🔐 MAUMIVU YA NDOA (21-----25) 😭😭😭😭



SEHEMU YA 21


“Mama inamaana kumbe wewe ndie uliyemuua Rayuu?”

Hakeem alistuka na kumuuliza Mama yake ambae alimuwahi na kumziba Mdomo ili Mtu yoyote asisikie katika jumba la kifahari la Mzee Mustapha.

Sauti ya glass kuvunjika ilisikika na kumstua Mama hakeem na Mwanae waliokuwa wanaongea chumbani kwa Hakeem.

Madame Asia ambae ndie alikuwa Mama Mzazi wa Hakeem alitoka chumbani kwa Mwanae na kujaribu kuangaza kama kuna Mtu yoyote atakuwa eneo hilo lakini wapi hapakuwa na dalili ya Mtu yoyote yule aliyekuwa hapo na kulionekana kupo kimya kama hakuna kilichotokea.

Alipotazama chini aliona vipande vya glass iliyokuwa imebeba juice ikiwa imevunjika. Hakeem pia alitoka nje alistuka kuona vipande vya glass na mama yake alionekana kukagua kitu na kuonekana akitabasam 

“Vipande vya glass iliyovunjika vimemjeruhi katika mguu wake” Madame aliongea huku akiwa anatazama tone la damu ambalo lilikuwa chini na kumfanya agundue kitu kisha aliinuka na kuelekea jikoni kwenda kumuona Mpishi Mkuu ili aweze kugundua ni nani aliyekuja kwenye mlango wa mwanae 

“Heshima hiwe juu yako Madame” Othman ambae ndio alikuwa ni Mpishi Mkuu wa jumba la kifahari la Mzee Mustapha aliinama na kumpa heshima yake ila alipoinuka alipokelewa na kibao kimoja takatifu.

“Mshenzi Mkubwa wewe, unawezaje kuruhusu Kijakazi kuja kumuhudumia Kijana wangu usiku mkubwa kama huu?” Madame aliongea kwa hasira na kumstua mpaka Othman mwenyewe ambae alionekana kushangazwa na taharifa hiyo.
“Madame mbona vijakazi wote wapo katika vyumba vyao vya kulala? Na kama Sheria inavyosema, hakuna Kijakazi yoyote anaeruhusiwa kuzurula katika jumba hili mida kama hii” Othman aliongea na Madame alipiga hatua kumsogelea

“Nahitaji kumjua Kijakazi ambae muda mfupi uliopita alikuwa mlangoni kwa Kijana wangu, alistuka baada ya kugundua naongea na kijana wangu na akavunja galss. Tafadhali tafuta kijakazi aliyeumia mguuni nina maswali nahitaji kumuuliza binafsi na akikisha Mzee hatambui jambo hili”

Madame aliongea kwa msisitizo huku akiwa anatetemeka kwa hasira, hakutaka Mtu yoyote atambue siri yake, hivyo kwa kitendo cha Kijakazi kuvunja glass mlangoni kwa Hakeem alitambua fika kuwa siri yake inaweza kuwa shakani

Wakati anatoka jikoni kuelekea chumbani kwa Hakeem alistuka baada ya kusikia sauti ya piano inasikika kutoka chumbani kwa Rayuu. Alisogea na kukuta taa inawaka.

“Bila shaka ni Rayuu mpya ndie anaecheza piano hii” Madame aliongea na kuonekana kuchukizwa kidogo

Ilikuwa ni sauti murua iliyomkumbusha mbali zaidi, alipokuwa anamtazama Shaymaa alikuwa kama anamuona Rayuu wake akicheza piano “Akika faraja yangu imerejea upya” Mzee Mustapha aliongea huku akiwa anafurahi, kicheko ambacho kiligubikwa na majonzi na kujikuta akianza kulia kama Mtoto Mdogo. “Rayuu wangu umerudii” aliongea mwenyewe huku akiwa analia kwa furaha
                        *******
Hakeem akiwa chumbani kwake alijikuta akijiuliza maswali mengi ambayo alikosa majibu yake “Kwanini Mama alimuua Rayuu? Kwanini anasema alimuua Rayuu ili Mimi nirithi mali inamaana Mimi sina urithi hapa?”

Kauli ya Mama yake ilimuumiza kichwa na alijikuta anakosa majibu sahihi kwa wakati huo. Wakati anatafakari hayo alijikuta akipata hofu na mstuko wa hali ya juu.

“Liyunaa” Alitaja jina la Mwanamke na kuonekana akistuka “kwanini umekuja chumbani bila taharifa”

Hakeem aliongea mwenyewe huku akifungua kabati ili akiwa anatafuta nguo na haikujulikana wapi alikuwa anataka kwenda

Alitinga koti lake kubwa na kofia iliyoweza kumficha uso wake na kutelemka chini kupitia ngazi. Alistuka baada ya kuona michilizi ya damu na aliinama na kuishika damu kwa umakini “Liyuna najua ni wewe na sidhani kama unaweza kutoka salama kwenye jumba hili” 

Hakeem aliongea na kuzidisha kasi ya kushuka ngazi kuelekea chini akionekana kama kuna Mtu alikuwa anajaribu kumuwahi

Wakati Hakeem anaenda huko, tayari Mr Othman akiongozana na Walinzi kadhaa wa Jumba la kifahari la Mzee Mustapha walikuwa wanaenda kufanya ukaguzi ili kumtambua msichana ambae aliumia na kuacha damu yake.

Hakeem aliingia pasipo hata kubisha hodi na kusababisha taharuki katika vyumba vya wasichana ambao hawakutarajia kupata ugeni ule.

Kila chumba kulikuwa kunalala Wasichana wawili wawili hivyo alifika na kuwaomba samahani “usalama wenu ni kuwakata vidole vyenu, inaweza msijue kwanini nafanya hivi ila mtakuja kunishukuru baadae. Yoyote kati yenu atakayethubutu kuema kuwa ni Mimi ndie niliyehusika na mchezo huu basi asifikiri atakuwa muaminifu mbele ya Mama yangu kwani huo ndio utakuwa ni Mwisho wake kuwepo katika Jumba hili”

Hakeem aliongea na kilihofuatia hapo ni kuwakata Vijakazi wale ambao kila Mmoja aliugulia kwa jinsi alivyoona inafaa kupoza maumivu kwa upande wake.

Kila chumba ambacho Othman aliingia akiwa na Walinzi kwenda kukagua alikuta wasichana wakiugulia maumivu tu wote wakiwa na majeraha mguuni na kila Mmoja akitoa maelezo ambayo alishindwa kuyaelewa kwa haraka “Nini kimetokea kwa wasichana hawa?” 

Othman aliwauliza Walinzi ambao walikosa kupata majibu na Badala yake walihisi kuna Mchezo unachezwa ambao unaweza hata kumuingiza Mkuu huyo wa idara ya mapishi matatizoni

DAKIKA KADHAA KABLA

Ilikuwa ni siku ambayo Liyuna alikuwa amepanga kumueleza jambo muhimu Hakeem. Alijua kuwa isingekuwa rahisi kwake kupandisha ngazi kuelekea katika chumba cha Hakeem pasipo kuulizwa chochote.

Alichoweza kufanya ni kumimina kinywaji na kuweka katika glass na kujifnaya kama lilikuwa ni agizo kutoka kwa Mtoto wa Boss. 

Alifika katika mlango wa Hakeem na kukuta umeegeshwa. Alishusha pumzi na kuufungua taratibu na hapo alistuka baada ya kumsikia Madame akiongea 

“Nilimuua Rayuu ili uje urithi hizi mali kama Mtoto wa kufikia, lakini naona ni jinsi gani haujitambui na utaiacha hii fursa ikupite. Kama utaendelea kugoma kumuoa basi kaa ukijua hatokuwa na Maisha hapa ndani na utanipa dhambi ya kuuwa Mwanamke mwengine ambae sikupanga kumuondoa Duniani”

Liyuna alistuka na kujikuta akishindwa kupumua na kuanza kutetemeka na alijikuta akikosa hata nguvu ya kuinua mguu ili aondoke 

“Mama inamaana kumbe wewe ndie uliyemuua Rayuu?”

Hakeem aliongea na kuzidi kumstua Liyuna na kujikuta akitetemeka na kuangusha glass iliyokuwa na kinywaji na vipande vilimkata mguuni na hapo alijikuta akipata nguvu na kuondoka eneo lile haraka sana

“Wewe mbona umenistua?” Sabrah ambae alikuwa ni msichana anayelala nae chumba kimoja alistuka baada ya kumuona Liyuna akiwa ameingia chumbani vile “Mguu wako unatokwa na damu” Sabrah alimwambia Liyuna ambae ndio kwanza alijigundua kama alikuwa ameumia mguuni.

Alichoweza kufanya ni kufunga kidole kilichokuwa kinatoka damu ili kuzibiti damu isiendelee kutoka huku akiwa anatetemeka kwa kile ambacho alichoweza kukisikia.

Ghafla Hakeem aliingia bila kubisha hodi na kumtazama Sabraha na kumtaka atoke chumbani. Sabrah alifanya hivyo na Hakeem alimfuata na kumkumbatia kisha akamuuliza “Kwanini ulikuja chumbani kwangu bila taharifa?” “Sikuwa na namna Hakeem, niliitaji kuja kukueleza kuwa mimi ni mjamzito”

Liyuna alimjibu kitu kilichomfanya Hakeem astuke na kumkumbatia zaidi “Liyuna, Mama akigundua kuwa ni wewe ndie uliyegundua siri yake basi hautakuwa na maisha katika jumba hili hata nje ya jumba hili napaswa kufanya kitu kwa ajili yako”

Baada ya hapo Hakeem aliamua kuwakata vijakazi wote ili kupoteza ushahidi wa mpenzi wake hasigundulike kuwa ndie aliyekuja chumbani kwa Hakeem na kutunza siri hiyo “Tafadhali Liyuna, najua umesikia kitu mimi sihitaji kujua. Naomba funga mdomo wako” Hakeem aliongea na Liyuna aliitikia kwa kichwa kuashiria kuwa amemuelewa 

                             *******

Shaymaa alistuka na kuacha kucheza piano na kujikuta akijongea alipo Mzee Mustapha na kujaribu kumuita “Baba” Ilikuwa ni sauti adhimu iliyokwenda kuusisimua moyo wa Mzee Mustapha na hakutegemea kama siku moja angekuja kuitwa Baba

“Umeniita Baba!!” Aliinua mikono yake akionekana kushangazwa huku akimuuliza Shaymaa aliyekuwa kiasi fulani anamuogopa akidhani kwa kufanya hivyo atakuwa amekosea sana

“Sa. Ma.. hani” Alipatwa na kigugumizi na kujikuta akimjibu kwa hofu “Hapana Rayuu hupaswi kuopa Mimi ni Baba yako” Mzee Mustapha aliongea na kumkumbatia kwa nguvu Shaymaa huku akiwa analia.

Madame aliingia na kustuka baada ya kumkuta Mumewe amemkmbatia Shaymaa “Baba Hakeem!! Ni nini icho unafanya na huyo Binti” Madame aliuliza kwa hasira na Shaymaa alijitoa mikononi mwa Mzee Mustapha huku akiwa anaogopa

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 22
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Shaymaa alistuka na kujitoa katika mwili wa Mzee Mustapha huku akiwa mwenye hofu

"Huna nini lakini wewe?" Mzee Mustapha alimshangaa Mkewe na kumuuliza 

Madame alimtazama Shaymaa kwa jicho kali na kusikitika 

"Sikuwahi kufikiri kama Mume wangu unaweza kufanya huu ujinga ambao unaufanya na huyu Binti" 

Madame aliongea kwa uchungu huku akijifanya kuumizwa na kile alichokiona chumbani.

"Kwanini unanikosea? Tafadhali usimuumize zaidi Binti yangu, unajua fika hali yake. Hivi unadhani naweza kufanya icho unacho maanisha?"

Mzee Mustapha aliinuka na kuongea kwa hasira huku akiwa anatetemeka.

Madame hakutaka kumpa nafasi ya kujitetea Mumewe badala yake alitoka kwa hasira na kubamiza mlango.

Shaymaa alijikuta akikaa chini huku akiwa analia "Rayuu...." Mzee Mustapha alijaribu kumuita huku akiwa anamsogelea 

"Tafadhali naomba usinisogelee" Shaymaa aliongea huku akiwa na hofu 

"Najua jinsi gani unavyojisikia ila tafadhali naomba unisamehe na ufichukue maamuzi mabaya. Nitalimaliza hili"

Aliongea kwa upole sana huku akiwa anamtaza Shaymaa ambae alikuwa akilia kilio fulani cha kutotoa sauti.
                   *****
Ilikuwa ngumu kwa Maganga kuepuka vishawishi vya Irina na bila kutarajia alijikuta ameshavunja amri ya sita na Mke wa Boss wake.

"Sikuwahi kufikiri kama wewe ni Mwanaume wa Shoka" Irina alimwambia Maganga huku akiwa anatabasam baada ya kulidhishwa na utendaji kazi wake.

Ilikuwa furaha kwa Irina ila ilikuwa ni udhuni kwa Maganga ambae alijutia kwa kitendo cha kutembea na Mke wa Boss wake 

"Kwanini lakini umeamua kufanya hivi?" Maganga alimuuliza Irina huku akiwa makini kumtazama

Irina alicheka na kujiweka sawa "Nafikiri hii ndio itakuwa njia sahihi ya kukunyamazisha" 

"Lakini kwanini unafanya vile na Mwanamke mwenzako?" Maganga alimuuliza na Irina alichukizwa Kidogo "Kwanini umefanya hivi na Mke wa Boss wako?" 

Irina alimuuliza na Maganga alikosa cha kumjibu na badala yake alivaa nguo zake na kuondoka zake.

Irina alimtazama na kutabasam mwenyewe akiashiria ushindi.
               *****

Madame aliingia chumbani kwake na kusogea katika dressing table yake na kujitazama.

Alifuta machozi na kuachia tabasam la kinafka "Samahani sana Binti umeingia kwenye mtego ambao hukupaswa kunasa wewe" Madame aliongea mwenyewe kwa sauti fulani ya ushindi.

Sauti ya mlango ilisikika ukifunguliwa. Madame alitumia kioo cha dressing table yake kugundua kuwa aliyekuja hakuwa mwengine bali ni Mumewe.

"Umefuata nini chumbani kwangu?" Madame aliuliza bila hata kugeuka kutazama 

"Asia unakosea sana, yule Mke wangu, hivi umesahau kifo ambacho Binti yetu alikufa?" Mzee Mustapha alimuuliza Madame na kumfanya ageuke na kumtazama.

"Hivi unafikiri Rayuu anafurahia ujinga unaofanya chumbani kwake kweli?" Madame alijiliza kinafki na kumfanya Mzee Mustapha azidi kujisikia vibaya.

Walionea kwa kirefu sana Mzee Mustapha akimwambia Mkewe kuwa hawezi kufanya kama anavyofikiria bali amefanya yote kumsaidia Shaymaa angalau aondoke na jinamizi la kutaka kujiuwa.

"Kama unahisi Mimi kuna jambo lolote baya nimefanya kwa yule Binti basi wewe fanya maamuzi ambayo yatakuwa sahihi kwako" 

Mzee Mustapha aliongea na kutaka kutoka nje lakini Mkewe alimshika na kumzuia.

"Samahani sana Mume wangu" Madame aliona game linakwenda kuharibika hivyo aliona ni bora ajishushe kwa kuomba msamaha 

"Hebu jaribu kuvaa viatu vya yule Binti!! Hata ukiniomba Mimi msamaha ni bure tu" 

Mzee Mustapha aliongea na Madame alizidi kumuomba msamaha na kumuomba Mumewe ampe nafasi kwa Mara nyingine azungumze na Shaymaa.

Mzee Mustapha alimtazama na kumpa onyo "Shaymaa kwangu ni kama Binti yangu Rayuu hivyo naomba kisitokee kitu chochote kitakachoweza kuvunja moyo wake. Nitafanya maamuzi magumu"

Mzee Mustapha aliongea na kuondoka zake akimuacha Mkewe akiwa anajifanya kujutia alichokifanya na Mumewe alivyoondoka alibaki akitabasam akisherekea ushindi.
              ******
"Hivi Shaymaa una mkosi gani wewe?" 

Shaymaa alikaa chini na kuongea Mwenyewe kama ilivyo kawaida yake 

"Napaswa kusimama imara katika hili, siwezi kulia tena, siwezi kurudi nyuma tena. Naamini mtetezi wangu ni Mzee Mustapha. Samahani sana Mama kwa kunielewa vibaya"

Shaymaa aliongea na muda huo mlango wake ulikuwa ukigongwa

'Karibu" Shaymaa aliongea na mlango ulifunguliwa hakuwa mwengine aliyeingia zaidi ya Madame.

"Samahani sana Madame akika sitakaa tena karibu na Mzee"

Shaymaa alipiga goti na kumuomba Madame aliyekuwa akitabasam muda wote.

"Samahani sana Shaymaa, ulishindwa kunielewa ila wala sikumaanisha kile kilichotokea hapa"

Madame alimjibu na kumshangaza Shaymaa kutokana na kauli yake.

Swali kubwa ambalo alijiuliza ni vipi Madame anasema hajamaanisha wakati alikuwa analia mbele yake?

Hakutaka kujaji sana badala yake alibaki kumsikiliza tu.

"Shaymaa wewe ni Binti mwenye bahati sana" Madame aliongea na kumshangaza Shaymaa 

"Kivipi mama? Kama kweli ningekuwa na bahati sidhani kama nifika hapa" "Unajua bahati huweiz kuiona mpaka pale itakapokukuta"

Madame aliongea na kusogea alipo Shaymaa

"Mimi na Baba yako tumekaa na kuamua tuwaozeshe wewe na Hakeem muwe Mke na Mume"

Madame aliongea na kumstua Shaymaa

"Mimi niolewe na Mtoto wenu?"

"Upaswi kustuka kiasi icho Shaymaa ila unapaswa kufurahi na kushukuru kwa mana hakuna Mwanamke ambae angependa kuipoteza nafasi hii adimu ya kuolewa na Mtoto wa Tajiri" 

NINI KITAENDELEA? USIKOSE EPISODE YA 23  
MAUMIVU YA NDOA 
SEHEMU YA 23
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Hakuna Mwanamke hasiyependa kuolewa katika hii Dunia ila sidhani kama kuna Mwanamke ambae atakuwa tayari kudhalilika kwa sababu ya ndoa.

Shaymaa alikaa kimya na kutafakari pasipo kumjibu Madame 

"Ujavutiwa na Kijana wangu?" Madame aliongea taratibu huku akitabasam

"Nawezaje kumkataa kijana mtanashati kama Hakeem?" Shaymaa alimjibu Madame huku akimtazama na kuonesha dhairi hakufuraishwa na jambo hilo na Madame hakuweza kulitambua badala yake alimfuata na kumkumbatia.

"Shaymaa!! Nakuahidi kuwa utakuwa mwenye furaha sana pindi utakapoolewa na Hakeem. Nimekufanya wewe kuwa chaguo la Mwanangu tafadhali usiniangushe"

Madame alimwambia Shaymaa ambae alitulia huku akiitikia kwa kichwa kuashiria kuwa ameridhia ombi la Madame.

'Nikutakie usiku Mwema Mkwe wangu " Madame aliongea na Shaymaa alionesha tabasam fulani la kujilazimisha na Madame alipotoka nje alijikuta akishikwa na kichefuchefu na kukimbilia bafuni kwenda kutapika.

Madame alipotoka nje alipatwa na Mstuko baada ya kumkuta Othman akiwa mlangoni anamsubiri.

"Othaman?" Alistuka na kumuita jina kwa ukali "Heshima hiwe juu yako Madame"

Othman aliongea na kuinama kumpa Heshima yake "unawezaje kuja kusubiri kwenye chumba cha Mkwe wangu?" 

Madame aliongea kiasi ambacho hata Othaman alishangaa "umeshamtambua Kijakazi aliyekuja kunyemelea chumba cha Kijana wangu?"

"Vijakazi wote wameumia Mguuni na imekuwa ngumu kuweza kumtambua ni yupi Muhusika" 

Othman aliongea na Madame alishangazwa "Inamaana kuna Mtu amecheza mchezo?" "Bila shaka Madame"

Othaman alimjibu na kumfanya Madame atafakari Kidogo kabla ya kumuuliza "Ni nani amethubutu kufanya hivyo?" Madame aliyliza na Othaman alimfuata na kumnong'oneza sikioni

"Whaaat?!! Hakeem ndie aliyefanya mchezo huo? Inamaana kuna kijakazi anatembea nae?"

Madame aliuliza kwa hasira huku akiwa anatetemeka na Othman aliishia kuinama kumpa heshima akiashiria ni kweli Hakeem alikuwa na Mahusiano ya ki mapenzi na mmoja kati ya wasichana waliokuwa wanafanya kazi katika jumba hilo la kitajiri la Mzee Mustapha.

"Ni aibu kwa Mtoto wa Mfanya biashara maarufu kuwa na mahusiano na kijakazi. Tafadhali naomba habari hii isivuje mara na ikawafikia waandishi wa habari. Naitaji kumjua huyu Kijakazi"

Madame aliongea na kuondoka zake.
                  *****

Baada ya kuambiwa na Liyuna kuwa alikuwa na mimba yake lilimchanganya sana Hakeem.

Akiwa chumbani kwake alishindwa kupata usingizi huku akifikiri ni vipi anaweza kumfikishia Mama yake taharifa hiyo bila kujua kuwa Mama yake alishapata taharifa bado kujua tu kama Mwanamke Mwenyewe ni Liyuna na tayari alikuwa ni mjamzito.

"Liyuna anapaswa kuondoka katika jumba hili kabla ya Mama hajagundua lolote"

Hakeem aliongea na kusitishwa kwa sauti ya Mama yake kubisha hodi.

Alisogea na kufungua mlango na Mama yake aliingia na kufikia kumfinya sikio lake 

"Kwanini unashindwa kujitambua? Hivi wewe wa kutembea na Kijakazi kweli? Baba yako akisikia unafikiri atakuelewa kwa upuuzi wako? Haujui kama wewe ni Mmiliki wa kampuni hii?"

Madame aliongea kwa hasira huku akimfinya sikio

"Lakini Ma....ma uuuh!!" Alishindwa kujitetea na kuugulia maumivu.

"Sitaki kusikia chochote kuhusu huyo mpuuzi wako na kuanzia leo unapaswa kutambua kuwa wewe ni Mume wa Mtu mtarajiwa na unapaswa kumuoa Shaymaa"

Madame aliongea na kumfanya Hakeem ashangae kidogo "Shaymaa ndio nani?"

"Ni huyu Rayuu mpya, unapaswa kumuoa kwa sababu Baba yako amevutiwa nae sana hivyo itakusaidia katika mbio zako za kuwa mrithi sahihi wa Mzee"

Madame aliongea na kumuacha Hakeem akijiuliza ni wapi amelisikia jina la Shaymaa na kujikuta akiwa hana kumbukumbu ila aligundua kuwa jina hilo halikuwa geni katika masikio yake.
                *****

Asubuhi na Mapema Shaymaa aliamka na kuendelea na kuingia jikoni na kuandaa kufungua kinywa cha Mzee Mustapha.

Mzee Mustapha alipoamka cha kwanza alienda katika chumba cha Shaymaa na kujaribu kugonga lakini aliona kimya

"Ameshaamka, amefanya mazoezi na sasa yupo jikoni" 

Mlinzi wake alimwambia Mzee na kisha aliinama na kumpa heshima yake "Hivi huyu Othman ni Mpuuzi? Anawezaje kumpeleka jikoni Binti yangu? Nilimwambia kama ni Kijakazi yule?"

Mzee Mustapha aliongea na kuelekea jikoni huku akiwa amechukizwa 

"Othman kitu gani unafanya? Toka lini Rayuu akawa Kijakazi katika jumba hili?" 

Mzee Mustapha aliongea kwa hasira huku akiwa amemtolea macho Othman.

"Hapana Baba ni Mimi ndio niliamua mwenyewe, nilitaka nikutengenezee mchemsho wa Mboga za majani, nilipokutazama kwenye macho yako niligundua una upungufu wa damu" 

Shaymaa aliongea na kusogea alipo Mzee Mustapha na kumuonjesha kidogo "Haya tafuna kidogo Baba" Shaymaa aliongea na Mzee hakuwa na jinsi zaidi ya kutabasam na kufungua kinywa ili aonje mapishi ya Binti yake.

Shaymaa alikuwa ni fundi katika swala la mapishi hivyo Mzee Mustapha alipojaribu kuonja mchemsho wa mboga za majani alizopika Shaymaa, alibaki ameduwaa!!

"Umepika Mwenyewe hii?" Mzee aliuliza huku akiwa anatafuna.

"Ni Mimi Baba nimejaribu tu ila samahani najua kuwa hautofurahia" Shaymaa alimjibu na Mzee Mustapha alifurahi zaidi.

"Sijawahi kuonja ladha adhim kama hii. Rayuu huwe unanitengenezea kila siku hii"

Mzee Mustapha aliongea na alisogea kwenye meza ya chakula tayari kuanza kula mchemsho maalum alioandaliwa na Shaymaa.
                   ******

Asubuhi na Mapema pili aliweza kubeba kila kilicho chake na kupakia kwenye mabegi yake aliyoweza kuyabeba "Nitaleta gari kuja kuchukua vitu vyangu vingine"

Pili alimwambia Feisal huku akiwa na udhuni utafikiri siyo yeye aliyekuwa akimpiga Mumewe.

"Nakutakia safari njema" Feisal alimjibu na Pili hakuweza kusubiri na badala yake aliamua kuondoka kwao huku moyo wake ukiwa na chuki dhidi ya Shaymaa.

Pili alifika kwao na kukabidhi talaka kwa Baba yake huku akiwa analia "Nimeachika Baba" Pili alimwambia Baba yake baada ya kutaka kujua nini kimemrudisha nyumbani.

Mzee Juma alionekana kutabasam baada ya kufungua na kuisoma talaka aliyokuja nayo Pili "Mumeo anakupenda sana Mwanangu ila wewe una matatizo. Hii siyo talaka" 

Mzee Juma aliongea na kumstua Pili aliyestuka baada ya kusikia maneno hayo na kuichukua talaka na kuipitia.

"Samahani Baba, naandika barua hii kwa maumivu makubwa sana kutokana na udhalilishaji ambao Mke wangu amekuwa akinifanyia kwa kunipiga kama Mtoto wake. Siyo kama nashindwa kumpiga hapana, ila nimekuwa nikithamini na kumuheshimu utu wake. Nimemdanganya kuwa nampa talaka hili aje huko walau apate kujifunza jinsi gani ya kuishi na Mumewe"

Pili alimaliza kuisoma barua aliyoandika Feisal kuja kwa Baba yake na kujikuta akilia na kumuomba Msamaha Baba yake huku akikiri kuwa amemkosea sana Mumewe

"Nimemkosea sana Feisal, kweli nilikuwa simtendei haki kama Mume wangu" 

Pili alilia na Baba yake alibaki akimshangaa "una bahati sana kupata Mwanaume mwelevu kama Feisal. Lakini nikwambie tu. Siku zote Mwanaume hakuna kitu hasichoweza kuvumilia kama kero, hapo hata nikisikia kuwa Feisal ana Mwanamke mwengine wa nje wala sitashangaa"

Baba alimwambia Mwanae huku pili akiwa makini kumsikiliza.
                  *******

"Heti nini? Mzee akunywa chai maalum ambayo nimekuagiza hawe anakunywa?"

Madame alistuka na kumuuliza Mmoja wa Kijakazi wake ambae alipewa kazi maalum na Madame 

"Anapaswa kunywa chai ile siku 90 mfululizo kabla umauti haujamfika. Sasa kwanini huyu Shaymaa anataka kunipanda kichwani? Yani siku moja tu kuingia humu anataka kujiona ni Mtu Maalum? Hata ndoa yake niliyopanga itakuwa ni ya Mkataba na ataachika baada ya Mzee Mustapha kufa"

Madame aliongea na Kijakazi wake katika chumba chake maalum. Na wakati wanaongea hayo Shaymaa alikuwa mlangoni akisikia kila kitu

"Inamaana Mama anampa sumu maalum Mzee Mustapha ili kumuua na Hakeem arithi mali? Kwani Hakeem siyo Mtoto halali wa Mzee Mustapha?"

Shyamaa alijiuliza maswali baada ya kugundua kuwa Madame alikuwa ameteuwa Mtu maalum wa kumpa sumu Mzee Mustapha ili afe baada ya miezi mitatu ......

NINI KITAENDELEA? SHYAMAA ATAFANYA NINI BAADA YA KUGUNDUA HAYO? 
MAUMIVU YA NDOA 
SEHEMU YA 24
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Hivi ni kweli unapaswa kuijua kila siri? Kuna wakati unaweza kujuta kwanini umeijua siri fulani kwani kwa kujua kwake kunaweza kukufanya ukose Amani na uishi kwa hofu baada ya kuijua siri hiyo

Baada ya kujua kuhusu Madame, Shaymaa alirudi chumbani kwake huku akiwa ametawaliwa na hofu akiwa hajui nini afanye kwa wakati huo “Nawezaje kumsaidia huyu Mzee?” Nitawezaje kumuondoa katika jambo hili? Hapana siwezi kufanya hivi naweza kuatarisha hata maisha yangu ni bora nitoroke katika hii nyumba”

Shaymaa alijiuliza maswali na kufikia muafaka baada ya kuona hawezi kupambana na Madame ni bora atoroke na kuondoka zake amuache Mzee Mustapha na Mkewe waendelee na maisha yao

“Lakini anawezaje kutaka kumuua Mwanaume mstaarabu na mwenye kujali kama Mzee Mustapha? Anaonekana ana upendo wa ajabu sana Baba wa Watu, lakini kwanini amuue?” 

Bado Shayamaa alikuwa na hofu na kujikuta angalau akitaka kujua zaidi kuhusu Madame.
                            *****
Hakeem alikuwa ni kijana mvivu anaependa starehe kupita maelezo huku jambo lake kubwa alipendalo ni kukimbiza gari za mashindano.

Akiwa amelala alisikia mlango unagongwa kwa nguvu kitu ambacho kilimkera na kujaribu kugeuka upande wa pili na kuziba masikio ili hasisikie kelele za Mtu anagonga mlango kubisha hodi. Kelele zilipomzidia aliinuka huku akiwa amechukia na kwenda kufungua mlango.

“Unapaswa kuwa Mkurugenzi wa kampuni, unawezaje kulala mpaka muda huu?” Madame aliingia chumbani kwa Mwanawe na Hakeem wala hakutaka kumsikiliza Mama yake badala yake alirejea kitandani na kulala tena.

“Nimekubali ombi lako la kukuruhusu kwenda Nairobi katika mashindano ya magari, pia nitakununulia gari mpya kama vile ulivyokuwa unataka” Madame aliongea na Hakeem alikurupuka kutoka usingizini utafikiri Mtu aliyekuwa ameota njozi ya kutisha

“Asante sana Mama” Hakeem alimrukia Mama yake na kumkumbatia huku akiwa haamini kile alichokuwa amekisikia

“Nimeshawaliana na Anko wako unapaswa kwenda kutazama gari aliyoichagua, lakini anasema ni nzuri na utaipenda, pia nimekuingizia pesa kwenye akaunti yako, tafadhali itumie kwa umakini”

Madame aliongea na kumuacha Mwanae akiwa na furaha tele baada ya kusikia taharifa hizo.

Hakutaka kusubiri muda uende na badala yake aliingia bafuni kwenda kuoga ili kwenda kutazama gari ambayo Mama yake ameshailipia na yeye anapaswa kwenda kuikagua kama ameipenda au lah
                          ******
Siku zote alikuwa akisikia kuhusu swala la Mtu kulia kwa furaha lakini hata siku moja hakuwahi kuhisi ni vipi Mtu anaweza kulia kwa furaha.

Akiwa nyumbani kwa Baba yake, Pili alijifungia kwenye chumba cha Mdogo wake, chumba ambacho alikuwa anakaa yeye kabla ya kuolewa na Feisal. 

Alifikiria jinsi alivyokuwa hamuheshimu Mumewe na alivyokuwa akimpiga “Kumbe Feisal alikuwa na uwezo wa kunipiga ila alikuwa akiniachia tu kwa sababu ananipenda Mkewe” 

Pili aliongea Mwenyewe na kujikuta akiangua kilio baada ya kugundua makosa yake kwa Mumewe “Ama kweli nimeamini Mwanamke Mpumbavu uvunja ndoa yake kwa mikono yake yeye mwenyewe” Pili aliongea Mwenyewe na kuangua kilio akiwa haamini kama kweli Feisal hakudhamilia kumpa talaka bali alimtaka ajifunze kutokana na makosa.

Akiwa anaendelea kulia, alisikia Mtu anabisha hodi kwa kugonga mlango, alijua atakuwa ni Mdogo wake Mayasa hivyo hakutaka kumuonesha kuwa alikuwa analia. Alifuta machozi haraka na kwenda kufungua mlango.

Hakuamini macho yake baada ya kumuona Feisal ndie aliyekuwa anabisha hodi. Feisal alikuwa amependeza kupita maelezo. Alimtzama Mkewe na kutabasam

Ilikuwa ni ngumu kwa Pili kuweza kujizuia, alimtazama Mumewe na kumkumbatia kwa nguvu “Asante sana Mume wangu” Pili aliongea huku akiwa amemkumbatia Mumewe

Waliingia chumbani na Pili alimuomba msamaha Mumewe na hakusita kumshukuru kwa wema alioamua kumtendea “Feisal wewe ni Mume bora sana kwangu tafadhali nisamehe sana kwa yote niliyokutendea. Akika Mimi sikuwa Mke bora kwako, nakuahidi nitajirekebisha na utajivunia kunioa”

Feisal alimshukuru Mkewe kwa kuweza kutambua makosa yake na kukiri mbele yake hivyo aliweza kumsamehe na kumwambia kuwa aliamua kumfanyia vile ili kuweza kumpa nafasi ya kutambua kuwa hata kama anampenda, hata kama anamuona dhaifu mbele yake basi anaweza kufanya maamuzi ambayo yanaweza kumuumiza zaidi.

“Umenifanyia Wema mkubwa sana Mume wangu, kuna jambo nilikuwa naomba unikubalie kama hautojali” Pili aliongea na Feisal alitulia kumsikiliza.

Nilikuwa naomba umuoe Shaymaa hawe Mke wako wa pili kwani natumahi atakuwa ni Mwanamke bora sana kwako pia atakuwa ni Mtu sahihi kwa mimi kujifunza kupitia yeye”

Pili aliongea na kumstua Feisal ambae alitoa miwani yake na kumtazama vyema Mkewe
                            ******
Madame alikuwa ameshagundua kuwa Hakeem alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Liyuna na tayari ana ujauzito wake.

Alichoamua kufanya ni kumpa furaha Mwanae na kumtengenezea mazingira ya kumuondoa katika jumba la kifahari la Mzee Mustapha pasipo hata yeye Hakeem kutambua kuna nini ambacho Mama yake anataka kufanya mpaka amemtimizia kila alichokuwa anahitaji tena kwa haraka zaidi.

Lakini pia aliweza kutambua kama Liyuna ndie Kijakazi aliyemsikia usiku akiongea kuhusu kifo cha Rayuu “Ameshaondoka” Mmoja kati ya wafanya kazi wake aliokuwa anafanya nao kazi zake Binafsi alimpa taharifa baada ya kumuona Hakeem ametoka katika jumba la kifalme

“Unapaswa kumuua Liyuna haraka sana kwani ana ujauzito wa Hakeem na sihitaji hiyo damu chafu kwenye familia yangu, na akikisha hakuna Mtu yoyote anayetambua jambo hilo” Madame aliongea na kijana wake mtiifu aliitika kwa kuinama kuashiria amekubali amri na kuondoka haraka.

Wakati anatoka alipishana na Sabraha aliyekuwa anakwenda kufanya usafi chumbani kwa Madame kiasi ambacho hata Madame alistuka 

“Nani amekwambia uje kufanya usafi muda huu?” Madame alistuka na kumuuliza Sabrah “Madame huu ndio muda wangu, samahani kama nitakuwa nimekukwaza” 
Sabraa liongea na Madame alichukia na kumfukuza huku akiwa na mashaka nae uenda amesikia mazungumzo yao.

“Liyuna tafadhali fanya juu chini utoroke la sivyo unauwawa” Sabrah alimwambia Liyuna aliyeonekana kustuka na taharifa hiyo na kutaka kujua zaidi.

Sabla alimwambia kila kitu alichosikia baada ya kwenda kufanya usafi chumbani kwa Madame na kukuta anaongea na Mfanyakazi wake wa Siri amabe hata Mzee Mustapha alikuwa hamtambui.

Liyuna aliumia sana baada ya kusikia taharifa hizo na kujikuta akilia “Mwanangu huna hatia hata kidogo ila Mimi Mama yako ndio Mwenye hatia” Aliongea huku akiwa ameshika tumbo lake

Hakutaka kusubiri na badala yake alichomoka kule kwenye vyumba vya vijakazi na kutazama ni vipi anaweza kutoroka.

Wakati anatoka na kutafuta njia ya kuweza kutoroka ghafla aliweza kumuona yule kijana na hakutaka kusubiri na badala yake alianza kukimbia na yule kijana kuona vile alianza kukimbia.

Liyuna alikimbia na kukunja kona na yule kijana wakati anakuja mbio alikutana na Othman Mpishi mkuu “Vipi Kijana, kuna tatizo?” Othman alimuuliza yule kijana baada ya kumuona anakuja mbio Yule kijana hakutaka kumueleza chochote badala yake aliishia kumtazama huku akiangaza kila upande
                             ******

Shaymaa akiwa chumbani kwake alikuwa akitazama picha za Mtu ambae alikuwa amefanana nae kwa kila kitu, picha ambazo Rayuu alizochora kwa mkono wake “Itakuaje kama Mzee Mustapha akijua kuwa na Mimi nina uwezo wa kuchora kuliko hata Rayuu?”

Shaymaa alijiuliza mwenyewe na kutabasam, lakini tabasam lake lilikatishwa na Mtu aliyeingia ghafla chumbani kwake pasipo kubisha hodi.

“Tafdhali naomba msaada wako nitoroke katika nyumba hii kabla Madame hajanifanyia kitu kibaya, ameshatuma Mtu ili aje kuniuwa” Liyuna aliongea huku akiwa anahema kiasi ambacho alimstua sana Shaymaa
                             *******
Ilikuwa ni gari ya ndoto yake na Mjomba wake alimwambia kuwa anaweza kuijaribu kwa kupiga misele kutwa nzima kabla Mama yake hajailipia.

Lilikuwa ni jambo ambalo Hakeem alitamani kulisikia na wala hakusubiri kuulizwa kwa mara ya pili na badala yake aliomba funguo na kupiga misele.

Akiwa kwenye gari mpya aliyopewa kupiga misele alikumbuka kuhusu Liyuna “Kabla siajaenda Nairobi napaswa kufanya jambo kwa ajili yake la sivyo Mama anaweza kugundua na akamfanya kitu kibaya”

Hakeema aliongea huku akiwa anaendesha gari lakini alikumbuka jambo na kuegesha gari yake pembeni akionekana kutabasam.
*****

Irina aliweza kufika hospital alipokuwa amelazwa Mume wake, alifika na kukuta Abdul akiwa amepata nafuu 

“Umepata taharifa yoyote kuhusu Shaymaa?” Abdul alimuuliza Mkewe aliyeonekana kuchukizwa baada ya kusikia swali la Mumewe

“Abdul ni vyema ungepata chakula kwanza kwa maana Dokta amesema kwa dawa unazotumia unapaswa kula zaidi” Irina alimjibu Abdul huku akijaribu kumlisha “Irina nawezaje kula ikiwa Shaymaa amejiuwa kwa sababu yetu? Wewe hujioni kama ni Mtu mwenye hatia?” Abdul alimuuliza Irina aliyeonekana kustuka kwa taharifa hiyo

“Shaymaa amejiuwa?” Irina aliuliza na kabla Abdul hajajibu kitu, simu ya Irina ilikuwa inaita.

Alichukua simu na kutazama na aligundua kuwa aliyekuwa anapiga hakuwa mwengine bali ni Hakeem, alichukua simu na kwenda kuongea pembeni kiasi ambacho hata Abdul alimshangaa

“Hivi siku ile Mumeo alipopata fahamu alikuwa anataja jina gani?” Hakeem alimuuliza Irina baada ya kupokea simu na Irina alimjibu haraka akitamani kujua kama Wanajuana “Shaymaa” Hakeem alifurahi baada ya kusikia jibu hilo na kugundua sasa Jina la Shaymaa ni wapi alikuwa amelisikia 

“Yule Mwanamke niliyekupa kazi ya kumuondoa nyumbani kwetu pia anaitwa Shaymaa siyo huyo Dada yake Mumeo?”

Hakeem aliongea na Irina alistuka baada ya kupata taharifa hizo ………… NINI KITAENDELEA? JE IRINA ATAMWAMBIA ABDUL KUHUSU SHAYMAA? VIPI SHAYMAA ATAWEZA KUMSAIDIA LIYUNA KUTOROKA? 

MAUMIVU YA NDOA 
SEHEMU YA 25
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Hivi ni nani aliyesema upele umempata mkunaji? Nilikuwa nataka kujua tu alimaanisha nini kuongea kauli hii?

Irikuwa ni taharifa ambayo ilimfuraisha sana Irina, alitamani kusikia huyo Shaymaa aliyekuwa nyumbani kwa kina Hakeem hawe Shaymaa anaemjua yeye 

“Hakeem unaweza kunitumia picha yake tafadhali?” Irina alimuuliza kwa shauku Hakeem huku akiwa na matarajio makubwa kuwa Shaymaa aliyekuwa kwa kina Hakeem ni huyo anayesemekana kuwa amekufa 

“Hapana sijabahatika kumpiga picha ila nitafanya hivyo nikirudi nyumbani kwa maana nahitaji ndani ya masaa 48 hawe ameshaondoka nyumbani” Hakeem aliongea na wakakubaliana na Irina sehemu ili waongee zaidi huku Irina akimwambia kuwa atamtumia location wapi wakutane

Baada ya kutoka kuongea na Hakeem, Irina alirudi kwa Abdul aliyekuwa amechukizwa na kitendo cha kumuona Mkewe akiwa ameenda kuongea na simu pembeni “Inamaana kuumwa kwangu ndio kumekupa fursa ya wewe kuchepuka?” Abdul alimuuliza Mkewe huku akiwa amechukia na kumfanya Irina atabasam kidogo

“Mume wangu mbona una wivu kiasi icho? Si kila jambo lazima niongee mbele yako Mume Wangu, wala usijali mimi siwezi kukusaliti”

Irina aliongea utafikiri kweli wakati usiku uliopita alitoka kulala na Maganga tena kwenye kitanda cha Mumewe. Alikusanya vitu vyake tayari kuondoka, alikumbuka kitu na kumgeukia Mumewe “Hivi ulisema Shaymaa amefariki?” Irina aliuliza na swali lake lilimuumiza Abdul ambae alikuwa ameguswa na kifo cha Shayamaa pasipo kujua kama mwenzake alikuwa hai anapambana na Watu wengine kwenye jumba la Mzee Mustapha
“Imeniuma sana kusikia kuwa Shaymaa amejiua, nilipigiwa simu wakati naenda kazini. Kiukweli nilistuka sana kiasi ambacho nilijikuta napata ajali” Abdul aliongea na kumfanya Irina agundue kuwa ajali ya Mumewe ilisababishwa na taharifa za kifo cha Shaymaa.

“Najua kuwa unampenda sana Shaymaa” Irina aliongea na kuondoka huku akiwa amechukizwa na kitendo cha Abdul kumwambia kuwa alipata ajali baada yakusikia kuwa Shaymaa amefariki
                          *******

“Tafadhali naomba unisaidie, nina Mtoto wa Hakeem tumboni” Liyuna alimwambia Shaymaa na kumfanya Shaymaa abaki na mshangao 

“Unaweza kunisababishia matatizo tafadhali naomba uondoke, Mimi ni Mgeni wala sijui ni vipi naweza kukusaidia utoke katika jumba hili” Shaymaa aliongea kwa upole na kumfanya Liyuna azidi kumng’ang’ania Shaymaa

“Najua kama wewe ni Mgeni ila umepata bahati ya kuaminika na Mzee, tafadhali naomba utumie fursa hiyo ili unisaidie nina Mtoto Mimi sipendi kumuona Mwanangu anakufa akiwa tumboni mwangu”

Liyuna alimsimulia kila kitu kuhusu Madame kuhusika na kifo cha Rayuu “Madame anawezaje kumuua Mwanae?” Shaymaa alistuka na kumuuliza Liyuna aliyeonekana kuwa na hofu akihofia maisha yake

“Inavyosemekana Rayuu si Mtoto wa Madame bali ni Mtoto wake wa kambo” Liyuna aliongea na kuzidi kumshangaza Shaymaa baada ya kusikia Madame alihusika na kifo cha Rayuu kwakuwa hakuwa Mtoto wake wa kumzaa.

“Anataka kuniua na kuna Mtu wake ambae ndie aliyehusika na kumuua Rayuu amekuja na alikuwa ananikimbiza. Anafanya yote ili nisizae na Hakeem tafadhali Shaymaa nao…………” Kabla Liyuna ajaendelea kuongea alinyamazishwa na sauti ya Mtu akigonga mlango akitaka kuingia. Wote walistuka kutazamana huku Liyuna akiwa anatetemeka na kutafuta kwa kujificha huku akiwa anaogopa
                    *****
“Unafikiri nitakuwa nimepoteza upendo juu yako” Feisal alimwambia Mkewe huku akiwa anamtazama “Hapana Feisal kuna vitu nimejifunza kama Mwanamke, pia unayo nafasi ya kuoa Wake wa 4 Mume wangu, umeshatumia nafasi moja bado unazo tatu kwanini usitumie hiyo nafasi kwa kumuoa Shaymaa”

Pili aliongea na kumfanya Feisal atabasam na kumsogelea “Nafikiri kuna kitu utakuwa umejifunza baada ya Mimi kukwambia kuwa nitamuoa Shaymaa, ila Mke wangu wala sijamaanisha bali nilifana vile ili tu kustua akili yako na unione na Mimi nina uwezo wa kufanya lolote na muda wowote”

Feisal aliongea na kumfanya Pili atabasam kidogo “Feisal nakupenda sana Mume wangu, tafadhali usije ukanifanyia kile ulichonifanyia. Naomba isije kutokea hata siku moja tukaja kuachana. Nakuahidi kuanzia sasa nitakuwa Pili yule uliyeniambia naomba nikuoe”

Binaadamu huwa tunatambua umuhimu au thamani ya Mtu au kitu endapo tu itatokea tumekipoteza. Hakuna kitu kizuri katika maisha kama kumuonesha Mtu ni jinsi gani ana thamani kwako kabla haujampoteza

“Feisal!! Shaymaa ni Mwanamke sahihi kwako hivyo sihitaji kuona unakaa nae mbali, tafadhali naomba umuoe” 

Pili alisisitiza jambo lake na safari hii Feisal alishindwa kujizuia na kujikuta akitoa kitambaa na kufuta machozi yake 

“Fei nimekukosea?” Pili aliuliza na Feisal alitikisa kichwa kuashiria kukataa jambo hilo “sasa kwanini unafuta machozi?”

“Shaymaa alipitia machungu sana kwenye ndoa yake, aliolewa na Mwanaume ambae hakuwahi kuthamini upendo wake hata siku moja, alimfanyia mengi yaliyovunja moyo wake” 

Abdul alimsimulia Mkewe kuhusu Shaymaa mpaka pale ambapo Baba yake alimuita na kumuomba akae nae na kuongea nae Shaymaa kwa yale anayopitia “Lakini kauli zako ambazo uliongea siku ile zilimuumiza Shaymaa na akaamua kuchukua maamuzi ya kwenda kujiua na mpaka leo hatujui wapi alipo na hatujui kama ni mzima au lah” 

Maneno ya Feisal yalimuumiza sana Pili na kumfanya ajisikie vibaya kwa kile ambacho Mumewe alimwambia “Kwasababu yangu Mimi nimesababisha Shaymaa amechukua maamuzi magumu? Najisikia aibu sana kuwa Mkeo” “Hapana usiseme hivyo Mke wangu, Shaymaa hawezi kufa naamini yupo hai na sikumoja atajumuika na sisi”

Kila mmoja ana haki ya kuongea kile akitakacho ila wakati mwengine unaweza kuongea kitu ambacho kinaweza kumuumiza Mtu na kumfanya afikilie kufanya kitu kibaya kwa ajili yako

Hiyo ndio hali ambayo alikuwa nayo Pili, kila alipokumbuka jinsi alivyoweza kumdhalilisha Mwanamke mwenzake alijiona dhairi ni Mtu mwenye hatia
                                *****
Sauti ya mlango ukigongwa ilizidi kusikika na Liyuna alizidi kuchanganyikiwa na kuangaika kila upande akitafuta sehemu ya kujificha.

Liyuna alipanda kitandani na kujifunika na shuka “Utaonekana hapo” Shaymaa alimwambia na kuangaza kila upande. “Tafadhali ingia kwenye kabati” Shayamaa aliongea na kabla hajamaliza kauli yake, tayari Liyuna alikuwa ameshaingia kwenye kabati

Shaymaa alimfungia Liyuna kwenye kabati na kuusogelea mlango huku akiwa anatetemeka “Karibu” Alifungua mlango na kumkaribisha aliyekuwa anabisha hodi.
                          *****
Ilikuwa ni gari ya kifahari iliyoweza kumstaajabisha Irina baada ya kumuona Hakeem akiegesha gari yake katika maegesho ya magari ya Mgahawa wa Misosi Lounge.

Hapo ndipo Irina alipokuwa amemkaribisha Hakeem ili wakutane na lengo lake ni kumvutia kijana huyo Mtanashati.
“Hongera sana Irina, napenda sana Wanawake wa aina yako, unajua hakuna jambo zuri kama unapomuona Mwanamke anaondoa ile dhana inayoitwa tegemezi”

Hakeem aliongea na kumfurahi baada ya Irina kumtambulisha kuwa mgahawa wa Misosi lounge yeye ndio mmiriki

Waliongea na kubadilishana mawazo na mbaadae waliingia kwenye agenda yao iliyokuwa imewakutanisha pale “kwanini unataka kumtimua Shaymaa?”

Irina ndie aliyekuwa wa kwanza kuuliza kuhusu Shaymaa huku akiwa anatabasam kinafki “Namchukia sana yule Msichana. Kwanza nilikuwa nataka kujua kuhusu yeye, yani ni Mwanamke wa aina gani maana Wazazi wangu wananilazimisha nimuoe wakati hata hawajui wapi alipotoka na mimi hofu yangu hasiwe tapeli labda anataka kutumia Mwanya huo ili kuwatapeli Wazazi wangu”

Hakeem aliongea na kumstua Irina ambae hakutegemea kama anaweza kusikia habari hiyo “Wewe umuoe Shaymaa?” Alimuuliza na Hakeem alijibu kuwa huo ndio ugomvi mkubwa wa yeye na Wazazi wake “Samahani naomba nikuulize kitu kama hautojali?” “Sawa unaweza kuuliza tu usijali”

Hakeem alimjibu na Irina alishusha pumzi kidogo kabla ya kuongea “Wazazi wako wanajimudu kidogo?” Irina aliuliza swali ambalo alijibiwa kwa swali pia kutoka kwa Hakeem ambae alimuuliza kwanini ameuliza hivyo “Kwasababu nataka nikwambie tabia za Shaymaa”
Baada ya kusikia hivyo, Hakeem hakutaka kumficha tena Shaymaa na alimwambia kuwa yeye ni Mtoto wa Tajiri maalufu anayeitwa Mustapha.

Irina alistuka baada ya kujua kuwa Hakeem ni Mtoto wa tajiri maalufu anayeitwa Mustapha “Samahani sikukwambia ukweli siku zile tuliponda kumtazama Mume wangu” 

Irina alijifanya kuudhunika ili kuongea uongo juu ya Shaymaa na lengo lake kubwa lilikuwa ni kuharibu kila kitu kwa Shaymaa 

“Shaymaa ni Mwanamke tapeli sana anayetumia Mwili wake kuwatamanisha Wanaume na kuwatapeli kisha anawateka na kuwafanyia kitu kibaya. Mume wangu alikutana na Shaymaa kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram na huko walianza kuwa na mahusiano kabla ya kumtapele na kumteka kama ulivyomuona hali yake”

Irina alimdanganya Hakeem bila hata kuwa na chembe ya aibu na baada ya kusikia Hakeem ni Mtoto wa tajiri aliona hiyo ndio nafasi sahihi ya kuwa nae Hakeem
                             ******
Alikuwa si mwengine bali Othman Mpishi mkuu katika jumba la Mustapha ndie aliyekuwa amebisha hodi na kuingia chumbani kwa Shaymaa

“Samahani sana kwa kuchelewa kufungua” Shaymaa aliongea huku akiwa anatetemeka kiasi ambacho hata Othman alimshangaa

“Akika wewe ni Malaika katika jumba hili la Mustapha” Othman aliongea na kuingia mpaka ndani akijaribu kuangaza “Kwanini unasema hivyo Baba?” Shaymaa aliuliza na Mzee Othman alitabasam kidogo kabla ya kumjibu “Mustapha alikuwa akiishi kwa hofu sana kabla ya ujio wako, lakini leo anaonekana ni Mtu mwenye furaha sana. Amenipigia simu ameomba umuandalie chakula maalum cha mchana kwani anaamini kuwa wewe ni Mtu ambae umeletwa kuja kumfanya afurahie maisha yake” 

Othman aliongea na kabla Shaymaa hajajibu kitu Madame akiwa na kijana wake waliweza kuingia “Hata Wewe Othman unaungana na huyu kunisaliti?” Madame aliongea na kumshangaza Othman na wakati huo Shaymaa akiwa anatetemeka akihofia Liyuna akionekana itakuaje

“Madame kuna nini? Tafadhali sina nikijuacho Mimi” Othaman aliongea na Madame hakutaka kuendelea na badala yake alimuamuru kutoka nje.

Baada ya Othman kutoka nje, Mdame alimtazama Shaymaa na kumzibua kibao cha nguvu “Mshenzi Mkubwa wewe, unathubutu vipi kuungana na Shetani ili kunidhuru Mimi?” Shaymaa hakuwa na cha kusema badala yake alianguka na kupiga goti na kuomba msamaha

Yule kijana aliingia bafuni kumtafuta Liyuna hakumuona, alitazama chini ya uvungu wa kitanda pia hakumuona “Madame ameshamtorosha hayupo humu” Yule kijana aliongea na Madame alizidi kuchukia.

“Hivi unataka kuwa nani katika jumba hili? Mimi ni Madame wewe unataka kuwa nani?” Madame alimuinamia na kuongea kabla ya kumvuta sikio na kumzibua tena kibao “Usalama wako ni kutaja wapi alipo Liyuna kabla sijakufanya kitu kibaya zaidi” 

Madame aliongea kwa sauti fulani ya msisitizo “Unanionea bure mi sijui chocho…………” Kabla hajamaliza alimtandika tena kibao “Keleleeeeeee!! Unataka kujifanya sungura si ndio?” Madame aliongea na kuinuka kisha akatazama kwenye kabati na kucheka

“Umemficha kwenye kabati si ndio?” Madame alimuuliza Shaymaa na kumfanya astuke na kuzidi kutetemeka “Zimbo hebu fungua kabati”

Madame aliongea huku akimtazama Shaymaa………… NNI KITAENDELEA? USIKOSE EP 26 

Post a Comment

Previous Post Next Post