Adelina 12

...............ilipoishia "Sasa dada diva ,utavaa nguo hii au hii ili tukashindane nipe mkono tushindane

Lakini diva alibaki kimya ,uku akiangalia upande wa pili hakuwepo na sisi kabisa ,tulijikuta wote tukiangalia kule "sheet alikuwa mama mdogo

Mama mdogo alivyotuona wala hakushituka alituangalia kwa dharau ,taratibu alimchukua mwenyeji wake na kuondoka eneo lile,bila kuongea chochote
Diva alibaki akilia tu ,maana ilionyesha dhahiri mama ake hana mpango nae ,sembuse huo uchungu

"Dada diva haina haja ya kulia ,mtu akiondolewa kwenye maisha yako na alikuwa mbaya inapaswa usiwe na unyonge ,sio ukae kwa udhuni hivyo,unafikiri kama sio Mungu sisi kupita uku tungekuonea wapi"nilimwambia

"Sawa dada adelina ila nasikia uchungu,mama anijali baba pia anizingatii kabisa kwani mimi ni yatima,sielewi nimekuwa na familia ya mama sijawai furaiya maisha,mpaka nikajikuta nabeba lana za ukoo ule"alisema diva

"Usijali diva haina haja ya kujilaumu sana,potezea mdogo wangu mambo mengine Mungu ana makusudio yake"nilimwambia

"Ni kweli adelina usemayo ,inabidi amuachie Mungu ,kama Mimi nilivyomuachia wala sikuwaza kulipiza kwa haya yote niliyotendewa,cha kufanya nikufurahi tu"alisema baba

"Adela Mpe boya na izo nguo,mkashindane na adelina ,inaonekana ni waoga sana nyie"

"Hamna baba ,akuna muoga hapa ngoja tukavae alafu tunakuja sasa ivi "alisema adela

"Hahahaha waoga hao,niliwaambia "
"Hahaha umeona eeeh ,sasa inabidi uwakimbize adi wakome ,maana huyo adela hamna anachojua katika maji ,ata kuendesha gari tu ni mtiani'alisema baba

"Tumerudi sasa,walisema kwa pamoja uku wakiruka ndani ya maji"
"Hamna kitu nyie,ngoja kwanza nikaongee na simu nakuja kushuhudia pambano"alisema baba  

"Mmekuja eeeh ,haya karibuni dada diva unaweza ogela kimbwa mbwa "nilimuuliza

"Kwani nani hawezi na ivi nini ,mie nimeanza kujifunza toka nipo uko ,sio hapa tu"alisema diva

"Haya jamani shindane ,mie nimekaa pembeni naangalia nani mshindi wa pambano ,maana kuna zawadi nimemuandalia"alisema baba.
*****************************************

"Subiri niendeshe gari mwenyewe ,maana adelina asaiv akili sio yake kabisa"alisema baba

"Hahahaha nimechoka ,maana nimewakimbiza sana ,"niliwaambia

"Muongo baba we mwenyewe ,umeshuhudia "alisema diva 

"Wote mmefanya vizuri wiki inayokuja nitawaita kila mtu atapata zawadi yake"alisema baba

Baada ya dakika 20 tulifika mbezi beach,baba alisimamisha gari

"Baba unaweza kutuacha apo tuchukue bajaji mpaka nyumbani "

"Kwanini leo msilale uku mabinti zangu,nyumba yote hii"baba alisema

"Alafu tukilala uku ,nyumbani kule tuvunjiwe ,we baba unapajua tandale"nilimuuliza

"Anyway ,basi shikeni nauli tutawasiliana alisema baba uku akitoa pesa nakutukabidhi

Tulipanda bajaji na kuelekea nyumbani tandale tulifika saa tano usiku nakuanza kutembea kuelekea nyumbani

"Oya nyie mademu ,simameni ivyo ivyo"ilisikika sauti 
"Nyie tusimameni alisema diva uku ,akitetemeka 
"Oya chodo vipi ,mbona tunatishana,"nilimuuliza
"Aaaaah kumbe sister niambie,sikukujua bwana "alisema chodo 

"Poa bwana ,sietunaingiza mida hii ,siunajua tena night kali hii,mambo yasiwe mengi"nilimwambia tuliachana nae pale nakuelekea nyumbani

Baada ya dakika kumi tulifika nyumbani ,kwakuwa tulikuwa tushakula tulifikia kulala moja kwa moja ,hatukuongea sana sababu kesho ,ilikuwa jumapili tungejipanga tu vizuri.

Nakumbuka ukiwa ushapita mwezi,nilitoka kazini na kumkuta dada diva amejiinamia kwa unyonge

"Dada diva ,mbona ivo ndio tuseme ujazoea kukaa peke yako"

"Dada diva mbona unalia tena,nilivyomuuliza ndiyo kilio kilizidi ,sikujua kwanini yupo katika hali ile

"Nataka kwenda shule"
Mmmh maskini ,sa itakuaje na ana mimba,nilijiuliza mwenyewe
Nilisogea nikaka karibu yake,usijali dada diva ukishajifungua tu ,we utaanza shule mie,nitalea huyo mtoto wako,ata usijali kuhusu ilo mambo yote yatakuwa sawa,nitaenda kukaa nae kule dukani,aniitie wateja 

Gafra! dada diva aliachia alicheka ,kwani watoto wadogo wanaitaga wateja ,wewe tu ubunifu wako na kuongea vizuri 

"Hahahah Adela yuko wapi kwani ,ajarudi adi saivi"

"Kasharudi,amejifungia anasoma uko "alinijibu

"Adela "uku nikigonga mlango 
"Abee dada aliitikia 
"umeamua ukae ndani kama utumbo,uwe unakaa na dada ako ata masaa machache au ndo kusoma 

"Ndio adelina,nilikuwa nasoma bwana,ila toka nimerudi mbona nilikuwa nae alisema 

"Haya sawa,mmekula teyari?
"Bado dada hatujala"
"Kwanini hupiki na wewe unajua kama mwenzako yupo katika hali gani

"Kuna kazi nilikuwa namalizia ,ila asaiv nilikuwa naenda kupika 
"Jumamosi hii,baba katuita tena itabidi twende jioni ,sawa diva"

"Ndio nimekuelewa alisema diva
"Sema nimekuelewa mdogo wangu,mie mdogo sana ,kuliko wewe dada diva tuseme maisha tu"nilimwambia

"Haya mtoto mzuri nimekuelwa"alisema diva 

hahahahaha tulicheka kwa pamoja
*****************************************

Nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi ,bado siku mbili tuelekee kwa baba ,nilifika nyumbani nakupokelewa na ukimya wa ajabu 

"Mmmm leo vipi,mbona umu ndani kimya "nilibisha hodi palikuwa bado kimya hakuna aliyeitikia

Nilipofungua mlango,nilikuta matone ya damu yamejaaa sakafuni,khaa! nikishituka ikabidi taratibu nianze kuyafatisha kwa tahadhari ,yaliingia chumbani,nilipofungua mlango nilimkuta dada diva amejaa damu mwili mzima akiwa sakafuni ,uku mkononi akiwa ameshika kisu ,kilichojaa damu pia.......................itaendea like tunaangushana like 200 tumekubaliana unaposoma hakikisha una like ili tumalize haraka hii sasa wengine wanategea🚶🚶 

Post a Comment

Previous Post Next Post