Kaka Utatuua 1

“Aliyekufa ni huyo Malaya wako, kwanini wewe unaumia, kwanini wewe unakasirika, yaani mwanamke alishakuacha, alikua anaenda kuolewa na mwanaume mwingine lakini leo umekaa unamlilia! Huyo mwanamke ni Malaya na amepata alichokua anakitaka!” Baba aliongea kwa hasira, nakumbuka ilikua ni siku ya jumapili, wiki mbili zilikua zimepita tyangu aliyekua mchumba wa Kaka yangu kufariki dunia.

 

Ni habari amabzo ziliniumiza kwani ni mtu ambaye tulikua tunamfahamu na kwa namna flani tulidhani labda ataolewa na Kaka, lakini haikua hivyo, kila siku walikua wanagombana kupigana kiasi kwamba ikaikia hatua ya kuachana. Baada ya kuchana na huyo mwanamke Kaka yeye alienda Kozi kusoma, Kaka yangu ni Mwanajeshi, lakini akiwa huko huyo mwanamke alipata mwanaume mwingine, walianzisha mahusiano, miezi minne tu baada ya kuachana na Kaka yangu huyo dada alimpeleka mwanaume mwingine nyumbani kwao kumtambulisha ili kuolewa.

 

Kozi aliyoenda Kaka ilikua ni miezi sita, akiwa kule hakuna mtu aliyemuambia kuhusu kuolewa kwa x wake kwani alikua anampenda sana na tulijua kama tukimuambia tutamchanganya. Lakini aliporudi alikuta ndiyo maandalizi ya harusi yanaanza, alikuja kuchunguza na kujua kuwa kumbe huyo mwanamke alikua na ujauzito tena mkubwa tu. Ilikua imepita kama miezi nane tu hivi, hivyo Baada ya Kaka kumuona na mimba kubwa alihisi kuwa ni mimba yake hivyo akaanza kumfuatilia kujua kama ni yake.

 

Lakini yule Dada alimkatalia, alimuambia kuwa mimba si yake na hana mpango na Kaka.

“Unajua nilimpa mimba akatoa?” Siku moja Kaka aliniuliza, ilikua ni asubuhi kwenye saa nne hivi, aliniambia nimsindikize sehemu, mimi nilikua likizo hivyo sikua na chakufanya, tuliingia kwenye gari yake, akaendesha mpaka kwenye hospitali moja hivi, mwanzo nilijua labda kaka anaumwa, lakini alipita sehemu ya hospitali na kuenda kupaki Gari kaqriobu na kiliniki moja hivi.

 

Alikua amepaki kwa kulificha huku tukichungulia kwenye kioo kuangalia watu waliokua wakiingia na kutoka. Mwanzo sikualewa mpaka nilipomuona X wake anaingia, alishushwa kwenye gari na Kijana mmoja ambaye nilimtambua, alikua ni mchumba wake. Nilikua namjua kwakua kipindi Kaka yuko na wifi nilishamuona mara kibao wakiwa pamoja, alikua ni radfiki wa X wake Kaka yangu, walisoma na Kaka yake hivyo walizoeana ingawa si kimahusiano.

 

“Nilimuambia anizalie lakini akakataa, yaani yule mbwa nilikua namuona kama Kaka ayke ndiyo kaenda kumjaza mimba mchumba wangu!” Kaka aliongea kwa hasira, nilimuona akitetemeka kwa hasira, jaso likimtoka.

“Lakini kaka wewe si ndiyo ulimuacha, nakumbuka wewe ndiyo ulimfukuza, ukasema humtaki, hata sisi mbona hatumtaki, kwanini unahangaika na huyo Malaya, yaani mtu anatembea na Kaka yake lakini bado unampenda, unamuona kama ni mwanamke!?” Nilimuuliza kwa hasira.

“Simtaki sawa lakini kwanini azae na mwanaume mwingine, sisi tumeachana yaani hata mwaka haujaisha kashapata mtu mwingine, hivi mimi ningetafuta mwingine angejisikiaje?”

 

Nilimshangaa Kaka kidogo kwani alikua na wanawake wengi sana, hata sababu ya kumpiga X wake kila siku ilitokana na kuwa na wanawake wengi. Kaka alikua amejenga, nyumba yake ilikua ni jirani tu na nyumbani kweu, kwakau muda mwingi alikua kazini, kambini basi mimi na ndugu zangu wengine tulipenda kwenda kushinda pale. Mara nyingi alikua anamleta huyo X wake, ndugu wanajua, mpaka Mama alikua anajua na kwakua alikua anatambulika basi tulimuona kama wifi yetu, alikua ni kama mke wake.

 

Pamoja na kuwa na mwanamke mmoja aliyekua anatambulika lakini kaka yangu alikua ni Malaya sana, alikua na wanawake wengi, alikua akiwabadilisha kama nguo na mara kwa mara X wake alikua anamfumania ila anaishia kupigwa. Nakumbuka kuna siku nilikua kwa Kaka, akaleta mwanamke wake ndani, sisi tulikuepo, wakati anafanya mapenzi huko wifi alikuja, aligonga mpango na kuingia mpaka sebuleni, akakaa, kaka akatoka zake huko na taulo, akaanza kumpiga ni kwanini alikua anakuja bila taarifa.

 

Wifi alimuambia kuwa yeye pale ni kwake kwania lishajitambulisha mpaka kwao na kutoa kishioka uchumba. Kaka alimpiga sana lakini wifi alikataa kuondoka, wakati anampiga sisi tulikua tukimtukana na kumuambia kuwa aondoke kwani mwanaume hapangiwi, Kaka alimsukuma mpaka nnje lakini wifi hakuondoka. Bila aibu Kaka alitoka na yule mwanamke, akampita wifi akiwa kakaa nnje, alimsindikiza yule mwanamke, akaondoka, aliporudi alimuambia kuwa ainmgie ndani, dada wa watu aliingia ndani ila alimpiga na kumfungia stoo, hapohapo Kaka alimpigia simu mwanamke mwingine, wakalala naye mpaka asubuhi, hapo ndipo alimfungulia wifi na kumuondoa asubuhi wakati yeye akiwa na mwanamke mwingine.

 

Kusema kweli ingawa ni Kaka yangu na nilikua ninamchukia wifi yangu lakini kama mwanamke kile kitendo kiliniumiza sana, nilishindwa kuvumilai na kuamua kumuuliza Kaka.

“Nimefanya makusudi, huyo mwanaume ni Malaya sana, ana wanaume wengi nilitaka tu kumuonyesha kuwa na mimi nawez akupata wanawake idadi yoyote ninayotaka hivyo asinisumbue!” Nilinyamaza kwakua nilikua namchukia huyo mwanamke lakini hali hiyo ilikua inaniuma.

 

Tulikaa pale kwa muda mrefu, wakaingia mpaka wakatoka Kaka yuko pale anaangalia tu, kulikua na ukimya sana, alikua anaonekana kuumia inngawa hakutaka kunionyesha.

“Bado uanmpenda?” Nililazimika kumuuliza.

“Hapana, mimi, nimpende yule Malaya, kwanza nashukuru Mungu tumeachana, alikua ananirudisha nyuma sana, huwezi amini baada ya kuachana naye mambo yangu sasa hivi yanaenda sana, nashukuru Mungu sana kwa hilo.”

“Sasa mbona unamfuatilia, si tondoke!”

“Namfuatilia kwakua ni mshenzi, mimi alitoa mimba zangu mbili, hakutaka kuzaa na mimi lakini huyu mbwa kamzalia, kinachoniuma nikuwa walikua wananizunguka, haiwezekani mtu tuachane siku mbili kashaapata mtu mwingine! Walikua wanajifanya marafiki kumbe ni wapenzi, nitawafanyia kitu kibaya hawatakuja kuamini, huyu mwanamke hanijui!”

 

“Lakini Kaka wewe ndiyo ulimpiga mpaka mimba zake zikatoka, tena ile ya pili kidogoa tolewe kizazi? “ Nilimuuliza, Kaka hakunijibu, aliniangalia kwa hasira bila majibu. Nakumbuka mimba ya kwanza sikuepo lakini wifi alikua analalamika kuwa Kaka kampiga mpaka mimba yake ya miezi minne ikatoka, alilalamika kwa Mama lakini kwakua Kaka alikua na pesa na ndiyo alikua anahudumia familia hakukua na mtu wa kumuongelesha chochote, kibao kilimgeukia wifi kila mtu akisema kuwa katoa kwa makusudi.

 

Hata mimi niliamini hivyo, ilikua ni rahisi kuamini kuwa alitoa yeye kulik0 kuamini kuwa Kaka yangu alikua ni mnyama kiasi hicho. Lakini mimba ya pili niliishuhudia mimi. Nakumbuka ilikua ni usiku, wifi alikuja nyumbani, pamoja na kwamba walikua hawaishi pamoja na Kaka lakini wifi alikua akitumia muda mwingi kwa Kaka, alikua anafanya kazi na alipangisha sehemu yake, lakini muda mwingi alikua kwetu kama mke wa Kaka.

 

Kaka alirudi usiku, alikua kalewa sana, wakati anaingia ndani alikua anaongea na mwanamke kwenye simu, wifi ndiyoa limfungulia, alipomuomba amkate simu Kaka limsukuma wifi, lakini kwakua alikua kalewa basi alidondoka yeye, alipepesuka akadondoka na kujigonga kwenye meza. Hapo ndiyo shida ilianza, Kaka alianza kumpiga akimuambia kuwa anataka kumuua,. Wakati huo wifi alikua na mimba ya miezi saba, alikua na tumbo kubwa tu, Kaka hakujali, alimpiga sana tena tumboani, mar azote wifi akipigwa tulikua tunabaki chumbani kujifanya kuwa hatujasikia.

 

Lakini siku hiyo ilikua tofauti, Kaka alikua anampiga sana, wifi alikua analia, alikua analalamika.

“Niue mimi lakini usimuue mtoto, acha kunipiga tumboni, nipige hata kichwani mume wangu!” Nilijikuta nanyanyuka na kwenda kumfuata Kaka, walikua sebuleni, taa inawake, wifi alikua kalala chini, kajikunja na kukumbatia tumbo lake, alikua anamzuia Kaka aliyekua anampiga mateke ya tumboni.

“Kaka unataka kumuua mtoto, hiyo mimbi ni ya kwako?” nilimuuliza huku nikimfuata na kumushika Kaka ilia muache wifi, lakini hakumuachia, aliendelea kumpiga huku akimshutumu kuwa ile mimba si yake hibvyo nimuachie amuue.

 

Lakini sikutaaka kumuachia, niliendelea kumshika, nilimvuta mpaka ndani chumbani kwake, nikamsukuma na kumfungia ndani, kurudi ili kumuangalia wifi alikua hapigi kelele tena, alikua kalala mkatulia.

“Kaka kaua…” Niliwaza, wakati nikihahahaha mdogo wangu wakiume alitoka, alimuangalia wifi na kukuta mapigo ya moyo yapo kidogo, aliniambia tumpeleke hospitalini, lakini kaka ndiyo alikua na funguo za gari, tulilazimika kumfungulia tukachukua funguo , lakini wakati tunatoka alilazimisha mpaka tukaingia naye kwenye gari, wakati huo ni kama pombe zimekata, alikua na wasiwasi sana kila dakika akiangalia mapigo ya moyo ya wifi, alikua anahisi kafa, kwa mara ya kwanza nilimuona Kak a yangu akiwa nauoga, alikua akitetemeka kabisa akijua kuwa kaua.

 

“Kadondoka wkenye ngazi, tukifika ndiyo itakua hivyo, siwezi kwenda polisi, nitafukuzwa kazi iikijuliakana.” Aliongea njia nzima, tulifika kwenye hospitali binafsi, ilikua ndogo na ni shemu ambayo Kaka alikua akijuana na Daktari, kwa maana hiyo tulibyosema sihu ya ngazi hawakuhitaji PF3 ingawa ilionekana moja kwa moja kuwa wifi kapigwa. Alitibiwa lakini hali ilikua mbaya, mimba ilikua imetoka na alihitajika kufanyiw3a upasuaji. Nakumbuka wakati nipo na mdogo wangu wakiume tunasubiria Kaka alikua anaongea na daktari.

 

“Mtoe kizazi ili umkomoe, huna haja ya kuhangaika, huyu kizazi kikitoka hataniacha, mimi nitazaa na wanawake wnegine lakini hataniacha kamwe!” Kaka laimuambia yule daktari ambaye ni rafiki yake, lakini alikataa katakata na kumuambia kuwa kimaadili ikijulikana atafungwa na kupoteza leseni yake. Walibishana sana lakini Doctor aligoma na kuondoka, alirudi ndani, Kaka alikuja na kukaa na sisi tukajifanya kama hatujasikia. Alituelezea hali yake na kutumbia kuwa hataki tumuambie mtu yoyote.

 

Mama alijua atachanganyukiwa, tutamuambia mimba ilitoka yenyewe. Tulikubaliana hivyo ndiyo maana nilishangaa ni kwanini Kaka alikua na hsira kuona kuwa X wake kapata mwanaume mwingine na wanakaribia kupata mtoto. Mimi nilidhani kuwa kashamuacha, hampendi ndiyo maana alikua anampiga na hata ilikua ndiyo sababu ya yeye kutaka kumtoa kizazi kwakua hakua na mpango naye.

 

Baada ya wale watu kuondoka Kaka aliwasha gari kuondoka, njia nzima alikua akiapa kuwa atamfanyia kitu kibaya na harusi haitafanyika.

“Usije kupiga, utafungwa!” Nilimuambia, kwa namana alivyokua na wasiwasi nlishindwa kuelewa ni kwanini alikua anafanya hivyo, nilishindwa kujua ni kitu gani anataka kwa mwanamke ambaye tayari alishamuacha. Sikujua atafanya nini lakini kwa nilibvyokua namfahamu Kaka yangu nilihisi kuwa atafanya kitu kibaya ingawa yeye alinihakikishia kuwa hatafanya kitu kibaya.

 

“Yule mwanamke ananipenda sana, najua kuwa yuko na huyo mwanaume kwakua mimi nimemuacha, nitaongea naye, nitamuambia kuwa nimebadilika na nina uhakika kuwa atanirudia!” Aliniambia.

“Kuhusu mimba, utakua tayari kulea mimba ya mwanaume mwenzako?” Nilimuuliza, alicheka na kuniambia kuwa mimba atatoa, watu wanatoa mimba za miezi nane sembuse ile ndogo namna ile.

“Hata asipotoa, akikubali nimuoe anaweza kuzaa mtoto amekufa tukazika basi maisha yakaendelea, simpendi ila kama mimi sijapata mke bado yeye hawezi kuoa, itakua ni aibu k3wangu, watu wataona kama vile mimi ndiyo nimeachwa, mimi ni mwanaume siwezi kuachwa, nitahakikisha kuwa nawaachanisha na yule mtoto hatazaliwa.

 

Kusema kweli nilikua nahofia kuhusu Kaka, nilijua atafanya kitu kibaya, nililazimika kumuambia Mama lakini hakujali, aliongea na Kaka kana kwamba ni kitu cha kawaida ila mwishoa limhakikishia kuwa akashamuacha wifi na hamtaki kabisa. Sikuzilienda, Kaka hakuzungumzia hicho kitu tena, harusi ilikua inakaribia na kila siku nikimuuliza atafanya nini alikua ananiambia kuwa nisubiri tu ila X wake hataolewa.

 

Kitchen Party ikafanyika, ilifanyika wiki moja kabla ya Send off, hapo ndiyo nilijua kuwa Kaka kashidwa, kashakubali ukweli,. Lakini nilimuona kama ana furaha, anaongea kuwa hawezi kuolewa labda kama yeye si mwanajeshi, nilimsikiliza lakini mwisho niliona kama ni maneno ya mkosaji, niliona kama vile anaongea tu ili kujifariji lakini hana uwezo wa kufanya kitu chochote.

 

Marafiki wa wifi ni walewale na marafiki wetu kwani walisoma na Kaka yangu hivyo walikua wanajuana na watu wa aina moja. Tulikua tunajau kila kitu kilichokua kinaendelea, mpaka siku ya Send off tulikua tunajua. Ingawa hatukualikwa lakini mimi nilikua nafuatilia sana, sijui kwanini lakini nilikua na wasiwasi sana nikihisi kuwa Kaka atafanya kitu kibaya. Kuna rafiki yangu mmoja alienda, alikua ananaijulisha kila kitu kilichokua kinaendelea.

 

Wakiwa ukumbini alinitumia picha ya kila kiti. Lakini kuna kitu kilikua hakiko sawa, kwa kawaida katika sherehe nyingi maharusi wanaingia ndiyo mambo ya kutambulishana, chakula au zawadi vinaanza na mambo mengine. Lakini mpaka kufika saa tatus usiku si bwana harusi wala Bibi harusi walikua washaingia, baadhi ya ndugu walikuepo lakini wazazi na ndugu wakaribu hawkauepo.

 

Wageni walianza kupewa chakula hata kabla maharusi hawajaingia, kusema kweli kila kitu kilikua ni tofauti, rafiki yangu alikua ananiambia mpaka nikawa na wasiwasi. Walikua hawajaambiwa chochote lakini kuna hisia mbaya zilijengeka, wapo waliosema Bini harusi kagoma kuolewa, wapo waliosema kuwa Bwana harusi kagoma kuoa na mambo kibao. Manenoyalikua mengi, niliamua kumtafuta Kaka yangu, alikua kambini na simu yake ilikua haipatikani.

 

Nilihangaika kumtafuta mpaka saa sita watu walikula na kuondoka lakinio maharusi hawkautokea na hawakuambiwa kitu, wageni wengi walikua washaondoka, hata rafiki yangu aliyekua akinipa matukio alitaka sana kuondoka lakini mimi ndiyo nilimzuia nikimuambia kuwa nataka kujua kilichokua kinaendelea. Ukimbi ulikua vurugu mecho, MC hana chakuongea, kila saa anawaambia watu maharusi wanakuja lakini hakua na taarifa yoyote.

 

Mpaka saa nane usiku kila mtua likua ashaondoka na hapo hapo ndiyo Kaka yangu alipatikana kwa whatsapp. Alikua kapost status ameandika “Alichokiunganisha Mungu shetani hawezi kukitengenisha.” Nilimpigia kwa whatsapp lakini hakupokea, kama nusu saa baadaye alinipigia simu, alikua amelewa na alikua ananiambia kuwa alisema kuwa ndoa haiwezi kufungwa sikumuamini. Aliongea maneni mengi sana ya kujisifia lakini mwisho wa sikua lisema kuwa X wake kaachwa na yeye hamtaki tena alitaka tu kumharibia.

 

Sikuelewa mpaka asubuhi, niliamka nakukutana meseji za yule rafiki yangu.

“Aisee kumbe jana Bibi harusi alishindwa kuingia ukumbini kwakua amefariki, aisee dada wa watu amekufa na tumbo lake!” Baada ya hapa meseji nyingi zilianza kuingia, watu waliokua wananifahamu walinipigia na kuniuliza ni nini, mimi nilikua sijui kilcihokua kinaendelea lakini kuna meseji ilisema kuwa Bibi harusi walikua amekunywa sumu na alipopelekwa hospitalini alikufa saa saba usiku na ndiyo sababu hakuna mtu alitokea ukumbini.”

 

Akili yangu ilihamia kwa Kaka, nilijua kuna kitu kafanya, nilijau kabisa kuwa anahusika kwani alishaahidi, pamoja na ukatili wa Kaka yangu lakini sikutaka kuamini kuwa anaweza kuua. Nilimpigia simu ikawa haipatikani, nikampigia mdogo wangu ambaye naye alikua anajua hizo taarifa.

“Unahdani Kaka anahusika? Jana alikua na raha sana ?” ndiyo kitu cha kwanza ambacho aliniambia baada tu ya kupokea simu, kusema kweli sikua najibu ingawa akili ilikua inaniambia kuwa ni kuwa ni kweli Kaka kamuua wifi yangu.

 

Kwa ushauri wa mija kwa moja hakikisha unanunua kitabu changu. Kwasasa nina vitabu vitatu, cha mahusiano ya kawaida hasa kwa wanawake, cha wanaume wenye changamoto ya kumfikisha mwanamke kileleni na cha Biashara, chagua kinachoendana na tatizo lako.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post