🔐 MAUMIVU YA NDOA (1----5) 😭😭😭😭


MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 01

Tafadhali simulizi hii ya mapenzi inayohusu Zaidi maumivu katika ndoa ni kweli inaumiza na kuudhunisha mno. Kama ulishawahi kuumizwa kwenye ndoa na una hisia za karibu naomba usisome simulizi hii. Ila kama utaweza kuvumilia basi soma kuna jambo unaweza kujifunza.

Neno NDOA siyo kitu kidogo kama uonavyo uchache wa herufi zake katika kuliandika na kulitamka. 

Ni ndoto ya kila Mwanadamu kuingia ndani ya ndoa kama maandiko na vitabu vya dini zote za Mwenyezi Mungu vinavyoamrisha katika Ndoa na kukataza Zinaa, ila wengi wetu Ndoa tunaichukulia kama jinsi ilivyo lakini niseme tu ndoa ni jambo kubwa ambalo linapaswa kufanyiwa mchakato na kuheshimika kama ambavyo limepata Baraka kwa kila upande.

Mshale wa sekunde ulikuwa ukisogea kuashiria masaa yalikuwa yanayoyoma na katika moja ya nyumba ya kifahari zilizokuwa katika mtaa ule ambao wanaishi Watu ambao kiuchumi walikuwa vyema kulionekana kupo kimya sana.

Ulikuwa ni usiku Mkubwa sana, ila ulitosha kuutambua Urembo wa Msichana aliyeonekana kuwa mpweke katika jumba lile la kifahari huku macho yake yakiwa yamekodoa katika saa uliyokuwa sebuleni na kuonekana kama Mtu aliyekuwa anazidi kuchanganyikiwa baada ya kuona ilikuwa imetimia saa saba na dakika 50.

“Eeeh Mwenye Mungu, tafadhali naomba umtumie malaika wa kheri Mume wangu ili aweze kufika salama hapa nyumbani” Aliinua ikono juu kumuombea Dua Mumewe ili arejee salama na kujipa moyo kuwa atakuwa njiani labda kuna jambo kidogo litakuwa limemtatiza

Alijitahidi kusubiri, hata mboni za macho yake zilipogubikwa na usingizi aliweza kujitahidi walau mume wake aweze kurejea na kumkuta yupo macho akimsubiri.

Masaa yalizidi kuyoyoma sasa ilikuwa imeshafika saa nane na nusu, lakini hapakuwa na dalili za Mume wake kurejea nyubani. Taratibu alishika simu yake ya mkononi na kujaribu kupiga namba ya Mume wake lakini wapi simu ilikuwa ikiita tu na Mume hakushika simu ya Mkewe.

Hofu ilizdi kutanda kwa mwanamke yule Mrembo aliyekuwa amevaa na kujifukiza vyema na nyumba nzima ilikuwa ikinukia uturi kwa lengo la kumfanya Mumewe atakaporejea nyumbani aguswe na furaha na kumuona Mkewe ni Mwanamke wa tofauti anayebadilika na kumvutia kila siku.

Taratibu alisogea katika meza ya chakula ambayo, ilikuwa imejaa maanjumati ambayo alikuwa amemuandalia Mumewe na sasa alitegemea Mume angerejea nyumbani mapema ili wapate pamoja chakula cha usiku. Lakini wapi vyakula vlikuwa vimsehapoa na radha kuwa imebadilika kabisa na hao hofu ilizidi kwa Bidada huyu na kujikuta akikaa chini na nguvu zikimuishia huku taratibu machozi yakiwa yanabubujika “Shaymaa upaswi kulia Mumeo yupo njiani anakuja, Mumeo amekuletea zawadi tafadhari jitahidi huwe na Subira” Masikini aliongea mwenyewe na kujifariji lakini haikuwa dawa ya kujizuia kulia na badala yake ilikuwa ni kama amebonyeza gia iliyokuwa imefungulia machozi Zaidi.

Kilio chake kilikatishwa na muungurumo wa gari aina ya prado v8 ambayo alikuwa akitembelea Mumewe na ghafla kilio chake cha udhuni kilitoweka na kujikuta akilia kwa furaha.

Alijongea mpaka dirishani na kuchungulia chini na kushuudia jinsi mlinzi alivyokuwa akimfungulia Mumewe geti na gari yake ikaingia ndani “Ni yeye Abdul wangu amerejea” Shaymaa aliongea na kujaribu kuonja vyakula haraka kuona kama bado vitakuwa na radha ili tu asimkwaze mumewe. 

Abdul liingia ndani huku akiwa amebeba mkoba na Shaymaa aliacha kila alichokuwa anakifanya na kwenda kumpokea Mumewe kwa heshima na adabu “Karibu nyumbani, Mume wangu” Alimkaribisha Mumewe huku akitabasam na kumtazama na Abdul alionesha tabasam la uchovu na kushukuru Asante sana” 

Abdul alimtazama mkewe kwa muda wa sekunde kadhaa kana kwamba kuna kitu alitaka kumwambia ila aliishia kuguna tu kisha akaamua kuingia chumbani kwao alifika na kujibwaga kitandani akionekana ni Mtu ambaye mwenye mazonge mno “Hapana upaswi kufanya hivyo” 

Shaymaa alimwambia Mumewe baada ya kumuona akiwa ameanza kulegeza kamba za viatu “Najua ni jinsi gani ulivyochoka Mume wangu, tafadhali naomba uniruhusu ili niweze kukusaidia kufungua kamba za viatu” Shaymaa aliongea kwa heshima na adabu na Saidi alimtazama na kutabasam kisha akamuonesha kwa ishara ya mkono kuwa anaweza kuendelea

Taratibu Shaymaa alijongea mpaka katika miguu ya mumewe na kuanza kulegeza kamba za viatu na kumvua viatu Mumewe huku Abdul akiwa anamtazama na kuonekana kuna jambo linamuumiza kichwa “Samahani sana Shaymaa” Abdul aliongea na kumstua mkewe aliyegeuka na kumtazama “Samahani ya nini tena Mume wangu” “Umekuwa ukinielekeza kila uchwao kuwa napaswa kuvua viatu kule chini kisha wewe utavichukua na kuweka sehemu maalum lakini kila siku nimekuwa mzembe wa kusahau” Abdul aliongea na kumfanya Shaymaa afurahi na kumwambia “Mwanamke anapoolewa anakuwa Mama wa watoto watakao zaliwa pia ni Mama wa Baba ambaye anatarajia kumzalia Watoto, hivyo wala usijali Mume wangu wewe ni kama Mwanangu”

 Shaymaa aliongea na alipomaliza kumvua viatu na socks na kuweka mahala panapohusika, alimuandalia taulo na kumuinua kwa upendo “tafadhali usiupe nafasi usingizi, twende ukaoge kisha tukapate chakula cha usiku mana hata mimi nilikuwa nakusubiri wewe tule pamoja” Shaymaa aliongea na aliumizwa na jibu jepesi kutoka kwa Mume wake. “nipatie taulo wewe nenda tu ukale mimi nimeshashiba”

Hakutaka kumuonesha Mumewe kuwa amechukizwa na alichomjibu na aliamini tu akiwa kama Mwanaadamu basi itakuwa ameteleza tu “Basi usijali Mume wangu kipenzi, kesho utakapopata wasaa utakula tu chukula nitakachokuwa nimepika”

Baada ya kuongea hayo, Abdul aliingia bafuni kwenda kuoga na kitu kilichokuwa kimemshangaza Shaymaa ni kumuona Mumewe anaingi bafuni na simu.

Masikini binti wa watu alishuka mpaka kwenye meza ya chakula na kutazama jinsi alivyomaliza ufundi wake katika kupika ili tu kumvutia mumewe, lakini wapi Mume ndio kwanza alimjibu kuwa ameshiba huko atokako tena amemjibu kwa urahisi kabisa.

Kijiko kilikuwa hakipiti mdomoni na chakula kiligoma kabisa kuingia na alijikuta akiangua kilio kama Mtoto mdogo “nakosea wapi mimi? Kwanini Mume wangu yupo hivi” Shaymaa alijiuliza lakini hakupata majibu kamili na kuamua kumuachia Mungu huku akimuombea Mumewe kwa Mungu hawe katika mstar ulionyooka
                          *****
Siku hiyo kwa Shaymaa ilikuwa ngumu kula na alilala bila hata ya kupata chakula na usingizi ulikuwa haupatikani kabisa. Muda wote Mwanaume alikuwa amekaa kitandani pasipo kulala akionekana akitafakari mambo

Shaymaa alitamani kukumbatiwa na Mumewe, alitamani kuambiwa maneno adhimu ya kumtia faraja, alimtamani sana Mumewe lakini wapi Mwanaume alionekana kutingwa na mbaya Zaidi hakupenda kumwambia Mkewe.

“Abdul tafadhali, naomba kuzungumza na wewe Mume wangu kama itakupendeza kufanya hivyo” Shaymaa aliinuka na kujitahidi kuongea na Abdul aliitikia na kichwa kumpa ishara aongeee “Kitu gani kimekubadilisha Mume wangu? Tafadhali kama kuna kosa naomba uniambie. Lakini sipendi jinsi hivi tunavyoishi” 

Abdul aliguna kumtazama Mkewe huku akisikitika “Shaymaa Mke wangu eeeh!! Mimi ni Mwanaume mjinga sana, siitaji kukwambia icho utakacho kwa sabau nahofia kukuumiza” Abdul aliongea na Shaymaa alizidi kutumia sauti yake ya madeko kumsisitiza mumewe aweze kumpa nafasi hiyo

“Niahidi kwamba hautonisamehe kwa huu upuuzi ninaotaka kukwambia” Abdul aliongea na kumshangaza shaymaa “Hapana Mume wangu wala usiseme hivyo, swala la kusamehe ni kawaida kwangu. Tutaishi vipi bila kusamehana?’ 

Abdul alimtazama Mkewe kwa sekumde kadhaaa na safari hii mpaka machozi yalimtiririka kwa jicho moja, kisha aliushika mkono wa Shaymaa na kumtazama usoni “Shaymaa Mke wangu nakuomba sana unisamehe kwa hiki nikwambiacho maana mimi ni Mwanaume mpumbavu sana” Aliongea na kumeza mate kidogo “Naomba uridhie hli nikupe talaka urejee kwenu”

Abdul aliongea na kumstua Shaymaa aliyekuwa amepigwa na butwaa kwa kauli ya mumewe “Unipe talaka?”…………

NINI KITAENEDELEA? USIKOSE SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI HII ASANTE.

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 02

SIMULIZI HII YA KUSISIMUA INA MAFUNZO MAKUBWA YA NDOA HIVYO KAMA UNA HISIA ZA KARIBU USISOME MANA UTAMIA MNO

Akika alikuwa ni Mwanamke mwelevu aliyepaswa kulipwa shehena ya upendo, upole na ukarimu wake haukustahili hata kidogo kupokea mshaara ambao Abdul aliona unafaa kumlipa.

Ilikuwa ni kauli kubwa kutoka katika kinywa cha Mumewe, hakika alijiona amefanya kila linalopaswa kufanywa na Mwanamke anayepaswa kuwa Mke wa Mtu, sasa inakuaje Mumewe anataka kumpa talaka?

Hilo ndilo swali ambalo lililokuwa limejirudia kichwani mwake, akika alikuwa anampenda Mumewe na hakutamani hata kidogo kuona ndoa yake inaweza kuvunjika tena katika mikono yake yeye mwenyewe.

Alivuta pumzi na kuziachia na kuhuruhusu ubongo wake kuchanganua maswali kazaa, lakini ilikuwa ngumu kuweza kuzuia hisia zake kwani wakati huu machozi yalikuwa yakibubujika machoni mwake na kila alipokuwa anajizuia kufanya hivyo alijikuta ndio kama alikuwa anayafungulia njia yatoke kwa wingi.

“Kuna kosa lolotea labda nimekutendea Mume wangu? afadhali naomba uniambie kwanini unataka unipe talaka” Hilo ndio lilikuwa swali pekee lililoweza kutoka kwenye kichwa cha Shaymaa. Abdul alishindwa kumtazama Mkewe na kujikuta akiinama na kusikitika kabla ya kumtazama tena na safari hii alionesha dhairi shairi alikuwa anamuonea aibu Mkewe “Unakumbuka kuwa nilisema usinisamehe kwahiki nitakacho kwambia?” Abdul alimuuliza Mkewe na Shyamaa aliitikia kwa ishara ya kichwa kuashiria kuwa anakumbuka huku masikio yake yakiwa makini kusikiliza ni nini ambacho Mumwe anataka kumwambia ambacho amemkosea na kinamfanya afikie maamuzi hayo mazito kwenye ndoa

“Shaymaa wewe ni Mwanamke mrembo sana, najivunia sana kukutambua kwani katika maisha yangu nimewahi kuona Mwanamke ambae anampenda mumewe kwa dhati. Kitu kimoja sikuwahi kukitambua ila nimetambua baada ya kukuoa wewe” Abdul aliongea usiku huo, huku Shyamaa akiwa makini kumsikiliza Mumewe ambae alianza kutoa walaka kwanini alikuwa anataka kumpa talaka. “Nimegundua unanipenda sana wewe na mimi sikupi hata robo ya kile unachonipa wewe, lakini kitu kibaya Shaymaa” Aliongea na kuvuta pumzi kidogo na kumtazama kwa umakini “Nimejikuta nimepoteza hisia na wewe yani kifupi tu sina mapenzi na wewe Shaymaa”

Safari hii kauli ya Abdul iliweza kuuchoma ipasavyo moyo wa Shaymaa tofauti na yeye alivyomaanisha labda “Samahani sana Mume wangu inawezekana Mimi kama Mwanamke kuna vitu sivifanyi kwa ufasaha kwako au labda inawezekana labda nimepoteza ufundi wangu katika kundaa chakula cha usiku tofauti na hapo hawali uliponio. Tafadhali naomba unipe nafasi walau nijirekebishe, nakuahidi utaona utofauti mkubwa kutoka kwangu, samahani sana Mume wangu kwa kutokugusa hisia zako tofauti na mwanzo tulipofunga ndoa yetu”

Shaymaa aliongea na Abdul alimtazama na kutabasam. Alimvuta kwake na kumkumbatia “Akika wewe ni Mwanamke mwelevu sana, kitu pekee usichokijua ni kwamba sipendi kukuona ukidondosha machozi mbele yangu tafadhali naomba ufute machozi yako” Abdul alimwambia Mkewe na haraka Shaymaa alifanya hivyo japokuwa ilikuwa ngumu mno kuyazuia machozi yasimwagike kutoka katika mboni za macho yake
Shaymaa alitumia wasaaa huo kuongea na Mumewe jinsi gani Mungu anavyochukia ndoa kuvunjika, hivyo yeye alikubali makosa yote ambayo amemkosea mumewe na kuzidi kumuomba msamaha kama vile aliambiwa anafukuzwa kazi na boss wake. Wakati akiongea hayo alisikia Mume wake anakoroma utafikiri alikuwa haongei na Mkewe 

Dakika kumi zilitosha kwa Abdul kupitiwa na usingizi utafikiri Mkewe alikuwa anaongea na Mtu mwengine na siyo yeye. Shaymaa alijaribu kumtazama Mumewe usoni na kutafakari kauli ambazo Mumewe alimwambia na kuna kitu kidogo kilimpa shaka “Hivi ni kweli Abdul alimaliza kuongea au aliamua kukatisha kwa sababu aliniona nalia sana na hapendi kuniona nikidondosha machozi?” Alijiuliza na kukosa majibu sahihi ya kwanini Abdul alikatisha maongezi na hata wakati yeye anaongea mwenzake aliuvuta usingizi na kukoroma.

“Mume wangu hana makossa na hajawahi kunikosea htaa siku moja, ni Mimi ndie mwenye makossa. Shaymaa hebu toka usingizini¬!! Unawezaje kukaa na kumtafakari Mumeo wakati shingo yako inapaswa kuwa kifuani kwake huku ukitumia kucha zako ulizobarikiwa kumfanya afurahie usiku wake” Mara nyingi alikuwa anapenda kujiongelesha Mwenyewe kama kuna Mtu alikuwa akiongea nae kichwani kwake na kweli alisogea alipo mumewe na kujilaza kifuani kwake huku akifanya kama ambavyo alijiambia kupitia kucha zake

“Shaymaa nashindwa kupumua, alafu itapendeza kama ukiniacha mwenyewe nilale sihitaji huo usumbufu wako tafadhali” Abdul aliongea kwa sauti furani ya kuchoka na Shaymaa wala hakusubiri aambiwe mara mbili, aliinuka na kusogea pembeni na kumuacha Mumewe apumzike kama ambavyo alivyoambiwa

“Amekuwa akiniambia hivi kila uchwao!! Hivi kweli naweza kurekebisha makosa yangu nikiwa kama sipewi nafasi?” Shaymaa alijiuliza huku akimtazama Abdul ambaye alikuwa hana hata habari masikini ya Mungu.

“Huwezi kumpata Mwanaume aliyekamilika hata siku moja, kila Mwanaume ana mapungufu yake hivyo unavyokubali kuolewa na Mwanaume basi kubali kuolewa na Mwanaume ambaye unahisi unaweza kuyavumilia mapungufu yake kama ambavyo wanaume wanavyotafuta mke. Mara nyingi utazama Mwanamke ambaye anahisi atamuoa na kumvumilia mapungufu yake” Shaymaa aliyakumbuka maneno ya Shangazi yake kwenye sherehe ya kumuaga nyumbani hivyo angalau alau alipata nafuu na kujikuta akirejea kitandani

“Inamaana Abdul kashindwa kuvumilia mapungufu yangu?” Shaymaa aliongea na alijikuta akijiuliza maswali mengi na kukosa majibu na aligundua kuwa Abdul alikuwa amelala vibaya, taratibu alimuinua ili kumuweka mto alale vizuri pasipo kumbuguzi.

Kwakuwa muda wa swala ulikuwa umefika, aliamka na kwenda kuswali na alipomaliza kufanya hivyo alianza kumuandalia kifungua kinywa mumewe na kumchagulia nguo za kazini alizoona Abdul akivaa anapendeza, alimnyooshea na kumuwekea vyema kisha taratibu alimsogelea na kumuamsha

Abdul alikurupuka na kutazama saa iliyokuwa ukutani na kuongea “Shaymaa Mke wangu buguza zako zimenifanya nichelewe kazini” “Samahani Mume wangu, nakuahidi kuwa nitakuwa mwangalifu kwako” Shaymaa alijibu kwa upole sana na Abdul aliingia bafuni na kwenda kuoga na alipomaliza kufanya hivyo alijifuta maji na kufungua kabati “Hapana upaswi kufanya hivyo, nimeshakuandalia nguo za kwenda kazini” Shaymaa aliongea na kumpatia nguo Abdul aliyeonekana kucheka “Shaymaa unapaswa ujifunze ni nguo gani ambazo napaswa kuvaa kwa wakati gani” Aliongea na kufungua kabati na kuchagua nguo aliyoitaka na kuvaa.

“Nimeshankuandalia kifungua kinywa twende ukapate kabla ujaondoka kazini” “Hapana nimeshachelewa nitakunywa huko niendako”

Abdul aliongea na kuondoka zake utafikiri alikuwa anaongea na Dada yake au Mtu wa kawaida “Mume wangu” Shaymaa alimuita na safari hii Abdul alichukizwa kidogo ila hakutaka kumuonesha mkewe ila sura ilisema tu kama hakupendwa kuitwa tena na Shaymaa.

Alimsogelea Mumewe na kumuweka vyema tai yake kisha akamwambia “nakutakia kazi njema na huwe mwangarifu jamani si unajua Mkeo sipendi nikuone hata umeumia?” Kisha akambusu na kumuaga lakini Abdul hakujibu kitu na alionekana akufuraia hata kidogo yote aliyoambiwa na Mkewe.

Ndoa nyingi huwa zinapotezaga upendo na kuwafanya Watu waishi kwa mazoea kwa sababu ya kutozingatia vitu vidogo au Watu wengi kutokuwa na kauli thabiti mbele ya wenzi wao nah ii upelekea baadhi ya watu kukata tamaa na kumua kukaa kimya kwani utakuta Mtu anaona hata nikimfanyia nini Mwenzangu yeye uchukulia kawaida.
                           *****
Kama ilivyokawaida Abdul alikataa kula asubuhi na kumuacha Mkewe akiwa na maswali kibao lakini hakutaka kujaji sana kwani aliamini Mumewe alikuwa amechelewa kwenda kazini.

Siku hiyo alipania kuanza shughuli kubwa ya kurejesha hisia za Mumewe kwake kwani aliambiwa na Mumewe kuwa amejikuta tu hana Hisia nae.

Shaymaa alifanya kila kitu alipika chakula kizuri akipendacho Mumewe, alivaa nguo nzuri ambazo aliamini Mumewe akirudi atamuona urembo wake na alipania na kujiambia mwenyewe kama kawaida yake “Abdul leo akirudi na kusema ameshiba basi jitahidi ale walau kijiko kimoja ili tu aonje ladha adimu ya mapishi yako” Shaymaa aliongea mwenyewe huku akifurahi lakini furaha yake alisitishwa na mshale wa sekunde kusonga mbela na hapakuwa na dalili za Abdul kurejea.

Mara kadhaa alijaribu kupiga simu yake lakini ilikuwa haipokelewi. “Shaymaa piga tena” alijiambia mwenyewe na wala hakujishauri Zaidi na kujikuta akipiga tena “Hallow” sauti nyororo ya Mdada ilipokea simu ya Abdul na kumfanya Shaymaaa apigwe na butwaaa!!

NINI KITAENDELEA? USIKOSE KUSOMA SEHEMU YA 03 LABDA IAKUWA NA MAJIBU SAHIHI

KUMBUKA UNAPOLIZA KUSOMA BASI LIKE KISHA WEKA COMMENT YAKO NA MTAG MWENZAKO. LIKE YAKO NDIO UFUNGUO WA EPISODE IJAYO.

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 03

Sauti nyororo ya Mwanamke ilisikika kutoka upande wa pili wa simu na kumfanya Shaymaa apigwe na butwaa akiwa haamini kile alichokisikia “Simu ya Mume wangu imepokelewa na Mwanamke” Alijikuta akijiuliza mwenyewe kichwani

“Samahani mwenye simu amesahau simu yake hapa Misosi Lounge, hivyo kama una mawasiliano nae mengine Mwambie aje kuchukua simu yake” Yule Mwanamke aliendelea kuongea na kumfanya Shaymaa apate afueni kidogo

“Misosi Lounge?” Shaymaa alistuka na kumuuliza na yule Binti aliendelea kumueleza kuwa Abdul walikuja kupata chakula cha usiku na hapo ndipo aliposahau na kama akimuelekeza basi atajua wapi alipoangusha simu.

Kutokana na maelezo ya yule Msichana aliyepokea simu ya Abdul, ilitosha sana kwa Shaymaa kugundua kuwa Mumewe alienda hapo Misosi Lounge kupata chakula ila hakuwa Mwenyewe

“kwanini anaenda kwenye mgahawa kupata chakula cha usiku wakati Mkewe nipo na kupika najua?” Swali la kwanza kujiuliza lilikuwa ni hilo lakini alijikuta tu akijiongeresha Mwenyewe “Itakuwa ni Boss wake upenda kwenda hapo hivyo anaitaji kampani ya Mume wangu. Inamaana Boss wake nae hajaoa ama ana tabia za Abdul hapendi kula kwa Mkewe?”

Unadhani ilikuwa ni rahisi kupata majibu Zaidi ya kujikuta akichanganyikiwa na wivu ulianza kumshika taratibu “Inamaana Abdul kwenye simu yake hajasave namba yangu kama Mimi Mke wake? Na kama amesave hivyo mbona huyu Dada hajanitambua na amepata tabu sana kunielekeza?”

Kabla hajajiuliza Zaidi alisikia muungurumo wa gari na alipotazama saa ya ukutani ilikuwa ni saa 9 kama kawaida yake aliyoanza kwa siku za hivi karibuni

“Karibu nyumbani Mume wangu, pole na uchovu wa kazi” Shaymaa aliongea na kumsogelea Abdul aliyekuwa amestuka kumkuta Shaymaa yupo macho “Hivi hauoni kama unajitesa? Yani hupo nyumbani unashindwa kulala unakaa na kunisubiri Mimi kweli?” Abdul aliongea huku akimtazama kwa mshangao “Hapana wala siteseki Mume wangu, huu ni wajibu wangu, lakini na wewe wajbu wako ni kujitahidi kurudi nyumbani mapema kama inapobidi ila kama utakuwa unabanwa na kazi basi mimi nitakuwa nakusubiri mpaka nikuone”

Shaymaa aliongea na kumfanya Abdul amtazame na kusikitika kisha akamwambia “Sawa kama unaona inafaa kukaa macho mpaka sahizi” Aliongea na kutaka kupandisha ngazi lakini Shaymaa alimshika mkono “Utakula kwanza kisha ndio uoge au utaoga kwanza ndio ule” “Aaah Sifanyi chochote kati ya hayo, nimeoga kazini pia sijisikii kula chochote naomba niache nikalale sijiskii vizuri nimechoka”

Abdul aliongea kama kawaida yake na leo Shaymaa alimshika mkono huku akimtazama kwa uchungu na chozi la uchungu alijikuta tu likimdondoka “Kwanini lakini Mume wangu unanitendea hivi?” Unajua ni vyema ukaniambia kosa langu kuliko adhabu unayonipa? Abdul siwezi Mimi, nasema siwezi Abdul tafadhali naomba unisamehe kwa kosa lolote ambalo nimekukosea, tafadhali Mume wangu!!” 

Masikini Shaymaa alilia na kuomba msamaha pasipo hata kujua nini amekosea ila alichokuwa anakitaka kwa Mume wake ni kumuona anaishi kama Mume wa Mtu na siyo kama Muhuni fulani ambaye ufanya chochote anachojisikia kwa sababu hakuna wa kumuuliza wala wa kumfanya ajali kuhusu yeye.

Unawezaje kula katika migahawa hali ya kuwa umeoa? Unawezaje kuzulura mpaka saa 9 za usiku huku nyumbani kwako umemuacha Mtoto wa watu amekaa roho juu akiwaza kuhusu wewe alafu wewe hata hujali eeeh?

Siku zote alikuwa anajificha hasionekane kama anaumia lakini leo ilikuwa ngumu kufanya hivyo na alijikuta akilia kwelikweli huku akijizuia kutoa sauti lakini alilia mpaka alikaa chini. Abdul alimtazama Mkewe jinsi anavyolia na kumuonea huruma. Alimsogelea na kumuinua.

“Twende tukale chakula Mke wangu” Alijikuta akiongea huku akiwa amemkumbatia Mkewe na kumfanya Shaymaa asisimkwe na mwili. “Unakumbuka siku ya kwanza nilipokutana na wewe?” Abdul aliongea na Shaymaa aliitikia kwa kutikisa kichwa kuashiria anakumbuka “Nilibahatika kuliona tabasam lako. Hata katika ile picha yetu kubwa ya harusi tuliyoiweka kule chumbani kwetu, inaonesha ni jinsi gani ulivyo Mrmbo pale unavyotabasam” Abdul aliongea na kumuita jina lake Mkewe na Shaymaa akaitikia na kuinua paji lake la uso na kumtazama huku macho yake yakiwa yamebadilika utafaikiri amekula kungu manga kumbe wapi macho yalikuwa yamevilia kwasababu ya kilio

“Binafsi napenda kukuona ukifurahi Zaidi kuliko ukilia. Kwa maana ukifanya hivyo huwa unapoteza haiba yako. Leo naomba tule sote, japokuwa nimeshiba ila nitafanya hivyo kwa ajili yako. Kisha tutaenda bafuni kuoga pamoja na masaa kadhaa yaliyobaki tutayatumia kuongea Mimi na wewe kama Mke na Mume”

Abdul aliongea na Shaymaa wala hakuweka pingamizi na walijongea pamoja mpaka katika meza ya chakula ambavyo Shaymaa alikuwa ameandaa kwa ajili ya Mume wake na alifanya yote haya ili kufuta makosa yake na akiweza ashike hisia za Mumewe kama ambavyo alitoka kuambiwa jana na Abdul kuwa hana hisia nae

“Ladha yake ni nzuri sana, akika wewe ni mbunifu katika swala zima la mapishi. Chakula chako kitamu unajua sana kupika na kwakweli sijawahi kula chakula hiki popote Zaidi yako na sijaona Mwanamke anaejua kupika akakufikia hata robo ya upishi wako”

Abdul alimsifia na Shaymaa alitabasam kidogo na kuguna kabla ya kushukuru “Asante Mume wangu kama na mimi najitahidi kwenye kupika”

Kuna wakati Mtu unapaswa kujua kitu gani mwenzako anapaswa kupewa na kwa wakati gani na ukifanya hivyo unaweza kuwa umeshika ufutio utakaoweza kufuta makosa yote yatakayokuwa kwenye moyo wa mwenzi wako.

“Hivi ni kweli Mimi najua kupika kuliko wapishi wa Misosi Lounge?” Shaymaa aliuliza na kumfanya Abdul abadilike na jicho lilimtoka utafikiri Mtu aliyesikia habari ya kutisha “Misosi Lounge? Wewe umepajuaje huko?” Abdul aliuliza na kuonesha kuchukizwa na habari ya Mkewe kujua kuhusu Misosi Lounge

“Nimejua baada ya kupiga simu yako na ilipokelewa nikajibiwa kuwa umeangusha kule mlipoenda kupata chakula” Shaymaa aliongea na Abdul alistuka na kujisachi na kweli aligundua kuwa amepoteza simu. Alimuuliza maswali kadhaa na kudadisi ili ajue kama Mkewe kuna kitu chochote anakijua kuhusu Misosi Lounge lakini aligundua kuwa hakuna ubaya wowote alioambiwa “Ni kweli kuna Rafiki yangu alikuwa na kikao pale hivyo aliniomba niwe nae”

Abdul alijitetea lakini Shaymaa hakutaka kujua Zaidi kuhusu Misosi Lounge na badala yake alijitahidi kumuonjesha vyakula vyake huku akimuuliza kuhusu ladha yake na lengo lake Zaidi lilikuwa ni kumfanya mumewe ajisikie huru  

Kweli siku hiyo kwadakika kadhaa walifurahi kwa kula pamoja na kwenda kuoga pamoja huku Shaymaa akimuomba Mumewe amsugue mgongoni na kweli Abdul alifanya hivyo. Kiukweli ilikuwa ni raha isiyo kifani na hayo ndio maisha ambayo Shaymaa alitamani waishi na mumewe angalau kila siku
                         *****
Baada ya kumaliza kuoga walikaa kitandani na Abdul alimuomba Shaymaa amsikilize kwa umakini sana “Kiukweli sitaacha kukupa sifa zako ulizobarikiwa na Muumba kuwa wewe ni Mwanamke mrembo, mkarimm na mwelevu, hakika unastahili kuwa Mke wa Mwanaume yoyote atakayetambua na kuheshimu sifa zako. Shaymaa tafadhali naomba unielewe” Abdul aliongea na Shaymaa alikuwa makini kumsikiliza Mumewe ambaye alikuwa anaongea kwa utulivu pasipo hata kumtazama usoni.

“Nitafurahi tu endapo utaraidhia ombi langu la mimi kukupa talaka” “Yani badala ya kuudhunika Abdul unasema kuwa utaurahi kweli? Kosa langu nini mpaka uniache Mume wangu? Hebu niambie nini ninachokosea mana Mimi ni Binaadam sijakamilika Abdul” 

Ilikuwa ngumu kidogo Shaymaa kumuelewa Abdul na kikubwa mno yeye alikuwa anakimbilia kwenye makosa, alihisi labda kuna jambo atakuwa amemkosea Mumewe na hataki kumwambia hivyo alimuomba sana walau apate kujua.

Ni kweli katika maisha tunapaswa kujishusha lakini wakati mwengine unapaswa kusimamia haki yako katika njia iliyonyooka ili tu kupata kile unachostahili kukipata lakini ukikimbilia njia ya kujikosoa pasipo hata kukosolewa basi kaa ukijua kuwa Watu watatumia Mwanya huo ili kukuadhibu

“Nitakuwa Mnafki endapo nitadanganya kuwa wewe umenikosea Shaymaa!! Hebu kwanza naomba utoke katika ukurasa huo na nataka utulize masikio yako na unisikilize. Sifa ulizo nazo wewe, mimi nafikiri haukustahili kuolewa na Mwanaume kama Abdul. Sihitaji kabisa kukuona nakuumiza, kuliko kudhurumu upendo wako wa dhati unaonipa basi ni vyema nikakupa talaka. Naamini Mungu anaweza kukutanisha na Mwanaume Mwelevu Zaidi atakayetambua na kuthamini upendo wako kwake ila kwangu kwa lolote utakalonifanyia itakuwa ni bure tu, tena mara nyingi naona kama karaha kwangu”

Angalau Abdul aliweza kufunguka na Shaymaa aliweza kumuelewa sasa nini alichokuwa anamaanisha ila alikuwa kama Mtu fulani anayezunguka Mbuyu wakati njia anaijua “Unataka kuniambia kuwa hauna mapenzi na Mimi?” Shaymaa alipata moyo furani wa kike na alijikaza kama Mwanamke na kumuuliza huku akiwa anamtazama kwa umakini

“Asante sana kwa kunielewa! Kwakweli najitahidi kukupenda lakini najiona kabisa ni kitu ambacho akiwezekani kwangu kwa sasa, tofauti na hapo hawali” Abdul hakutaka kupindisha hata mstari mmoja na kauli yake ilimfanya Shaymaa akae sawa na kumtazama Zaidi na ukimya ulipita wa sekunde kadhaa kabla hajamuuliza “kwanini ulinioa? Au nilikulazimisha uje kunioa? Kilichokufanya mwanzo unipende na kunioa ni kipi na kinachokufanya upoteze mapenzi na mimi kwa sasa ni kipi?” Maswali ya Shaymaa yalimfanya Abdul ashushe pumzi na kumtazama na safari hii aliongea taratibu Zaidi “samahani sana Shaymaa naomba usije ukanisamehe kamwe, kwa muda wako niliokupotezea ila kiufupi tu nilikuoa kwa bahati mbaya”

Kauli ya Abdul ilimfanya Shaymaa apoteze ule ukakamavu aliokuwa amejipa kwa dakika kadhaa kama Mwanamke na chozi la uchungu lilimtoka huku akiwa anatetemeka na kujikuta akitaka kulia na aliupeleka mkono wake wa kuume mdomoni ili kujizuia kutenada icho ambacho Abdul alimwambia hapendi kumuona anakifanya.

“Nimegundua hayo kuwa wewe siyo Mwanamke wa aina yangu Baada ya Mimi Abdul kuweza kupata Mwanamke Mwengine Anayeitwa Irina. Na mara kadhaa nimekuwa nashindwa kumdanganya huyu Mwanamke. Yeye ndie aliyenizoesha kwenda kula pale Misosi Lounge kwani yeye ndio Mmiliki wa Mgahawa ule. Na mara kadhaa unaponiona nachelewa kurudi basi huwa namsubiri mpaka pale watakapofunga biashara kisha tunaenda nyumbani kwake na mimi ndio Napata wasaa wa kurudi nyumbani. Nampenda sana Irina nahisi ndio Mwanamke wa Ndoto zangu”

Sidhani kama Abdul aliweza kuhisi hata chembe ya maumivu ambayo Shaymaa aliyopitia kwa sekunde kadhaa tokea alipoanza kuzungumza kuwa amepata Mwanamke mwengine. Ilikuwa ngumu kwa Shaymaa kuweza kukizuhia kilio maana ndio njia pekee iliyobaki ya kutoa maumivu yaliyokuwa moyoni na hakuwa na jinsi Zaidi ya kulia mfululizo¬¬¬¬¬¬¬¬!!

Yani Mtu amekuoa kwa furaha zake tena yeye ndie aliyekuja kukuchumbia nawe ukamtazama ukajibu yes nipo tayari kuolewa nae na mkafunga ndoa na kusherekea harusi leo anakwambia alikuoa kimakosa, na yupo Mwanamke wa ndoto zake ambaye amebahatika kukutana nae baada ya kufunga ndoa na wewe hivyo anakuomba akupe talaka na kwakuwa wewe ni Mwanamke mwelevu basi utapata Mwanaume bora Zaidi yake kweli? Yani kirahisi hivyo?

Daaaaah!! Mpaka Huruma ebwana eeeeh Kwa leo naomba tuishie hapa mpaka wakati Mwengine Mungu atakapotupa uzima na wasaa wa kumaliza masaa ya kuwa kwenye laptop basi nisema USIKOSE SEHEMU YA 04 YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA YENYE MAFUNZO MENGI NDANI YAKE. MSHTUE NA MWENZAKO MWAMBIE TUMEWASHA MOTO HUKU

MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 04

Yupo wapi Mtu aliyewahi kusema Mapenzi ni hisia zinazoumiza lakini hazichoshi? Ukimuona huko alipo basi jaribu kumpa kongole

Neno Mapenzi kila Mmoja ameweza kulidadavua kwa jinsi ajuavyo na kuleta michangunuo tofauti kwa vile aonavyo yeye inafaa. Hata Mama zetu zamani walikuwa wakiandika jumbe tofauti kwenye sehemu tofati wakijaribu kuyazungumzia mapenzi. Wapo waliowahi kuandika Penzi ni kikohozi kukohoa uwezi, na wengine walifika mbali na kusema “Ndoa ni sawa na kutia mkono gizani utoke na Mume au utoke na Shetani”

Ilikuwa ni tarehe 13 siku ya jumamosi mwezi wa pili yaani siku moja tu kufika maazimisho ya siku ya wapendanao Duniani kama wenyewe wasemavyo. Shaymaa aliumia sana, kila wasaa alipokuwa anamtazama Abdul aliyekuwa hana cha kufanya mbele yake zaidi ya kumtazama kwa aibu na kujiinamia kwa upuuzi wake aliotoka kumwambia. Sauti ya kauli yake mara kadhaa iliweza kujirudia katika kichwa cha Shaymaa huku akiwa haamini kama Mwanaume aliyemuoa miei michache tu iliyopita tena wakiwa hata hawajafaidi ndoa yao leo anaweza kumwambia kuwa alimuoa kwa bahati mbaya

“Tafadhali naomba ulale Shaymaa kwa sababu hivyo unavyolia naona kama unajiumiza zaidi” Abdul alimwambia Shaymaa aliyekuwa anamsikiliza huku akiendelea kulia Mtoto wa watu “Abdul wewe lala tu Mume wangu kipenzi wala usijali, kwa maana kulia kwangu Mimi ndio kuondoa sumu kubwa iliyokuwa moyoni mwangu”

Shaymaa aliongea na Abdul wala hakusubiri mara mbili, aligeuka upande wa pili na kujifunika shuka “Unaweza kunizimia taa?” Abdul aliuliza na Shaymaa alimjibu kwa vitendo kwa kuizima taa

Shaymaa wala hakuitaji kukaa kitako na yeye, alichukua Mto na kuegamiza kichwa chake na kulala kwa kutazama juu, huku kilio cha kwikwi kilichokuwa kimeambatana na maumivu makali kiliendelea kusikika katika masikio ya Abdul

Wakati fulani kama Binaadam aliweza kujisikia vibaya sana kwa jinsi ambavyo Shaymaa alikuwa analia. Aligeuka na kumtazama na kuongea kwa utulivu wa hali ya juu “Samahani sana Shaymaa akika mimi ni Mwanaume mbaya sana ambaye sipaswi kusamehewa hata kidogo” Abdul aliongea na alipata majibu tofauti kutoka kwa Shaymaa tofauti na alivyotegemea yeye “Abdul samahani naweza kulala kifuani kwako?” Ilikuwa ni sauti ya upole ambayo imehisi upweke na kumfanya Abdul amuonee huruma na kumvuta mpaka kifuani kwake

Kilio alichokuwa amelia kwa muda mrefu kiliweza kupandisha joto la mwili na kumfanya Shaymaa apatwe na homa za usiku na kiasi fulani alikuwa akimuunguza mpaka Abdul.

Aliinuka na kumimina maji kwenye grass na kumpatia “Mwili wako unaunguza sana tafadhali kunywa maji” Abdul alimwambia huku akimpa maji Shaymaa aliyegunda kama sekunde kadhaa kumtazama na kujiuliza maswli kwenye kichwa chake ”Nini kimekupata Abdul wangu mpaka umeangukia kwa Wadada wa Mjini?” Alijiuliza na kupokea maji na kunywa kidogo na Abdul alimsisitiza anywe zaidi na Shaymaa alifanya hivyo na vitendo vyake vya kumuonesha kuwa anamjali, ndivyo vilikuwa vikimuumiza zaidi Shaymaa japo angalau alijisikia faraja kwa Mumewe kumjali lakini aliumia kuona kuna Mwanamke anaitwa Irina anakuja kuchukua nafasi yake.

Baada ya Shaymaa kupata maji kidogo walirudi kulala huku Abdul akiwa amemkumbata Shaymaa na kujifunika shuka nusu “Sipendi kukuona ukiwa unalia hata kidogo” Abdul aliongea na Shaymaa alishangaa mwenyewe na hapo aligundua kuwa siku zote Abdul amekuwa akiongea hivyo lakini hakuwa akimaanisha “kama kweli hapendi kuniona nikiwa nalia, kwanini yeye ndio ananiliza?” Shaymaa alijiuliza Mwenyewe na kuishia kunyamaza pasipo kuongea chochote”
                              *****
Kwakuwa jana walichelewa kulala na muda mwingi Shaymaa alikuwa analia, hivyo usingizi ulivyompitia ulimpitia haswaa. Alipokuja kukurupuka usingizini alikuta Abdul ameshaondoka nyumbani.

“Ameondoka pasipo kuniamsha? Hivi ndio anamuwahi huyo Irina?” Shaymaa aliamka na cha ajabu alikuta Abdul akiwa amemuandalia kifungua kinywa na kumuandia kijimemo alichokuwa amekiweka mezani “Samahani kwa kile kilichotokea jana, hata hivyo sikuwahi kujua kama unakoroma sana, unajua jana nimeshindwa kulala kabisa tokea ulipopata usingizi? Fungua simu kuna video yako”

Abdul aliandika na Shaymaa hakuitaji kusubiri, haraka alifungua simu yake na kukuta video kweli Abdul amemrekord wakiwa wamelala na Shaymaa anakoroma. Kisha akamtumia vichekesho tofauti na kumfanya kwa kiasi furani Shaymaa afurahi mno “Abdul bana inamaana unaniloga alafu unanitibia mwenyewe?” Shaymaa aliongea baada ya kuona vituko vya Abdul kwenye simu.

Akiwa anaendelea kufurahi huku akipata kifungua kinywa mara ujumbe uliingia katika simu yake “Chini ya sahani iliyokuwa na mayai kuna ujumbe wako” Abdul aliandika na Shaymaa aliinua haraka sahani ili aone Abdul kaandika nini? Huku akiamini labda Abdul anaweza kuwa ameshabadilika kwa kiasi fulani

Haikuwa karatasi ya ujumbe mfupi bali ilikuwa ni barua ambayo juu ya bahasha Abdul aliweka picha yao ya ndoa lakini ikiwa imechanwa sehemu ya Abdul. Shaymaa alistuka na kujiuliza “anamaanisha nini kuchana picha hii ya ndoa?” 

“Hawali ya yote natumahi utakuwa umefurahia kifungua kinywa nilichokuandalia, wala usishangae kuniona nimepika kwa maana mimi ni mpishi mzuri sana sikuhizi” Shaymaa alichana bahasha na kuanza kusoma barua ilivyokuwa ndani yake

“Ningependa kuchukua fursa hii ya kipekee kukutaka radhi kwa kile ambacho kimetokea jana, unajua kiukweli jana ulilia sana kiasi ambacho nilikuonea huruma mno. Ila Shaymaa eeeh!! Mimi sipendi hivi ninavyokutendea tafadhali naomba uridhie nikupe talaka”

Ilikuwa ni barua iliyaharibu kabisa furaha yake na kujikuta akiichanachana na kuitupa psipo hata kuimaliza kuisoma “Sitakubali kuweza kukupoteza Abdul labda itokee nikiwa nimetangulia mbele ya haki. Ila kwakuwa mimi ni mzima, basi nitaakikisha napambania ndoa yangu mpaka inakaa katika mstari ulionyooka

Shaymaa aliongea mwenyewe na kujiaminisha kuwa lazima ataakikisha kuwa Abdul anakaa salama usalimini katika himaya yake. “Lazima nimjue huyo Irina ni Mwanamke wa aina gani” Shaymaa aliongea Mwenyewe na kuonekana kupania nini cha kufanya
                          *****
Baada ya kukaa na kutafakari aliona ni bora amtafute Irina ili aweze kujiakikishia mwenyewe na kumuona huyo Irina alikuwa ni Mwanamke wa aina gani ambaye anaweza kumchukulia Mumewe

Asikwambie Mtu ndugu yangu siyo kila ukimuona chizi mapenzi basi ukajua amelogwa hapana, wengine wamevulugwa na kuchanganywa na wapenzi wao ambao waliwapenda ikapitiliza. Shaymaa alichukua kadi yake ya bank na kutoka zake na kuelekea mjini kwenda kuitafuta Misosi Lounge ilipo ili tu apate kumuona huyo Irina Mwanamke anayechanganya kichwa cha Abdul mpaka anataka kumpa talaka.

Alijua fika mida hii ya mchana mchana basi Abdul lazima atafika eneo lile kuja kupata chakula. Alichokifanya Shaymaa ni kuvaa juba lake na kuficha sura yake ili hasijulikane na kuelekea mawindoni kwenda kumuwinda Mume ”Naomba nipeleke Misosi Lounge” Shaymaa aliongea na kupokelewa na tabasam lenye bashasha kutoka kwa dereva wa bajaji kwani siku hiyo hakutaka kabisa kutoka na gari yake “Oooh unataka kwenda wa Dada Irina? Bila shaka sahizi unaenda kupata mchemsho wa kuku wa kiswahi mana leo si jumapili?” 

Yule dereva alimuuliza Shaymaa na kumuuliza kitu ambacho Shyamaa alimjibu bila hata kuwa na hofu utafikiri alikuwa anamjua huyo Irina.

Njiani kote yule dereva alikuwa akimsimulia Shaymaa kuhusu Irina huku akimpamba kuwa ni mkali wa kupika na kwa mjini hapa hana mpinzani kabisa “Unaonekana unamkubali sana” Shaymaa alijaribu kujichekesha na kumuuliza lakini moyoni hakupenda kusikia hizo sifa “Ni mteja wangu mkubwa sana, kabla hajanununua gari na bajaji ya kusambaza vyakula vyake basi alikuwa ananitumia mimi na kunilipa kwa mwezi

Safari yao iliwapeleka mbali kidogo huku wakiendelea na maongezi yao na Shaymaa akitumia nafasi hiyo kumdadisi huyo kijana “Lakini Mimi namjua Irina hana uwezo wa kufungua mgahawa mzuri kama ule” “ni kweli usemacho dada yangu, unajua Irina alikuwa anasambazaga chakula kawaida tu hata Mgahawa hana. Sasa nasikia kapata Mume wa Mtu ndio kamfungulia” Jamaa alizidi kuuza habari bila kujua kuwa maneno yake anayoropoka basi anamchoma mteja wake

Shaymaa aligundua kuwa Mumewe amemfungulia biashara kimada huku yeye akimfanya ni Mama wa nyumbani tu tena akimuona kuwa amemuoa kwa bahati mbaya

Alifanikiwa kufika misosi lounge na kustaajabu kukuta mgahawa mkubwa na wakisasa ambao unamilikiwa na Irina mwanamke ambaye alikuwa anatoka na mumewe

Alifika na kuagiza mchemsho wa kuku kama yule kijana alivyomwambia. Na hakutaka kuagiza kingine bali alitaka kujua je ni kweli Irina ni fundi katika swala zima la kupika mchemsho wa kuku wa kienyeji?

Kiukweli Misosi Lounge walikuwa wanajitahidi atika swala zima la chakula kiasi ambacho hata Shaymaa alijikuta anapenda “Jamani wateja wetu leo tutakuwa na surprise kidogo hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu ambao utakaojitokeza ila litakuwa ni zoezi la muda mfupi mno wala hatutawabuguzi sana” 

Alikuwa ni mdada mmoja aliyevaa na kupendeza zaidi alisimama na kuongea huku akionekana ni mcheshi “Irina leo umependeza sana” Dada mmoja aliekuwa karibu na Shaymaa aliongea na kumstua Shaymaa baada ya kusikia jina la Irina.

Akiwa ameduwa kumkodolea Shaymaa mara alimuona Abdul akiingia na kuonekana Mtu mwenye tabasam kubwa mno Alifika na kusalimiana na Irina tena kwa kubusiana pasipo hata kuhofia Watu waliokuwa wakipata chakula cha mchana “Inamaana Abdul anafanya ujinga huu?”

Shaymaa aliongea na Ghafla alistushwa za milio ya fataki na aliweza kumshuhudia jinsi Abdul alivyostuka na kuduwaa. Waliingia vijana waliovaa nadhifu na kumuimbia wimbo wa happy birthday.

Shaymaa ndio akakumbuka “Kumbe leo ni tarehe 14 birthday ya Mume wangu? Alijikuta akiongea mwenyewe huku jicho kali likiwa limemtoka akimtazama Abdul anavyofurahi na Irina.

Wateja wote waliokuwa wanakula waliinuka na kumpigia makofi Abdul ikabidi Irina nae ainuke baada ya kugundua ni yeye pekee ndie aliekuwa kwenye kiti ametulia akiwa amepigwa na butwaa “Asanteni sana Wateja wetu wa Misosi Lounge kwa kushiriki katika tukio hili muhimu kwa Mume wangu mtarajiwa” Irina aliongea na kauli yake ilizidi kumchoma Shaymaa na kujikuta akiuma meno kwa hasira na kuanza kujiongeresha kama kawaida yake “Shaymaa tafadhali naomba ujitambue na ujiongoze mwenyewe usije ukatia haibu hapa, kumbuka una kwako” Aliongea kimya kimya bila Mtu yoyote kumsikia na akasikia Irina anawaomba wateja kuja kushiriki kula keki maalum ya kuzaliwa kwa Abdul

Wateja wote walitoka kwenda kula keki lakini Shaymaa alijikuta miguu imekufa ganzi kwenda mbele na alitamani hasiende kabisa “Tafdhali dada, leo ni siku ya wapendanao hivyo tunaomba uje kula keki hii muhimu kwetu na itakuwa maalum kwako kwa Mtu umpendae”

Irina alimwambia Shaymaa bila kujua kuwa Mwanaume ampendae ndio huyo aliyemuiba yeye na kujifanya anampenda. Shaymaa aliinuka na kujongea alipo Abdul huku macho yake yakiwa yamevilia kwa uchungu. Wakati Abdul akitaka kumlisha keki Shaymaa hapo ndipo alipomtazama kupitia paji lake la uso na wala hakuitaji kumtazama mara mbili kwani aligundua kuwa huyo ni Mke wake wa ndoa Shaymaa alikuwepo pale

WEWE UNAFIKIRI NINI KINAKWENDA KUTOKEA? USIKOSE SEHEMU YA 05 YA SIMULIZI HII TAMU NA YA KUSISIMUA


MAUMIVU YA NDOA
SEHEMU YA 05

Abdul alimtazama kwa umakini Mteja wa mwisho ambaye amekuja kula keki na kumfananisha na Mkewe na alipomtazama kwa umakini aligundua kweli alikuwa ni Shaymaa aliyekuwa amevaa niqab kuficha sura yake!!

Shaymaa alimtazama kwa hasira Abdul na kuvua niqab iliyokuwa imeziba uso wake na kumfanya aonekane vyema “Hongereni sana akika mmependezana” Shaymaa aliongea na kurejesha niqab yake na kuziba uso wake. Kisha aliichukua keki ya birthday na kuondoka zake huku akiwa ameishika mkononi

Ilikuwa ni ngumu kwa Irina kuweza kutammbua chochote kuhusu Shaymaa kwani lilikuwa ni tukuio ambalo lilichukua muda mfupi mno na kumuacha Abdul kubaki ameduwaa na kumtazama Shaymaa akiishia zske huku keki ikiwa mkononi “Vipi mbona unamtazama sana yule Dada? Unamjua?” Irina alimuuliza Abdul ambaye aliitikia kwa kichwa ila hakutaka kujionnesha kama kuna chochote baina yake na Shaymaa
                           *****
Baada ya kutoka pale, Shayaa alitembea kwa umbali mrefu sana pasipo kupanda usafiri wowote na akijiuliza maswali kadhaa kichwani Mwake “Hivi nitalia mpaka lini? Mimi ni Mwanamke wa aina gani?” Shyamaa alijiuliza na kabla hajajibu kitu alistushwa na mlio mkali wa honi.

“Samahani sana Dada” Ilikuwa ni sauti ya Mwanamke aliyekuwa anaendesha gari ambayo alitaka kumgonga Shaymaa. Shaymaa alistuka na kumtazama, na kwa weredi wake aligundua kuwa huyo dada hakuwa sawa hata kidogo “Yani Mimi ndio sipo sawa au yeye pia hayupo sawa?” Shaymaa alijiuliza na kushangaa baada ya kuona yalikuwa ni makosa yake lakini cha ajabu yule Dada alimuomba msamaha Shaymaa badala ya kumsema kuwa anapaswa kuwa mwangalifu.

“Nitakuwa nimekustua? Nisamehe sana Dada yangu nilikuwa mbali kimawazo ila wakati mwengine nitajifunza kuwa mwangalifu kwangu na Watu wengine” Yule dada aliongea na wakati wote huu Shaymaa alikuwa makini kumtazama. Yule Dada alimuonea huruma Shaymaa na alita ampe lifti, lakini Shaymaa alikataa na yule Dada alimsisitiza na mwishowe Shaymaa alikubali.

Wakiwa njiani yule Dada alionekana kugombana na Mtu kupitia simu yake ya mkononi na kuptupiana maneno makali kila wakati, na Shaymaa alipochunguza zaidi aligundua kuwa yule Dada alikuwa anagombana na Mumewe “Sikiliza nikwambie Ibrah, siwezi kulazimisha mapenzi kwako, ulishaonesha siku nyingi kama huna mapenzi na Mimi hivyo fanya lolote ujualo lakini Mimi siwezi kuishi na Mwanaume ambaye hajali hisia zangu. Hisia zangu ni muhimu na zina gharama zaidi ya kitu chochote hivyo siwezi na sitakubali kuona Mwanaume yoyote aninyanyase kwa mapenzi yangu kwake”

Yule Dada alikuwa akiongea na simu na kuonekana akibishana na Mwanaume wake na alionekana kuwa alikuwa anadai talaka kwa Mumewe “Inamaana Matatizo ya Wanaume yanafanana?” Shaymaa aliongea baada ya ukimya wa muda mrefu na kumstua yule dada aliyekuwa anaongea na simu muda wote.

“Unanyanyaswa na Mume wako?” Yule Dada alimuuliza na swali lake lilikuwa kama amefungulia koki iliyokuwa imefunga kilio cha Shaymaa “Mume wangu anaitaji kuniacha kwakuwa tu amepata Mwnamke mpya” Shaymaa aliongea na kumfanya yule Dada atake kujua zaidi.

Shaymaa alishukuru kupata nafasi ya kukutana na Mtu ambaye matatizo yao yalikuwa yakishabiana, hivyo alitumia fursa hiyo kumfungukia yule dada asiye mjua ili angalau atoe sumu iliyokuwa imeganda ndani ya moyo wake

Simulizi ya maisha ya Shaymaa ilikuwa kubwa mno hivyo waliweza kutafuta sehemu na kuegesha gari na kupata kahawa huku Shaymaa akiwa anamsimulia yule Dada matatizo yake na Mumewe.

Alishusha pumzi na kumtazama kwa makini huku akiwa anasikitika “Pole sana mpenzi wangu” Yule Dada aliongea na Shayma aliitikia asante huku akiwa anafuta machozi yaliyokuwa yanamwagika kwa wingi kwenye mboni za macho ya Shaymaa “Naitwa Amina” Yule Binti aliinua mkono na kujitambulisha na Shaymaa alipokea mkono wake na kisha alishukuru kukutana nae na kumtajia jina lake na hapo waliweza kufungua ukurasa mpya wa urafiki kwa sababu walihisi matatizo yao yalikuwa ni sawa.

Amina alikuwa ni msicha Mrembo aliyeshabiiana vyema na Shaymaa hivyo kwa kitendo cha kupinga ushoga, kilikuwa ni kitu sahihi kwake na Amina kwa ujumla “Kitu kikubwa nilichojifunza katika ndoa yako ni Mwanaume aliyekuoa wewe hana furaha na wewe” Amina aliongea na Shaymaa wala hakumpinga zaidi ya kuitikia na kuomba ushauri zaidi

“Unajua Wanaume wengi wana sifa ambazo zinafanana, Siku zote wakishamiliki bidhaa na kuitumia watakavyo basi wanaona bidhaa hiyo haina thamani tena, na hapo wataanza vituko na ukichunguza utakuta ana bidhaa nyingine. Wala usiogope kuanza upya mpenzi, kuolewa na kuachika ni sehemu ya maisha ila ukiruhusu Mtu akufanyie atakalo na wewe ukaishia kusononeka tu. Basi kaa ukijua kuwa unaweza hata kupoteza maisha ambayo ndio yana thamani kuliko kitu chochote”

Maneno ya Amina yalimuingia ipasavyo Shaymaa huku Amina na yeye akimsimulia kuhusu maisha yake na Mumewe na ilikuaje mpaka anaamua kudai talaka

“Asante nashukuru sana kukutana na wewe” Shaymaa aliongea baada ya kufika nyumbani kwake na walibadilishana namba za simu na Amina aliondoka zake.

Shaymaa aliingia ndani na alipatwa na mstuko baada ya kumkuta Mumewe akiwa ndani anamsubiri “Habari ya sahizi Mume wangu” Shaymaa alimsalimia Abdul huku akimtazama na Abdul aliitika na kumuomba wazungumze kidogo

Shaymaa alisogea alipo Abdul na kuketi karibu yake huku akionekana kuwa kimya akimsikiliza “Nilikwambia Shaymaa Mimi sipendi nikuone ukiwa unaumia kwa ajili yangu kwa sababu Mimi ni Mtu ambaye nimefanya maamuzi magumu dhidi yako. Kwa mfano leo ulipokuja pale misosi Lounge. Nilikuona dhairi una maumivu je nini kilikutuma uje pale na kwa idhini ya nani” Abdul aliongea huku akiwa kama Mtu anayetafuta sababu fuulani

“Abdul Mimi sitalia tena kwa sababu yako kwa sababu umeshaniambia kuwa hauna Hisia na Mimi na umefika mbali kwa kuniambia kuwa unataka kunipa talaka ili umuoe yule dada si ndio?” Shaymaa alimuuliza na Abdul aliitikia kukubali na Shaymaa aliendelea kuongea lakini alionekana kuwa tofauti na siku zote jinni anavyoongea kuhusu Abdul

“mimi sitamani hata kukupoteza Abdul, kiukweli sidhani kama naweza kuishi bila ya wewe!! Mapenzi yangu kwako sidhani hata kama huyo Irina wako anaweza nifikia hata robo. Lakini sitaumia kwasababu wewe ni Mwanaume wa Tofauti sana” Shaymaa aliongea na kumfanya Abdul kutaka kujua tofauti yake na Wanaume wengine

Shaymaa alimsifia kwa moyo wake wa ushujaa wa kumwambia ukweli kuliko angejifanya anapenda kumbe wala hampendi “Kwakuwa wewe haunipendi. Icho siyo kigezo cha kunifanya mimi nisikupende”

Abdul alishusha pumzi na kuwa makini kwa sababu alijua kuwa Shaymaa alishanyooka lakini sasa alimuona kama bado ni Mtu ambaye alikuwa hataki kuachika “Dini yetu inaruhusu Mwanaume kuoa Wanawake wanne hivyo wewe Mume wangu umeitumia nafasi moja tu, kwanini usimuoe Irina kama Mke wako wa pili?”

Ilikuwa ni kauli iliyomfuraisha Abdul baada ya kusikia Mkewe amemruhusu kuoa Mke wa pili “Utaishi kwa Amani na upendo ukiwa kama Mke Mkubwa?” Abdul alimuuliza huku akiwa na furaha “Ni wajibu wangu kumpenda Mke mwenzangu kama Mwanamke ninae jitambua, hivyo kuliko kufanya zinaa, kwangu bora ni ufunge nae ndoa”

Yupo wapi yule aliyesema ukishindwa kushindana nae basi ungana nae? Shaymaa aligundua njia sahihi ya kuushika moyo wa Abdul na ili amshike ni lazima ajifunze kupenda vitu avipendavyo
                            *****
Baada ya kupewa ruksa ya kuoa Mke wa pili, Abdul hakutaka kufanya ajizi kwani haraka alifika kwa Irina ili kwenda kuongea nae “Irina Mama akika una bahati sana” Abdul aliongea huku akiwa anamkanda mabega Irina “Bahati ya nini?” “Mke wangu amekubali nikuoe Mke wa pili”

Abdul alimwambia Irina na kumfanya astuke “Yani Mimi Irina niolewe Mke wapili?” “Ndio tena Mke wangu amefurahi sana baada ya kukutambua, ni yeye ndie aliyenituma kuja kuongea na wewe”

Abdul alionge na kumfanya Irina acheke kicheko cha kebehi “Sikiliza Abdul Mimi siwezi kuolewa Mke Mwenza, kwanza mambo ya ku share Mwanaume siwezi. Sijakushikia bango wala sijatuma watu kukuomba unioe. Chagua moja, uachane na Mimi na ubaki na Mkeo au umuache Mkeo haraka sana na ikiwezekana leo usikuu umpe talaka arudi kwao na Mimi na wewe tufunge ndoa”

Irina aliongea na kumfanya Abdul apate na kigugumizi cha mdomo ajue nani amchague kati ya Irina au Mke wake Shaymaa

UNADHANI NINI KITAENDELEA? USIKOSE SEHEMU YA 06 

Post a Comment

Previous Post Next Post