Adelina 15 MWISHOO

................ilipoishia Baada ya kula vijiko kadhaa nilimsikia baba ,bi ashura ,wakianza kujishika tumbo"jamani tumbo mbona hivi"alisema bi ashura alifuatia adela kulala mika ,mmmh baba nini niliwauliza akati nataka niwafate nilianza kuona giza uku tumbo likiniuma vibaya aikujulikana kwenye chakula kimewekwa kitu gani......nilijikuta nikipoteza fahamu

Nilikuja kupata fahamu kesho yake,nilipofumbua macho niliwashuhudia familia nzima ikiwepo tofauti na mama mdogo
"Nesi ameamka"alisema Adela
"Nesi alifika ,nakuanza kuniluliza maswali kadhaa,kuona kama Nina kumbukumbu vizuri,alipojidhihirisha na majibu yangu aliongea machache

"Pole mgonjwa kwa yaliyokukuta,wenzako wote walipata nafuu jana,sababu hawakupata madhara makubwa walitumia maziwa kupunguza madhara hayo ,kwa upande wako hukuwa na bahati yaliishia njiani kabla ya kukufikia ndo mana ukazidiwa,ila kwa sasa uko salama jioni tunaweza kukuruhusu"aliongea nesi alipomaliza aliondoka

"Uko salama mtoto wangu"aliongea bi ashura 
"Nipo salama ,mama sijui nyie,niliwajibu 

"Sie tuko salama,adelina" alisema adera 
"Vipi kuhusu mama mdogo"niliwauliza
"Uyo shetani ,anashikiliwa na polisi oysterbay toka Jana ,tena achana nae kabisa ,alitaka kutuua kizembe sana"alisema diva.

Nilikaa hospital, ilipofika jioni niliruhusiwa kurudi nyumbani ,tukakaa sebreni tukiongea mawili matatu

"Kuanzia leo nyie watoto wote mtakaa hapa'hii nyumba inabidi muda wote iwe moto"alisema bi ashura

"Sawa ila mie kodi yangu itapoisha ila hawa wanafunzi itabidi wabaki hapa"

"Tumeambiwa tubaki wote,ata wewe mwenyewe inabidi uanze shule "alisema diva
"Hahahaha mie shule wapi na wapi "

"Acheni kelele bwana,diva na adela kaleteni supu ,leo nimeamua nipike mwenyewe"alisema baba

"Hahahaha leo,tutashuhudia maji ya nyama "nilisema

Baaada ya kunywa supu na vyakula vyengine,tulifanya kikao kifupi kuhusu mama mdogo tulikubaliana mama mdogo hakuna kuwekewa dhamana ,sheria ifate mkondo wake maana ipo siku angetuua wote ,maana alianza na mama akajaribu na sisi ,hitimisho la kikao ni kuwa mama mdogo tusimfatilie ,zaidi ya kwenda kutoa ushuhuda tu.

Jioni nilivyotoka kwa baba ,niliamua kwenda polisi oysterbay ,sijajua ni kipi kilichonipeleka kule ila nilijisikia kwenda kuonana na mama mdogo kwa muda huo

Nilivyofika pale oysterbay polisi ,nilitoa maelezo kadhaa kwa polisi wakaniletea mama mdogo ,

Aliponiona machozi yali mdondoka taratibu mashavuni kwakwe 

"Najua nimewakosea ,ila haya ndo malipo yangu"alisema mama mdogo

"Pole mama mdogo,tatizo ujawai kubadilika utaki kukubali uhalisia wako, sometimes matatizo mengine unataka mwenyewe,na mpaka muda huu dhamana imefungwa sijui itakuaje

"Unaweza kuniambia kwanini ulituwekea sumu "
"Ni shetani tu ata sijui kwanini niliwafanyia vile,ila nilikuwa na tamaa na mafanikio yenu"

"Aisee muda umeisha ,mnafikiri mpo nyumbani nini ,si awekewe dhamana kama mnamuitaji sana "alisema polisi aliyekuwa zamu

Taratibu nilielekea nyumbani ,ila leo nitakuwa mpweke sana maana wale wote waongeaji nimewaacha kwa baba ,ivi mama mdogo ,ni kiumbe gani nashidwa pata jibu ujue nilijiuliza nikakosa majibu ikabaki kitendawili tu.

Miaka mitatu baadae ,tulikuwa mahakamani tukisikiliza kesi ya mama mdogo baada ya kukaa mahabusu ukonga kwa miaka mitatu ,alikuwa amekonda vya kutosha ila hii haimkufanya hakimu kutoendelea na majukumu yake ,tulitoa ushahidi wetu na mama mdogo alitoa wake ila alizid kuomba msamaha akilalamika ni shetani hakimu alitoa hukumu ya miaka nane na faini ya shilingi milioni tatu,hukumu ilipotoka hatukuwa na la ziada zaidi ya kuelekea nyumbani

"Kwaiyo chuo,umechagua udsm"nilimuuliza diva
"Yeah ndo chuo nilichokuwa na kipenda ,toka miaka hiyo"alisema diva

"Kozi gani unaenda kusomea "nilimuuliza
"
"Law in Swahili sheria"alisema uku akibinua midomo

"Duh kumekucha adi kingereza,ndo miaka mingap unasomea "
"Miaka mitano ,adi Adela atanikuta chuo"
"Na Mimi nitasoma ,chuo hiko hiko nikimaliza tu kidato cha sita" alisema adela
"Nyie bwana,maneno mnamaliza nyie tu,ebu acheni kelele huko nyuma "alikuwa bi ashura

"Ebu achana nao ,maana kuna wasomi na wafanya biashara hapo ,kila mtu anaongea lake,ebu ona hii video "alikuwa baba

"Alafu baba tuelekeni kariakoo,niacheni pale kazini kwangu "niliwaambia

"Watu na kazi zao mjini ,ila hatujawai kwenda bora leo tukatembee kwenye duka letu "alisema diva

Baaada ya dakika kadhaa tulifika mtaa wa sikuu ,ila kulikuwa na msongamano wa watu kama kawaida yake ",tushafika ni hapa "bi ashura alisema 

"Kumbe unapajua mama,"diva aliuliza 
"Eeeeh sehemu ,hii nilimtafutia Mimi"alisema bi ashura

"Waooooh ,bora la hard ware uku akishuka ndani ya gari sasa mbona ujaandika adelina hardware"aliuliza diva

"Chawa wengi ,waandishi waabari watakuja kunioji maana mie mtu mkubwa '"niliwaambia

"Aisee umepiga hatua ,huu mradi wako sio chini ya milioni 40 hapa hakuna haja ya kutuomba mtaji tena ,bi ashara imekuwa"alisema baba

"Et hii soft but bei gani"aliuliza diva

"Faraja ebu watembeze umu watajie bei ya vitu vyote ,hakikisha wanaelewa"nilimwambia faraja ambae alikuwa mfanyakazi wangu .

Baada ya miaka mitano ,tulikuwa chuo kikuu cha dar es salaam kwenye mahafali ,ya diva na adela ,wote walikuwa wanaitimu siku moja ,diva akimaliza degree ya sheria ,uku adela akimaliza degree ya uhasibu aliyosomea miaka mitatu

"Aiseee mmejua kupendeza wanangu"alisema baba
"Hasa kama mie kipindi kile namaliza cbe"alisema bi ashura
"Asanteni walijibu kwa pamoja "leo adela na diva hawakuwa waongeaji

"Sasa ndugu zangu,naona leo mpo kama wali ata maneno hayatoki"niliwaambia

"Acha wivu kwanza tupige picha kwenye gari hili zuri ,sijui la nani"alisema diva

"Tokeni mtanichafulia gari langu,ilikuwa v8 mpya plate namba ilisomeka adelina ,nilinunua miezi minne iliyopita ila hawakuwai kuliona

"Dah unatufanyia ivi ,"aliongea diva
"Tutanunua yetu tu ,walisema uku wakikaa pembeni"

Gafra! Magari mawii aina ya rangerover discover six yalikuja na kusimama karibu yao ,uku yakiwa yamepambwa vizuri

"Mbona mnataka kutugonga"aliongea adela uku bado akiwa amechukia

Gafra! alishuka bi ashura na baba wakachukua fungua na kuwakabidhi

"Baba na mama ya kwetu haya"
"Yakwenu wanangu ,tumepambana sana kwanini msiendeshe vitu vizuri,baba aliongea

"Mimi na baba yenu tumeamua kuwanunulia ,kwaiy wanangu msijali ,uyo mwengine atajinunulia mwenyewe"

"Asante baba na mama ,wote tulikumbatiana ,machozi ya furaha yalitutoka taratibu 

"Njoo utupige picha kwenye magari yetu"alisema diva

"Kaeni hapo,hii kamera kwa ajiri ya mapicha yenu"niliwaambia

"Acheni ushamba,mapozi gani hayo ,rusheni kofia juu"niliwaambia

Tuesabu kwa pamoja ,moja mbili tatu ,walirusha kofia juu ,sikuchelewa nikawapiga picha.

Leo hii niko nimeshika picha hii histori ndo ikanijia nikaona sio vibaya kushare na nyie ,ni miaka mingi imepita nishaolewa na Nimebahatika kupata mtoto mmoja ,niliposoma hadithi Facebook nikaona ni mtafute mtunzi na kumpatia hadithi hii ili hawafikishie na nyie,mpate cha kujifunza na natumaini mmejifunza asanteni na Mungu awabariki ,nitapitia maoni maoni yatayonigusa nitampatia zawadi Mimi mwenyewe tofauti na mwandishi wa hadithi hii 


**********MWISHO***********

Post a Comment

Previous Post Next Post