🔐 MAUMIVU YA NDOA (16-----20) 😭😭😭😭


SEHEMU YA 16


Baada ya kuona gari ya Irina imeegeshwa sehemu, Jack alimwambia dereva wa bodaboda wageuze na kurudi nyuma.

Waligeuza na kweli walifanikiwa kuikuta gari ya Irina ikiwa imeegeshwa sehemu. Jack aliteremka katika bodaboda huku akiwa anatabasam baada ya kugundua kuwa kweli ilikuwa ni gari ya Irina.

Aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpatia dereva wa bodaboda. Lakini ghafla alipatwa na mshangao baada ya kumuona jamaa akitoka saluni huku akiwa ameshika funguo na kuingia katika ile gari ya Irina na kuiwasha kuashiria alikuwa anataka kutoka

“Inamaana nimefananisha” Jack alijiuliza mwenyewe huku akiwa ameshangaa. Alitupa macho mpaka kwenye namba ya gari na kugundua kuwa ilikuwa ni kweli gari ya Irina “ Nini kimetokea hapa mbona nashindwa kuelewa?” Alijiulza na wakati huo gari ilikuwa imeshageuzwa na kuingia barabarani na kuondoka kwa kasi ya ajabu

Hakuwa na jinsi ilimbidi amwambie dereva wake wa bodaboda warejee nyumbani kwao kwani atakuwa amefananisha gari, uenda haikuwa gari ya Irina 

Walitembea kidogo na alipatwa na Mstuko “Simama” jack aliongea na dereva wa Bodaboda alisimama tena “Vipi tena Mdau?” Dereva alimuuliza baada ya kusimamisha pikipiki “Yule changudoa itakuwa amenichezea Mchezo, yupo katika ile gari tuliyoifuata pale” Irina aliongea pasipo kumtazama Dereva wake.

“Inamaana Irina hataki kumuua Bwanaake?” Jack aliongea na kucheka mwenyewe huku akiamini kuwa Irina hana ujanja mbele yake.

Kama ambavyo Jack alivyokuwa anahisi kuhusu Irina ndivyo ambavyo ilivyokuwa, ni kweli alikuwa amejificha kwenye siti ya nyuma.

Irina aliweza kulala pasipo Irina kumuona na walipotembea kwa umbali kidogo aliweza kujitokeza katika gari na kumuuliza yule kijana aliyekuwa na hasili ya kiarabu “Vipi wanatufuatilia?” Irina aliuliza na yule kijana alitabasam na kumjibu hapana “hata kama wangetufuatilia, wasingeweza kutupata huu moto mwengine dada”

Yule kijana aliongea na Irina alifurahi na kupita kiti cha mbele na kukaa huku akifunga mkanda na kujiweka sawa

ILIKUAJE MPAKA YULE KIJANA ALIWEZA KUENDESHA GARI YA IRINA?

Baada ya Irina kuhisi Jack anaweza kumfuatilia, aliamua kuegesha gari nje ya saluni moja ya kiume na kushusha kiti chake ili asubiri walau kwa dakika kadhaa ili kujilidhisha kama Jack alikuwa anamfuatilia au lah!

Baada ya kugundua kuiona pikipiki ya Jack ikipita kwa speed ya hali ya juu alistuka na kuingia Saluni.

“Samahani naomba msaada kama kuna Mtu anaweza kuniendesha nitamlipa, nina tatizo kidogo” Irina aliongea na Watu waliokuwa mule saluni kwa pamoja walitaja jina la Hakeem.

Alikuwa ni kijana fulani mwenye asili ya kiarabu ambaye anasifika vyema kwa uwezo wake wa kukimbiza magari. Irina alimdanganya kuhusu Jack na kumwambia ni rafiki yake anayetaka kumtapeli hivyo anataka kumkwepa.

“Sawa itabidi wewe jifiche humo kwenye gari na funguo nipe Mimi, akija hapa nitamuonesha michezo” Hakeem aliongea na kuwafanya wenzie wafurahi.

Irina alimpa maelezo ya kina Hakeem kuhusu Jack jinsi alivyo na yeye aliingia kwenye gari na kujificha kama jinsi ambavyo walivykuwa wamekubaliana.

Kama walivyotegemea na ndivyo Jack alipokuja na Bodaboda yake na Irina akiwa kwenye gari alikuwa akiogopa na kutetemeka akihofia Jack kumuona. Hakeem aliingia kwenye gari na kupiga gia akiwaaacha kina Jack wakiwa wamepigwa na butwaa
                          ****
Feisal aliweza kurudi hospital kule ambapo alipokuwa amelazwa Mjomba na Watu wote walikuwa makini kusikiliza majibu kutoka kwake.

Alijiinamia na kujikuta machozi yakimtoka na kujikuta akishindwa kuongea “Niambie nini kimemkuta Mwanangu? Feisal sema nini kimemkuta Dada yako” Shangazi yake alimwambia na Feisal alijikuta akiwatazama na kusikitika.

“Sijafanikiwa kupata taharifa zozote zinazomuhusu Shaymaa” Feysal aliongea na kauli yake ilimchosha kila mmoja aliyekuwa pale ambapo walitegemea labda Feisal anaweza kuja na majibu mazuri kuhusu Shaymaa.

“Mimi nafikiri ili si jambo la kumuachia Feisal pekee bali sote tunapaswa kugawana, wachache wabaki hapa na wengine tuingie mtaani kwenda kumtafuta Shaymaa” Mmoja kati ya wana ndugu aliongea na kauli yake iliungwa mkono na baadhi ya Watu waliokuwa pale.

Dokta alitoka na kuita ndugu wa Mzee Majaliwa, ambapo wachache waliingia akiwemo na Feisal “Kutokana na vipimo vya hawali ambavyo Mzee Majaliwa ameweza kufanyiwa, imegundulika kuwa kutokana na mstuko alioweza kuupata, umeleta shida kidog katika mfumo wake wa damu hivyo, mpendwa wetu amepooza upande mmoja wa mwili wake” Dokta aliongea kwa upole na kuzidisha simanzi kwa ndugu zake huku Feisal akionekana kuchanganyikiwa zaidi.

Baada ya majibu hayo, Mzee Majaliwa alipaswa kuendelea kubaki hospital na ndugu walipaswa kurejea nyumbani huku Dada yake mzee majaliwa akitaka kupigana na Wifi yake akimtuhumu kuhusika na matatizo ya kaka yake pamoja na Shaymaa kwa roho yake mbaya na kumtaka abebe kila kilicho chake na kuondoka nyumbani kwao.

“Hivi wewe una akili timamu kweli? Yani unawezaje kumuhisi Kaka yangu ajiusishe kimapenzi na Mpwa wake?” Dada yake Mzee majaliwa alifoka huku Watu wakimtuliza

Busara za watu ziliweza kutumika na Shagazi alikuwa mpole utafikiri alikuwa kamwagiwa maji ya barafu.
                             ****

Irina na Hakeem waliweza kufika mpaka hospital na kufanikiwa kuingia katika wodi ambayo aliyokuwa amelazwa Abdul. 

Irina alipomuona Abdul jinsi alivyo alishindwa kujizuia na kujikuta machozi yakimtoka. Hakeem alimshika mkono na kumbembeleza na kumwambia asife moyo.

“Tumekuja kuchukua sindano ya sumu ya kumuua Abdul endapo tutakuta bado anapumua” Irina alijikuta akimtazama Abdul na kukumbuka kauli ya Jack na kujikuta akitetemeka “Hapana siwezi, Abdul nisamehe sana” Irina aliongea mwenyewe kiasi ambacho hata Hakeem alikuwa akimshangaa

Kauli ya Irina iliweza kumfanya Abdul afumbue macho na kuanza kuita
“Shaymaa!! Shaymaa nakufa!! Shaymaaaaa” fahamu zilimrejea Abdul na alikuwa akiita jina la Shaymaa. Irina alimtazama na kuchukizwa na kauli za Abdul Baada ya kuzinduka na kutaja jina la Shaymaa “Inamaana Mimi ananiona Shaymaa?” Irina alijiuliza Mwenyewe huku akiwa amechukizwa

“Naomba mtupishe tafadhali, muda wa kuwaona Wagonjwa umeisha” Nesi aliwaondoa na kuendelea kumuhudumia Abdul

“Hongera sana, Mume wako anaonekana anakupenda sana” Hakeem aliongea wakiwa wanatoka nje huku Irina akiwa anatembea kama anaenda kuzima moto akiwa amechukizwa na Abdul “kwanini unasema ananipenda?’ Irina alimuuliza Hakeem huku akiwa hamtazami

“Inaonekana Mumeo alikuwa akiwaza kuhusu wewe ndio maana alipopata fahamu tu, Mtu wa kwanza kutaja jina lake ulikuwa ni wewe” Hakeem alimwambia na Irina aliishia kuguna tu

“Mimi siitwi Shyamaa ila hilo ni jina la Bibi yake kijijini huko inawezekana amemkumbuka” Irina alijibu na kumfanya Hakeem ashangazwe na majibu yake.

Walipotoka nje ya geti walistuka baada ya kumkuta Jack akiwa amesimama huku akimtazama Irina na kusikitika na Irina alimkumbatia Hakeem kwa nguvu na kuwa karibu yake

“Abdul amelazwa wodi gani?” Jack alimuuliza Irina huku akiwa ameshika bomba la sindano jambo ambalo lililomfanya Irina astuke na kuogopa.

“Tafadahali Jack usifanye hivyo tafadhali nakuomba” Irina alimuomba Jack huku akionekana kuwa na hofu.

Jack alimtazama Hakeem na kumuuliza Irina “huyu ni nani?” Irina alimtazama Hakeem na kujikuta akiropoka “Ni Mpenzi wangu” “Naitwa Hakeem”

Hakeem alijibu bila hofu na kumpa mkono Jack na Jack hakusita kuupokea mkono wa Hakeem “Irina nina maongezi ya siri Mimi na wewe, Vipi tunaweza kwenda pamoja?” Jak aliongea na Irina alionekana kushangazwa baada ya kumuona Jack akiongea sauti ya kike tofauti na vile alivyomzoea.

Irina alikaa bila kujibu na kutafakari kwa sekunde kadhaa na aligundua kuna kitu Jack alitaka wakafanye na yeye alichomwa na maneno ya Mama yake Jack “Tunaweza kwenda nyumbani Baby?” Irina alimwambia Hakeem huku akimfinya mkono akimtaka akubali na Hakeema alitabasam na kukubali yupo tayari.
                           ******
Waliungana kwa pamoja kuweza kumtafu Shaymaa kila kona kila Mtaa lakini wapi Shaymaa hakuweza kujulikana wapi alipo wala taharifa zake hazikuweza kupatika kwa haraka.

Ndugu waliamua kwa pamoja kwenda kufanya matangazo kupitia vyombo vya habari ili kuweza kuona ni vipi wanaweza kumpata Shaymaa kwa haraka.

Usiku ulipoingia Feisal aliweza kurudi nyumbani kwake huku akionekana kuchanganyikiwa.

Pili alimjibu vibaya na kutaka kumpiga Feisal ambae siku hiyo alikuwa amebadilika na kutaka kumuonesha kuwa yeye ni nani.

Aliamua kumuandikia talaka huku akimuweka wazi kuwa endapo atafanikiwa kumpata Shaymaa basi kitu pekee atakachofanya ili kumfuta machozi ni kumuoa Shaymaa.

Baada ya kumaliza kuandika talaka, Feisal alimpa Pili ambae aliamua kuichana talaka na kumwambia hawezi kukubali kuachika hata siku moja
                           ******
Feni ya juu ikiwa inazunguka, macho ya Mtu yanaonekana yakitazama feni hii huku akionekana kushangazwa. Anajaribu kuinua mikono yake anagundua kuwa imefungwa na kamba kwenye kitanda alichokuwa amelalia.

Miguu yake miwili inaonekana kufungwa pamoja na alipojaribu kupiga kelele aligundua kuwa amefungwa kmba mdomoni iliyokuwa inazuia hasipige kelele. 

Alichoweza kufanya ni kuuunguruma akiashiria kuomba msaada kama kuna Mtu anaweza kuja kumsaidia.

NINI KITAENDELEA? …………… 

NI NANI HUYU? JE KWANINI ALIKUWA AMEFUNGWA? NI NANI ALIYEKUWA AMEMTEKA NYARA?

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 17
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Alijitahidi kujifungua kwa kutikisa mikono na miguu huku akiwa anaunguruma, lakini wapi kamba zilikuwa zimemshika ipasavyo na hasingeweza kufanya lolote.

Uwezi kuamini alikuwa ni Shaymaa ndio Mwanamke aliyefungwa katika kile chumba kilichoonekana kimejaa thamani ya kila aina na palionesha dhairi mwenye chumba alikuwa ni Mtu tajiri sana

Mlango ulifunguliwa na Mwanaume mmoja wa makamo aliyekuwa na ndevu nyingi aliyekuwa na asili ya kiarabu aliweza kuingia na kumtazama Shaymaa kisha akasogea kwenye kabati kubwa ambalo lilikuwa ukutani na kutoa kisu na kumsogelea Shaymaa. Kitendo cha yule Mzee kutoa kisu, kulizidi kumfanya Shaymaa kuogopa na kutetemeka akimuhofia Yule Baba.
                          *****
Hakeem akiwa na Irina pamja na Jack, aliwapeleka mpaka nyumbani kwa Irina, walifika na kuingia ndani.

Jack alionekana kuwa na furaha tofauti na siku zote, alionekana amechangamka huku akimkaribisha kila wakati Hakeem utafikiri yeye ndie mwenye nyumba.

“Nashindwa kukuelewa kabisa una nini wewe?” Irina alimuuliza Jack huku akiwa anamtazama. Jack alifurahi na kumvuta pembeni na kuzungumza nae “Hata Mimi sijajijua nina nini leo ila hali hii imenipata baada ya kukutana na yule kijana”

Jack aliongea huku akimuelekezea kwa Macho Hakeem aliyekuwa yupo bize na simu yake ya mkononi. Irina aligeuka kumtazama Hakeem kisha akamtazama Jack “Unataka kuniambia kuwa umempenda?” Irina alimuuliza na Jack hakuwa na chakumjibu zaidi ya kutabasam.

Irina alishangaa kumuona Mpenzi wake nae ameanza kupenda. “Hivi umemtazama vizuri lakini yule kijana? Unajua ni handsome wa kweli?” Jack aliongea na Irina alibaki kucheka tu 

“Dada samahani kidogo” Hakeem alitazama saa yake ndogo ya mkononi na kumuita” Hakeem akimuita Irina ambae alisogea karibu yake kwenda kumsikiliza.

“Nipo nje ya ratiba zangu, samahani naweza kuondoka tafadhali. Maana naona wewe na Rafiki yako hakuna tatizo tofauti na ulivyoniambia” “ooh samahani sana, ila amebadilika tu baada ya kukuona wewe, hata hivyo asante sana” Irina aliongea na kufungua pochi yake na kutoa kiasi cha pesa kama laki mbili na kumpatia

Hakeem alitazama zile pesa na kutabasam kabla ya kuzipokea “Naweza kukusindikiza” Jack aliingilia na Hakeem alimwambia kuwa hakuna shida ataitisha tax

“Basi nikusindikize mpaka hapo si unajua ukiitisha gari huku utapata tabu sana” 

Jack aliongea na Hakeem alimtazama Irina kama atamruhusu na Irina alitabasam tu kitua ambacho Hakeem hakuwa na hofu na kumwambia Jack kuwa tunaweza kwenda.

Wakati jack anatoka na Hakeem, Irina alibaki kushangazwa na hapo aligundua utanashati wa Hakeem. “nawezaje kumruhusu Jack amchukue Mwanaume mzuri kama Hakeem” Imekuaje Jack amebadilika ghafla wakati miaka yote amekuwa akichukia Wanaume? Hapana siitaji kukupenda Hapana siitaji” Irina aliongea mwenyewe baada ya kurudi chumbani kwake na kila alipojaribu kujituliza alijikuta mawazo ya Hakeem yanampitia na kumuona akilini Mwake

“Hapana Jak niachie Mpenzi wangu, ni Mimi ndie niyeanza kumjua kabla yako! Alafu kwanini nimefanya upuuzi wa kumpa nafasi Jack wakati nilipaswa kutumia fursa hile? Lakini Jack hana urembo wa kumvutia Mwanaume yoyote nitampata tu”

Irina aliongea mwenyewe huku akionekana kufuraishwa na kusahau kabisa kama Mume wake alikuwa yupo hospital anaumwa.
                           *****
Yule mzee wa Makamo alimsogelea Shaymaa na kukata kamba aliyokuwa amemfunga mdomoni na kumpa uhuru wa kuongea “Tafadhali usiniuwe, nakuomba usiniuwe tafadhali nakuomba”

Shaymaa aliongea kwa hofu ya hali ya juu akimuomba yule Baba hasimuue “Mimi ni Mtu Mwema kwako. Yule Mzee aliongea na kabla Shaymaa hajajibu kitu walisikia mlango unafunguliwa na aliingia Mama wa makamo ambae alikuwa amejitanda kichwa chake na alikuwa ameshika sahani iliyokuwa imejaa matunda.

Alifika na kumsogelea Shaymaa karibu na kumtazama pole sana Mwanangu “Mimi na Mume wangu ni Watu Wema sana” Yule Mama aliongea na Shaymaa lishindwa kuelewa hapo yupo wapi na amefikaje.

“Hakeem yupo wapi? Mzee aliuliza na Mama alionekana kustuka kidogo, nauliza Hakeem yupo wapi” Mzee aliongea tena kwa sauti ya ukali sauti ambayo ilimstua mpaka Shaymaa na Mzee akajistukia katika hilo.

Kijana Mmoja aliyekuwa amevalia suti aliingia baada ya kusikia sauti ya Mzee akipayuka “Samahani Mzee ni uzembe wangu” Yule kijana aliongea na Mzee alitazama saa yake na kumwambia “Saa 4 usiku hii, Mwanangu wa pekee yupo nje ya nyumba yangu? Umeweza kuruhusu kwenda kwenye michezo yake ya magari?”

Mzee aliongea na kumtaka yule Mtu aliyeonekana kuwa ni Mlinzi akamtafute Hakeem haraka.

“Samahani nilikuwa naomba mniruhusu nirudi kwetu” Shaymaa aliongea huku akionekana dhairi kuwa nahofia kuwepo hapo “Hapana hatuwezi kukuruhusu kwenda popote kwa maana uhai wako hupo mikononi mwetu” 
 Mzee aliongea na kumstua Shaymaa “Uhai? Kivipi Uhai wangu huwe mikononi mwenu?’ Shaymaa aliuliza na yule Mama alimjibu kwa kumuuliza swali “Inamaana haukumbuki kama ulitaka kujiuwa?”

Swali la Mama lilimfanya Shaymaa aweze kurejesha kumbukumbu zake ilikuaje mpaka akafika kwenye hiyo familia ambayo hakuweza kuijua kabla.

Baada ya kuandika barua na kuiacha kitandani, Shaymaa aliamua kutokomea sehemu ambayo alikuwa haijui hata kidogo. 

Akili yake ilimtuma akajiuwe ili kuupumzisha mwili na akili yake kutokana na mateso amabyo anakutana nayo. Akiwa njiani alianza kuona maumivu ya kichwa yakiwa yanampasua. Alikaa kwa dakika kadhaa kuugulia kichwa na kilipopungua aliingia katika daladala ambayo alikuwa hata ilikuwa inaenda wapi.

Lishuka sehemu na kuendelea kutembea taratibu huku mawazo akiwa juu ya aliyekuwa Mumewe. Alijua fika bila Abdul wala hasingekutana na mfadhaiko aliokuwa anaendelea kukutana nao

Ubaridi mkali ulikuwa unapiga huku upepo ukiwa unavuma na hapo aliweza kugundua kuwa alikuwa yupo pembezoni mwa bahari. Akiwa amekaa chini huku akiwa hajitambui na maumivu ya kichwa yakiwa yamerudi na safari hii kichwa kiliuma mapaka alishindwa hata kujitambua.

Alijikuta tu usingizi Umempitia na alipokurupuka kulikuwa kumekucha na ndipo alipoamua kujiingiza kwenye bahari taratibu ili kujiuwa kwa maji.

Mzee Mustapha Mfanya biashara Mkubwa ambaye upenda kufanya mazoezi kila mwishoni mwa juma upenda kukimbilia maene ya ufukweni akiwa na waliznzi wake na mtaalam wake wa mazoezi ya viungo.

Wakiwa wanaendelea na mazoezi yao walimuona Shaymaa akiingia kwenye maji taratibu. Mwanzoni walihisi ni Mtu tu yupo busy na mazoezi, lakini alizidi kuingia kwenye maji na hapo wakaanza kuwa makini nae kumtazama. Ghafla Shaymaa alianza kutapatapa na kuonekana akinywa maji na Walinzi wa Mzee Mustapha waliweza kwenda kumuokoa na kumpa huduma ya kwanza na wakati huo Shaymaa alikuwa tayari ameshakata pumzi.

Shaymaa aliweza kukumbuka mpaka pale alipoingia kwenye maji na kaunza kunywa maji na aliweza kuona aWatu wamekuja kumuokoa ila hakujua nini kiliendelea

“Ilikuaje mapaka ukataka kujiuwa” Mama alimuuliza na Mzee alimkatisha “naomba Binti yangu aandaliwe, abadilishwe nguo na apewe chumba chake. Mungu amemchukua Rayuu kwa kupitia maji lakini leo bahati ilioje nafsi ya Mwanangu imerudi kupitia Mwili wa Mtu Mwengine tena kupitia maji yale yale yaliyomchukua Rayuu wangu”

Mzee aliongea kwa furaha huku akimtazama mara mbili Shaymaa kama vile Mtu aliyekuwa haamini kumpata shaymaa.
                             ******

Jack aliweza kumpeleka Hakeem mpaka sehemu ambayo aliona inafaa yeye kufika. “Asante sana hapo panatosha” Hakeem aliongea na kutaka kuteremka gahfala simu yake ilikuwa inaita. Aliitoa mfukoni na kutazama, alionekana kustuka kidogo na kumtazama Jack kisha akapokea 

“Najua fika kama wewe ni mpenzi wa mbio za magari, lakini si kwa hatua hiyo ambayo unaishi” Mzee Mustapha aliongea na Hakeem hakuwa na chakusema zaidi ya kusema “Samahani DaDy” “Rayuu wetu amerudi tena, Rayuu amerudi akiwa mwenye tabasam tele tafadhali rudi nyumbani haraka”

Mzee Mustapha aliongea na kumstua Hakeem aliyeonekana kutaka kujua zaidi kuhusu kurudi kwa Rayuu “Inawezekana vipi Mtu aliyekufa mwaka mmoja uliopita akarejea leo?” Hakeem aliongea na kumstua Jack aliyeonekana kutamani kujua na japo alishindwa kufanya hivyo.
                         *****
Hakeem aliweza kurejea nyumbani kwao huku akiwa na shauku ya kutaka kujua kuhusu Dada yake kipenzi kureje nyumbani.

Alifika na kukuta kuna tafrija ndogo imeandaliwa na wakati anafika yeye na Rayuu ndio alikuwa anatolewa ndani huku akiwa amevalishwa gauni refu ambalo lilikuwa linasaidiwa na wadada wa kazi wa jumba la mzee Mustapha.

Inamaana wazee wangu wamezeeka kiasi hiki? Ilikuaje huyu Binti akawadanganya kuwa yeye ni Rayuu?” Hakeem aliongea na kusogea kwenye meza aliyokuwa amekaa Shaymaa na kumuinua “Unaweza kusema wewe ni nani? Tafadhali sema umetoka wapi wewe tapeli Mkubwa siyo Rayuu wewe!!” Hakeem aliongea na kupaza sauti kiasi ambacho Watu wote wa pale walipatwa na Mshangao.

Hakeem alitaka kumchapa kibao Shaymaa na ghafla alijikuta akipatwa na mshangao baada ya kumuona Shaymaa kwa karibu “Wewe ni………………!!” Alijikuta akipata na kigugumizi na kushindwa kuongea

NINI KITAENDELEA JE HAKEEM ANATAKA KUONGEA NINI? USIKOSE SEHEMU YA 18 
MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 18
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa Mustapha Muzhir. Katika jumba lake kubwa la kifahari aliagiza kuandaliwe tafrija fupi ya kumpokea Binti yake aliyekuwa ameshafariki mwaka mmoja ulopita.

Waliitwa wafanyakazi wote ambao walikuwa wanafanya kazi katika jumba la Mustapha na kutambulishwa kurudi kwa Rayuu ambae alirudi katika mazingira mengine kabisa.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu, Mimi na Mke wangu tulipatwa na udhuni baada ya kuondokewa na Mpendwa wetu kwa kipindi cha Mwaka Mmoja, lakini leo Mungu amejibu maombi yetu kwa kuamua kuturejeshea Rayuu wetu” Aliongea Mzee Mustapha huku akimuoneshsa haymaa aliyekuwa kama haelewi chochote.

“Duniani wawili wawili, unajua huyu Dada amefanana sana na Rayuu?” Mmoja wa wafanyakazi alimwambia mwenzie ambae alimuunga mkono “Lakini wametofautiana tabia, huyu anaonesha na mstaarabu tofauti na Rayuu mwenyewe” 

Mzee Mustapha aliamrisha kuandaliwe tafrija fupi ya kumpokea Rayuu, hivyo alitaka Shaymaa apendezeshwe na kutengenezwa kama Rayuu kwani alifurahi kukutana na Binti ambae anafanana na Mwanae

Shaymaa alivalishwa na kutengenezwa stayle ya nywele kama Rayuu na hapo ndio urembo wa Shaymaa uliweza kuonekana zaidi. Baada ya kutengenezwa. Mzee Mustapha alifurahi na kumpigia simu kijana wake ambae alimtaka arudi mara moja kwani Dada yake amerejea tena.

Hakeem alishangazwa na kauli hiyo ya Baba yake baada ya kuambiwa kuwa Rayuu amerejea nyumbani na alijiuliza inawezekana vipi kwa Mtu aliekufa kuweza kurejea Duniani?
                             *****
Hakeem hakutaka kabisa kusubiri kusimuliwa. Aliachana na Jack huku akiwa hataki kuonesha yeye ni Mtu wa aina gani, alifika mpaka sehemu aliyokuwa ameegesha gari yake ya kifahari ambayo upenda kuitumia kwenye michezo ya kukimbiza magari na kurejea nyumbani kwao.

Shauku yake kubwa ilikuwa ni kumuona Dada yake akiwa amerejea na aliona kuwa itakuwa maajabu kwa upande wake.

Hakeem aliweza kufika mpaka nyumbani na hakuitaji hata muda zaidi kuweza kutambua kuwa aliyekuwa mbele ya meza kuu hakuwa ni rayuu.

Alipiga hatua za hasira na kumsogelea Shaymaa, alifika na kumkunja kwa hasira na kumkoromea.

Hakeem alitaka kumchapa kibao Shaymaa na ghafla alijikuta akipatwa na mshangao baada ya kumuona Shaymaa kwa karibu “Wewe ni………………!!” Alijikuta akipata na kigugumizi na kushindwa kuongea huku akimtazama Shaymaa “Wewe ni nani? Wewe ni naniiiii?” Alijikuta akipaza sauti na kupiga kelele

“hivi wewe umechanganyikiwa” Mzee Mustapha alisimama na kuongea kwa ukali. “Haiwezekani anawezaje kufanana na Rayuu kiasi hiki?” Hakeem aliongea na Mustapha alimtazama na kufurahi huku akimuonesha siti akae “Upaswi kuhoji utukufu wa Mungu pindi anapoamua Kumtunuku Mja wake, Huyu si Rayuu bali ni Neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu”

Mzee Mustapha aliongea na Hakeem alizidi kumtazama Shaymaa ambae aliamini labda alijifananisha na Rayuu ili kutimiza malengo yake ambayo alitaka kuyafanya kwenye familia hiyo.
                              ********
Ilikuwa ngumu kuamini kama kweli Feisal anaweza kumpa talaka. Pili aliweza kuchana talaka huku akimuambia kuwahaweza kumuacha kwa sababu ya umalaya wake hivyo vyovyote itakavyokuwa ni lazamia ataendelea kubaki kuwa Mke wake

“Talaka ni maamuzi ya dhati ya ndani ya moyo, kutoka myoni nilishakuacha kwa talaka tatu, hizo karatasi ulizochana wewe ni uthibitisho wa kupeleka kwa wazazi wako. Sasa kwakuwa umechana mi sina haja ya kufanya hivyo tena. Ila nilikuoa huwe Mke wangu ambae utanijali, utanikarim na kunitunzia heshima yangu ya nje na ndani. Yote hayo yamekushinda na mbaya zaidi unanipiga na kunitukana matusi ya nguoni. Hivi wewe unadhani Mimi nilikuwa nashindwa kukupiga pindi ningeamua kufanya hivyo?”

Feisal aliongea na kutaka kuingia ndani lakini Pili alimfuata na kumuangukia huku akiwa analia “Tafdahli Feisal naomba usiniache, nitajirekebisha makosa yangu yote mbele yako, tafadhali nakuomba” Pili alimshika mguu Feisal huku akiwa analia.

Siku zote usijaribu kutaka kuyazoa maji pindi yanapokuwa yameshamwagika. Unapokewa Mke wa Mtu unapaswa kutambua mipaka yako, tambua kuwa wewe umeolewa. Kiburi na jeuri mbele ya Mume wako wala siyo kigezo kinachoweza kukufanya ukawa Mke Mwema.

Jiulize zipi sifa sahihi ambazo mumeo aliziona kwako mpka akaamua kukuchumbia hili huwe Mkewe? Acha kudanganyika na Watu wanaokutongoza na kukusifia huku wakionesha kuwa wanaweza kukupa kilicho bora zaidi kuliko upatacho kwa Mume wako. Ndugu yangu tafadhali usiadaike, tulia na Mume wako. Kama wanakwambia wewe ni mrembo waambie aliyetambua urembo wangu tayari ameshaniweka ndani hivyo nampenda, namuheshimu na kikubwa natambua thamani yake kama yeye alivyotambua yangu mpaka akaniweka ndani.

Feisal aliweza kutafakari kwa sekunde kadhaa akikumbuka matukio ya Mkewe jinsi alivyokuwa akimdharirisha na kumdhiaki akimuona yeye ni Mwanaume dhaifu sana mbele yake.

‘Hata siku moja haukuwahi kuonseha kuwa unajivunia kuolewa na Mwanaume kama Mimi. Kwa bahati mbaya, kitabu cha ndoa hakina hakina ufutio ambao unaweza kuyafuta yale yote uliyokosea kuandika tokea siku ya kwanza unapoingia katika ndoa. Hivyo basi unapaswa kuandika kwa taadhari ili usiwe unakosea kitabu hiki ambacho ukijaribu kufuta tu, unaweza kukuta unakichafua zaidi”

Feisal aliongea na kutoa mikono ya Pili katika Mguu wake na kumaanisha kuwa alichokuwa ameongea alikuwa amemaanisha wala hakuwa tena na sababu ya kuweza kutengua kauli yake na isitoshe alikuwa ameshaamua kumpa talaka tatu hivyo aliamu kumpa tu ushauri endapo atafanikiwa kuingia katika ndoa mpya basi anapaswa kutambua mipaka yake kama Mke wa Mtu kama Feisal alivyokuwa akitambua mipaka yake kama Mwanaume wa Mtu

Feisal alitoka ndani akiwa na talaka nyingine aliyokuwa ameiandika upya baada ya ile ya hawali kuchanwa na Pili “Kwakuwa nimekuacha talaka tatu, basi hata eda unapaswa kwenda kukaa kwenu na si hapa kama ambayvyo sheria za Dini zinavyotuongoza”

Pili alilia sana kuona kwa upuuzi wake ameweza kumpoteza Mume bora ambae alimpenda na kumsikiliza ila yeye mwenyewe tu aliutumia vibaya upendo aliopewa.

Waswahili wanasema “Usimpende Mtu na akajua kama unampenda” Hivi kwanini hiwe hivyo? Inamaana kama nakupenda sipaswi kukuonesha kuwa nakupenda? Yani nikupende alafu nijifiche kwa kuhofia kuwa utaanza kunitesa ukitambua kuwa nakupenda? Mtu anapokupenda na ukatambua kuwa anakupenda basi jitahidi kumlipa kwa mapenzi ya dhati
                             *******
Habari kubwa kwa jack na Irina ilikuwa ni kuhusu Hakeem, Jack alikuwa akimsifia Hakeem huku akisema kuwa hajawahi kukutana na Mwanaume mwenye mvuto kama Hakeem.

Jack aliongea na Irina alianza kumkumbuka Hakeem jinsi alivyokuwa akiendesha gari, jinsi alipojitambulisha ni Mpenzi wake kwa Jack na kuendelea “Lakini si unakumbuka kuwa nilikwambia yule ni shemeji yako?” Irina alimwambia Jack ambae alicheka sana na kumwambia “Mimi na wewe hatuna ubaya tunaweza ku share tu bila tatizo”

Jack aliongea huku akianza kumtomasa Irina ambae alikumbuka maneno makali ya Mama Jack aliyokuwa anamwambia kuhusu mchezo wao Mchafu waliokuwa wakiufanya na Jack 

“Hapana hatupaswi kuendelea kuwa hivi” Irina alimwambia Jack na kumtoa mkono wake “Mi najua kama umempenda sana Hakeem kutoka moyoni mwako” Aliongea huku akimtaza na Jack akajibu kwa ishara kukubali kuwa anampenda Hakeem “sasa kama kweli unampenda Hakeem, Mimi pia kwa sasa nampenda kwa dhati Mume wangu ila nahisi kama anataka kurudisha moyo wake kwa Shaymaa. Je hupo tayari nikuunganishe na Hakeem na wewe unisaidie ili tumuue Shaymaa”

Irina aliongea na kumfuraisha Jack aliyemuona kama kaongea kitu cha maana sana “Kama kweli unampenda Hakeem unapaswa kubadilika kuanzia sasa yani huwe Mwanamke kweli na siyo Mwanamke Mwanaume”

Irina aliongea na kuuliza kivipi? “Unapaswa upendeze, nikupodoe na uache kuvaa nguo za kiume na hili nitimize hayo ni lazima ukubali kufanya kazi yangu ya kumuua Shaymaa haraka hiwezekanavyo”
                               ******
Baada ya tafrija kuisha Shaymaa alipelekwa rasmi kwenye chumba ambacho kilikuwa ni cha Rayu.

“Mwenzako aikuwa anapenda sana kupiga piano na kuchora. Michoro yote hii uionayo, ni michoro ambayo Mwenzako alichora kwa mikono yake”

Mama yake na Rayuu aliongea huku akimuonesha na hapo Shaymaa aliweza kuangaza na kutazama kila upande.

Kilikuwa ni chumba kizuri kilichopambwa na kila aina ya mapambo. Nguo za kila aina zilizokuwa za thamani ya hali ya juu zilikuwa kwenye kabati na yingine zilitundikwa utafaikiri Rayuu alikuwa ameenda kazini au alikuwa anaoga na ameandaliwa nguo ili atoke.

“Rayuu alikufa maji kwa sababu ya mapenzi kama wewe ulivyotaka kujiua, je na wewe ulitaka kujiua kwa sababu ya mapenzi?” Mama yake Rayuu alimuuliza na Shaymaa aliinama na kuchezea vidole vyake na aliona aibu kuongea na badala yake alijikuta akitokwa na machozi

“Pole sana Mwanangu, bila shaka unafanana kila kitu na Rayuu, Mwenzako alifanya hivyo baada ya sisi kumkataa Mwanaume aliyekuwa amempenda, Je wewe nini kilikupata?” “Nitakwambia wakati Mwengine Mama” Shaymaa aliongea na kwa kitendo cha kumuita Mama, kilimfanya Mama Rayuu ajisikie fahari na kumkumbatia 

“Asante sana Rayuu bila shaka ni wewe” Mama Rayuu alimkumbatia kwa nguvu na kumwambia. Kisha alimuachia na kufungua kitambaa kimoja kilichokuwa kimefunika picha ya Rayuu aliyokuwa ameichora kwa mkono wake na hapo Shaymaa alibaki ameduwaa baada ya kuona kiasi fulani alikuwa amefanana na huyo Binti 

“kasoro yangu na yeye ni macho tu” Alijikuta akiongea Mwenyewe na ghafla walisikia mlango ukigongwa.

“Mama unaweza kutupisha nizungumze na Mdogo wangu?” Hakeem alimuomba Mama yake ambae alifurahi kusikia hivyo na kutoka kuwapisha ili wazungumza.

“Asante Mungu umejibu kwa wakati maombi yangu, naomba Hakeem amuoe huyu Binti maana ulifanya sahihi kumleta kwenye nyumba hii najua Mwanangu atampenda na kumjali”

Mama Rayyuu alinyoosha mikono juu na kumshukuru Mungu akiamini Mwanae atakuwa ameshaanzakumpenda Shaymaa ambae wao walikuwa wakimuita Rayuu

WEWE UNAFIKIRI NINI KITAENDA KUTOKEA? JACK AMEMPENDA HAKEEM NA RAFIKI YAKE YUPO TAYARI KUMSAIDIA KWA SHARTI LA KUMUUA SHAYMAA ……… FEISAL AMEMPA TALAKA MKEWE AKIWA NA MATUMAINI YA KUMTAFUTA SHAYMAA NA AMFUTE MACHOZI KWA KUFUNGA NAE NDOA ………… MAMA RAYUU ANAOMBA MUNGU MWANAE AMPENDE SHAYMAA NA IKIWEZEKANA AMUOE. UNADHANI NINI KITATOKEA??

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 19
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Ilimchukua sekunde kadhaa Hakeem akimtazama Shaymaa utafikiri Mtu aliyekuwa anamchunguza kama kuna tukio atakuwa amelifanya.

“Ilikuwa miaka mingapi kutengeneza muonekano huu ili tu uwashawishi Wazazi wangu na wakukaribishe nyumbani kwetu”

Hakeem alimuuliza Shaymaa aliyeonekana kushangazwa kidogo na swali lake na kuishia kumtazama “Najua mpaka umefanya mchezo huu basi kutakuwa na jambo ambalo umekusudia kulifanya, tafadhali niambie. Unajua nini kuhusu Dada yangu? Niambie wewe ni nani na kwanini umefanana na Rayuu?” Hakeem aliendelea kumuuliza Shaymaa ambae sasa alionekana kuchukizwa na maswali yake

“Sikiliza nikuambie Kaka, hata Mimi siitaji kukaa katika hii nyumba nilikuwa nahitaji ruksa tu ya Anko ili nirudi kwetu. Na kuhusu kufanana na Dada yako, Mimi nafikiri yeye ndio atakuwa amefanana na Mimi ila Mimi sijawahi kufanana na Mtu yoyote”

Shaymaa alimjibu Hakeem ambae alimpigia makofi na kumwambia kuwa “Safi sana, sijawahi kushindwa kumtambua Mtu kwa wakati, ila Mimi ndio Watu wanashindwa kunitambua kwa Wakati. Unaonesha wewe ni jeuri sana na kama umekuja hapa ukitegemea utapata huruma kutoka kwenye familia yangu basi nikwambie tu huna bahati hiyo na karibu kwenye vita”

Hakeem alikuwa ni kijana Mmoja hivi Mtanashati, aliyekuwa na majivuno kwa kiasi kukbwa sana. Aliongea kwa dharau na kuubamiza mlango na kutok nje.

“Mamaa! Inamana ulikuwa hapa mlangoni ukisikiliza naongea nini na huyu Binti?” Hakeem alimwambia Mama yake ambae alimkuta akiwa anasikiliza nini walikuwa wakiongea na Shaymaa

“Umenisikitisha sana Hakeem, hivi wewe unajikuta ni nani haswa? Unajiona wewe ni bora kuliko Watu wote? Unadhani utampata Mwanamke gani ambae atakubali kuolewa na wewe? Sssa nimekuchagulia huyu Mwanamke ili hawe Mke wako wa ndoa” Mama hakeem aliongea na kumfanya Mwanae acheke na kuuuliza “Yani Mimi nimuoe huyu changudoa?” Hakeem aliuliza na kupokea kibao kutoka kwa mama yake “Mshenzi Mkubwa wewe! Utake au usitake huyu ndio Mwanamke utakayemuoa”

Mama Hakeem aliongea na Hakeem aliondoka huku akiwa amechukia na Mama yake akimuagaizia maneno akimuona Mwanae ni Kijana Mwenye tabia mbaya sana.

Alitamani kuzuia macho yake kutotoa machozi tena, hakupenda kulia tena. Alitaka hawe Mwanamke mpya ambae atafungua ukurasa mpya baada ya kukutana na Watu waliompenda na kumtahamini lakini kwa kitendo cha Hakeem kumuita ni changudoa kilimuumiza sana

“Ni Mwanaume Mmoja tu katika Dunia hii ndio alifanikiwa kushuudia Mwili wangu, tena alifanya hivyo baada ya kufunga ndoa na Mimi, leo hii inawezekana vipi Mtu akaniita Changudoa”

Shaymaa aliweza kujiuliza kwa sauti kama ilivyotabia yake ya kupenda kuongea Mwenyewe na kwa kitendo cha kuruhusu maswali kichwani mwake, ilikuwa ni chanzo cha machozi kutiririka. Alifungua Dirisha na kutazama nje huku akianza kutafakari kwanini Hakeem aliweza kumwambia maneno yale.

Sauti ya mlango ilisikika Mtu akibisha hodi na Shaymaa alijitahidi kufuta machozi yake kwa haraka zaidi na ili hasigundulike kama alikuwa analia, lakini alikuwa amechelewa kufanya hivyo na Mama yake Hakeem alikuwa tayari ameshaingia chumbani

“Samahani sana, najisikia aibu kuwa Mama wa kijana ambae anashindwa kutambua thamani ya Wanawake wengine, wakati Mwengine nitajitahidi kumfundisha Mwanangu kuwa na tabia njema mble ya Wasichana” Mama Hakeem aliongea kwa utulivu sana huku akionekana kuwa na aibu mbele ya Shaymaa.

“Mbona hakuongea kitu chochote kibaya tulipokuwa humu ndani? Alihitaji kunijua tu wapi nilipotokea mi sidhani kama ni vibaya Mama” Shaymaa aligeuka na kujaribu kulazimisha tabasam

Kitendo cha Shaymaa kugeuka kulimfanya Mama Hakeem agundue kama Shaymaa alikuwa anatokwa na machozi na hapo alihisi Shaymaa kuumizwa na kauli za Hakeem ila tu anajaribu kuficha

“Hapana Mwanangu, najua kama utakuwa umesikia kauli ya Hakeem aliyoongea hapo nje ndio maana unalia, najua kama wewe ni muungwana, tafadhali niwie radhi Mimi mama yako. Nitajitahidi kumuepusha Hakeem kuwa karibu na wewe”

Mama Hakeem aliongea huku akimtazama Shaymaa aliyekuwa analazimisha tabasamu “Mama mimi silihi kwa sababu nina maumivu, ila nalia kwasababu macho yangu yamepigwa na upepo. Mara nyingi huwa napenda kuutazama upepo lakini kwa bahati mbaya upepo umekuwa ukiniliza. Hata hivyo nimempenda sana Hakeem, ni Mtu mzuri mwenye msimamo sana”

Shaymaa aliongea aliongea na kumstua Mama Hakeem aliyeonekana kufuraishwa na kauli ya Shaymaa na kujikuta akimkumbatia kwa nguvu kabla ya kumuachia “Rayuu akika wewe ni Malaika, hebu twende tukakae pale dirishani ili na Mimi nipigwe na upepo nilie kama wewe” Mama Hakeem aliongea na angalau Shaymaa alijikuta akifurahi kwa kiasi fulani.

Alijisikia furaha sana kukutana na Mama Mkarim na mwenye nidham ya hali ya juu. Lakini ukweli wa moyo wake, Shaymaa alitokea kumchukia sana Hakeem baada ya kumuita yeye Changudoa. 
Lakini kwa kitendo chake cha kusema anampenda Hakeem ambapo alisema hivyo ili tu kumfuraisha Mama Hakeem na kumfanya asijisikie vibaya kulimfanya Mama Hakeem aamini labda Shaymaa atakuwa ametokea kuvutiwa na kijana wake.
                             *****
Ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Hakeem na alijikuta kuchukizwa ghafla na uwepo wa Shaymaa nyumbani kwao “Huyu Binti anapaswa kuondoka hapa nyumbani”
Hakeem aliongea mwenyewe huku akiwa anapiga hatua kadhaa chumbani kwake utafikiri Mtu aliyekuwa amechanganyikiwa

“Kuna kitu anaitaji kufanya huyu si bure, inawezekana akawa amekuja hapa kutafauta faida zake binafsi. Alafu kwanini Mama ametokea kumuamini ghafla? Yani Mimi nimuoe yule mpuuzi yule? Siwez hata hiweje na lazima ataondoka tu hapa hata hiweje”

Aliongea mwenyewe na kutafuta mbinu ni vipi anaweza kumuondoa Rayuu wa uongo ambae aliamini kuwa aliamua kujifananisha na Marehemu Dada yake ili tu atomize malengo yake

“Baba anaweza kuwa upande wangu?” Hakeem aliongea Mwenyewe na kupinga mawazo yake baada ya kukumbuka jinsi alivyopaza sauti pale kwenye tafrija “Kama aliwahi kusema hakuna Mtu yoyote anayepaswa kutumia chumba cha Rayuu hata hiweje, lakini leo ameweza kutoa funguo na kutamka kuwa kuanzia leo chumba icho kiwa mali ya Rayuu mwengine”

Hakeem alijiuliza pasipo kupata majibu na kujikuta akichanganyikiwa na mwisho alijibwaga kitandani na kupiga yowe ambalo lilimstua mpaka Baba yake na akaingia chumbani kwake “Una nini wewe?” 

Mzee Mustapha aliongea kumuuliza kijana wake “Baba Mama ananikosea sana Mimi” 

Hakeem aliongea na kumfanya Mzee Mustapha asogee karibu na kumtuliza zaidi akitaka kujua “Mama anataka nimuoe huyu mpuuzi mliomuokota huko” Hakeem aliongea na kunyamazishwa na kibao kutoka kwa Baba yake aliyeonekana kuchukizwa na kauli ya kijana wake

                              ******
Alikuwa ni Mama fulani mwenye uwezo wa kumfanya Mtu ajisikie vyema kwa wakati. Alimfanya Shaymaa kama Binti yake na alijua fika kuwa Shaymaa hakuwa sawa ila alitaka kumfuraisha yeye hivyo walifurahi na walitoka nje na kukaa katika bustani wakiongea maneno machache

“Usije kumwambia Baba yako kama Hakeem aliongea vile mbele yako” Mama aliongea kwa upole huku akimtazama Shaymaa “Kwanini nifanye hivyo Mama? Sitaweza kuongea nae chochote alafu mbona Mimi sijachukia Mama”

“Unajua Baba yako kipenzi chake kilikuwa ni Rayuu, ndio maana hata kifo cha Rayuu kimemfanya kuwa na matatizo kidogo, ni mwaka umepita tokea Mwanae Rayuu amefariki na kipindi chote icho hatujawahi kuona tabasam lake. Ila cha ajabu baada ya ujio wako wewe humu ndani, nimemuona Mume wangu akitabasam tena”
“Kwanini mlinifunga kamba kama vile mlikuwa mmeniteka?” Shaymaa aliuliza swali ambalo Mama hakeem ilimchukua sekunde kadhaa kuweza kujibu. “Dokta alituambia kuwa ulikuwa na msongo wa mawazo hivyo tulikuwa tunapaswa kufanya jambo ambalo linaweza kukustua na kurejesha uwezo wako wa kufikiri upya. Tuliogopa usije ukatamani kujizur tena kwani Rayuu wetu alijiuwa kama wewe ulivyotaka kujiuwa katika maji na ulikuwa ni uzembe wetu kuweza kugundua hilo. Hatukupenda kukupoteza wewe Baada ya Baba yako kukupata katika mazingira ya kutatanisha”

Safari hii Mama Hakeem alishindwa kujizuia na kujikuta machozi yakitoka katika mboni za macho yake baada ya kumkumbuka Binti yake na jinsi alivyoweza kufa katika mazingira ambayo hawakuyatarajia 

“Kwanini Mama unalia? Tafdhali naomba usilie” Shaymaa alimwambia Mama Hakeem huku akiwa anamfuta machozi “Nadhani upepo utakuwa umepiga mboni za macho yangu ndio maana machozi yananitoka” Mama Hakeem aliongea na wote walijikuta wakifurahi

“Kwanini unataka kuipoteza furaha ya Mtoto mapema sana?” Mzee Mustapha alifika na kuanza kumfokea Mkewe 

“Kuna nini tena Mume wangu mbona nashindwa kukuelewa?” Mama Hakeem alimuuliza Mumewe huku akionekana kushangazwa kidogo

“Hakeem hana sifa ya kumuoa Rayuu, tafadhali uthithubutu kurudia tena ujinga huo. Hakuna hasiyejua kama kijana wetu ni mpuuzi. Anapenda kwenda club na muda wote anaangaika na wasichana huko lakini mbaya zaidi Hakeem siyo muoaji hivyo siwezi kuruhusu kumuona anaondoa furaha ya Binti yangu” Mzee Mustapha aliongea na kutaka kumchukua Shaymaa 

“Unampelaka wapi sasa Mtoto?” “Jamani wewe si umekaa nae mmasaa kibao na umeshindwa kufanya nilichokuagiza na badala yake unataka kumpeleka sehemu ambayo unataka ajutie”

Waliongea na Kubishana huku kila mmoja akimvuta Shaymaa akitaka hawe nae

Hakeema alifunua dirisha na kuona jinsi Wazazi wake wanavyomgombea Shaymaa “Inamaana huyu Binti ndio kawachanganya kiasi hiki?” Hakeem aliongea na kuonekana kuchukizwa na kitendo kile

Alifunga dirisha na kutafakari kidogo kabla ya kupata jibu ni vipi anaweza kumtoa Shaymaa nyumbani kwao

Alichukua simu yake na kuonekana akitafuta namba na kuipiga huku akiwa mwenye tabasam
                           *****
Irina akiwa amelala na Jack aliona simu yake ikiwa inaita aliinuka na kuipokea pasipo kutazama jina “Mr Handsome?” Irina alistuka na kuuliza baada ya kusikia sauti ya Hakeem

“Unajua kama leo nimekusaidia jambo lako, je na wewe hupo tayari unisaidie jambo langu?’ Hakeem alimuuliza na Irina aliamka na kwenda kuongea nae pembeni ili Jack asimsikie

“Nashindwaje kukusaidia Mr handsome?” Irina aliongea na kumfanya Hakeem afurahie kwa majibu hayo “Kuna msichana amevamia nyumbani kwetu naitaji tucheze mchezo ili tuwaaminishe vibaya Wazazi wangu”

Hakeem aliongea na Irina alishusha pumzi na kumjibu “Hilo ni jambo dogo sana wala usiwe na hofu Mr Handsome wewe sema jambo linguine”

NINI KITAENDELEA? JE IRINA ATAFANIKIWA KUMUONDOA SHAYMAA KWA KINA HAKEEM? TUKUTANE EPISODE YA 20 
MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 20
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Lilikuwa ni jambo la furaha kwa Irina kuzungumza na Hakeem kwa muda kama ule tena Hakeem akiwa anaomba msaada kutoka kwa Irina

Alishusha pumzi na kutabasam, huku akongea mwenyewe “huyu kijana atakuwa amenipenda tu, si bure” Aliongea na kugeuka ili arudi chumbani ila alipatwa na mstuko wa hali ya juu baada ya kumkuta Jack akiwa anamsikiliza

“Kwanini unafanya hivi lakini?” Irina alistuka na kumuuliza Jack huku akiwa anahema juu juu utafikiri Mtu aliyetoka kukimbizwa

Jack alimtazama pasipo kumjibu huku akipiga hatua taratibu na kumsogelea huku akionekana kuchukizwa na kumtazama kwa jicho fulani la hasira kiasi ambacho hata Irina mwenyewe alianza kumuogopa.

“Kutoka moyoni nilikuwa nimeshaamua kuwa napaswa kuwa Mwanamke kama walivyo Wanawake wengine. Na niliamua hivi baada ya kumjua Hakeem na hapo ndipo nilipojikuta Napata hisia kama Mwanamke. Lakini naona we hapo unapenda jinsi Mimi nikiwa Mumeo kuliko kuwa Rafiki yako”

Jack aliongea kwa upole lakini akionesha dhairi kuumizwa na kitendo cha kumkuta rafiki yake anaongea na simu usiku na Hakeem huku akionesha na yeye kumtamani

“Lakini Jack unapaswa kunisikiliza kwanza” “Sina muda huo Irina, unapaswa kutambua kuwa ufunguo wa Mimi kubadilika au kuendelea na tabia zangu unazo wewe”

Jack aliongea na kuondoka zake na Irina alimkimbilia Mpaka nje huku akimuomba asindoke “Unaenda wapi sasa? Unajua mimi ni………” Irina alinyamazishwa na kinywa cha Jack aliyeamua kumbusu kama vile wafanyavyo na Irina hakuwa na uwezo wa kumkataza badala yake walifanya hivyo kwa dakika kadhaa huku Mlinzi akiwa anaona kila kitu na kubaki amepigwa na butwaa baada ya kuona Wanawake wakiwa wanafanya mambo ya ajabu.

“Mungu wangu!!” Irina alistuka na kumtoa Jack kwenye mwili wake baada ya kumuona Mlinzi akiwa anawatazama kwa kitendo chao walichokuwa wakifanya

Lilikuwa ni jambo la aibu baada ya kufumwa na mlinzi wakaifanya utumbo wao. Jack aliondoka zake na Irina aliingia chumbani kwake huku akiwa na aibu ya hali ya juu

Aliingia mpaka ndani na kuanza kujutia kwa kile ambacho walichokuwa “kwanini lakini Jack umefanya hivi kwanini?” Irina aliongea mwenyewe na kujilaumu na kujikuta akikosa mpaka hamu ya kupata usingizi

Baada ya kutafakari kwa muda kidogo, alionekana kupata mashaka na Mlinzi wao “Yupo karibu sana na Abdul, hivi ni kweli anaweza kunitunzia siri hii?” Irina alijiuliza na kukosa majibu lakin baadae alipata wazo.

“Tafadhali naomba ingia ndani na upandishe ngazi uje chumbani kwangu” Irina alipiga simu kwa mlinzi na kumfanya Mlinzi astuke kidogo “Nipande ngazi na nije juu?” “Inamaana ujasikia au jeuri yako?” Irina alimjibu na Mlinzi alipandisha ngazi na kuelekea chumbani kwa Mke wa Boss wake.

“Maganga kuna mende chumbani kwangu nashindwa kulala, naomba umuondoe” Irina aliongea kwa sauti fulani ya madeko na Maganga hakuonesha kujali jambo hilo na badala yake aliingia chumbani kwenda kumtafuta Mende “Yupo wapi?” Aliuliza na ghafla Irina alipiga yowe na kuogopa na akamrukia Maganga ambae alitamani kumdaka lakini alishindwa na wote wakajikuta wakienda mpaka chini huku Irina akiwa amemkalia juu Maganga na kumtazama kwa jicho fulani la kumtamani.

                                 *****
“Asante sana Feisal, kosa langu kubwa ni kukupenda. Lakini kaa ukijua kuwa Hautaifurahia hiyo ndoa yako, yani uniache Mimi na ukamuoe Mwanamke niliyekufumania nae?” Pili aliongea sana na kuonekana kupania kuwa atadili na Shaymaa kwa maana bila yeye wala hasingeachika

Hakuwahi kuona mapungufu yake na siku zote alijiona kuwa yeye ni mkamilifu na katika swala la kuachwa na Feisal bado alimuona Shaymaa anahusika kwa jambo hilo

“Shaymaa hausiki na lolote, ila ningependa kukushauri nenda kajifunze jinsi ya kuishi na Mwanaume na utambue Mwanaume anapokupenda na kukupa nafasi haimaanishi kuwa yeye ni dhaifu”

Feisal aliongea na kuondoka zake na kumuacha Pili akiwa bado analia.
                               *****

Mzee Mustapha alifanikiwa kumshinda Mkewe kwa na kweli ilikuwa ni zamu yake kumchukua Shaymaa.

“Rayuu alikuwa anapenda sana kucheza piano na vyombo vingine vya mziki” Mzee Mustapha aliongea baada ya kuingia na Shaymaa kwenye chumba maalum cha kupiga vyombo vya Mziki 

“Najua itakuwa ngumu kuvaa viatu vya Rayuu ila naitaji angalau kuona unathubutu kufanya hivyo” Mzee Mustapaha aliongea huku akifunua kitambaa kilichokuwa kimefunika piano kubwa iliyokuwa kwenye chumba icho.
Alivuta kiti taratibu na kumruhusu Shaymaa aketi kabla ya kumshika mikono yake na kuanza kumfundisha jinsi ya kucheza piano

Shaymaa aliweza kucheza piano na kuhisi furaha kubwa moyoni mwake “Hakika huyu Mzee alikuwa akimpenda sana Binti yake”

Shaymaa aliongea Mwenyewe baada ya kuhisi upendo wa Baba aliokuwa anampa binti yake, sasa ameamua kumpa yeye “Wewe ni Mtoto wangu, Wewe ni zawadi kutoka kwa Mungu. Jisikie huru na jione kuwa wewe ni Mtoto wa Mustapha”

Mzee Mustapha aliongea huku akionesha kuvutiwa na aina ya uchezaji piano wa Shaymaa “Sijawhi kufikiri kama ungeweza kuwa mchezaji mzuri sana wa Piano kwa haraka kiasi icho” Shaymaa alishangazwa na kauli ya Mzee na kujikuta akifurahi kwa aina ya furaha aliyokuwa akimpa na kujiona kweli atakuwa amezaliwa upya
                             ******
“Nafikiri nitakuwa nimepoteza haki zangu zote za msingi wa kuwa Mtoto katika hii familia” Hakeem aliongea na kujinunisha baada ya kumuona mama yake ameingia chumbani mwake 

“Kila siku nakufundisha kuwa unapaswa kuwa Mkubwa tofauti na unavyojifikiria wewe” Mama yake aliongea na kumtuliza 

“Lakini Mama mnapaswa kutambua huyu Binti siyo Mjinga hata kidogo” Hakeem aliongea kumtilia mashaka na Mama yake alionekana akiwa kimya anatafakari

“Alipokufa Rayuu, tulizani kuwa sasa kile kisiki kilichokuwa kinatuzuia kitakuwa kimeondoka kumbe ni tofauti. Baba yako anaweza kumfanya huyu Binti kuwa ndio kila kitu kama ujaamua kustuka, lakini wewe ukimuoa huyu Binti huoni kama utakuwa umeupitia denge utajiri” Mama aliongea na kumfanya Hakeem hasikitike

“Nilijua tu kama upendo wako kwa yule Binti utakuwa na sababu, lakini Mimi wala sijavutiwa nae kuwa Mke wangu ila naitaji aondoke humu ndani”

Mama yake na Hakeem alikuwa na maana yake kumtaka kijana wake afunge ndoa na Shaymaa kwani alijua fika kuwa Mzee atakuwa amechanganyikiwa nae na hivyo anaweza kumpa urithi wote

Ulikuwa ni ubishi Mkubwa baina ya Mama na Hakeem, huku Mama akimtaka Mwanae kufunga pingu za maisha na Shaymaa na Hakeem akisema kuwa hawezi kumuoa Shaymaa 

“Unataka na huyu nimuue kama nilivyomuua Rayuu” Mama aliuliza kwa msisitizo na kumfanya Hakeem astuke baada ya kauli hiyo “Inamaana Mama wewe hapo ndio umemuua Rayuu au alikufa kwa maji?” Hakeem aliuliza na Mama yake alikuwa tofauti na siku zote

“Nilimuua Rayuu ili uje urithi hizi mali kama Mtoto wa kufikia, lakini naona ni jinsi gani haujitambui na utaiacha hii fursa ikupite. Kama utaendelea kugoma kumuoa basi kaa ukijua hatokuwa na Maisha hapa ndani na utanipa dhambi ya kuuwa Mwanamke mwengine ambae sikupanga kumuondoa Duniani

NINI KITAENDELEA?? MAMA HAKEEM ANATAKA KUMUUA MWANAMKE GANI MWENGINE?

Post a Comment

Previous Post Next Post