ADELLINA 04


..........ilipoishia "Ivi ni kweli baba amebaka,amembaka diva wakati gani akati diva tuliondoka mbona sielewi hili jambo imewezekana vipi,mda huo baba aliendelea kupigwa maana polisi walikuwa hawajafika...

"Nyie sikilizeni ,ndio mtoto amebakwa kama mnavyosema ,mlienda kituo gani ,mlienda kumpima hospitali"kuna mtu mmoja aliuliza kwenye umati ule 

Gafra! polisi walifika,walimchukua baba,mamdogo na diva ,kwa kipindi hiko hatukuweza kuelewa chochote maana tulikuwa wadogo sana ila kuhusu kubaka tulikuwa tunajua ila kwa uelewa mdogo sana

"Sasa adela usilie,baba atarudi"nilimwambia baada ya kuona anazidi kulia kwa hofu nakumbukaga ,hatujawai kuona polisi kuja nyumbani nadhani hii ilituletea hofu hasa baada ya kusikiaga polisi wanakamata wa halifu tu.

Baada ya masaa mawili ,mama mdogo na diva walirudi ,walikuja na vitu vingi vya kula ,kwakuwa njaa ilikuwa inatuuma tulivila kwa pupa,zilikuwa keki na soda na vikolokolo vingi tu.

Zilipita siku tatu,baba hakurudi lakini ajabu mama mdogo hakuondoka aliendelea kuwepo ,na tulijikuta tunafurai uwepo wake,na baba hatukumuwaza tena ,sikujua kwanini lakini ndo ilivyokuwa.

Siku zilienda adi ukafika mwaka lakini ajabu hatukuwai kumkumbuka baba mpaka leo najiuliza lakini sikuwai kupata jibu ,mwaka mmoja upoisha hali ilianza kubadilika baada ya kuingia darasa la tano ,nakumbuka mama mdogo alituambia maneno haya "itabidi muame shule muamie msasani shule ya msingi"aliongea mama mdogo siku moja 
"Kwanini mama ,adi na dada diva nae ?"nilimuuliza 

"Hapana ,dada yenu diva mpaka akimaliza form four ataendelea kusoma good samarta "alisema mama 

Tuliangaliana na adela hatukuwa na cha kuongezea ,tukaendelea na kuosha vyombo

Siku ziliendelea kwenda,uku tukiendelea kusoma msasani shule ya msingi ,maisha hayakuwa mazuri kama apo awali ,ila tuliona sawa kwa upende wetu ,tuliendelea kusoma ila gari lilibaki moja ,magari yote matatu mama mdogo alikuwa ashayauza .

"Ivi adelina mimi sielewi ujue"siku moja Adela aliuliza 

"Kwanini mdogo wangu"
"Mama alifariki,na baba aliendaga wapi,unajua sielewi jambo hili"
"Ata Mimi pia sielewi ,najiuliza baba atakuwa wapi? nakumbuka toka darasa la nne mpaka leo la sita,inamaana hatukuwai kumkumbuka"nilimwambia adela

"Tumuulize mama mdogo itakuwa anajua baba alipo"alisema adela 

Jioni moja tulikaa tukimsubiri mama mdogo ,mishale ya saa mbili aliludi akiambatana na mkaka moja ivi mweusi mfupi 

"Shikamoo mamdogo ,tulimsalimia"alituangalia juu mpaka chini "marhaba akajibu "

"Mmmmh ,mbona mama mdogo anazidi kubadilika ,bora aondoke tu ,"niliendelea kujiuliza na kujipa maoni moyoni mwangu

"Mama mdogo ,baba etu yuko wapi"aliuliza Adela

"Hahahaha mama mdogo alicheka sana,baba yenu ni huyu apa ,uku akimshika yule kijana aliyekuja nae ,ooooh au mnazungumzia yule mbakaji ,yule yupo kwa wabakaji wenzake"aliongea mama mdogo uku akicheka

"Ulinimbia mnaishi wanne ,mbona sijamuona huyo wa nne "aliuliza yule mgeni

"Ooooh yule anakaa shule ,kule kule ukilipa milioni tatu kwa mwaka unachagua mwenyewe mtoto akae shule au arudi nyumbani"alisema mama mdogo

"Na nyie mnashangaa nini tokeni apo"alisema mama mdogo

"Yani Mimi sina sketi ,ya shule mama analimlipia dada diva milioni tatu,unajua hii inafanana na ile stori ya yatima adeki kumbe kweli haya mambo yapo"aliniambia adela

"Usija adela,twende zetu chumbani kuna kitu nikakwambie nazani kitakupa furaha,nilimshika mkono nakuingia nae ndani.

Usiku akati nimelala nikaisi kitu cha tofauti ,nilihisi mtu akinishika shika ilikuwa kama ndoto ,lakini nilipofungua macho nilishituka! Kulikuwa giza alikuwa baba mdogo.

"Baba mdogo "nilimuita kwa taharuki maana sikutegemea kitendo kile,sababu mlango nilifunga kwa funguo ,iweje nimkute chumbani kwa muda ule,tena akiwa ndani ya kitanda nacholala Mimi na mdogo wangu ..............itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post