MREMBO MCHARUKO-2



MTUNZI-LATIFA NTANGA
0763361677

Nilianza kujuta kwanini nilipunguza sketi yangu nakuwa fupi iliyoniacha wazi, basi nikaanza kuishusha chini lakini haikusaidia. Mwalimu akasogea nakusimama mbele yangu akiniangalia.
"Lisa ukitoka shule naomba unione sawa"
alisema nikamuitikia tu basi akaniruhusu kutoka.
Nikashukuru Mungu maana sikutegemea kama ningeachwa salama, nilirudi darasani nakumkuta mwalimu wa Sayansi anafundisha, huyu mwalimu kijana mdogo tu ni kipenzi cha wanafunzi micharuko maana akijua unademu anakupongeza sana kuna mmoja anaitwa Said huyo anamademu watatu shuleni mwalimu alimfuma, amekumbatiana nje ya darasa alimpongeza nakumpa pesa.
"Huo ndo urijali sasa"
Alimwambia akicheka nakuwaacha hapo.
Somo la sayansi linahusu mengi wanaelezea mwili wa binadamu nayeye akifundisha matusi matupu yani wanafunzi ndio wanampenda balaa.
"Mrembo wa shule karibu" aliniambia akiniangalia nilikuwa nimenuna hapo yaliyonikuta kwa mwalimu mkuu sikusahau.
"Mbona umenuna? Yani umeamua utumalize kabisa na kimini chako"
Aliongea mwalimu akinitazama kwa matamanio makubwa.
Darasa zima walicheka wakinitazama, sikutaka kuongea nikarudi kwenye dawati nakukaa kimya.
Mwalimu alifundisha hadi alipomaliza akasema.
"Lisa nifuate ofisini"
Nilijikuta nanuna zaidi hadi nilijuta.
"Sivai tena hii sketi mimi"
Niisema huku nikitamani kulia, mwalimu alitoka namimi nikaanza kujishauri niende au nisiende wezangu wakanza kunitania
"Lisa leo unamajanga kuitwa na walimu ofisini mbona utakoma"
"Mwezangu hiko kimini chake kimezua tafrani leo" mashoga zangu Tina na Nasra walinichokoza.
Maneno yao yalinikera nikatoka nikiwa nimenuna sana.
Nilifika ofisini nakumkuta mwalimu amekaa alinitazama juu hadi chini huku akitabasamu.
Nikajisikia aibu niliinamisha kichwa chini sikutaka kumuangalia usoni.
"Lisa mtoto mzuri mbona muoga sana ila umependeza leo"
alisema akionekana amenitamani, nilitetemeka juku jasho likinitoka mwilini.
Ghafla mwalimu Deo akanisogelea nilipo nakunishika.
"Mwalimu usiniguse"
nilimwambia lakini hakusikia akazidi kushika mapaja yangu nilitetemeka moyo ukienda mbio sana.
Nilijikuta namsukumiza kisha natoka mbio mule ofisini hadi darasani nikihema sana. Sikutaka kubaki tena shule nilichofanya nikabeba begi langu nakutoka kurudi nyumbani.
Nilikuwa na pesa nikapanda bodaboda iliyoniwahisha nyumbani kwetu nilishuka nakuingia ndani nikashangaa kumuona kaka Gedion amekaa sebuleni anatizama TV.
"Wow mrembo mcharuko huyo kulikoni leo mapema?" Aliniuliza sikumjibu nikampita tu nakuingia chumbani kwangu nikavua nguo za shule nakuvaa gauni nikatoka nje nimenuna balaa hata kakayangu aliponiona hakuniuliza kitu alinitazama tu.
Mkononi nilishika ile sketi ya shule nikaingia jikoni nakumkuta dada wa kazi sikumsalimia wala hakuniuliza anaujua mcharuko wangu sichelewi kumchamba basi nikatafuta kibiriti nakutoka nje ya nyumba nikaiweka nguo chini nakuwasha moto, moshi mwingi uliingia ndani nakufanya kaka Gedion aje haone nachoma nini.
"Haaa wee Lisa unachoma sketi ya shule?" Alisema kwa mshangao sikumjibu kitu.
"Si naongea nawewe yani baba katoa pesa zake wewe unachoma nguo kweli" alizidi kunipandisha hasira zangu nikatoa msonyo wa nguvu hadi alibaki kanitolea macho.
"Sikia wewe kinyago usinizoee tena niache kama nilivyo"
Nilimwambia.
"Yani Lisa mimi kinyago sawa tu" aliongea akitoka nakuingia ndani akachukua simu nakumpigia baba akamwambia nimechoma sketi moto.
Basi nilipomaliza nikaingia chumbani kwangu nakujifungia mlango sikutaka kuongea na mtu yeyote.
Nilipitiwa na usingizi hadi niliposikia mlango unagongwa nikainuka kiuvivu nakuufungua nikamuona mama kumbe ilikuwa jioni imefika.
"Shikamoo mama"
Nikamsalimia
"Marahaba mwanangu, unaumwa au na umekula leo?"
"Hapana uchovu tu wala sijala"
"Haya pole oga basi upate nguvu uje mezani nakuandalia chakula"
Nikamuitikia alitoka nikaingia kuoga nilipomaliza nikatoka kwenda mezani nilikuta chakula tayari nikaanza kula hadi nilipotosheka.
Mara kaka Gedion akaja
"Mama huyu mwanao leo kachoma sketi ya shule moto" alinichongea nikamkata jicho baya.
"Wee Lisa kwaninii umechoma moto Sketi?"
Mama aliniuliiza
"Fupi imenipa usumbufu"
"Nani alikutuma ukate sasa? We sindo ulipeleka kwa fundi lakini"
"Mama bwana kaninunulie sketi ndefu"
Niliisema Gedion akacheka sana.
"Mrembo mcharuko kapatikana anataka sketi ndefu" alisema akiinuka alinikera, Basi nilimaliza kula nikaingia chumbani nakupiga pasi nguo zangu za shule nilichukua sketi yangu ya mwanzo ndefu kidogo ila haifiki chini kabisa.
Nikaziandaa nakulala zangu, siku hiyo baba alichelewa kurudi akanikuta nimelala.
Hatimae asubuhi ilifika wakashangaa nimevaa sketi ya mwanzo.
"Wewe mjinga umenikera kuchoma moto nguo ya shule yani nakungojea maliza hilo la saba lako nakutafutia mwanaume akuoe sitaki kabisa kukuona hapa nyumbani"
Baba alifoka kwa hasira
"Mumewangu lakini maneno gani unamwambia mtoto huyo mume atampa nini huyu bado mdogo"
Mama alinitetea
"Lisa ni mtu mzima hana utoto wowote na ataolewa tu pumbavu! Gedion twende"
Alimaliza kufoka akamuita kaka nakupanda gari wakaondoka. Mama naye akanishika mkono tukapanda gari letu akanipeleka shuleni.
"Leo jioni nitakuletea sketi mpya mwanangu"
aliniambia kwa upole.
"Sawa mama nashukuru" namimi nikajifanya mwema tena.
"Lisa mwanangu jitahidi kusoma ufauru nikupeleke shule nzuri yakulipia ukiferi ndoa inakuhusu si umemsikia babayako leo eeeh?"
Maneno yake yaliniogopesha sana nikajikuta nakuwa mnyonge nikaitikia tu.
Basi nilifikishwa shuleni akaniacha nakuondoka ile naingia tu darasani wezangu wote macho kwangu hadi nikaogopa imekuwaje ikabidi niwaulize.
"Mwalimu mkuu anakutafuta jana ukaondoka bila kuaga hee utakoma leo"
alisema Mwanahawa shogayangu huyo nae kabla sijakaa sawa naona mwalimu amefika darasani akaita.
"Lisa Charles nifate ofisini" akasema nakutoka nikaangua kilio kikubwa darasa zima wakacheka.

Itaendelea.full stori elfu mbili.0719618409 Lisa Ntanga. 

Post a Comment

Previous Post Next Post