“Hata kama amekupiga lakini huwezi kumfunga mume wako, ondoka lakini si kumfunga, ni mume wako wa ndoa na si hawala uliyemuokota okota huko mtaani, hao wanaokushauri kuwa usifute kesi wanakudnaganya, hivi unafikiri kama akifungwa na kuozea jela utapata faida gani?” Mama aliniambia, nilikaa hospitalini kwa wiki moja baada ya kutolewa kizazi, niliporuhusiwa sikurudi nyumbani kwangu, mume wangu alishatoka kwa dhamana lakini bado kesi ilikua inaendelea.
Kwa kuhofia hadhi yake, kwa kuhofia kufungwa kwani mashahidi walikua wengi mume wangu aliniomba sana msamaha, alituma ndugu zake, mshenga na viongozi wa diniili kuniomba msamaha. Walinishauri sana kuachana na kesi yangu kwani hata kama nikishinda sitapata faida yoyote.
“Huna kazi, huna chochote, mume wako akifungwa unafaidika nini? Unajua kuwa akifungwa anapoteza kazi, hivi hufikirii hata wanao kwakweli, unaona kama ni sawa tu kuwa watoto wako hawatasoma kwakua Baba yao kafungwa?”
Mama aliniambia, Baba alikua mkali sana kuhusu mimi kurudi kwa mume wangu na kumsamehe. Wadogo zangu walinisema sana lakini nilimuelewa zaidi Mama, baada ya kupona sikuona sababu ya kuendelea na ile kesi. Mume wangu alibadilika, alianza kunihudumia, alikua ananitumia matumizi, pamoja na kufanya kazi lakini bado alikua akinihudumia na kila siku alikua akiniomba msamaha akiniambia kuwa kajifunza kutokana na makosa hatarudia tena. Kwa miezi miwili alikua ni mtu wa kunipigia simu asubuhi, mchana na jioni, mtu wa kuomba msamaha, hakuwahi kunifokea nha hata nilipokua nikimjibu vibaya basi alikua akiniomba msamaha yeye.
Kuna upendo alikua akiuonyesha mpaka nilianza kumuamini, sikua na sababu tena ya kuendelea na ile kesi, niliifuta na baada ya kama miezi mitatu hivi tulirudiana. Mume wangu alibadilika sana, hakua akinipiga, aliniacha kufanya kazi kwa uhuru, aliahca kunionyesha wanawake zake, kila kitu kilikua kizuri sana. Kwa mwaka mzima niliishi na mume wangu bila kuwa na tatizo lolote, lakini mwaka wa pili baada ya kutolewa kizazi Mama mkwe alianza kuumwa, alikuja nyumbani kwaajili ya matibabu na mimi ndiyo nilikua nikimhudumia.
Sikujua kama ndugu wa mume wangu wana kisasi na mimi na wananichukia mpaka kipindi hiki. Alikuja na wifi yangu ambaye alikua kaolewa ndoa ikamshinda akaachika, alikuja kumuuguza Mama yake. Hapo ndipo maneno yalianza, kumbe bado walikua na hasira za mimi kumpeleka mtoto wao mahabusu, kitendo cha mume wangu kukamatwa na kulala ndani kiliwakera sana. Yalianza maneno ya chini chini, dharau za hapa na pale kila mara Mama mkwe akinitenga, kukataa chakula nilichopika mimi na mambo mengine madogo madogo.
Mimi nilivumilia kwani nilijua kuwa ni mambo ya kupita tu, sikutaka kuyapa kipaumbele hata kwa mume wangu sikulalamika. Lakini baada ya wao kuona kama mimi silalamiki wala sijali walianza kufanya mambo waziwazi. Wakijua kabisa kuwa mimi nimetolewa kizazi na siwezi kupata mtoto tena Mama mkwe alianza kulalamika kuwa anataka mjukuu mwingine, alianza kusema kuwa watoto wawili hawatoshi. Mwanzo alikua akiongea nasikia kwa majirani lakini alipoona sijali alianza kuongea waziwazi akimshurutisha mume wangu kuwa anahitaji mkujuu mwingine.
“Wewe ni Mwanaume unaweza kuoa mwanamke mwingine, huna haja ya kubaki na mtu ambaye hazai!” Siku moja tukiwa mezani Mama mkwe wangua liongea, mume wangu alimtuliza na kumuambia kuwa hayo mambo yashapita yeye hahitaji mtoto mwingine.
“Hata kama hutaki lakini mimi nataka mjukuu, huyu mke wako aliamua mwenyewe kutoa kizazi chake, angekataa unafikiri madaktari wangekitoa, kwanini hakukushirikisha, wakati anatoa kizazi eti wewe uko jela, walitaka kukufunga ili wabaki na mali lakini bado unaendelea kuishi na mwanamke wa namna hii!”
Mama mkwe aliongea, mume wangu alibaki kimya na kumuacha Mama yake kuongea meneno mengi ya kashfa, si Mama yake tu hata mdogo wake aliongea na mume wangu hakujibu chochote. Nilikasirika na kwenda chumbani, niliwaacha wakati wanakula na kwenda chumbani nikaanza kulia. Mume wangu alikaa huko mpaka usiku wa manene ndipo alirudi, alinikuta abdo niko macho nimekaa kitandani nalia, hakunisemesha alipanda kitandani na kulala, nilikaa macho mpaka kesho yake, sikua nikiumizwa na maneno ya Mama mkwe wangu kwani nilishajua kuwa ana hasira na mimi, nilumizwa kwa namna ambayo mume wangu alikaa kimya bila kuniteta.
Hali ile iliendelea kwa wiki mbili hivi, mume wangu bado alibaki kimya, ni kama alikua anafurahia hiyo hali kwani aliwasikiliza na wakati mwingine kucheka bila kuchangia. Nilivumilia nikashindwa, siku moja usiku baada ya kuwaacha sebuleni wakila niliamua kuuliza.
“Hivi mbona unaacha Mama yako ananitukana namna hiyo?” Nilimuuliza, alijifanya kama hajalewa swali na kutaka kulipotezea lakini nilimbana tena ili aongeee.
“Kwahiyo unataka nini? Unataka nimjibu Mama yangu na kumkosea heshima unataka niseme nini? Au unataka nimfukuze Mama yangu?” Aliniuliza kwa hasira.
“Hapana, lakini angalau….”
“Angalau nini, hivi unanitaka nini wewe mwanamke, nimekuvumilia mwaka mzima nimebadilika lakini naona hufuraghii, umeanza kisirani chako na nikikupiga kidogo uanenda kutoa mimba sijui na kutoa kizazi, sasa kizazi huna sijui sasa hivi utaenda kutoa utumbo!”
Niliumizwa sana na maneno yake kwani kwa namna alivyokua anaongea ni kama vile alikua ananishutumu mimi kwa kutoka kwa kizazi changu, alikua anaungana na Mama yake.
“Kwahiyo unakubaliana na Mama yako?” Nilimuuliza.
“Ndiyo, kwani Mama kaongea nini kibaya, mbona kila kitu kipo wazi tu, kizazi ulitoa ili ufanye umalaya wako bila kubeba mimba, wanawake wangapi wanapigwa na waume zao lakini hawatoi vizazi!” Mume wangu aliongea hukua kitoka nnje kwa hasira, hakurudi tena, alienda kulala chumba cha wageni, asubuhi aliamka kanuna, hakunisemesha aliingia chumbani akavaa nguo zake na kuondoka.
Nilikua kama mimi ndiyo nimemkosea, mum wangu alibadilika kabisa, hakutaka tena kuongea na mimi, alikua akiwaachia matumizi ndugu zake, akirudi anacheza na watoto lakini mimi hanisemeshi. Niliamua kumchunia kwa muda lakini nilishindwa, hali ilizidi kuwa mbaya siku hadi siku, hata chakula nilichopika alikua hali. Baada ya kuona vile niliamua kujishusha, niliomba msamaha bila kujua kosa langu ndipo mume wangu aliamua kunisamehe na kurudi chumbani tukaanza kuishi kama zamani ingawa amani bado ilikua haipo kwakua Mama mkwe kila siku alikua akilalamika kuwa hataki kufa kabla ya kupata mjukuu mwingine.
***
Mama mkwe alipata nafuu na kuondoka kurudi kwake lakini mume wangu alibadilika sana, suala la mtoto lilichukua nafasi kubwa sana, alianza kuchepuka waziwazi na kila nilipokua nikiongea alisema kuwa watoto wawili hawatoshi hivyo kama sitaki achepuke basi niondoke na kumpa nafasi ya kuoa mwanamke mwingine. Nilikua katika kipindi kigumu sana katika maisha yangu, bado nilikua na umri mdogo hivyo kila nikiwaza kuondoka kichwa kilikua hakikubali, sio kwamba sikua na kazi au sikua na uwezo wa kuondoka na kuanza maisha yangu mwenyewe, hapana, nilikua na uwezo huo lakini nilikua naogopa.
Kila mara nikiwaza kuishi peke yangu niliogopa zaidi, tayar nilikua sina kizazi hivyo nilifahamu kuwa hakuna mwanaume ambaye angekubali kuishi na mimi halafu nisimpe mtoto. Niliamua kukubaliana na ile hali nikiamini kyuwa kama mume wangu akipata mtoto mwingine nnje basi atabadilika kwani atakua na amani, niliona kuwa kwangu ni bora kubaki na mume wangu ambaye tayari nina watoto wawili naye kuliko kuondoka kutafuta mwanaume mwingine ambaye naye angetaka watoto na nisingweza kumpa.
Nilivumilia kila kitu mume wangu alichokua akinifanyia kwa imani kuwa anaweza kubadilika, sikua na mtu wa kumuambia matatizo yangu, ndugu zangu walishanichoka, Mama alikua akiniambia kuwa nimedekezwa sana ndiyo maana nalalamika kila siku sijui kuishi kwenye ndoa. Maisha yangu yalikua ya upweke sana, mume alikua ni mtu wa kurudi asubuhi na akiwahi sana ni saa nane usiku, ukichelewa kufungua au kumpa chakula kilichopoa basi ni kipigo, nilipigwa sana mpaka nikazoea na kuona kama ni sheemu ya maisha ya ndoa.
Siku moja nilipigiwa simu na mwanamke ambaye nilikua simjui, ni binti mdogo tu ambaye ni mwanafunzi wa chuo, alikua akinitukana na kuniambia kuwa yeye ndiyo kaolewa na mume wangu kwania na kizazi na mimi kazi yangu ni kujaza choo tu. Kwakua nilishachoka hata sikumjibu, nilimkatia simu na alipotuma meseji zake wala sikuzisoma nilizifuta, sikumuambia mume wangu wala kumuuliza chochote. Lakini siku mbili baadaye mume wangu aliwahi kurudi nyumbani, haikua kawaida yake, saa moja na nusu usiku alirudio, mimi ndiyo nilikua nimetoka kazini na kupumzika kidogo hivyo nilikua napika chakula cha usiku.
Alinikuta jikoni niko peke yangu tu, watoto walikua sebuleni. Ile kuingia tu alianza kutukana.
“Naona unanichokonoa, yaani kwakua wewe kizazi chako umetoa unataka kuniulia na wanangu, hutaki nipate mtoto mshenzi mkubwa wewe!” aliongea, mimi sikumuelewa, sikujua anazungumzia nini.
“Nimeshakuamba kuwa nataka kuzaa nnje ya ndoa, sasa nini kumpigia mwanamke wangu na kumuambia kuwa utafanya kila kitu kuhakikisha kuwa hazai! Nikuambie tu hiyo mimba ikitoka nakuua mimi mwenyewe mshenzi mkubwa na uchawi wako!”
Kusema kweli siku nikimuemewa, sikua nikijua anazungumzia nini, sikujua ni mwanamke gani nilimpigia na kumuambia maneno hayo, wala sikua nikijua kuwa kuna mwanamke ana mimba yake. Nilijaribu kumuuliza alikua anamanisha nini lakini ni kama nilimtibua.
“Unanidhihaki, unaniona mimi mjinga eee! Hivi unanichukulieje, yaani kwakua sijakufukuza kwaajili ya watoto ndiyo unataka kunikalia kichwani!” Aliongea huku akianza kunipiga, alinipiga sana huku akiokota kila kitu kilichokua mbele yake pale jikoni na kunipiga nacho, hakuchagua ni kitu gani, kila alichokiokota alikitumia kunipiga.
Alinipiga sana nilijaribu kujitoa kwake kwa kukimbia lakini alinikamata na kunipiga, alipoona sisikii bado napambana alichukua mchi, mtwangio mdogo niliokua nikitumia kutwangua vitunguu swaumu na kunipiga nao sehemu mbalimbali za mwili, nilipiga kelele kuomba smaada, nilikusanya nguvu na kumsukuma ili nitoke akapeepsuka kidogo. Wakati napambana ili kutoka jioni alichukua ule mchi akanirushia ukanipiga kichwani pembeni kidogo ya kisogo, nilidondoka chini na kupoteza fahamu.
Wanawake wengi wanaopigwa wanaamini kuwa atabaidlika, wanavumilia makofi na mpaka kufikia kupigwa hivi basi wanakua washazoea na wanaona kama kitu cha kawaida, kama ulipigwa makofi juzi basi jua huna tofauti na huyu dada, wewe hukuondoka hembu jiulize je huyu ataondoka? Nisikuchoshe fuatilia simulizi hii ya kweli hapahapaSIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!---SEHEMU YA SITA
Nilikuja kushtuka saubuhi, nilikua katika kachumba kadogo hakuna helwa, nilinyanyuka taratibu kwa shida huku nikipapasa papasa mlango, ndani kulikua na giza nene. Nilijua kuwa niko stoo. Nilienda kugonga mlango, niligonga sana lakini sikufunguliwa.
“Nifungulie nakusikia unavyopumua hapo mlangoni.” Nilipiga kelele kwani nilikua nikisikia mtu akipumua mlangoni. Ukimya kidogo ulitanda, nilipiga tena kelele kumuomba anifungulie mlango huku nikitaja jina la binti yetu wa kazi ambaye mume wangu ndiyo alimleta.
“Dada Baba kasema nisikufungulie mpaka arudi anaogopa utaenda tena Polisi.” Aliongea, nilimsihi sana nikimuambia kuwa nipo kwenye maumivu makali na kamwe siwezi tena kwenda Polisi lakini hakujali, hakufungua mlango, nilisogea mmpaka Dirishani nikawa nagonga na kupiga kelele lakini watu hawakusikia, nyumba yetu ilikua ndani ya Geti hivyo hakuna mtu aliyesikia. Baada ya kuona napoteza nguvu niliamua kukaa ili kumsubiri mume wangu arudi na kunifungulia mlango.
Njaa ilikua kali, lakini kwakua ilikua stoo mwanga ulipoingia kidogo nilichukua maji na kunywa, nilikula Nyanya na vitu vingine ambvavyo vilibaki pale stoo. Kila baada ya kama nusu saa Binti wa kazi alikua akija na kuniira, ni kama alikua anataka kujua kama niko hai au la, nilihisi alikua anampelekea taarifa mume wangu ambaye alishaenda kazini. Niliamua kukaa kimya kwani nilijua kama akimuabia mume wangu kuwa siongei angekuja ghafla, kweli ilitokea hivyo, baada ya kutokumjibu kwa kama masaa mawili hivi mume wangu alikuja, alifungua mlango na kunikuta nimelala nimechopka.
Alinibeba mpaka kitandani, alianza kuniomba msamaha na kuniambia kuwa ni shetani alimpitia.
“Yule mwanamke alinichanganya sana, alisema wewe ni mchawi unataka kumuua mtoto wake ndiyo mimi nikapaniki, wewe si unajua mimi nilivyo, nina hasira za karibu, wewe ukanijibu kwa dharau mimi nikakasirika, sikupanga kukuumiza hivi mke wangu nisamehe…” Aliendelea kulalamika, mimi sikumjibu, nilikua nimechoka na kichwani nilikua na maumivu makali, kuongea ilikua shida lakini nilijitahidi kumuamba.
“Naomba unipeleke hospitali mume wangu, nimeumia sana kichwa, kichwa chote nakiona kizito, nisaidie mume ….”
“Hapana, siwezi kukupeleka, hii ni mara ya pili nakupiga, kama nikikupeleka watadai PF3 kabla ya kukutibu na safari hii nitafungwa. Vumilia mke wangu, chukua dawa hizi, utapona, unaona ninavyokupenda, pamoja na yote hayo lakini bado nakuwaza wewe. nakupenda sana mke wangu lakini wakati mwingine shetani anakua ananitawala mpaka nashindwa kuzuia akili yangu. unaona kazini sikua na amani, nawaza hivi mke wangu akifa hawa watoto nitalea na nani, nimelia sana ofisini, sikua sawa kabsia, ona nimekueltea dawa kunywa mke wangu…”
Aliongea kama mtu vile, alinipa Panadol ili ninywe, sikua na namna zaidi ya kuzichukua, hakuruhusu nitoke na simu zangu alizichukua zote. Kila akitoka alikua akinifungia ndani, na alipoona Panadol hazisaidii alikua akinipa dawa za usingizi. Hivyo kila nikiamka nikilalamika maumivu alikua ananilazimisha kunywa dawa za usingizi nalala. Kwa wiki nzima hali ilikua hivyo, nilikunywa dawa zaa usingizi mpaka huwezi amini usingizi ulikata nikawa silali tena, niliamua tu kupona, pamoja na maumivu makali niliweza kuvumilia na kujifanya nishapona ili aniruhusu kwenda kazini.
Aliniruhusu lakini kwa misamaha mingi ambayo iliambatana na vitisho kama nikiongea.
“Najua uko karibu sana na yule mzee, safari hii ukienda kutangaza matatizo ya familia yetu kwa watu basi mimi nitadili na wewe, utaondoka hapa na hawa watoto hutawaona mpaka unaingia kaburini!” Alinitishia, nilimuahidi kuwa siwezi kuongea kitu chochote hivyo awe na amani kwani najua kuwa nikimuambia mtu nitamkera. Nilienda kazini na kukuta kuwa alishaniombea ruhusa kuwa nimefiwa na Mama yangu mdogo nipo kijijini, nilifika na kushangaa napewa pole nyingi za msiba ambao haukuepo.
Kama kawaida yake, mara nyingi mume wangu akishanipiga na kuniumiza sana basi hubadilika na kuwa mtu mzuri kwa muda kabla kisirani chake hakijajirudia na kuwa na hasira tena. Safari hii hakubadilika sana lakini angalau alikua hanjipigi tena, mwanake wake aliyekua amemuambia kuwa ana mimba yake alimdanganya kuwa imetoka hivyo aliendelea kuhisi labda mimi ndiyo nimemloga hivyo akazidisha kisirani kwangu. maisha yaliendelea, kichwa kilipona na niliendeklea kufanya kazi zangu vizuri tu. Mume wangu aliendelea kuchepuka wazi wazi kwa madai ya kutafuta mtoto lakini hakumpata.
Kila siku alikua akinilaumu mimi kuwa ndiyo namloga, Mama yake ndiyo alizidisha kelele kila siku kunipigia simu kunitukana. Sikua na chakusema, sikua na mtu wa kumuambia matatizo yangu zaidi ya mdogo wangu wa kiume ambaye mara nyingi alipenda kuniuliza. Kila mara alikua akiniambia ni kwanini naendelea kumvumilia mwanaume mshezi kama mume wangu. Sikua na jibu la maana kwani kama ni kazi nilikua nayo tena ya kipato kizuri tu, ningeweza kuondoka na kujitegemea, nikawa na maisha yangu ambayo hayamhusishi yeye kabisa lakini bado sikua na ujasiri wa kuondoka.
Nilikua mpweke sana, najua mtashangaa lakini pamoja na yote hayo bado nilikua nampenda mume wangu na kuna wakati nilikua sioni kabisa kuwa naweza kuwa na furaha nnje ya ndoa. Mume wangu alikua akiniaminisha kuwa mimi sina thamani, alikua akiniambia kila siku kuwa kama akiniacha basi siwezi kupata mwanaume mwingine wa kunivumilia kwani mimi ni mjeuri, sina akili, nina kiburi na sina kizazi hivyo kupata mwanaume mwingine basi itakua shida sana. Niliamini hivyo mpaka kufikia hatua ya kuwa nafanya kila kitu anachokitaka yeye na si ninachotaka mimi.
Pamoja na mume wangu kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha, pamoja na kuwa na msmahara mkubwa kuliko mimi lakini baada tu ya mimi kuanza kazi na yeye kuona kama nina kipato basi alikua anahakikisha kuwa natumia pes ayangu yote. Yeye alikua akilipa ada ya mtoto, lakini chakula, umeme, maji na kila kitu ilikua mimi. Kila nikimuomba pesa alikua anahakikisha namuelezea namna nilivyontumia pesa zangu zote mpaka senti ya mwisho ndipo hutoa pesa zake. Katika kuwekeza kila kitu kilikua kwa jina lake, nakumbuka kuna kipindi nilikua najikusanya ili kununua Gari.
Nilitaka kununua gari ya milioni 12, nilikusanya mpaka kufikisha milioni 10, mume wangu aliniambia ataniongezea ili ninunue, akachukua pesa akaagiza gari lakini kuja lina jina lake akanikabidhi tu funguo. Sikuongea chochote, nililipokea na kukubali matokeo kwani nilijua kabisa kuwa kama nikiongea basi nitaishia kupigo tu na gari sitapewa. Nilijiona mfungwa na nilijua kuwa siwezi kuwa na furaha katika maisha yangu kama sitakua na mume wangu, hivyo mdogo wangu aliponiuliza niliishia kumuambia tu kuwa “Wewe ni mwanaume huwezi kujua, halafu hujaingia kwenye ndoa,s ubiri uoea ndiyo utajua.”
***
Sikumoja nilikua kazini, sikua nikiumwa wala kujisikia vibaya lakini wakati natembea nilijikuta nadondoka, nilianza kujirusharusha, kwa bahati nzuri kuna Mama mmoja alikuepo pale, akawaambia watu wanishike na kunipanua mdomo, waliangalia kitu cha kuniweka mmdomoni walikosa wakachukua kikatia kucha na kuniwekea. Nilikua nang’ata mdomo kwa nguvu, nilipelekwa hospitalini baada ya vipimo waliniambia kuwa nina Kifafa. Nilishtuka sana kwani katika maisha yangu na katika familia yangu hakukua na historia ya ugonjwa huo.
Waliniuliza maswali mengi ambayo sikua na majibu nayo lakini kwa namna walivyokua wanaongea nilijua tu kuwa tatizo linatokana na mimi kupigwa pigwa na mume wangu hasa kipindi kile aliponigigha kichwani. Niliruhusiwa kuondoka lakini kwa uangalizi maalum, baada ya hapo matukio ya kudondoka yalikua yanazidi, ilikua haipiti hata wiuki mbili kabla sijadondoka kifafa. Kazini kazi zilikua hazifanyiki, nililazimika kuomba likizo ya miezi mitatu kwaajili ya matibabu, lakini bado sikupona nikaomba likizo ya Bila malipo ya miezi sita.
Mwanzoni mume wangu alikua Bega kwa bega na mimi wakati wa matibabu, lakini baadaye alikua kama kanisusa kwani maneno yalizidi kuwa najidekeza, nimelogwa na nina laana. Nikimuamba yeye ndiyo kasababisha kwa kunipiga alikua akiruka futi mia na vipigo huanza tena. Baada ya kuona hali inakua mbaya, siwezi kukaa na mtoto, siwezi kukaa peke yangu kwani matukio ya kudondoka yalikua mengi mume wangu alinirudisha nyumbani kwetu ili nikatibiwa.
Nyumbani walijua sababu ya mimi kuwa vile, hapo dipo nilianza kuona kutengwa, kila mtu alikua akinilaumu mimi, akiniambia kuwa ni uzembe wangu na ujinga wa kumvumilia mwanaume kama yule. Mtu pekee ambaye alinifariji alikua ni mama yangu, najua alikua akijisikia vibaya kwani yeye ndiyo alikua chanzo cha mimi kluvumilia manyanyaso. Alinifariji na alikua bega kwa bega na mimi katika kutafuta matibabu, baada ya kuhangaika na dawa za hospitalini ikashindikana basi tulihamia kienyeji na kwenye maombi, mambo yalitulia kidogo lakini si sana.
Nikawa nadondoka lakini si ile mpaka ya kungata ulimu, nilikua nikidondoka nakuwa kama nimepoteza fahamu kidogo kiosha narudia katika hali ya kawaida baada kama ya nusu saa. Baada ya kuona nimepata nafuu kidogo nililazimika kurudi kwa mume wangu ili niweze kurudi kazini. Baadhi ya ndugu zangu walikua hawataki lakini nilishaanza kujiona mzigo, walikua wakiniambia nibaki lakini wakitoka ni manyanyaso, amsengenyo na kuniteta hivyo nikaona bora tu kuondoka.
Mume wangu alinipokea vizuri na kwa kumuangalia alikua anajisikia vibaya, ingawa alikua hakubali ukweli lakini alikua akijishtuia kila mara akiahidi kubadilika na kuniambia kuwa hjatanupiga tena.
“Hata ukiwa vipi mimi sitakuacha, nakupenda sana mke wangu, kuna wakati nakosea na kupendwa na hasira lakini hizo ni hasira tu, haimaanishi kama sikupendi.” Aliniambia maneno ya kunipa moyo, nilijipa moyo labda kabadilika lakini bado nilikua na wasiwasi. Hali ile ilipoa kidogo nikarudi kazini kuendelea na majukumu yangu baada ya likizo ya bila malipo kuisha.
Nilifanya kazi kwa muda wa kama miezi miwili tu hali ile ilianza kujirudia tena. Nilianza kudondoka na hospitalini waliniambia kuwa nipunguze kufanya kazi kwani nikichoka sana ndiyo hali inajirudia. Nilijitahidi kufanya kazi na kuficha lakini ilishindikana. Siku moja Bosi aliniita ofisini na kuniambia kuwa natakwa kupumzika, walinipa barua ya kusimamisha mkataba wangu kwani nilikua siwezi kutimiza majukumu yangu kutokana na hali yangu. Niliumia sana, sikua na chakulalamika kwani tayari walishanibeba snaa.
Nilichukua kilichochangu na kuondoka kurudi nyumbani, nilimuambia mume wangu kilichotokea, alilipokea vizuri na kuniahidi kuwa atanisaidia kunipa mtaji ili nifungue Biashara. Alinipa moyo na kunifariji sana, maisha yaliendelea nikiwa sina kazi, nikawa mtu wa kukaa nyumbani tu, mawazo mengi nadondoka mara kwa mara kiasi kwamba siwezi tena kukaa mwenyewe, hata kukaa na binti wa kazi ilikua ni shida kwani nikidondoka anashindwa kunishika na kuniwekea kijiko mdomoni ili nising’ate ulimi.
Maisha yalibadilika sana, pamoja na mume wangu kujitahidi kunichangamsha, kujitahidi kunitoa out lakini sikua na furaha, nilikua na huzuni kila wakati nikawa mtu wa kulia tu. Siku moja mume wangu alichelewa kurudi nyumbani, alikuja usiku wa manane akalewa chakari, alishaanza kubadilika hivyo nilishangaa kumuona vile, lakini sikumuuliza kwani nilihofia kipigo. Alibadilika kidogo na kuwa na hasira, alianza kuongea maneno ambayo hayaeleweki, niliona kabisa alikua anatafuta ugomvi.
Nilijua kabisa kama nikimesemesha au kulalamikia chochote basi ningeishia kupigwa, kwasababu hiyo niliamua kunyamaza kimya bila kusema chochote. Lakini alishapanga mambo yake kichwani, aliniambia mwenyewe.
“Mimi nimechoka, hatuwezi kuishi maisha ya namna hii, naona bora uende nyumbani kwenu wakakuhudumie huko, mimi nitakua nikituma tu pesa, lakini siwezi kuendelea kuishi na wewe tena, nimechoka nataka uondoke, kesho kusnaya vitu vyako ondoka usije ukanifia hapa!” Mume wangu aliongea huku akinyanyuka na kutoka nnje, hakusubiri hata jibu langu aliondoka kabisa nyumbani na kuniacha pale nikiwa sielewi chakufanya.
Kuna watu wengi wakisoma hapa wanakua na hasira nas kumuona HiLdA kama vile hana akili kwanini avumilie haya? Nataka nikuulize swa wewe mara ya mwisho ulipopigwa ulifanya nini? Alipokuambia kuwa atabadilika na akakupiga tena ulifanya nini? Kabla ya kumtukana HiLdA basi tafakari hivi lile kofi lingekua ni kitu umepigwa kichwani leo ungekua na tofauti na HiLdA naomba nisikuchoshe endelea kufuatilia simulizi
Tags:
RIWAYA