MFALME RAI 01


Rai, mfalme wa Ughaibu , alikuwa mfalme namna ya peke yake duniani. Alikuwa na tabia iliyohitilafiana kabisa na tabia za watu wengine wa zamani zake. Tabia yake ilijigawa katika theluthi tatu mbalimbali kama rangi ya ngozi ya punda milia. Kwa theluthi ya kwanza alikuwa msuluhifu akapendwa na watu, Kwa theluthi ya pili alifanana na Daud akaheshimiwa kama mtunzaji mkuu wa wanyama, na kwa theluthi ya tatu alikuwa kama Suleiman akatiiwa na majini. Kutawala suluhu na mapenzi ya wanadam, utunzaji wa wanyama, na utii juu ya viumbe wasioonekana kama majini hutaka uwezo mkubwa sana. Kwa hivi, fikiri wewe mwenyewe jinsi Rai alivyojipambanua mwenyewe na wafalme wengine.

Katika miliki ya mfalme huyu kodi ilitozwa juu ya mifugo ya wanyama. Kodi hii ilihalalishwa kwa sababu Ughaibu ilikuwa nchi ya mifugo. Ughaibu ilipokuwa juu ya kilele cha usitawi mifugo yake ilikuwa hailingani kwa ubora na mifugo ya nchi yoyote nyingi

Post a Comment

Previous Post Next Post