UMAKINI KATIKA MAISHA



Usipokuwa MAKINI katika jambo dogo unaweza ukawa muhanga wa kukosa fursa katika jambo kubwa.Mambo madogo na yenye kudharauliwa na watu wengi ndio mambo pekee yenye kuharibu kwa ukubwa kamili malengo ya watu wengi.Kuna wakati mazingira yanaweza kukudanganya na ukikubali kuyafuata unapotea.

Kuna wakati katika Maisha ya MTU yeyote yule mazingira Fulani yanaweza kukuhamasisha uamini uongo kuliko ukweli.Mazingira yanaweza yanaweza kukupa fursa ya kutoka hapo ulipo ikiwa ni eneo sahihi na kwenda eneo jingine ambalo huenda sio sahihi.

Mazingira yanaweza kukuonyesha uchungu mkubwa na kukupa ushahidi wa wewe kuuamini uongo kuliko ukweli.WATU wengi wamejikuta wakifanya maamuzi ya hovyo sana kutokana na kutokuwa MAKINI na mazingira yanayokuja mbele yao.

Wapo wengi waliodanganyika na kuingia mahali pasipo faa katika Maisha kutokana na hali ya kukosa umakini katika Maisha yao.Taarifa unazozipokea kutoka kwa watu wengine Lazima uwe nazo MAKINI na uzichambue vizuri kuliko kuchukua HATUA kwa haraka.Mazingira unayokutana nayo yenye mbele yako yenye utata lazima uwe nayo makini ili usipotee.

Mazingira yanaweza kuwa mema sana kwako na yakakupa raha sana lakini kumbe yanakuandaa kuwa mtumwa hapo baadae.Ni kweli unaweza ukayapenda sana na kuyaishi lakini yatakupotezea muda Na utakapogundua kuwa ulikuwa mahali sio sahihi utakuwa umechelewa sana.Ni heri kuwa MAKINI katika kila HATUA unayoipitia.

Kuna wengi wanaofikiri kupitia mazingira magumu ndio maandalizi ya mafanikio hivyo kujiingiza katika maumivu kwa sababu duni.Kitu ambacho sio kweli ,sio kila Mara utafanikiwa baada ya kujeruhiwa unatakiwa kujua kuna wakati utafanikiwa bila hata kujeruhiwa kabisa.

Mazingira yanayokuja mbele yako yasikudanganye ukahama sehemu uliyopo kwenda sehemu nyingine.Mazingira yasiongoze Maisha yako.


Post a Comment

Previous Post Next Post