SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO! 8-----9. MWISHOOO

SEHEMU YA SABA

Mume wangu alikazania sana mimi kuondoka na kurudi nyumbani kwetu, nilimuambia kuhusu watoto akaniambia watoto ni wake na hawezi kunipa mimi watoto kwani ni mlemavu. Sikua na namna, ingawa sikupenda lakini nilirudi nyumbani, walinipokea vizuri kwani safari hii mume wangu ndiyo alimpigia Baba simu kumuambia kuwa kanirudisha nyumbani ili nikapumzike. Nilijua rasmi niemshachika, niliumia sana kwani mabli ya kuwa nilikua nimemzoea mume wangu lakini niliwamiss sana wanangu, niliumia zaidi kwakua sikua na pakukimbilia, sikua na kazi na kutokana na hali yangu nisingeajiriwa popote.

Nilikaa nyumbani kwa miezi sita bila kutoka ndani, nilikua mtu wa kushinda ndani, kulia, mume wangu hakutaka hata niwaone wanwangu akisema kuwa hawatakiwi kuniona katika hali ile4 wataogopa, aliwadanganya tu kuwa nimesafiri. Katika kipindi hicho ndipo ndugu zangu walijua kila kitu mume wangu alichokua ananifanyia, kila mtu alinishangaa ni kwanini nilikua namvumilia mwanaume wa namna ile. Mama aliishia kuniomba msamaha kwania lijilaumu kwa kila kitu, hakusita kuniambia kuwa yeye ndiyo alikua kasababisha kwani hakunisikiliza tangu mwanzo.

Pamoja na kuwa na hasira naye lakini sikua na namna, nililazimika kumsamehe kwani ni mama yangu, hakuna kitu ambacho angekifanya kingenifanya kumchukie, isitoshe kwa wakati huo sikua na namna kwani yeye pekee ndiyo alikua na muda wa kunihudumia. Niliendelea kuhudhuria kiliniki kila wiki kuangalia maendeleo gani, hakuna aliyejua hasa kifafa changu kilisababishwa na nini ingawa madaktari walisema inawezekana vipigo vya mara kwa mara vilisababisha kwani waliona nina mpasuko ambao ulishapona kwenye fuvu, Xray ilionyesha kuvujwa mbavu mbili ambazo zilishaunga hivyo walidhani hiyo ndiyo sababu.

Nilianza kupata nafuu, ingawa nilikua nikidondoka mara kwa mara lakini si kamja zamani, wakati huu nilikua nadondoka tu kawaida, sipotezi fahamu na wala sing’ati ulimi tena. Madaktari aliniambia inawezekana kuwa niemshapona lakini kutokana na msongo wa mawazo, kukaa peke yangu kila siku na kuwa mtu wa kuwaza wanangu basi labda ndiyo maana nadondoka. Walinishauri kuwa nawaona ona wanangu, nilimuomba mume wangu kuwaona lakini alikataa katakata, hali ilizidi kuwa mabya kwani nilikua napata msongo wa mawazo, nashituka na kudondoka mara kwa mara.

Ndugu zangu waliingilia kati, wakaenda ustawi wa jamii mume wangu akaitwa na kulazimishwa kuniruhusu kuona watoto. Kila wiki nilitakiwa kukaa nao siku mbili jumamosi na jumapili. Kweli ilinisaidia ingawa sikuacha kudondoka lakini nilikua amani na furaha zaidi. Baada ya kuona sipati nafuu kama walivyodhani madaktari walinisihi sana kutoka ndani na kutafuta kitu cha kufanya. Kwakua nilikua siajiriki ndugu zangu walijichanga wakanipa mtaji na kunifungulia duka, nilikua nikikaa dukani pamoja na mfanyakazi, ingawa duka halikua kubwa lakini kutokana na hali yangu basi nilikua nahitaji mtu wa kuwa naye wakati wote ili nisijekudondoka na kujidhuru.

Biashara ilienda vizuri, kutoka kwangu nnje ilikua ni kama kitu kipya kwangu, nilikua kama vile ndiyo naanza kuona watu, mbali na kwenda hospitalini nilikua na zaidi ya miezi nane sijawahi kutoka nnje ya nyumbani. Hali ilianza kuwa nzuri, ile ongea ongea na watja ilikua inanipa nafuu mimi na nilianza kuzoea mazingira, nilitengeneza marafiki na watu walikua wanacheka na mimi bvila kujua nina matatizo nilifarijika sana na kusikia raha kuwa angalau nilikua nakutana na mtu hata mmoja ambaye hayafahamu matatizo yangu.

Nilifanya Biashara kwa miezi sita, ikawa inapanuka vizuri, nilikua ninaifanya kwa nia nzuri na nilikua najiona kabisa nafanikiwa, lengo langu lilikua ni mimi kujikusanga ili nihamie kwangu kwani nilikua na kiwanja nilitaka kujenga ili niwachukue wanangu. Lakini katika kipindi hiki nilipata tatizo jingine, mume wangu alipata ajali ya gari, alivunjika nyonga na kulazwa hospitalini kwa miezi minne. Mimi bado nilikua mke wake, pamoja na kwamba alinirudisha kwetu lakini alikua bado hajanipa talaka, alikua akiishi na mwanamke mwingine lakini baad aya kupata ajali aliondoka na kumuacha, kumbe alikua ni mke wa mtu na mume wake alikua mkoani.

Mume wangu alikua analijua hilo na hakujali, alipopata ajali mwanamke aliondoka hivyo ndugu zake walianza kunitafuta kuwa mimi ni mke wake natakiwa kumhudumia. ndugu zangu wengine walikataa kabisa na kuniambia nimuache apambane na hali yake, lakini Mama alikazania kuwa niende, Baba alikataa ila kwa nguvu aliyokua nayo Mama aliishia kuniambia kuwa nitaamua mwenyewe. Binafsi nilitaka sana kwenda kumhudumia mume wangu, nilikua bado nampenda na moyoni kuna kitu kilikua kinaniambia kuwa labda ajali itambadilisha na kumfanya kuwa mume mwema.

Pamoja na kwamba hata mimi nilikua naumwa lakini nilijiona nina nafuu, mume wangu alikua ni mtu wa kulala tu, kusogezwa, kunyanyuliwa, kuogeshwa, alikua ni wa kujikojolea na kusafishwa. Kazi zote hizo nilizifanya mimi kwa miezi minne, kutokana na kuwa bize na mume wangu baishara nayo ilisimama kwani msichana niliyemuacha aliniibia nakuondoka hivyo nikalazimika kufunga. Mdogo wangu wakiume ambaye alikua ananisaidia kusimamia alisusa na kuniambia hatakai kudili tena na mimi kwani nimeamua kurudi kwa mwanaume mshenzi, yeye aliona kuwa ile ajali ilikua ni malipo na mume wangu alistahili kufa kabisa.

Lakini mimi niliona ajali kama kitu cha kumabadilisha mume wangu, niliona labda ajali itamfanya kuwa mnyenyekevu na kama nikimhudumia vizuri basi atakumbuka wema wangu na kuniona kuwa mimi ni mwanamke sahihi kwake akanirudia. Kweli alinoomba smamaha, kila siku kitandani alikua akilia, alikua akijutia kwani katika miezi hiyo minne ndugu zake ni kama walimtelekeza. Dada zake walikua wakija mara moja moja, ldba Mama yake pekee ndiyo alikua akihangaika na mimi lakini ndugu wengine kila mmoja alikua na maisha yake, ziadi ya kuchanga changa pesa za matibabu hakuna aliyekua anamhudumia kihivyo.

Mama mkwe alijipendekeza kwangu, aliniomba msamaha karibu kila siku, mimi nilishamsamehe kwani nilikua na amani. Sikua nikidondoka tena mara kwa mara, katika miezi minne ya kumhudumia mume wangu nilidondoka mara mbili tu kitu ambcho kilinipa amani na kuhisi nimepona ingawa madaktari waliniamba bado na kuniambia kuwa niendelee hivyo hivyo kuacha kuwaza kwani msongo wa mawazo uanchangia kwa kiasi kikubwa mimi kudondoka. Mume wangu aliruidi nyumbani akiwa anatembea ingawa kwa shida si kama mwanzoni. Aliweza kurejea kazini na maisha yalianza kurudi kama zamani.

Nilipoona kapona nilirudi nyumbani, sikua nataka lakini sikutaka kujipendekeza. Nilitaka mume wangu kujiongeza, kwakua alikua kanifukuza yeye na kuniambia kuwa nirudi nilitaka aje kunichukua yeye. Kweli baada ya kurudi kwetu mume wangu alimuita mchungaji, alikuja na ndugu zake na badhi ya wazee, akaomba smamaha na kushika Bibilia kabisa kuwa hataninaynaysa, hatanipiga tutaishi kwa amani. Ndugu wengine bado waliniambia niachane naye nishikilie biashara yangu lakini Mama alishikilia msimamo kuwa nirudi, Mchungaji na wazee wengine walinisihi kurudi kwa mume wangu na mwisho wa siku nilirudi na kuanza kuishi kama zamani.

Maisha yaliendelea, yalikua na furaha mwanzoni kwani mume wangu alibadilika na kuwa mtu wa kuonyesha upendo. Lakini kadri siku zilivyokua zikienda mume wangu alianza kuwa mpole, mpweke na mtu wa hasira, kitandani alikua hataki nimguse, baada ya kupona tulikaa miezi saba bila kufanya mapenzi na kila nilipomuuliza alikasirika na kuniambia kuwa mimi ni Malaya, yeye abdo hajapona nataka nimuumize, nilivumilia lakini nilikasirishwa na namna alivyokua kaanza kuchepuka, nilianza kuona meseji za wanawake katika simu yake na nilipomuuliza aliishia kunitukana.

Niliumia sana na kutishia kuondoka lakini aliishia kuniomba msamaha ila kuhusu tendo la dnoa alishindwa kabisa. Mara kadhaa alijaribu kufanya mapenzi na mimi lakini uume ilikua hausimami kabisa, alikua ahasisimki, alikua anaweza kuniandaa na kunishika shika kila sehemu lakini hasisimkwi kabisa. Nilianza kupata wasiwasi na kumuuliza kama ana tatizo ila alinigeuzia kibao, alianza kunitukana akiniambia kuwa mimi ndiyo nina tatizo kwani akifanya mapenzi na wanawake wengine anakua sawa, aliongea bila kujali hisia zangu.

Ni kama alikua hajui kama kwa kuniambia hivyo ni kama kakiri kuwa anachepuka. Niliishia kuomba msamaha na kujisafisha mara kwa mara, nilijiona kama mimi sivutii, nikajiona labda kama ni mchafu na kujilaumu sana. Kwakua nilikua nikiona picha za wanawake wengine wakimtumia nilijua mimi ndiyo nina tatizo labda sivutii. Lakini siku moja wakati nakagua vitu vyake nilona dawa flani, nilishtuka nikidhani labda mume wangu kaathirika ni ARV, niliamua kuingia google kuziangalia, nilichokiona hakikunistua sana, zilikua ni dawa za kuongeza nguvu za kiume, nilianza kuwaza kama mimi ndiyo tatizo ni kwani anatumia hizo dawa.

Lakini pia niliwaza kama zinasaidia kwanini hafanyi mapenzi na mimi anafanya na wanawake wengine. Niliumia sana, nilitaka kuvumilia lakini nilishindwa, niliamua kumuuliza ni zile dawa ni za nini na kwanini hazitumii na mimi. Kwanza alishtuka lakini baadaye aliniambia ukweli kuwa baada ya ajali alipoteza nguvu za kiume na kahangaika sana ila hajapata suluhu, aliniambia kuwa anazitumia hizo dawa lakini hazifanyi kazi ndiyo maana hafanyi mapenzi na mimi, aliniomba sana kubaki na yeye na kuniomba nimlindie siri yake kwani watu wakijua haini tena sababu ya kuishi.

Unadhani Hilda ataondoka au atabaki, vipi kama akiondoka je nyumba itakua na amani? Nisikuchoshe fuarilia mwenyewe kwa kubonyeza kwenye ukurasa wangu na kulikeSIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!---SEHEMU YA NANE

Nilikua na amani kidogo aliponiambia kuwa ana tatizo la nguvu za kiume, sijui kwanini lakini nilidhani labda atatulia, hatakua akibadilisha wanawake na kwakua mimi najua ana tatizo basi atabadilika na kunipenda mimi peke yangu. lakini haikua hivyo, alizidi kuwa na hasira aliendelea kubadilisha wanawake na kunitukana mara kwa mara kuwa mimi ndiyo tatizo, mimi ndiyo ambaye simsimui kwani akiwa na wanawake wengine anakua kawaida na anakua anawafikisha kileleni.

Nilivumilia kwakua sikua na kazi, ndugu zangu waliokataa mimi kurudi kwa mume wangu walinitenga flani kasoro Mama yangu. mume wangu pamoja na kunifanyia madudu yote hayo, pamoja na kuwa na mahusiano na wanawake wengi wengi lakini bado alikua na wivu sana na mimi. Alikua hataki nitoke ndani, alikua hataki niwe na marafiki, alikua hataki niwasiliane na ndugu zangu, kwakua tayari walishajua tabia zake hawakua wakimuona malaika kama zamani basia liwachukia na kila alipoona naongea na simu na ndugu zangu basi alikasirika, alitukana akisema kuwa wao ndiyo wananiharibu na wanafanya hivyo ili mimi nimuache.

Nilianza kuwasiliana na ndugu zangu kisirisiri, nilikua naishi kwake kama mfungwa, nikitoka ni lazima kuaga na nikifika huko ni yeye kupiga simu zaidi ya mara kumi. Siku moja nilipigiwa simu kuwa Mama anaumwa, alikua kadondoka chooni na alikua kalazwa hospitalini, ilikua ni saa nane mchana. Nilimpigia simu mume wangu kumuambia hali ya Mama yangu, aliniambia nisubiri anakuja nyumbani kunipeleka Hospitalini, nilisubiri saa nane, tisa, kumi mpaka saa nne usiku mume wangu alikua hajar8udi nyumbani.

Mwanzo alikua akiniambia kuwa yuko bize kazini lakini baadaye nikipiga simu nilikua nikisikia anapokea yuko Baa kwani kunakua na kelele nyingi, nilivumilia nikashindwa, Kaka yangu mmopja mtoto wa Mama mkubwa alinipigia simu na kuniambia kuwa hali ya Mama ni mbaya na kama sina usafri amtume mdogo wangu kuja kunichukua. Nilimuambia naenda lakini mpaka saa nane usiku mume wangu alikua hajarudi, alirudi saa tsa usiku tena akiwa kalewa chakari. Nilimuambia kuhusu Mama akaishia kunitukana na kuongea maneno ya kuudhi.

“Kwani wewe ni saktari, kama ni mtu wa kufa atakufa tu, hawezi kupona kwakua tu umeenda, kwanza Mama yako mwenyewe kashazeeka, unafikiri atapona kweli muacha afe kwa amani si kwenda kumlalamikia lalamikia!” Aliongea kwa dharau akiwa kalewa, kweli niliumia, nilichukua simu na kumpigia Kaka yangu, nilimuomba kuja kunichukua usiku uleule. Mume wangu kusikia kuwa nimewapigia simu ndugu zangu alikuja juu, alikasirika na kusema kuwa nimemdharau namuona yeye si mwanaume an kuongea maneno mengi mengi ya ajabu ajabu.

Lakini mimi nilishakasirika, nilikua naudhina na vimaneno maneno vyake vya kila saa, sikutaka kuendelea kumsikiliza kwani nilijua tutagombana, nilinyamaza tu kimya na kumuaacha abwabwaje mpaka achoke, alipoona simjibu alifunga mpango, akachukua funguo na kuniambia kuwa siondoki mule ndani hata kama ndugu zangu wakija. Tulianza kugombania funguo ndipo mume wangu alianza kunipiga, alinipiga sana nikawa napiga kelele, wakati huo kaka zangu walikua washafika, walikua nnje ya geti wakigonga. Baada ya kusikia kelele kwakua Geti lilikua limefungwa waliligonga na gari likafunguka, nilikua nikipiga kelele sana hasa baada ya kusikia Honi nnje nikajua ni ndugu zangu.

Kwakua walikua wanafahamu mambo ambayo mume wangu alinifanyia huko awali hawakutaka kusubiri. Walivunja geti la nnje na kuingie kisha wakaja na kuvunja mlango wa ndani. Aliingia, alikua Kaka yangu mkubwa wa Mama mkubwa, mdogo wangu wa kiume na Dada yangu wa Mama mdogo. Nilikua chini damu zinanitoka mume wangu bado anaendelea kunipiga. Mdogo wangu wa kiume kuona vile alimvamia mume wangu na kuanza kumpige, yeye ana hasira sana, alimtandika sana mume wangu mpaka Kaka mkubwa alipomshika na kumuambia amuache.

Ulikua ugomvi mkubwa, hakutaka kumuacha alitaka kuendelea kumpiga na ndipo dada yangu alimuambia.
“Muache, acha kuendeleza haya mambo, Mama yako ndiyo amekufa na nyie mnaanza kugombana…”Dada aliongea huku akimsihi mdogo wangu kutulia. Kwa kauli yake ndipo niligundua kuwa kumbe Mama yangu alikua amekwisha kufa, niliuliza mara mbili, kumbwa walishajua muda lakini hawakutaka kuniambia, mume wangu kusikia vile ndipo alishtuka, pombe zikamuishia na kuanza kuaniomba mimi msamaha akidai alikua hajui chochote.

Hakuna mtu ambaye alimsikiliza, mdogo wangu alitaka tumpeleke polisi lakini Kaka yangu alisema haitasiadia, waliniambia niwachukue watoto tuondoke zetu. Tuliondoka usiku uleule mpaka nyumbani, Mama alifariki kwenye saa nane usiku, ikimaanisha kuwa kama ningewahi na kwenda kumuona ningemkuta Mama yangu akiwa hai. Niliumia sana kutokana na kifo cha Mama yangu, nililia sana, nilimlaumu mume wangu kwa kila kitu, aliniomba sana msamaha lakini sikua tayari kumsamehe, nilikua na hasira nyingi sana, hata kwenye mazishi nilishindwa klwani kila dakika nilikua ni mtu wa kuzimia.

Ndugu wa mume wangu walikuja, sikuweza hata kuonana nao kutokana na hasira nilizokua nazo juu yao, mume wangu naye bila aibu alikuja na alitaka kuonana na mimi lakini watu walimkataza. Baada ya mazishi niliendelea kubaki nyumbani, mume wangu alituma wazee kuja kuniomba msamaha lakini Baba yangu na ndugu zangu wengine walikataa katakata. Nilikataa na waliniambia sitakiwi kuendelea kuishi na mume wangu, aliondoka na kuendelea kunitumia meseji kila siku akisema kuwa kabadilika na kajifunza lakini sikumuamini.

Nilifunguliwa tena duka na ndugu zangu, nikawa nafanya Biashara nakaa nyumbani, mume wangu tulikua tukiwasiliana tu kuhusu watoto, mimi ndiyo nilikua naishi naye na alikua akihudumia tena vizuri sana. Alikua akituma pesa nyingi sana kuliko hata mahitaji yote hiyo kunionyesha kama amebadilika. Pale nyumbani wadogo zangu walikua chuo na wengine wana maisha yao, muda mwingi nilikua mwenyewe na wanangu pamoja na Dada wa kazi, Baba alikua bize na mabo yake, alikua ni mtu wa kusafiri safari tu, pamoja na kupata kila kitu lakini nilikua mpweke sana.

Sikua na marafiki, sikua na mtu wa kuongea naye zaidi ya mume wangu ambaye mara kwa mara alikua ananipigia simu tunaongea hata masaa mawili. Yeye ndiyo alikua ananiondopelea upweke na kweli kila nikiongea naye nilimuona kama kabadilika, baada ya kukaa miezi kama nane hivi niliona nibora kumpa mume wangu nafasi nyingine. Nilimuona kabisa kuwa kabadilika, niliwaambia ndugu zangu kuwa narudiana na mume wangu lakini hawakutaka, walikataa ila niliona kuwa kila mtu ana maisha yake, niliona wao wanafuraha na mimi sina furaha na njia pekee ya kuwa na furaha ni kwakurudiana na mume wangu.

Nililazimisha kuondoka nikarudi kwa mume wangu ndipo siku moja mdogo wangu aliniambia “Nimaisha yako, rudi, umeamua hivyo lakini usije kutusumbua tena, siku akikuua sisi tutakuja kuchukua maiti yako!” Ndugu zangu wote walionekana kukerwa na maamuzi yangu, hakuna mtu hata mmoja ambaye aliniunga mkono, si Baba, Shangazi wala jirani. Niliumia sana na kumkumbuka sana Mama yangu kwani nilijua wakati kama huo yeye ndiyo anakua upande wangu. lakini nilijipa moto kuwa mume wangu atakua kabadilika, ataka kajifunza na hawezi kuninyanyasa tena.

Maisha yalikua mazuri kwa muda mfupi tu, lakini bado mume wangu alikua na tatizo la nguvu za kiume hivyo kisirani chake kilirudi palepale, kwakua alikua anajua sipatani na ndugu zangu hata simu zangu hawapokei absi alizidi kuninyanyasa,a liifunga tyena Biashara yangu nikawa mtu wa kikaa nyumbani tu. Nilikua nimekata tamaa kabisa ya maisha nikijiaminisha kuwa laba ipo sikua tabadilika. Lakini niliposoma kisa cha David hapa kwa Kaka idi ndipo niligundua kuwa mume wangu hatabadilika na naweza kuondoka hapa nikiwa mati.

Bado niko kwa mume wangu, sijui cha kufanya, manyanyaso ya kila siku yamezidi, hanipigi kwa sasa lakini kila siku ni matusi na kejeli, kubadilisha wanawake ni kama kawaid ain gawa sijui kama anafanya nini nao wakati kwangu hakuna kitu. natamani kutoka katika hii ndoa lakini sina uajsiri, nimesoma Post nyingi zako Kaka naomba unipe ujasiri, naomba unisaidie ni kitu gani chakufanya kwani ndugu wamenitenga hawataki kunisikia kwani hata nikisema naondoka hawaniamini tena. Napitia comment za watu najiona kama mjinga ila sijui nifanye nini kwani kwa sasa sina kazi na hakuna ndugu wakunisaidia tena, naomba nisaidie kaka nifanye nini naona kama maisha yangu yamesimama.

****MWISHO 

Post a Comment

Previous Post Next Post