PENZI LISILO SAHAULIKA 13---14😘

ZANZIBAR
Baada ya Steve kumaliza kumuangamiza kijana huyo aliondoka muda huo huo mbele ya wale vijana wengine waliokuwa wamejipanga kwenye ule mstari akawa anazipiga hatua kuifuata gari yake ili aondoke.Hakuwaongelesha kitu chochote alibaki kimya tu,sasa baada ya kuifikia gari yake aliingia ndani na kisha kuiwasha na kuondoka huku akiwaachia maswali mengi vijana wake yasiyojibika."Aaaah!! Jamani hata kama ni uzwazwa huu umepitiliza aisee,haya manyanyaso anayoyafanya boss Steve yameshaanza kuvuka mipaka,binafsi maisha haya ya kibabe nimeshaanza kuyachoka".Ilisikika sauti ya kijana mmoja aliyekuwa amevaa koti jeusi refu akiyaongea maneno hayo."Sasa wewe na akili zako hizo za bata unatakaje kwa mfano? Hapa hujalazimishwa ukichoka unajisepea tu maana hakuna anayekulazimisha,njaa zako ndizo zilizokufanya uje hapa". Aliongea Mr Mluto na hapo ndipo kulipozuka malumbano baina yao,wakawa wanabishana sana na mwisho yakajitenga makundi mawili ambayo yalianza kugombana sana,kundi moja lilikuwa ni la wale waliokuwa wakimuunga mkono Steve na jingine lilikuwa ni lile ambalo lilikuwa likiyapinga yale yaliyokuwa yakifanywa na Steve,ila pamoja na yote hayo kundi ambalo lilishinda lilikuwa ni lile ambalo lilikuwa likimuunga mkono Steve.Kwa upande wa Steve baada ya kuondoka ndani ya ngome yake alielekea moja kwa moja hadi mahakamani maana ule muda wa Ben kuhukumiwa tayari ulikuwa umeshaanza kusogea......alifika huko kama dakika ishirini tu na akakuta tayari watu kadha wa kadha wameshajiandaa kwa ajili ya kuisikiliza hukumu ile,Steve alikaa nyuma kabisa akawa anajishika puani tu huku akimuangalia Ben aliyekuwa amesimamishwa mbele akisubiri hukumu .Muda wa hukumu ulipowadia hakimu alisimama akatoa nafasi mbili tu za mashahidi wa ile kesi upande wa washtaki,,,Steve alinyoosha mkono nae akapewa nafasi ya kuzungumza.Alisimama kwa maringo sana kisha akaitengeneza vizuri suti yake,na baada ya hapo akapita mbele na kwenda kutoa heshima kwa hakimu.Alikohoa kidogo kisha akaanza kuzungumza mbele ya maiki."Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana mheshimiwa hakimu kwa kunipa nafasi hii adimu,unajua katika dunia hii siku zote usimuamini sana mtu hata kama ni ndugu yako wa damu,,,Okey eneway tuachane na hayo,,,jana kwenye mishale ya saa kumi na moja ndani ya hotel kubwa ya kimataifa ya Savannah,nikiwa katika matembezi yangu ya kawaida tu nilimuona huyu mtuhumiwa akiwa amekaa site moja na marehemu Adera wakinywa sijui pombe sijui nini,nikawa nawatazama tu,sasa kwa vile niliamini marehemu yupo na mumewe sikuwa na hofu juu yao.Niliingia vizuri ndani ya hotel hiyo ilaaaa......??" Kabla Steve hajamalizia sentensi yake ghafla mbele yake akaonekana Adera akiwa amesimama huku kwenye mkono wake wa kushoto akiwa ameshikilia kisu kirefu akimsonta Steve kwa hasira,,,, Alikuwa amevaa gauni refu ambalo lilikuwa limegusa chini na kuifunika miguu yake."Nooo!!...Nooo!! Adera ,,Adera,Aderaa!
!".Steve aliyatamka hayo kisha akatimua mbio kutoka nje akiwaacha watu ndani ya ile mahakama wakiwa mdomo wazi."Amepatwa na nini huyo mfuateni tafadhariii".Hakimu alitoa amri ,Steve akawahiwa na kisha kurejeshwa tena ndani."Sasa kijana mbona hatukuelewi,unaongea harafu unatimua mbio kutoka nje,tunahitaji utuambie ni kipi ambacho kimekufanya ukimbie nje?" Aliuliza Hakimu na kumuacha Steve afunguke ni kitu gani kimemfanya hadi aanze kukimbia.Huku hayo yakiendelea Ben nguvu zilianza kumuishia akawa anatetemeka na hazikupita hata dakika tano akandondoka chini na kupoteza fahamu.Hali ya sintofahamu ilizuka ndani ya mahakama hiyo,watu wakawa wanashangaa tu huku wasiamini ni kitu gani kimetokea....maaskari watatu walimfuata Ben alipokuwa amedondokea wakamkuta yupo hoi sana huku muda huo povu jingi likimtoka mdomoni na puani,,,haraka haraka walimbeba juu juu na kisha kumkimbiza hospitalini haraka.Steve nae hakuweza kuwaambia kitu chochote kwani alitimua mbio hadi nje kunako gari yake akapanda na kuondoka fasta eneo lile bila kupoteza muda.Sasa kwa vile mambo yalivurugika,hakimu ile kesi aliiahirisha mpaka pale mambo yatakapokaa sawa.
Ben akawa amepelekwa hospitalini,alipofikishwa huko alikuwa na hali mbaya sana maana hata kuhema tu alikuwa akihema kwa taabu.Madaktari walipokuja kumpima waligundua presha yake ilikuwa imepanda maradufu huku mapigo yake ya moyo yakiwa yameshuka sana.Hawakuwa na cha kupoteza walianza kuhaha kuhakikisha wanayaokoa maisha yake haraka sana maana hawakuwa na kitu kingine cha ziada.
Kwa upande wa Steve baada ya kufika kwake alimuamru kijana mmoja amtolee kiti akae pamoja na maji ya kunywa maana kiu ilikuwa imemteka vya kutosha,Alipoletewa hayo maji,ile anayapeleka tu mdomoni kufumba na kufumbua yaligeuka na kuwa damu."Pwaaaaaa!!" Steve aliyamwaga chini na kisha kama roboti alisimama na kujaribu kutimua mbio,,,alipiga hatua chache tu vijana wake wakamuwahi na kumkamata."Boss vipi mbona hatukuelewi?" Aliuliza Db K huku akiyaangaza angaza macho yake."Aisee vijana wangu hali imeshaanza kuwa tete,hapa mambo yameshaanza kuharibika". Aliongea Steve kwa sauti ya uwoga huku akitetemeka."Kivipi boss hebu tufafanulie" Aliongea kijana mwingine aliyekuwa akijulikana kwa jina la Adam."Ni nguvu tu nilizozitumia kuchomoka ndani ya ile mahakama maana bila ya hivyo almanusura niuongee ukweli wote kuhusiana na kifo cha Adera , kwenye koo langu kuna kitu kilikuwa kikinisukuma kufanya hivyo nikaona ni bora nichomoke tu maana hakukuwa na namna nyingine.Kibaya zaidi nilimuona Adera akiwa amesimama mbele yangu na ilionekana alikuwa na hasira sana". Aliongea Steve huku jasho likimtoka makwapani na shingoni."Boss acha utani,Adera si amekufa? Acha utani boss". Aliongea Mr Mluto."Hapa nchini siyo sehemu ya kuishi tena,inatakiwa tuhame haraka maana tukiendelea kukaa humu basi tumekwisha". Aliongea Steve na vijana wake wakawa wamemuelewa na hapo mipango ya wao kuihama nchi ikaanza mara Moja .Siku tano mfululizo zilipita hatimaye mwili wa Adera ukawa umezikwa na kubaki historia tu kwamba palikuwepo binti mmoja mrembo sana aliyekuwa akiitwa Adera.Mpaka mazishi hayo yana malizika bado Ben alikuwa hajapata fahamu na ubongo wake kwa muda huo ulikuwa haufanyi kazi kabisa.
MWEZI MMOJA BAADAE .
Ben alizinduka mule hospitalini lakini alikuwa amechanganyikiwa vya kutosha na alikuwa hana tena uwezo wa kuongea maana ulimi wake ulikuwa mzito na alikuwa amegeuka kuwa bubu.Madaktari walipojaribu kumuweka katika hali ya utulivu zaidi aliwashinda nguvu nae akachomoka katikati yao na kuanza kutimua mbio kuelekea pande za kusini.Walijaribu kutuma watu wamkimbize lakini haikuwezekana kwani aliwashinda mbio na kukimbilia kusipojulikana.Ben alifika mbali sana kisha akaelekea kwenye jalala moja hivi akaenda kukaa humo na kuanza kuimba nyimbo zisizojulikana . Upande mwingine ile mipango ya Steve na wenzake kuhama ilifikia patamu na kesho yake ambayo ilikuwa ni siku ya juma nne ilikuwa ndo siku ambayo walitaraji kuihama nchi ili waende nchi za mbali.Usiku wa kuelekea siku hiyo Steve alifanya kikao kikubwa sana na vijana wake hao wakawa wanapanga ni nchi gani wataelekea kwa usalama wao.Basi kwa pamoja walikubaliana waelekee Madagascar ili wakaishi huko bila ya kubuguziwa na kitu chochote kile.Walipomaliza kikao chao hicho kila mmoja akapewa uhuru wa kufanya chochote ndani ya Usiku huo kabla hakujapambazuka
.Mishale ya saa mbili kamili Adam na mwenzake mmoja walielekea ndani ya baa moja kwenda kupata viburudisho vya hapa na pale,,,Walifika ndani ya baa moja wakanywa sana mpaka wakaanza kulewa.Waliporidhika walisimama kwa pamoja wakawa wanakokotana kutoka nje huku wakiweweseka,,,Kwa vile giza lilikuwa limetanda kila mahali hawakujua waelekee wapi ukizingatia akili zao zilikuwa zimefunikwa na pombe,,,Walitem
bea kwa mwendo huo huo mpaka wakafanikiwa kuipata barabara moja hivi ya changarawe iliyokuwa imezungukwa na nyasi fupi fupi pembeni yake.Sasa wakiwa wanatembea ghafla mbele yao ikawa inakuja gari yenye rangi nyekundu,ikafan
ikiwa kuwafikia na ikawa imesimama mbele yao.
**************
"We....weee...we Dereva acha ufala,pisha njia tupiteee". Aliongea Adam huku akiweweseka.Kioo cha kushoto cha gari ile kilipofunguliwa dirishani alichungulia msichana mmoja mrembo sana ambaye alikuwa amevaa miwani ya urembo machoni mwake."Samahanini Kaka zangu,nauliza njia ya kuelekea Bagamoyo mnaweza kunielekeza ?". Aliuliza mrembo huyo huku akiivua miwani yake."Ahaa!! Kumbe unaulizaa hivyooo! Poa barabara ile paleee umeiacha ifuate hiyo hiyooo". Aliongea Adam kwa sauti ya kilevi."Asanteni Kaka zangu na Samahanini kwa usumbufu". Mrembo yule aliyaongea yale kisha akakirudishia kikoo cha gari yake na kisha kuanza kuondoka.Sasa cha ajabu ile gari haikujulikana ilielekea wapi au ilipitia wapi maana ndani ya dakika tano tu,Adam na mwenzake hawakuiona tena pamoja na kuyaangaza macho yao kuitafuta."Oya ile gari imepitia wapi mbona siioni?" Aliuliza Adam kwa mshangao huku pombe ikianza kumtoka."Jamaa angu wewe ni mtu wa ajabu sana unaniuliza gari imeelekea wapi wakati hapa tulikuwa wote?" Aliuliza rafiki yake huyo ."Haya tusibishane sana,tuendelee na safari yetu". Aliongea Adam nao wakazidi kuchanja mbuga kuelekea mbele.Baada ya kuziacha hatua chache tu nyuma ile gari ilionekana tena ikija mbele yao.....ilipowafikia ilisimama na kwa mara hii yule mrembo akashuka ndani ya gari ile na kuanza kuwafuata.

INAENDELEA..................................... 

SEHEMU YA 14.

Alipowafikia aliinama kidogo kana kwamba kuna kitu alikuwa amekidondosha chini ili akiokote,,,,baada ya kusimama wima aliwapungia mkono Adam na mwenzake kama ishara ya kuwasimamisha baadae nao wakasimama na kuanza kumsubiria mrembo huyo.Walianza kuulizana kimya kimya kwa ishara kisha Adam akajikohoza na kumwambia mwenzake amsubiri hapo ili yeye amsogelee zaidi yule mrembo,Alizipig
a hatua za haraka haraka huku akiweweseka akawa anamkaribia.....cha kushangaza kadri alivyokuwa akimkaribia mrembo huyo ndivyo ile pombe ilivyozidi kumtoka zaidi.Alifanikiwa kumfikia wakawa wamesimama kwa kuangaliana."Samahani Kaka yangu unaitwa nani?" Aliuliza mrembo huyo.Adam huku akianza kujichekesha chekesha alimjibu "Mrembo mimi ni handsome boy au niite Adam". Alijibu Adam kwa sauti ya kishalobaro."Aha,sasa Adam naomba unisaidie yaani hapa nilipo nimetoka sehemu za mbali na kwa Usiku huu sijui hata pa kulala,natapa tapa tu". Aliongea mrembo huyo.Kitu ambacho Adam hakukijua yule mrembo alikuwa si mrembo wa kawaida bali ule ulikuwa ni mzimu wa Adera ambao uliamua kuja duniani kwa ajili ya kulipiza kisasi na ikiwezekana kumuokoa Ben ambaye alikuwa matatizoni.Sema tu kwa wakati huo mzimu uliamua kujivisha sura ya kike na yenye mvuto zaidi ili ufanikiwe kuwanasa maadui wote ikiwemo Steve mwenyewe."Mrembo hilo halina shida ,kwa hapa Mimi nitakusaidia wala usijali kabisa". Aliongea Adam huku akimkodolea macho mrembo huyo ."Utanisaidia kivipi Adam?" Aliuliza."Labda nikuulize tu ,upo tayari kulala na mimi gest?" Aliuliza Adam huku akilitumbulia macho wowowo kubwa la mrembo huyo.Mrembo alitazama pembeni akawa anacheka kimya kimya huku kidole chake cha mwisho cha mkono wa kulia akiwa amekiweka mdomoni."Nijibu basi mrembo?" Aliongea Adam huku akionekana kuwa na shauku kubwa ya kwenda kulila tunda la kati la mrembo yule ."Aaaah ! Kizuri hakihitaji haraka Adam mi nilikuwa nafikiria ni kwa namna gani nitaweza kulijibu swali lako hilo,ila hamna shida mi nimekubali tutaenda kulala wote huko,ila hatutafanya kitu chochote kile zaidi ya kulala tu". Aliongea mrembo."Unamaanisha nini kusema hivyo?" Aliuliza Adam."Namaanisha hatutafanya mapenzi maana Mimi nipo kwenye siku zangu". Alijibu mrembo huyo ."Sawa mi nimekupata ila hujaniambia jina lako ,unaitwa nani kweli?" Aliuliza Adam."Mimi naitwa Recho". Mrembo alimjibu muda huo huo bila kupoteza hata sekunde mbili.Adam baada ya kuonekana tayari ameshaelewana na Mrembo Recho alimfuata yule mwenzake kisha akamfikia na kumnong'oneza kwa takribani dakika tatu baadae akamsogelea tena yule mrembo."Mrembo Recho tunaweza kuondoka sasa maana kila kitu nimekiweka sawa". Aliongea Adam huku akimsogelea na kumshika mkono wakawa wanaondoka kuelekea mjini kwa ajili ya kutafuta gest."Mrembo Recho si niliona kama umeshuka ndani ya gari yako?" Aliuliza Adam."Akaa! Mi wala sijashuka ndani ya gari,mi nilikuwa natembea kwa miguu tu...sina gari wala nini". Aliongea Mrembo yule.Adam alimkubalia tu pasipo kujua chochote kile nao wakazidi kutoka kwenye kile kinjia na hatimaye wakafanikiwa kuipata barabara ya lami iliyokuwa imezungukwa na taa upande wa kulia na upande wa kushoto.Baada ya wao kuondoka,yule rafiki yake na Adam alibaki pale akishangaa tu maana ile gari alikuwa akiiona bado ipo pale na Mrembo hajaondoka nayo.Sasa akiwa anaendelea kuitumbulia macho alishtukia gari ile imewashwa ,jamaa moyo wake ukapasuka paaaah! .Huku akitetemeka aliamua kuisogelea kujua ni nani aliyeingia ndani ya gari hiyo kimya kimya na kuiwasha,,alizipiga hatua za kunyata akawa anaisogelea.Alipoifikia alichungulia kwa kujificha ficha na baada ya kukiona kile alichokishuhudia kwa macho yake nguvu zilimwishia .Ndani ya ile gari alimuona mtu ambaye si wa kawaida kabisa .... alikuwa ni mtu mwenye kichwa kama fuvu pamoja na mwili uliokuwa umetapakaa funza na kulikuwa na harufu kali sana ilikuwa ikitoka humo.Alijikuta akitetemeka mpaka magoti yake yakagusa chini.Akiwa hajui afanye nini ghafla nyuma yake akasikia kama kuna mtu anakuja,aligeuka haraka lakini wala hakumuona mtu huyo.Wazimu ulimjia akasimama kama kichaa na kisha kuanza kutimua mbio kuelekea kichakani,,,Alienda kuingia ndani ya kile kichaka ila kabla hata hajatulia alisikia kicheko kikali mithili ya kile cha mtoto."Hahahahaha!! Hahahahaha!!".A
lichomoka kama risasi ndani ya kile kichaka akawa anatimua mbio bila kugeuka nyuma mpaka akafanikiwa kufika kwenye ile ngome ya boss wao Steve.Alifika huko akiwa taabani sana."Vipi Rashid mbona unahema sana kulikoni?" Aliuliza Steve aliyekuwa amekaa nje ya ngome yake huku vijana wake wapatao nane wakiwa wamemzunguka."B
oss.....Boss!! Nimekutana na shetani,boss nimekutana na shetani". Aliongea Rashid huku akiyaangaza angaza macho yake."Umekutana na shetani? Ahahahaha! Pombe wadau ni mbaya sana aisee,mmemsikia huyu jamaa? Eti amekutana na shetani daah!!". Aliongea Steve huku akimkazia macho Rashid."Boss sijalewa bado,nimekutana na shetani kabisa". Aliongea huku akizidi kutetemeka."Na mwenzako Adam umemuacha wapi?" Aliuliza Steve huku akicheka."Ameenda gest na Mrembo mmoja hivi,ila huyo mrembo ni jini,ni jiniiiii". Aliongea Rashid Steve ikambidi awaamuru vijana wawili wamuingize ndani akalale ili pombe zimtoke na akili itulie.
Upande mwingine alionekana Ben akiwa anakula mkate jalalani muda huo huo akiwa ameivua suruali yake iliyokuwa imechanika makalioni.Mkate ule wakati akiula alikuwa akicheka cheka tu na wakati mwingine kuongea maneno ya kumng'unya mng'unya yasiyoeleweka maana ule uwezo wa kuongea maneno ya kawaida hakuwa nao maana kwa muda huo alikuwa kashakuwa bubu.Sasa wakati akiendelea kuula huo mkate mara kwa nyuma yake akasikia sauti ya kike ikimuita kwa upole."Ben!! Ben".Ile sauti aliitambua vizuri sana ila akashindwa kuijua ni sauti ya mtu gani kutokana na akili yake kutokuwa sawa.....aligeuka na kumkuta msichana mmoja aliyekuwa amevaa gauni refu jeupe akimtazama kwa upole sana."Buuuuh!! Jidubuuu!! Dadaaadaa!! Buuuuh,,Ftuuuuuh". Aliongea Ben yule msichana machozi ya uchungu yakawa yanamtoka maana alimhurumia sana."Ben mi ni mkeo Aderaa ". Aliongea yule msichana ila Ben wala hakuelewa chochote kile."Ben mume wangu yaani umekuwa hivi jamani?" Aliongea kisha akainyoosha mikono yake yote akawa ameruka na kumfikia Ben alipokuwa amekaa.Alinyoosha mikono yake kisha akaiweka juu ya kichwa cha Ben nae akawa ametoweka muda huo huo na kumuacha Ben akiendelea kula mkate wake bila ya wasiwasi wowote ule.Kwa upande wa Adam baada ya kufika gest na yule mrembo walipata chumba kimoja kizuri kiasi wakaingia humo kisha kwa pamoja wakaenda na kukaa juu ya kitanda kiichokuwemo humo.
****************
"Adam naomba nielekee bafuni nikaoge maana nahisi nina uchovu sana". Aliongea yule mrembo na Adam bila kinyongo akamruhusu nae akaelekea bafuni kwenda kuoga.Akiwa humo bafuni baada ya kuzivua nguo zake,mwili wote ulikuwa ukivuja damu na kuna wakati ulikuwa ukitoa vijidudu furani hivi vya kutisha.Aliachama,mdomo wake ukawa na meno marefu mithili ya misumari baadae akacheka sana huku akiinyoosha mikono yake iliyokuwa ikichomoza kwa makucha marefu kama mishale.Wala hakuoga humo zaidi ya kufanya vituko vya hapa na pale tu.Baada ya dakika tano alitoka humo akaelekea tena chumbani mule alimokuwemo Adam."Mrembo una mashine mikononi mwako nini?" Aliuliza Adam huku akimtazama kwa matamanio."Kawaida tu". Aliongea mrembo huyo huku akikaa juu ya kitanda."Recho mimi hamu zimenizidi mwenzio naomba unihurumie nisije nikafanya kitu cha ajabu". Aliongea Adam huku akianza kumshika shika."Niachie basi Adam mbona we siyo muelewa?" Aliongea mrembo huyo."Hapana nipe niingize hata kichwa tu". Aliongea Adam huku akianza kuvua nguo zake zote."Si nilikuambia nipo kwenye siku zangu jamani? Au unataka nikuambukize ugonjwa?" Aliuliza mrembo.Adam kutokana na hamu kumzidi hakuweza kuelewa chochote wala kumsikiliza yule mrembo.Alimkama
ta kwa nguvu kisha akamlaza pale kitandani na kisha kujiandaa kumbaka,,,akiwa anahangaika kumchomolea ile kanga,ghafla uso wa yule mrembo ukageuka na kuwa uso wa Adera mwenyewe.Adam aliruka pale kitandani kama chura akaenda kuangukia mlangoni."Hahah
ahaha!! Ahahahaha!!" Alicheka kwa sauti kali ,kufumba na kufumbua ule mwili wa Adera nao ukajitokeza dhahiri."Hahahahaha!! Adam njoo unibake sasa,si unajifanya una nguvu na unajua kubaka njoo unibake Hahahahaha!!". Adera alishuka pale kitandani akiwa na gauni refu jeupe akawa anamsogelea Adam huku akimcheka sana."Noo...Nooo...we Shetani nakuamuru tokaaaa !! Shetani tooo.....tokaaaa ".Alipayuka Adam huku akiyasugua chini makalio yake kusogea nyuma."Shetani nani kati yangu na wewe? Sasa mfikishie salamu boss wako kwamba nimerudi tena,na damu yangu mtailipa ". Adera aliongea huku kichwa chake kikianza kuwa kama fuvu.Adam macho yalimtoka akawa anatetemeka sana huku kinyesi kikianza kumpa tahadhari kwamba kipo njiani."Ni.....ni.... Nisamehe". Aliongea Adam ,Adera akamcheka na kisha kumtandika kofi moja tu la usoni lililokitoa kinyesi chote kilichokuwa kikibisha hodi.Adera baada ya kumtandika kofi hilo alitoweka muda huo huo ,,,,Adam baada ya kuyashuhudia hayo alisimama kama ana spring miguuni ,akaupiga teke mlango nae akachomoka akiwa uchi na kuanza kutimua mbio kuelekea nje huku kile kinyesi kikiendelea kuvuja mithili ya punda anayejisaidia wakati akishushiwa mijeredi.
ITAENDELEA..................... 

Post a Comment

Previous Post Next Post