...................ilipoishia Nilipofungua mlango,nilikuta matone ya damu yamejaaa sakafuni,haa! nikishituka kwa uoga ikabidi taratibu nianze kuyafatisha kwa tahadhari yalielekea chumbani nilishika kitasa taratibu uku natetemeka ,nilifungua mlango wa chumbani,nilipofungua mlango nilimkuta dada diva amejaa damu mwili mzima akiwa sakafuni ,uku mkononi akiwa ameshika kisu ,kilichojaa damu pia........haaa! nilijikuta naogopa
"Adelina ,uko wapi"nilichanganyikiwa na kujikuta namuita mtu asiyekuwepo,uku nikijikuna kichwa hamna siku niliyochanganyikiwa kama hii
"Kwa haraka nilichukua simu na kumpigia baba.
"Baba naomba ufike nyumbani,mara moja kuna tatizo ,ndio hapa tandale makaburini"adi maneno nilishindwa kumaliza.
Baaada ya nusu saa baba alifika tulimpakia na kuanza safari ya kuelekea hospitali,dakika kumi na tano mbele tulikuwa hospitali,tulipokelewa na manesi waliokuwepo zamu kwa jioni hiyo.
Tulikaa kwenye benchi lakini halikukalika wasiwasi ulitujaa tusijue ni kitu gani kimemkuta diva ,ni nani aliyefanya mauaji yale
"Kwani Adelina imekuwa vipi"aliuliza baba
"Ata najua basi,mie nimerudi nimemkuta ametapakaa damu,uku mkononi akiwa na kisu na mpaka asaiv sijui imekuaje
"Mmmh sijui itakuwa ni nini ila cha muhimu kisu kisiguswe,maana polisi wanaweza itaji maelezo kama alijichoma kisu au maelezo ukajikuta hatiani"alisema baba
"Sijakigusa ,ila sijui adela kama atokigusa maana ,hana taarifa yote "
"Kwani yuko wapi,yani adi nimesahau kuuliza"
"Alivyoenda shule nadhani ,atakuwa amechelewa leo,may be kuna kazi wamepewa siunajua ,wanakaribia kufanya mitiani"nilimwambia
Gafra! doctor alitoka uku akijifuta jasho,akatuangalia akakohoa kidogo kama ishara yakuweka umakini na usikivu
"Mgonjwa wenu anaendelea vizuri,alitaka afanye jaribio la kutoa mimba ,bahati mbaya ikamletea matokeo mabaya
"Baba adelina njoo tuongee kidogo,"doctor alimuita baba pembeni na kwenda kushaurina nae mawili matatu
"Masikini dada diva ,ila Mungu atamsaidia atapona nilijisemea moyoni
Baada ya dakika tano baba ,aliludi uku akionyesha tabasamu kwa mbali
"Baba doctor kasemaje kwani"
"Mgonjwa anaendelea vizuri ,kesho jioni atatoka,mimba ilikuwa ndo tatizo alisema baba
"Ooooh ni vizuri na afadhali, sijui Adela atakuwa amerudi na kama karudi saiv atakuwa anaangaika kututafuta na zile damu,sijui kule inakuaje
"Tuondoke mgonjwa amepumzika tutamfata kesho "alisema baba
Kwa unyonge nilimfata na kupanda gari kuelekea nyumbani,uku kichwani nikiwa na mawazo au kwakuwa alikuwa anataka kusoma je angekufa ingekuaje maana mie pia kisu nilikigusa,je ndo ingekuwa amejichoma kisu ,cha kushukuru alikuwa anajaribu kutoa mimba sio kujiua,yani unaweza kwenda jela bila kuwa na hatia
Nakumbuka nilitolewa kwenye msongo wa mawazo kwa kutikiswa bega
"Adelina unawaza nini muda wote"
"Haa kumbe tumefika ,nilijikuta nashangaa"
"Mda sana mdogo wako ,nimemkuta kajiinamia analia ,sijui alifikiri mtakuwa wapi"
"Hahaha mwambie aache uoga bwana,itakuwa zile damu zimemtisha"
"Nafikiri , kesho nitakupitia tukamcheki mgonjwa ,uwe una usiku mwema"alisema baba ,kisha akapanda gari nakuelekea kwake,
Siku ya jumamosi tulivu ,tukiwa tumekusanyika kwa baba ,ilikuwa mida ya saa kumi jioni ,ila siku hii ilikuwa tofauti kidogo ,mpaka jioni hii nyumba ilikuwa ishapendeza na mezani vyakula vya kila aina vilikuwa vimeandaliwa
"Hahaha najua mnajiuliza leo kuna nini sindiyo"baba alituambia
"Kama ulikuwepo vile,tunaitaji kujua"
"Basi kaeni kwa kutulia ,mambo mazuri hayataki haraka" ,alisema baba
Baada ya dakika kumi kulikuwepo na ugeni pale sebreni ,
"Naomba niwatambulishe wanangu Hapa kama mnavyomuona ,huyu ndiye mke wangu muiteni mama au bi ashura kwa sasa,baada ya miaka kadhaa kupita ,nikiwa naangaika katika jiji la dar es salaam,ndipo nilipokutana na mama yenu huyu ,ambae ndiye alinisaidia kwa mawazo ushauri na mambo mengi tu kama pesa na maitaji mengine mengi ,ikiwemo ata hii kazi ya asaivi yeye ndo alinisimamia pale kazini"alisema baba
"Kwani apo adelina ndo yupi?aliuliza yule mama
"Mimi nilimjibu ,uku nikitaka kujua anadhumuni gani la kuuliza hivyo
"Nimepata habari zenu kwa kipindi kirefu sana ,na nlikuwa na hamu ya kuwaona ,maana nawajua kwa majina na sio kwa sura akaanza kuyataja adelina,adela na diva ,sasa naomba niwajue kwa sura leo
"Mimi naitwa adelina na huyu ni adela ,yule pale ni dada diva "niliwatambulisha
"Oooh sawa nimefurai kuwajua maisha yenu yalinigusa sana,kwa kiasi kikubwa ipo kama historia ya maisha yangu nadhani baba yenu ashawai kuwagusia kidogo ,na kama bado basi siku moja atawagusia.
Cha pili adelina ,adela na diva mlifanya mashindano ya kuogelea ,sikuwepo lakini zawadi zenu nimekuja nazo zipo nje apo zimetoka bandarini ,nimewaletea gari aina ya nadia zipo tatu ,kila mtu ataendesha lake,gari la kampuni naomba lisitumike tunaelewana ,maana nasikia adelina wiki ile uliendesha vibaya sana"
"Asante sana mama,tumefurai zawadi ulizotuletea , na tunakukaribisha rasmi katika familia yetu,
"Karibu mama ,alisema diva na asante kwa zawadi ulizotuletea hakika Mungu akuzidishie"
"Usijali diva na pole kwa yaliyokukuta , nafikiri mwakani utasoma ,kwa kushirikiana na baba yenu mambo yote yatakuwa sawa ,eeeeh na wewe Adela unasemaje maana sijakusikia kuongea chochote"
"Mimi gari,naweza kuendesha ila sina leseni ,nisije nikadakwa bure"alisema adela
"Usijali tutakukatia ,ukimaliza kidato cha nne sawa,alafu Adela ebu pakueni chakula kwanza ,maana njaa ishaanza kutusumbua ,leo ni siku ya kula bata tu alisema baba
Akati naenda mezani kwa ajiri ya kupakuwa chakula gafra! Mlango ulifunguliwa mama mdogo aliingia
Haaa! Nilishituka sababu sikujua nani alimuonyesha tunapokaa ,na kikubwa zadi alifata kitu gani.nilikuta na wasiwasi baad ya kumuona baba mdogo.............itaendelea baadae usiku ikifika like mia mbili namalizia epsod zilizobaki unaposoma hakikisha una like
Tags:
RIWAYA