PENZI LISILO SAHAULIKA 01--- 02

 ZANZIBAR 

"Ben huku machozi yakimlenga lenga hakuamini kabisa kwa kile alichokuwa akikiona mbele yake....Mpenzi wake na mke wake mtarjiwa Adera alikuwa amelala mbele yake katikati ya barabara huku damu zikimtoka puani pamoja na mdomoni na povu furani hivi jeupe nalo lilikuwa likimtoka,Ben aliyaangaza macho yake kulia kushoto akaiona gari ya mrembo huyo ikiwa imepakiwa pembeni.Alitimua mbio kumsogelea Adera mithili ya mwendawazimu akawa amemfikia na kumbeba juu ili amkimbize hospitalini."Ben mpenzi wangu naomba kwa muda huu japo kidogo uniweke chini karibu na hii gari yangu nina machache sana ya kukuambia kabla sijamfuata baba ". Aliongea Adera kwa taabu sana huku akiigeuza geuza shingo yake kuashiria ni kwa kijinsi gani alivyokuwa akipatwa na maumivu."Adera unasemaje Adera??" Aliuliza Ben huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio sana."Ben naomba unipe mkono wako wa kulia". Aliongea Adera na Ben muda huo huo akampa huo mkono nae akaupokea na kuuweka kifuani kwake ."Ben nilitamani sana mapenzi yetu yadumu tuje kuishi pamoja kama mke na mume lakini kwa Sasa imebaki kama ndoto tu isiyokuwa na mwanzo maalumu katikati ya usiku mnene wa giza".Alisema Adera kwa sauti ya chini huku akijitahidi kuyafumbua macho yake yaliyokuwa yametapakaa machozi yenye mchanganyiko wa damu,Ben nae kwa muda huo machozi yalianza kumtoka bila kutarajia."Ben mpenzi wangu najua utaumia sana kumpoteza kipenzi cha roho yako katika mazingira usiyoyatarajia ila kumbuka tu hii ni dunia na ina Kila kitu chenye uhai na sisicho na uhai......ningali bado natamani niwe na wewe katika hii dunia lakini ndo hivyo tena muda wangu na siku zangu za kuishi zimefikia tamati,,tumetoka mbali sana katika safari ya mapenzi yatu ila ndo hivyo tena sina jinsi ya kukuaga kwamba ipo siku tutaonana tena.Siku zote sikujua kama rafiki yako uliyetoka nae mbali angeweza kunifanyia unyama kama huu,ila Mimi nimemsamehe....nimemsameheee!! Nimemsameheee!! Ba......baaa.....baaaaa....bakiii salama mpenzi wangu Bennnn!!!.....?????".Adera hakuwa na kingine cha kuzungumza kwani alibaki kimya na hapo ndipo ile shingo yake ilipolala mazima."Nooooooo!!!......Adera......Aderaaaaaaa??? Adera amkaaaaa!!! Amka Aderaa.....Aderaaaa????????!!!!.

*****************************************************************

Miaka kumi iliyopita kijana Ben kutokana na ugumu wa maisha mara baada ya yeye kuhitimu elimu yake ya kidato cha nne na kushindwa kufanikiwa kuendelea na masomo aliamua kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta maisha .Huko alikwenda kutafuta kazi yoyote ile ambayo ingeweza kumpatia ridhiki ya Kila siku ikiwemo kupeleka mkono kinywani,,,Baada ya kijana huyo kufika huko alianza kutaabika sana kutafuta kazi pamoja na kwamba kwa muda wote ule alikuwa akiishi na rafiki yake kipenzi ambaye nae alikuwa katika harakati za kutafuta maisha.Rafiki yake huyo alikuwa akiitwa Steve na walikuwa wakipendana sana kama ndugu wa karibu .Basi siku zikawa zinasonga hatimaye Ben na Steve wakapata kazi moja ya kusafiri na gari la taka kwa ajili ya kuzunguka mitaani kukusanya taka,,,kazi hiyo waliifanya kwa muda wa miezi miwili na baada ya hapo wakaamua kuacha kazi ili waangalie kingine cha kufanya.Mwaka mmoja baadae Ben alifanikiwa kupata mtaji wake na hivyo akawa amemuomba rafiki yake Steve aende kwingine kwa ajili ya kujitegemea.Steve hakumkatalia rafiki yake huyo alimruhusu nae akawa ameondoka na kuhamia mtaa mwingine mbali kidogo na pale alipokuwa akiishi Steve.Basi maisha yakawa yanazidi kusonga huku Ben Sasa akijitegemea kwa Kila kitu kwani tayari alikuwa na chumba chake mitaa ya Kariakoo.Muda mfupi baadae alifungua kibanda chake cha kuuza vitu mbali mbali ikiwemo mchele,maharage na vingine vingi na hapo ndipo alipoanza kukomaa .Biashara yake hiyo alikuwa akiipenda sana huku akijipa malengo mengine makubwa ya kufika mbali zaidi kibiashara,,,Ndani ya miezi mitano tu tayari kijana huyo alikuwa kashafanikiwa kujitwalia wateja wengi na uhakika,,Si kwamba Ben alikuwa akitumia masuala ya kishirikina katika Biashara yake hiyo hapana! Bali moyo wake wa ukarimu na ucheshi kwa wateja wake ndio uliokuwa ukimpamba na kumpa sifa kedekede katika Biashara yake.Kutokana na kujulikana kwake watu mbali mbali kutoka mitaa mbali mbali walijikuta wakivutiwa sana na kijana huyo na kuwafanya wasiende kokote kununua mchele zaidi ya ule wa Ben.Ilifikia hatua Ben akabatizwa jina la Mr Mchele kutokana na kuuza mchele mzuri na unaovutia.

  Siku moja juma mosi ,Ben akiwa amekaa kwenye kibanda chake alisikia gari ikilia na baadae kuzimwa ikambidi asimame kujua ni kina nani wamekuja maana kwa upande wake baada ya kusikia mlio wa gari alijua ni askari wamekuja kwa ajili ya vitu ambavyo si vizuri.Sasa aliposimama kidogo mapigo ya moyo wake yalipungua baada ya kuiona gari aina ya Yutong ikiwa imepakiwa umbali wa mita ishirini kutoka kwenye kibanda chake.Alishangaa sana akawa anajiuliza kimoyo moyo ni nani yumo ndani ya gari ile,,,Aliendelea kuitazama ile gari bila kupepesa macho na punde si punde alishuka mrembo mmoja ndani ya gari ile mapigo ya moyo wa Ben yakaripuka paaah!! Na akawa anamshangaa sana yule binti.Mrembo yule aliyekuwa amevaa miwani ya aina yake alikuwa mithili ya miss wa dunia nzima huku akijariwa kuwa na urembo wa kimataifa na usiokuwa na mfano,kwa kumuangalia alionekana kama mzungu,mwarabu si mwarabu,Msauzi Afrika si msauzi Afrika yaani kitu hicho kilimchanganya sana Ben lakini akajipiga konde kianaume maana hata wazo la kumtongoza hakuwa nalo kabisa kwa muonekano wake tu na ule wa binti,yaani ilikuwa ni sawa na panya kumpanda paka jike kitu ambacho hakiwezekani kabisa.Basi yule binti akawa anakisogelea kile kibanda cha Ben na baada ya dakika tatu akawa amekifikia.

**********************

"Karibu sana dada yangu hapa kwetu ,nina Mchele nina machoko choko yaani ni wewe tu ".Alisema Ben kwa uchangamfu ikabidi yule binti aivue miwani yake amtazame vizuri Ben.Baada ya kujiridhisha alitabasamu kidogo kisha akatoa noti ya shilingi elfu kumi."Nipimie kilo tano". Aliongea binti yule huku akimtazama tazama Ben aliyekuwa akiyachengesha chengesha macho yake ."Unajua dada yangu hapa duniani ni Bora uwe na moyo uliobeba chuma kuliko kuwa na moyo uliobeba pesa zisizokuwa na amani hahahaha!!". Aliongea Ben kisha akacheka kidogo ."Harafu dada yangu ulipokuwa ukija kidogo tu nikusalimie goodmorning American girl ila nikasita nisije nikapigwa risasi,haya kilo zako dada hizi hapa".Alisema Ben huku akimkabidhi ule mchele binti yule."Ila kaka wewe una vituko kweli haya bwana hii hapa pesa yako".Alisema binti yule."Sawa,dada ubarikiwe sana na Mungu ,aaa! Nimesahau kukuongezea".Haraka haraka Ben alitoa chenchi akampa yule dada baadae akampimia na mchele kidogo kama nyongeza yake kitu ambacho kilimfanya yule binti asichoke kumtazama kijana huyo."Asante kaka yangu kwa ukarimu wako,hivi unaitwa nani?" Aliuliza binti ."Naitwa Benjamin au Ben kwa kifupi."Mimi naitwa Adera naishi humu humu Kariakoo mtaa wa pili kutoka hapa."Haya dada usijali tupo pamoja na karibu tena". Aliongea Ben huku akiukusanya kusanya mchele wake."Asante kaka yangu".Alisema Adera kisha akaanza kuondoka,,,Sasa baada ya kuifikia gari yake alisimama mbele ya mlango wa gari bila kuingia ndani kwa takribani dakika tano baadae akazipiga hatua kumfuata Ben pale kibandani kwake tena,alipofika alisimama mbele akaita "Ben" Ben akaitika huku akisimama."Niambie dada yangu mbona umerudi au nimesahau kukurudishia chenchi ?" Aliuliza Ben kwa sauti ya huruma iliyoutetemesha moyo wa Adera."Hapana kaka yangu,nilisahau kukusalimia,,,Ben mambo!!" Aliongea Adera huku akijishika kifuani."Poa tu dada yangu".Alijibu Ben kwa uchangamfu."Haya Poa kaka Ben nitakuja siku nyingine tena".Adera alitembea kwa kusita kidogo baadae akatembea haraka na kufanikiwa kuifikia gari yake akapanda ndani.Humo binti huyo alijishika tama huku akiikumbukia kumbukia sauti ya Ben asijue kabisa ni kipi kimeupata moyo wake tena kwa ghafla kiasi hicho ."Huyu kaka mbona mpole na mcheshi kiasi hiki?? Sijawahi kuona kijana wa namna hii hapa Dar es salaam".....

ITAENDELEA........

PENZI LISILOSAHAULIKA

      SEHEMU YA 2.

                   Adera hakuweza kabisa kupata majibu kwa maswali yake yale aliyokuwa akijiuliza.....Alibaki kimya kwa muda wa dakika saba kisha akaulalia usukani wa gari yake mawazo chungu nzima yakawa yanazidi kumuandama na asijue hata cha kufanya binti wa watu .Aliinuka kidogo baada ya kuulalia usukani wa gari yake kisha akaiwasha na kuondoka eneo lile akiwa na duku duku kubwa sana moyoni mwake.Baada ya dakika kumi alifika nyumbani kwao akauweka pembeni ule mchele kisha haraka akaelekea chumbani kwake kwenda kulala.Kwa vile mama yake alikuwepo ndani ya nyumba ile alishangaa sana baada ya kumuona bintiye Adera akiwa katika hali ile,alijiuliza ni kipi kimemsibu ila akaona ni bora amfuate humo humo chumbani kwenda kumuuliza mwenyewe.Basi mama Adera akawa amenyanyanyuka pale sebuleni alipokuwa amekaa akazipiga hatua hadi chumbani kwake na Adera,baada ya kufika alikaa pembeni mwa kitanda akawa anamtizama kwanza mwanae huyo aliyekuwa ndani ya dimbwi zito la mawazo kwa huruma."Adera?" Aliita kwa mara ya kwanza lakini Adera wala hakusikia pamoja na kwamba alikuwa macho na alikuwa amelala chali kwa kuiweka miguu yake kwa mfumo wa nambari nne."Adera?...Adera!!" Aliita tena kwa mara mbili mfululizo lakini Adera bado hakuweza kusikia chochote kile,sasa mama yake ikambidi amuite kwa nguvu huku akimtikisa."Aderaaa?" Adera aliitika kwa kukurupuka mithili ya mtu aliyeshtushwa usingizini akawa anayaangaza na kuyafumba fumba macho yake."Mwanangu Adera kipi kimekusibu na kwa nini upo katika hali hiyo Mwanangu?" Aliuliza mama Adera kwa sauti ya upole."Hapana mama mbona Mimi nipo kawaida tu!!" Alisema Adera kwa kuzuga."Mwanangu hapana haupo sawa hata kidogo,mimi wewe nimekuzaa na ninakufahamu kwa Kila kitu,naomba usinifiche Mwanangu maana kwa kufanya hivyo utapelekea hata Mimi mama yako nianze kuumia maana huwa sipendi kabisa kukuona ukiwa katika hali ya unyonge na huzuni". Aliongea mama yake huku akizidi kumkazia macho."Ni kichwa tu mama yangu kinauma ila kidogo tu". Aliongea Adera."Sasa Mwanangu si uende hospitalini au?" Aliuliza mama yake."Hapana kitapoa tu kwa Sasa naomba mama nipunguzike tu humu humu kitapoa chenyewe".Alijibu Adera."Sawa Mwanangu ngoja Mimi nikuache upumzike,huyu Alice ngoja nikamwambie akuchemshie chai ili jioni hii upate kuburudika kidogo na maumivu yapoe au siyo mwanangu?" Aliuliza mama yake huku akisimama."Acha tu mama".Alijibu Adera na hapo mama yake akabaki kimya na kutoka moja kwa moja humo chumbani.

Upande mwingine alionekana Steve akimalizia kuzipiga hatua kwenda ghetoni kwa rafiki yake Ben jioni ile,na ilionekana tu ndani ya moyo wake alikuwa na duku duku kubwa maana wakati anatembea alikuwa akitabasamu na wakati mwingine kujikuta akicheka peke yake.Baada ya kufanikiwa kuufikia mlango wa chumba cha Ben alianza kubisha hodi na hazikupita hata dakika tano akawa amefunguliwa mlango na Ben mwenyewe nae akawa ameingia moja kwa moja hadi ndani."Ben Sasa rafiki yangu umezidisha ugumu,yaani baridi lote hili hata demu huna? Duuh utakuja kufa rafiki yangu acha hizo". Aliongea Steve huku akikaa kwenye kitanda cha Ben kilichokuwa kimepakana na mlango wa kuingilia."Wanawake rafiki yangu wenyewe wapo tu katika hii dunia na hilo Mimi nalifahamu ila acha kwa sasa nitafute kwanza pesa,kuhusu baridi kuna blanketi nitajifunika tu na maisha yataendelea". Aliongea Ben huku akijikuna kuna kichwani."Siyo kihivyo rafiki yangu au ulizinguliwaga nini?" Aliuliza Steve kwa kuzuga ."Ni kweli rafiki yangu,mimi mapenzi niliamua tu kuwaachia wenyewe maana Mimi sina bahati ya kupendwa na nimeshaumizwa vya kutosha na ndio maana nikaona ni bora nitafute pesa tu mapenzi acha wayafanye wenye bahati nayo sisi wengine hatuna bahati nayo". Aliongea Ben kwa sauti ya masikitiko kidogo."Siyo wasichana wote Ben wapo hivyo wengine mbona wapo poa tu". Aliongea Steve huku akimtazama rafiki yake huyo kwa macho ya huruma sana."Siamini rafiki yangu ila ninachokiamini mimi kama bahati yangu ipo basi kuna siku itaonekana dhahiri machoni mwangu". Aliongea Ben."Sawa rafiki yangu ....sasa ujio wangu hapa,nimekuja kukuhabarisha jambo moja ambalo nimelipata na ni bahati sana kwa upande wangu". Aliongea Steve kisha akameza fundo la mate."Jambo gani hilo Steve?" Aliuliza Ben huku akimkazia macho."Unakumbuka ile siku niliyokuambia nina vyeti mpaka vya vyuo kikuu tena kwa degree ya masuala ya kibiashara na uchumi?" Aliuliza Steve na kumfanya Ben abaki akiumung'unya tu mdomo wake."Ndio Steve nakumbuka vipi umeshalamba shavu nini?" Aliuliza Ben."Aise Mwanangu Mungu ni mkubwa,baada ya kuhangaika hatimaye na Mimi sasa nimepata kazi na shavu la maana sana,nimeipata hiyo kazi katika kampuni moja la usindikaji wa vyakula na vitu mbali mbali,na nisikufiche mshahara ambao nitakuwa nikiupata utakuwa ni kama kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mwezi". Aliongea Steve ,mapigo ya moyo ya Ben yakaongezeka."Hongera sana rafiki yangu naona sasa kwa upande wako maisha yameshakuwa mazuri,naomba unikumbuke na Mimi pale tu panapowezekana japo mimi elimu kwa sababu ya umaskini wangu ilinipita kushoto". Aliongea Ben kwa sauti ya upole na iliyojaa masikitiko.

**********************

"Usijali rafiki yangu mimi na wewe urafiki wetu ni wa muda mrefu sana maana tumekuwa marafiki tangu tukiwa sekondari hivyo siwezi kukuacha hivi hivi jamaa angu". Aliongea Steve na kumhakikishia rafiki yake kwamba hatomuacha kwa vyovyote vile."Haya Ben ngoja mi niende tutawasiliana".Baada ya kuyaongea hayo ,Steve aliinuka pale kisha akatoka nje akiwa ameambatana na Ben wakawa wanatembea taratibu huku wakipiga story za hapa na pale.Ben alipohakikisha amemtoa mbali kidogo Steve alirudi tena ghetoni kwake.Basi masaa ya jioni nayo naliyoyoma sana hatimaye giza likaingia na usiku sasa ukawadia.Kulipopambazuka kesho yake ilikuwa ni siku ya juma pili ,siku ambayo Ben huwa haendi kazini kwake yaani kibandani kwake maana siku hiyo kwa asilimia zaidi huwa anaitumia kwa ajili ya kumuabudu Mungu na alikuwa akiithaminisha sana siku hiyo,,,,Kutokana na hivyo,siku hiyo nayo ilipita hatimaye juma tatu ikafika.....juma tatu ambayo ilionekana kuwa kama ni tulivu sana hasa kwa upande wa Ben.Asubuhi na mapema katika siku hiyo aliwahi kibandani kwake kwa ajili ya kwenda kuendelea na biashara yake.Baada ya kufika huko alipanga vizuri vitu vyake vyote na Kila kitu kilipokaa vizuri ,Ben alikaa ili asubirie wateja wake.

Sasa akiwa hajui hili wala lile.....kwa mbali walionekana askari watano wakiwa wanakuja mbele ya kibanda cha kijana Ben na wote kwa pamoja walikuwa wameshikilia bunduki.Walipofika pale walikizingira kile kibanda na kisha wakamkurupusha Ben bila yeye kutarajia."Kijana kama ulivyo,simama hivyo hivyo". Aliongea Askari mmoja huku akionekana kutokuwa na utani hata kidogo,Ben alisimama huku akitetemeka asijue cha kufanya."Sogea pale mpuuzi wewe.....unaendekeza biashara inayotokana na ujambazi?".................

ITAENDELEA...... 

Post a Comment

Previous Post Next Post