Adelina 14

............ilipoishia 
 Nilishituka! baada ya kumuona mama mdogo sababu sikujua nani alimuonyesha tunapokaa ,na kikubwa zadi alifata kitu gani.,wote tulibaki tukimuangalia tu ,

"Wewe ni nani na unashida gani"aliuliza baba
"Mimi ni zuwena ,najua nimewakosea sana ,ila marehemu mama adelina ndiyo alienileta hapa "aliongea uku akilia 
"Huyu ndo zuwena yule,aliyekusabishia matatizo"aliuliza bi ashura

"Ndiye huyu ashura "alijibu baba
"Sawa tumekusamehe ,unaweza kwenda au kuna kitu umekisahau"nilimuuliza

"Vipo tena vingi tu,ambavyo hamvifahamu ,na inapaswa mvijue sababu marehemu mama adela aliniambia niwaambie"

"Mmmmh makubwa malipo ni hapa hapa duniani Kama vipi kwa mfano au ndo ilimradi utuaribie furaha yetu "Adela alimuuliza

"Hapana adela ,ila ipo ivi vyote nilivyofanya naombeni mnisamehe sikuwa Mimi alikuwa ni shetani ,nakumbuka mwaka 1999 nilikuwa na shida sana ya mtoto,na mume wangu kwa kipindi iko ,alikuwa ni tajiri mkubwa ,alikuwa akiitaji sana mtoto kwa njia yoyote na kwa bahati mbaya sikujaliwa kizazi,

Hivyo basi niliangaika sana kwa waganga bila kupata msaada,na mume wangu alisema kuwa kama sitozaa mwaka huo atoshughulika na mimi tena ,kanivumilia zaidi ya miaka saba .

 Mambo haya yalinitatiza sana,nilijikuta nakata tamaa ya maisha sababu pesa nilikuwa nazitaka za mume wangu ,niliamua kwenda hospitali ili niweze kupata mtoto,nakumbuka nilipofika pale hospitali
"Kwaiyo utanipa bei gani,nikikupatia mtoto,maana kuna dada atazaa watoto mapacha muda sio mrefu "alisema nesi

"Ntakupa milioni mbili na nusu "
"Sawa ila iwe siri yako,ikigundulika hii itakuwa ni kesi kubwa"
"Usijali mie natetea ndoa yangu,na wewe unatetea kazi yako"

Basi baada ya masaa kadhaa nilipatiwa mtoto wangu nakumpa jina la diva

"Haaa! Mama kumbe Mimi sio mwanao"aliuliza diva

"Ndio diva wewe sio mwanangu ,ndo mana kuna muda nakuwa sina machungu na wewe"alijibu mama mdogo uku akilia

"Uchungu wa mwana ajuae mzazi,ndo mana kumbe ulitufanyia vile"nilimuuliza

"Hapana ila naombeni mnisamehe,"alisema mama mdogo

"Ok baada ya kupata mtoto"aliuliza bi ashura 

"Baada ya kumpa diva ,mume wangu alifurai sana akawa anishirikisha kila sehemu,apo ndo nilipoanza kumfirisi ukijumlisha na dawa za kienyeji nilikuwa nimemfunga vibaya sana ungemsikia akisema ivi

"Mama diva ,mbona account kila siku inapungua pesa si chini ya laki saba"
"Kama umenichoka niambie ,niondoke sawa we kenge"
"Basi sawa mke wangu yaishe"alikuwa kama zezeta dawa kubwa ilikuwa ni diva ,yani amuonapo diva akili yake ndo inaendelea kutofanya kazi,baada ya kutumia pesa vibaya hatimaye ziliisha wakaka wadogo wadogo walinifilisi.

Nikawa naona diva ana umuhimu tena sababu pesa zilimuishia na bado dawa imebaki kwenye damu mpaka leo hii bado kapooza alisema mama mdogo

"Aiseee ukisitaajabu ya musa utayaona ya firauni"alisema baba

"Na kuhusu mama adelina kusema ukweli hakuwai kuwa ndugu yangu,mama angu alikuwa na tatizo kama langu ,hivyo mama adelina alichukuliwa hospitali na kuhusu bahati nzuri alipata dawa ,ndipo aliponizaa nafikiri sijui hili ni tatizo la kurithi,ndo mana nilikuwa namuonea wivu masaa yote yani ,kumbe hiki ndo kilikuwa chanzo hakuwa ndugu yangu

"Nilimuonea wivu sana kwa maendeleo aliyofikia yeye na mume wake,ndo nilipoamua kumuendea kwa mganga,na ikiwezekana Mali zao nizilisi ,
"Kwaiyo unataka tumfanyeje"aliuliza mganga
"Nakuachia wewe mganga"
"Inabidi tumuue taratibu,ili isijulikane tutampa ugonjwa wa kancer ya damu huu utamaliza mapema sana"
"Nashukuru bwana saika"

nilipotoka uko kwa mganga ni kweli mama adelina alikaa wiki kadhaa alifariki dunia laiki ajabu mume wake akuwai kunitongoza ,sijui dawa ziligoma ,ndo nikaamua kumpa kesi ya ubakaji,na sijui kwa nini alitoka bado dawa zilishindwa kufanya kazi nadhani ni Mungu tu mwenyewe aliamua

"Wallah jamani ,we mama ni mnyama sana dah! sijawai kusikia hii"alisema bi ashura 

Baba kwa asira aliinuka na kuingia ndani bi shura alimfata kwa haraka sikujua walienda kuongea nini

Mama mdogo alibaki akilia uku amelala chini ,akionekana kujuta kwa alichokifanya

Diva na adela taratibu waliinuka na kwenda jikoni kuchukua majagi ya juice ,ni kabaki Mimi na mama dogo kuna kitu nilitaka kumwambia gafra! Simu yangu ikaita nikaelekea nje nakumbuka.

Baada ya dakika tano ,nilirudi sebreni watu wote walikuwa washarudi ,nikaa kwenye sofa kuwasikiliza wameamua nini uku mama mdogo akiendelea kujiinamia

"Watu wote hawakupendezewa na ulichokifanya,ila bado Mungu anakupenda nimemshauri mume wangu sana na amekubali ,tukupe milioni mbili,ukafanyie biashara na kuhusu hii familia naomba usiifate tena"alisema bi ashura

Mama mdogo alikubali kwa kutikisa kichwa uku macho yakiwa yamemvimba

Cha kula kiliwekwa tukaaanza kula taratibu ,kila mtu alijichagulia anachokitaka,ata mama mdogo alichukua chakula chake alionekana kuwa na amani sasa

Baada ya kula vijiko kadhaa nilimsikia baba ,bi ashura ,wakianza kujishika tumbo"jamani tumbo mbona hivi"alisema bi ashura alifuatia adela kulala mika ,mmmh baba nini niliwauliza akati nataka niwafate nilianza kuona giza uku tumbo likiniuma vibaya aikujulikana kwenye chakula kumewekwa kitu gani.............itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post