Kaka Utatuua. Sehemu YaPili (02)

Nilijaribu kuwapigia watu ili kujua nini kilikua kimetokea lakini sikupata majibu, nilimpigia Mama na kumuambia, alionekana kujua lakini aliongea kwa wasiwasi.

“Kaka yako yuko hapa lakini hayuko vizuri kabisa, kwani kuna nini?” Mama aliniambia, sikuaka kujibishana anaye, nilitoka nikachukua Bajaji nikaenda mpaka nyumbani. Kaka alishajua kuwa X wake amekufa.

“Umemfanya Nini dada wa watu?” Nilimuuliza baada tu ya kuingia.

“Wewe una akili kweli, kwanini unaanza kumshutumu Kaka yako na ujinga wako! Kwani ni yeye kamuua, si ameamua kujiua yeye mwenyewe, kwanini unataka kumshutumu Kaka yako!” Mama aliongea kwa hasira, Kaka alikua kanyamaza kimya lakini machozi yanamtoka, alionekana kulia sana huku akilalamika.

“Ni mimi ndiyo nimemuua, Mama hata unityetee vipi lakini mimi ndiyo nimemuua!” Kaka alipiga kelele, alionekana kujutia.

“Kwahiyo umempa suimu!?” Nilimuuliza kwa mshangao lakini kabla ya kujibu Baba aliingilia.

“Hakumuua, yule mwanamke alikua ni Mlaya, anatuma tuma picha za uchi, ni bora umezitoa mapema kwani huyo mwanaume angeweza kuziona na kuoa mikosi, umemsaidia mwanaume mwenzako!”

Baba aliongea, nilikaa chini na kuuliza kilichokua kimetokea kwani nilikua siwelewi.

“Wewe ulisema kuwa utafanya kitu ili kuhakikisha kuwa hawaoeni, ni kitu gani? Nilimuuliza Kaka, aliniangalia huku akilia, alifuta machozi na kuanza kuniambia.

“Kuna picha nilimtumia mchumba wake, nikawatumia na wazazi wake na wakwe zake, nilitaka kumuaibisha ili tu aachike nimuoe mimi lakini sikujua kama tajiua, niamini nikikuambia kuwa kama ningejua kuwa atajiua basi nisingezituma.” Aliniambia, nilimuuliza ni picha gani lakini hajkua tayari kuniambia, nilimuaomba kuziona ila akaniambia kuwa ameshazifuta.

“Huyo mwanamke alikua anapiga picha anatumia wanaume, sasa Kaka yako naye katumiwa na mwanaume wake mwingine, alitumiwa kipindi wapo pamopja, sas andiyo sijui waligombana akakasirika na kuziituma, si unajua kwenye mapenzi ukiumizwa wakati mwingine unakua na hasira. Muache Kaka yako apumzike, kaumia sana, muache ana mawazo ameumia sana!” Mama aliniambia, waliongea mamboa ambayo sikuyalewa, yaklikua hayaingii akilini, kwa nilivyokua namfahamu wifi, kwa namna Kaka alivyokua anamchunga niliamini kuwa kama ngekua anachepuka na kuona picha za uchi amabzo amepiga na mwanaume mwingine basi angemuua.

Nilijaribu kuulizia na kutaka kujua lakini Bbaa alinikataza, aliniambia niondoke kwani Kaka kaumizwa sana na msiba wa X wake hivyo nisimsumbue. Niliondoka lakini sikurudi nyumbani, nilimafuta rafiki yangu amabye alienda kwenye msiba, niliatka kuoanana naye lakini hakutaka kunioa, alisingizia yuko bize lakini sikukubalia, nilikua najua ofisini kwake hivyo nilijitahidi mpaka nikaenda huko.

Aliniona na hakua na namna, ilikua ni lazima kuongea na mimi, nilitaka kujua kuwa ni kiu gani kimetokea.

“Hivi Kaka yako ana akili wkeli?” Alianza kwa kuniuliza.

“Kwanini, mbona unanichanganya, kwani kafanya nini?” Nilimuuliza kama nalazimishia kwani niliona kama anazunguka zunguka sana, sikutaka kuendelea kuzungushwa.

“Kaka yako alikua anataka Dada wa watu aachane na mchumba wako ili warudiane, lakini Dada wa watu alikataa, kumbe Kaka yako alikua na picha za uchia mabzo alimpiga, sijui na mavideo wakkiifanya mapenzi, akamtishia kuwa atazisamabza lakini Dada aligoma kabiasa kurudiana naye, hapo ndipo alikasirika na kuanza kuzisambaza.

Alichukua namba za wazazi na ndugu wa karibu wa mwanaume nakuwatumia video na picha za ucni, akamtumia Baba wa bibi harusi na ndugu wengine, kisha akamtumia na mwanaume. Dada wa watu kuja kuona basi akapaniki, alipopigiwa simu kuwa kuna picha zake na sijui ni nani alimpigia basi akatumiwa naye hizo picha na ndugu yake, unaambiwa alichukua vidonge na kumeza.

Yaani huwezi amini Kaka yakoa livyomshenzi kazituma wakati dada wawatu anatoka kazini, sijui sasa walimpigia simu, sijui ilikuaje lakini ndiyo hivyo, amerudi nyumbani, kaingia kachanganay vizonge unaambiwa zaidi ya mia kanywa….” Aliongea maneno mengi lakini sikutaka kuamini kuwa kweli Kaka anaweza kufanya vitu kama hivyo, ni kweli Kaka yangu alikua ni smhenzi sana lakini si kwa kiwango hicho.

“Lakini huyo mwanamke si ndiyo alikua anasambaza mwenyewe video zake, mna uhakika gani kuwa ni Video za Kaka yangu, kama ni wanaume wengine wameamua kutuma, kwani Kaka alitumia namba yake?”

“Aisee mimi sijaziona lakini kwenye hizo video Kak ayako hata hajajificha, nasikia anaonekana na alipokua anatuma alijirekodi kabisa akimtukana mchumba wa marehemu kuwa hata kama anaoa asijekudhani kuwa anapendwa balia naoa Malaya. Sijui lakini ndiyo hivyo, kaka yako anahusika na kila mtu analia, ndiyo amaana sitaki hata kuonekana na wewe, nyie watu ni mashetani, kumbe mlikua manajua kuwa Kaka yenu anampiga na kumnyanyasa huyo mwanamke lakini mkakaa kimya, hapana, ondoka sitaki ushoga.”

Maneno yake yalinichoma lakini nilijiafnaya sijui chochote, nilimuambia mimi sijui kitu ndipo alinishushua.

“Kila mtu anajua, kila mtu anaijua familia yenu, huna haja ya kuigiza na kudanganya, unafikiri nani hajui kwua mlimtoa mimba mbili na mlitaka kumtoa kizazi. Yule Daktari ni rafiki wa familia, alisoma na Binamu wa marehemu, au ulikua hujui, na kipindi hicho yeye ndiyo alimuambia ilia aachane na Kaka yako kwani atakuja kumuua, kila kitu kiko wazi, jinsi Mama yako alivyuokua anamtetea Kaka yako.

Mtoto wa watu alikua anapigwa mnamfungia ndani na kumtishia asimuambie mtu, kila kitu kinajulikana, aisee toka hapa sitaki hata kuonekana na mtu kama wewe! Nyie ni mashetani aisee na Kaka yako kaua!” Aliniambia huku akinisukuma nitoke, kweli nilitoka kwa aibu kwani kila kitu alichokua akikiongea kilikua ni kweli. Nilitoka nnje na kumpiigia simu mdogo wangu, aliniambia kuwa yuko nyumbani na Kaka hali yake si nzuri kwani naye anatishia kujiua, anajisikia vibaya kwa kusababisha kifo cha X wake.

Kusema kweli nilijua kabisa kuwa Kaka anaigiza, sikutaka kuamini kuwa ana uchungu. Lakini siku ile alishindwa kwenda kazini, muda wote alikua ndani akijuita kitu alichopkua amekifanya. Roho ilikua inaniuma, kwa mara ya kwanza nilivaa viatu vya wifi na kumuona Kaka kama shetani, kusema kweli nilimchukia sana. Kila nikikumbuka namna yule dada alivyokua anapigwa nilihisi kutapoka.

Sikuenda nyumbani mpaka siku ya tatu, ilikua ni siku ya mazishi ya X wa Kaka yangu. Nilienda kwakua Mama alinipigia simu.

“Njoo uongee na Kaka yako, anataka kufanya kitu cha ajabu!” mama aliniambia, nilisangaa na kumuuliza ni kitu gani, akaniambia kuwa Kaka alikua anataka kwenda kwenye mazishi ya X wake. Kweli kilikua ni kitu cha ajabu, lakini Kaka alisisitiza, nilienda kumuona ili kuongea naye. lengio lilikua ni kumshawishi ili asiende lakini nilipofika hatkuata kabisa kuniona, alikua anataka wkenda na alishajiandaa.

“Nataka nikamuombe msamaha kabla hajazikwa, nataka watu wanione, kama nikuniua waniue, nimemfanyia makos amakubwa sana!” Kaka aliongea, alikua analia kama mtoto na kusisitiza ni lazima aende.

“Itabiodi uende naye, hawezi kwenda peke yake!” Baba aliniambia, nilimuangalia Baba kwa mshangao, niliona kama na yeye kachanganyikiwa, yaani baada ya yote hayo nipeleke sura yangu katika ile familia? Hapana, sikua tayari kwa huo ujinga, kwangu ilikua ni bora kufa kuliko kufanya hivyo.

“Unaniangalia nini? Nimekuambia unaenda na Kaka yako, yule alikua ni rafiki yako, wanakufahamu, Kaka yako hawezi kwenda peke yake, kwa hali yake hapani! Anaweza kufanya vurugu, muite na mdogo wako muende wote!” nilijaribu kupinga lakini haikusaidia, kaka alishaamua kwenda na wazazi wangu hawkaua tayari kumuacha aende peke yake. Kusema kweli nilijihisi kuchanganyikiwa, kwa mara ya kwanza niliichukia familia yangu, nilikua natamani ningezaliwa na wawazi wengine.

Sikujua ni kitu gani kingetokea lakini nilijiandaa kukimbia, nilivaa suruali ndani, raba nikavaa na gauni juu ili mambo yakibadilika basi nikimbie. Tuliiingia kwenye gari, mimi ndiyo niliendesha mpaka kwenye msiba. Ilikua ni mchaana kwenye saa anne hivi na wakati tunafika watu walikua wanapita kuaga. Kaka alitangulia na sisi wengine tukaw atuko nyuma, watu walituangalia, msiba ulikua na watu wengi sana kiasi hata kupita ilikua ni ngumu.

Watu walikua wanajua kuwa Bibi harusi kajiua kwasababu ya picha za uchi kusambaa, ingawa hawkaua wengi kihivyo lakini walikua wanajua ila walikua hawamjui aliyezisamabza. Kaka yangu hakua anajulikana sana kwa mwanamke, hata ndugu waliokua wanamjua walikua ni wachache wale wa karibu, kwa maana hiyo tuliweza kupenya tukapanga mstari kuaga huku mimi nikijificha kwa kujifunika.

Wapo watu ambao walimtambua Kaka yangu, lakini hawakufanya chochote kwani ni wachache wlaikua wanajua kuwa yeye ndiyo katuma hizo picha mpaka kupelekea Bibi harusi kujiua. Nilishukuru Mungu kwa hilo huku nikimihi kaka kujificha na kuhakikisha anaaga kimya kimya, nilimuomba asilie wkani ndugu wakaribu watajua kuwa amekuja na itakua shida. Lakini Akaka hakujali alikua anatembea kama vile hajafanya kitu chochote, alikua akilia kimya kimya kila dakika akifuta machozi.

Tulipokua tunakaribia jeneza macho yangu yaligongana na mdogo wa marehemu wakiume, alituona, akamuona Kaka, hakuongea kitu aliondoka alipokua amesimama pembeni kidogo ya jeneza lililokua na mwili wa dada yake. Baada ya kama dakika moja hivi walikuja watu wawili ambao sikuwafahamu, walimfuata Kaka na kumuomba aondoke pale lakini kaka alikataa.

“Nimekuja kumuaga mpenzi wangu, mpaka anakufa tunapendana, anapaswa kunisamehe hivyo siwezi kuondoka hapa mpaka anisamehe!” kaka aliropoka kwa nguvu, watu waliokua pale walishtuka na kuanza kumuangalia, baada ya kuona kuwa analzimishjia kukaa pale wale watu aliondoka. Walimuacha aendelee kuaga. Lakinia likuja mchumba wa marehemu, yule Kaka amabaye alikua amepanga kuoana na marehemu. Alinifuata mimi na kuniuliza.

“Mnafanya nini, hembu kuwanei hata na aibu, kwahiyo mkajikusanya familia nzima kuja kuhakikisha kuwa amekufa kweli? Muacheni mke wangu apumzike kwa amani!” Aliongea kwa sauti ya chini sana lakini iliyojaa majonzi, machozi yalikua yanamtoka akijizuia. Mimi nilinyamaza kimya nikishidnwa hata cha kujibu.

“Wewe ndiyo umemuua, usingemchukua mchumba wangu asingeniacha, wewe ndiyo umesababisha ajiue!” Kaka alimgeukia mchumba wa marehemu na kumuambia. Ni kama Kaka alitaka kuleta ugomvi, ila yule Kaka alikua mstaarabu hakujibu chochote.

“Nakuhakikishia utajuta kuzaliwa, hunijui vizuri, kitu ambcho nitakufanyia basi hutatamani kuishi, uatatamani ungekufa wewe na si mke wangu. Kwa taariffa yako mimba aliyokua nayo marehemu ni yangu!”

Kaka alikua anapandisha sauti, nilimshika kumsihi anyamaze lakini ndiyo kwanza nilikua nampandisha hasira. Kuona hivyo yule Kaka aliondoka harakaharaka ili kuepusha sahari. Kaka alitaka kumfuata kama ampige lakini nilimshika.

“Umekuja kuaga na kuomba smamaha, fanya hivyo.” Nilimuambia,a likubali tukatembea mpaka kwenye jeneza, kusema kweli mimi sikuweza kuangalia mwili wa marehemu, nilikua najisikia vibaya na kuona aibu. Lakini kaka alipofika alipiga magoti, alianza kulia kiama mtoto mdogo, kila mtu alimshangaa, kuna watu walitaka kumshika lakini ndugu wa marehemu waliwaambia wamuache. Dakika tano nzima Kaka alikua kapiga magoti, analia, anaomba msamaha na kuongea maneno mengi mengi, mwisho alikuja Mchungaji, akamshika na kumuombaa anyanyuke, alikubali akanyanyuka akatoka nnje na sisi tukamfuata.

Kila mtu alikua anamshangaa lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye alimsemesha. Baadhi ya ndugu wamarehemu wa karibu walikua pale nnje, tuliwapita wakitushangaa, tukaondoka mpaka kwenye gari. Kaka aliingia kwenye gari na kutaka kuendesha yeye, nilitaka kumzuia lakini alilazimishia, nikaona isiwe shida, anaweza kuleta vurugu na kuharibu mambo kabisa. Aliendesha gari kwa kasi lakini hakurudi nyumbani, alienda mpaka baa na kuanza kunywa, hatukuweza kumuacha mpaka usiku alipokunywa akazidiwa mpaka akazima ndiyo tukambeba na kumuweka kwenye gari kisha kiumrudisha nyumbani.

***

Baada ya vituko alivyokua amevifanya siku ya msiba kila mtu alimjua Kaka, kila mtu alijua kitu alichokua kakifanya. Picha za uchi zilitumwa kwa ndugu wa karibu, kwa maana hiyo watu wengine walikua wanajua kuwa kuna dada kasambaziwa picha za uchi lakini hakuna ambaye aliwahi kuziona. Hata sisi hatukuziona na Kaka alitumbia kuwa ni picha ambazo nayeye aliumiwa na mwanaume mwingine ikionyesha kuwa marehemu ndiyo alikua anazisambaza kwakua ni Malaya.

Ingawa mimi sikuamini lakini wazazi wangu waliamini hivyo na walimuona Kaka kama malaika, waliona kama anahukumiwa bure.

“Umemsaidia mwanaume mwenzako, unafikiri usingemuonyesha akamuoa Malaya ingekuaje?” mara kwa mara Mama alikua anamuambia Kaka, alikua anamuambia kumpa moyo kwakua tangu mazishi Kaka alikua ni mtu wa kukaa ndani, akitoka anakunywa m,paka anarudishwa, hata kazini alikua haendi, simu zake hapokei. Ilibidi Baba kwenda kumuombea ruhusa kwani alikua akifahamiana na baadhi ya watu Jeshini.

Huwezi amini w3laianza kumuambia kuwa aoe, atafute mwanamke mwingine aoe kwani marehemu ni kama kamuachia gundu na bila kuoa anaweza asipate mwanamke mwingine tena. Kaka hakutaka, alikua na mawazo mengi na kila wakati alikua ni mtu wa kujilaumu tu. Pamoja na kujilaumu yeye lakini alikua pia anamlaumu mchumba wa X wake, mwanaume ambaye alitaka kumuoa, alimlaumu kwakua kabla alijua ni rafiki wa kawaida lakini aliumia kwakua anamuoa mchumba wake.

“Walikua wananidanganya, muda mrefu ananiambia ni rafiki yake, ni kama ndugu lakini kumbe wananigeuka?” Kaka akilewa alikua anaongea.

“Huwezi amini hata mimi tulishakuaga marafiki, yaani yule ni shateni, nilishawahi kumnunulia bia zangu kumbe anatembea na mke wangu!” Aliongea kw3a hasira, ingawa hakusema kitu chochote lakinia lionekana kama ni mtu mwenye kisasi, ni kama alipanga kumfanyia kitu yule mwanaume. Mimi nilikua namsihi kuwa aachane na hayo mambo lakini alijifanya kama hamna kitu ni wasiwasi wangu tu.

“Kwahiyo unaniona mimi mnyama, uandhani naweza kufanya kitu chochote kibaya?” Aliniuliza, nilimuambia hapana lakinia anapaswa kuwa makini.

“Wale watu wameumia, wanaomboleza, yule Kaka hana kosa, wewe ulishaachana na wifi hivyo alikua na haki….”

“Haki haki gani? Nyie wanawake ni Malaya sana, kwahiyo na wewe unaweza kufanya mambo kama aliyokua amefanya huyo marehemu, nimemsamehe lakini naumia sana, halafu anaenda kujiua kisa picha za uchi, mimi nilituma ili waachane lakini si kujiua…

Ningejua nisingetuma, yaani, naumia sana, kwanini ameamua kufanya hivi….” Alianza kulia tena, ni kama dakika mbilia anjilaumu yeye, dakika mbili anamlaumu mchumba wa X wake na dakika mbilia namlaumu X wake kisha anarudi kujilaumu. Kusema kweli ilikua inaboa, tulilazimika kuwa naye karibu kwani wazazi wangu walikua wanhdani anaweza kujidhuru. Kusema kweli niliona kama anaigiza kwa namna nilivbyokua namfahamu Kaka nilijua kuwa hajaumia kihivyo ila kwa jinsi wazazi wangu walivyokua wanauliza uliza kila saa, kuonekana kuwa labda yeye dniyo kaumizwa ilimfanya Kaka kudake kama mtoto.

“Hawa ndio wanamharibu! Huyu hajaumia chjochote, namfahamu!” mdogo wangu aliniambia, naye alishachoka tabia za Kaka lakini hakua na namna, yeye ndiyo alikua ndugu wapekee wakiume, alitakiwa kukaa naye ili tu asijidhuru.

‘Kaka ni mshenzi, linakua kama llitoto, unajau anamlaumu mchumba wa Marehemu eti ndiyo kasababisha, yaani ujicha mtupu, na Mama anamdekeza yaani kama yeye dniyo kafiwa.” Nilimuambia.

“Anaigiza mshenzi huyu, juzi kaenda kukuatana na mwanamke mwingine, jana kaondoka nyumbeni kaenda kwake, kalala na mwanaume na kampiga dada wa watu, namuuliza ananiambia kuwa bado ana hasira za huyo X wake, Kaka sio kabisa!”

Kila mtu alichoka na baada ya mdua tuliacha kukaa na Kaka, wiki mbili baadaye aliacha kujidekeza na akarudi kazini, maisha yaliendelea kama kawaida. Siku moja usiku tukiwa nyumbani kwa Kaka, mimi na mdogo wangu ndiyo pekee tulikua tukiishi pale kwani Kaka alikua kambini na hatukutaka kwenda nyumbani. Usiku kwenye saa mbili hivi kuna mtu alikuaj na kugonga mpango. Nilienda kufungua, ila nafungua tu na kutana uso kwa uso na aliyekua mchumba wa marehemu.

Alinisalimia wakati nashangaa na kuniomba kuingia ndani, kusema kweli nilishindwa ni jibu nini nilishikwa na butwaa lakini kabla hata sijamjibu kitu aliingia ndani na kufunga geti, gari yake aliiacha nnje.

“Haitachukua muda sana,” Aliniambia akiongozana kuingia ndani.

“Lakini Kaka hayupo kama ndiyo ulikua unmamtaka.” Nilimuambia, nilihisi labda kuna vitu anataka kuongea na Kaka.

“Hapana, si mhitaji yeye, najua hayupo, ameenda Iringa, kuna kazi katumwa na atarudi baada ya siku tatu, sikuja kumuona yeye bali ninataka kuonana na wewe na mdogo wako nyie pia si mlikua mnaishi na marehemu hapa?” Aliniuliza, nilimuitikia ndio ingawa sikujua sababu lakini nilidhani labda ana maswali kuhusu maisha ya marehemu.

Niliona labda alikua ameshindwa ku move on ndiyo maana kaamua kuja, niliwaza mambo mengi lakini yeye hata hakujalli kuwa mimi sikuwepo. Aliingia mpaka sebuleni, bila karibu alikaa chini, akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa flash.

“Hii Tv yenu si inatumioa flash?” Aliongea hukua kitembea kuelekea kwenye TV kubwa pale sebuleni, aliiwasha na kuchomeka Flash, alifanya kama mwenyeji, ingawa sina kumbukumbu lakini ni kama alishawahi kuingia pale, alichomeka flash na kuniambia nikamuite mdogo wangu kwani kuna kitu anataka kutuonyesha.

Alirudi kwenye Sofa na Kukaa, nilitoak na mdogo wangu ambaye naye alishangaa kumuona pale, lakini yeye hakujali, alituambia tukae pembeni yake, ingawa alikua anaongea kawaid alakini ni kama alikua analazimishia flani, tulikubali na kukaa.

“najua mnaishi na Kaka yenu, mnajua tabia zake na mnawaza hivia kija kujua kama nimekuja nyumbani kwake atafanya nini? Msijali hatafanya chochote.” Aliongea na kunyamaza kidogo kisha akaendelea.

“Ninajua kuwa mnajua tabia zake, mnajua ushenzi wake lakini kuna kitu nataka muone, nataka mjue kuwa maisha yenu kuanzia siku ya leo yatabadilika sana, kuna vitu nitavifanya mpaka mtatamani hamkuwahi kuzaliwa ila wakati ninavifanya nataka mjue ni kwanini navifanya.”

Aliongea kwa sauri ya chini kabisa, lakini alionekana kumaanisha, ilijaa hasira sana na visasi. Flashi iliwaka, kwanza ilianza kuonyesha picha mbalimbali, zilikua ni picha zamarehemu za kawaida, kisha zikafuata picha za uchi, alionyesha picha nyingi za uchi za marehemu, akiwa amepigwa Kalala, nyingine amepigwa akiwa anajuakama vile kajiandaa kupigwa, picha akijichezea mwili wake na picha nyingine za ajabu ajabu.

Baada ya hapo zilifuata video, video ya Kwanza ilikua inemuonyesha Kaka yangu, yupo uchi wa mnyama anamlazimisha marehemu kukaa vizuri ili wafanye mapenzi na kuonekana kwenye kamera. Kusema kweli nilishindwa kaungalia nikajikuat naangalia pembeni.

“Hivi kwanini unatuonyesha, si uache haya mambo yapite, hapo unamdhalilisha Marehemu!” Nilimuambia, alinigeukia kwa hasira kisha akaniambia.

“Bado hujaanza kuona, nataka uone kila kitu, nataka ujue kitu alichokiafanya kaka yako!” Aliongea kwa hasira, alinilazimisha kuangalia, ile nageuza tu macho nilitamani kutapika kwa kitu alichokua anakifanya Kaka!”

NB; Kuna vitu katika maisha tunavifanya tukiviona vya kawaida ila mwisho wa siku vinaumiza wengine. Watu wanauliza hivi hii stori ni ya kweli? Mimi nawauliza, ni video ngapi za uchi ushawahi kuziona mitandaoni zimevujishwa na wanaume tena wengine watu tulikua tunawaona wamaana. 

Je unafikiri hao mabinti wanakua katika hali gani wakidhalilishwa, naongea nao, kuna watu wshenzi, Binti, mwanaume akikuambia umtumia picha ya uchi muambie hapana, akinuna kwakua hujamtumia muambie kwaheri! Nasikia mengi sana naona mengi sana, and yes hiki kisa kinamhusu mtu!



INAENDELEA


Post a Comment

Previous Post Next Post