama Siyo Ernest baba yako mzazi?
Emmy Bali,
Mama- Baba Mariam ambae ni baba yako mlezi.
Nilikata simu na kumuomba Mungu kwanza kwani nilihisi kuchanganyikiwa. Nilimuomba Mungu anisamehe niliyo yakiri na kuyawaza pia. Nilianza kuugua moyo na baada ya muda mfupi ile hali ilinirudia tena.
Nilianza kutoka damu puani na baadae nilianza kutapika damu, niliumwa kwa wiki nzima na hata shule sikwenda tena nilijua nimekwisha kwani yule ndiye kila kitu kwangu. Na ndiye anaye nisomesha na ndiye ninapoumwa ananiangalia sasa leo anaumwa itakuaje? Niliumwa sana na tena kwa muda mrefu.
Mama alipiga tena simu na kusema haya Ester baba yako amelazwa KCMC nilimwambia sawa mama nitakuja kumwona. Hali yangu iliendelea sawa mama nitakuja kumwona. Hali yangu iliendelea kunitatiza baada ya kama wiki mbili kuisha ile hali ilipotea na kuendelea vizuri nilienda KCMC kumwangalia baba machozi yalinitoka nilihisi kama nitakuwa kichaa nilitamani kupiga yeuwi lakini sikuwa na jinsi nilizidi kulia kwa uwoga muda alikuwa amelala na mimi nilikuwa niki mwangalia.
Nilizidi kumwangalia tu. Baada ya muda mfupi, aliamka na kugeuka na kuniangalia nilianza na salamu :-
Emmy Shikamoo baba
Baba Marahaba Ester hujambo
Emmy Sijambo
Baba Pole na masomo na kuumwa pia
Emmy Asante baba lakini pole wewe zaidi
Baba Asante Ester
Emmy Baba unaendeleaje tangu ufike hospitalini?
Baba Naendelea vizuri namshukuru Mungu
Emmy Pole sana baba Mungu atakuponya baba.
Niliumia sana kwani sikuwa na msaada mwingine zaidi yake niliendelea kuwa moyoni na akilini mwangu pia siku ziliendelea kwenda baba hali yake nayo inaendelea kuwa mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda. Na akili yangu nayo inazidi kuchoka zaidi.
Siku moja nikiwa nimetoka shule nilielekea moja kwa moja hospitalini, nilipofika nilimsalimia baba na baada ya salamu baba alinihoji maswali mengi na alianza kwa kuniuliza.
Baba Ester waalimu wanasemaje? Vipi kuhusu ada ya shule
Emmy Baba tumeshaanza kurudishwa.
Baba Usijali nitapona na nitakulipia ada yote endelea kuniombea
Emmy Sawa baba.
Niliitwa Ester na wengine walipenda kuniita Emmy. Jina la Ester nilipewa na wazazi wangu hawa wawili, Ruth Mwakalinga pamoja na mumewe Stephen Ngome baada ya kubatizwa kwa maji mengi katika kanisa la E.A.G.T Chemchem na Paster Kabese ambapo ndipo tulipo sali jina nililopewa tangu nilipo zaliwa ni Emiliana na baada ya kubatizwa wazazi wangu hawa walipenda kuniita Ester na tangu hapo ndipo lilikuwa jina langu ingawas kwa wengine jina hilo hawaliwezi kutokana na kuzoea kunita Emmy.
Baada ya muda mfupi mama alifika hospitali kwa ajili ya kuleta chakula cha wagonjwa na alitokea maeneo ya KCMC kwa mjomba wangu ambae atamwita binamu nilimsalimia na aliendea kumuhudumia mgonjwa. Tuliendelea kupiga stori za hapa na pale. Baba alikuwa ni mtu wa vituko aliendelea pia kutuchekesha na kutufanya tumuone kama vile si mgonjwa. Alituambia hivi:-
Baba hivi ukiambiwa uvae kiatu au nguo utachagua kipi?
Kwa upande wangu lilikuwa ni fumbo kubwa sana lakini mama alicheka na kusema:-
Mama Baba Mariami bwana,ebu tuondolee vituko vyako. Kwani wewe ungechagua kipi?
Mimi nilinyamaza kimya wala kiufahamu na kimawazo, sikuwa pamoja nao. Na neno lile liliendelea kuwa fumbo kwa upande wangu kwani kwa wakati ule alikuwa acheki: kitu ambacho niliona kauli ile ilimaanisha kitu fulani:
Muda wa kuona wagonjwa uliisha na kuambiwa na manesi tutoke nje nilimuaga baba kwa uchungu na kumuahidi kesho nikitoka shule nitakuja kukuona. Alinijibu usijali mwanangu nitapona na utasoma kwa amani sawa. Nilimjibu sawa baba. Baada ya hapo tulimuaga kwa pamoja na tuliondoka mimi na mama.
Tulitoka nje na nilimuuliza mama maswali: mama kweli ilikuaje hadi baba kulazwa? Mama alinijibu Ester ata sijui nikueleze vipi. Nilimwambia niambie tu mama alianza hivi. Baba yako alikuwa amesafiri kwenda Dar es Salaam kwa muda wa wiki mbili. Na baada ya hapo alijitayarisha kwa ajili ya safari ya kurudi nyumbani Arusha akiwa kwenye gari alijisikia vibaya sana.
Na baada ya hapo aliamua kunipigia simu na kunieleza. Alifika salama na kwenda hadi Airport kabla ya kufika nyumbani akiwa uko aliendelea kujisikia vibaya zaidi na ndipo wafanyakazi wenzake walipoamua kumpeleka Mount Meru na walipofika waliambiwa wamlete KCMC na baada ya kumfikisha hapa ndipo akalazwa na baadae waliamua kunipigia simu na kunieleza. Ndiyo hivyo sasa unavyomuona baba yako.
Tulimaliza maongezi na baadae nilimuaga mama na kumwambia acha mimi niende kesho nitakuja nikitoka shule. Niliachana na mama nakuelekea nyumbani kwani mimi niliishi kwa mjomba wake nay eye aliishi kwa mtoto wa mjomba huyo maeneo ya KCMC na mimi niliishi Uru kitandu juu ya KCMC niliondoka nikiwa na maumivu makali moyoni mwangu na maswali mengi.
Na ile hali ya baba ilinichanganya zaidi na yale maongezi yake yaliniweka kwenye wakati mgumu pia. Sikupata majibu ya maswali niliyojiuliza nilifika nyumbani na kuwaeleza hali halisi ya mgonjwa na kuwaimiza waendelee kumwombea. Palikucha na mimi kama kawaida nilielekea shule na kuwaeleza baadhi ya marafiki na waalimu pia. Nilimwambia kwa lengo la kuwaomba wamuombee zaidi.
INAENDELEA
Tags:
RIWAYA