RISASI YA KICHWA 01


 "Hellow genero nakuomba unisikilize kwa umakini na uwelefu kuna Mali itakuja usiku wa kesho na Mali iyo inapitia kwanjia ya bahari hivyo andaa vijana wako kwa ajili ya kuvamia mahala hapo na uchukuwe Mali zote ambazo zitakuwa katika meli iyo. Na kuomba usifanye makosa maana izo Mali zilizo kuwa humu ni Mali ya muheshimiwa rais amezawadiwa na rais wa misiri ." waziri wa mambo alitoa maelezo yote na kumfamisha vyema genero Tonga.

"Nimekusikia vyema waziri lakini ujaniambia ni Mali gani ambazo tunakwenda kuziiba".? Aliuliza genero Tonga.

"A,a,a,a,ah ninini, masunduku yalikuwa na dhahabu na almasi. Na pia naitaji uzitunze pindi utakapo ziiba mpaka tukapo onana na tutaagawana Mali nusu kwa nusu. Alizungumza muheshimiwa waziri wa mambo ya ndani na kumuwahidi watawagawana Mali nusu kwa nusu.

" oh basi sawa hakuna tabu mi nitaifanya iyo kazi na sitaki niuzwe katika jambo hili na hili diri tuna fahamu Mimi na wewe tu"aliongea genero Tonga kwa msisitizia muheshimiwa Wazir wa mambo ya ndani asilete usaliti.

Baaada ya maongezi kati ya waziri na genero Tonga alikata simu na kuchukua sigala yake na kuwasha sigala kwa njiti ya kibiriti na kuanza kuifuta sigala ile kwa taratibuuuuu kabisa huku akikumbuka mbali sana.

Katika kambi ya genero Tonga ilikuwa msituni ilikuwa na vijana wengi mno wa kila rika wakike wakiume na wao wote hao walikuwa wanafanya kazi chini ya Genero Tonga ni kama baba yao na pia vijana wakiume wakiongozwa na kijana wa kisomary aitwaye Abdi na katika upande wa wasichana walikuwa wanaongozwa na msichana aitwaye rose na rose pia alikuwa anamahusiano ya kimapenzi na abdi kijana wa kisomari.

Ilivo Timia usiku katika kambi ya Genero Tonga aliwaita vijana wake na kuwakusanya wote kwa pamoja na kutaka kuwaeleza mission ya kwenda kufanya uvamizi katika bandar na katika bandari hiyo kutakuwa na Mali nyingi sana ambazo zitawasadia kuwa na silaha kubwa kubwa badaye na hata kuiteka nchi na kumuondoa Rais aliye kuwa mabadarakani. Waliwambia hivyo vijana wake na vijana wake walikuwa na furaha kubwa pindi watakapo iteka nchi yao na kumuondoa rais mabadarakani.

Wakati hayo yanazungumzwa na genero Tonga pembeni yake kulikuwa amesimama Abdi na kwa upande wa kushoto amesimama msichana mzuriii aitwaye rose. Lakini katika wale vijana ambao walikuwa wamesimama na kumsikiliza genero Tonga kwa umakini kulikuwa na kijana moja ambaye alikuwa anavahamika kwa jina la sneper yani mlengaji . na alikuwa ana mtizama sana Abdi kwa hasila sana huku akikunja mikono yake kwa hasila kwa sababu alikuwa anatembea na rose na yeye snepear alikuwa anampenda Sana Rose sema anashindwa kumueleza tu.

Baada ya maongezi na ile habari mpya aliyo itoa Genero Tonga kwa ajili siku ya kesho kwenda kufanya uvamizi katika bandari aliwaruhusu vijana wake wa pumzike na vijana wengine walikuwa doria wafanye doria kwa umakini.

Vijana walitawanyika na wakaelekea katika vijumba vyao kwa ajili ya kujipumzisha lakini Abdi na rose walikwenda kulala pamoja na snpear yule mlengaji wa masafa malefu alililiona lile Rose anakwenda kulala na Abdi. Alikasilika Sana tena Sana na kuhapa lazima amuendoe dunia Abdi.............

ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post