🔐 MAUMIVU YA NDOA (6----10) 😭😭😭😭

Abdul alijaribu kumshawishi Irina akubali kumuoa Mke wa pili lakini ilikuwa ngumu na Irina aliendele kuwa na msimamo wake kuwa kama anaitaji kumuoa basi lazima akubali mashart yake.

“Abdul wewe ni Mwanaume na naamini Wanaume huwa mnasifika katika swala zima la kufanya maamuzi. Hebu fuata moyo wako unachokipenda”

Irina alimwambia Abdul na kumpa mtihani mkubwa sana na kushindwa kutambua nini afanye kwa Shaymaa ambae anafanya kila jambo ili kunusuru ndoa yake.

“Liwalo na liwe, waswahili wamesema bhana ukitaka kumuua nyani basi usimtazame usoni” Abdul aliongea mwenyewe akiwa katika gari yake aliyoiegesha katika maegesho ya magari katika mgahawa wa Misosi Lounge. Alichukua simu yake na kuandika ujumbe uliosomeka “Nimefanya juhudi kubwa mno kushindana na moyo wangu, lakini naona limekuwa jambo gumu kama maji kupandisha mlima. Shaymaa wewe ni Mwanamke Mrembo sana, una kila sifa ya kuwa Mke wa Mtu ila kwangu naona itakuwa ngumu”

Baada ya kuandika ujumbe huo, aliusoma mara kadhaa na kurudia huku akionekana kutafakari kabla ya kukata shauri na kubonyeza send katika namba ya Shaymaa.

Masikini Shaymaa akiwa anendelea na shughuli zake za nyumbani, alisikia mlio wa ujumbee ukiita katika simu yake kuashiria kuwa kuna ujumbe umeingia. Alisogea na kushika simu yake na kutabasam baada ya kuona ujumbe umetoka kwa Abdul. Kama hajausoma, aliatabsam na kuikumbatia simu yake na kuongea mwenyewe “Abdul natamani kila saa kuona jumbe zako kwenye simu yangu, huwa najisikia faraja sana pindi ninapoona unnitumia ujumbe. Lakini sijui kwanini huwa ufanyi hivi sikuhizi toafauti na mwanzoni.

Unajua siku zote mapenzi ya mwanzoni huwa yana raha sana asikwambie Mtu, watu wengi kwenye mapenzi huwa wanavutiwa sana na kipindi kile cha mwanzo unaweza kujiona kama malaika mana Mtu anaweza kukwambia usitembee kwenye jua utayayuka mi sipendi. Utafikiri umekuwa barafu.

Tabasamu lilipotea katika uso wa Shaymaa na ghafla alijikuta akiudhunika na kutetemeka mikono utafikiri alikutana na taharifa ya Msiba wa Mtu wake wa karibu. “Unamaanisha Nini Abdul wangu? Unamaanisha nini lakini?” Shaymaa aliongeaa na kukaa chini na kujikuta akilia.

“Shaymaa wala usilie, tafadhali usitoe mchozi wako nakuomba, Abdul ni wako” Kama kawaida yake alijiongelesha mwenyewe na kujaribu kujinyamazisha lakini wapi ilikuwa kama anajidanganya. Kili kilichukua nafasi yake na aliona hakuna tena njia mbadala ya kumzuia Abdul hasimpe talaka.
                            ******
Baada ya kuwaza na kuwazua Shaymaa aliona njia pekee ya kunusuru ndoa yake ni kwenda kwa Mshenga wake kuweza kuzungumza nae kuona kama anaweza kumsaidia “Nimesikitika sana kwa icho anachotaka kukifanya Abdul, nikiwa kama Mshenga wake kiukweli naona hata aibu kukutazama” Babu Ally ambae ni Mshenga wa Abdul aliongea huku akimtazama Shaymaa aliyekuwa anatiririkwa na machozi.

“Tatizo siyo kuachika Babu Ally, ninachotaka kujua ananiacha kwa makossa gani ambayo nimeyatenda kwake? Ili hata nikirudi nyumbani najua naenda kujifunza nini?”

Shaymaa aliongea na kumfanya Mshenga ashindwe cha kumjibu Shaymaa badala yake aliganda tu akimtazama
                              *****
Ilikuwa tayari ameshafanya maamuzi kabla hata hajarudi nyumbani. Japokuwa ilikuwa ngumu kwa upande wake kumuacha Mwanamke kama Shaymaa lakini ilikuwa ngumu kwake kuushinda moyo wake kwani kila alipokuwa karibu na Irina, moyo wake ulikuwa unaenda mbio. “Samahani sana Shaymaa” ndio kauli pekee aliyoweza kuongea kwa wakati huo kisha akionekana kuitafuta simu yake.

Alinyanyua simu yake na kuipiga namba fulani na sauti ya kike ilisikika baada ya simu kupokelewa upande wa pili wa simu “Naomba tuonane muda huu” Abdul aliongea na Sauti ilisikika ikiuliza tunakutana wapi?” “Nakutumia location” “Sawa Boss”

Pembezoni mwa ufukwe ndio sehemu ambayo Abdul alikuwa anasubiri huyo Mtu aliyekuwa amemtumia location ili wakutane. Ilichukua kama dakika 10 tokea Abdul asimame eneo lile na gari ndogo ilionekana ikiegeshwa na kushuka Mwanamke aliyekuwa amevaa viatu virefu na huku macho yake akiwa ameifunika kwa miwani meusi.

Alipovua miwani yake ili kumsalimia Boss wake, uwezi kuamini alikuwa ni Amina Mwanamke ambaye alikutana na Shaymaa jana na kutaka kumgonga na gari Shaymaa na wakaunga urafiki baada ya kumpa rift na kubadilishana namba za simu. Ni nani huyu Amina?
                          **** 
Anaitwa Amina Azizi Mwanamke ambae ni Rafiki yake wa siku nyingi na mara kadhaa amekuwa akimtuma katika mambo yake haswa pale anapokuwa na dili ngumu.

Kabla ya Abdul kwenda Misosi Lounge, ambapo alifanyiwa surprise na Irina. Alikuwa ofisini kwake akiongea na Amina “Naitaji kumuacha Shaymaa” Abdul aliongea na kumfanya Amina astuke na kumuuliza kwanini?” Kwakua alikuwa ni rafiki yake, wala hakumficha kitu chochote kuhusu Irina.

Alimpa kazi ya kumfuatilia Shaymaa na atengeneze nae urafiki na ikiwezekana amshauri ujinga na kumsimulia story ya uongo kuhus maisha yake ili hata akimpa talaka basi Shaymaa achukulie ni jambo la kawaida. “lakini si unakumbuka kama nilikuwa kwenye ndoa yako? Unadhani Shaymaa hatoweza kunitambua?” Amina alimuuliza na Abdul alimuakikishia kuwa Shaymaa hamtambui hata kidogo.

Amina alikubali kufanya kazi ya Abdul na alimuahidi atamlipa kiasi kizuri cha pesa. Baada ya kuongea machache alitoa pesa kiasi na kumpatia kisha akamtoa out kwenda kupata nae chakula cha mchana pale Misosi Lounge.

Baada ya Shaymaa kuja kula keki na kuondoka kwa hasira, Abdul alimuita Amina na kumtuma afanye kazi yake na kweli Amina alienda na kukutana na Shaymaa na kufanikiwa kumshawishi na kumpa siri na Amina akajifanya anaongea na simu na kugombana nae ili Shaymaa aone kawaida mambo anayofanyiwa na Abdul
                             ***** 

Baada ya Amina kukutana na Abdul, alionekana kushangazwa kidogo kutokana na Boss wake kumuita ghafla “Naitaji kujua kuhusu Shaymaa” “lakini Boss si uliniambia niachane na habari za Shaymaa” Amina alimuuliza na Abdul alimjibu kuwa alidhani Irina angekubali kuolewa Mke wa pili ila amekataa “Sina budi kumpa tala lakini natafuta sababu ya kufanya hivyo” Abdul aliongea na kumfanya Amina ajisikie vibaya kidogo.

“lakini Boss, Shaymaa anakupenda sana na ukimuacha sidhani kama Irina anaweza kuvaa viatu vyake” “Siitaji unishauri lolote katika ili, naomba ufuate amri yangu” “Sawa Boss Amina aliitikia huku akiwa anatazama chini “hebu mpigie, najua atakusimulia tu, kutokana na ujumbe niliomtumia na hapo naomba umshawishi achukue talaka”

Amina alichukua simu na kumpigia Shaymaa ambae kama bdul alivyofikiria ndivyo ilivyokuwa. Shymaa alimsimulia kila kitu Amina mpaka alivyoenda kwa Mshenga “kama anataka kukupa talaka wewe chukua naamini atakuja kukumbuka” Amina aliongea na kukata simu. 

“Amina alienda kwa Mshenga wako, na hivi ninavyoongea na wewe Mshenga yupo nyumbani anakusubiri” Amina aliongea na Abdul alifurahi na kumwambia kuwa nimeshapata sababu ya kutoa talaka.

Kweli Mshenga alikuwa nyumbani kwa bdul akimsubiri abdul ili aweze kunusuru ndoa yao kama ambavyo Shaymaa alimuomba kufanya hivyo.

Babu ally alikaa mpaka saa 4 usiku lakini Abdul hakuweza kurejea na simu yake alikuwa ameizima kabisa. Kumbe Abdul alikuwa amerejea nyumbani na kuegesha gari yake pembeni ya nyumba yake akisubiri Babu Ally atoke nyumbani kwake.

Babu Ally alitoka na kuondoka zake huku Abdul akiwa anamtazam na baada ya Babu Ally kuondoka Abdul alirudi nyumbani akiwa na Hasira za kuigiza. “karibu nyumbani Mume wangu” Shaymaa alimsogelea na kupokelewa na kibao kilichompeleka mpaka chini “Malaya Mkubwa wewe, yani wewe wa kutembea na Babu Ally”

Abdul alifoka pasipo hata kumpa nafasi Shaymaa aliyekuwa anajaribu kujietetea kwanini babu Allya alikuja hapoa “Ulipotoa Mguu wako hapa kwenda kwa Babu Ally ulimuaga nani?” Abdu alimuuliza na Shaymaa alijiona amekosea na kumuomba msamaha lakini Abdul hakutaka kumuelewa badala yake alichukua karatasi na peni na kumuandikia tala na kumkabidhi.

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 07
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Hakuna jambo linalouma katika maisha kama Mtu akuzushie kitu ambacho hukuwahi kufanya wala ujawahi kufikiria kufanya. Shaymaa alimtazama Abdul wakati anampa talaka na kumuuliza.

“Unafanya yote kwasababu ya Irina? Amekataa kuolewa uke wenza?” Shaymaa alimuuliza Abdul ambae hakumjibu kitu na badala yake alimpa tu talaka na kumtaka akajifunze kwao jinsi ya kutambua thamani ya Mwanaume ni nini? 
Alijua fika kuwa Shaymaa hakuwa na makossa, ila waswahili wanasema ukitaka kumuua Mbwa basi mbatize jina kwanza “Kupitia wewe nimechuma na umenikuta na mali zangu ila sitajali kwa kile nilichochuma hapo hawali kabla yako. Naomba tugawane sawa na nakupa uhuru wa wewe kuchagua nyumba uitakayo kati ya hizi nyumba mbili tulizonazo. Ili ghorofa na nyumba ya kule mbezi” Abdul aliongea huku akimtazama Shymaa aliyekuwa analia muda wote huku akiwa tayari ameshapokea talaka yake.

“Kwako nilifuata upendo wa dhati, faraja na ukarimu wakonikijua utakuwa Mwanaume bora kwangu ambaye utakuja kuwa Baba wa wanangu na ndio maana nikakubali kuolewa na wewe na nikakubidhi moyo wangu. Kosa langu kubwa nililowahi kulifanya katika maisha yangu ni kukubali kuolewa na Mwanaume aliyekuwa amenipenda kimakosa. Katika kanuni 12 za mapenzi nilizowahi kujifunza, nafikiri kutakuwa na kanuni ya 13 ambayo Mtu anaweza kukupenda kimakosa, na utakapokutana na kadhia hiyo ni hatua gani ya haraka unapaswa kuchukua”

Shaymaa aliongea na kupiga hatua kuingia ndani na Abdul alimuonea huruma, alitamani hata kuchana ile talaka lakini alijiambia mwenyewe moyoni “Irina amechukua nafasi kubwa katika moyo wangu, nitampa tabu kama nitaendelea kuishi nae” Abdulaliongea moyoni huku akimtazama Shaymaa.

“Nakusikiliza” Shaymaa aliongea baada ya kusimamishwa na Abdul “Bado sijajua chaguo lako katika mali tulizochuma” “Sihitaji chochote kati ya hizo mali zako, nafikiri itakuwa vyema kama utagawana na Irina kwa maana kupitia yeye umeweza kunifanya Mimi niumie” Shaymaa aliongea na kuingia ndani na kufungasha mizigo yake na kutoka kisha akamkabidhi Abdul funguo ya gari ambayo alimnunulia kama zawadi baada ya kufunga nae ndoa. “Lakini ili lilikuwa ni lako?” “Itapendeza pia kama litakuwa la Irina”

Shaymaa alingea kama Mwanamke na alifanya maamuzi magumu sana. Alionesha kweli alimpenda Abdul na alijitahidi kujiweka kama Mke wa Mtu ili tu kumridhisha Mumewe lakini wapi Abdul hakuwa na shukrani juu ya upendo wa mwenzie hata kidogo.
                              *****
Ilikuwa ni siku iliyoweka doa katika moyo wa Shaymaa. Hakuwahi kufikiri katika maisha yake kama kuna siku anaweza kuja kuachika. Alifanya kila kitu ambacho kwake alikiona bora, alijiweka Mwanamke bora, mchamungu na mwenye heshima na Mumewe lakini wapi yote ilikuwa ni bure.

“Hii kweli ni talaka, Mumeo amekuacha kwa talaka moja” Mjomba aliongea huku akimtazama Shaymaa ambaye alishusha pumzi baada ya kusibitika kweli ilikuwa ni talaka “lakini sitaki kuamini hiki kilichosababisha ndoa yenu kuvunjika. Mbona umeniangusha sana Shaymaa” Mjomba aliongea bila kutaja icho kilichoandikwa humo, hakutaka Mkewe ajue.

“Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mshenga wangu” Shaymaa aliongea kwa upole na Shangazi yake alistuka kwa sauti “Eeeeh!! Hivi wewe unajitambua kweli? Abdul akusingizie unatembea na Mshenga wako yeye hana akili?” Shangazi alifoka akimbwatiza Shaymaa pasipo kujua kuwa alikuwa anamuumiza sana mwenzake 

“Umetutia aibu sana, Hivi sisi tutamtazama vipi huyo Mwanaume wako?” “Inatosha, wala upaswi kumfokea kama Mtoto Mdogo, ameshasema hakuwahi kufanya hivyo, namuamini sana Shyamaa hawezi kufanya ujinga huo” Mjomba aliongea na kumfanya Shangazi achukie.

“Inamaana Mimi Sipaswi kumsema huyo Mpwa wako? Sawa mambo yenu nawaachia wenyewe mtajuana” Shangazi aliongea na kuinuka zake huku Mumewe akimtazama tu 

“Nakumbuka sana kifo cha mama yako, siku moja kabla ya kifo chake alinifuata usiku na tukaongea sana, aliniambia anataka kusafiri anaenda mbali mno ili kukwepa karaha za mawifi zake waliokuwa wakimshtumu kwa Mambo mengi mno haswa kutokana na kifo cha Mumewe yani Baba yako Mzazi. Kikubwa alichoniomba usiku ule ni kukulea katika maadili yaliyotuka ili tu usije ukapata tabu katika swala zima la kujitegemea na kutambua thamani ya Mwanaume katika ndoa” Mjomba alikuwa akiongea kwa upole na kumfanya Shaymaa atulie na kusikiliza.

Ndoa ya mama yako na Baba yako iligubikwa na migogoro ya mara kwa mara, na kitu kikubwa kilichokuwa kikiwagombanisha kilikuwa ni wivu wa Mapenzi na Mama yako ndie aliyekuwa Mkorofi kwa Mwenzake mpaka pale Baba yake alipokutwa amekufa. Inasemekana aliamua kujiua Mwenyewe, lakini ndugu zako walikuwa wakimuusisha Dada yangu na kumuua Mumewe ili tu afurahie maisha yake. Basi siku hiyo alipokuja kwangu kumbe na yeye alikuwa ameazimia kufanya maamuzi. Alijinyonga usiku ule na kuniachia wewe ukiwa umebaki katika mikono yangu”

Ilikuwa simulizi iliyogusa moyo wa Shaymaa na kujikuta akilia kwa mara nyingine tena “Sitamani kusikia umefanya jambo lolote baya kwako, Kama Abdul amekushinda basi yeye hakuwahi kukabidhiwa na Mama yako zaidi ya Mimi. Ili kulinda Nasaba na kutafakari hali ya baadae, kutoa fursa ya kujirudi na kusahiisha makossa, unapaswakwenda kukaa heda kwa Mumeo” Mjomba aliongea na kumstua Shaymaa “Lakini Mjomba………” “Hakuna cha lakini, sheria inasema hivyo. Labda katika kipindi hiki cha Eda, Mumewo anaweza kutafakari kitu na kuona wapi alipokosea”
                         ****
Ilikuwa ni siku yenye furaha kwa upade wa Abdul haswa baada ya kumuondoa Shaymaa nyumbani kwake, lakini pia zilikuwa ni taharifa njema kwa upande wa Irina baada ya kusikia kizuizi pekee kilichokuwa kimekaa mbele yake ili hasiingie kwenye ndoa kilikuwa kimeondolewa.
Siku hiyo walifanya sherehe katika mgahawa wa Misosi Lounge na watu walisherekea ipasavyo “Nafikiri sasa nimetimiza vigezo vya kuwa Mume wako halali wa ndoa” Abdul aliongea na kumfanya Irina atabasam na kumjibu “hapana” na kumfanya Abdul afinye na wote walifurahi “Abdul tafadhali naomba usikawie kukata kiu yangu haraka iwezekanavyo, naitaji kuingia kwenye ndo sasa. Nataka niwe Mkeo ili nikuoneshe kuwa haujafanya makossa kumuondoa yule kibwengo nyumbani kwako” Irina alimwambia Abdul ambaye alionekana kuchukizwa kidogo kwa kitendo cha Irina kumuita Kibwengo Shaymaa

“Leo nataka twende sote nyumbani kwako” Irina alimwambia Abdul aliyeonekana kustuka kwa taharifa hizo na kuonesha kuzifurahia.

Hawakusubiri siku hiyo kufunga mgahawa, bali waliondoka mapema sana na kwenda kufanya shoping na kurejea nyumbani kwao.

“Una nini wewe leo?” Abdul alimuuliza Mlinzi wake baada ya kumuona kama kuna kitu anatamani kumwambia na alipomsogelea, mlinzi hakusita kumuuma sikio na kumfanya Abdul abadilike na kuonekana kuchukizwa kiasi “Nani alikuruhusu kufanya hivyo? Nilikwambia nini wakati natoka hapa?’

“Baby kuna nini?” Irina aliuliza na Abdula alimtazama bila kujibu na kuingia ndani kwa hasira huku Irina akimfuata nyuma.

Waliingia ndani na kumkuta Shaymaa akiwa na Mjomba wake wakiwa wamekuja “Mjomba talaka yangu si inajieleza lakini?” Abdul aliongea kwa hasira huku akimtazama Mjomba na Shaymaa na Irina nao wakitazamana kwa jicho kali.

“Hivi unafikiri huyu hana moyo? Unadhani hii ni kuni uliyoinunua sokoni? Yani ukiamua utaiweka jikoni ama utaipasua ili uichochee utakavyo?” Mjomba aliinuka na kuongea kwa utulivu “Nawezaje kuendelea kuishi na Mwanamke ambae ananisaliti kwa kutembea na Mshenga wangu” Abdul aliongea na Mjomba alicheka kidogo kisha akamtazama “Ni rahisi sana kutudanganya sisi, lakini unadhani unaweza kumdanganya Mungu wako? Dhambi unayoitenda leo, kaa ukijua itakutafuna kesho. Mimi sina Mengi wala sina sababu ya kukufanya umuone Binti yangu bora kuliko huyu uliyempata, ila sheria ya dini inasema Shaymaa anapaswa kukaa eda yake nyumbani kwako, tena unapaswa kumtimizia mahitaji yake”

Mjomba aliongea na kuondoka zake akiwaacha wanamtazama. “Baby naomba umpe chumba cha wageni akakae hiyo Eda yake na sisi twende zetu tukapumzike” Irina aliongea na Shaymaa akimtazama huku akitabasam akionesha kuwa hajachukizwa na kile alichokiongea Irina.

Lakini moyoni kuna kitu kikubwa kilimfukuta, hakutegemea kama Abdula angekuwa haraka hivyo kumleta Mwanamke nyumbani kwake.

NINI KITAENDELEA? SHAYMAA ATAWEZA KUKAA EDA NYUMBANI KWA ABDUL? VIPI KUHUSU IRINA NA ABDUL?

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 08
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Simulizi hii ya kusisimua yenye mafunzo ya Ndoa, unaweza kuisoma kupitia whatsapp kwenye group maalum.
Ulishawahi kujiuliza unaweza kuishi vipi kwenye nyumba ya Mtu ambae ameshakupa talaka? Unaweza kuvumilia ukimuona analala na Mwanamke Mwengine?

Ilikuwa ngumu sana kwa Shaymaa kuishi katika nyumba ya Abdul hata kama Abdul alikuwa anampa kila kitu alichokuwa anapaswa kuhudumiwa. Kitu kikubwa kilichokuwa kinamuuma ni kuona ameachika baada ya kumpata Irina ambaye pia amegoma kuolewa matala, kwa lugha nyepesi unaweza sema Irina ndio msababishaji mkuu wa Shaymaa kuachika.

Irina alikuwa anafanya vibweka vya kila aina ili tu kumuumiza Shaymaa “Hivi unajijua kuwa una moyo wa jiwe?” Irina alimuuliza Shaymaa baada ya kukutana nae akiwa anashuka kwenye ngazi kuelekea kwenye mambo yake “Mwanamke mwenye akili timamu, hawezi kukubali kuwa sehemu ya kuvunja ndoa ya Mwanamke mwenzake, hipo siku dhambi yenu itakuja kuwatafuna” Shaymaa alimjibu na Irina aliangua kicheko utafikiri alikuwa anamcheka kinyago.

Shaymaa alimtazama na hakutaka kuendelea na aliamua kupandisha ngazi kuelekea chumbani kwa Abdul “Unaenda wapi?” Irina alimuuliza “Naenda kuonana na Abdul nina jambo nataka kuzungumza nae” “Unataka kuonana na Abdul kwa idhini ya nani? Unawezaje kwenda kumuona Mume wangu pasipo kuniomba ruksa?” Irina aliuliza na kumshangaza Shaymaa “Hivi huna haya kumuita Mume mwanaume ambaye hata hajakuoa? Wewe unadhini kama machangudoa wengine wafanyavyo” 

Kauli ya Shaymaa ilimchefua sana Irina na alijikuta akimzibua kibao Shaymaa kilichompeleka mpaka chini na hapo unyonge ulimtoka Shaymaa alijikuta akimvaa Irina na wakaanza kutupiana Makonde

Abdul aliwakuta na kuwaamulia na kumsukuma kwa nguvu Shaymaa aliyepiga yowe la maumivu baada ya kuanguka vibaya “Abdul siwezi kuishi kwako wala siitaji kuolewa na wewe naomba niondoke zangu” Irina alijiliza na Abdul alikuwa anamzuia asifanye hivyo kuliko kumsaidia Shaymaa aliyekuwa anaugulia maumivu kwa kuanguka vibaya.
“Irina nisamehe mimi, tafadhali naomba unisamehe mpenzi wangu. Niambie tatizo nini?” Abdul aliongea huku akiwa anamnyenyekea Irina aliyekuwa anajiliza kinafki

“Mwanamke wako kanitukana sana, kaniita changudoa na kasema ataakikisha mimi na wewe hatufungi ndoa. Tafadhali Abdul niache nirudi kwetu nisije nikalogwa kwa sababu yako”

Maneno ya Irina, yalimchukiza sana Abdul na hakutaka kusikiliza kwa upande wa Shaymaa na badalaka yake alimsogelea na kuanza kumfokea “Hivi wewe nini kimekurejesha nyumbani kwangu? Umekuja kaka eda au umekuja kuvuluga mambo yangu?” Nimeshakupa talaka basi jaribu kuachika tafadhali, na nikwambie tu hakuna jambo lolote ambalo unaweza ukafanya na mimi nikamuacha Irina. Huyu ni Mwanamke wa ndoto zangu na wewe tafuta Mwanaume wa ndoto zako wala usijali, au ulitaka nikupe talaka tatu ndio ujue kuwa sikuhitaji tena na nimefunga ukurasa dhidi yako” 

Abdul aliongea maneno makali kwa Shaymaa ambaye aliishia kumtazama pasipo kumjibu kitu chochote huku akiwa analia kilio cha kwikwi. Abdul baada ya kufanya hayo alimsogelea Irina na kumshika mkono na kuondoka nae kazini.

Abdul alifika alipo Shaymaa na kumtupia pesa “Hiyo ya matumizi, kwa maana si umefuata pesa nyumbani kwangu”

Ilikuwa ni dhiaka ya hali ya juu kwa Shaymaa kutupiwa pesa na kuambiwa kuwa alichokifuata kwa Abdul ilikuwa ni pesa na si kingine.

Kitu kikubwa alichoamua ni kumuandikia ujumbe na kumtumia kwenye simu yake “Samahani sana Abdu, kilichonileta kwako ilikuwa ni kutihi sheria na kufuata taratibu za dini kama zinavyoelekeza. Ila kwakuwa umenifikiria tofauti nasema Asante sana”

Aliandika ujumbe na kuutuma na wakati huo simu ya Abdul alikuwa ameishika Irina “Nani huyo?” Abdul aliuliza baada ya kusikia muito wa ujumbe. “Malaya wako” Irina alijibu pasipo hata kuwa na hofu kwa kumuita Mwenzake jina ambalo hata yeye hasingejisikia furaha kuitwa hivyo “Unanionea bure Irina, inamana hautaki kuamini kama kweli Mimi na yeye tumeachana?” “Mngekuwa mmeachana basi asingekuja kukaa pale eda na kuanza kunichimba vijembe. Ndio maana nilikwambia mambo ya Uke wenza siwezi Mimi”

Irina aliongea na alijifanya amechukia na muda wote Abdul alikuwa akimbembeleza na kumuakikishia kuwa yeye hayupo pamoja na Shaymaa “Kama kweli haupo pamoja nae naomba nijibu Mimi huo ujumbe” Irina aliongea na Abdul alikataa lakini Irina alimuomba hashuke kwenye gari na amuache waendelee na mpenzi wake.

Hata kama unampenda Mtu, ila upaswi kufanya kila kitu hata vile ambavyo vipo nje ya uwezo wako, heti wewe unalazimika kufanya ilimradi atambue tu ni jinsi gani unampenda. Mpendwa, kaa ukijua kufanya vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako ikiwemo vya kuwaumiza wengine kwa ajili ya upendo wako, basi kaa ukijua hipo siku unaweza kujutia maamuzi ya kile ulichokifanya kwa mpenzi wako kwa sababu wala hasikudanganye kuwa mtaingia kaburini pamoja. Mtaachana na kila mmoja atakuwa na mahusiano mapaya na kitakachokuwa kinawaumiza ni hayo mambo uliyokuwa ukimfanyia kumuonesha kuwa unampenda haliyakuwa yalikuwa yanakucost kwa kiasi kikubwa mno.

Abdul alimtazama Irina aliyekuwa amenuna akitaka kupewa simu ili tu amjibu Shaymaa na kujifanya aliyejibu ujumbe huo alikuwa ni Abdul. Shika simu ila Mimi sipendi mtukanane hata kidogo” Abdul aliongea na Irina hakuitaji kumpa nafasi zaidi. Alichukua simu ya Abdul na kuingia katika uwanja wa kuandikia ujumbe mfupi na kuanza kuporomosha yale aliyoona yanafaa kumtumia Shyamaa.

“Koma kunitumia ujumbe wowote unaoujua wewe, alafu kwenu mna dhiki sana si ndio? Familia yako imeshindwa kukuonea huruma mpaka mnakaa kikao nakukurudisha nyumbani kwangu? $#%&@ Tusi”

Ujumbe uliingia katika simu ya Shaymaa na alipokwenda kuufungua alikuwa ni Abdul ndie aliyekuwa amejibu. Lakini aliposoma alishindwa kuamini kile ambacho ameandika Abdul na kujikuta akiishia kulia “nakuchukia sana Abdul” Hiyo ndio kauli pekee aliyoweza kuizungumza kutoka katika kinywa chake na kujikuta akisimama kama Mtu aliyekuwa na nguvu na kujiongeresha kama ilivyo kawaida yake. Aliumizwa na maneno ya Abdul na kujikuta akirejea mara kadhaa kusoma kile kilichokuwa kimeandikwa na Abdul “lakini sijawahi kumuona Abdul akitukana matusi kwa namna hii” Shaymaa aliongea na kutafakari mwenye na hapo alianza kuhisi labda Irina alituma ujumbe kupitia simu ya Abdul. “Shaymaa, unapaswa kuwa na msimamo katika kile ukisemacho, Abdul hakupendi hata kidogo. Anawezaje kumpa Mwanamke simu yake ili akutukane?”

Baada ya hapo Shaymaa alirudi nyumbani na kumuelezea kila kitu Mjomba ambae alimwambia abaki nyumbani na aachane na Abdul kwani Mungu ni Mwema kwake na labda hipo sababu ya yeye kukuepusha pale.

Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuachika. Ni bora uachwe na Mtu ambaye ulikuwa huna upendo nae, kuliko Mtu ambae unampenda tena mbaya zaidi unaachwa na mwenzako anakuja kuchukua nafasi yako huku ukishuudia. Upweke ndio kitu kilichokuwa kinamuumiza Shaymaa na siku zote alijiona hakuwa na hatia kuachwa na Abdul “Hivi kitu gani kinakuliza siku zote?” Shangazi alimuuliza Shaymaa huku akiingia chumbani kwake “Naumia Shangazi, Abdul nilimpenda sana” Shamyaa alimjibu Shangazi huku akimtazama.

Shangazi hakupendezwa hata kidogo kwa kitendo cha Shaymaa kuja kukaa hapo kwa Mjomba wake kwani yeye aliona kama ni Mtu aliyekuja kuongeza mzigo katika familia yake “Shaymaa sikiliza nikwambie, Abdul hawezi kukuacha tu bila sababu ya Msingi, wewe utakuwa na shida ambayo sisi hauwezi kutuambia. Ila kama umekimbilia kudai talaka ukitegemea hapa kwa Mjomba wako, basi kaa ukijua umeula wa chuya” Shangazi aliongea huku akiwa amemkazia macho yake makubwa utafaikiri Mchawi alikuwa anataka kumloga Mtu
                          *****
Irina alishinikiza kuolewa haraka hiwezekanavyo na Abdul hakuweza kupinga hilo kwani alikuwa anampenda na kumsikiliza kwa kila jambo.

Ndoa ya haraka ilifungwa iliyokuwa imeudhuriwa na Watu wachache walioalikwa kufika katika sherehe hiyo. Na baada ya kufunga ndoa, walikwenda zao Zanzibar kwenda kula fungate na baada ya hapo maisha ya Bibi na Bwana yaliendelea kama vile ambavyo alivyokuwa anapenda Abdul.

Siku moja Abdula alirudi nyumbani na ghafla alsituka baada ya kusikia kitu kilichomshangaza, alifika na kumuuliza Mlinzi ambaye alishindwa kumjibu na kuona aibu “Shemeji ………” Ndio kitu pekee ambacho Mlinzi alichoweza kujibu

Abdul alivuta mlango kwa nguvu na kuingia ndani na alichokikuta sebuleni aliishia kuduwaa na kutazama……………………

NINI KITAENDELEA? ABDUL AMEKUTA NINI NYUMBANI KWAKE? VIPI KUHUSU SHAYMAA?

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 09
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Sauti ya Mziki ilikuwa imefunguliwa mpaka juu huku Irina na marafiki zake wakiwa wamevalia nguo fupi wakilewa na kucheza Mziki na kupiga kelele utafikiri walikuwa wapo clubu. Mmoja kati ya wale wasichana waliokuwa wamejazana mule alikuwa anavuta Sigara na kupuliza moshi uliokuwa unasambaa ndani huku akiwa amevaa mavazi kama Mwanaume

Abdul aliwatazama na kuishia kupigwa na butwaa kwa kile ambacho amekikuta Mke wake anakifanya katika nyumba yake. Hakuitaji wala kuwasemesha badala yake aliwapita na kupandisha ngazi na kuelekea chumbani kwake. “Shemeji yenu ndio huyo” Irina alizima mziki na kuongea kisha akamfuata Abdul chumbani

“Hivi umeonesha tabia gani mbele ya marafiki zangu?” Irina aliingia chumbani na kumfokea Abdul. “Yani umewakuta Marafiki zangu alafu unawapita bila hata kuwasalimia! Maana yako nini Abdul? Sijapenda tabia yako naomba twende ukawaombe msamaha”

Irina alizidi kuongea huku Abdul akiwa anamtazama kwa hasira ya hali ya juu na kujikuta akitetemeka “Irina hivi unawezaje kuthubutu kufungua kinywa chako na kuongea upuuzi mbele yangu? Yani Mimi niwaombe msamaha au wewe ndio uniombe msamaha? Hivi wewe haujui kama ni Mke wa Mtu? Nani alikupa mamlaka ya kuwachukua wale machangudoa na kuwajaza nyumbani kwangu?” “Machangudoa? Inamaana Mimi na Marafiki zangu ni machangudoa si ndio?” Irina alichukizwa na kumuuliza na Abdul alizidi kutilia mkazo kwa kuwaona machangudoa wasio jitambua kutoka na jinsi walivyokuwa wamevaa na mambo waliyokuwa wanayafanya ndani kwake.

Waliendelea kujibishana huku Irina akiwa anamjibu jeuri Abdul utafikiri alikuwa anajibishana na Mwanamke mwenzie “Sikiliza Abdul, nina haki yangu ya Msingi kama Mkeo. Ujanioa kuja kuninyanyasa umesikia? Mimi siyo yule mshamba wako uliyokuwa unamuendesha utakavyo na laiti kama ningejua kama una tabia za kipuuzi kiasi icho wala nisingekubali kuolewa na Mpuuzi kama wewe”

Kitendo cha kumuita Mpuuzi kilimkwaza Abdul na kujikuta akimkunja Irina na kumsukuma mpaka kwenye ukuta na kumkandamiza, wakati huu mkono wake ulikuwa juu akitaka kumtandika kibao, lakini kabla hajafanya hivyo, alisitishwa na sauti ya mlango wa chumbani kwao uliokuwa ukigongwa kuashiria kuna Mtu alikuwa anabisha hodi. wote waligeuka kutazama anaebisha hodi kisha wakageukiana na kutazamana
Irina aliutoa mkono wa Abduli, uliokuwa umemkandamiza na kwenda kufungua mlango “Sisi tunataka kusepa so kama vipi fanya utusindikize, naona huyo Mduanzi wako kashaanza kuwaka, hisiwe kesi” Yule msichana aliyekuwa anavuta sigara ambaye pekee ndie aliyekuwa amevalia mavazi tofauti aliongea kihuni utafikiri Mwanaume fulani anaevuta bangi. 

“Nani unamuita Mduanzi? Nakuuliza unamuita nani Mduanzia nakuuliza?” Abdul alipaniki na kumfuata yule binti aliyekuwa anaongea kihuni.

“Jack tafadhali tangulieni nakuja” Irina alimzuia Abdul na kumwambia Jack aondoke “Babu usinichukulie poa hata kidogo naweza kukalisha mbele ya Mkeo alafu ukajisikia aibu. Umemuoa huyo ujatuoa wote sawa?” Jack aliongea huku akimtazama kwa dharau Abdul aliyekuwa anataka Irina amuache ili apigane nae

“Ole wako utoe miguu yako uwasindikize hawa kunguni, nakwambia kwa hilo sitakuelewa hata kidogo” Abdul alimkoromea Irina aliyeonekana kushangazwa na kauli zake “Abdul kama unataka kugombana na Mimi wewe tugombane tu, ila sitaacha kuwasindikiza Marafiki zangu kwa sababu yako” “Alafu mbona babu ujiamini au kibamia wewe?” jack aliongea na kauli hii ilimuingia Abdul na kushindwa kujizuia. Alikurupuka na kwenda kumvaa Jack

Ilikuwa ni aibu kwa Abdul kwani Jack hakuwa Mwanamke kama alivyomchukulia, alisitukia amepewa ngumi moja ya jicho iliyomkalisha mpaka chini na Irina alimuwahi Jack na kumkamata na kelele za Irina ziliwastua wenzao waliokuwa sebuleni na kuja mbio kumsaidia kumzuia Jack aliyekuwa anataka kuendelea kumshushia kichapo Abdul.
                            *****
Baada ya kuona Shangazi ameanza vitimbi dhidi yake, Shaymaa aliona ni bora aongee na Mjomba ikiwezekana ampe nauli ili arudi zake kijijini.

“Hapana Mjomba, kwa hali yako jinsi ilivyo wala hautaweza kuishi kijijini, na isitoshe kama ujuavyo kule Bibi na babu yako walishafariki, amebaki Dada na Mumewe na Watoto wake hivyo naona kama unaweza kuwa mzigo kwao” Mjoma aliongea na kumuuliza kama kuna tatizo lolote baina yake na Shangazi yake swali ambalo lilimfanya Shaymaa atafakari kidogo kabla ya kujibu.

“Hapana hakuna tatizo lolote, Shangazi amekuwa mkalimu sana kwangu na mara zote amekuwa akinihusia na kunipa mafunzo kama Binti yake ikiwemo kujua ni jinsi gani naweza kuishi katika ndoa pindi Abdul atakaponirejea au kama nitabahatika kupata Mwanaume mwengine ambae atakuwa tayari kunioa na nitamridhia” Shaymaa hakutaka kuongea chochote ambacho kitasababisha ndoa ya mjomba wake kuwa shakani ila kiukweli Shangazi hakuwahi kuonesha upendo kwake hata kidogo.

Hakuna jambo jema kwa Mwanaume kama pale anaposikiwa Mkewe amepewa sifa ambazo hakuzitarajia kuzisikia kwa upande wa ndugu zake. Mjomba hakuwa na jicho la tatu la kung’amua kilichopo ndani ya moyo wa Shaymaa. Alifurahi kusikia Mkewe na Mpwa wake wanaishi kwa upendo, kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na jambo ambalo limejificha.

“Sasa Mjomba!! Najua wewe ni msichana na una mahitaji yako binafsi ambayo ungetamani kuyafanya na siyo kila wakati unaweza kuniambia” Mjomba aliongea na kutoa pochi yake na kuhesabu kiasi cha pesa na kumpatia “Mjomba pes azote hizo? Una majukumu mengi na unapaswa kuyashughulikia. Mimi bado nina akiba yangu” “hapana upaswi kukataa anachokupa mjomba wako, hata wewe ulipokuwa kwa Mumeo ulikuwa ukinipa pesa pasipo kujali. Ni laki moja tu hii wala siyo nyingi”

Mjomba aliongea na kutabasam, na tabasam lake lilikatishwa na sonyo la Mkewe. 

Shangazi alitokea na kuwatazama, alichukia baada ya kumuona Mjomba anampa pesa Shaymaa na hakuongea kitu badala yake aliwapita kwa kumpiga kikumbo Shaymaa “lakini tabia gani hiyo?” Mjomba aliuliza na Shangazi hakujibu kitu na badala yake aliingia zake ndani.

Mjomba alimpa pesa Shaymaa ambaye alizikataa lakini Mjomba alimlazimisha mpaka Shayamaa alizichukua huku akiwa na hofu na Shangazi.

“Tunapaswa kumtendea wema Shaymaa, nadhani unatambua hali yake. Hayupo sawa kabisa na kiasi fulani anaonekana ameathirika na talaka aliyopewa na Mumewe” Mjoma aliongea na Shangazi alisikiaka akibwata na kupaza sauti

“Mmezaliwa Watatu, Dada yako Mkubwa ambae ndio Mama yake Shaymaa alishafariki. Shaymaa maisha yake yote amelelewa na mama yake Mdogo sasa kama ameshapewa talaka kwanini asirudi huko?” “Hivi hauoni fahari na sisi tunaonekana tuna Binti kwa wakati huu?” Tumeishi kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 38 na hatukuwahi kupata Mtoto. Hebu tumchukulie Shaymaa kama Mtoto wetu wa kumzaa”

Mjomba aliongea na Shangazi alipinga vikali Shaymaa kuwepo hapo huku akiamini kuachika kwa Shaymaa ni kutokana na tabia ake chafu ambazo hawezi kuzitaja. “Shaymaa hawezi kuwa na tabia chafu hata kidogo, Ni Binti tuliyemlea katika misingi ya dini na maadili yaliyotukuka. Alafu mbona Shaymaa ameongea mazuri juu yako? Inakuaje unaonesha tabia chafu mbele ya Mtoto?” Mjomba alimgombeza Mkewe ambaye hakutaka kumuelewa na aliona kuja kwa Shaymaa kutamfanya Mumewe kwenda kasi ili kutimiza matakwa ya Shaymaa.

Wakati yote yakiendelea chumbani kwa Mjomba. Shaymaa alikuwa akisikiliza yote ambayo Shangazi alivyokuwa anamjibu Mumewe “Eeeh Mwenyezi Mungu naomba umjaalie Shangazi hawe na kauli thabiti mbele ya Mumewe. Nahofia kuwa sehemu ya kuvunja ndoa hii iliyodumu kwa miaka mingi” Shaymaa alipiga magoti na kumuomba Mungu.

Baada ya kupishana kauli na Mkewe, Mjomba hakutaka kukaa nyumbani na aliona ni bora aondoke na kuepusha shetani amabe aliona anajaribu kuingia katika familia yake.

“Shaymaa!! Shaymaa!!” Shangazi aligonga kwa nguvu mlango wa Shaymaa na Shaymaa alifungua mlango huku akimtazama kwa uoga. “Mjomba wako amekupa sh ngapi?” Shangazi alimuuliza kwa ukali huku akimtazama utafaikiri Mke Mwenzie “Amenipa laki moja” “Amenipa laki moja” Shangazi alimuigiza kwa kubana pua yake “Mpuuzi mkubwa wewe nataka uniambie una nini kinachoendelea baina ya wewe na Mjomba wako?”

Shangazi alimuuliza Shaymaa na kumfanya Astuke na kumtazama kwa umakini “Shangazii!!” Shaymaa alimuita kwa Mshangao na Shangazi alipokea Shaymaa na kibao cha maana kilichotua kwenye shavu lake.

NINI KITENDELEA? UNGEKUWA SHAYMAA UNGEFANYA KITU GANI IKIWA MKE WA MJOMBA WAKO AMESHAANZA KUHISI VITU VYA KIPUUZI DHIDI YAKO? VIPI KUHUSU ABDUL NA MKEWE?

Episode ya 10 itakuwa na majibu. Je unapata tabu kusoma simulizi zangu? Je kuna vipande huwa vinakupita? Karibu ujiunge katika group maalum la whatsapp ambalo litakufanya usome simuizi kwa haraka zaidi. Pia kama kama umepitwa na vipande basi nitakutumia ili tuwe sawa.

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 10
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Kuna wakati katika maisha unaweza kujihisi kama Mtu mwenye bahati mbaya kutokana na yale ambayo unayopitia. Lakini nikwambie tu hakuna Mtihani ambao unaweza kupitia na usiwe sahizi yako. Ndio maana wanasema matatizo ni kipimo cha akili. 

Shaymaa alikuwa amekaa na kupitia baadhi ya nukuu tofauti alizokuwa anaitaji kuzisikia baada ya kupitia maneno machafu kutoka kwa shangazi “lakini kosa langu nini? Hivi mimi nitakuwa nimekosa ustaarabu kiasi gani mpaka nifikie hatu ya kutembea na kaka wa mama yangu Mzazi?”

Shaymaa aliongea Mwenyewe kabla ya kuinua kiganja chake cha mkono wa kulia na kufuta chozi ambalo lilikuwa katika mboni ya macho yake na kuinua mikono yake juu na kumuomba Mungu wake amuongoze katika njia iliyonyooka ili kushinda mitihani anayopitia

“Hivi Abdul alishawahi kuhisi walau chembe ya maumivu utakayopitia baada ya kukupa talaka? Hawezi kukumbuka kwa sababu yeye anae Mtu sahihi kwa wakati huu na wewe aliweza kukuoa kimakosa tu. Shaymaa unapaswa kumsamehe Abdul kwa maana ni Mungu pekee ndie anayepaswa kutoa hukumu baina yetu”

Shaymaa alikuwa na kajitabia fulani ambacho wakati mwengine ukimtazama unaweza kuhisi ni kama vile alikuwa amechanganyikiwa. Mara nyingi alikuwa anapenda kujishauri mwenyewe, yani unaweza kusema alikuwa akiwaza kwa sauti na alikuwa akiamini ilikuwa ni njia sahihi kwake kuweza kujipa hamasa pale anapohisi kukata tamaa ya jambo fulani.

“Wewe Msungo!!” Shangazi alifika na kumuita jina ambalo lilimkera sana Shaymaa “Shangazi Mimi ni Msungo?” “Sasa kama siyo Msungo uliwezaje ukashindwa kudumu kwenye ndoa yako? Mwanamke aliyefundwa akafundika kamwe hawezi kuachika katika mazingira ya hajabu kama yako wewe” Shangazi aliongea huku akimtazama kwa dharau na kuendelea “Mume wangu amekupa laki moja na huna kazi nayo yoyote. Nenda katoe elfu 70 na unipe. Alafu ole wako nisikie umemwambia Mjomba wako” Shangazi alimwambia Shaymaa ambaye hakutaka wala abishane nae. Alitoa pesa na kuhesabu Tsh elfu 70 na kumpatia kama ambavyo Shangazi alitaka na shangazi akachukua na kumtazama kwa jicho pembe “Kama unahisi viatu vinakubana, basi unaweza kuvua na ukatembea peku ama ukae chini na usitishe safari”

Shangazi aliongea na kuondoka zake na kumfanya Shaymaa amtazame na kujikuta akicheka mwenyewe “mpumbavu akipumbaa nawe pumbaa nae, akiingia mwituni basi unaachana nae” shaymaa aliongea na kumchukulia Shangazi ni mpuuzi kama walivyo Wapuuzi wengine na njia nyepesi ya kutoumizwa na Mpuuzi ni kufurahia upuuzi wake

Hakuitaji Mtu amshikie bakora kuweza kutambua kama Shangazi hakuwa Mtu mwema kwake. Aligundua kuwa Shangazi amechukizwa na kuwepo kwake pale “Napaswa kuishi kwa tahadhari, sipendi kuona ndoa yao inavunjika kwa sababu yangu” Shaymaa aliongea na kuona kupitia ile Tsh elfu 30 aliyopata basi ni bora aanzishe biashara ambayo itamfanya hawe busy kuliko kushinda nyumbani na kugombana na Shangazi.

Shida ilikuwa ni biashara gani anaweza kufanya ambayo itamuweka busy nayo tofauti na kushinda nyumbani na ukizingatia pesa aliyokuwa nayo ilikuwa ni ndogo na ilikuwa ngumu kwake kupata wazo la biashara.
                           *****
Jack na wenzake waliweza kuondoka huku Irina akiwasindikiza na kumuacha Abdul akiugulia maumivu.

“Samahani sana Jack, naomba muomzoee Mume wangu kwa maana ni Mswahili sana” Irina aliongea na marafiki zake huku Jack akionekana kuchukizwa “Ilikuaje Mjanja kama wewe unaenda kuolewa na Mshamba kiasi kile? Au umepagawa na hiki ki ghorofa chake?” Jack aliongea huku Mlinzi akiwa anawasikiliza na kujifanya kama amewapotezea

Baada ya kutoka kuwasindikiza Irina alirudi ndani na kumkuta Abdul akiwa amekaa kwenye dressing table akijitazama jicho lake. Shaymaa alirudi na hakumuongelesha kitu Abdul na badala yake alifika na kufungua kabati na kubadilisha nguo ambazo alionekana kama Mtu ambae alikuwa anataka kuondoka. 

“Wapi unaenda?” Abdul alimuita Mkewe baada ya kumuona anafungua mlango anataka kutoka “Naenda kwetu Abdul, hivi unafikiri labda umenitoa mtaani tu? Hivi ndugu zangu watafurahia unyanyasaji ulionifanyia leo mbele ya marafiki zangu? Ujisikii Aibu Mume wa Mtu kupigana na Mwanamke ambae ni Rafiki wa Mkeo?” Irina aliongea na Abdul alikaa kimya hakuwa na sababu ya kujitetea mbele ya Mkewe 

“Lakini Irina, ni Marafiki wa aina gani umewaleta nyumbani kwangu? Nikiwa kama Mume wako siwezi kuruhusu kuwa na Marafiki ambao hawastahiri kuwa na Mke wa Mtu, Tazama yule binti aliyekuwa anavuta bangi, kweli amethubutu kupigana na mimi tena nyumbani kwangu?” 

Abdul alijaribu kujitetea lakini mbele ya Irina alionekana dhairi kuwa alikuwa na makosa na hakupaswa kufanya alichowafanyia marafiki zake

“Samahani Mke wangu, najua nimekukosea nakuhidi sitarudia tena” Abdul alimuomba samahani Irina na kosa kubwa amabalo irina amefanya ni kumuonesha kuw anampenda kupita kiasi hivyo na Irina aliweza kutumia udhaifu huo ili kumuendesha

“sawa nimekusamehe ila kamwe usije ukarudia tena, na ukiendelea kuwa na tabia yako ya gubu na wivu wa kipuuzi basi kaa ukijua sitaendelea kuwa nawe” 

Irina aliongea na kunyamazishwa na mlio wa simu yake ambayo ilikuwa inaita. Alichukua simu na kuitazama na kushindwa kupokea na kubaki akimtazama Mumewe. “pokea simu taadhali” Abdul alimwambia na Irina alishusha pumzi ndefu na kumtazama Mumewe na hasijue nini afanye na mwishowe akaamua kuikata hiyo simu
                                 *****
Akiwa chumbani kwake anatafakari ni vipi anaweza kufanya bishara, ghafla alisikia tena mlango wake ukiwa unagongwa. 

Shaymaaa alichukia kwa sababu alijua fika kuwa ni Shangazi ndie aliyekuwa anagonga mlango.

“Shangazi unaweza kuniacha tafadhali? Si nimeshakupa pesa au kuna kingine ulikuwa unaitaji kutoka kwangu?” Shaymaa aliongea na Mjomba alikohoa kidogo na kuita. “Hapana ni Mimi” Shaymaa alistuka na kujitanda vyema kabla ya kufungua mlango na sura yake ikatawalia na tabasam zaidi “Feisaaaal” Shaymaa aliita kwa sauti na kumkumbatia kwa nguvu baada ya kumuona Feisal.

“Haya nimekuletea Mumeo wa maisha ili uzungumze nae, utanisamehe kwa kuwa mbea maana ni mimi ndie niliyemwambia kuwa hupo nyumbani kwasasa”

Mjomba aliongea na kumfuraisha Shaymaa ambaye alimtazama Feisal kwa sekunde kadhaa na kumkumbatia tena. Na mjomba aliamua kuondoka na kuwapisha.

LISAA LIMOJA KABLA
Mjomba alikuwa ni Mtu fulani mwenye hekima na busara, alijua fika kwa hali ambayo Shaymaa yupo nayo alipaswa kuwa na Mtu ambae anaweza angalau kumfanya asahau matatizo yake kwa kiasi fulani. Alichukua simu yake na kupiga namba fulani 

“Shikamoo Baba” Sauti ilisikika kutoka upande wa pili wa simu baada ya kupokelewa “Naitaji kuonana na wewe haraka” Mjomba aliongea pasipo hata kuitikia salam, hali ambayo ilimstua mpaka Feisal “Kuna tatizo?” Feisal aliuliza na mzee alimjibu “Inaamana mimi sipaswi kuonana na wewe mpaka kuwe na tatizo?” Mjomba aliuliza na Feisal alitihi haraka na kuahidi kuwa anakuja na wakapanga ni wapi wakutane.

Hakupenda kabisa kumkwaza Baba yake, na akikumbuka alimpotoa kwake alikuwa ni zaidi ya baba. 

Baada ya Feisal kufiwa na wazazi wake kwa ajali ya gari na kukosa malezi kutoka kwa ndugu na kujikuta ametelekezwa, aliyekuwa rafiki wa Baba yake alichukua jukumu la kumlea na kumsomesha kama Mtoto wake wa kumzaa na siku zote Feisal alikuwa alikuwa akimuona Mzee Majiliwa ni zaidi ya baba yake Mzazi.

Feisal alilelewa na Mzee Majaliwa na alikuwa akimuita Shaymaa Binam na alikuwa rafiki yake wa utotoni na kila Shaymaa alipokuwa anakuja likizo kwa Mjomba basi rafiki yake mkubwa alikuwa ni Feisal ambaye walikuwa wakitaniana Mke na Mume.

“Mkeo ana matatizo sana” Mzee majaliwa alimwambia Feisal baada ya kukutana nae. Hakutaka kumficha kitu, alimwambia kila kitu kuwa Shaymaa ameachika na kwasasa hayupo sawa ki saikoloji. Hivyo alimtaka atumie fursa hiyo anagalau kumfanya ajisikie huru
                           *****

Feisal alimtazama Shaymaa na kumwambia “Naitaji nikutoe out nenda kavae na tutoke” Ilikuwa ni kauli ambayo hakuwahi kuisikia kwa muda mrefu sana.

Shaymaa alifurahi na kwenda kuvaa haraka na walitoka na Feisal katika moja ya mgahawa maarufu na kwenda kupata chakula.

Ilikuwa ni siku nzuri sana kwa Shaymaa kwani alipokuwa na Feisal waliongea na kufurahi na ilipofika sehemu ya udhuni Shaymaa hakuacha kulia na Feisal alimbembeleza na kumlaza kifuani kwake.

Ghafla shaymaa alimwagiwa kinywaji usoni na Mwanamke aliyeonekana kuchukizwa baada ya kuwakuta Shaymaa na Feisal wapo katika pozi ambalo hakupendezwa nalo “Malaya mkubwa wewe mwizi wa wanaume za Watu” Yule Binti alitukana na wakati huo wateja wote walikuwa wameacha kufanya kila kitu na waligeuka kuwatazama. Shaymaa alijisikia vibaya sana huku akiwa amejiinamia kwa aibu pasipo kuwa na jambo lolote la kujitetea. Aliona ni bora ainuke na kuondoka lakini alitulizwa chini na yule msichana “Kaa chini Malaya Mkubwa wewe” Yule Binti aliongea na kutaka kumchapa kibao lakini ghafla alidakwa mkono na kugeuka kumtazama ni nani aliyemdaka huku Shaymaa akiwa ameinama na kukinga mikono usoni ili kuzuia hasiumizwe usoni……………………

NINI KITAENDELEA? NI NANI HUYU ALIYEKUJA KUMSAIDIA SHAYMAA? JE HUYU BINTI NI NANI? NA KATOKA WAPI? LEO NATOA NAFASI YA WASOMAJI WANGU KUTOA JINA KWA MSHIRIKI HUYU ALIYEINGIA KWENYE STORY. UNADHANI NI JINA LA MWANAMKE AMBAO MARA NYINGI WANAKUWA WAKOROFI? JINA AMBALO LITAPATA LIKE NYINGI NDILO NITAKALO LITUMIA KWENYE STORY EPISODE ZIJAZO


Post a Comment

Previous Post Next Post