NIACHE NILIE 09 ๐Ÿ˜“๐Ÿ˜“๐Ÿ˜“๐Ÿ˜“

Ilipoishia…

Palikucha na mimi kama kawaida nilielekea shule na kuwaeleza baadhi ya marafiki na waalimu pia. Nilimwambia kwa lengo la kuwaomba wamuombee zaidi.

Songa nayo…



Shule ilipotoka niliendelea moja kwa moja hadi hospitalini nikiwa na rafiki zangu. Tulipofika tulimwombea baba na baada ya hapo rafiki zangu waliniomba waende niliagana nao na baba pia aliwashukuru na kuwaaga nao waliondoka. Baada ya muda mfupi mama alikuja na chakula cha mgonjwa alimhudumia na muda wa kutoka ulipofika tuliondoka.

Siku ziliendelea na hali yangu ikawa imetulia ingawa bado damu zinanitoka puani lakini sehemu nyingine nilikuwa sawa kabisa siku moja nikiwa nyumbani mama alinipigia simu na kuniambia baba yako ameruhusiwa lakini ameambiwa apumzike mahali na asipande gari kwa mwendo mrefu kutokana na moyo kwa hiyo nitakuwa kwa Paul. Baada ya hapo nilimwambia basi kama ni hivyo kesho nikitoka shule nitakuja kukaa huko ili tusaidiane. 

Mama aliniambia Ester na hiyo hali yako utaweza kweli, nilimjibu nitajitaidi mama. Siku iliyofuata nilienda shule na baada ya masomo nilielekea KCMC kwa mjomba wangu Paul ambapo ndipo baba alipoenda kupumzika nilifika salama na niliwakuta, wote niliwasalimia na kumuuliza baba, baba unaendeleaje? Alinijibu naendelea vizuri kabisa naamini kesho nitaamka salama kabisa na nitarudi nyumbani Arusha kwani nimewakumbuka sana watoto wangu.



Nikamwambia hata mimi naamini kesho utaamka salama kabisa na ninaamini hata sasa ni mzima. Alimjibu kesho nitaamka mzima na nitakapoenda Arusha itabidi niende kazini moja kwa moja kwani ninakazi nyingi na kuna ndege za kwenda kupaka rangi. Naamini Ester nikifanya kazi kwenye ndege moja tu nitakulipia ada yote na kukununulia mahitaji yako ya shule. Sawa nilimjibu sawa baba lakini katika kujibu kule moyo ni nilikuwa na uchungu na nilitamani kulia pia.

Muda ulisogea siku ziliendelea kwenda na mkuu wa shule bado akawa anaturudisha ada ya shule. Niliumia sana kwa wakati ule kwani wa kumwambia suala la ada yuko kitandani. Nilizidi kumuomba mwalimu na alinielewa. Tuliendelea kumuuguza baba na watumishi wa Mungu waliendelea na maombi kila kukicha. 

Aliombewa na mchungaji kabese ambae ni mhumini wake na tena ni mzee wake wa kanisa na pia aliombewa na mchungaji Masalu aliyeishi Mbauda Kerai Arusha aliombewa pia na waumini wa makanisa mbalimbali na Paster Haule ambae ndiye alikuwa mchungaji wake wa kwanza kabla ya kufunguliwa kwa tawi la chemchem chini ya Paster Kabese ambae ndiye mchungaji wake . 

kuisahau familia ya Sabiti ambae anaishi Airport Kia ambapo baba alifanya kazi pia. Mungu alisikia maombi ya watu wake baba aliendelea vizuri na kurudi Arusha ingawa aliporudi hakuweza kwenda kazini aliendelea na mapumziko. Na mimi nilirudi nyumbani Uru kitanda nilipokuwa nikiishi na babu yangu ambae ni mjomba wa mama yangu Ruth Mwakalinga.

Niliendelea na shule kama kawaida siku moja nikiwa shule nilianza tena kuumwa na baadae nilipelekwa nyumbani na mwalimu Rose Mery na kuendelea na mauguzi niliisi kuwa utakuwa ni mshtuko kutokana na ile hali ya baba yangu mlezi nilianza tena kutapika damu na nyingine kutoka puani hali yangu ikawa mbaya zaidi kwani kwa wakati ule mama yangu alikuwa katika wakati mgumu. Na pia kuja Moshi kwake ilikuwa ni ngumu kwani anamuuguza baba. 

Hali yangu ikawa mbaya zaidi na ndipo mchumba wangu Deodath Joseph Kimario alipofikishiwa ujumbe na mtoto wa babu yangu kwa jina la Deodath Hendry Chua. Alipoenda dukani kwa Deodath Joseph Kimaro na kumueleza hali yangu halisi alifika nyumbani na kumuomba babu anipeleke hospitali babu alikubali na baadae tuliondoka.

Tulipokuwa kwenye gari alikuwa akiendesha aliniambia Ester tumeshaangaika kwa madaktari mbalimbali lakini bado hali ni hii jaribu tena kwenda, kwa wataalamu nikamwambia haitawezekana kwa waganga sintakaa niende alinijibu utakaa hivyo hadi lini? Nilimwambia nitakaa hivi hadi mwisho alinijibu hali hii siyo yakuchezea na usipoangalia utakufa. Nilimjibu acha nife kwani nitakuwa wakwanza kufa? Kwanza kufa mbona ni kitu cha kawaida. Alinijibu sitakubali nitaangaika na mimi nione.

Tulifika hospitali na kupata matibabu na niliambiwa ni malaria na presha. Nilipewa dawa na baadae nilirudi nyumbani lakini nilipofika tu na kuanza kutumia dawa zile nilianza kutapika zaidi na hali yangu ikawa mbaya zaidi tulisita kumwambia mama kwani tuliisi atachanganyikiwa. Na pia mama alikuwa ni mjamzito kwa wakati huwo. Niliendelea kumuomba Mungu na pia Deodath Joseph ambae alikuwa ni rafiki yangu kwa msemo mwingine nilishaanza kumuona ni mchumba wangu aliendelea kuangaika. 

Baada ya muda mfupi aliniletea dawa akaniambia niwe naogea asubuhi na jioni nami nilijikuta nikifanya vile na nilishasema sitaki madawa ya waganga lakini nilijikuta naanza kutumia dawa zile hali ilibadilika na zile dawaza hospitali niliziacha. Na niliendelea na ile dawa ya kuoga lakini cha ajabu nikaifanya kuwa siri yangu sikupenda mtu aone. Siku zilisonga hali ikawa nzuri kabisa nilianza kwenda shule kama kawaida siku moja nilitoka shule na nilipofika nyumbani nilikuwa na hamu ya matembere.nikiwa shambani nilianza kuhisi kizunguzungu na maumivu makali ya kichwa yaliendelea ndani yangu nilichuma haraka haraka na kutoka shambani. Nilielekea nje na kuanza kuchambua mboga. 

Bibi yangu alirudi sokoni kwani alikuwa ni mfanya biashara wa maandazi sokoni, babu yangu alikuwa ni baba wa nyumbani kutokana na hali yake ya udhaifu wa mguu hivyo yeye alikuwa akiangalia mifugo yake pamoja na kazi za shamba.

Nikiwa nafanya kazi zangu za hapa na pale na uku nikiwa nachambua mboga gafla simu ikapigwa na nilipopokea nilikuta ni mama yangu. Nilipokea na mama hakuwa na mazungumzo mengi maana nilimsalimia lakini hakuitika. Aliniambia moja kwa moja bila kujali Ester mwambie babu yako baba ameshafariki. Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 6/4/2010 siku ya jumanne saa 2: kasoro dk 25 nilichanganyikiwa kwa sababu nilipokuwa na wasiliana na mama alituambia anaendelea vizuri ingawa kazini bado ajaweza kwenda. 

Baada ya simu ile sikujua kilichoendelea baada ya muda niliamka na kumbe nilikuwa nimezimia nilimpigia mchumba wangu Deodath simu na kumueleza na baadae nilianza kuondoka na kwenda Arusha siku ile ile niliondoka na kuelekea Arusha nakumbuka nauli pamoja na matumizi madogo madogo nilipewa na mchumba wangu huyo.

Niliondoka Moshi saa 6:00 jioni nikiwa nimeambatana na mjomba wangu mdogo Deodath Hendry Chua. Tulianza safari na tulifika Arusha saa 10 usiku nilipokelewa na ndugu zangu, ilikuwa ni huzuni tupu kwani nilizidi kuumia nilipomwangalia mama yangu na ile hali aliyoachwa nayo. Tuliendelea na mipango ya msiba na muda ulipofika tulizika salama. Amini usiamini mama yangu aliachwa katika wakati mgumu sana kwani ni mjane aliyeachwa akiwa ni mjamzito bado kuna watoto wanahitaji kusoma. Tulimaliza msiba salama na baada ya mapumziko mafupi nilirudi Moshi kuendelea na masomo. 

Maswali yalianza kunijia, nikaanza kujiuliza moyoni mwangu. Sasa baba ndiyo hivyo Mungu kampenda zaidi yetu ada sijalipiwa bado kidogo kufanya mtihani na mwalimu anasema mtu ambae ajatoa ada atafanya mtihani sasa mimi si ndiyo nimekwisha. Nililia sana na hali yangu kiafya ilianza kubadilika nilianza kukonda tena na pia hali ya ugonjwa ikazidi kuendelea na yote hayo yaliendelea kutokana na mimi kufanya yale niliyoambiwa nisifanye kwani madaktari wengi walinishauri niepuke sana .

i. Kukasirika

ii. Kushtuka

iii. Kukemewa kemewa

iv. Kutokuwaza

Sasa yote yanaanza kutokea na hizi hali zinaendelea kutendwa, kutokana na mimi kutoeleweka na hasa pale unapokuta muda mwingi nikiwa nalia. Maana hata kulia pia nilinyimwa kutokana na yale maumivu ya kichwa. Siku moja nikiwa nyumbani Deodath alinipigia simu niende dukani kwake na nilipofika yaliendelea haya:-

Deodath Vipi Ester

Ester Poa

Deodath Unaendeleaje?

Ester Naendelea vizuri.

Deodath Pole na msiba

Emmy Asante

Deodath Ester ngoja ni kwambie kitu huku siyo wakati wa wewe kuendelea kuumia na wala si wakati wa wewe kuanza kusema hivi Mungu hivi Mungu hivi Mungu hapana huu ni wakati wa wewe kuwaza mtihani wako sisi tuko katika safari moja leo yeye kesho sisi je tuweje? Na siyo kuwa katika hali hiyo ya mawazo na unajua hali yako ilivyo ebu jaribu kupunguza hayo unayo yawaza.

Nilimjibu

Ester Haiwezekani

Deodath Haiwezekani nini?

Ester Ni ngumu sana kutokuwaza kuwaza nilazima kwani sielewi nitaishije.

Deodath Mungu atakusaidia Ester kama alieza kukuumba atashindwa kujua utaishi vipi?

Ester Hapana Deo.

Deodath Hapana nini hakuna linalo shindikana Ester muombe Mungu atakusaidia

Ester Sijui maana hali ngumu.

Deodath Kuna nini Ester mbona haueleweki na pia punguza kulia ebu ongea vizuri ili nielewe. Siyo wakati wako wakulia huu ebu sema.

Ester Deodath hapa unaponiona sielewi mbele ni wapi wala nyuma ni wapi na sijui pazuri ni wapi na pabaya ni wapi.

Deodath Kwa nini unaongea kauli kama hizo.

Nilianza hivi:-

Deodath rafiki yangu kwa sasa naona mambo magumu sana kwangu, kama nilivyokwambia baba yangu mzazi alishanikataa na hata mimi mwenyewe simpendi na ndugu zangu wenyewe ndio hao wamesikia babayangu mlezi amefariki lakini hata kuja kuzika imekuwa ni ngumu kwao na wakati wanajua ndiye aliyekuwa ananitunza lakini imekuwa ngumu kwao na isitoshe mama yangu ni mama wa nyumbani sasa kwangu itakuaje? Ndugu zangu hao tangu nikiwa mdogo hakuna mwenye mpango na mimi nimeteseka lakini hakuna aliyejigusa na hata kumsaidia mama yangu ela ya matibabu hawakuweza ukizingatia mimi ni damu yao na nimatajiri, sasa ndiyo wakati wa kuwa chokoraa umefika.

Deodath Usiseme hivyo Ester unamkufuru Mungu Ester

Ester Simkufuru Mungu simkufuru Mungu hata kidogo nina ndugu Deo, ni matajiri lakini hawataki kunisaidia sasa baba Mariamu aliyenijali aliyenipenda kama watoto wake, aliyenithamini aliyejua uchungu wa mtoto ni upi aliyejua kuwa nikiumwa natakiwa kupelekwa hospitali aliyejua nikirudishwa ada natakiwa ada sasa leo hayupo nitakuwa mgeni wa nani mimi.

Deodath- Mungu atakupa msaada mwingine usiogope endelea kumwomba tu.

Ester Hakuna na hatatokea baba kama baba mariamu.

Baba anayejua utu ni nini anayemthamini mtu kama anavyojithamini mwenyewe.

Deodath Ester tuachane na hayo kwani unatatizo gani?

Ester- Kwanzia mwaka umeanza Deo sijalipiwa ada ya shule na mwalimu amesema mwanafunzi ambae ajatoa ada hatafanya mtiani.

Deodath Kwani ada ni sh ngapi?

Ester Bado sijajua

Deodath Fuatilia alafu uje uniambie.

Ester Asante Deo, nitafuatilia.

Tuliachana na mimi kuelekea nyumbani baada ya kufika nyumbani bado niliendelea kumfikiria Deo na kujiuliza maswali kwa nini ameniambia vile?

******



Niliendelea kumuweka Deodath moyoni nilimuona ni mtu wa pekee sana kwangu na ni msaada mkubwa sana maana siku ya msiba hakujali kuacha kazi zake na kuja kuambatana nasi katika wakati mgumu tulionao. Niliendelea kumuheshimu sana na kumuona ni mtu bora sana kwangu. Siku zilizidi kusogea niliona sinakimbilio tena. Nilienda shule na ile hali ikuwa imepotea nilimfuata mkuu wa shule na kumuuliza kiasi nilichokuwa nikidaiwa ilikuwa hivyi:-

Emmy Shikamoo mwalimu

Mwalimu Marahaba Emmy hujambo

Mwalimu Pole na msiba

Emmy Asante mwalimu

Mwalimu Vipi Emmy kuna nini?

Emmy Mwalimu naomba kujua nadaiwa sh ngapi?

Mwalimu aliniambia kiasi nilichodaiwa kuwa ni laki mbili na kumi . nilishukuru nakuondoka kuelekea darasani niliendelea na masomo na baada ya masomo nilitoka shule na nilipofika nyumbani nilimpigia Deodath na kumueleza kwani alinimbia nikishauliza nimpe jibu. Nilimwambia na kuniambia kuwa atazilipa hizo fedha.siku inayofuata nilienda shule na alikuja kweli na kuzitoa zile fedha. 

Nilishukuru Mungu. Nilimpigia simu mama na kumweleza mama alishukuru sana na kusisitiza kumueshimu sana Deo. Siku zilisogea na mwaka uliendelea kusogea, na siku ya kufanya mtihani wa kuitimu elimu ya sekondari ilikaribia. Yapata kama mwezi tufanye mtihani hali yangu ikaanza kuwa mbaya tena, hali za damu zilianza upya kutapika kutoka puani, utosini na blidi isiyoisha.



Mambo yalikuwa mabaya na hali nayo ikawa mbaya zaidi. Nikiwa nyumbani Deodath alifika na kuikuta hali ile. Alichukua uwamuzi wa kuniweka kwenye gari na kunipeleka kwa mtaalam aliyejulikana kama Dokta Chua yaani Mganga Chua niliudumiwa na kupewa dawa za koga na za chai pia. Niliporudi nyumbani kwa kuwa sikuwa naishi na Deo nilitupa dawa zile chooni na kuziacha zile za kuoga tu. 

Nilizitumia kwa muda mfupi na baadae nilizitupa chooni. Hali yangu ikawa nzuri kidogo nikaanza kwenda tena shule na siku ya kufanya mtihani ikawadia. Nilifika shule na kupangwa katika chumba cha mtihani na ninakumbuka ilikuwa ni tarehe 4/10/201. 

Baada ya kuingia tu darasani kichwa kilianza kuniuma lakini nilimuomba sana Mungu anisaidie, nilianza mtihani wangu wa kwanza na baada ya muda mchache nilianza kutoka damu puani na ilinibidi kutoka nje. Nilifanya mtihani kwa shida sana kwani nilitoka shule nikiwa namaumivu makali sana kichwani nab ado damu ziliendelea kutoka puani. Siku inayofuata nillienda shule na nilipofika nilimomba sana Mungu anisaidie nifanye mtihani ule salama. 

Niligiia darasani na kuanza mtihani wa kwanza nilifanikiwa kuumaliza salama tulitoka mapumziko kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa pili kukiwa tunajiandaa kuingia darasani hali ilikuwa mbaya na mkuu wa shule alichukua uwamuzi wa kumpigia mama yangu simu na kumueleza, mama alimwambia atakuja, na baada ya hapo aliwasiliana na mjomba wangu Paul na kumueleza maadamu yeye alikuwa anaidhi karibu na shule aliahidi kufika hali ilikuwa si yakawaida. 

Wenzangu waliingia darasani na kuanza mtihani niliumias sana nilimwambia mwalimu naomba nikajaribu tena mwalimu alikubali ni kaenda kukaa kwenye dawati langu ambalo lilikuwa nje ya darasa. Waalimu walibidi kuniweka nje barazani mwadarasa langu kutokana na ile hali ya kutapika damu.

Kwasni iliwafanya wanafunzi wenzangu kulia badala ya kufanya mtihani. Nilikaa kwenye dawati langu na kusali baada ya hapo niligeuza karatasi ili nianze kufanya yale yaliyo nihusu kufanya. Baada ya kugeuza tu karatasi sikuweza kuona andishi ata moja niliona karatasi lote jeupe yaani halina kitu chochote. Niliinamisha kichwa chini msimamizi alinigusa na kuniambia vipi tena? Nilipoinuka tu damu zilianza kunitoka puani nilisitishwa tena kufanya mtihani ule na kupelekwa moja kwa moja hadi ofisinin. Waalimu walinisaidia lakini bado hali yangu ilizidi kuwa mbaya zaidi baada ya muda mfupi nilianza kutapika damu na hali hapo hapo ikabadilika kabisa. 

Nilianza kutapika na baadae mwili ulianza kufa nguvu muda mchache tu alikuja Deodath ambae ni rafiki yangu alifika aikwa na pikipiki kutokana na ile hali niliyokuwa nayo ilibidi arudi nyumbani baada ya muda tena mama yangu alifika na baadae kuondoka alichanganyikiwas na hali aliyonikuta nayo. 

Punde si punde Deodath alifika tena shuleni akiwa na gari na ndipo alipoamua kunipeleka hospitali. Tuliongozana na mkuu wa shule pamoja na Deodath tulifika hospitali na kufanyiwa vipimo, lakini vipimo havikuonesha chochote zaidi damu ziliendelea kutoka tu. Waliniingiza wodi na baadae walinitundikia driu na kunipa dawa. Kwa mara hii nilipelekwa hospitali ya mkoa wa Mawenzi nilikuwa pale kwa muda ambao mtihani uliendelea. 

Nilifanyiwa vipimo vyote lakini bado havikuonesha tatizo, mitihani ilimalizika na mimi nikawa mzima kabisa, niliruhusiwa kutoka hospitali lakini wenzangu walikuwa wamesha maliza mitihani yote siku na jinsi nililia sana na mwalimu wangu mkuu aliuzunika na kunipa pole lakini bado alikuwa na maswali moyoni mwake. 

Aliniambia kweli huyo mama wako wakambo ajakufanyia haki hata kidogo kwa nini wakati wamitihani unakuwa mgonjwa alafu ikiisha tu unakuwa mzima? Sikuwa na jibu nilibaki naila tu, sikuwa na njia ya kufanya kwa hiyo nitihani siku fanya zaidi ya mitihani mitatu tu lakini hata hiyo mitatu nilifanya nusu nusu sikuwa nimeimaliza. 

Nilizidi kuumia sana kwani hata nilivyokuwa shule matokeo yangu hayakuwa mazuri nilikuwa nasahau yaani mwalimu akisha fundisha akitoka darasani ukiniuliza mwalimu kafundisha nini nilikuwa sijui tena. Wazazi wangu walihuzumika sana ndugu zangu waliumia sana kwani mimi ndiye wa kwanza kwa mama yangu.

Nilimshukuru sana Deodath kwa moyo aliouonyesha kwangu kwani aliangaika na mimi tangu shuleni na alionesha kuwa mtu wa karibu sana kuliko hata ndugu zangu. 

Alikuwa anamiliki pikipiki yake binafsi lakini nilipopata tatizo lolote hakusita kuomba magari kwa rafiki zake pale kijijini. Nilimwambia kuwa asante kwa kuwa bega kwa bega nami tangu kidato cha pili hadi sasa lakini kwa kuwa mtihani umemalizika na wanafunzi wameshaanza kusambaratika basi na mimi sina budi kumaliza taratibu zilizobaki shuleni alafu nirudi nyumbani Arusha. 

Kwani ndipo nilipokuwa naishi na wazazi wangu. Alinijibu Ester baki tu hapa Moshi kwani uanvyotaka kurudi Arusha ni kwamba unaenda kumsumbua tu mama yako na unaelewa kuwa Yule ameachwa ni mjane atafanya mangapi na mangapi aache? Nilimjibu hata hawa ninaoshi nao wamesha choshwa na hii hali acha tu nirudi nyumbani kama nitapona sawa kama nitakufa pia sawa. 

Alinijibu sawa yote ni maamuzi yako. Nilimaliza kufuatilia maswala ya shule na kuagana na waalimu wangu ingawa walilia sana lakini sikuwa na jinsi.

Nilianza kujitayarisha kwa ajili ya safari ya kurudi nyumbani Arusha. Muda ulifika nilielekea moja kwa moja kwa Deodath na nilipofika nilimuaga na alinisaidia nauli na mi kuondoka alinisindikiza hadi stendi na kuhakikisha nimepanda gari kuelekea Arusha. 

Tuliagana na zaidi aliahidi kuendelea kuniombea na kunisisitizia kutoacha kumuomba Mungu. Nilimshukuru na hatimae kuagana nae.

Nilifika salama nyumbani nilikutana na mama yangu pamoja na familia yetu walinipokea kwa huzuni na hata wengine walilia. Bado mama alikuwa na huzuni kwa mimi kutofanya mtihani. Tulianza maisha ya nyumbani pamoja na mama yangu mzazi Ruth Mwakalinga na maisha yalikuwa ni magumu sana kwa upande wetu kwani baba alifariki na kutuacha kwenye nyumba ya kupanga na mama akiwa ni mjane mwenye mtoto mchanga hivyo maisha kwa upande wetu yakawa magumu sana.

 Tuliishi kwa shida maisha yakazidi kuwa magumu sana kwa upande wetu. Baba alifanya kazi na alikuwa na mshahara mzuri lakini fedha zake zilikuwa zakusaidia yatima na wajane na watu wasiojiweza na kwa huduma za makanisani.hivyo kutuacha bado tukiwa kwenye nyumba ya kupanga. Ingawa alikuwa amejenga nyumba lakini bado hadi sasa. Baba yangu mlezi huyo alinilea tangu nikiwa darasa la sita hadi form four mwanzoni alipofariki.

Baba alifariki kwa ugonjwa wa moyo alituacha katika wakati mgumu sana na hadi sasa bado, maisha hayajawa sawa kwa upande wa mama yangu Ruth Mwakalinga. Mungu amlaze mahali pema Ameni. Nilikuwa nyumbani kwa muda kama wa wiki mbili hivi na baada ya hapo nilipigiwa simu na rafiki zangu na waliniambia kuwa tunahitajika kupeleka passport za kuweka kwenye vyeti vya shule na hivyo kupelekea mimi kumueleza mama.

SOMA VICHEKESHO KUPITIA SIMU YAKO

INAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post