PENZI LISILO SAHAULIKA 03---04

"Jamani kwani kosa langu ni lipi hadi mnikamate namna hii ?" Alihoji Ben huku akitia huruma sana."Tangulia utajua huko huko usijifanye kujitoa ufahamu".Afande mmoja alimjibu huku akimshikilia kwa nguvu nyuma ya suruali yake ambayo tayari ilikuwa imeshaanza kuteremka chini.Ben kwa huruma aliutazama ule mchele wake akatamani awaambie wamuache walau aukusanye vizuri na kuufunika kwa gunia kuu kuu lililokuwepo pale lakini akashindwa kufanya hivyo na kubaki akiwa kimya tu,wale maaskari baada ya kumkamata vilivyo walienda nae hadi ndani ya gari wakapanda kisha wakaondoka.Huku hayo yakiendelea Steve rafiki yake na Ben alikuwa ndani ya ofisi yake mpya kama meneja masoko,sasa pamoja na kwamba taarifa za kukamatwa kwa Ben alizipata lakini wala hakuwa na muda kabisa wa kujua hata cha kumsaidia yaani ilionekana kama amemsahau vile."Steve nasikia rafiki yako Ben yule muuza mchele amekamatwa kwa tuhuma za wizi na uporaji...sasa sijajua wewe kama rafiki yake unamsaidiaje huyu jamaa maana kwa ninavyojua atasota sana mahabusu endapo tu atakosa mdhamini".Alisema kijana mmoja hivi mfanyakazi mwenza na Steve."Kila mtu ataubeba msalaba wake ,sasa kama ameamua kutojishughulisha na kile alichonacho na kuamua kuanza kuiba atajua mwenyewe na Mimi kama Steve kwa kweli siwezi kumsaidia huyu jamaa hata kama ni rafiki yangu,Labda kama angekuwa amesingiziwa". Aliongea Steve huku akiwa ametazama pembeni na wakati mwingine alikuwa akitabasamu kabisa bila ya wasiwasi.Ukweli ni kwamba hakukuwa na kosa lolote ambalo Ben alilifanya ila kuna kitu kilichorwa ili kumrudisha shimoni yaani kumfirisi kabisa kwa kile alichokuwa amejikusanyia,na hili lilipangwa na marafiki zake Ben marafiki ambao walikuwa ni wa karibu sana nae ."Sasa Steve si umuonee huruma tu,kumbuka yule ni rafiki yako na mumetoka nae mbali sana na isitoshe mumetoka katika Kijiji kimoja huko Tanga,msaidie yule ni kama ndugu yako Steve". Aliongea tena yule kijana."Bwana ee,kama wewe una muonea huruma basi msaidie,si unapesa ase msaidie tu wala tusitake kurumbana sana....kwa upande wangu nimesema sipo tayari kumsaidia harafu wewe una bwabwaja tu eti msaidie yule ni kama ndugu yako,upumbavu mtupu,harafu hii mida ni ya kazi ingependeza kama utaniacha niendelee na shughuli zangu maana naona huna cha maana zaidi ya kunipigia kelele na kunipotezea muda wangu bure". Aliongea Steve na yule kijana kwa aibu isiyokuwa na kifani akaona ni bora atoke tu humo asije akazua mambo mengine.Baada ya kijana huyo kutoka ,Steve alitabasamu kisha akaachia kicheko baadae akaichukua simu yake ya mkononi,aliibofya mara mbili akaiweka sikioni."Oya fanya fasta sitaki mpoteze muda,hilo dau nitalivunja mkileta mambo ya kinunda".Alizungumza maneno hayo haraka akakata simu yake.
 Kwa upande wa Adera mchana ule bado chungu nzima ya mawazo ilikuwa imekiandama kichwa chake ,Adera alionekana kama amevamiwa na ugonjwa usiojulikana na tena ugonjwa hatari zaidi ya ukimwi.....usema ukweli hisia Kali za mapenzi tayari zilikuwa zimeshauteka moyo wake tena kwa zaidi ya robo tatu ya huo moyo wake,Alitokea kumpenda sana Ben na hilo pekee lilitambuliwa kwenye himaya ya moyo wake na kumfanya asile asinywe kwa sababu ya kijana Ben."Adera ....Adera.....Aderaaa??" Mama yake aliita kwa mara tatu mfululizo baada ya kumkuta binti huyo akiwa amekaa ndani ya garden yao ya maua huku akiwa amejishika shavu."Adera mwanangu hivi umefanyaje lakini? Tangu juzi umekuwa katika hali hii ya mawazo kulikoni binti yangu,au kuna mtu amekuchanganya humu ndani?" Aliuliza mama yake muda huo huo kijana mfanyakazi wa maeneo ya nyumba yao akisogea karibu ."Mama labda umuulize wewe maana Mimi nimejaribu kumuuliza nikawa kama nimechokonoa mzinga wa nyuki na ndio maana nikasogea mbali kuendelea kushuhudia picha la kihindi linavyokwenda". Aliongea kijana huyo machachali kwa uongeaji aliyekuwa akijulikana kwa jina la Jeff ."Hayakuhusu wewe kijana,unaponiona nipo na malkia wangu hutakiwi kuhoji mambo yako ya kipuuzi kama hayo....yaani bado umesimama tu,tokaaaa!! Kuna mlinzi wa getini kule nenda kapige nae story huko,usiingilie mambo yasiyokuhusu". Aliongea mama Adera kwa sauti ya ukali na kumfanya Jeff aondoke haraka hapo huku akigeuka geuka mithili ya komediani."Mama nitakuambia tu ila kwa muda huu niache kwanza niyamalize mwenyewe". Aliongea Adera na hapo ndipo mama yake alipowaka kwa hasira kali."Pumbavu...mshenzi mkubwa wewe,yaani unanificha mimi mama yako niliyekunya nikakutoa wewe!! Sasa sikia mimi nimetangulia kuliona jua kitambo sana na hicho unachonificha nitakijua tu,ila kaa ukijua kama kuna kijidubwana cha kijana kimeanza kukusumbua na kukufanya uwe katika hii hali aisee nikikijua walau halali yangu maana nitakitoa ubongo bila kupepesa macho". Aliongea mama Adera kisha akasonya kwa nguvu na kumfanya Adera ashtuke na kuanza kutumbua macho huku akijishika kifuani.Mama Adera baada ya kumaliza kuyazungumza hayo hakuwa na muda wa kupoteza kwani aliondoka muda huo huo na kumuacha Adera akiwa hajui kinachoendelea.

Steve baada ya kutoka kazini kwake tayari jioni ilikuwa imeshawasiri,jioni hiyo akaelekea moja kwa moja hadi nyumbani kwake .Baada ya kufika huko alimtuma mfanyakazi wake wa ndani aliyekuwa akiishi nae amletee kiti nae akafanya hivyo na Steve akawa amepumzika karibu kabisa na nyumba yake.Dakika kama ishirini hivi zilipita hatimaye kwenye muda wa saa kumi na nusu hivi zilikuja gari mbili aina ya Tax tena kwa Kasi sana zikasimama karibu na usawa wa pale alipokuwa amekaa Steve,,Haraka haraka walishuka jamaa kumi kwenye hizo Tax,watano Tax moja na wengine Tax ile nyingine wakawa wanatembea kibabe kumsogelea Steve.Jamaa hao wote kwa pamoja walikuwa wamevaa makoti meusi marefu pamoja na miwani nyeusi za jua machoni mwao,jamaa wawili katika ya hao walikuwa wameshikilia briefcase mbili mikononi mwao.Sasa walipomfikia Steve walisimama kwa kumzunguka huku lijamaa limoja likisimama nyuma yake na kukaa kibabe likiwa limeshikilia bastora mkononi,,,Steve akiwa amekaa huku amekunja nambari nne alitoa ishara ya kichwa,na hapo hapo zile briefcase zikafunguliwa . Briefcase moja ilikuwa na noti nyingi za elfu kumi kumi na nyingine ilikuwa na madawa ya kurevya yaliyokuwa kwenye vijimfuko vingi vidogo vidogo,baadae briefcase hizo zikafungwa."Babu kubwa washkaji,sasa huo mzigo nataka kufikia kesho uwe umeshauzwa na hiyo pesa niipate siku hiyo hiyo,sawa?" Aliuliza Steve."Sawa mkuu".Waliitikia kwa pamoja ."Okey mnaweza kwenda".

********************

Kwa upande wa Adera baada ya kuona uvumilivu umemshinda aliamua kuinuka pale alipokuwa amekaa akawa anatembea haraka haraka kuusogelea ule mlango wa geti,gari yake hakuwa na muda nayo kabisa.Sasa baada ya kuufikia mlango wa geti hilo mlinzi alimzuia baada ya kumuona akitaka kutoka fasta bila hata ya kuongea chochote."Binti muda kama huu mama yako si ameshakuambia hataki kukuona ukitoka humu ndani,sasa niambie unataka kwenda wapi?" Aliuliza mlinzi huyo huku akimkazia macho Adera ......ilimbidi Adera atunge maneno ya uwongo kumuambia."Samahani naomba uniruhusu nitoke maana nataka niwahi haraka dukani kununua dawa,kichwa kinaniumaa!!" Alijibu Adera ."Si unitume mimi nikakuletee hizo dawa kulikoni kwenda wewe ili hali unaumwa! Aliongea mlinzi."Tafadhari sana mlinzi wangu naomba unielewe niruhusu niende mwenyewe sitokawia kurudi".

INAENDELEA........................... 
PENZI LISILOSAHAULIKA.

                    SEHEMU YA 4.
     
                  
"Adera kumbuka hiki kibarua nimepewa na mama yako tena kwa masharti magumu na wewe hilo unalifahamu kabisa,sasa kwa kusema hivyo unaweza kunisababishia matatizo makubwa sana mdogo wangu....na ukizingatia giza limeshaanza kuingia tayari".Alisema mlinzi yule baada ya Adera kumsihi amruhusu atoke ndani ya geti hilo."Hivi we mlinzi una akili kweli wewe ? Mi nadhani huna akili timamu hata kidogo, na kaa ukijua mimi hapa ninao uwezo wa kukusababisha hadi ukafukuzwa kazi kwa namna yoyote ile,sasa we endelea na misimamo yako ya kipumbavu,pisha nipite mie".Adera alimpushi kwa nguvu mlinzi kisha akatoka haraka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kukimbia kimbia mpaka akatoweka ndani ya maeneo ya nyumba yao.Alipita kwenye kinjia kimoja cha uchochoroni baadae akakata kulia na kunyoosha haraka hadi kibandani kwa Ben.Sasa baada ya kufika huko kwa bahati mbaya hakufanikiwa kumkuta Ben wala mizigo yake hapo maana tayari ilikuwa ni jioni mno na yeye akilini mwake akajua huenda Ben tayari amesharudi kwake kwa ajili ya kuusindikiza usiku.Cha kufanya hakuwa na muda wa kupoteza pale aliondoka mara Moja akawa anasonga mbele zaidi....aliyaangaza macho yake nyuma baadae kulia akamuona mmama mmoja akaamua kumfuata.Mama huyo alikuwa ameuegemea ukuta wa nyumba moja kuu kuu iliyojengwa kwa matofauli ya bloko."Mama shikamoo!! Alisalimia Adera huku akigeuka geuka utadhani alikuwa akihisi kuna mtu anamfuatilia."Marahaba mwanangu mzima wewe?" Aliitikia mama huyo wa makamo ."Mi mzima tu mama yangu,mama hapa nilipo nina shida moja naomba unisaidie kama hutojali".Alusema Adera kwa sauti ya upole."Sema tu mwanangu wala usijali". Aliongea yule mama na kumfanya Adera atabasamu kidogo."Mama unamfahamu yule Ben muuza mchele kwenye kile kibanda?" Aliuliza Adera ."Ndio namfahamu Ben,si kale kacheshi na kapole kembamba kembamba hivi?"......"Ndio ndo huyo mama yangu,sasa naomba unielekeze anapoishi maana nina shida nae tena mhimu sana". Aliongea Adera haraka haraka huku akiendelea kugeuka geuka kwa woga."Aha! Unaiona ile nyumba yenye rangi nyeupe?"....."Ndio naiona"...."Sasa isogelee hiyo harafu utakapoifikia kata kushoto utakutana na geti jekundu,na ukiingia humo Ben bila shaka kama yupo utamkuta maana ndimo makazi yake yalimo". Aliongea mama yule,Adera akatabasamu kwa furaha kubwa sana."Asante mama yangu ubarikiwe".Adera alichomoa noti ya shilingi elfu kumi kwenye ile suruali ya jinz aliyokuwa ameivaa kisha akampa mama yule na baada ya hapo akamuaga na kuondoka.
Kule mahabusu mpaka jioni inaingia bado Ben hakujua hatima yake ni ipi na kosa lake ni lipi lililomfanya mpaka wakamkamata mithili ya mnyama,alijaribu mara kwa mara kuhoji ni kipi amekifanya kilichokibaya lakini hakuna aliyemwambia ukweli zaidi ya kumtuhumu kwamba yeye ni mwizi na biashara yake ile ya mchele anaiendesha kwa magendo ya wizi,,Na huo ndio uliokuwa msimamo wao na wakampa masharti kwamba ili wamuachie ni lazima atoe pesa za kitanzania zisizopungua milioni kumi kama dhamana yake na wakamuambia hadi kufikia kesho yake kuanzia mida ya saa saba za mchana ,endapo atakutwa bado hajazitoa hizo pesa basi atafungwa moja kwa moja .Ben hizo pesa wala hakuwa nazo kwani kwenye akaunti yake alikuwa na laki saba tu tena zingine zikiwa ni za mtaji wake."Ukweli ndio huo walimwengu wenzangu,pesa niliyo nayo ni laki saba tu ila kama mtakubali kuipokea nipo tayari kuwapa ila mkikataa basi nipo tayari mnifunge maana ndivyo mnavyotaka".Maneno hayo aliyaongea Ben baada ya maafande kumsihi atoe milioni kumi kama dhamana yake ya kuwa huru."Kijana sisi msimamo wetu ni ule ule kwamba iwapo utashindwa kuzitoa hizo pesa mpaka kufikia kesho majira ya saa saba za mchana basi usitulaumu".Askari mmoja aliyaongea hayo na baadae Ben wakamtwaa hadi ndani ya chumba kimoja cha giza wakamuacha humo.

  Kwa upande wa Adera baada ya kuifikia ile nyumba alipita ndani ya lile geti akawakuta wakaka wawili wakifua,aliwasalimia kisha akasimama mbele yao huku akiwa amejishika kiunoni."Samahani kaka zangu".Alisema Adera kwa sauti nyororo,wale jamaa wakamkazia sana macho."Bila samahani dada".Waliitikia kwa pamoja."Mnamfahamu Ben?" Aliwauliza."Ben? Ben ndo nani mbona hapa hakuna anayeitwa Ben?" Waliongea kisha wakanong'onezana."Dada Ben sisi hatumfahamu labda utakuwa umekosea nyumba maana hapa hakuna mwenye hilo jina ". Waliongea na kumfanya Adera azidi kuchanganyikiwa zaidi,alijiuliza au amekosea kweli nyumba,,,akiwa anajiuliza kimya kimya wale jamaa wakamtazama tena."Dada ila wewe ni mrembo unaonaje ukiwa na mimi?" Jamaa mmoja aliuliza Adera akamsonya kwa hasira."Kaka sikujui hunijui,naomba tuheshimiane,hata kama heshima inagharamiwa nipo tayari kukuongezea kipato chake". Aliongea Adera muda huo huo mama mmoja akaonekana akitoka ndani ya chumba kimoja kilichokuwa upande wa kushoto nyuma kabisa ya nyumba zile zenye mchoro wa "L".Alisogea hadi karibu na Adera."Dada kulikoni?" Aliuliza mama yule."Eti mama yangu Ben yule muuza mchele anaishi hapa?" Aliuliza Adera."Ben muuza mchele!!!!" Aliongea mama huyo kwa mshangao."Ndio".Alijibu Adera."Ben huwa anaishi hapa hapa tena chumba chake kile kulee". Aliongea mama yule na kumfanya Adera ageuke na kukitazama chumba kile huku akiwa na shauku ya kukifuata....Sasa wale vijana baada ya kuona wameumbuka walianza kunyanyuka na kuondoka mmoja mmoja kimya kimya."Asante sana mama ngoja Mimi niende po kwenye hicho chumba". Aliongea Adera mama yule akamkazia macho."Ila sidhani kama Ben yupo maana leo asubuhi walikuja maaskari kibandani kwake wakamkamata na pia nasikia ili wamuachie anapaswa kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi". Aliongea mama yule."What???!! What??? asante mama,asante mama".Adera aligeuza akatoka ndani ya lile geti mbio mbio kuelekea kwenye kituo cha polisi .Tayari giza lilikuwa limeshatanda ila Adera hilo wala hakulijari kabisa muda huo alikuwa akiuona ni kama muda wa majira ya mchana tu.Alifika huko kama mishale ya saa moja na nusu,ile anajitazama miguuni mwake kumbe hakuwa amevaa chochote kile , alikuwa yu peku ila hilo nalo akalipotezea,uzuri simu yake kubwa alikuwa nayo."Afande shikamoo nina shida na wewe". Aliongea Adera baada ya kumfikia Afande mmoja hivi aliyekuwa akizunguka zunguka."Bila samahani binti,vipi mbona unahema sana?" Aliuliza Afande yule huku akimkazia macho Adera."Haaaa!! We si ni binti wa marehemu Mr Gambo mfanyabiashara mkubwa na mtoto wa bi Marry ?" Aliuliza Afande baada ya kumtambua vilivyo Adera."Ndio mimi ila hilo wala lisikutishe sana hapa nimekuja kwa jambo moja tu".

**********************

"Jambo gani hilo? Au wamekuibia!"alisema Afande huku akimmezea mate kimya kimya Adera maana kiukweli binti huyu kama kuumbika tu alikuwa ameumbika siyo Siri,ukikutana nae kama wewe ni mwanaume rijali lazima utammezea mate tu na kutamani uwe nae hata kwa dakika mbili tu kitandani."Hawajaniibia wala nini!! Hapa nimekuja kumuulizia kijana mmoja anaitwa Ben naomba aliyemkamata na kuweka mahabusu niitie nizungumze nae". Aliongea Adera na kumfanya Afande yule ashtuke kama amekurupushwa usingizini."Ben? Ben ni nani yako?" Aliuliza Afande."Ni rafiki yangu wa mhimu sana kwani tumemaliza nae chuo na tulisoma wote". Aliongea Adera kwa kupambiza uwongo."Ahaa Sawa,ila siyo mpenzi wako si ndiyo?" Aliuliza Afande."Afande we fanya kile nilichokuagiza masuala ya kuanza kuniuliza swali kama hilo utaenda kinyume na maada". Aliongea Adera na hapo yule Afande akaenda hadi ndani ya chumba kimoja na punde si punde akatoka na Afande mmoja hivi mwenye kitambi."Haaa!! We si ni Adera?". Afande yule aliuliza kwa mshangao."Ndio ndo mimi ,sasa Afande nimekuja unisaidie jambo moja,naomba umtoe Ben niondoke nae gharama zote nitatoa mimi tena ninaweza toa hapa hapa kwa njia ya M-PESA". Aliongea Adera,afande yule mwenye kitambi mimacho ikamtoka mithili ya ile ya chura aliyekanyangwa na taili la gari."Aaaaa .....aaaah!! Saa...saa..Sasa Adera pesa,kitu gani wewe,,,ila huyo Ben kwani ni nani yako???".

ITAENDELEA.................

SHARE..........
LIKE................
COMMENT............ 

Post a Comment

Previous Post Next Post