Nilimwambia mama na mama alinielewa na nilianza safari siku iliyofuata yakuelekea Moshi kwa babu yangu ambae ni mjomba wa mama na ndiko nilipokuwa nikiishi tangu nilipoanza kidato cha tatu. Nilifika Moshi na kupokelewa na Deodath ambae ndiye aliyenisindikiza wakati naelekea Arusha na ndiye tuliyeanza nae urafiki tangu nikiwa kidato cha pili. Nilifika salama na kuanza kufuatilia mambo ya shule baada ya muda mfupi Deodath aliniita na kuniuliza maswali machache.
Alianza :-
Deodath Vipi Ester kwanzia umeenda Arusha ulikuwa unafanya kazi gani?
Ester- Amna kazi niliyokuwa nafanya zaidi ya kuwa nyumbani tu kama unavyoelewa mama yangu hana kazi yeyote ile kwa hiyo alikuwa anapika chapatti alafu mimi nabaki na mtoto nyumbani.
Deodath Sasa ukimaliza kufuatilia masuala ya shule unataka kufanya nini?
Ester- Nitarudi nyumbani.
Deodath Sasa utakuwa unaangaliana na mama yako tu.
Ester Hapana nitakuwa namsaidia mama kukaa na mtoto wakati anauza chapati zake.
Deodath Hapana Ester njoo hata uuze dukani kwangu alafu mimi nitafungua lingine kuliko uende ukakae nyumbani tu.
Ester Hapana siwezi kumuacha mama yangu peke yake nitarudi tu nyumbani.
Deodath alinisisitizia zaidi mimi kutokurudi tena Arusha, lakini bado nikawa mkaidi sana. Nilifuatilia mambo yangu ya shule na baada ya kumaliza nilianza kujitayarisha kwa safari ya kurudi Arusha. Nilimshukuru sana babu yangu na kumwambia asante sana babu kwa kuishi na mimi vizuri na sasa nataka kurudi nyumbani zaidi babu naomba uendelekuniombea.
Nilielekea kwa Deodath kwa ajili ya kwenda kumuaga tena. Lakini nilipofika kwake alinikaribisha na kuniandalia kinywaji na baadae aliondoka na kuniambia nisubiri nakuja sasa hivi alafu nitakusindikiza, nilikubali na alivyotoka alifunga mlanngo baada ya muda niliona saa zinazidi kwenda na Deodath harudi niliamua tu kuondoka niliandika karatasi kumjulisha kuwa nimeshaondoka kwa hiyo asinitafute.
Nilisimama na kuusogelea mlango kwa lengo la kufungua mlango na kuondoka, lakini nilipofungua mlango haukufunguka ulikuwa umefungwa na ufunguo. Nilijiuliza maswali mengi ya siyo na majibu nilisema moyoni ameenda kuletsa watu waje waniuwe au? Niliwaza mengi na muda ulizidi kusogea.saa tatu bado hajarudi saa 4 usiku ndiyo akaingia . na baada ya kuingia sikuweza hata kuongea zaidi nilikuwa nikilia alinibembeleza nilimuomba anipeleke nyumbani kwa babu yangu kwani kutoka hapo kwao na kwetu si mbali ni maji rani.
Alinijibu lala nitakupeleka kesho sasa watu wamesha lala nilibaki nalia tu lakini hakunielewa zaidi ya kunibembeleza tu. Nilimwambia kwa sasa babu yangu anajua nimeshafika Arusha alafu niko hapa je akimpigia mama itakuwaje? Lakini Deodath hakunielewa nilizidi kulia labda atanionea huruma lakini hakuliona hilo nilizidi kulia hadi nilipopitiwa na usingizi palikucha kwenda Arusha nikaogopa kurudi kwa babu nayo nikaona ni aibu kwani nilikuwa nimelala nje ya nyumbani hiyo nikaona ile ni aibu sana. Na hivyo huo ndiyo ukawa mwanzo wangu wa kuishi na Deodath.
Nilianza kuishi na Deodath maisha kwa upande wangu yalikuwa mazuri, alienda kutoa taarifa kwa wazazi wangu na baadae walijua kuwa niko kwa Deodath. Ndugu zangu waliongea mengi walianza kusema huyo mwanaume hata weza kuishi na Ester, kwanza anamatatizo kibao na pia majirani wa Deo walimuambia acha na huyo mwanamke mwenye matatizo anaanguka mwenyewe anatoka madamu ovyo, kwanza ni tasa. Deo aliwajibu nimempenda kama alivyo pamoja na matatizo aliyonayo nimempenda hivyo hivyo.
Walimjia kwa njia nyingi hadi mimi nikawa nakosa amani na kulia lakini Deo alinitia moyo na kuzidi kuniambia kuwa atakuwa bega kwa bega na mimi. Niliishi na Deo na mama yake ambae alishakuwa mama, mkwe wangu nilikaa kwa muda mfupi sana, matatizo yalianza damu zilianza kutoka tena upya. Nipo Deo alipoamua kunipeleka kwa mganga Chua na kupewa dawa ya kuweka kwenye chain a nyingine ya kuoga na yakuchoma.
Nilizitumia dawa hizo kwa muda lakini bado hali ilizidi kuwa mbaya zaidi niliendelea tu kutumia kwa kujipa moyo labda ndiyo napona lakini nilizidi kuugua tu. Hali ilikuwa mbaya sana kuliko ile ya mwanzoni.ilibidi niache hizo dawa na baadae tulienda sehemu nyingine TPC msitu wa tembo nilikutana na babu ambae ni muuguzi na kuanza kumueleza. Nilikuwa na Deo a ndiye aliyenipeleka makusudio yake ni mimi kupona.
Nilimueleza babu Yule na kunipa dawa ya chai yakuoga na yakuchoma na nyingine yakupaka nilizitumia na kuanza kuona mabadiliko lakini kila nilipo kasirika hali ile ilijitokeza kwani siku ruhusiwa
i. Kulia
ii. Kukasirika
iii. Kugombezwa
iv. Kuwaza
v. Na hata kushtuliwa
*****
Kwani nilikuwa nikifanya haya hali inajirudia tena niliendelea kutumia hizo dawa na baadae hali iligeuka na kupelekwa hospitalini na kulazwa tena ingawa nililazwa lakini hakuna kilicho onekana. Deo aliendelea kuangaika na kulazimika kurudi tena kwa Yule babu wa TPC msitu wa tembo, natulipofika babu aliamuru wa watumishi wake kwenda kuchinja mbuzi baada ya muda alikuja na damu kwenye kiganja cha mkono na kuanza kutulambisha tulilamba mimi pamoja na Deo na kukabidhiwa dawa za kwenda kutumia.
Tulirudi nyumbani na baada ya kwenda kutumia zile dawa hali haikubadilika hali ilizidi kuwa mbaya zaidi zilianza kutoka tena kila mahali.
i. Utosini ingawa palikuwa hapajatoboka.
ii. Masikioni ingawa yalikuwa hayana maumivu yoyote
iii. Machoni kwani kila nilipolia machozi yalitoka machozi ya damu.
iv. Puani damu zilipokuwa zikitoka nilisikia maumivu makali sana ya kichwa.
v. Nilianza kutoka blidi isiyo katika
Niliugua kwa muda mrefu na ilimbidi kurudi tena katika hospitali ya Mkoa wa Mawenzi na nilivyofika madaktari walitishwa sana na ile hali na baadae hata kabla ya kunipa huduma walisema hawawezi kunisaidia kwa hiyo tunaomba kama unaweza kwenda KCMC uende lakini hapa kweli hatuwezi, maana hatujawahi kuona hii hali Deo hakukata tamaa tuliondoka na kurudi nyumbani. Hatukuweza kurudi tena KCMC kwani ndiko nilikotibiwa tangu nikiwa kidato cha pili hadi namaliza lakini bado hali ni ile ile.
Tulirudi nyumbani na palipokucha tulirudi tena kwa Yule babu na tulipofika tulimueleza babu hali halisi na baadae Yule babu aliniambia kuwa jina la Emiliana ni jina la bibi yangu ambaye alishafariki siku nyingi kwa hiyo huyo bibi alikuwa na bangili ambayo mimi natakiwa kuwa nayo, ili hayo matatizo yaniishe. Deo alikubali na kumwambia, tutarudi kesho. Tuliondoka moja kwa moja tulielekea hadi maduka ya wahindi na kutafuta bangili tulipata na Deo kuinunu kwa sh elfu kumi. Tulielekea hadi nyumbani hali ikizi kuwa mbaya zaidi.
Palipokucha tuliendelea TPC msitu wa tembo kwa Yule babu na tulipofika tulimkabidhi ile bangili na aliifanyia mambo yake na kunivalisha na kuniahidi kutokuumwa tena. Alitukabidhi tena dawa za kwenda kutumia nakumbuka ilikuwa tarehe 23/11/2011 jumanne. Tulipofika nyumbani nilianza kutumia dawa zile nikiwa na ulinzi wa bangili mkononi nilitumia dawa zile hadi nilichoka lakini bado hali iliendelea kuyumba.
Nilimaliza dawa na hali ikawa bado ni mbaya. Muda ulienda nikaendelea kuteseka baada ya muda mfupi matokeo ya kidato cha 4 yalitoka na Deodath, alifuatilia na aliporudi aliniambia jina lako lipo lakini hakuna kilichoandikwa haionyeshi kuwa una ziro wa laa, wameandika jina halafu wakaacha wazi. Ingawa Deo aliwasiliana na mkuu wa shule lakini mwalimu naealidai kuyapokea yakiwa hivyo hivyo. Niliendelea kuumia lakini bado sikuwa na njia nyingine ya msaada. Deodath aliendelea kunitia moyo na kuahidi kuwa maisha yake yakiwa mazuri ataniendeleza kielimu. Nilimshukuru sana.
Siku zilisogea na bado hali yangu ilikuwa mbaya mama mkwe alianza kuchoshwa na hali yangu na hata upendo kwangu kupungua kabisa lakini namshukuru Mungu Deo aliliona hilo na kuendelea kunitia moyo huku akiniambia siku moja Ester utaishi kwa amani na furaha kabisa na mimi nitahangaika na wewe hadi sumli, yangu ya mwisho usijali Ester niko nawe bega kwa bega hadi Mungu atakapoamua. Niliendelea kulia na mambo yaliendelea kuwa magumu kwangu.
Tulirudi tena kwa babu na alituambia turudi twende siku inayofuata. Siku inayofuata hatukurudi tena kutokana na hali yangu kuwa mbaya zaidi nakumbuka ilikuwa ni tarehe 3/12/2010 . niliamka nikiwa na hali mbaya zaidi Deo alibaki kulia tu kwani aliponipeleka hapakuwa na jibu niliumia sana kuona mwanaume akiwa analia mbele yangu lakini sikuwa na njia zaidi tulizidi kulia wote.
Hakuna ambae hakuuumizwa na mwenzie Deo hakupenda mtu yeyote kunikera wazazi wake walianza kumwambia unirudishe kwetu alikerwa sana na hayo maneno ya wazazi wake na ndipo wazazi wake wakaanza kumchukia na yeye pia na kumwambia unaangaika na mwanamke ambae hana faida yoyote zaidi anakufilisi tu maana akiumwa tu kidogo hospitali na hospitali ni hela inatumika.
Walizidi kusema walivyojua na baada ya muda mfupi nilianza kulazwa na njaa kutokana na Deo kuambiwa anirudishe nyumbani na kugoma ilimbidi kununua vyombo na kuanza kupika mwenyewe kwa ujumla alianza kufanya kila kitu peke yake kupika kufua na kuangaika wakati mwingine kuniogesha peke yake na huku akiendelea kuuza duka lake. Hali ilikuja kutulia na Deo alipata safari ya kwenda Dar es Salaam ilimbidi amuombe mtoto wa dada yake aje kuniudumia hadi atakaporudi kutokana na mama mkwe kukerwa na ile hali . Deo alisafiri na kwenda Dar es Salaam kwa muda wa wiki 1 kabla ya safari nilimwambia Deo sasa unasafiri si utakuwa mwanzo wa mimi kuanza kuishi maisha ya mateso na yakunyanywasa?
Alinitia moyo na kuniambia
Deodath Siyo kwamba naenda Dar kustarehe mke wangu na siyo kwamba nakukimbia. au labda na mimi nimekuchoka hapana.
Nilimuliza :-
Ester Mume wangu kama siyo kunikimbia unaenda Dar kufanya nini?
Deodath Ester mke wangu usiwaze hayo unayowaza, nakupenda kuliko unavyofikiria na niko tayari hata wazazi wangu kunitenga lakini siko tayari kuendelea kuona wewe unaishi kwa mateso.
Ester Sasa tufanyeje? Maana mimi kubaki na mama yako sita weza lakini bado ujanieleza unaenda Dar kufanya nini?
Alianza kunieleza anachoenda kufanya Deodath Ester mke wangu nakupenda naomba usilie maana, unaniumiza mwenzako. Naomba uelewe naenda kuhangaika kwa ajili yako maana haya maisha ya wewe kuishi na mama mkwe wako bila amani sipendi kuona na wewe kila siku ya Mungu lazima ulie hali ambayo inaniumiza mimi.
Hivyo naelekea Dar kuna chumba ambacho nilikuwa naishi kabla sijaja Moshi na wakati naondoka nilimpangisha mtu kwa kuwa kodi yangu inaisha 2013 kwa hiyo ikabidi nimuweke mtu sasa ngoja nikamuombe Yule niliyempangishia aame alafu nikirudi tuondoke tukaishi Dar hata kama utalala chini, hata ukila chumvi lakini nione unakaa kwa amani tu. Sawa mke wangu. Nakupenda Ester sifurahi ninapokuona unateseka nilimwambia haya:-
Ester Sasa kutokana na hii hali yangu ukienda kuishi na mimi mbali huoni itakuwa ni mateso?
Alijibu :- Deodath Acha niteseke na niko tayari kuteseka kwa ajili yako hadi nihakikishe umekuwa mzima.
Nilimkubalia na hatimaye aliniaga na kuondoka na alivyo, ondoka aliniacha na mtoto wa dada yake ambae aliendelea kunihudumia huku akiendelea kuuza duka la mjomba wake ambae ni mume wangu. Alifika Dar es Salaam na kukamilisha mipango yake. Baada ya wiki kumalizika alirudi Moshi na alipofika alinieleza habari za LOLIONDO na kuniambia nitafanya juu chini nikupeleke mke wangu, yaani nitaangaika hadi nione mwisho. Nilimuuliza LOLIONDO nani amekwambia? Akaniambia nilivyokuwa Dar nilisikia stori nyingi za LOLIONDO na watu wanasema wanapona kwa hivyo twende tu mke wangu na wewe utapona.
Nilimwambia siendi popote pale kama nikuzunguka nimeshazunguka na hadi sasa nimeshapewa hadi vitu vya ajabu kwa hiyo siendi popote pale sawa? Alinijibu usiseme hivyo huwezi kujua uponyaji wako uko wapi huenda uko ukapona.
Nilikataa kata kata siku ziliendelea kwenda hali nayo ilibadilika zaidi tumbo liliendelea kunisumbua na Deo kaamua kunirudisha hospitali ya Mkoa wa Mawenzi na baada ya vipimo waliniambia nauvimbe kwenye tumbo la uzazi nilipewa dawa za kwenda kutumia kwa muda wa siku tano na baada ya hapo ni kae baada ya miezi mitatu nirudi tena.
Niliendelea kujiuliza yaani natapika damu halafu wananiambia eti ni uvimbe kwenye uzazi kwa hiyo huwo uvimbe ndiyo unatoa damu kwa mdomoni? Sikupata jibu na Deodath aliendelea kuchanganyikiwa na majibu ya madaktari.
Yanayoeleza mambo ambayo hayaendani na hali yangu. Nilitibiwa mawezi katika wodi namba 5 ya wazazi na dokta Masawe aliyetambulika zaidi ya jina la mkombozi wa wamama, na aliendelea kunitibu kupitia oda ya kutoka Muhimbili kwa jina la Mama TARIMO ambae alisaidiana na dokta. Masawe kwa maelekezo na mama huyu yuko Muhimbili hospitali Walihangaika na hali yangu lakini bado sikupona.
Ndipo Deodath baada ya kuchoka na hospitali alinibembeleza tuelekee LOLIONDO kwa ajili ya kwenda tena kupata nako dawa. Nilimkubalia kutokana na hali halisi ambayo iliendelea kwangu na kuona kama vile kukataa namtesa maana anahangaika kwa ajili yangu na hakuna anayemsaidia hata mmoja na nilikuwa na ndugu pale Moshi lakini hakuna, aliyeungana nae kumsaida alibaki akiendelea kuangaika peke yake hakuna aliyekuwa akisaidiana nae hata kimawazo zaidi ya mama yangu mzazi kuwasiliana na Deo zaidi ya kuendelea kuwasiliana nae kwa njia ya simu, Deo hakupenda kumsumbua mama yangu kwani alimuonea huruma kwa kuwa ni mjane, na hana kazi na pia alishachoshwa na hali yangu sasa hata akimwambia juu ya hali yangu haitasaidia chochote zaidi mama aliendelea kulia tu kila alivyoambiwa juu ya hali yangu hivyo Deo kuamua libaki kama jukumu lake.
Hakuna lakufanya kaka wa watu alikuwa na pikipiki yake kwa ajili ya kwenda nayo mjini kuchukua vyombo vya dukani, hivyo ilimlazimu kuuza hiyo pikipiki ili kupata fedha ya nauli ya kuelekea LOLIONDO. Na ndipo majirani walipoanza kumwambia lazima ufilisike mwaka huu kwa ajili ya mwanamke, si uachane nae kwani wanawake wameisha?deodath akuangalia hilo ingawa hadi wazazi wake walimwambia. Wakamwambia kila siku unashika madamu ya mwanamke hii unaona ni sawa? Aliwajibu :- ndio mimi naona ni sawa kabisa kwa kuwa Mungu ameamua kunipa kwa hiyo nimfukuze? Au nimuuwe? Walimjibu :- Achana nae tafuta mwingine, mbona wapo wazuri zaidi yake achana na mwanamke anayezidi kukufilisi mali zako, ona sasa leo umeuza pikipik kwa ajili ya mwanamke sasa kesho kutwa si utauza nyumba? Niliyasikia hayo niliumia sana lakini la kufanya sina na sikuwa na anaye nipenda hata mmoja kutokana na hiyo hali tofauti na mume wangu, mama mkwe yeye alivumilia kwa ile mara ya kwanza tu lakini siku zilivyozidi kwenda alinichukia kabisa na hadi kufikia kumchukia mwanae kwa ajili yangu.
*******
MWISHO
Tags:
RIWAYA