JIFUNZE KUTOFAUTISHA KATI YA MAPENZI NA FARAJA. ❤ & 💔

Huenda ulimuhitaji sana ila akakukataa, akasema haiwezekani nyie kuwa pamoja kwamba wewe sio chaguo lake yupo yule anayempenda na kumthamini. Ambaye anamfanya atabasamu kila anapomuona na ajione bora kila anapokuwa naye.

Kisha akakurahisishia maelezo kwa kusema kama unavyompenda yeye, naye pia kuna mtu anampenda kwa dhati na kwakiwango hicho unachompenda yeye.

Haikuwa rahisi ila ikabidi tu umuelewe kwamaana hakuna shujaa aliyewahi kuushinda ukweli. Kama uyajuavyo maisha ni kama maji ya bahari na mawimbi yake. Miezi kadhaa imepita kule alipopenda mambo yamekuwa kinyume na matarajio yake. Ameachwa!

Sasa amerudi kwako anasema ameamua muwe pamoja kama Adamu na Hawa, mjenge familia yenye furaha, amani na upendo 🥰.

Ngoja nikwambie kitu, rudi hatua kadhaa nyuma halafu niskilize. USIKUBALI HARAKA. Jifunze kutofautisha kati ya Mapenzi ya kweli na Faraja kamwe usijaribu kuchanganya.

Mara nyingi mtu aliyeachwa na anayempenda na kutaka kuwa nawewe kisa uliwahi kuonyesha kumpenda. Huwa hasukumwi na Nguvu ya Upendo bali huhitaji Faraja.

Kidonda alichosababishiwa na aliyempenda anataka kipate tiba, ukikubali haraka utajipoteza utajikuta unageuka kuwa tiba kwake badala ya mpenzi.

Siku akipona au akipata unafuu wa kidonda chake atamtafuta yule anayempenda na kukuacha. Kuwa makini.

Zingo Zingo ❤️

Post a Comment

Previous Post Next Post