PENZI LISILO SAHAULIKA 15---16


ZANZIBAR
Adam wakati akiendelea kutimua mbio kuelekea nje,kabla hata hajafika common room ya ile gest alishtukia akidondoka chini kama gunia la mzigo.....haraka haraka alisimama na kuendelea kutimua mbio hatimaye akaifikia ile common room akawa anatapa tapa kuutafuta mlango wa kutokea huku macho yake akiwa ameyatumbua mithili ya chura aliyekanyagwa na mguu wa tembo,aliendele
a kutapa tapa hatimaye mhudumu wa ile gest akaja pale na kumshuhudia akitapa tapa kama kipofu,maana hakuna alichokuwa akikifanya zaidi ya kuzunguka zunguka tu.Mhudumu yule kwa vile alikuwa ni wa kike ilimbidi ajiinamie aanze kucheka maana kile alikiona kama ni kituko cha mwaka,alijishika kunako sehemu yake ya mbavu kisha akasimama na kuanza kumtazama Adam kwa kumshangaa."Kaka kulikoni? Mbona unazunguka zunguka tu kama kipofu? Harafu upo uchi,ni kipi kimekupata?".Baada ya Adam kuyasikia maswali hayo yalikuwa kama yamemfumbua macho vile......Aliuona mlango wa kutokea nae akachomoka mle kama risasi akawa anatoka nduki za hatari.Ile gest aliiacha ikitema harufu kali ya kinyesi....na mhudumu baada ya kuligundua hilo ilimbidi Usiku huo huo aanze usafi kabla hakujapambazuka .Adam baada ya kukimbia vya kutosha alifanikiwa kufika ndani ya ngome yao na kwa bahati nzuri kwa muda huo bado Steve na vijana wake walikuwa hawajalala pamoja na kwamba tayari mishale ya saa sita za Usiku ilikuwa imeshawadia.Alifika speed speed akadondoka mbele yao na kuwafanya waengue kicheko kwa jinsi Adam alivyokuwa akionekana."Hahahahaha!! Daah hii dunia haitaishiwa vituko,huyu jamaa kama hajafumaniwa sijui". Aliongea Mr Mluto huku akiendelea kucheka."Twafaa jamani twafaa". Aliongea Adam huku akiwa amechanganyikiwa sana."Twafaa nini? Tunapowaambia mpunguze pombe na bangi muwe mnatuelewa,ukipewa uhuru jitahidi kuutumia kwa kiwango cha wastani.Wewe utakuwa umefumaniwa tu na ndio maana ukachomoka ukiwa katika hii hali". Aliongea Steve."Hapana boss ,Adera amerudi dunia kivingine na amesema amekuja kulipiza kisasi kwa mabaya yote tuliyomfanyia... almanusura tu anitoe roho ila akaniacha na kuniambia niwafikishie hii taarifa kwamba cha moto tutakiona". Aliongea Adam huku akitetemeka."Hahahahaha!! Unajua Adam unachekesha sana wewe,eti Adera amerudi duniani kuja kulipiza kisasi!! Bila shaka pombe pamoja na kufumaniwa vimeuchanganya ubongo wako,,na ndio maana unatapa tapa tu ,Boss kama vipi huyu jamaa tumpeleke chumbani kwake akalale labda pombe itamtoka na atakuwa sawa". Aliongea Mr Mluto kisha wakambeba kwa nguvu na kumpeleka hadi chumbani kwake.Sasa wakati wakilifanya hilo jambo walisikia sauti kali ya kilio cha Rashid kutoka ndani ya chumba chake,wakapigwa na butwaa.Haraka haraka walimtupa Adam kitandani kwake na kisha kuufunga mlango nao wakatoka nduki hadi kwa boss wao Steve."Nini kimetokea ,nini kimetokea?" Aliuliza Steve huku akiwa amesimama."Hatujui boss,hatujuiii ila tumesikia kilio cha nguvu kikitokea ndani ya chumba cha Rashid ila tumeshindwa kutambua ni kipi kimemfanya alie,labda anaota tu".Walijibu kwa pamoja wale vijana waliokuwa wamempeleka Adam chumbani kwake kwenda kulala."Hapana ,hicho siyo kilio cha mtu anayeota!! Kuna kitu kitakuwa kimempata au ameng'atwa na nyoka....Hebu nendeni mkamtazame ".Alitoa amri Steve nao wakatoka mbio hadi chumbani kwa Rashid,walipoufikia mlango waliusukuma nao ukafunguka muda huo huo maana haukuwa umefungwa kwa ndani......Hawakuyaamini macho yao baada ya kukiona kile walichokuwa wakikishuhudia.Damu mithili ya mtaro wa maji ilikuwa ikimchuruzika Rashid kutoka shingoni mwake huku akionekana kutokuwa na dalili zozote za uhai.Walijikaza huku wakitetemeka kimya kimya wakawa wanausogelea ule mwili kujua ni kitu gani kimetokea na kusababisha maafa kama hayo ."Daah! Wadau nini kimempata Adam?" Aliuliza kijana mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Hans.Hakuna hata mmoja ambaye alionekana kulijibu swali la Hans maana wote walikuwa wakitetemeka tu .Walipouchunguza zaidi mwili wa Rashid kwenye ile shingo waliona kama amechinjwa Kwa kutumia kisu kikali....wakazidi kuchanganyikiwa zaidi.Wakiwa hawajui waanzie wapi mara walisikia sauti ya kicheko "Ahahahahaha!! Ahahahahaha!!" Ikafuatiwa na kivuli cha mtu aliyekuwa akiishia ishia ukutani.Macho yaliwatoka...Wa
kasukumizana nje wote na kuanza kutimua mbio huku wakipiga makelele ya ajabu."Nyiee...
.Nyieee!!" Steve baada ya kuwaona wakikimbia bila mpangilio wowote ule aliwaita nao wakamfuata huku wakiwa hawaamini kabisa kwa kile walichokiona."Nyie vipi ,mjue siwaelewi kabisa...nimewatuma mkachunguze ni kitu gani kimempata Rashid lakini cha ajabu mmetoka mkiwa mnakimbia,tatizo ni nini??". Aliuliza Steve huku akichomoa bastora."Mkuu ngome imevamiwaaa.... Ngome imevamiwa mkuu ". Aliongea Hans huku akiachia ushuzi."Hahahah
aha".Alicheka kijana mmoja baada ya kuusikia ushuzi kutoka kwa mtu mwenye heshima zake kama Hans."Unacheka nini sasa? Acha ujinga ndugu yangu,,kwa muda huu hatupo kwenye utani". Aliongea Hans kwa hasira."Nini kimetokea,eti Jamal unaweza kutuambia ni kipi mmekikuta ndani ya chumba cha Rashid."Boss!! Huwezi amini kabisa,tumemkuta Rashid akiwa amekufa huku shingo yake ikiwa haitamaniki....
cha ajabu baada ya kuonekana tukiwa hatujui tuanzie wapi tulisikia sauti kali ya kicheko cha kike pamoja na kivuli cha mtu kilichokuwa kikiishia ishia ukutani na ndio maana tulitoka mbio ndani ya chumba hicho". Aliongea Jamal huku kijasho chembamba kikimtoka."Boss hali imeshaanza kuharibika cha msingi hapa tunatakiwa tuhame mara Moja maana tusipokuwa makini tutaangamia ndani ya dakika chache". Aliongea Hans huku akiwa amechuchumaa.Adam akiwa amelala ndani ya chumba chake huku usingizi ukionekana kumgomea kabisa ,Mara aliona kivuli cha mtu kikijitokeza na kutoweka."Haaa!! Aliamka pale kitandani na kukaa huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio.Kile kivuli kikazidi kufanya vituko....kwa mara hii kilionyesha umbo la kike huku sura ikionekana kuwa ni ya Adera kabisa."Mamaaaaaa !! Mamaaaaaa".Adam alianza kupiga kelele huku akiusukuma mlango wake ili achomoke nje haraka."Hahahahaha!!".Sauti ya kicheko ilisikika na hapo hapo ule mlango ukajifunga wenyewe.
"Adam....Adam!! Ahahahahaha!! Chagua nikuue kifo cha aina gani kwa kosa la kutaka kunikimbia?".Sauti ilisikika na kumfanya Adam arukwe na akili hapo hapo....Sasa kwa vile chumba chake kilikuwa na dirisha la wazi ,aliamua kujitoa ufahamu na kuruka kwenye hilo dirisha mara Moja .Sasa aliporuka tu na kufanikiwa kufika chini tayari tumbo lake lilikuwa halitamaniki maana lilipasuka na kutoa vijiutumbo vyote vya ndani na Adam akawa amepoteza maisha hapo hapo."Hahahahaha!! Hahahahaha!!" Sauti ya kile kicheko ilisikika hatimaye Adera akaonekana mbele ya mwili wa Adam....Aliyanyanyua macho yake juu huku kichwa chake kikibadirika na kuwa fuvu akaunyanyua ule mwili na kisha kuurusha hadi kwa kina Steve na wenzake."Pwataaaaa!! Puuuuuh!!".Ulipodondoka na kutoa sauti hizo wote walitoka nduki na kumuacha Mr Mluto pekee akiwa ameyatoa macho yake."Adam.....
Adammmm....Adam??" Alipayuka Mr Mluto na kuwafanya wale waliokuwa wamekimbilia kwenda kujificha waanze kurudi mmoja mmoja....Alianza Db K na wa mwisho kurudi alikuwa ni Hans.Adera baada tu ya kuwarushia ule mwili alionekana akichomoa kijidudu kimoja mithili ya funza chenye macho makubwa kutoka ubavuni mwake....alipok
ichomoa alikirusha juu kikaenda kudondoka juu ya kichwa cha Hans.Alicheka kisha akatoweka mara Moja eneo lile."Boss au twende kwa mganga wa kienyeji maana siamini macho yangu kabisa kwa hiki ninachokiona.....ndani ya dakika tano tu tumewapoteza wenzetu wawili ,, Rashid na Adam,,,na tumebaki wanane na wewe ukiwa wa tisa.....Sasa tulitazame hili kwa jicho la tatu maana haiwezekani Adam afe kwa kifo cha kutisha kama hiki". Aliongea Mr Mluto baada ya kuufunika mwili wa Adam kwa kutumia shuka la kimasai alilokuwa amejifunika."Itabidi kesho tuahirishe safari tuende kwanza kwa huyo mganga,nahisi kabisa Ben atakuwa anatufanyia umafia". Aliongea Steve.Wakiwa wanaendelea na mazungumzo yao ghafla Hans alianza kutetemeka.
************************
"Nakufa jamani nakufaaaa".Alilia Hans kwa uchungu na kuwashtua wenzake .Walimzunguka na kumshikilia huku wakiwa wamepigwa na bumbuwazi."Jamani nakufaaaa".Alipotamka tu hayo,Hans alianguka chini akawa ametulia kimya."Hans.....Hans....Hans".Akiita rafiki yake Jamal huku akianza kulia kwa uchungu."Amepat
wa na nini?? Amepatwa na nini jamani?". Aliuliza Steve huku akitetemeka."Boss wewe ni mpumbavu,nini hiki?? Boss nini hiki?? Wewe ni Mpumbavu". Alijibu Jamal huku akiendelea kulia ,Steve hakuwa na maamzi ya kumfanya chochote kile Jamal kama alivyozoea ,alimuacha tu.Dakika mbili baada ya Hans kudondoka chini na kutulia kimya,harufu kali ilianza kuzuka eneo lile.Waliziba pua zao huku wakiyaangaza macho kujua ni kitu gani kimeanza kutoa harufu hiyo.Mara ule mwili wa Hans ukaanza kubadirika,ile ngozi ilianza kuonekana kama inatokota vile baadae harufu ikawa inaongezeka."Wewe ni Mpumbavu boss,,,boss hufai,,,hufai,,, wewe ni mjinga,,,hufai"
.Aliendelea kutukana Jamal,uvumilivu ukamshinda Steve akaamua amtwange risasi tu."Nimekuvumil
ia vya kutosha ila kwa sasa uvumilivu acha niuweka kando". Aliongea Steve kisha akatoa bastora na kummiminia risasi saba mfululizo za kichwani.....Jamal akaanguka chini na kufa hapo hapo."Hahahahaha!! Ahahahahaha!! Nakutamani sana wewe Steve,yaani siku ya kifo chako ikifika utakufa kwa matesoooo".Sauti hiyo ilizuka hewani ......Steve na wenzake wote wakatawanyika kila mmoja njia yake wakawa wanatimua mbio."Ngome imevunjwaaaa kila mmoja afanye yakeeee!!". Aliongea Steve huku akitimua mbio kuelekea mjini,,,Alikimbia bila kupumzika akafanikiwa kufika Airport ya mwalimu Nyerere ili ikiwezekana apande ndege akimbilie mbali zaidi.Tayari kwa muda huo mishale ya saa kumi za Usiku ilikuwa imeshawadia.
INAENDELEA..................... 

SEHEMU YA 16.

Tayari kwa muda huo mishale ya saa kumi za Usiku ilikuwa imeshawadia.Steve alitembea kwa mwendo wa haraka haraka kulisogelea benchi moja la kisasa lililokuwa limewekwa upande wa kusini ....alilifikia kisha akakaa na kuanza kuyaangaza macho yake huku akionekana kuwa na wasi wasi wa hali ya juu sana.Aliitazama saa yake ya mkononi na kumfanya akitikise kichwa chake kana kwamba haamini kwa kile alichokiona kwenye saa hiyo,binafsi aliona masaa kama yanaenda taratibu sana.Akiwa amekaa kwenye benchi hilo,, ghafla kufumba na kufumbua ilikuja gari nyekundu mbele yake ikamfikia na kusimama nae akabaki akiitumbulia macho tu huku akijikuna kuna kichwani.Dakika tatu baada ya gari hiyo kusimama alishuka mrembo mmoja aliyekuwa amevaa sketi nyeusi iliyokuwa imeishia kwenye magoti pamoja na blauzi nyekundu iliyokuwa imembana kiasi,,,miguuni alikuwa amevaa viatu virefu kidogo vya kuchechemea vyenye rangi nyekundu..... Mrembo huyo alizipiga hatua kumfuata Steve pale alipokuwa ameketi akawa amemfikia na kisha kusimama mbele yake ."Mrembo mambo?" Alishoboka Steve pasipo kujua chochote kile kuhusiana na mrembo huyo."Poa tu Kaka,samahani ninaweza kukaa pembeni yako hapo?" Aliuliza mrembo huyo na Steve bila kufikiria mara mbili mbili alimruhusu nae akakaa.Mrembo huyo alianza kumtazama sana Steve huku akiwa kimya,Baadae akamshika begani na kuzungumza "Kaka kwa majina naitwa Recho,nimetokea Bagamoyo ila kwa hapa sina pa kwenda na isitoshe hapa jijini mimi ni mgeni hivyo kama hutojali nahitaji msaada wako". Aliongea na Steve akamkazia macho huku akimeza fundo la mate."Unataka nikusaidie Kivipi mrembo?" Aliuliza."Sina pa kulala natamani nikalale kwako harafu kesho asubuhi naondoka". Aliongea mrembo huyo na kumfanya Steve aanze kucheka ."Sasa mrembo hapa yamebaki masaa mawili tu papambazuke,si ungelala hata ndani ya gari yako ile". Aliongea Steve."Hapana Kaka yangu nahitaji sana msaada wako,hebu kwanza nitazame usoni kwangu ".Steve alimtazama mrembo huyo kisha akatikisa kichwa kama ishara ya kukubali ."Unanionaje kaka?" Aliuliza mrembo huyo huku akimtazama Steve kwa macho ya kumrembulia."Uko vizuri mrembo".Alijibu Steve huku akitazama pembeni."Kama nipo vizuri nisaidie sasa na kilicho kizuri zaidi nitakupa". Aliongea."Sijakuelewa......una maanisha nini kusema utanipa kilicho kizuri?". Aliuliza Steve."Nitakupa tunda langu la katikati ili ulifurahie".Alijibu mrembo huyo na kumfanya Steve afikirie zaidi,,alinyamaza kimya akawa anajiongelesha kimoyo moyo huku akimtazama mrembo yule kwa macho ya kuibia."Kwani huyu binti ametokea wapi huyu? Na kwa nini anifuate mimi kuniomba nimsaidie wakati kwenye eneo hili tupo wengi,,,nisije nikamsaidia harafu yakanitokea puani aisee....maana hili jiji halina utofauti na Zanzibar,nisije nikamsaidia nikajikuta nimesaidia jini,,potelea mbali siwezi kumsaidia huyu". Alijiongelesha Steve."Kaka vipi mbona kimya?" Aliuliza mrembo huyo."Dada kwa kweli mimi hapa labda nikuambie ukweli tu ,,,pamoja na kwamba unaniona nina kitambi lakini sivyo unavyofikiria.Na siyo kila mwenye kitambi ana pesa ,wengine wana vitambi lakini hawana pesa .Kuwa na kitambi siyo kigezo cha kuwa na pesa au cha kumiliki pesa,kwani kuna vitambi vingine vina asili ya utapiamlo". Aliongea Steve."Sijakuelewa Kaka,ina maana hutaki kunisaidia au?". Aliuliza mrembo."Siyo kama sitaki kukusaidia,kukusaidia nataka sana ila uwezo wa kukusaidia sina....mimi ni mlala hoi tu,nimeamua kuja hapa kupunguza maumivu ya kunguni kwenye kigodoro changu cha mbili kwa nne .Nimewakimbia kunguni dada yangu na ndio maana unaniona napiga miayo hapa". Aliongea Steve huku akionekana kuwa siriazi kwa kile alichokuwa akikizungumza."Kunguni ndo wadudu gani hao Kaka yangu?" Aliuliza mrembo huyo na kumshangaza zaidi Steve."Ona sasa huwajui hata kunguni,,,na ndio maana nikakwambia mimi uwezo wa kukusaidia sina,,nimewakimbia kunguni kwenye kigodoro changu cha ajabu .Kunguni dada yangu wasikie tu ni afadhari ungw'atwe na mbu kuliko wadudu hao". Alijibu Steve."Kaka mimi nipo tayari hata kama wataning'ata nitajikaza tu ili mradi kupambazuke". Aliongea mrembo huyo na kumtia hasira Steve."Dada tafadhari sana usitake kuniharibia pozi langu na isitoshe nina mambo mengi ya kuyafikiria kwa muda huu,sasa naomba usimame tu uondoke nisije nikakufanyia kitu kibaya". Aliongea Steve kwa ukali ."Yamekuwa hayo tena?". Aliuliza mrembo yule."Ndio kama ulivyosikia,nataka usimame uondoke kabla sijakufanyia kitu kibaya maana Mimi akili yangu naijua mwenyewe". Aliongea Steve na hapo hapo yule mrembo akasimama na kumtazama kwa muda wa dakika tano kisha akaanza kuondoka mbele yake huku akigeuka geuka nyuma.
Alitembea taratibu hadi akaifikia gari yake na kupanda hadi ndani....Sasa baada ya kukaa kwenye usukani,mrembo yule alianza kujibadirisha.Kufumba na kufumbua akawa Adera na gauni lake jeupe.....Damu ilianza kumvuja kunako sehemu yake ya siri huku akicheka sana kwa kicheko ambacho hakikuwa cha kawaida,,,Aliidrive ile gari akakata kona moja tu ,gari ile ikapotea eneo lile bila kujua ilielekea wapi.Saa kumi na mbili ilifika na Steve akaanza kutafuta uwezekano wa kupata tiketi ya ndege ili aondoke nchini maana kwake aliona hali imeshakuwa tete akizembea kidogo tu yata mtokea puani,,,,Alielekea kunako sehemu wanapokata tiketi hizo,,akajaribu kupapasa mifuko yake ya suruali akajikuta hana hata senti tano.Alichanganyikiwa akajiengua kwenye ile line akawa anakazana kuelekea pembeni huku akiichomoa simu yake.Alibofya namba moja ya Mr Mluto simu ikaanza kuita.......Adera aliusikia ule muito wa simu ya Mr Mluto akaufuata na kwenda kujitokeza hadi ndani ya nyumba ya jamaa huyo ....alipofika humo aliachama kidogo yakatokea meno marefu kinywani mwake kisha akaichukua ile simu na kuipokea huku sauti yake akiwa ameibadirisha na kuifanya ifanane na ile ya Mr Mluto mwenyewe."Haloo Mr Mluto,mbona unachelewa sana kupokea simu?"....."Nilikuwa naoga boss ,kwani kuna nini?"....."Nimesahau ATM card yangu ya Benki"...."Benki gani ?"....."CRDB"......."Sasa unataka nikusaidieje kwani ?"...."Nenda kwenye ngome yangu haraka kisha niletee hiyo ATM ndugu yangu maana ina pesa nyingi sana"......"Boss kwani we upo wapi muda huu?"...."Nipo Airport nina mpango wa kuihama nchi niende nchi za mbali".
******************
"Boss labda nikuambie ukweli tu kwamba huna haja ya kukimbia kwa sababu tu ya yale maruweruwe,tayari nimeshaweka mambo sawa na ngome imerudi katika hali yake ya kawaida,rudi ngomeni boss".Maneno yale yalimvutia sana Steve na kumfanya ayaamini bila kujua kama aliyaongea Adera kwa kujifanya yeye Mr Mluto.Haraka haraka huku akitabasamu Steve aliamua kuighaili safari yake na kurudi tena ngomeni.Sasa Adera baada ya kumaliza hilo alichokifanya ni hiki alichomoa nywele zake chafu zilizokuwa na vijidudu sita akazirusha hewani nazo zikatawanyika na kutoweka.Kumbe nywele hizo zilikuwa na lengo maalumu la kuwarudisha kwa nguvu vijana wote wa Steve pale ngomeni bila kujali kwa muda huo walikuwa maeneo gani.Sasa baada ya dakika zipatazo ishirini,,,Mr Mluto alionekana akitimua mbio kuelekea kwenye ile ngome huku akihema sana,,,alipofika alimkuta Db K akiwa ameshawasiri kitambo nao wakakaa kwa pamoja huku wakitazamana.Baadae kama dakika saba hivi na vijana wale wengine nao wakawa wanachomoka mmoja mmoja kutoka katika sehemu zao huku wengine wakiwa wameyavua mashati yao.Walipokamilika wote ,Boss wao Steve nae aliwasiri hapo ngomeni."Boss njaa mbaya sana aisee,,maisha ya kitaa yamekuwa magumu ndani ya masaa matatu tu,ndio maana tumeamua kurudi tena hapa". Aliongea kijana mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Matt."Harafu boss nimepata suruhisho la tatizo letu kama vipi tulit.....??" Matt hakuimalizia sentensi ile,wakajikuta kwa pamoja wakitumbua macho baada ya kumuona Ben akija mbele yao huku akiwa amevaa kaptura nyeupe iliyokuwa imetapakaa uchafu mweusi pamoja na shati refu jekundu lililokuwa limetoboka mgongoni,,,Udenda nao ulikuwa ukimtoka kwa Kasi sana."Huyu jamaa kashakuwa kichaa wa kutupwa sasa". Aliongea Mr Mluto na kumfanya Ben achukue jiwe kubwa na kulitia kwenye mkono wake wa kulia."Huyu ndiye anayetutesa kama vipi tumuue ili tuishi kwa amani". Aliongea Db K na wenzake wote wakamuunga mkono kasoro kijana mmoja tu aliyekuwa akiitwa Mathew."Jamani tusimuue ,tutakuwa na hatia kubwa sana,cha msingi kama itawezekana tumsaidie tu....tuweni na huruma jamani". Aliongea Mathew huku akimtazama Ben aliyekuwa akitembea kwa kuchechemea chechemea."Kati ya maboya wewe Mathew ni boya wa kupindukia,hili chizi tukiliacha hai litatukositi tuliuwe tu".Alisema Mr Mluto huku akimkazia macho Mathew."Hapana,cha kufanya ni hiki mkamatane kisha nendeni nae mkamtupe baharini afie huko". Aliongea Steve nao wakasimama na kuanza kumsogelea Ben kasoro Mathew tu aliyekuwa akiwakodolea macho.
ITAENDELEA....................... 

Post a Comment

Previous Post Next Post