PENZI LISILO SAHAULIKA 17---18💖💖


ZANZIBAR
Aliongea Steve nao wakasimama na kuanza kumsogelea Ben kasoro Mathew tu aliyekuwa akiwakodolea macho....walisogea haraka haraka hatimaye wakawa wamemfikia,ile wanajiandaa kumkamata mara mikono yao ikaonekana kama imetiwa ganzi wakabaki wakibishana wenyewe kwa wenyewe na kumuacha Ben akiwacheka tu huku akiwatishia kuwarushia jiwe alilokuwa amelishikilia mkononi mwake ."Twendeni tumkamate bwana....aisee twendeni bwana".Walihamasishana wakawa wanamfuata hivyo hivyo bila kujali mikono yao imepigwa gazi wala nini.Sasa baada ya kumfikia walimkaba kwa nguvu na kufanikiwa kumbeba,,,ile wanazipiga hatua mbili tu kutokea pale walipomkamatia ghafla alibadirika na kuwa Adera badala ya Ben."Pwaaaaa!! We....we...we....tunakufaaa".W
alimuachia kisha wakadondoka chini kwa kishindo na hapo hapo Adera akasimama na kuanza kuwakodolea macho.Wakati hayo yakiendelea boss wao Steve kwa muda huo yeye alikuwa ameshaelekea ndani kwenda kupumzika hivyo hakujua chochote kile kilichokuwa kikiendelea nje zaidi ya kupiga usingizi wake tu.Adera akiwa peku na gauni lake jeupe na refu alianza kuwafuata kwa mwendo wa taratibu huku akicheka sana."Hahahahaha!! Ahahahahaha!!" Aliendelea kucheka hatimaye akafanikiwa kuwafikia pale walipokuwa wameangukia maana hata nguvu za kuwafanya wakimbie hawakuwa nazo.Aliinyosha mikono yake juu kisha akawapiga upofu wote kasoro Mathew kisha akacheka tena na kutoweka eneo hilo.Walianza kutafutana huku wakilia na kugaa gaa chini..... Mathew yeye hakuendelea kubaki pale baada ya kuona amenusurika,ali
simama akawa ametimua mbio kuelekea porini.Alifika huko akawa ameenda moja kwa moja kujificha ndani ya kichaka kimoja hivi kilichokuwa kikionekana kuwa na utulivu wa kutosha.Ghafla ndani ya kichaka hicho kukasikika sauti ya vigeregere vilivyomkurupusha Mathew kwa woga na kumfanya atoke nduki kwenye kichaka hicho huku akipiga makelele ya nguvu....alikimbia hatua chache tu kisha akajikwaa na kudondoka chini.Kabla hajanyanyuka mara alihisi kama kuna kitu kimemnyanyua akasimama wima."Mathew... Mathew,wewe pekee ndiye nitakaye kusamehe kati ya wale wenzako wapumbavu.Na sababu iliyonifanya nikusamehe ni ule moyo wako wa huruma,,,wewe ndiwe utakaye kuja kuwa rafiki wa ukweli wa Ben hapo baadae baada ya kazi hii kumalizika.Kabla sijaondoka kwenda kuwashughulikia wale wapumbavu naomba uelekee mitaa ya Manzese kwenye jalala kubwa la Mtaa huo utamkuta Ben akiwa amelala,,,ukish
ambeba nenda nae hadi nyumbani kwako .Muda wote ule hatakuwa akijitambua,,,subiria hadi saa sita za Usiku .Muda huo ukiwadia mchukue uende nae hadi nyumbani kwetu nadhani unapajua,,,ukis
hafika huko mlaze pembeni mwa mlango wa geti la kutokea nje kisha wewe utaondoka muda huo huo,ila kesho yake uhakikishe unawahi kwenye muda wa saa kumi na moja za alfajili".Alisema Adera kwa sauti ya mwangwi kisha akajitokeza mbele kabisa ya Mathew nae akanyata mara tatu akatoweka pale mithili ya upepo.Mathew akiwa haamini kwa hicho alichokiona alitimua mbio hadi nyumbani kwake na kwenda kulala moja kwa moja pamoja na kwamba tayari majira ya mchana yalikuwa yameshawadia.Baada ya Adera kuondoka pale alielekea tena hadi kwenye ngome ya Steve na kwa mara hii alidhamiria kwenda kuwateketeza kabisa vijana wote wa Steve ili Steve mwenyewe awe wa mwisho kushughulikiwa tena kwa uchungu zaidi.Alifanikiwa kufika ndani ya ngome ile akawa amesimama mbele ya vijana wale kisha akajishika kiunoni kana kwamba anawashangaa.Al
iunyoosha mkono wake wa kulia akawafumbua macho yao nao wakawa wamesimama na kujaribu kukimbia,,,Walijaribu kufanya hivyo lakini hawakuweza maana miguu yao haikuwa na nguvu hata kidogo.Adera bila kupoteza muda alirusha juu vitu furani hivi vya ajabu vikaenda kuwanyonga shingoni kwa pamoja wakadondoka chini na kupoteza maisha hapo hapo.Aliinyanyua miili yao kisha akaivurumisha kwa hasira kama makaratasi ikaenda kwa kasi mithili ya upepo nayo ikaenda kudondoka ndani ya Bahari ya Hindi na kuzama moja kwa moja.
Masaa yalizidi kuyoyoma hatimaye ikawa imetimia saa kumi na mbili kamili za jioni,,, Mathew akiwa bado amelala kitandani kwake huku akiota ndoto kadha wa kadha za kutisha na za kuvutia,,,aliku
rupushwa na sauti kali "Mathew,,, Mathew amkaaa,,fanya kile nilichokuagiza.Pesa zipo chini ya uvungu nimekuletea nazo zitakusaidia kwa matatizo ya hapa na pale".Sauti hiyo ilisikika kisha ikatoweka masikioni mwa Mathew.Mathew alitoka haraka pale kitandani kwake kisha akatoka nje ya nyumba na kuanza kukimbia kuelekea mitaa ya Manzese kumfuata Ben.Alipofika ndani ya mitaa hiyo alinyoosha hadi kwenye jalala kubwa la mtaa huo akawa anamtafuta Ben kwa umakini mkubwa sana.Alimtafuta bila ya mafanikio mpaka akaanza kuchoka na kukata tamaa,,,alitaka kutoka ndani ya jalala hilo ila moyo wake ukasita akaamua aendelee tu kumtafuta huenda akafanikiwa kumpata.Akiwa anaendelea kufanya hivyo mara kwa mbali akaona kitu kimelala mithili ya mzoga akaamua kukifuata ,,,alitembea kwa tahadhari kubwa sana,akawa amekifikia.Kumbe siyo mzoga wala nini bali alikuwa ni mtu amelala . Mathew alichuchumaa na kuanza kumchunguza na mwisho akamtambua kwamba huyo ndiye Ben.Bila kujali uchafu wowote aliokuwa nao Ben , Mathew alimbeba kisha akamuweka mgongoni na kuanza kuelekea nae nyumbani kwake.Ben alikuwa hatamaniki hata kidogo,,,mwili wote ulikuwa ukinuka na kwa muda huo alikuwa amejisaidia haja zote,yaani haja kubwa na ndogo.Mathew hayo hakuyajali bali alimbeba hivyo hivyo na kufanikiwa kufika kwake.Alienda kumlaza kitandani akawa anasubiria mishale ya saa sita za Usiku iwadie aondoke nae tena hadi nyumbani kwa kina Adera kama alivyoelekezwa na mzimu wa Adera .
**********************
Giza totoro lilianza kuingia na jua nalo likawa linazama kwa kasi Sana.... taratibu Usiku ukaanza kuwadia na hatimaye ukatimia.Ilikuwa ni mida ya saa mbili za Usiku Steve alipokurupuka kitandani kwake na kutoka nje ili akawaangalie vijana wake maana kwa muda huo alishangaa kuona hakuna kelele za aina yoyote zikitokea nje ya ngome wakati siku zingine mishale kama hiyo huwa anasikia lapusha lapusha za hapa na pale kutoka kwa vijana wake hasa pale yeye anapokuwa ndani amepumzika.Alitoka nje kwa mwendo wa kunyata huku akiyaangaza macho yake kwa tahadhari,,,Ili ajiweke katika hali ya usalama zaidi alichomoa bastora yake akawa anatembea taratibu.Baada ya kufanikiwa kutoka ndani ya chumba chake alikwenda na kusimama nje akawa anaita "Oya mko wapi wadau??......Mr Mluto uko wapi aisee!! .....Oya wadau mko wapiii??" Aliita lakini hakuna sauti yoyote ile ambayo ilimuitikia zaidi ya kupokelewa na ukimya tu.Alizunguka hadi nyuma ya ngome akaendelea kuita."Mko wapi vijana wanguu!! ......Oya wadau mko wapi?? Ina maana mmekimbia au mmeenda kwenye mishe zenu??.....Oya wadau jitokezeni basi!!!.....Wadau mko wapi aisee".Aliita ghafla akasikia sauti kali ya kitu kama sufuria kubwa kikidondoka chumbani kwake ikifuatiwa na sauti hii "Mdau tupo humu ndani,,,,boss njoo tupo humu ndaniiii".....
INAENDELEA......................... 

SEHEMU YA 18.

"Nani wewe ??". Aliuliza Steve huku akigeuka kwa woga kuelekea chumbani kwake."Aaaah!! Boss kwa mara hii umeshanisahau?" Sauti ile ilimuuliza swali ,Steve alishindwa kuitambua kabisa sauti ile maana haikuwa ikifanana hata kidogo na moja ya sauti yoyote ile kutoka kwa vijana wake."Kwani wewe ni nani?" Aliuliza tena huku magoti yake yakianza kugongana kwa woga."Mimi ni kijana wako Mr Mluto".Sauti ile ilimjibu na hapo ndipo Steve alipoamua kujitoa ufahamu kuelekea chumbani kwake,,sasa baada ya kufika humo alishangaa kukuta sufuria kubwa likiwa limedondoka kitandani kwake .Akiwa haamini huku akiyaangaza macho yake juu ya paa la chumba hicho alishtukia mlango wa chumba ukijifunga wenyewe.Alipaniki akaitoa bastora yake na kuanza kuumiminia risasi mlango ule huku akipiga kelele za kuomba msaada.Sasa pamoja na kwamba alifanya hivyo lakini kelele zile wala hazikumsaidia maana ngome yake ilikuwa mbali sana na makaazi ya watu na kwa kipindi hicho giza nalo tayari lilikuwa limeshatanda.Ghafla bastora ikaishiwa risasi na kumfanya Steve azidi kuchanganyikiwa zaidi.Akiwa hajui afanye nini au ashike kipi alishtukia akirushwa na kubamizwa ukutani bila ya kumtambua aliyemrusha.Alinyanyuka kwa haraka kisha akalishika dirisha la chumba chake lililokuwa upande wa nyuma akaling'oa jumla jumla na kujirusha nje ......Alipotua tu chini kabla hata hajanyanyuka mara Adera akajitokeza mbele yake huku akiwa na hasira kali .Steve alimtambua vilivyo ikambidi awe mpole na ajaribu kumuomba msamaha."Ni samehe Adera,nisamehee!!". Aliongea Steve huku kijasho chembamba kikianza kumtoka usoni."Kamwe sitokusamehe wewe,lazima nikuue ili ahadi yangu itimie".Alisema Adera muda huo huo akianza kumfuata kwa mwendo wa kunyata."Adera nisamehe sitarudia tena". Aliongea Steve huku akianza kulia kwa uchungu,,,,Adera hakumsikiliza wala kumhurumia bali aliendelea kumfuta hadi akamfikia,,,baada ya kumfikia alimnyanyua kwa juu kwa kutumia mkono wake wa kushoto kisha akamkaba shingoni kwa nguvu na kumsukumizia kwenye mti mmoja mnene uliokuwa umepakana na ukuta wa kile chumba.Baada ya kumsukumizia hapo alimfuata tena."Adera nisamehee".Alizidi kuomba msamaha Steve."Sitaweza kukusamehe wewe,umeua watu wengi sana na umeuvunja uhusiano wangu na Ben kwa kuutoa uhai wangu,sasa leo na wewe ni lazima ukawasalimie kuzimu".Alipomaliza tu kuyazungumza hayo alimkamata shingoni na kumlarua kwa makucha marefu kisha akaing'oa shingo hiyo na akawa ameitenganisha na kiwiliwili .Hakuishia hapo alilipasua tumbo lake na muda huo huo akaubeba mwili mzima na kuurusha hewani.Mwili wa Steve ulionekana ukipepea kama karatasi ukaenda na kudondokea katikati ya msitu mmoja mnene na wa kutisha."Hahahahaha!! Nae ameshalipa". Aliongea Adera na kisha kutoweka pale kama mvuke.Baadae alikuja kutokelezea tena kule msituni akasimama mbele ya mzoga wa Steve na kuanza kuushuhudia mzoga huo ukishambuliwa na fisi waliokuwa wakiula na kuuzonga zonga huku wakifukuzana."Kazi imeisha na jukumu langu nimelikamilisha,ila kabla sijarudi kaburini lazima nimshuhudie Ben akiwa mzima tena ". Aliongea kisha akapotea pale na kutokomea sehemu za magharibi.
Baada ya masaa ya Usiku kusogea sana hatimaye saa sita kamili iliwadia...huo muda Mathew aliukumbuka vilivyo maana yale maagizo kutoka kwa mzimu wa Adera hakuwa ameyasahau.Alim
beba Ben akiwa hajitambui akafanikiwa kutoka nae nje ya chumba chake akasimama na kuonekana akiwaza kitu furani kwa takribani dakika mbili.Aliupiga konde moyo wake kisha akaanza kuzipiga hatua kuelekea nyumbani kwa kina Adera.Alitembea kwa mwendo wa haraka haraka sana ,na baada ya dakika kadhaa kupita alifika huko .Kabla hajamshusha Ben aliyaangaza macho yake kulia kushoto na baada ya kujiridhisha hakukuwa na mtu yoyote yule maeneo yale ,alimkimbiza haraka Ben na akawa amemlaza karibu na mlango wa geti la kutokea.Alitizama tena kushoto kulia akamalizia na upande wa nyuma yake na baada ya kujiridhisha alichomoka mbio kuondoka eneo hilo haraka sana . Alifanikiwa kufika kwake kwenye mishale ya saa saba kamili na bila kupoteza muda aliingia ndani moja kwa moja akawa ameenda kuumalizia usingizi wake ili ifikapo saa kumi na moja aamke tena.
Ilipowadia tu hiyo saa kumi na moja aliamka tena na kuanza kutembea kwa mwendo wa kukimbia kimbia kuelekea nyumbani kwa kina Adera.Alifika na kisha akajibanza ukutani kwa umakini zaidi akawa anasubiria wenyeji wa jumba hilo watoke ili nae ajitokeze endapo tu watamuona Ben eneo lile.Dakika ziliendelea kwenda mbio hatimaye saa kumi na mbili nayo ikaingia....Huku ndani alionekana Agnes mfanyakazi wa ndani wa kutumainiwa katika familia ile akizipiga hatua kuelekea kwenye mlango ule wa geti huku kwenye mkono wake wa kulia akiwa ameshikilia ufagio mrefu.Kwa vile bado kwa kipindi chote kile tangia mama Adera amuue mlinzi wake wa geti hakuwa amepatikana mlinzi mwingine,Agnes alifika hapo na kisha kuufungua huo mlango moja kwa moja......baada ya kutoka tu alijikuta macho yakimtoka kwa woga na bila kutarajia alianza kupiga makelele mpaka yakasikika na kumkurupusha mama Adera aliyekuwa amelala chumbani kwake. ."Agnes vipi ? Mbona unapiga yowe? Kwani kuna nini?" Aliuliza mama Adera huku akikimbia kimbia kutoka ndani ya chumba chake."Mamaa...mama njoo ujionee". Aliongea Agnes huku akiivirusha rusha vidole vyake."Kwani kuna nini ?" Aliuliza mama Adera huku akifika kwenye mlango ule wa geti."Ben....mama Ben". Aliongea Agnes muda huo huo Mathew akijitokeza pale alipokuwa amejifichia."Ben? I can't believe". Aliongea mama Adera huku mapigo ya moyo wake yakianza kwenda kwa kasi."Ndio mama...ni Ben sijui yupo hai,sijui amekufaa?" Alizidi kupayuka Agnes na hapo ndipo mama Adera alipotoka haraka ndani ya geti lile na kujikuta nae akiyatumbua macho yake kwa woga."Ben....Be
n....Ben".Alianza kuhaha huku akiwa hajui hata cha kufanya maana kwa mawazo yake baada ya Ben kupotea na kumtafuta bila mafanikio alidhani nae alifariki kama mwanae Adera."Mama kulikoni?" Aliuliza Mathew huku akianza kuwasogelea."Sa
mahani Kaka,huyu ni mkwe wangu,naomba utusaidie tumkimbize haraka hospitalini". Aliongea mama Adera huku akiingia tena ndani na kuiendea gari yake haraka ili akishaitoa nje ya geti wampandishe Ben na kumpeleka hospitalini.Ali
iwasha na kuitoa haraka humo akawa ameisogeza pembeni kidogo.Watatu hao walimbeba Ben na kumuingiza ndani ya gari kisha Mama Adera na Mathew wakapanda na kuingia humo ili waelekee kwa pamoja hospitalini.Sasa kabla hawajaondoka,,Mzimu wa Adera ulijitokeza mbele ya ile gari nao ukawa unatabasamu kabla haujatoweka.Hakuna hata mmoja ambaye aliuona mzimu huo.
*******************
"Mama kama hamtojali natamani na mimi niongozane na nyinyi kuelekea huko hospitalini". Aliongea Agnes na kumfanya mama Adera atabasamu kidogo.Sasa wakati mama huyo akitabasamu ule mzimu wa Adera ulijitokeza tena na kwa mara hii ulisimama nyuma ya gari na kuanza kutabasamu .Uliendelea kutabasamu kama dakika mbili hivi baadae ukapotea bila mtu yeyote kuuona."Na usafi je,au mwanangu ukirudi ndo utaufanya huo usafi?" Aliuliza mama Adera huku akiendelea kutabasamu,,,kwa muda wote ule baada ya Adera kufariki dunia na kupita siku nyingi,,Agnes mfanyakazi wa ndani wa nyumba ile alikuja kuonekana kama mbadala wa kuliziba pengo la Adera.Mbali na kwamba binti huyo mwenye umri wa miaka ishirini alikuwa mfanyakazi wa ndani tena wa muda mrefu ,mama Adera alikuja kumchukulia kama mwanae wa kumzaa huku akijiapiza moyoni mwake kutokuja kumpoteza kwa namna yoyote ile.Pia alipanga kumleta mfanyakazi mwingine wa ndani ili Agnes abaki kuwa kama mtoto wa pale na asimamie mambo makubwa ya kibiashara na masuala mengine mengi aliyokuwa akiyamiliki mama Adera.Kitu pekee ambacho kilimfanya mama huyo ampende Agnes na kuamua kumfanya kuwa kama mwanae kwa kipindi chote hicho ndiye aliyekuwa akimfariji na kumriwadha hasa pale tu anapomkumbuka mwanae Adera."Sawa mama,kwa hilo wala usijali". Aliongea Agnes huku na yeye akitabasamu na kuufanya mwanya wake uliobeba meno meupe uonekane waziwazi."Au acha tu mwanangu,huyu Jimmy anayelala mpaka saa mbili akiamka ndiye atafanya mambo hayo ya usafi.Panda twende mwanangu".
ITAENDELEA................. 

Post a Comment

Previous Post Next Post