πŸ’–πŸ’–PENZI LISILO SAHAULIKA ( MWISHOOO) πŸ’–πŸ’–


ZANZIBAR
Kabla hawajafika huko bustanini Agnes akiwa amemshika mkono Ben aligeuka na kisha kumpungia mkono wa kwa heri dokta Ahmed ambaye kwa muda huo alikuwa akiishia kutabasamu tu ...."Dokta asante sana kwa wema huu uliotutendea japo hatuna cha kukulipa ila Mungu tu ndiye atakulipa ,tunakuombea maisha marefu na afya njema katika dunia hii".Alisema Agnes muda huo huo Ben akigeuka kumtazama Dokta Ahmed."Dokta nadhani kwa upande wangu sina budi kukushukuru kwa kunisaidia katika kipindi kile kigumu nilichokuwa nacho,,,Mungu na akubariki sana na baraka zake ziwe juu yako,nitakutembelea siku nyingine ili tuje tuongee zaidi".Alisema Ben,Dokta Ahmed nae hakubaki kimya alizungumza "Asanteni sana wapendwa huu ulikuwa ni wajibu wangu tu na ndio kazi yangu kuhakikisha afya za watu zipo madhubuti,na hili siyo kwamba tunalifanya tu kwa kutegemea akili zetu bali pia huwa tunamtegemea sana Mungu kwa maana yeye ni muweza wa yote". Aliongea Dokta Ahmed huku akianza kuzipiga hatua za mwendo wa taratibu."Ben Mungu na azidi kukutia nguvu katika maisha yako tutaonana tena Mungu mwenyewe akipenda".Alisema Daktari kisha wakaagana nae akaondoka na kutoka nje ya geti.... alielekea hadi kunako gari yake akaenda na kupanda akaondoka muda huo huo kurudi kazini kwake kuendelea na majukumu ya kila siku.Huku nyuma baada ya Dokta kuondoka Agnes na Ben walifika pale garden wakakaa kwa kutazamana."Pole sana Ben kwa yote ambayo yalikupata najua hayo yalikuwa ni mapito tu". Aliongea Agnes huku akimshika kwenye bega lake la kushoto."Nilishapoa Ag,ila Adera mke wangu yupo wapi?" Aliuliza Ben na kumfanya Agnes ajiinamie,aliinua kichwa chake na kuanza kumtazama sana usoni,,, alishindwa aanzie wapi ila akajikaza na kuamua kufunguka tu ukweli wote."Ben Adera tulishamzika mwaka mmoja sasa umepita na ndio maana nikaanza kwa kukupa pole kwa yote uliyokuwa ukiyapitia".Baada ya Agnes kuyaongea hayo.....Ben alianza kukumbuka hapo hapo matukio yote kuhusiana na Adera mke wake,,,akakumbuka vilivyo kwamba ni kweli Adera alimtoka tena mbele ya macho yake mawili.Kwa uchungu Ben alijiinamia kisha chozi likawa linamtoka .....ikafikia kipindi akawa analia kabisa mithili ya mtoto mdogo.Agnes aliuvaa ujasiri wa hali ya juu akamnyanyua Ben juu na kuanza kumtuliza kwa kumkumbatia."Pole Ben,najua una uchungu mzito sana kumpoteza Adera ila ndo imeshatokea hatuna budi kuukubali tu ukweli.Ninachokijua mimi hii ni njia ya wote kwani hapa duniani sisi tu wapitaji na makao yetu ya milele yapo mbinguni.Adera yeye ametangulia nasi tutamfuata,, ukiendelea kulia Ben hata Mimi pia utanifanya nilie maana binafsi sipendi kukuona ukiwa katika hali hii.Ya dunia ni mengi Ben nyamaza usilie". Agnes kwa sauti ya upole alimbembeleza sana Ben mpaka akafanikiwa kumtuliza.Ben alinyanyua uso wake akawa anamtazama Agnes, Agnes nae vivyo hivyo akawa anamtazama pia japo yeye alikuwa na aibu furani hivi.Waliendelea kutazamana huku Ben akianza kufarijika."Huyu binti kwa nini ana busara na hekima? Huyu atafaa kumrithi Adera wangu niliyempoteza katika mazingira ya kutatanisha".Al
ijisemea Ben huku akimkumbatia kwa nguvu msichana huyo.Agnes baada ya kukumbatiwa na Ben,joto la mwili wake alihisi limevamiwa na joto la mwili wa Ben,,, kidogo kidogo hisia za mapenzi zikaanza kumuijia akajikuta akijilaza kifuani kwa Ben huku nae chozi likianza kumtoka na kuishia kudondoka kifuani kwake,alikinyanyua kichwa chake kisha akayafumba macho yake na kumbusu Ben,dakika mbili tu denda la kimataifa lilianza kutembea na baada ya kulimaliza walikaa tena na kuendelea na mazungumzo yao."Nikabidhi mimi moyo wako Ben ili nami nikukabidhi moyo wangu....hisia za mapenzi zote zimehamia kwako,nitakufariji na kukusahaurisha uchungu wako wote.Na nitakupenda daima,,,nitaendeleza pale alipoishia Adera nami nitakuwa mama watoto wako na wewe nitakuita baba watoto wangu". Aliongea Agnes kwa upole na sauti ndogo sana huku akimshika mabegani Ben."Agnes wewe ndiwe mrithi wa Adera,naomba tuungane kwa pamoja ili tuyaendeleze maisha yetu ya hapa duniani".Waliendelea kupiga story zingine huku wakifurahi na kucheka kwa pamoja na wakati mwingine kutaniana.
Upande mwingine ulionekana mzimu wa Adera ukiwa umesimama kaburini huku kaburi hilo likitetemeka kwa mipasuko mikubwa ambayo haikuweza kusikiwa na mtu yeyote yule,Mzimu wa Adera kwa muda huo ulikuwa ukitokwa na machozi huku ukitetemeka sana tena kwa mtetemo wa uchungu.Ulipiga kelele mara Moja tu nao ukatokomea ndani ya kaburi hilo na hali ya hewa ikawa shwari.Basi kwa upande wa Agnes na Ben mapenzi baina yao yaliendelea kunawiri huku wakizidi kupendana maradufu,,,Mama Adera nae kwa kulitambua hilo alitia baraka zake kwa wawili hao aliokuwa akiwaita wanae nae akawapa baraka zingine zote za kuwatakia mema katika maisha yao.Mathew nae kwa muda huo aligeuka na kuwa rafiki wa kutumainiwa kwa Ben na urafiki wao ukawa imara sana maana kama ule msemo wa ndege wenye manyoya yanayofanana huruka kwa pamoja,Ben na Mathew walipendana sana katika urafiki wao huo.....ulikuwa ni urafiki mmoja mzuri sana urafiki usiokuwa wa kinafiki kama ule wa Steve.Baadae Ben na Mathew waliokoka vikamilifu nao wakawa washirika wa Yehova kama ilivyo kwa Agnes na mama Adera ambao kwa muda huo wao walikuwa wameshaokoka kitambo sana.Walianza kushirikiana kwa mambo mengi sana ikiwemo ya kibiashara na kimaisha kwa ujumla.....maisha yao yakawa ni ya kumtanguliza Mungu katika kila jambo walilokuwa wakilifanya."Daah! Shemeji naona sasa hadi kitambi kimeshaanza kujitokeza daah! Kweli ukiwa na rafiki mwema pamoja na upendo hakuna linaloshindikana".Maneno hayo aliyaongea Agnes wakati wakiwa wamepumzika ndani ya beach moja ya kuvutia."Unajua shemeji,mimi zamani nilijua ili uwe na kitambi au afya yako iwe nzuri ni lazima uwe na pesa kumbe ndivyo sivyo..... Kumbe ukiwa na pesa bila amani ikiambatana na furaha ni kazi bure .Kwa sasa kama unavyoona nina amani na furaha na ndio maana afya yangu inaimalika kama ilivyo kwa rafiki yangu Ben hahaha". Aliongea Mathew huku akimtingisha bega Ben aliyekuwa akichezea game kwenye smartphone yake."Umeona ee,yaani Mathew huo ndio ukweli wenyewe,kuwa na pesa si kigezo cha wewe kuishi maisha mazuri,kuna matajiri wengi sana wana pesa za kutosha tu ila wanaishi ndani ya maisha ya kitumwa sababu tu ya kukosa amani katika maisha yao". Aliongea Ben.Basi Waliendelea na mazungumzo yao mpaka wakayamaliza na kisha kuondoka sehemu hiyo kurejea nyumbani.
MIEZI SABA BAADAE (SEVEN MONTHS LATER).
"Bwana Benjamin Benedicto una kubali Bi Agnes Mwengulo awe mke wako? Na je utampenda na kumlinda katika maisha yake?"....."Ndio nakubali"....."Chukua Pete hii na kisha umvarishe mkeo kama ishara ya upendo na umoja katika maisha yenu ya ndoa "....."Bi Agnes Mwengulo una kubali Bwana Benjamin Benedicto awe mume wako? Na je utampenda na kumheshimu kama mume wako wa ndoa?"....."Ndio nimekubali Benjamin Benedicto awe mume wangu,nami naahidi kumpenda na kumheshimu hadi pale kifo kitakapo kuja kututenganisha"......"Basi nawe Chukua Pete hii kisha mvishe mumeo kama ishara ya upendo na umoja katika maisha yenu ya ndoa". Yalikuwa ni maneno ya mchungaji katika ndoa ya Ben na Agnes iliyofungwa kwa maneno ya Mungu ndani ya kanisa lake takatifu.Harusi hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu wengi ikiwemo wadogo zake na Ben pamoja na mama Adera ilikuwa ni sherehe moja ya kipekee sana kuwahi kutokea.Ndoa hiyo ilifungwa na ikawa imehalalisha kuwa sasa Ben na Agnes ni wana ndoa halali
***************************
"Mama,Mathew,wadogo zangu,Jimmy pamoja mke wangu kipenzi Agnes leo hii natamani niyazungumze maneno haya mbele ya mboni za macho yenu.Nimegundua kumbe katika maisha ya hapa duniani ni bora uwe na rafiki mchafu na masikini utaishi nae kwa amani kuliko kuwa na rafiki mwenye pesa ambaye atakufanya uishi nae kwa mashaka.Steve mimi tulitoka nae mbali sana na hata siku moja sikudhani kama angekuja kunifanyia ubaya wote ule,,,ila napenda niseme tu kokote kule alipo Mungu na amrehemu maana hakuwa anajua lile alitendalo.Ni kweli Adera alinitoka katika kipindi kigumu sana tena kwa kifo cha uchungu na mateso ila najua kokote kule alipo Mungu tayari ameshaiweka roho yake pahala pema peponi.Nikiwa naishi nae katika maisha yetu ni mambo mengi sana ambayo tuliyapanga ikiwemo kuzaa watoto watakao kuja kutusaidia baadae,ila ndo hivyo tena kaburi limeshammeza.Sasa Mungu amenijalia neema nyingine tena ya kunipa mke mwema mwenye hulka ya Adera ambaye ni Agnes,,nampenda sana na nitazidi kumpenda hadi mwisho wa maisha yangu,,,,,Jina la Adera naapa sitolisahau,na kwa kuzingatia hilo endapo Mungu atanijalia mimi na mke wangu Agnes kumpata mtoto wa kike basi tutamuita jina la Adera kama kumbukumbu isiyofifia na mtoto huyo atakuwa zawadi kwako wewe mama yangu Bi Marry mzaa chema ambacho hakikudumu".Maneno hayo aliyaongea Ben wakati akiwa ameketi mbele ya watu wake hao ndani ya jumba la kifahali.Alitoa ahadi hiyo na historia ikaandikwa likabaki ni swala la muda tu.Siku moja ya juma mosi mnamo majira ya saa kumi za jioni.......Ben,Agnes pamoja na Mathew walionekana wakimalizia kuzipiga hatua za mwendo wa pole pole kuliendea kaburi ambalo Adera alizikwa wakiwa na mashada ya gharama kwa ajili ya kwenda kuyaongezea pale kama ishara ya upendo waliokuwa nao kwa binti Adera ambaye uhai wake ulidhurumiwa.Walikwenda na kuyaweka pale kisha wakamalizia na Sara kabla hawajaondoka."REST IN PEACE ADERA".Ben aliyaandika maneno hayo kwenye kijikaratasi kimoja kisha akakiweka juu ya kaburi la Adera na kumkumbatia mkewe Agnes..... Agnes nae akampokea na wote kwa pamoja wakalia,, Mathew aliongezeka pale nae akawakumbatia huku akiwatuliza.Walipoachiana walianza kuondoka pole pole."Twende mume wangu Ben tukayaendeleze maisha maana jua bado linaendelea kuchomoza,,,maisha yapo na yataendelea kuwepo,siku zetu zikiisha nasi tutaifuata njia ya utimilifu aliyoiendea Adera". Aliongea Agnes kisha wakashikana mikono na kuondoka pale kurejea kwao kuendelea na maisha.

MWISHO.
ASANTENI SANA WAPENDWA KWA KUWA NAMI
By Dannysimulizi

Post a Comment

Previous Post Next Post