MREMBO MCHARUKO-1

  







MREMBO MCHARUKO-1

MTUNZI-LATIFA NTANGA
0763361677

"Hodiiii fundi, Shikamoo! Sketi yangu hii ya shule nataka huipunguze maana ni ndefu sana"
nilifika tu kwa fundi cherehani nikaanza kuongea bila kumpa nafasi.
"Duh we binti sijui nikujibu nini" alisema huyo fundi akiniangalia.
"Sio lazima kujibu wewe ikate hapo ishone mie nakungoja sababu kesho ni naenda shule" nilimwambia.
"Lakini hii sketi mbona ipo vizuri ndefu ya heshima inafaa" aliongea akiangalia.
"Sketi ndefu kama naenda msikitini kuswali akuu sitaki we ikate ifike juu ya magoti" nilisema
"Mtumee we mtoto unalaana eeh"
"We babu usitafute kichambo nakwambia kama kazi huwezi sema"
nilichukia huyu fundi anamaneno mengi.
Nikachukua nguo yangu nakuondoka nikaenda kwa fundi mwengine huyo hakuuliza sana akanipunguzia sketi ikawa fupi nilifurahi nikarudi nyumbani sasa, njiani nikakutana na shogayangu ninaesoma nae Nasra.
"Hee mambo"
"Poa shosti unatoka wapi?" Aliniuliza nikamwambia nimetoka kupunguza Sketi yangu
"Bora mwezangu maana ilizidi refu kama unaenda kuimba kwaya"
Nasra akanisapoti
"Umeona eeh shogayangu hadi nilikuwa natia aibu"
Basi tukajazana ujinga hapo kisha tukaagana yeye alikuwa anaenda dukani namimi nikarudi nyumbani.
Wazazi wote walitoka nyumbani nikabaki mimi na kakayangu Gedion yeye yupo Secondari kidato cha pili namimi nipo darasa la saba.
Tofauti mie mcharuko balaa ila kakayangu mpole hadi wazazi wanampenda mimi sina hata anipendae kutwa napigwa tu kwa umapepe wangu.
Baba ni Mwanajeshi halafu mama yeye ni Daktari Muhimbili.
Familia yetu kidogo inajiweza, kama kakayangu Gedion anasoma shule ya kulipia na akili anazo ila mimi nilipelekwa shule ya Serikali.
"Wewe Lisa unatoka wapi?" Nilipoingia tu kaka Gedion akaniuliza.
"Aah umekuwa mumewangu hadi uniulize ebu nipishe mie"
Nilimwambia nikampita nakuingia chumbani kwangu, ananijua akili zangu hovyo hakuniuliza tena, baada ya muda mfupi baba alirudi Gedion akatoka kumpokea mimi nilimsikia lakini sikutoka nikabaki chumbani maana mimi na baba haziivi kabisa nikikaa karibu nae lazima anipige kutokana na ujeuri wangu.
Ghafla nikasikia mlango wangu unagongwa,
Gedion akaingia
"Unaitwa na baba uko"
"Anataka nini mwambie nimelala"
Mara nikamsikia baba anaongea mlangoni
"Wewe Lisa hivi unajua kesho shule, nenda jikoni kasaidie kupika uwahi kulala" alisema nikaanza kujifanya naumwa nikajikamua machozi ya uongo sipendi kupika kilasiku nakimbia jikoni.
"Baba tumbo linauma uwiiii mamaaa weeee nakufaaaa"
Nilipiga kelele nikigalagala kitandani hadi wakashtuka, Mara mama nae akarudi kelele zangu alizisikia akaja mbio chumbani nakuniuliza kuna nini kwakuwa yeye Daktari anajua akawaambia watoke nje anipime nini tatizo.
"Upo kwa siku zako kwani?" Aliniuliza nikakubali wakati sipo akanambia ndo mana naumwa nisijali nitapona kisha akatoka nakuelekea chumbani akaniletea vidonge nimeze kupunguza maumivu nikapokea alipotoka nikavitupa uvunguni mwa kitanda.
Basi chakula kiliiva tukala pamoja kisha nikaingia ndani kulala.
****
Asubuhi kulikucha nikaamka nakujiandaa kuelekea shule, nilipotoka wote walinishangaa sketi ya shule imekuwa fupi sana.
"Hee we mtoto"
Mama alisema akitoa macho mi hata sikumjali, baba nae akapigwa na butwaa.
"Hivi we Mtoto nikufanyaje mimi? Lisa utanipa kesi nitakukata shingo wewe"
Baba alipandwa na hasira ila nilimzoea hata sikuogopa kupigwa nilishazoea nakuona kawaida tu.
"Halafu nina wasiwasi we mwanamke huyu mtoto ulimuiba hospitali sio mwanangu" Baba alisema nakumgeukia mama, niliangua kicheko kwa sauti,
"Heheh haloooo"
Baba alianza kunisogelea anipige lakini mama akamzuia.
"Muda wa kazi huu mumewangu ebu wahi kazini mwanao mzoee tu utamuumiza bure mtu mwenyewe haelewi"
"Unamtetea huyu chizi ipo siku nitamuua mimi"
Baba alitoka huku anafoka akapanda gari na kuondoka na kakayangu mie anaenipeleka shule mama basi tukatoka nje tukaingia kwenye gari hakuniongelesha kitu akanifikisha shuleni nakuniacha.
Mamayangu mpole sana mwenye huruma lakini mtoto aliemzaa sasa majanga.
Basi shuleni kila mwanafunzi ananiangalia mimi na kimini changu sababu nimejaaliwa shepu ya maana makalio makubwa halafu nina miguu minene ya bia basi sketi ilinipendeza hadi raha.
"Hapana chezea Lisa wowowo yani unatuua tu wenzio"
Mashoga zangu walianza kunisifia nimependeza.
Darasani hakukukalika wavulana wakaanza kunisumbua.
"Lisa mapumziko nitafute nina zawadi yako" alisema Bakari
"Akaa unikome usinipake shombo mie zawadi kampe bibi yako"
Japokuwa nilikuwa mcharuko lakini sikujihusisha na mapenzi shuleni.
Basi ghafla mwalimu mkuu akaingia darasani alikuwa anafundisha Hisabati akaanza kuandika akielezea mimi hata sikumuelewa analofundisha ndo kwanza nikainamia dawati nakulala.
"Pumbavu nani alielala uko nyuma aje mbele hapa"
Mwalimu alifoka, nilishamzoea baba mkali anasauti kubwa kama anaongea kwenye spika hata sikuogopa nikazidi kulala tu.
Wanafunzi wenzangu wakageuka kuniangalia huku wakicheka maana shule yetu wengi wamevurugwa, wapo wavulana wanamademu zaidi ya wawili, wasichana pia wanamabwana hadi walimu, kuna wavuta bangi humo wezi wapo yani tafrani hata walimu hatuwaogopi.
Basi mwalimu mkuu akazidi kufoka nikainuka huku nimejishika tumbo nakusogea mbele.
"Mwalimu naumwa"
Nilisema nikiwa mnyonge nikijikamua machozi.
"Wewe mwanafunzi hii sketi mbona fupi mno"
Aliongea akinitolea macho
"Mwalimu unanionea mbona wengi wanavaa sio mimi tu"
Nilijitetea lakini ni kweli wasichana wengi wanavaa nguo fupi ila tatizo mimi umbo langu kubwa tofauti na wengine wao maumbo yao madogo.
"Unajitetea poyoyo wee nenda ofisini nikukute uko" alisema mwalimu nikageuka kuelekea ofisini kwake.
Aliendelea kufundisha alipomaliza akaja ofisini nakunikuta nimekaa mapaja yote nje na yalivyonona nikamuona ametoa macho anayaangalia.
"Hivi unaitwa nani wewe binti?"Aliniuliza
"Naitwa Lisa Charles"
"Unajina zuri kama wewe mwenyewe! Unajua Lisa unaweza kuponza mwanaume akafungwa kwaajiri yako?"
Mwalimu aliongea kwa upole hadi nikashangaa wakati ni mkali balaa akainuka nakufunga mlango! mapigo ya moyo yalienda mbio Mwalimu mkuu akanisogelea karibu.

Itaendelea

Post a Comment

Previous Post Next Post