🔐 MAUMIVU YA NDOA (11----15) 😭😭😭😭

SEHEMU YA 11

“Siwezi kumlaumu sana, Inawezekana yule Mwanamke alimpenda zaidi kuliko hata nilivyompenda Mimi”

Shaymaa aliongea kwa upole na utulivu wa hali ya juu baada ya kutoka out na Feisal. 

“Pole sana Shaymaa, unajua wakati Mwengine upaswi kujilaumu kwa kila jambo. Huwezi jua Mungu amekuepusha nini katika ndoa yako. Jambo kubwa ambalo unapaswa kujifunza ni Mapenzi yanapokwisha wala usitumie mabavu kuyalazimisha, ndio maana Marehemu Shaaban Robat aliwahi kuandika kwenye moja ya tungo zake “Penzi ni majani makavu, ukanywagapo ulia, hayaitaji mabavu bali utulivu kutulia”

Feisal aliongea na kwa kiasi fulani maneno yake yaliweza kumuingia Shaymaa aliyeonekana kutabasam

“Feisal wala haujabadilika Mpenzi wangu, kiukweli nimekumbuka sana maneno yako matamu na utani wa mchumba uliokuwa ukinitaniaga. Bila shaka Mwanamke uliyemuoa atakuwa anafaidi mno”

Shaymaa aliongea na kumfanya Feisal apaliwe na kinywaji na haraka Shaymaa, alimpa pole huku akimuuliza kama yupo sawa. “Bado haujabadilika Shaymaa, nakumbuka sana pindi ulipokuwa unanijali, pindi Mama alipokuwa ananinyima chakula nawe ulikuwa unaniibia chakula unanipa. Bila shaka Mumeo alikuwa anafaidi sana ukarimu wako”

Feisal alimrudishia Shaymaa ambaye alionekana kunyongea baada ya kauli hiyo na taratibu alianza kuchezea vidole vyake na kujaribu kujizuie walau asidondoshe chozi mbele ya Feisal.

“Feisal mimi sijawahi kuwa na bahati na ndoa yangu. Mume wangu hakuwahi kuona thamani yangu, sijawahi kufurahia ndoa yangu zaidi ya zile siku za mwanzoni” 

Shaymaa aliongea na Feisal alimtazama na kutabasam wala hakuonesha kumuonea huruma kwa kile ambacho alikizungumza Shaymaa.

“Umejifunza nini kutokana na icho ulichopitia wewe?” Feisal alimuuliza swali Shaymaa ambaye alionekana kutafakari na kumjibu “Nimejifunza kuwa wanaume wote Mwalimu wenu ni Mmoja, katika maisha yangu, sidhani kama nitakuja kufungua moyo wangu na kumkabidhi kiumbe yoyote anayoitwa Mwanaume”

Feisal alimtazama na kutabasam kisha akamwambia “Watu wengi huwa wanafanya makosa hayo ya kuhukumu Watu wengine kupitia makosa ya Mtu mwengine”

Shaymaa alitulia kwa makini na kumsikiliza Feisal na macho yao yalikutana na Feisal aliamua kummiminia juice ya matunda iliyokuwa kwenye box na kumpa anywe kidogo 

“Katika mapenzi kila Mtu ana matatizo yake, Wakati wewe unapoona Wanaume ni Watu wabaya mno, basi kuna Wanaume pia wameumizwa na wanawake kama wenzio nao pia wanaona Wanawake ni Watu wabaya huku wakiamini kuwa Mwalimu wa wanawake ni kipofu. Kifupi jifunze kumuhukumu Mtu kutokana na makosa yake. Mtu yoyote pasipo kujali jinsia yake anaweza kuwa Mzuri ama mbaya”

Ilikuwa ni muda mfupi tokea wamekutana lakini iliwatosha kubadilishana mawazo na kujaribu kushauriana “Feisal natamani hata ungekuwa Abdul” Shaymaa aliongea na kumfanya Abdul afurahi na kumtazama “Kuolewa na mchekeshaji haimaanishi kuwa utakuwa na furaha ya kudumu. Unaweza kuniona Mimi ni sahihi kwako kumbe pengine ndio ningekuwa chachu ya kukufanya uhumie zaidi”

Feisal aliongea na kuzidi kumfanya Shaymaa ajisikie furaha “Kiukweli nimefurahi sana Feisal, ulikuwa wapi siku zote, tafadhali Usikae mbali na mimi hata kidogo, haswa katika kipindi hiki kigumu ambacho nipo nacho”
                           ********
Abdu alimtazama Irina aliyeshindwa kupokea simu na kuikata na kumuuliza “Kwanini unakata simu?” Shaymaa alishusha pumzi na kumtazama “Abdul kwanini unapenda tugombane? “Inamaana sina haki ya kuuliza kama mumeo?” “Jack ndie aliyenipigia, namjua tabia zake hivyo sitaki kuongea nae, najua anataka tuongee kuhusu wewe na sipendi nikukwaze” 

Irina aliongea na Abdul alimuelewa kwa kiasi fulani na aliona haitakuwa jambo jema kugombana na Mkewe kila wakati.

Simu ya Irina illita tena na Jack ndie aliyekuwa anapiga kama kawaida yake “Pokea na niongee nae, nimuombe Msamaha kwa kile kilichotokea” 

Abdul aliongea na Irina alifurahi kusikia hivyo na kupokea simu ya Jack na alifanya kama ambavyo Mumewe alivyomwambia “Samahani sana kwa kile kilichotokea leo” Abdul aliongea na Jack hakuwa na kinyongo na kumwambia kuwa anapaswa kuwa Mume siyo bwana wa Irina.

Baada ya kuongea na Jack, Abdul alimtama mkewe na kumuuliza “Bila shaka umefurahi” “nimefurahi Mume wangu na umeonesha ni jinsi gani ulivyo Mwanaume kamili”

“Sawa nafurahi kusikia hivyo Mke wangu. Umenipikia nini leo?” Abdul alimuulia Irina ambae wala hakupepesa macho na alimjibu hawezi kupika “Alafu Abdu mimi nishamaliza kula fungate na wewe hivyo kaa ukijua kuwa naitaji kuingia ofisini, naomba utafute dada wa kazi”

Irina aliongea na Abdul alishnagazwa kidogo na kauli za Mkewe kuwa hawezi kupika na kumtaka watafute Dada wa kazi. Alikumbuka jinsi Shaymaa alivyokuwa fundi wa kupika na mara kadhaa alikuwa akimsubiri mpaka usiku wa manane ili wale pamoja.

“Sawa jiandae ili tutoke out” Abdul aliongea na Irina alifurahi na kutafuta kigauni fulani cha kutokea usiku ambacho kilikuwa kinaonesha sehemu kubwa ya mwili wake

“Mke wangu!! Yani unataka tutoke ukiwa umevaa nusu uchi?” Abdul alishangaa na Irina alionekana kuchukizwa na kususa huku akimuona Mumewe kuwa na mambo ya ajabu ambayo yeye hakupendezwa nayo

“Nenda kale mimi siwezi kwenda” Irina aliongea na Abdul alimuomba msamaha Mkewe na kulidhia watoke akiwa na kigauni ambacho amekipenda Irina.
                              *****

Ilikuwa ni siku nzuri sana kwa Shaymaa kwani alipokuwa na Feisal waliongea na kufurahi na Shaymaa alimsimulia zaidi jinsi alipojitahidi kuinusuru ndoa yake lakini alikutana na vitu ambavyo kiukweli viliweza kuvunja moyo wake.

Shaymaa alipokuwa anamsimulia Feysal matatizo ya Abdul, alishindwa kujizuia na kujikuta akilia. 

Feisal alimtazama na kumuonea huruma, alijikuta akimvuta na kumlaza begani kwake na kumbembeleza.

Ghafla shaymaa alimwagiwa kinywaji usoni na Mwanamke aliyeonekana kuchukizwa baada ya kuwakuta Shaymaa na Feisal wapo katika pozi ambalo hakupendezwa nalo “Malaya mkubwa wewe mwizi wa wanaume za Watu” Yule Binti alitukana na wakati huo wateja wote walikuwa wameacha kufanya kila kitu na waligeuka kuwatazama. 

Abdul na Irina pia walikuwa wameingia katika mgahawa huo kuja kupata chakula cha usiku na walistuka baada ya kumuona Shaymaa akitukanwa matusi ya nguoni.
Irina alimtazama Shaymaa na kuangua kicheko “Inamaana X wako amefikia hatua ya kuiba wanaume wa Watu?” Irina alimuuliza Abdul huku akiwa anamkumbatia zaidi. 

Abdula hakupendezwa na kitendo ambacho Shaymaa anamfanyiwa na alijikuta akimtazama jicho kali Feisal aliyekuwa amekaa chini huku akiruhusu yule Mwanamke kumkashifu Shaymaa.

Shaymaa alijisikia vibaya sana huku akiwa amejiinamia kwa aibu pasipo kuwa na jambo lolote la kujitetea. Aligeuka na kumtazama Feysal na kumwambia “Fey jaribu kuongea nae basi na umwambie mimi ni nani kwako?”

Lakini Feisal hakuwa na majibu yoyote badala yake aliendelea kukaa kimya utafikiri alikuwa hasikii nini ambacho Shaymaa alikuwa anafanyiwa. 

Shaymaa aliona ni bora ainuke na kuondoka lakini alitulizwa chini na yule msichana aliyekuwa akimtukana na kumtuhumu kumuibia Mumewe ambae hakujulikana huyo Mumewe kama ni Feisal au lah! “Kaa chini Malaya Mkubwa wewe” Yule Binti aliongea na kutaka kumchapa kibao lakini ghafla alidakwa mkono na kugeuka kumtazama ni nani aliyemdaka huku Shaymaa akiwa ameinama na kukinga mikono usoni ili kuzuia hasiumizwe usoni.

“Hivi unajisikiaje kumdhalilisha Mwanamke Mwenzako mbele ya watu wengi? Unapaswa kumlaumu Mumeo kwa maana yeye ndie aliyepeswa kumwambia Shaymaa kuwa Mimi ni Mume wa Mtu”

Hakuwa mwengine bali alikuwa ni Abdul ambae alifika na kumdaka mkono yule Binti na kuongea huku akiwa amemkazia macho.

Shaymaa alistuka na kujikuta akiita Abdul? Feisal nae aliweza kutambua kuwa huyo ndie aliyekuwa Mume wa Shaymaa baada ya kusikia Shaymaa ametamka jina lake.

“Ni haibu kwa Mwanamke uliyepewa talaka kwa tabia chafu alafu unaanza kuiba Wanaume wa Watu badala ya kujituliza nyumbani na kujirekebisha tabia zako chafu zilizo kufanya upewe talaka”

Irina alipiga hatua kimadaha huku viatu vyake virefu alivyokuwa amevaa vikiwa vinasikika jinsi alivyokuwa anajongea na kuongea kauli hizo chafu zilizomuumiza zaidi Shaymaa……………

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 12
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Tabasam ndio silaha kubwa ya kumuangamiza Adui yako pindi unapomuona amekuzidi kwa mbinu zote na hauna njia nyingine ya kuweza kupambana nae.

Shaymaa alirusha nywele zake nyingi zilizokuwa zimejaa usoni mwake kisha akamtazama Irina na kutabasam. Na alifanya hivyo makusudi ili kumuumiza Irina kwasababu alijua fika kwa kuuonesha kuwa anaumizwa na maneno yake kutamfanya amuumize zaidi.

“Siku zote Muungwana akivuliwa nguo uchutama ila ni mpuuzi pekee ambae uvimba kichwa na kusimama. Labda tu niwaambie sijaumizwa hata kidogo na maneno yenu ya kipuuzi ila najaribu kuepusha shari katika biashara ya watu na sitohitaji kugombana na Wapuuzi ili nami nionekane ni Mpuuzi” Shaymaa hakutaka kuwa mnyonge mbele ya Abdul kwani alitaka kutumia nafsi hiyo kumchoma adui yake

“Usingekuwa Mpuuzi wala usingeachika katika ndoa yako na kuiba Wanaume wa watu” Irina alijibu na safari hii alionekana amepaniki kidogo 

Shaymaa alicheka kidogo huku akisikitika na kumtazama Irina “Kicheko chako kinamaanisha nini lakini? Inamaana unajiona bora mbele yetu au unajionaje?” Yule Binti mwengine aliuliza na kumsogelea Shaymaa “Pili inatosha” Feysal alifungua kinywa na kuongea kwa ukali kiasi ambacho hata Pili mwenyewe alishangaa. 

“Unawezaje kunikoromea kiasi icho? Inamaana Huyu Malaya wako ndio anayekupa kiburi si ndio?” Pili aliongea na alijikuta akipokea kibao takatifu kutoka kwa Abdul “Nilishakwambia chunga kauli zako pindi unapoongea na Mwanamke Mwenzako lakini kumbe huna Adabu?” Abdul aliongea kumkanya Pili baada ya kumtandika kibao cha shavu na Pili alishindwa kuvumilia na alianza kumtukana Abdul huku akitaka kumpiga na Feisal alimzuia na kusababisha vulugu kubwa ambayo walinzi waeneo lile iliwabidi kuingilia na kumkamata Pili na kumtoa nje

Feisal alitulia tuli kama kawaida yake, hakujaribu kufanya chochote zaidi ya kukaa mbele ya Shaymaa kumkinga kwa lolote isije Irina au Pili kutuumia fursa hiyo ili kumuumiza.

Baada ya pili kufanya vulugu, na kutolewa nje Feisal alifungua pochi yake na kutoa kiasi cha pesa Shaymaa “tafadhali naomba urejee nyumbani, huyu ndio Mwanamke niliyemuoa mwaka Mmoja uliopita,” Feisal aliongea haraka haraka Huku akiwa amenyoosha mkono kumpatia pesa Shaymaa aliyekuwa muda wote ameganda akimtazama. Hakuwa na jinsi ilimbidi tu apokee zile pesa mana hakuwa na njia nyngine ambayo ingeweza kumrudisha nyumbani

“Muwindaji mzuri ni yule anayekwenda porini na kuwinda Mnyama ambaye ana matarajio katika swala zima la kitoweo. Kama unahisi mnyama aliyekuwa mbele yako huna matarajio nae, na wala hajaonesha dalili zozote za kutaka kukujeruhi, tafadhari usitumie risasi yako kumuwinda mnyama huyu”

Abdul alimshika mkono Feisal aliekuwa anaondoka baada ya kumpa pesa Shaymaa “Mwanaume huwa haongei mafumbo, mambo hayo tuwaachie hawa, Mimi nafikiri unapaswa kuwa muwazi” Feisal alimjibu Abdul aliyeonekana kutopendezwa na Majibu ya Feisal lakini alipiga moyo konde na kumjibu

“Kama umekutana na Mwanamke Mwelevu na mwenye sifa ya kuwa Mke wa Mtu, tafadhali usipende kumtumia ki ngono, Shyamaa si haina ya Mwanamke wa kutukanwa na Mwanamke wako ni vyema ukamuheshimu kuliko kumpotezea muda wake” Abdul aliongea kwa upole huku kauli zake zikimkwaza Mkewe na kumfuraisha Shaymaa kwa kiasi fulani aliyekuwa akimtazama Irina kwa jicho fulani la kebehi

“Kabla ujamnyooshea kidole mwenye kibanzi jichoni, unapaswa kuondoa bolt jichoni kwako. Nafikiri ungetambua hayo mapema, sidhani kama leo Shaymaa angekumbana na kadhia hii anayokutana nayo” Feisal alimjibu Abdul na kuondoka zake akimuacha Abdul akiwa kwenye Taharuki

“Samahani sana Shaymaa kwa kauli ambazo Mke wangu amekwambia, Irina umemkosea sana Shaymaa naomba umuomba samahani” Abdul alimwambia Shaymaa na kumfanya Irina astuke “Heti nini? Abdul tafadhali naomba usinikosee adabu na kama unaniona Mimi napaswa kumuomba msamaha huyu kinyago wako basi baki nae na mpate chakula cha usiku” Irina aliongea na kisha akamsogelea Shaymaa na kumtazama kwa dharau

“Kaa mbali na Mume wangu, na ukiendelea kumfuatili basi kaa ukijua nitakuja kukufanya kitu kibaya sana” Shaymaa alimtazama na kuguna kabla ya kumjibu “Siku zote Mbwa uwabwekea watu hasiowajua, hivyo wala sikaraishwi na kelele za Mbwa hasiye nijua” “Inamaana Mimi ni Mbwa?” Irina aliuliza na hakushindwa kusubiri majibu na badala yake alimvaa Shaymaa mpaka chini na kuanza kupigana nae na Abdul kwa kushirikiana na Wateja wengine waliweza kuwaamulia.

Abdul alimchukua Irina na watu walimzonga Shaymaa huku kila mmoja akisema lake na wengi wao walimuona Shaymaa kama Mwizi wa Wanaume wa watu “Mdada mrembo kama wewe unashindwa kweli kutulia na ukapata Mume akuoe?” Mama Mmoja alimwambia Shaymaa ambae hakutaka hata kumjibu na badala yake aliamua kuondoka zake
                               *****

Shaymaa akiwa kwenye gari aliyokodi akirudi nyumbani alijikuta Mwenye mawazo mengi sana akitafakari yaliyomtokea usiku huo aliokuwa ametoka out na Feisal “Kwanini Feisal alikaa kimya bila kunisaidia chochote? Inamaana Feisal atakuwa anapitia magumu kwenye ndoa yake?” Shaymaa alijiuliza Mwenyewe pasipo kupata majibu.

“Tumeshafika Dada” Dereva wa tax aliongea baada ya kufika eneo ambalo Shaymaa alitaka afikishwe
                          *****
Inawezekana ukawa unapitia mambo magumu sana katika maisha yako. Inawezekana ukajiona una mkosi au una bahati mbaya sana katika hii dunia kiasi ambacho ukafikia mpaka kukufuru Mungu.

Basi utakuwa unakosea sana, kuna watu wengi wanapitia matatizo ambayo kama unapata nafasi kuwa nao karibu au wanakusimulia basi unaweza hata kujiona wewe huna matatizo kabisa.

Kama ambavyo Shamaa alivyokuwa anafikiri kuhusu Feisal kuhusu ndoa yake uwenda anapitia shida kwenye ndoa hiyo basi ni kweli. 

Nyumbani kwa Feisal kulikuwa ni vulugu tupu, Pili aikuwa akibwata huku akitupa vitu na kufanya uharibifu ndani “Malaya mkubwa wewe, usiyeridhika na Mkeo unafanya kazi ya kuangaika na Machangudoa, wewe si ulisingizia Baba ndie aliyekupigia simu?’ Pili alikuwa akiongea na kuvunja vitu ovyo 

“Mke Wangu, mbona unapenda kunidharau? Alafu kwanini unapenda kuaribu vitu ambavyo tunatumia pesa nyingi kuvinunua? Jaribu kuwa Muelewa basi, yule ni Binamu yangu na Baba aliniita ili kwenda kuongea nae na kama hauniamini basi chukua simu hii na umpigie” 

Feisal aliongea na kumpa Pili simu yake aina ya iPhone na Pili aliichukua na kuibamiza chini “inamaana wewe na Baba yako mnashirikiana kufanya uzinzi si ndio? Basi nyinyi familia nzima ni wanzinzi wakubwa $%&*&^”

Pili aliongea na kutukana matusi ya nguoni akimtukana mumewe na familia yake na Feisal alikaa kimya pasipo kuongea jambo lolote. Mara nyingi amekuwa akikaa kimya pindi Mkewe anapokuwa anabwata bila sababu ya msingi kwani anapofanya hivyo ndio hasira za Mkewe zinapungua lakini pindi anapokuwa anamjibu basi Mkewe anazidi kuwa mkali na mara kadhaa Feisal amekuwa akipigwa na Mkewe

Pili aliongea na alipomuona Feisal amekaa kimya bila kumjibu chochotea alimsogelea na kuanza kumshushia kichapo Mumewe “Nisamehe Mke wangu tafadhali naomba unisamehe”

Masikini Feisal alikuwa kama Mtoto mdogo mbele ya Mkewe. Upole wake ulimponza na hakuweza kupata heshima anayostaili kama Mume mbele ya Mke wake.
                        ****
“Simtaki nasema aondoke nyumbani kwangu” Shaymaa alipofika nyumbani kabla hajafungua mlango tu alisikia sauti ya kelele ikitoka ndani na Shangazi alikuwa anagombana na Mjomba “Shaymaa hawezi kuondoka hapa nyumbani hata hiweje” Mjoma aliongea na baada ya hapo sauti ya vyomboa vilisikika na vikianguka na walionekana kama walikuwa wanagombana

Mlango wa mbele ulikuwa wazi na Shaymaa aliweza kuingia ndani na kuingia chumbani kwake. Huku akiwa anasikiliza kelele za Mjomba na Shangazi wakiwa wanagombana.

“Unatembea na mpwa wako, ndio mana mimi sina kauli kwako. Nipige nakwambia mpaka uniue kwa maana Mimi sina thamani lakini ukiniacha hai basi Mtaa mzima utajua kama wewe unatembea na Mpwa wako”

Maneno ya Shangazi yalizid kumchefua Mjomba na alishindwa kujizuia na kujikuta akimpiga kipigo cha maana na Shangazi alikuwa akilia kama Mtoto Mdogo.

“Mzee tafadhali fungua mlango” Mmoja kati ya wapangaji wao alisikika akigonga mlango kabla ya wenzake kuungana na kumgongea mjomba ambae aliamua kufunga.

“Mzee vipi mbona mnapigana sahizi? Mnatufunza nini sisi Watoto wenu?’ “Huyu Malaya anatembea na Mpwa wake, ana laana huyu Mzee” Shangazi alipaza sauti na Watu wote waliokuwa pale walipatwa na aibu.
Shaymaa akiwa chumbani kwake aliweza kusikia kila kitu na kujisikia vibaya sana kutokana na tuhuma ambazo alikuwa anapewa Mjomba wake na Shangazi 

“Samahani sana Mjomba, kwa maamuzi haya ambayo nimeamua kuyachukua. Samahani sana Feisal nimeshindwa kutambua nini kinachokusibu kwenye ndoa yako”

Shaymaa aliongea mwenyewe huku akiwa analia kisha akachukua peni na karatasi na kuanza kuandika 

Mjomba!! Nakupenda sana, najua ni jinsi gan unanipenda na hakutamani hata kidogo Mpwa wako nipitie kwenye matatizo. 

Lakini Mjomba Mimi Mpwa wako nimeamua kuchukua maamuzi magumu sana. Sitapenda kuona Mjomba wangu unafedheeka na mimi nikishuudia.

Najua utaumizwa sana na maamuzi yangu lakini niseme tu Mjomba asante sana kwa kila jambo. Tafadhali usimuache Shangazi na usipende sana kumpiga. Jaribu kumuelekeza na atakuelewa tu………………

Shaymaa aliendelea kuandika huku akiwa anajizuia kilio chake kisiweze kusikika na watu waliokuwa nje waliokuwa akisuluisha ugomvi wa Mjomba na Mkewe.

Shaymaa aliandika barua na kuikunja ipasavyo kisha akanyoosha mikono yake juu na kumuomba Mungu wake msamaha na kumshukuru kwa kila jambo “Asante sana Mungu wangu, najua ni kosa hiki ninachotaka kukifanya, lakini nipo radhi kuja kutumikia adhabu nikiwa kwako kuliko kuadhibiwa na Mwanadamu mwezangu”

NINI KITAENDELEA? UKIPATA NAFASI YA KUONGEA NA SHAYMAA KWA MUDA HUU UNGEMWAMBIA MANENO GANI? VIPI KUHUSU ABDUL NA MKEWE 

NO MONEY NO SLEEP ... NO LOVE NO LIFE ....  
MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 13
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Msongo wa mawazo ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku.
Mtu hupata msongo wa mawazo pale anaposhindwa au kukosa namna ya kukabiliana na jambo linalomsumbua.
 
Shaymaa alikuwa ni Mtu aliyepatwa na Msongo wa Mawazo na ilikuwa ngumu kwa akili yake kuweza kufanya upembuzi yakinifu na kitu pekee alichoweza kuamua katika ubongo wake ni kujiua tu.

Masikini Shaymaa aliandika barua yake vyema na kuikunja na kuiweka sehemu ambayo aliona inaweza kuonekana kwa haraka kisha akatulia na kuomba Mungu sana amsamehe kwa kile alichokuwa anataka kukifanya.
                       ****
Katika nyumba ya Abdul mambo yalikuwa yamewaka moto, Irina alichukia baada ya Abdul kuweza kumsaidia Shaymaa na kumwambia amuombe Radhi “Inaonesha ni jinsi gani wewe bado unampenda Shaymaa, sasa niambie moja kama umenichoka naomba unipe talaka yangu” Irina aliongea na kumfanya Abdul astuke na kumpigia magoti Mkewe “Tafadhali naomba tusifikie huko, alafu Mimi nilimsaidia baada ya kuona anadhalilishwa na yule Binti”

“Sasa kama anadhalilishwa wewe ilikuwa inakuhusu nini? Mwanamke wako ni Mwizi wa Wanaume wa Watu ulitaka aachiwe tu?” Irina alifoka na Abdul alikuwa Mdogo kama kidonge huku akikubali makosa yote kuwa ni yake na akimuahidi Mkewe kuwa hatorudia tena kuwa karibu na Shaymaa wala kumsaidia kwa jambo lolote lile.

Alingea bila kujua kama mwenzake alishakata tamaa ya kuwepo katika ulimwengu huu baada ya kuona mambo kibao yanamuelemea
                           *****
Asubuhi na mapema Mjomba aliamka na kama ilivyo kawaida yake huwa anapenda kabla ya kuondoka hawe ameonana na Shaymaa. 

Alifika mpka katika mlango wa Shaymaa na kutaka kubisha hodi lakini alisita kufanya hivyo akihofia kumchosha kumuamsha kutoka usingizini “inawezekana atakuwa amechoka” Mjomba aliongea mwenyewe na kugeuka ili kuondoka zake kwenye miangaiko yake huku sura yake ikitawaliwa na tabasam.

Moyo wake ulilipuka na akili ilimwambia asiondoke kwanza, aligeuka na kuutazama vyema Mlango wa Shaymaa na aliona arudi ili kwenda kumuamsha Mpwa wake.

“Unataka kufanya nini?” Mkewe alitokea na kumuuliza baada ya kumuona akitaka kwenda kwenye chumba cha Shaymaa. “Nataka kumgongea nimsalimie kwani tatizo lipo wapi?” Mjomba alimjibu Mkewe ambae alionekana akisikitika na kumtazama Mumewe huku akiamini kuwa Mumewe atakuwa na kitu na Shaymaa.

Mzee majaliwa hakutaka kubishana na Mkewe, alisogea mpaka kwenye mlango wa Shaymaa na kujaribu kugonga huku akimuita Shaymaa lakini wapi, kulikuwa kimya na hakuna Mtu yoyote aliyeweza kuitikia.

Mzee majaliwa alihisi labda Shaymaa atakuwa hajarudi alitoa simu na kumpigia Feisal, lakini namba ya Feisal ilikuwa haipatikani. “Mke wangu Mtoto haitikii humu” Mzee Majaliwa alimwambia Mkewe lakini Shangazi alijifanya kama hamuoni.

Mzee majaliwa alianza kuingiwa na hofu na alipojaribu kuufungua mlango aliukuta ulikuwa umeegeshwa.

Alipoingia hakuweza kuamini macho yake. Alishusha pumzi na kushukuru Mungu baada ya kukuta chumba kikiwa cheupe na Shaymaa hakuwepo.

“Mpango umeenda kama nilivyotaka, Feisal anapaswa kumuoa Binamu yake. Pili siyo aina ya Mwanamke anayepaswa kuishi nae” Mzee Majaliwa aliongea na kuonesha kuwa alikuwa amedhamiria kumkutanisha Feisal na Shaymaa ili lengo lake ni kuwafanya wapendane.

Aligeuka na kutaka kuondoka lakini nywele zake zilimsisimka na alihisi kitu na haraka aligeuka na kutupa jicho kitandani. Alistuka baada ya kuikuta barua iliyokuwa imeandikwa na Shaymaa na kuwekwa vyema kitandani.

Mjomba alisogea na kuanza kuisoma Barua iliyokuwa imeandikwa na Shaymaa na alijikuta akipata mstuko kwa kile ambacho alichokuwa amekiona kimeandikwa na Shaymaa.

Macho yalimtoka na pumzi zilikata na kujikuta akishindwa kupumua. Mkono wake mmoja akiwa ameshika kifuani kwake huku akijitahidi kupambana na mapafu yake kuitafuta pumzi iliyokuwa imepotea alijikuta amepiga yowe ambalo liliweza kumstua mpaka Mkewe.

Shangazi aliingia ndani na kustuka baada ya kukuta hali ambayo amemkuta nayo Mume wake. Alitaka kumsaidia Mumewe lakini alishinda na alitoka nje na kuomba msaada kwa kuwaita Wapangaji wake ambao waliingia na kumkuta Mzee akiwa hajitambui huku akiwa anaunguruma na mkononi akiwa ameshika ile barua aliyokuwa ameandika Shaymaa.

“Mungu wangu, Shaymaa amejiuwa” Mmoja kati ya wapangaji wao aliongea baada ya kuisoma ile barua aliyokuwa ameiandika Shaymaa na kuwastua watu wote waliokuwa wanajaribu kumpa huduma ya kwanza Mjomba.

MASAA KADHAA YALIYOPITA KABLA HAKUJAKUCHA

Usiku wa manane pembezoni mwa barabara, Alionekana Shaymaa akiwa anatembea huku akionekana Mwenye mawazo sana. 

“Tazama watu jinsi wanavyotembea na magari yao wakiwa wanatoka maeneo tofauti kula starehe. Akika hawa ndio Watu ambao wanapaswa kuishi katika ulimwengu huu. Mimi sidhani kama nina haki ya kuishi katika ulimwengu huu hata kidogo”

Shaymaa aliongea huku akiwa analia na ghafla alianza kuhisi maumivu makali ya kichwa na alitafuta sehemu na kukaa chini huku akiwa anaugulia maumivu makali ya kichwa aliyokuwa anayasikia.
                   *****
Ilikuwa ni siku mbaya kwa Abdu na kila alichokuwa anajaribu kukifanya kilikuwa kigumu kwake.

Moyo wake ulikuwa kama unamwambia kuna kitu anapaswa kukifanya lakini alikuwa hajui ni kitu gani.

Aliingia bafuni na kufungulia bomba la maji na kuacha maji yamwagikie pasipo kufanya jambo lolote kwa dakika kadhaa huku akijitazama katika kioo na alihisi kama nafsi yake inamwambia kitu “Kwanini nimekuwa hivi?” 
Abdul alijiuliza mwenyewe bila hata kupata majibu sahihi, na badala yake aliamua kuoga na kutoka zake na kujiandaa ili kwenda katika mishughuliko yake.

Akiwa kwenye gari aliona mikono inatetemeka kabisa na alishindwa kuendesha gari na kujikuta moyo wake ukiwa unamuenda mbio na akiwa na hofu ya hali ya juu “Nini kimenikuta lakini?” Abdul aliongea huku akiwa anajitazama mikono yake jinsi anavyotetemeka

“Shaymaaa!!” Alijikuta akipiga kelele kama vile Mtu aliyekurupushwa kutoka kwenye njozi.

Alitoa simu yake na kujaribu kutafuta namba ya Shaymaa ili ampigie lakini haikuwepo katika simu yake na hapo alikumbuka kitu

“Kwanini unakaa na namba ya Mwanamke ambae umeshaachana nae?” Irna alimuuliza Abdul huku akiwa anachezea simu ya Mumewe “Ulikuwa unataka nifanyaje Mke wangu?” Abdul alimuuliza Irina aliyekuwa amelala miguuni mwake.

“Siitaji kuona kitu chochote kinachomuhusu Shaymaa, naomba futa picha zake na kila kitu chake” Irina alimwambia Abdul ambae alimpa ruksa afanye atakacho.

Irina alimtazama Mumewe na kumbusu na baada ya hapo ni kufuta namba za Shaymaa katika simu ya Abdul na kufuta picha pamoja na massage zote.

Akuishia hapo, alichoma moto picha zote za ndoa ya Abdul na Shaymaa, ili tu Mume wake asiwe na kumbukumbu na Mwanamke wake huyo aliyempa talaka.

Abdul alimaliza kukumbuka na kujikuta akiumizwa na tukio hilo, alikaa na kutafakari ni vipi anaweza kupata namba ya Shaymaa. Alionekana kukumbuka na kushuka kwenye gari na kuingia ndani.

Alifika na kupekuwa katika nyaraka zake muhimu na alifanikiwa kupata cheti cha ndoa alichokuwa ameoana na Shaymaa na alipotazama aliona namba ya Shaymaa.

Alichukua namba haraka pasipo mkewe kumuona na alirudi kwenye gari na kuipiga namba hiyo huku akiwa anaendesha gari.
                             *****
Hali ya Mjomba ilikuwa mbaya na haraka wapangaji wake walichukua gari na kumpakai mjomba ili kumkimbiza hospital. Wakiwa wanatoka chumbani, walisikia simu inaita. Mpangaji mmoja aligundua kuwa simu ya Shaymaa ilikuwa ndani kumbe Shaymaa aliacha simu ndani “Hallo”

Abdul alisikia simu ya Shaymaa imepokelewa na aliposikia sauti ya kike alijua ni Shaymaa “Shaymaa vipi ulifika salama jana?” Abdul aliuliza na yule Binti alikaa kimya na Abdul alimuita mara kadhaa

“Shaymaa amefariki” Yule Dada alijibu na Abdul alipata mstuko na kujikuta akikanyaga break za ghafla na gari iligeuka na kuama upande wa pili na kishindo kikubwa kilisikika baada ya gari ya Abdul kugongwa na gari nyingine iliyokuwa kasi!!

NINI KIATAENDELEA? JE ABDUL ATAKUFA? VIPI KUHUSU SHAYMAA? 

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 14
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Gari ya Abdul iligongwa na kugeuka ilipokuwa inatoka na kuwafanya Watu waliokuwa Eneo lile kupatwa na mstuko na kumkimbilia hili kwenda kumpa msaada.

Bahati nzuri kwa Abdul alikuwa amefunga mkanda hivyo ilikuwa nafuu kwake kuweza kupata madhara zaidi. Akiwa ametulia huku usukani wa gari aliyokuwa anaendesha ukiwa umembana ipasavyo na hakuweza kutikisa hata kidole chake cha shahada bali aliganda na kutazama huku damu zikiwa zinamtiririka

Sura ya Mwanamke mrembo aliyekuwa amevalia mavazi meupe alikuwa akimtazama kwa udhuni huku akiwa anamuita kwa ishara akihitaji amfute alipo. Alijitahidi kutoa macho ili kumtazama vizri na hapo aligundua kuwa alikuwa ni Shaymaa.

Aliweza kumtazama jinsi alivyokuwa anaisogelea gari yake huku akiwa anatabasam na yeye akijikuta akiruhusu kufungua mdomo wake na kutabasam na kadri alivyokuwa anamtazama Shaymaa ndivyo nuru ilivyokuwa ikitoweka katika mboni za macho yake na kujikuta akipoteza fahamu.

Hapakuwa na Shaymaa katika eneo hilo isipokuwa yalikuwa ni Mawazo yake ndio yalikuwa yamemsukuma kufikiri hivyo.

Wasamalia wema waliweza kumkimbilia na hili wamchomoe na ikiwezekana akimbizwe hospital
                           ******
Habari za kifo cha Shaymaa ziliweza kumfikia Feisal, ambaye alikuwa akiendesha gari yake kuelekea Nyumbani kwa Baba yake huku akiwa Mwenye mawazo tele.
“Ni uzembe wangu!! Najua ni uzembe wangu, Sijawahi kufikiri wala kuhisi kama nitakuwa nimekukosea kiasi icho” Masikini Feisal alikuwa akijihisi pasipo kujua kitu gani kilichopelekea Shaymaa kuamua kuchukua maamuzi magumu dhidi yake

Alijua Shaymaa atakuwa amefikia maamuzi hayo magumu baada ya Feisal kushindwa kumsaidia jana usiku na akamuacha katika mazingira magumu.

Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuishi kwa dhana, epuka na ogopa kuishi kwa kudhani, unaweza kujihukumu kwa kosa ambalo hukutenda wala uhusiki kwa lolote.

Feisal akiwa anaendesha gari huku akiwa amechanganyikiwa na hasijue nini cha kufanya baada ya kuambiwa Baba yake alipatwa na mstuko huku Shaymaa pia akiwa amejiua.

Akiwa kwenye gari aliweza kufika eneo ambalo Abdul alikuwa amepata ajali na alikuwa akitolewa kwenye gari yake. Kwakuwa ilikuwa mbali kidogo alipo yeye na sehemu ambayo Abdul ampeta ajali kutoka na foleni ndogo iliyojitokeza, hivyo hakuweza kutambua ni nani ambae alikuwa anatolewa kwenye gari

“Habari za sahizi mamdogo” Feisal alishusha kioo na kumsalimia Mdada aliyekuwa anapita jirani na gari yake “Salama” Yule Dada aliitikia huku akiwa ametulia akimsikilizia labda kuna jambo anaihitaji kumwambia “Kuna nini pale?” “Kuna ajali imetokea muda mfupi uliopita, naona jamaa amekufa ndio anatolewa kwenye gari” Yule dada alongea pasipo hata kuthibitisha alichokuwa anakiongea.

Feisal alishangazwa na eneo ambalo Feisal amepata ajali na hapo alijisi ni uzembe wa dereva kwa maana hapakuwa na lolote zaidi ya barabara kunyooka. Hakutaka tena kubaki eneo hilo. Alichekecha gari na kujaribu kupita eneo linguine

“Nakuchukia sana Abdul, najua ni wewe ndie uliyebadili taswira ya Shayamaa. Dada yangu alikuwa mrembo sana, lakini kupitia wewe Mjinga umesababisha mpaka amefikia maamuzi magumu”

Feisal aliongea pasipo kutambua Mtu aliyekuwa anamuongealea ndio huyo hapo aliyeambiwa kuwa amekufa muda mchache baada ya kupata ajali
                             ******
Abdul alipoingia chumbani kuja kutafuta cheti cha ndoa Irina alimuona sana lakini alijifanya amelala kama hajamuona.

“Bila shaka kuna namba alikuwa anachukua, lakini mbona kama alikuwa anaonekana anahofia kufanya alichokuwa anakifanya?” Irina alijiuliza huku akisogea kwenye kabati na kuvuta draw ili kujua ilikuwa ni namba ya nani aliyokuwa anaichukua

Irina alistuka baada ya kujua kuwa Abdul alikuwa amechukua namba katika cheti cha ndoa yake na aliyekuwa Mkewe “inamaana Abdul amechukua namba ya Shaymaa?” Aliuliza huku akiitafuta simu yake na kuonekana amechukizwa.

Wasamalia wema waliokuwa wamekuja kumsaidia Abdul, wengine walikuwa kazini. Kijana mmoja na wenzake waliweza kuokota simu ya Abdul na kuondoka kabisa eneo la tukio. “Oya msala Mke wa huyu jamaa anapiga” Mmoja kati ya wale vibaka aliongea na Mwenzake akamshauri apokee

“Sijategemea kama ulikuwa unatafuta namba ya mpuuzi wako katika cheti cha ndoa yenu, Abdul naomba talaka yangu” Irina aliongea baada ile simu kupokelewa na yule kijana alikaa kimya kwanza kumsikiliza pasipo hata kuongea chochote.

“Unaonekana huna adabu na Mumeo, sasa tu nikwambie Mumeo amepata ajali asubuhi hii na hali yake ni mbaya sana sijui kama atakuwa yupo hai au amekufa, muwahi hospital akakupe talaka kabla hajakata roho, fanya haraka wamemkimbiza Amana. Hii namba usipige haitakuwa hewani kwani Vijana wastaarabu ndio tuliookota hii simu na tutaipeleka kwenye misaada ya watu wenye uitaji maalum”

Yule kibaka aliongea na kukata simu na kisha waliangua kicheko utafaikiri alikuwa ameongea jambo la maana. Baada ya kufanya hivyo waliizima simu na kuendelea na jambo la kutafuta mteja.

Zilikuwa ni taharifa ambazo zilimstua sana Irina, alijikuta akichoka na kuanza kumuomba samahani Mumewe kwa kumuhisi vibaya 

“Itakuwa alichukua namba ili amwambie asimfuatilie maana Mimi nilimkataza kuwa nae karibu” Irina aliongea mwenyewe huku akiwa analia na haraka alijiandaa ili kwenda hospital.

Akiwa anajipodoa aliona simu yake inaita na alipotazama jina alikuwa ni Jack ndie aliyekuwa anapiga simu. Alipuuza na kuitupa simu pembeni “Siwezi kuongea na wewe kwa wakati huu utanisamehe” 

Irina aliongea huku akiwa anapachika hereni ktika sikio lake utafikiri alikuwa anaenda kwenye jambo la sherehe kumbe alikuwa anaenda kwenye jambo gumu ambalo limemkuta Mumewe
                               ****
Feisal alifika nyumbani kwa Mjomba na kwa bahati mbaya alikuwa ameshachelewa na kuambiwa kuwa Mjomba ameshakimbizwa hospital. 

“Amepelekwa hospital gani?” Feisal aliuliza na kujibiwa kuwa amepelekwa Amana.

Baada majibu hayo hakutaka kuuuliza tena na kupiga hatua kuifuta gari yake, lakini alikumbuka jambo na kurejea “Maiti ya Shaymaa imepelekwa hospital gani?” Aliuliza na wapangaji walitazamana kabla Mmoja wao hajatoa barua na kumpatia.

“Jana usiku kulikuwa na ugomvi hapa nyumbani, Mama yako alikuwa anamtuhumu baba yako kutembea na Shaymaa kitu ambacho kinaonekana kumkwaza Shaymaa na kuamua kuandika barua hiyo, Mpaka sasa bado hatujajua ni wapi alipoenda kujiuwa” Feisal alistuka baada ya kusikia maneno ya yule mpangaji

“Shaymaa hawezi kutembea na Baba!! Wala Baba hawezi kuthubutu kutamkia upuuzi huo Mtoto wa Dada yake” Feisal aliongea kwa ukali mpaka Watu wote walimshangaa

“Baada ya kuandika hivi, mnaweza kuniambia Shaymaa alitumia njia gani ili kuondoa uhai wake?” Feisal aliuliza na Wapangji walikosa majibu.

“Sasa kwanini mnatangaza kama Shaymaa amekufa wakati hakuna Mtu aliyeweza kuthibitisha kifo chake? Shaymaa hajafa, nasema Shaymaa hawezi kufaaaa”

Feisal alipaza sauti tena na safari hii alikuwa akiongea kwa uchungu huku chozi likiwa linatiririka.

Hakuitaji kuongea zaidi badala yake aliondoka eneo hilo ili kuelekea hospital.

“Feisal tafadhali naomba uniambie nini kimemkuta Shaymaa na Baba yako” Alikuwa ni Shangazi aliyepiga simu huku akiwa analia. “Wifi yako ndio chanzo cha yote” Feisal alimwambia kila kitu Shangazi yake aliyeonekana kuchukizwa zaidi.

“Nipo kwenye gari nakuja, ila Mwambie Mama yako wa kambo, akifa Mtu yoyote kati ya Kaka au Shaymaa basi ajue atakula hiyo maiti adharani” Dada yake Mzee Majaliwa aliongea kwa hasira huku akiwa analia.

Alimtuma Feisal kuzunguka mitaani kumtafuta Shaymaa ili kujua kama kweli amejiuwa au yalikuwa ni maneno ya hasira na kuna sehemu ameamua kuenda ili kukaa mbali na maneno ya Shangazi yake, huku akimwambia kuwa yeye yupo njiani anakuja
                                 *****
Jack alipiga simu mara kadhaa lakini Irina hakuweza kushika simu yake na alifanya alichokuwa anataka kufanya na kuingia kwenye gari yake kuelekea Amana Hospital.

Wakati anatoka na gari yake nje ya geti alistuka kumuona jack akiwa amesimama akimtazama.

Irina alisimamisha gari na Jacka aliingia kwenye gari “Tabia ya kutopokea simu yangu umeanza lini?” Jack alimuuliza huku akiwa anamtazama kwa umakini.

“Mume wangu amepata ajali, yani hapa sijui kama ni mzima au lah! Nimechanganyikiwa Jack, Samahani sana” Irina alijitetea na kumfanya Jack atabasam kidogo kabla ya kuonesha hasira tena.

“Umefikia hatua hiyo? Inamaana Mumeo ni bora kuliko mimi?’ Jack alimuuliza na Irina alikosa cha kumjibu “lakini Jack……” “Shuka kwenye gari na twende ndani kwako nina maongezi na wewe.

Irina alijaribu kumuomba Jack amruhusu aende hospital lakini wapi Jack hakuitaji kusikia jambo hilo na alimlazimisha na kweli Irina alirudisha gari ndani na wakaingia mpaka chumbani.

Walipofika chumbani huku Irina akiwa analia kwa kitendo icho ambacho Jack amekilazimisha na alionekana dhairi hana maamuzi dhidi yake.

Jack alipoangaza ukutani aliona picha ya ndoa ya Irina na Abdul ikiwa ukutani kwenye flem maalum, aliichukua na kuibamiza chini na kioo cha flem kilivunjika kiasi ambacho hata Irina Mwenyewe alistuka

“Jaaaaaack!!” Alijikuta ameita kwa hasira na Jack aligeuka na kumtazama “Unawezaje kutubutu kuniita jina langu?” Jack aliongea huku akimsogelea Irina aliyekuwa anarudi nyuma huku akimuogopa “Umeudhunishwa na taharifa za kifo cha Abdul? Umesahau nini kilikuleta katika nyumba hii?” 

Jack alimuuliza Irina aliyeonekana kutetemeka akimuogopa “Nakumbuka” Alijibu huku akimuogopa “Umeshampenda kweli si ndio?” “Hapana Jah………” Alitaka kumtaja jina lake lakini alisita baada ya kumuona anamtazama kwa umakini “Abdul anapaswa kufa haraka iwezekanavyo, hiwe kwa ajali au kwa mikono yako ili urithi hii nyumba, Sasa kama Abdul amekufa nini kinakuuma? Unapaswa tusherekee”

Jack aliongea na kumvuta Irina katika mwili wake na alichokifanya ni kupeleka kinywa chake katika mdomo wa Irina kama ambavyo Mwanaume na Mwanamke wafanyavyo lakini cha ajabu hawa walikuwa ni Wanawake watupu waliamua kubusiana

Kumbe Irina alikuwa na mahusiano na Mwanameke mwenzake ndio maana Jack aliona wivu siku zile na kumchapa ngumi Abdul………………

WEWE UNAFIKIRI NINI KITAKUJA KUENDELEA? JACK ANAMKUMBUSHA IRINA KUWA AMEOLEWA ILI KUMUUA ABDUL NA WALITHI NYUMBA NA JAMBO BAYA ZAIDI WAWILI HAWA WANAONEKANA NI MTU NA MPENZI WAKE.

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 15
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Iliwachukua dakika kadhaa kutenda walichokuwa wanakitenda katika chumba cha Irina tena katika kitanda ambacho alikuwa analala na Mumewe.

“Tafadhali Jack Mimi sihitaji tuendelee na haya Mambo, umeshaniathiri vya kutosha” Irina alimwabia Jack huku akiwa anatetemeka utafikiri alikuwa anaongea na nani.

Jack hakutaka kumsikiliza badala yake alimvuta Irina na kufanya nae ushetani ambao ni aibu hata kuusimulia.

Baada ya kumaliza walichokuwa wanafanya, Jack na Irina walitoka na kuelekea Hospital kwenda kumuona Abdul na kujua hali yake jinsi anavyoendelea.

“Tafadhali naomba tupitie nyumbani kwanza” Jack aliongea na Irina alionekana kuchukizwa na jambo hilo “Lakini Honey………” Irina aliongea na Jack alimkatisha huku akiwa anamtazama “Nafanya kila kitu kwa ajili yako, tafadhali naomba twende nyumbani” 

Kauli moja ya Jack ilitosha kumfanya Iina kubadili uelekeo na kuelekea nyumbani kwa kina Jack huku akiwa hajui nini ambacho walikuwa wanaenda kutenda nyumbani kwa kina Jack
                              ******
Feisal alitembea maeneo yote pasipo kumuona Shaymaa. Alijaribu kumtafuta kila kona, alienda hospital zote kujaribu kuulizia lakini wapi hapakuwa na taharifa yoyote inayomuhusu Shaymaa.

“Napaswa kuonesha kama Mimi ni Mwanaume niliyekamilika” Feisal aliongea Mwenyewe huku akiwa amechanganyikiwa na hasijue wapi alipo Shaymaa.

“Hapana hatuna taharifa za huyo Mtu” Naomba nitazame hata chumba cha kuifadhia maiti, labda naweza kuona maiti yake” Feisal alijaribu kuomba kwenye moja ya hospital ambayo alihisi anaweza kupata taharifa sahihi zinazomuhusu Shaymaa!!

“Hatujapokea maiti yoyote jana inayohusu Msichana kujiua, hata hivyo unapaswa kutoa taharifa polisikabla ujafika huku kuja kuulizia” Alijibiwa na kujikuta akichoka na hasijue nini afanye.

Feisal alipiga hatua kuelekea katika gari yake na alipofika kwenye gari aliingia na kukaa kwa dakika kadhaa akitafakari ni wapi anaweza kumpata Shaymaa “Shaymaa naomba ujitokeze, tafadhali nakuomba Shaymaa, naitaji nikuambie kitu kizuri ambacho sijawahi kukuambia kipindi tupo Watoto” Feisal aliongea na kutoa simu yake na kutazama picha kadhaa alizopiga na Shaymaa usiku wa jana.

“Inamaana jana ilikuwa ni siku ya mwisho kuona tabasam lako? Mimi ni mzembe Shayamaa si heti eeeh? Sijui kwanini niliweza kuruhusu ukaumizwa tena” Feisal aliongea na kujikuta akilia kwa kupiga kelele huku akiwa ameinamia usukani wa gari na mikono yake ikaminya batani ya honi bila kujua na honi ikawa inapiga kelele bila hata yeye mwenyewe kujua.
                              *******
Gari ya wasamalia wema iliyokuwa imembeba Abdul iliweza kufika hospital na Abdul alishushwa katika gari na kupakizwa kwenye kitanda kuwaishwa wodini moja kwa moja huku akiwa hajitambui.

Abdul akiwa katika kitanda anapelekwa wodini alipishana na Mjomba aliyekuwa aamepakizwa katika wheelchair akipelekwa katika wodi maalum ya uchunguzi dhidi yake. Walipishana bila kutambua huku kila mmoja akiwa hajitambui

Ilikuwa ni kama movie ambayo iliwahusisha Watu wawili ambao matatizo yao yalihusishwa na Mtu mmoja. Mjomba alipatwa na mstuko baada ya kusoma barua ya Shaymaa huku Abdul akipatwa na mstuko baada ya kuambiwa habari ya kifo cha Shaymaa na kujikuta akipata ajali
                             ******
Nje ya nyumba ya kina Jack, Irina aliegesha gari yake ambayo alipewa zawadi na Abdul, gari ambayo mwanzoni Abdul alikuwa amemnunulia Shaymaa kama zawadi baada ya kufunga nae ndoa ila baada ya kuachika Shaymaa hakutaka kuondoka na kitu chochote nyumbani kwa Abdul na kuamua kuondoka yeye na nguo zake.

“Tafdahli naomba usiteremke kwenye gari hii” Jack aliongea na kutaka kufungua mlango “Lakini ujaniambia nini kilichotuleta huku” Irina alimuuliza Jack ambae alitabasam kidogo na kumjibu “Tumekuja kuchukua sindano ya sumu ya kumuua Abdul endapo tutakuta bado anapumua” Jack aliongea kawaida na kushuka kwenye gari lakini Irina alistuka na kujikuta akitetemeka

“Inamaana napaswa kumuua Abdul? Nawezaje kufanya hivyo Mimi?” Irina aliongea mwenyewe huku akiwa anatetemeka

Akiwa bado anatafakari nini afanye alisikia mtu akimgongea kupitia kioo cha gari yake na alipomtazama alikuwa ni Mama Mtu mzima. 

Aligundua ni Mama yake Jack, alishusha kioo na kumsalimia. Lakini Mama yake Jack hakuitikia salam ya Irina na Badala yake alimtazama na kusikitika “Nilijua ni Mimi pekee ndie niliyezaa Mtoto Shetani. Kumbe kuna Mwanamke Mwenzangu amezaa Shetani mwengine ambae ni Wewe?”

Mama jack aliongea kwa masikitiko huku akimtazama Irina ambae alibaki kupigwa na butwaa na hakutegemea kama Mama Jack anaweza kumwambia maneno mazito kama hayo.

“Mama Mbona unaniongela maneno makali kiasi icho?” “Mimi nakuongelea maneno makali ila Mungu atakuja kukuchoma na moto mkali zaidi na utaungua kuliko hata ukali wa maneno yangu” Mama Jack aliongea na kuanza kupaza sauti

“Hivi mnadhani uchafu wenu mnaofanya kwa siri wewe na Jack, utaendelea kuwa siri ya milele? Kama uikuwa hujui Mungu huwa anawaumbua Mashetani kama nyinyi ambao mlilaaniwa na Wazazi wenu na hamtakuja kuiona pepo yake hata siku moja”

Mama jack aliongea maneno makali yaliyokuwa yanauchoma moyo wa Irina na kujikuta akitetemeka kwa uoga “Utaenda kumjibu nini Mungu wako aliyekuumba uje utumike kwa ajili ya Mwanaume atakayekuoa na Wewe unatumika kwa ajili ya Mwanamke mwenzio tena unamuita Mume? Alafu ulivyo mrembo, tena nasikia umeolewa lakini unamsaliti Mumeo kwa kutembea na Mwanamke mwenzio?”

Mama Jack alipaza sauti na wapita njia walianza kusimama wakimshangaa Irina kitendo ambacho kilimfanya Irina kuna aibu kwa maneno ya Mama Jack na kujikuta akiwasha gari na kuondoka huku akiwa analia

“Una laana wewe, Mungu akulaani wewe na Wasichana wenzako woote manoshiriki uchafu huo”

Mama Jack alimsindikiza na maneno Irina na wakati huu Jack alikuwa anatoka kutokea ndani na kumkuta Mama yake akiwa anabwata “Hivi kwanini unaingilia mambo yangu?” Jack aliongea kwa hasira huku akimtazama Mama yake “Unalaana wewe, hata ufanye nini wewe ni Mwanamke, sijakuzaa Mwanaume Mimi, wala sifungamani na dhambi uzitendazo”

Mama jack aliongea na Jack hakutaka kumsikiliza na badala yake alisimamisha pikipiki ili kumfukuzia Irina huko alipoenda kwenda kutimiza matakwa yake.

Aliamini endapo Irina atafanikiwa kumuua Abdul basi Irina atarithi nyumba ya Abdul na baadhi ya mali zake huku yeye akiwa Jike Dume wa Irina na wataendeleza kufanya ujinga wao

Kama nawe msomaji unaesoma simulizi hii ni mmoja wa kushiriki mambo hayo machafu yanayopingwa na dini zote za Mwenyezi Mungu, tafadhali Muogope Mungu na jaribu kutubu dhambi zako kama vitabu ama dini yako inavyokuongoza.

“Kweli Mimi ni Muovu mbele yako Mungu wangu, hebu tazama Mimi ni Mwanamke wa aina gani? Leo hii nimeweza kumsaliti Mume wangu kwa kutenda dhambi na Mwanamke mwenzangu” ……… Irina aliongea na kulia mwenyewe “Jack sikuhitaji tena katika maisha yangu tafadhali naomba uondoke”

Irina aliongea na kuzidi kukanyaga mafuta lakini machele yalimcheza alihisi uenda Jack atakuwa anamfuatilia na hakutaka kuwa karibu nae kwani alijua kwa kitendo cha kwenda na Jack hospital kunaweza kumfanya akampoteze Abdul.

Aliisogeza gari pembeni na kuigesha kwenye moja ya saluni kubwa ya kiume na kushusha kiti huku akiomba Jack hasimuone.

“tafadhali Abdul naomba usife, nahitaji nikuoneshe upendo wangu wa dhati ambao sijawahi kukuonesha hapo kabla” Irina aliongea huku akiwa analia na kukatishwa na pikipiki iliyokuwa inaenda mbio na alitazama kwa umakini kweli aliweza kumuona Jack akiwa amepakizwa.

“Tafadhali simama” Jack alimwambia Dereva wa bodaboda ambae haraka aliweza kusimama. “Kuna nini?” “Nimeiona gari ya Irina ikiwa imesimama sehemu, itakuwa amejiongeza anatusubiri”

Jack aliongea na kweli waliweza kugeuza na kurudi walipokuwa wameiona gari.

Walifika na Jack aliitazama gari na kutabasam “Abdul kwisha habari yako” Jack aliongea mwenyewe na kutoa pesa kumlipa mwenye bodaboda
                             *****
Feisal alirudi nyumbani akionekana kama Mtu aliyechanganyikiwa. Alifika sebuleni kwake na kuonekana akienda huku na huku pale sebuleni na mara kadhaa alionekana kuongea anachokijua Mwenyewe 

“Mwanaume Malaya uliyeshindikana wewe ani kutwa nzima ndio unarudi kweli?” Pili alitoka chumbani na kumwambia Mumewe “Hiyo ndio salamu?” Feisal alimtazama kwa hasira na kumuuliza 

“Salamu gani unayoitaka mbwa mkubwa wewe? Nasemaje na leo utanitambua” Pili alisogea na kutaka kurusha konde kama kawaida yake lakini siku hiyo alikuwa amepotea njia.

Feisal aliudaka mkono wake na kuanza kuuminya kwa kuuzungusha “Mpuuzi mkubwa wewe, Mwanaume huwa hapigwi wala hafokewi kama ufanyavyo, nafasi niliyokupa naona unaitumia vibaya” 

Feisal aliongea kwa hasira na Pili alipiga kelele kama Mtoto mdogo “Fei unaniumizaaaaa!!” “Acha nikuumize mpuuzi mkubwa, kwa sababu yako wewe umesababisha Shaymaa ametoroka nyumbani na kunifanya nionekane mzembe”

Feisal aliongea na kumsukuma chini ambapo Pili alikuwa anaugulia maumivu “Leo nakupa talaka, tena nakupa talaka tatu ili husiwe na matarajio na Mimi hata kidogo”

“Heti nini? Unataka kunipa talaka?” Pili aliongea na kustuka “Ndio nakupa talaka tena unapaswa kujua Muda wowote nitakaofanikiwa kumpata Shaymaa, nibora nimfute machozi kwa kufunga nae ndoa”

Feisal aliongea huku akiwa anaandika talaka kumpa mkewe Pili katika mazingira hata Pili Mwenyewe hakuyaamini kama kweli itafikia siku Feisal anaweza kumpa talaka

NINI KITAENDELEA? JE WAPI ALIPO SHAYMAA? VIPI KUHUSU MJOMBA? VIPI KUHUSU IRINA NA JACK?


Post a Comment

Previous Post Next Post