"HOUSE BOY" 21---22----+23



ENDELEA.....
""""Baada ya Mama Amina kuhisi ndani ya bafu kuwa kuna watu alisogea karibu alipojaribu kuufungua haukufunguka,alihisi kitu hapo alipofikiri vizuri alikumbuka Kuwa Mme wake yupo anamtafuta Amina,alimwita Amina akijua Amina atakuwa bafuni humo na Mama Amina machale yalianza kumcheza.

""""""Mama Amina aliita kwa sauti ya Chini sana, akisema ""Lauson fungueni mlango ni mimi Mama Yako nataka niwasaidie Baba yenu anawatafuta fungueni mlango,Lauson na Amina walikubalina wafungue mlango.

""""Mama Amina alishanga sanaa kumuona Lauson akiwa uchi huku Amina akiwa ndani ya Taulo tu,alishangaa kuona mashine ya Lauson iliyokuwa imevimbaa na kusimama kwa hasira zaidi,Mama Amina aliwaambia""Mme wangu anakuita Amina na akikukuta humu ukiwa na Lauson hatokuelewa kabisa .

'""""'Mama Amina alipiga mahesabu ya haraka akawashauri kitu, alimwambia Lauson atoke bafuni humo na akimbie kuelekea chumbani kwake,Amina abaki bafuni humo ili Mzee James atambue kama Amina alikuwa bafuni,Lauson alivaa haraka akachukua nguo zake akatoka bafuni na kukimbilia chumbani kwake.

"""""Lauson alikimbilia chumbani kwake kwa haraka na baada ya kufika chumbani alifika anajilaza kitandani huku akiwa na mawazo sanaa kilichotea mda si mrefu, aliona mda wowote kinaweza kunuka hapo nyumbani alijiandaa kwa kila kitu kitakachotokea akijisemea moyoni mwake kuwa yupo tayari kukabiliana nacho.

''''''''Mzee James alipokuwa alirudi sebuleni baada yaa kumuita mda mrefu Amina bila yeye kuitika,alipokuwa amekaa sebuleni hapo aliona Mama Amina akija mbio akafika anamwambia'''' Amina yupo anaoga ulivyokuwa unamuita alikuwa hakusikii" duuh! Mzee James kusikia hivyo alisikasilika sanaa akasema""""Kwahiyo sauti yangu yote hiyo namuita unataka kuniambia alikuwa haisikii.

""""""Mzee James hasira zilimpanda zaidi alipokumbuka kuhusu ile chupi aliyoiona pale sebuleni chini ya Meza alizidi kuvurugwa zaidi na alipojumlisha yale matukio yote aliyoambiwa na Mzee Kimola hasira ndivyo zilivyozidi kumpanda zaidi .

""""Mama Amina aliingia jikoni kuendelea na mapishi,Amina baada ya kumaliza kuoga aliingia chumbani kwake kubadili nguo kwa haraka ,alipomaliza kubadili nguo aliona amtumie meseji Lauson" Mpenzi Baba leo anahasira sana sijui leo itakuaje duuh? ngoja mimi niendee nikamsikilize, kisha akamtumia ujumbe Lauson kwenye simu halafu yeye akaenda sebuleni alipokuwa baba yake.

""'Lauson meseji iliingie kuifungua akakuta ujumbe Wa Amina alipousoma aliuelewa kisha akamjibu' Mpenzi wewe usijari mimi nipo hapa kwa ajiri yako lolote litakalo tokea nishitue nije nimfundishe huyo Mzee Adabu" alimjibu Lauson Amina na akawa ameutuma.

"""""Tukirudi kwa upande wa Amina,Amina alijianda haraka na mda huo alikuwa akitembea kuelekea sebuleni,ghafla simu yake iliingia ujumbe kutoka kwa Lauson aliuufungua na kuusoma, baada ya kuusoma alitabasamu tu moyoni alifarijika na roho ya woga iliyokuwa imeutawala moyo wake ilimtoka.

""'"Amina alitembea hadi sebuleni ,alipofika tu alikutana na sura ya Baba yake iliyokuwa imekunjamana na kujaa hasira,Mzee James alipomuona tu Amina alimuuliza"" we mtoto toka nakuita unataka kuniambia kuwa ulikuwa hunisikii au ni dharau tu unazonionyesha Mimi Baba yako" naomba unijibu kwanza naomba ukae hapo usinisimamie kama mbele yangu kabla sijakuzabaa vibao hapa!!

    
""""Duhh!! Amina alibaki kumshanga Baba yake ambaye kwa wakati huo hata macho yake yalikuwa yameshakuwa mekundu,Alimuuliza Amina"""we Amina mdogo wako yupo wapi? Amina alimjibu amelala chumbani kwake anaumwa!!,Mzee James baada ya kusikia Martha anaumwa hasira zake zilizidi kuongezeka mara dufu! kwanza alisimama.

""''" Akamuuliza tena Amina umesema anaumwa Martha? toka lini anaumwa mbona mimi sina taarifa,Amina alimjibu akimwambia Baba Martha na Lauson walipata ajari ya gari walipokuwa wametoka mjini wakija nyumbani.

'""""'Mzee James alishangaa zaidi kwa taarifa mpya alizozipata,hata Mama Amina aliyekuwa jikoni akiendelea na mapishi ili bidi asitishe kwanza mapishi akaja sebuleni alipokuwa Mme wake na Amina ili kupata taarifa zaidi kwani taarifa hizo kwake zilikuwa ngeni.

""""''Waliongozana Mama Amina,Mzee James na Amina moja kwa moja hadi chumbani kwa Martha ,walipofika tu Baba Amina alifika anamuamusha Martha wakisaidiana na Mama Amina,Martha aliamuka na kukaa kitandani hapo ingawa alikaa kwa shida sana ila alijitahidi kukaa hivyo hivyo.

"""""Baba Amina na Mke wake walianza kumuuliza maswali kwa mkupuo kwani walikuwa wakimpenda sana ntoto wao huyo kwakuwa alikuwa mpole sana na msitalabu kuwazidi watoto wote wa Mzee James ,hivyo Martha alipendwa sanaa,Martha alimjibu baba yake akimwambia "Baba mimi na Lauson tulipata ajari wakati tukirudi nyumbani,Martha aliwaonyesha michubuko aliyoipata kutokana na ajari hiyo aliyoipata.

'""""Mzee James alimuuliza vipi unaweza kutembea? Martha alimjibu akimwambia" Baba mimi naweza kutetembea ila natembea kwa kuchechemea,Mzee James baada ya kusikia hivyo ndivyo alivyozidi kupagawa zaidi kwani siku ya jumatatu ya wiki iliyokuwa ikifata ingetakiwa Martha aende chuo kuendelea na Masomo ila kutokana na hali yake hiyo asingeweza kuopona kwa mda wa siku nne.

"""""""Mama Amina alishangaa sanaa kumuona mtoto wake akiwa katika hali hiyo wakati ni asubuhi tu alimuacha nyumbani akiwa mzima na akitembea vizuri tu,Mzee James alimuuliza Martha'' Mwanangu niambie Lauson yeye amepata jeraha wapi? anaweza hata kutembea kweli' akitegemea kupewa jibu kuwa Lauson amevunjika mguu na hawezi kutembea ila jibu alililo lipata hakuamini kama lingekuwa ndio jibu sahihi kwake yeye kulipata katika wakati huo.

"""""Martha alimweleza Baba yake kila kitu"""alimwambia Baba Lauson ni mzima na hana jeraha lolote zaidi tu ya mikwaluzo na michubuko ila anatembea vizuri na kila kitu anaweza kufanya tofauti na mimi,Baba Amina kisikia hivyo alizidi kuchanganyikiwa zaidi alitoka chumbani kwa Martha mbio hadi chumbani kwa Lauson.

"""''Mzee James alipofika mlangoni kwa Lauson hakutaka hata kubisha hodi alizama hadi ndani,kwani mlango ulikuwa wazi alipitiliza hadi kitandani alipokuwa amejipumuzisha Lauson,kufika kitandani hapo alifika anavuta shuka alilokuwa amejifunika Lauson,Lauson akili yake haijaa kaa sawa alishitukia kofi nzito likitua kwenue mashavu yake paaaaah!!!.

"""""""Lauson alisimama kitandani hapo kwa hasira alipotaka kumludishia kofi mzee James alifikiria kitu baadae akawa ameushusha mkono wake,alikaa kitandani huku akiwa na hasira na jaziba,Mzee James alianza kuporomosha matusi kwa Lauson""""hivi wewe kijana unatafuta nini kutoka katika familia yangu ulikuwa umempeleka wapi mwanangu? nijibu si nina kuuliza we mpumbavu kweli.

""'"'Lauson hasira zilizidi kumpanda zaidi hadi akaanza kutetemeka,Mzee James siku hiyo aliyatoa mambo yote yaliyokuwa moyoni mwake kuhusu Lauson,'''''' aliedelea kutukana we malaya unafikiri mimi sijui tabia zako chafu unazozifanya humu ndani ebu niambie ile asubuhi ile chupi niliyoikuta pale sebuleni chini ya Meza ilikuwa ya nani?

""""""Lauson mda huo alikuwa kimya tu,Mzee James alipoona Lauson hajibu kwa akili yake alijuwa ni dharau anazo muonyeshea'" ,alipaniki zaidi akamshika Lauson pale kitandani alipokuwa amekaa na akamnyenyua juu kwa hasira zaidi,Lauson uvumilivu ulimshinda aliona sasa huo ndio mda wake yeye kujitetea na kutumia nguvu zake.

""""""Mzee James alishangaa gemu inambadilikia aliona mikono yake ikitolewa shingoni mwa Lauson, Lauson alimshika koo yake akamkabaa kwa nguvu sanaa na ukizingatia Lauson alikuwa na nguvu za kutosha kutokana na mazoezi ya mara kwa aliyokuwa akiyafanya, Lauson hasira zilikuwa zisha mpanda zaidii alizidii kumyonga Mzee James huku Mzee James akianza kupumua kwa shida.

""""Ndugu msomaji unadhani kitaendelea kitu gani.
Usikose sehemu ya ishirini na mbili,, pia usisite kulike ,kukomenti na kushare.

ITAENDELEA... 

CHOMBEZO: "HOUSE BOY"
SEHEMU YA: 22
MTUNZI: "ENOCH LIBERATUS"

WHATSAPP NO: 0622412420.

TULIPOISHIA.
Katika sehemu ya ishirini na moja tuliishia pale Lauson alipokuwa akiendelea kumkaba Mzee James huku Mzee James akianza kupumua kwa shida.

ENDELEA......
"""'Mzee James alikuwa akipumua kwa shida zaidi na Lauson hakuwa tayari kumuachia alizidi kumnyonga,Amina na Mama yake wakiwa Chumbani kwa Martha walisikia sauti ya mtu akipumua kwa shida sana,Mama Amina akamuulza Mwanangu nawe siunasikia sauti ya mtu akipumua kwa shida? Amina akajibu akisema "ndiyo Mama" au atakuwa ni Baba wazo la Baba yake lilimjia Amina hapo ni baada ya kukumbuka kuwa Baba yake alitoka chumbani humo kwa hasira sana huku akitembea kwa haraka na usoni akionekana wazi mtu mwenye hasira.

"""'Amina alimwambia Mama yake itakuwa ni sauti ya Baba hiyo ngoja twende tukaone,walikimbia mbio mbio hadi chumbani kwa Lauson kufika chumbani kwa Lauson hawakuamini walichokiona mbele yao ""walimkuta Mzee James akiwa amekabwa vibaya sanaa a huku akishindwa hata kupumua vizuri zaidi tu akitoa macho kama panya aliyebanwa na mlango.

""""""Mama Amina na Amina walifika wanamkimbilia Mzee James na kuitoa haraka mikono ya Lauson iliyokuwa katika shingo la Mzee James ,duuuh baada ya Mzee James kutoka tu katika mikono ya Lauson alianzaa kukohoa ko!!! ko!!! ko!!! kama vile kuna kitu kimemkwama kwenye kooo!!, Amina alimshika Lauson akimuomba amuache Baba yake asimrudie tena kumnyonga kwani mda huo Lauson alikuwa bado na hasira sana .

"""""""Lauson aliona Mzee James amevuka mipaka ndipo akaona amfundishe adabu kidogo na wangechelewa kuja kumuokoa Mzee James huenda Lauson angemnyonga zaidi hadi kufariki kwasababu alikuwa na hasira sana na alikuwa ameshashindwa kuzizuia na kuzidhibiti hasira zake.

"""Kwa jinsi Lauson alivyomnyoga Mzee James ukizingatia alikuwa na hasira sana ,Mama Amina na Amina kama wasingeshituka kuja chumbani kwa Lauson siku hiyo Mzee James angegeuka maiti mda huo huo,kweli Mzee James hakuamini kitu alichofanyiwa na Lauson,Mzee James alikabwa manusula shingo na koo yake itolewe.

""""Mama Amina alikimbia sebuleni kuchukua Maji kwa ajili ya mme wake ili aweze kupunguza kukohoa kutokana na kukabwa kooni mda mrefu, kwakuwa alikuwa akikohoa sana katika mda huo,baada ya Mzee James kumaliza kunywa maji angalau alipataa nafuu, kukohoa kulipungua Mzee Lauson alikuwa na Maneno yafuatayo kwa Lauson.

  
"""""Mzee James alimwambia Lauson kwa sauti ya upole akimwambia"" Lauson kwa mara ya kwanza ulipokuja hapa ulikuwa bado kijana mdogo sana ila saivi umeshakuwa binafsi siwezi kukufukuza ila naomba utoke hapa nyumbani kwangu""alipaza sauti akimwambia'"" Naomba Kufikia kesho jioni nikitoka kazini nisikukute hapa nenda unakokujua na kaishi maisha yako mwenyewe ila naomba iwe mwiko wewe kuja hapa nyumbani kwangu.

''''''"Mzee James alimaliza maongezi yake kiivyo, kisha akaondoka Mama Amina alijaribu kumbembeleza Mme wake ili aweze kumsamehe Lauson na kumpunguzia adhabu aliyompatia ya kuweza kumufukuza kabisa nyumbani hapo ,wakati ukizingatia Lauson hakuwa na kazi yoyote ya kufanya zaidi tu ya kutegemea kila kitu kutoka kwa wanawake waliokuwa wakimuhonga baada ya yeye kufanya nao mapenzi.

"""""Amina pia alijaribu kumbembeleza Baba yake Ila Mzee James alikuwa ameshatoa maamuzi yake ya kumfukuza kabisa Lauson nyumbani hapo,Mama Amina alimfata Mme wake chumbani akijaribu kumuombea sana msamaha Lauson ili apate kumhurumia Lauson ila Mzee James alikataa katu katu na hakuwa tayari.

""""Amina alizidi kulia huku akimuomba Baba yake aweze kumuacha Lauson ili aendelee kuishi nyumbani hapo kwani alikuwa akimpenda sana Lauson,na siku hiyo Mzee James alishangaa sana kuona Mke wake na Mtoto wake jinsi walivyokuwa wakimlilia sana Lauson ili azidi kubaki nyumbani hapo.

"""'Mzee James alishangaa sana kuona kitendo hicho kilichomshangaza sana ndipo akakumbuka yale Maneno aliyoambiwa na rafiki yake Mzee kimola na alipojumlisha matukio yote aliona dhahiri Lauson atakuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Mke wake na Mtoto wake Amina,pia alipokumbuka kuhusu ile chupi aliyoiona ikiwa imeloa ute!! ute!! alihisi moja kwa moja Lauson atakuwa sio mtu mzuri katika familia yake hiyo.

  
""""" Mzee James alipomgeukia Mke wake alishangaa sanaa kumuona akilia sana kiasi kwamba akijigalagaza sakafuni , kama mtu aliyefiwa na mtu mpendwa sana katika maisha yake ,Mzee James alizidi kupagawa zaidi aliingiza mkono wake kabatini akatoka na bastola kisha akaenda moja kwa moja hadi chumbani alipokuwa Lauson.

"""""Alipofika chumbani kwa Lauson hakutaka maelezo alifika anamnyoshea bastola usoni akimwambia""Lauson paki kila kilicho chako uondoke hapa "tena fanya haraka kabla sijabadili maamuzi yangu! ,ukizubaa hapa nakutwanga risasi ya kichwa, Lauson alipomuangalia Mzee James hakuonyesha sura ya huruma wala utani wowote tena alikuwa siliasi,aliona akizubaa kweli Mzee James angeweza kumtwanga risasi ya kichwa akaona akusanye kila kilicho chake tayari kwa kuondoka.

"""""Lauson alipaki kila kilicho chake haraka chini ya usimamizi wa Mzee James huku akiwa amemshikiwa bastola ,Mama Amina alipojaribu kuingilia maamuzi ya Mme wake,Mzee James hakuonyesha utani wowote juu ya hilo alimshikia bastola Mama Amina akimwambia"""Mama Amina rudi ndani kabla sijakushuti bastola hapa'""tena fanya haraka.

"""""'Hakuna aliyejitokeza kumsaidia Lauson katika mda huo,Lauson alipomaliza kupaki kila kitu,Mzee James alimsindikiza hadi nje ya geti,na alipofika getini alimuamulu Fabiano aweze kufungua geti haraka ili Lauson apite na baada ya Lauson kutoka nje ya geti Mlinzi Fabiano alifunga geti ,Lauson alionekana mtu mwenye mawazo sana katika wakati huo Lauson alikaa nje ya geti baada ya kufukuzwa huku akitafakari sehemu ya kwenda kujiegesha katika usiku huo.

"""""Lauson akilini mwake alikuwa na msongo wa mawazo zaidi alikuwa akitafakari tukio hilo lililomkuta la kufukuzwa kama mbwa nyumbani hapo kwa Mzee James ambapo Lauson alimchukulia kama Baba yake Mzazi ila kutokana na kitendo hicho kilichomkuta Lauson hakika alikosa mwelekeo tena ukizingatia hakuwa na ndugu yeyote aliyekuwa akimfahamu katika jiji hilo kubwa ukizingatia katika wakati huo ilikuwa imeshaingia giza tayari mda huo ilikuwa mida ya saa tatu za usiku.

  Usikose sehemu ya 23.
 
 ITAENDELEA..... 

CHOMBEZO: "HOUSE BOY"
SEHEMU YA: 23
 MTUNZI: "ENOCH LIBERATUS"

WHATSAPP NO: 0622412420.

TULIPOISHIA.
Katika sehemu ya ishirini na mbili tuliishia pale baada ya Lauson kufukuzwa na Mzee James nyumbani kwake huku akiwa amemushikia bastola.

  ENDELEA......
Baada ya Lauson kufukuzwa nyumbani kwa Mzee James alishindwa aende wapi kwani hapo jijini Dar hakuwa na ndugu yoyote aliyekuwa akimufahamu,alifikiria sana sehemu pa kwenda katika usiku huo alipakosa na ukizingatia mda ulikuwa umeenda katika mda huo ilikuwa tayari imeshafika mida ya saa tatu na robo za usiku Lauson alikuwa bado yupo nje ya geti akitafakari sana sehemu pakwenda kulala.

""Tukirudi kwa upande wa Mzee James baada ya kuhakikisha Lauson ametoka nje ya geti la nyumba yake,alirudi ndani huku mkononi akiwa bado ameshika bastola alipitiliza hadi chumbani alipokuwa mke wake,kabla ya Mzee James kuingia chumbani kwake alipokuwa Mke wake alipokuwa mlangoni tu alipokelewa na sauti ya mke wake iliyokuwa ikiashiria majonzi na kulia.

  """Mama Amina alikuwa akilia kwa sauti kubwa kama Mtoto mdogo anavyolia hakika Mama Amina alikuwa akimpenda sana kiasi cha kuweza kulia kwa ajili yake, baada ya Mama Amina kusikia mlango wa chumba chake ukifungulia ,Mama Amina alijifuta machozi yote haraka na zile kwi! kwi! zote zilizokuwa zikisikika zilikata zote,Mama Amina alinyamanza kimya kama mtu ambaye hakuwa analia.

"""""Mzee James baada ya kuingia ndani alimsogelea Mke wake akamwambia ""kama unampenda sanaa huyu House boy "malaya wako" uliyemuokota Morogoro mfate huko huko!! na ujue ukisha ondoka hapa nisikuona tena ukienda uende moja kwa moja" usirudi tena hapa nyumbani kwangu ,Mama Amina alimugeukia Mme wako ili kumuangalia kama anachokiongea amemaanisha kweli na alipogeuza shingo yake kumtazama usoni,Mzee James uso haukuonyesha sura ya utani kabisa juu ya kitu alichokizungumza baada ya Mama kuona hivyo alitulia mwenyewe hivyo alikuwa mpole na akatulia kabisa.

""""Mama Amina alirudi jikoni kuendelea na mapishi kwani alijuwa endapo hatafanya hivyo lazima angeipoteza ndoa yake na lazima angechezea talaka siku hiyo kwasababu Mzee James sikuhiyo alikuwa na hasira sana na hakuonyesha utani wowote juu ya maamuzi aliyokuwa akiyatoa na kutokana na hasira alizokuwa nazo katika siku hiyo Mzee James mtu yeyote angejichanganya kumuudhi au kumvuruga akili yake lazima angechukuliwa hatua kali hata kupigwa risasi angeweza kupigwa.

""""""Tukirudi kwa upande wa Lauson mda huo alikuwa akitembea kuelekea pasipo julikana,kwani na yeye kichwani mwake alishindwa aende wapi,alizidi kutembea huku akionekana kuwa na mawazo sana njia nzima"" ,aliona kama dunia yote imemulemea na inataka kumuangukia.

""""Alipojikagua vizuri mfukoni alitoa noti ya shilingi elfu kumi,tumaini la kulala ndani ya gesti alilipata hapo hapo baada ya kubaini mfukoni mwake kuna pesa ,hapo hapo alipokumbuka gesti maarufu hapo jijini Dar inayoitwa "kibalo Guest House" ambayo gharama zake ni nafuu sana kwakuwa ilikuwa na vyumba vya watu V.I.P na vyumba vya watu wakawaida,Lauson aliona aende katika gesti hiyo kwakuwa bei za gesti hiyo zilikuwa za kawaida tu.

'""""""Lauson aliona atembee kwa mguu haraka na kutokana na pesa aliyokuwa nayo alishindwa kuchukuwa Teksi kwasababu angeitumia tu huenda isingetosha kutokana na matumizi yake atakapo fika katika gesti ya Kibalo ,aliona abene matumizi ya hiyo pesa ili isije ikamuishia kabla hajapata ata chumba cha kulala katika usiku hui ,alipokuwa njiani akiendelea kutembea aliona teksi nyeupe ikisimama pembeni yake, alishanga kuona dereva teksi akimuita tena kwa kulitaja jina lake"Lauson" ,Lauson alishituka ila aliona asogee Karibu na hiyo ili kumjua mtu huyo aliyekuwa akimuita, alisogea karibu yake kumuangalia vizuri hakuamini macho yake alikuwa ni rafiki yake kipenzi "Muheza" dereva teksi.

""""''Lauson hakuamini kama wakati huo Muheza angeweza kujitokeza ,Lauson aliingiza mizigo yake ukizingati Lauson hakuwa na mizigo mingi alikuwa na begi moja tu kubwa ndilo alillokuwa amepakia nguo zake na vitu vyake, baada ya kuingia ndani ya gari alianza kumsimulia rafiki yake huyo alimwambia kila kitu kwanzia siku ile walipoachana baada ya kupata ajari hadi mda huo ambao wako nae,Muheza akimwambia Lauson kuwa yule dereva Fuso waliyepamiana siku ile ndiye amemsaidia kuitengeneza teksi yake na kuifanya iwe nzuri na mpya zaidi hadi Lauson mwenyewe alishangaa sana kuona teksi ya rafiki yake ilivyokuwa tofauti na awali,pia Muheza alimuhurumia sanaa rafiki yake baada ya kusimuliwa kila kitu alichofanyiwa na Mzee James, kwakuweza kumfukuza kama mbwa nyumbani kwake .

"""""Lauson alimuomba Muheza ampelekee katika gesti ya kibalo, Muheza alimuuliza" Lauson kwa nini nisikupeleke nyumbani kwangu ukalale pale badala ya kwenda kulala gesti" Lauson alimwambia naomba tu kwa leo nilale gesti kwako nitakuja hata kesho ila nashukuru sana kwa msaada wako hakika wewe ndiye rafiki yangu wa pekee katika jiji hili umenisaidia kwa vingi sana Mungu azidi kukuzidishia.

"""""waliendelea na safari huku wakipiga stori na kukumbushana mambo yaliyowakuta walifurahi zaidi baada ya Muheza kumuuliza Lauson kuhusu mpenzi wake Amina,Lauson alimwambia Muheza""bro kwa saivi nimeacha kilio pale nyumbani kwa Mzee James ,Lauson akajitamba akisema siunajuwa wote pale walikuwa wanaelewa mambo yangu wote walicheka kwa pamoja.

"""""Muheza alifinya breki baada ya kufika nje ya gesti ya "Kibalo",Lauson alishuka haraka akakimbia kwenda reception kuuliza kama kuna vyumba baada ya kufika pale alimkuta Mariamu ambaye kila siku aliyokuwa akija hapo gesti lazima walikuwa wakionana ,Lauson alimsalimia mrembo Mambo "Mariamu aliitikia salamu hiyo kwa kuguna""""mhhhh!! mimi Mrembo tena haya bana mimi niko poa!,akasema Karibu Handsome

"""'Lauson alimuuliza "Mrembo vipi vyumba vya kulala wageni vya kawaida vipo? Mariamu alimjibu ndio vipo vipi leo umekuja na shemu wetu nini? Mariamu alimuuliza,""Lauson alimjibu acha zako bana leo sina mtu niko nwenyewe,"" Mariamu aliguna tu mhhhhh!! moyoni akijisemea""" Yani huyu kijana mimi nampendaga sana tu yani kama leo yupo yeye mwenyewe lazima nihakikishe na lala nae usiku wa Leo.

""""Lauson alirudi nje alipokuwa Muheza pale nje ya gesti ak amtaarifu akimwambia """ Ndugu yangu vyumba vipo ngoja leo nilale hapa kuhusu ratiba ya kesho tutaongea ila nashukuru sanaa kwa msaada wako"",Lauson alimuaga Muheza akawa amechukua begi lake na akazama ndani hadi kweny chumba cha mapokezi,alimkuta Mariamu pale akamwambia amupe funguo ya chumba atakacho tumia usiku huo.

"""""Lauson alipewa funguo za chumba namba 6, akazijichukua mkononi mwa Mariamu ila wakati Mariamu akimkabidhi Lauson funguo alimukonyeza,Lauson alibaki kushangaa tu akawa haelewi lengo la Mariamu kumkonyeza,Lauson alipokuwa akiondoka kuelekea katika chumba namba 6 alisikia nyuma mhudumu Mariamu akimuita" we Handsome usifunge mlango baadae nakuja kukutembelea chumbani kwako.

""""" Lauson hakushituka sana alijuwa ni utani wa Mariamu kwani Mariamu alikuwa mtu wa matani sanaa, Lauson aliingia chumbani kwake katika gesti hiyo, kwakuwa alikuwa akisikia joto sana aliona aoge kwanza ndio ale chakula,alipomaliza kula alibadilisha nguo kisha akashika simu na kupiga moja mapokezi.

""'"''"""Simu ilipokelewa kwa upande wa pili halo!! Lauson alijitambulusha akataja shida yake kuwa anahitaji chakula kiletwe chumbani kwake,Lauson aliletewa msosi na mfanyakazi wa gesti hiyo tofauti na Mariamu ,Lauson baada ya kuletewa msosi alikula chakula hicho ambacho kilikuwa wali na nyama kisha akajipumuzisha
kwakuwa alikuwa amechoka sana katika siku hiyo.

""""'"Lauson akiwa katika usingizi mzito alisikia mlio wa simu yake ukiita alipojikulupua na kuangalia mpigaji ilikuja namba ngeni,akapokea hallo!! nani mwenzangu? sauti kwa upande wa pili ilisikika ""Handsome wangu nakuja saivi jiandae!!! sauti haikuwa ya mtu mwingine bali ilikuwa ya Mariamu .

"'""Lauson alishindwa kumuelewa Mariamu!!! haikupita mda Lauson alisikia mlango ukigongwa alipoangalia mda ilikuwa saa tano na nusu usiku,Lauson alienda kufungua mlango,kufungua mlango tu Mariamu alizama ndani na akafunga mlango""

  Usikose sehemu ya 24 ya chombezo hii.

  ITAENDELEA.... 

Post a Comment

Previous Post Next Post