🔞🔞🔞🔞🔞 MSIBANI TANGA 13

Jun 22, 2021

Nilibaki na mawazo kede kede kwamba kwa nini jamaa aniache mimi tanga ilhali tumekuja wote na yeye ndo mwenyeji wangu?



Nilianza kupata wasiwasi kwamba labda ameshtuka kwamba nilipita na mdogo wake



Hata hivyo nilisimama nikawaza zaidi na zaidi sikuwa na namna nilitakiwa niondoke nirudi Dar siku ile ile



Ilibidi nimtumie ujumbe kumuuliza 



"Vipi mwanangu AZ, uko wapi??" nilituma ujumbe



Nilisubiri kama dakika tano lakini hakujibu, ikabidi niongeze mwingine



"Mi nasepa zangu DSM kaka maana sikuelewi elewi" Nilisema



Hakujibu kitu ndipo nikaamua sasa kuchukua nafasi yangu ya kuondoka.



Nilitembea kwa miguu huku nikiwa nasikilizia pikipiki iweze kunichukua inipeleke stand nikapande gari ya mkoani.



Nikiwa natembea tembea kwa mwendo wa taratibu, nilisikia honi nyuma yangu ndipo nikageuza shingo na kutazama nyuma,



Kulikuwa na gari fulani nzuri ya mtu binafsi, nikaona bora nigongee lift, nikaipiga mkono



Kweli ile gari ilisimama na dereva alishusha kioo na kunitazama, alikuwa mwanamke mmoja mweupe halafu mwenye miwani ya jua, nyeusi halafu akanitazama 



"habari?" Aliniuliza



"Safi niaje?"



"Safi"



"Samahani naomba lift" Nilimuambia



"Unaelekea wapi?" aliniuliza



"Naenda maramba, nikapande gari niende hadi TANGA mjini" nilisema



"Ok powa twende" Alisema mwanamke yule huku akiwa ananifungulia mlango na mi nikazama ndani



Nilivuta pumzi "Mpffffff asante sana jamani khaa!" Nilisema kwa furaha na kufunga mlango safari ikaanza.



Tulitembea kwa dakika kama 10 hatujaongea ndipo akaanza mwenyewe "Yaani khaaaa" alisema kwa hasira nikamgeuzia shingo



"Vipi?" Nilimuuliza



"Yaani hizi barabara ni mbovu jamani yaani sijui serikali ina kazi gani jamani" alisema kwa hasira



"Ni kweli, makorongo kama yote"



"Yaani ni vibaya sana, ni kutembea polepole tu maana gari hii itaharibika ujue" alisema



"ni kweli bwana. Ila tutafika kwenye barabara nzuri tu" nilimtia moyo



"Kweli, wewe unakaa huku kwetu au mgeni?" Aliniuliza



"Hamna mi Nilikuja tu msibani kwani kuna jamaa yangu alifariki"



"Anhaa.....yule nani, Khalid?" aliniuliza



"Ndio ndio.....!" nilijibu



"Haya buana. Mi naitwa Zuwena, wewe je?" aliniuliza



"Ahaa, Zuwena, mi naitwa Jawabu"



"Anhaa, Jawabuuu....umenikumbusha mbali jina kama la rafiki yangu mmoja muhaya yule, alikuwa bitozi hahaha" alisema kwa furaha huku akiendesha gari lake taratibu



"Ndio, wewe unaelekea kazini au?"



"Hamna, mi naenda Dar now, nilikuja wiki iliyopita kusalimia"



"Mmmmh? Dar??" niliuliza kwa furaha huku nikijitia moyo naweza pata lift



"Ndio, mbona unaguna?"



"Hamna, nawaza hapa kama naweza kupata lift maana mwenyewe naenda hadi Dar"



"aaaah kumbe" alisema



"Ndio"



"Ahah.....basi vizuri Dar unakaa sehemu gani?"



"Vingunguti"



"Wooow!!....mi naishi Kwa Aziz Ally"



"Dooh....basi bwana, niambie kwanza tunaenda wote au?" niliuliza



"Usijali, utanichangia hata mafuta tu sawa?" Alisema 



"Usijali" 

Post a Comment

Previous Post Next Post