Adelina 10/11

....................ilipoishia wote tulistaajabu tulijikuta tunatoa macho kwa tulichokiona ,"haaaa! nyie huyu si diva "niliuliza 
"Ndio tena ana mimba maskini kwa iyo kumbe alikuwa asomi"adela aliuliza

"Malipo ni hapa hapa duniani ,anyway adelina washa gari tuondoke "alisema baba

"Hapana baba,najua kakosea ila hali kama ile kutembea usiku haifai "nilishauri

"Dada diva ,we dada diva"adela aliita uku akifungua mlango wa gari

"Diva alipoangalia machozi yalimtoka ,baada ya kutuona,alipokutana macho kwa macho na baba kidogo alisita kuja

"usijali dada diva ,baba ame shakusamehe na sisi pia kwaiyo jisikie amani njoo tu usiogope"nilimwambia

Taratibu alianza kuja uku akichechemea ,akionekana amechoka sana aliingia kwenye gari ,na taratibu nilitoa gari ,nyuma ya gari baba na adela hawakuongea chochote ,

nilijikuta navunja ukimya"dada diva jisikie amani sie tushakusamehe,tunajua ni mama ako aliesababisha sio wewe,imekuaje dada angu upo katika hali hii"nilimuuliza

Alizidisha kilio,niliendelea ku myamazisha taratibu alinyamaza ,hata amu ya kushuka kuingia jangwani hatukua nao ,tuliishia sehemu ya maegesho pale jangwani

"Adela ,adelina na baba najua nimewakosea sana tena sana ,hasa baba angu nadhani Mungu analipa kwa haya yatokeayo"aliongea uku akilia

"Usijali dada diva ,tupo pamoja na tunajua umekosea na tunakusikiliza,mpaka kupanda kwenye gari hili maana yake tushalishakusamehe"nilimwambia
"Baba ,baba" aliita diva kwa masikitiko ya hali ya juu 

"Niambie mwanangu"kwa mara ya kwanza baba aliitikia maana alikaa kimya kule nyuma yeye na adela wakiendelea kusikiliza haya anayoongea diva

"Nakumbuka ile siku mama aliniita chumbani na kuniambia haya,"alisema diva
"Mwanangu diva "
"Naaam mama "
"Ivi unapenda maisha haya ,yasiyo na mbele wala nyuma ,mpaka ela za kula tuombe kwa mama mkubwa wako "
'hapana mama ,lakini mama milioni mbili alizokupa mama mkubwa si ungefanyia biashara umeenda kumtunza jamila wa vikoba milioni moja ,ukaishia tu kupigiwa makofi kwanini mama"
"Tena funga bakuli lako ,mbwa wewe nimekuzaa leba kwa uchungu,alafu unanifundisha cha kufanya,alafu utaenda kukaa kwa mama mkubwa wako uko maana ushaanza umbea wako"alisema mama

Basi nakumbuka baada ya wiki alinileta pale ,nyumbani nikawa naishi pale kw mama mkubwa lakini kwa miaka ile ,tuseme ulikuwa utoto nilishidwa kutofautisha baya na zuri,chochote mtachokuwa mmezidi nilikuwa nikimwambia mama angu ,ata navyoingia chumbani kwa kina adela nikikuta chochote ambacho mie sina nilikuwa nikimwambia mama angu ,yani iliendana na nahau hii "mtoto wa nyoka ni nyoka "nilijikuta tu nazidi kuwa mtu mbaya mama angu aliishia kuniambia ,yani hivyo vitu ataviacha atatangulia kaburini "mara nyingi alikuwa akiniambia hivyo"alinyamaza kidogo uku taratibu machozi yakimwagika kwa wingi alishindwa kuongea

"Pole dada diva ,yamepita hayo nyamaza dada angu "nilimwambia

alijifuta machozi kwa viganja vyake akaendelea kuniambia"basi nilipokaa pale kwa mama mkubwa kuna siku aliniambia ,muache aringe mwezi huu atomaliza ,atenda na maji"
"Kwanini mama ,kwani umejuaje kama atomaliza kwani we ni Mungu 
"Mungu mtu mimi alisema mama alidiriki kujiita adi Mungu mtu

Niliendelea na masomo,lakini siku mmoja mama alinipigia simu na kuniambia nirudi nyumbani ,asije mtu akafa nikaonekana Mimi ,sikumnishia niliamua nirudi zangu nyumbani,lakini baada ya wiki nilisikia mama mkubwa amefariki niliumia kwakuwa alikuwa ana roho nzuri na sijui kwanini niliumia vile,baada mazishi mama aliniambia nirudi pale kwa mama mkubwa

"Rudi kwa mama mkubwa wako"
"Mama lakini Mimi,nataka kukaa na wewe "
"Nimekwambia rudi mbwa wewe ,mama mama unanijua sana"
"Lakini mama"
"Funga bakuli lako,kesho usirudi apa
Aiseee nilikuwa najiuliza mbona kama huyu sio mama angu ,ata baba angu pia nilishangaa Niko nae tofauti alikuwa aongei chochote juu ya mama ,yani alikuwa mwanaume yule ambae hana sauti mbele ya mama.

Nakumbuka siku mmoja ,asubuhi kabla sijaenda shule nilimpigia mama simu na kumwambia baba anaumwa leo hawezi kwenda kazini ,gafra! alishituka sikujua sababu ila aliniambia kuwa ,nipitie nyumbani kuna jambo la muhimu ,baada ya masaa kadhaa nilifika nyumbani ,sikumkuta mama kwakua aliniambia nimsubiri nilibaki nikiangalia television.

 Mida ya saa nne gafra! walitokea watu watatu,waliingia mpaka ndani,nilipowauliza ,wanashida gani waliniziba mdomo walinibaka aisee ile ndo siku niliyopoteza usichana wangu hakuna siku nilioumia kama siku ile ,baada ya dakika kumi mama alifika na kuanza kunishangaa

"haaa! mtoto umeanza umalaya "
"Hapana mama nimebakwa "
"Umebakwa ushahidi uko wapi,mbwa wewe"
"Cha kufanya nenda kwa baba ako ,kafanye ufanyavyo aonekane yeye ndo kakubaka"
"Lakini mama "
"Hakuna cha lakini mamae"

Niliondoka na kurudi kwa baba ,na kwenda kufanya kama mama alivyoniambia ,gafra! mama alitokea na kumfokea baba akaniambia nikifika polisi niseme baba ndo kanibaka ,nilitoka pale tukaenda hospital nikapimwa kweli nimebakwa na muhusika mkuu akiwa baba mkubwa

Basi mama akanipeleka shule ya bodi ,sikujua baba alivyoenda polisi ilikuaje ,yeye mwenyewe ndo anajua ,ila ukweli ndo ulikuwa hivyo"alisema dada diva

"Dah pole dada diva nyamaza ,inauma sana yani kama sio mama ako ,anakosa utu kabisa"
"Asante nishapoa ,alisema diva"
"Sasa dada diva ,na hiyo mimba imekua vipi"aliuliza adela

diva alianza kulia tena kilio cha kwikwi ,hamna siku aliyolia sana kama siku hii ilifikia hatua adi Mimi nikawa nalia kwa stori yake ilivyonigusa
"Kuhusu hii mimba, ilikuwa hivi mama alinisomesha vizuri kila nikitaka kurudi nyumbani alinikatalia siku jua kwa nini ,lakini gafra nilishangaa siku moja ananifata na kuniamisha shule na kunipeleka shule ya laki nane,toka milioni mbili

"Mama mbona ivi ,unaniamisha shule"
"Sina ela ,unachezea hela sana shule gani milioni mbili,akati miaka yote mama mkubwa alinisomesha mpaka kidato cha kwanza na hakuwai kuniamisha ,lakini alipofariki nimesoma miezi sita mama kaniamisha

Nilisoma kwa shida sana,kiasi nilikuwa nakosa ela ya kununua vifaa vya shule,ilifikia hatua nikawa natembea na dereva boda boda ili nipate maitaji ya msingi maana mama kila nikimwambia alikuwa ananiambia hana pesa yoyote,kama vipi nimfate mama mkubwa makaburini

Dah! Majibu yalinichosha sana,mwishoe nilijikuta napata mimba bila kutegemea ,na ndo hapo nilipofukuzwa shule,na yule boda boda sikumuona tena aliama kijiwe kabisa.

Nilipofika nyumbani mama alinitukana sana,hakujali kuwa nimeteleza na mimi ni mtoto kwake 

"Umedanga umepata mimba ,sasa hapa kwangu mkataba umeisha kwanza wewe sio mwanagu siwezi kuwa na mtoto kahaba nilikupata baada ya kusumbuliwa sana kukosa mtoto nikaamua nikununue,toka filauni mkubwa mamae"aliniambia 

Basi toka siku hiyo nazurula tu mtaani ,Nina kama wiki tatu naishia kuchezewa na wanaume kila mwanaume mwenye elfu tano nilikuwa nalala nae

"Dah alinikumbusha mbali sana ,kazi ambayo niliifanya bila kupenda",yote haya ni mama mdogo ,ama zake ama zangu niliongea kwa sauti bila kujua

"Tulikuwa tunakaa pale mbezi makonde kule masaki tulishaama ,nilipomuuliza mama kuhusu nyie alisema baba aliwafata "alisema diva

"Dah pole diva kazi ya Mungu haina makosa ila Mungu atamuadhibu tu "alisema baba

"Tuingieni ndani bwana,uyo mama mdogo asituaribie furaha yetu,"alisema adela

Tulishuka ndani ya gari na kuingia ndani ya seabreaz aisee! nilishabadisha nguo kabisa nilifikia kujitupa tu phaaaa!

"Duh kichwa kibovu kama kambale unavyoyajua kuyaoga"alisema baba

Wote tulitabasamu ,"ata Mimi naweza kuogelea "alisema diva 

"Sasa dada diva ,utavaa nguo hii au hii ili tukashindane nipe mkono tushindane

Lakini diva alibaki kimya ,uku akiangalia upande wa pili hakuwepo na sisi kabisa ,tulijikuta wote tukiangalia kule "sheet alikuwa mama mdogo ................itaendelea like 200 naachia kingiene unaposoma hakikisha una like leo ntajibu maoni machache😁 

Post a Comment

Previous Post Next Post