ADELLINA 3

Ilipoishia...
Kitenge kililetwa ,tulipomfunika baada ya dakika kadhaa alikuwa kimya"mama mama tulijitaidi kumuamsha akuamka baba alimfika na kumuamsha "mama adela mama adellina "baba alijitaidi kumuamsha lakini hakukuwa na mafanikio

Alipomuangalia machoni kiini cheusi hatukukiona ,sio wote hatukujua maana yake nini kiini cheusi kisipoonekana nilimuona tu baba akidondosha chozi.

"Baba vipi kwani "nilimuuliza kwa kipindi kile sikuweza kuelewa kabisa mama alikuwa amepatwa na nini?

Adela alibaki kulia tu ,baada ya kumuona baba akilia "tunampeleka hosptali,amezidiwa huyu "baba alisema

Tulimbeba mama taratibu na kumpakia kwenye gari na kuanza safari ya kumpeleka hospitai ,baba alikuwa akiendesha gari kwa mwendo mkubwa uku akiendelea kuongea na simu na kuwapa watu maelekezo ila nilimsikia akisema hivi"ndio amefariki,labda Mungu afanye miujiza,tunaenda apo tmj mikocheni,sawa haina shida"alisikika baba akiongea na mtu fulani kabla ya kukata simu na kuongeza mwendo wa gari

Baada ya dakika kumi ,tulikuwa tmj hospital maandishi ya blue yalisomeka katika jengo moja refu 

manesi walitupokea,walimtoa mama na kumpakiza katika kitanda cha magurudumu matatu,uku baba akiendele kuongea na simu ,alionekana dhahiri amechanganyikiwa.

Baada ya lisaa limoja kuwa pale ,tuliludi ndani ya gari "baba mbona tumemuacha mama peke yake"aliuliza Adela

"Tunaenda kumfatia chakula"alisema baba 
"Baba mbona unalia sasa"nilijikuta namuuliza hivyo 

"Hamna adellina mama ako anaumwa sana ,turudini nyumbani tukamtayarishie chakula"alisema baba

Tulifika nyumbani majira ya saa saba mchana,mmmh nilijikuta nashituka! nyumba ilijaa watu wakiomboleza "adela kwani apa kuna nini"nilijikuta namuuliza mwenzangu
"Mie sijui,mama. mdogo yule analia ,au mama amefariki"adella aliuliza

"Hamna bwana ,baba si kasema tunampelekea chakula ,"nilimjibu

Tulishuka kwenye gari,tulianza kupewa pole na watu waliofika kwa ajiri ya kuhudhuria mazishi yale 

Mamdogo alilia adi alivimba macho nikabaki najiuliza huyu si ndo aliyekuwa amjibu mama mesege zake ,mbona analia hivi nikakosa majibu
.Gafra! machozi yalianza kunitoka nikaanza kukumbuka yote tuliofanya na mama ,hakika sitoisahau ile siku ,nilihuzunika sana kwa kipindi kile,japo nilikuwa na umri mdogo ila nilielewa ni nini maana ya kuondokewa na mzazi.

Mazishi yalifanyika salama ,katika makaburi ya kinondoni ,kiukweli watu walikuwa wengi sana ,ni jinsi gani mama alivyokuwa na upendo,watu walikuwa wengi mno

Msiba uliisha miezi ilipita ,tulikuwa tukiishi wanne pale ,nyumbani mimi Adela,baba na diva ambae msiba ulivyoisha alibaki na sisi ,ila mama ake alishidwa kuomba chochote kutoka kwa baba maana ,ndugu yake ndo alishafariki tena ,baada ya miezi mitatu kupita mama mdogo alizidi kuchakaa ,weupe wote ulimuisha ,haikujulikana ni nini sababu,naweza kusema labda alipenda sana mserereko .

Nakumbuka ikiwa ishapita miezi sita tulikuwa tushaingia darasa la tano ,siku moja asubuhi tulimuona baba ametulia kwenye kochi uku ameshika tama

"Baba mkubwa mbona ivo"diva alimuuliza baba
"Najisikia vibaya kichwa kinanisumbua nataka niende hospital baadae kidogo"alijibu baba

"Pole baba ,leo nikitoka shule nakuletea zawadi"alisema adella 

Piiiiiiiii honi ilipigwa kwa fujo, tunakimbia nje kuwai gari,maana tukichelewaga dereva anaondoka na baba huchukua majukumu ya kutupeleka na gari lake mpaka shule.

Ilipofika saa nane tulirudi ,tuliludi nyumbani lakini hali haikuwa shwari,watu walifurika kwa wingi uku kila mtu akiongea lake "jamani huyu baba ,mwishoe atabaka wanae,msomi gani huyu"kuna mama alikuwa akiongea na mwenzake

"Yani kukupa mwanagu ,unilelee ndo unibakie,kwanini usibake wanao na hii kesi umeinunua "aliongea mamdogo kwa hasira,nakumbuka nilimuona miezi mitatu nyuma kabla ya leo ,mama mdogo jamani aliisha leo ,leo alikuwa akimnasa baba makofi
"Nyie watoto mnajisikiaje baba anavyowadharirisha"kuna mama alituuliza 

Kabla sijapata jibu nilimsikia baba akisema"jamani sijabaka wala siwezi fanya uo upuuzi yani binadamu hawana utu kabisa" baba alisema uku ajifuta majasho "kelele libaki likubwa wewe ,kula wanao"kuna mama moja aliongea kwa hasira

"Ivi ni kweli baba amebaka,amembaka diva wakati gani akati diva tuliondoka mbona sielewi hili jambo imewezekana vipi,mda huo baba aliendelea kupigwa maana polisi walikuwa hawajafika............itaendeleaADELLINA 04
Whatsap 062868079
Rogers Richard jr
Call 0628680792

..........ilipoishia "Ivi ni kweli baba amebaka,amembaka diva wakati gani akati diva tuliondoka mbona sielewi hili jambo imewezekana vipi,mda huo baba aliendelea kupigwa maana polisi walikuwa hawajafika...

"Nyie sikilizeni ,ndio mtoto amebakwa kama mnavyosema ,mlienda kituo gani ,mlienda kumpima hospitali"kuna mtu mmoja aliuliza kwenye umati ule 

Gafra! polisi walifika,walimchukua baba,mamdogo na diva ,kwa kipindi hiko hatukuweza kuelewa chochote maana tulikuwa wadogo sana ila kuhusu kubaka tulikuwa tunajua ila kwa uelewa mdogo sana

"Sasa adela usilie,baba atarudi"nilimwambia baada ya kuona anazidi kulia kwa hofu nakumbukaga ,hatujawai kuona polisi kuja nyumbani nadhani hii ilituletea hofu hasa baada ya kusikiaga polisi wanakamata wa halifu tu.

Baada ya masaa mawili ,mama mdogo na diva walirudi ,walikuja na vitu vingi vya kula ,kwakuwa njaa ilikuwa inatuuma tulivila kwa pupa,zilikuwa keki na soda na vikolokolo vingi tu.

Zilipita siku tatu,baba hakurudi lakini ajabu mama mdogo hakuondoka aliendelea kuwepo ,na tulijikuta tunafurai uwepo wake,na baba hatukumuwaza tena ,sikujua kwanini lakini ndo ilivyokuwa.

Siku zilienda adi ukafika mwaka lakini ajabu hatukuwai kumkumbuka baba mpaka leo najiuliza lakini sikuwai kupata jibu ,mwaka mmoja upoisha hali ilianza kubadilika baada ya kuingia darasa la tano ,nakumbuka mama mdogo alituambia maneno haya "itabidi muame shule muamie msasani shule ya msingi"aliongea mama mdogo siku moja 
"Kwanini mama ,adi na dada diva nae ?"nilimuuliza 

"Hapana ,dada yenu diva mpaka akimaliza form four ataendelea kusoma good samarta "alisema mama 

Tuliangaliana na adela hatukuwa na cha kuongezea ,tukaendelea na kuosha vyombo

Siku ziliendelea kwenda,uku tukiendelea kusoma msasani shule ya msingi ,maisha hayakuwa mazuri kama apo awali ,ila tuliona sawa kwa upende wetu ,tuliendelea kusoma ila gari lilibaki moja ,magari yote matatu mama mdogo alikuwa ashayauza .

"Ivi adelina mimi sielewi ujue"siku moja Adela aliuliza 

"Kwanini mdogo wangu"
"Mama alifariki,na baba aliendaga wapi,unajua sielewi jambo hili"
"Ata Mimi pia sielewi ,najiuliza baba atakuwa wapi? nakumbuka toka darasa la nne mpaka leo la sita,inamaana hatukuwai kumkumbuka"nilimwambia adela

"Tumuulize mama mdogo itakuwa anajua baba alipo"alisema adela 

Jioni moja tulikaa tukimsubiri mama mdogo ,mishale ya saa mbili aliludi akiambatana na mkaka moja ivi mweusi mfupi 

"Shikamoo mamdogo ,tulimsalimia"alituangalia juu mpaka chini "marhaba akajibu "

"Mmmmh ,mbona mama mdogo anazidi kubadilika ,bora aondoke tu ,"niliendelea kujiuliza na kujipa maoni moyoni mwangu

"Mama mdogo ,baba etu yuko wapi"aliuliza Adela

"Hahahaha mama mdogo alicheka sana,baba yenu ni huyu apa ,uku akimshika yule kijana aliyekuja nae ,ooooh au mnazungumzia yule mbakaji ,yule yupo kwa wabakaji wenzake"aliongea mama mdogo uku akicheka

"Ulinimbia mnaishi wanne ,mbona sijamuona huyo wa nne "aliuliza yule mgeni

"Ooooh yule anakaa shule ,kule kule ukilipa milioni tatu kwa mwaka unachagua mwenyewe mtoto akae shule au arudi nyumbani"alisema mama mdogo

"Na nyie mnashangaa nini tokeni apo"alisema mama mdogo

"Yani Mimi sina sketi ,ya shule mama analimlipia dada diva milioni tatu,unajua hii inafanana na ile stori ya yatima adeki kumbe kweli haya mambo yapo"aliniambia adela

"Usija adela,twende zetu chumbani kuna kitu nikakwambie nazani kitakupa furaha,nilimshika mkono nakuingia nae ndani.

Usiku akati nimelala nikaisi kitu cha tofauti ,nilihisi mtu akinishika shika ilikuwa kama ndoto ,lakini nilipofungua macho nilishituka! Kulikuwa giza alikuwa baba mdogo.

"Baba mdogo "nilimuita kwa taharuki maana sikutegemea kitendo kile,sababu mlango nilifunga kwa funguo ,iweje nimkute chumbani kwa muda ule,tena akiwa ndani ya kitanda nacholala Mimi na mdogo wangu ..............itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post