ADELLINA 2. (Nastahiri kulipa kwa haya)


...............ilipoishia Baada ya lisaa limoja ,nikiwa nimtoka kuamka nikawa naelekea jikoni kuchukua utupoti za chakula ,mmmmh alufu ya nyama iliendelea kunukia nyumba nzima nilifika pale nilimkuta mamamdogo ila nilishituka kwa nilichomkuta anakifanya ,nilimuona anafungua kitu kwenye fundo la kanga yake,na kutoa unga mweusi akanuia maneno machache na kuutia kwenye bakuli moja wapo la supu,nilishituka! Ila kwa kipindi kile sikujua ,kutokana na uwelewa wangu kuwa mdogo

Alivyoniona alishituka! sana akaniambia"nilisahau kuweka chumvi umu ,yani supu imeiva bila chumvi sijui ingekuaje"alijiongelesha

Naivi nilikuwa situmii nyama basi ata sikumfatili,nilichukua chakula na kuelekea zangu zebreni kwa ajiri ya kupata lunch .

"Wewe tena na uloho wako "mama aliongea

"Mama kwani nimefanya nini,mbona tunasemana asubuhi asubuhi"nilimwambia uku nimekunja mdomo kwa kipindi kile kukunja mdomo ilikuwa kawaida yangu nilishajizoesha

"Ndio adela ujamuita diva nae,achaga uchoyo muone kwanza,unafikiri ukiwai kula ndo utashiba"aliongea mama

Baada ya nusu saa wote tulikuwa tumekusanyika mezani ,mama akibadilishana mawazo na mdogo wake ,mimi nikipiga mawili matatu na adella sambamba na diva ,siku iliisha hivyo.

Baada kama majuma mawili nakumbuka ilikuwa jumanne ,tulirudi nyumbani tulikuta mama amejiinamia "mama "adella aliita taratibu mama aliinua kichwa kama kuna kitu alikuwa akikiwaza kwa muda mrefu 

"Mama kuna shida gani kwani "nilimuuliza 

"Hamna shida wanangu niko sawa"mama alijibu kiutaratibu sana

"Mama mbona unalia? "adella alimuuliza ni kweli mama alikuwa akilia machozi yalimtoka taratibu alijitaidi kutabasamu lakini ilishindikana ,machozi yalilowanisha nguo yake,hii ilikuwa mara ya kwanza kwa mama kumuona akilia hivi.

"Mama na mbona ujaenda kazini leo "nilimuuliza maana nilikuwa simuelewi kwa chochote kwa muda ule

"Jamani mna maswali wanangu,niko likizo bwana "mama alijibu uku akijifuta machozi "wanangu mkijitaidi kufaulu la nne ,nitawapa zawadi nzuri"aliongea kwa furaha akaendelea "Niko sawa wanangu niliwamisi tu kwa mnavyonipenda adi machozi yananitoka tu"kwa umri wetu sikuweza kugundua kinachomsumbua mama ni kitu gani hasa

Jioni baba aliludi ,hakuonekana kuwa na furaha kama siku zote ,sikujua kuna shida gani? lakini tulipouliza hatukupata jibu sahihi basi miezi ilikatika kama miwili hivi ,tukawa tunakaribia kufanya mtiani wa taifa wa darasa la nne.

"Mama sikuizi anakonda ujue ,"aliniuliza adela "ata Mimi naona sijui mama anaumwa nini ,au anajua atutofaulu ,sie tutafaulu bwana nilijikuta nalia"sikujua machozi yalitokea wapi ,basi nakumbuka siku tunaenda kufanya mtiani wa taifa mama alituita na kutuambia machache "jamani wanangu mtiahani uo mkafanye vizuri ,kumbukeni Nina zawadi zenu ,shauri zenu "mama aliongea kwa shida ,pembeni akiwepo na baba ,"sawa mama tumekuelewa tulitoka nje tukapanda gari la shule na kuelekea shule.

Siku tuliyomaliza mtiani ,tuliludi nyumbani kama saa tano tulimkuta mama kajifunika na shuka"mama unakaa peke yako diva yuko wapi"nilimuuliza

"Diva kashaondoka kwao,mama ake alimpigia simu aludi ,na nashangaa mdogo wangu yule naumwa ajikuniona "mama alisema

"Kwani mama unaumwa nini,si utuambie tu"nilimuuliza mama 

"Wanangu ,hamuwezi kuelewa ,ila iko hivi nimegundulika na kansa ya damu ,ugonjwa huu umenipata gafra! tu na sikuwai kuugua ila imetokea lakini nitapona wanagu sawa,apa ndo naelekea kupona "alisema mama 
"Nikama maleria tu wanangu,adelina siushawai kuumwa malaria ukapona"mama aliniuliza

"Ndio mama "nilimjibu kwa tabasamu

"Wote tulijikuta tunapata furaha,baada ya kusikia hivyo,ata mama alichangamka

"Mpigie mama mdogo wako"mama alinimbia 

"Mama situmepigia zaidi ya mara saba na sms juu kwani ajaona tu"nilimwambia

"Mpigie tena mama aliambia "dah ilikuwa inachosha unapiga simu haipokelewi

"Mama apokei bwana."nilimwambia "mtumie sms mwambie hivi mdogo wangu ubusy gani ,au ndo iko kiduka kinakupa ubusy kama hizo milioni tano zimeisha niambie nikutumie sio kukaa kimha ukumbuke dada ako anaumwa ,toka juzi nakupigia uji kuniona mdogo wangu ,au nimekukosea"aliniambia niandike hivyo nilipomaliza nikatuma.

Tuliendelea kupiga stori masaa mawili ,mama mdogo akujibu ilipofika saa nne usiku alituma tu text "nitakuja kesho jioni "alituma hivyo nilipomwambia mama ,aliitikia kwa kichwa 

"Mama vipi tena"nilimuuliza ,ata kujibu alikuwa anashidwa ,baada ya dakika kadhaa alianza kutetemeka ,hatukujua ni nin shida "adela kalete kitenge mama siunamuona ali yake,tumfunike 

Kitenge kililetwa ,tulipomfunika baada ya dakika kadhaa alikuwa kimya"mama mama tulijitaidi kumuamsha akuamka baba alimfika na kushuka "mama adela mama adellina "baba alijitaidi kumuamsha

Alipomuangalia machoni kiini cheusi hatukukiona ,sio wote hatukujua maana yake nini nilimuona tu baba akidondosha chozi........itaendelea like 170 nandosha kingine sasa ivi  

Post a Comment

Previous Post Next Post