PENZI LISILO SAHAULIKA 11-12💋


ZANZIBAR
Alichekelea kimoyo moyo maana alijua tayari lengo lake litatimia na kisasi juu ya Adera kitatimia vizuri ."Lakini kwa nini tusiende wote tu maana hakuna litakalo haribika ". Aliongea Ben huku akiweka mkono wake wa kushoto shingoni mwa mke wake Adera."Aaaah! Ben ubaya haupo ila kwa Sasa itakuwa ni vigumu kidogo,niache niondoke na Adera shemeji yangu kwani hatutakawia kurudi hapa,ndani ya dakika thelasini tu tutakuwa tumesharudi ,cha msingi wewe endelea kupata juice tu". Aliongea Steve huku akichomoa noti ya elfu kumi na kumpa Ben."Hicho kidogo naomba ukipokee ili uendelee kunywa juice kwa uzuri zaidi". Aliongezea Steve huku akiachia tabasamu la uwongo ,tabasamu ambalo Ben hakuligundua ."Sasa hapa mtarudi mida gani maana naona kama jua limeshaanza kuzama ".Alizungumza Ben huku akimkazia macho mkewe."Tutarudi kwenye mishale ya saa kumi na mbili na nusu".Alijibu Steve haraka haraka ."Ben acha nikuage ili niambatane na shemu Steve nitarudi tena kama Shemu Steve alivyosema ". Aliongea Adera kisha Ben akakubali nao wakasimama kwa pamoja."Sogea mume wangu nikuage kwa kukukumbatia". Aliongea Adera nae akamkumbatia mumewe huyo kisha akamalizia kwa kumbusu ."Nendeni salama na mfike salama huko,mwenyezi Mungu na awatangulie".Aliwaaga Ben nao wakawa wanaondoka mbele yake huku akiwatumbulia macho ...walizipiga hatua kuelekea nje ,walipofika huko walisimama kidogo ."Shemu haujaja na gari yako tutumie gari yangu ili tuwahi kufika?". Aliuliza Adera."Hapana Shemu nilikuja kwa miguu maana niliona hakuna haja ya kuja na gari yangu ". Alizungumza Steve huku akiwageukia kiujanja ujanja na kuwakonyeza jicho la Siri vijana wake waliokuwa wamesimama nje ya Tax yao umbali wa mita kumi kutoka pale walipokuwa wamesimamia yeye na Adera ."Basi shemu haina shida mi naona tuondoke sasa".Waliisogelea gari kisha wakapanda hadi ndani,vijana wake na Steve nao wakaingia ndani ya ile Tax yao."Shemu unaonaje ukiniachia nidrive mimi?" Aliuliza Steve kwa mtego.Adera hakuweza kumkatalia maana aliamini huyo ni shemeji yake wa ukweli na wa kipekee na hakuwaza kabisa kama kungekuwa na ubaya wowote ule kutoka kwake.Basi Adera alikaa pembeni na Steve akashika usukani nao wakaanza kuondoka pale huku ile Tax ya wale vijana ikiwafuata kwa nyuma.Steve baada ya kuiondoa gari ndani ya maeneo yale ya hotel ,aliikwepa barabara ya kuelekea nyumbani kwake akaishika barabara nyingine tofauti kabisa,barabara hiyo ilikuwa ni ya kuelekea mjini Bagamoyo na pembeni yake ilikuwa imezungukwa na miti mirefu pamoja na vichaka vingi vingi."Shemu hii barabara mbona naona kama ni ya kuelekea Bagamoyo?" Aliuliza Adera kwa mshangao."Shemu hii barabara ni shortcut ya kuwahi mapema nyumbani kwangu na wala si ya kuelekea huko Bagamoyo,sema zimefanana tu ". Steve alimdanganya huku akizidi kupanga mikakati mingi moyoni mwake.Adera ilimbidi abaki kimya tu maana alijua huenda ni kweli ile barabara ni shortcut na inaelekea nyumbani kwa shemeji yake huyo.Steve aliacha kumtazama Adera akawa anazidi kukanyaga mafuta ya gari,aliongeza spidi maradufu kisha akakata kona ya haraka na kuiacha ile barabara ya lami akaingia ndani ya lile pori kwa kutumia kinjia kilichokuwa kimegubikwa na nyasi ndefu."Shemu hapana aisee,naomba turudi ,tunaenda wapi huku? Hapana Steve".Adera alianza kupaniki baada ya kuona shemeji yake huyo haeleweki.Sasa kabla Steve hajamjibu chochote aliitokomeza gari hadi ndani kabisa ya pori lile kwa spidi kisha akaisimamisha na kuanza kumtumbulia macho Adera."Shemu nadhani hapa ndo nyumbani kwangu". Aliongea Steve kwa kejeli muda huo huo ile Tax ya wale vijana ikija kwa kasi na kwenda kusimama mbele."Shemeji mbona sikuelewi? Tafadhari nirudishe kwa mume wangu Ben". Aliongea Adera huku mapigo ya moyo wake yakianza kwenda kwa kasi.Steve alianza kucheka sana na hapo hapo akabadirika na kuwa Steve yule mwenye roho mbaya ."Hahahahaha! Siku zote mbio za sakafuni huwa zinaishia ukingoni ,Adera ziko wapi sasa zile nyodo zako ulizokuwa ukinifanyia? Haha,niliamua kutumia akili ili nikukate ngebe.Mathalani nimekuleta hapa basi jua kabisa huwezi toka salama humu....Maana tunda lako kwa namna yoyote ile ni lazima nilile!!". Aliongea Steve kisha akaita "Waeswataaa!!".Muda huo huo wale vijana watano wakachomoka mbio kutoka kwenye ile Tax waliyokuwa wameisimamisha mbele,wakaja fasta kwenye gari ya Adera wakiwa na bastora zao."Steve kumbe wewe ni shetani kiasi hiki,umenileta hapa ili uniuwee??" . Aliongea Adera huku akianza kulia ."Haswaaaa! Mimi ni shetani wa ukweli na mapembe yake".Alisema Steve huku akiupiga teke mlango wa Kushoto wa gari nao ukafunguka.Baad
a ya kushuka chini tu aliwaamuru vijana wake wamtoe nje haraka kisha yeye aanze kufanya yake."Niachieniiiii!! Niachieniiiii!! " Adera alianza kupiga kelele lakini kelele hizo wala hazikuweza kufika popote pale maana ule msitu ulikuwa ukizimeza kelele zake hizo."Wananiuwaaaa!! Wananiuwaaaa!! .....Nisaidieniiiii!! Nisaidieniiiii!
!".Alizidi kupiga kelele Adera bila mafanikio ,vijana wale walimbeba juu juu wakawa wanatokomea nae kukifuata kichaka kimoja kilichokuwa kimezungukwa na nyasi ndefu,huku Steve akiwafuata kwa nyuma.
Walipofika kwenye kichaka kile walimuweka chini Adera kisha wakamlaza chali,vijana wanne walimshikilia vizuri na kijana mmoja akatoa kamba na vitambaa viwili vyeusi akaanza kuifunga haraka miguu ya Adera kwa kutumia zile kamba akamalizia na kuifunga mikono yake pia.Usoni alimfunga kitambaa kimoja cheusi na mdomoni pia kwa kutumia kile kitambaa kingine,na hapo ndipo walipomweza Adera maana hakuwa na ujanja tena wa kuendelea kupiga kelele zaidi ya kubaki tu akijitingisha tingisha mithili ya bata aliyekatwa shingo kwa kuchinjwa.Vijana walisimama pembeni wakawa wanamcheka Adera kwa dharau muda huo huo Steve akivua suruali yake .Baada ya kumaliza kuvua alimsogelea Adera aliyekuwa akitingishika akamchomolea sketi yake nyeusi pamoja na nguo ya ndani,nae akaanza kumbaka kwa nguvu huku akiziminya minya chuchu zake,aliporidhika alimwachia Adera akasimama pembeni na kutoa ofa kwa vijana wake."Oya kama kuna mwingine anataka kujisevia ruksa maana mbuzi kafia kwa muuza supu". Aliongea Steve bila huruma na wale vijana nao wakawa wanambaka Adera mithili ya mnyama tena kwa zamu mpaka wakaridhika,walipomaliza kumfanyia unyama huo walimvisha ile sketi yake kisha wakamfungulia zile kamba na vitambaa walivyokuwa wamemfunga ,Kwa muda huo Adera nguvu zilikuwa zimemuishia na alikuwa akitokwa na damu puani,huku sehemu yake ya Siri nayo ikivuja damu."Boss mi nadhani huyu tummalize tu maana tukimuacha hai atakuja kutusababishia matatizo makubwa baadae". Aliongea kijana mmoja aliyekuwa akiitengeneza vizuri suruali yake."Aisee umeongea ukweli mtupu,shoot hiyo mbwa haraka,au nendeni mkamtembezee kichapo ili afe kwa mateso". Aliongea Steve na vijana wawili wakachomoka na kwenda kuanza kumpiga Adera,walianza kumkanyaga tumboni kwa nguvu kisha wakamalizia kifuani,,,walipodhani amekufa walimbeba na kumpeleka ndani ya gari yake.Haraka haraka Steve aliingia ndani ya gari ile akaiwasha kisha akaitoa ndani ya lile pori na kuipaki pembezoni mwa barabara ile ya lami."Oya mshusheni chini kisha we Mr Mluto,no!! We Mr Db K andika namba hizi za yule boya umpigie". Aliongea Steve muda huo huo wakipanda ndani ya Tax yao ili waondoke.Baada ya Db K kuziandika zile namba ,Steve alitoa amri ya kuondoka fasta pale ili wasikutwe na watu ndani ya eneo lile.
************************
Ben akiwa hajui hili wala lile huku akiendelea kupata juice yake,mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita ,aliitizama kidogo akasita kuipokea .Simu iliita mpaka ikakata,dakika mbili tena ikaanza kuita akaona ni bora aipokee tu maana ilikuwa ni namba ngeni kwake.Sasa baada ya kuipokea alikutana na maneno haya."Ben wahi haraka kwenye barabara iendayo Bagamoyo mkeo yupo katika wakati mgumu sana".Kabla hajazungumza chochote simu ilikatwa na alipojaribu kupiga namba ile haikupatikana tena ,Ubaya sauti ile Ben hakuitambua na hakujua ni nani huyo ambaye alimpigia.Ben alichanganyikiwa akatoka mbio ndani ya ile hotel akawa anakimbia njia nzima bila kupumzika mpaka akafanikiwa kufika ndani ya lile eneo.Ben huku machozi yakimlenga lenga hakuamini kabisa kwa kile alichokuwa akikiona mbele yake.......Mpenzi wake na mke wake Adera alikuwa amelala mbele yake katikati ya barabara huku damu zikimtoka puani pamoja na mdomoni na povu furani hivi jeupe nalo lilikuwa likimtoka,Ben aliyaangaza macho yake kulia kushoto akaiona gari ya mrembo huyo ikiwa imepakiwa pembeni.Alitimua mbio kumsogelea Adera mithili ya mwendawazimu akawa amemfikia na kumbeba juu ili amkimbize hospitalini."Ben mpenzi wangu naomba kwa muda huu japo kidogo uniweke chini karibu na hii gari yangu nina machache sana ya kukuambia kabla sijamfuata baba". Aliongea Adera kwa taabu sana huku akiigeuza geuza shingo yake kuashiria ni kwa kijinsi gani alivyokuwa akipatwa na maumivu."Adera unasemaje Adera??". Aliuliza Ben huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio sana."Ben naomba unipe mkono wako wa kulia". Aliongea Adera na Ben muda huo huo akampa huo mkono nae akaupokea na kuuweka kifuani kwake.
"Ben nilitamani sana ndoa yetu idumu tuje tuzae watoto watakaotusaidia baadae lakini kwa Sasa imebaki kama ndoto tu isiyokuwa na mwanzo maalumu katikati ya Usiku mnene wa giza".Alisema Adera kwa sauti ya chini huku akijitahidi kuyafumbua macho yake yaliyokuwa yametapakaa machozi yenye mchanganyiko wa damu,Ben nae kwa muda huo machozi yalianza kumtoka bila kutarajia."Ben mpenzi wangu na mume wangu najua utaumia sana kumpoteza kipenzi cha moyo wako katika mazingira usiyoyatarajia ila kumbaka tu hii ni dunia na ina Kila kitu chenye uhai na kisichokuwa na uhai.......Ningali bado natamani niwe na wewe katika hii dunia lakini ndo hivyo tena muda wangu na siku zangu za kuishi zimefikia tamati,,tumetoka mbali sana katika safari ya mapenzi yetu ila ndo hivyo tena sina jinsi ya kukuaga kwamba ipo siku tutaonana tena.Siku zote sikujua kama kikulacho kinguoni mwako na adui yako mkubwa ni nduguyo wa karibu.Rafiki yako Steve ndiye aliyenifanyia ubaya wote huu.......Lakini nakuambia kamwe hautoonekana mjinga kama utamsamehe kwa yote aliyokutendea maana pamoja na yote haya,ipo siku atakuja kuyalipa ,mimi pia nimemsamehe kwa huu unyama alionifanyia ila ipo siku atakuja kuulipa.Ba....baaaa......baaaaa....baki salama mume wangu Bennnnn!!???".Adera hakuwa na kingine cha kuzungumza kwani alibaki kimya na hapo ndipo ile shingo yake ilipolala mazima.Ben alipaniki akajaribu kumuita Adera wake asiitike,akajaribu kumtikisa asitikisike,alipomshika kwenye kifua chake akakuta mapigo ya moyo yamekoma,Kumaanisha kwamba Adera tayari alikuwa amesha kata roho."Noooooo!!
......Nooo!! ....hapana ,Hapana Aderaaaaaa!!!..
...Aderaaaaaa ?????".

ITAENDELEA................................ 

SEHEMU YA 12.

Ben alilia sana akashindwa hata cha kufanya maana kipenzi chake Adera ndo hivyo tena alikuwa kashatangulia mbele za haki,,uchungu usiokuwa na mfano ulianza kuuzonga zonga moyo wake huku machozi mithili ya maji yakimtoka na kuishia kukilowanisha kifua chake.Nguvu nazo zilikuwa zimeshamwishia ila akajitutumua kwa kadri ya uwezo wake akaubeba juu mwili wa Adera mkewe ili ajue anaelekea wapi.Sasa baada ya kuubeba tu huku machozi yakiendelea kumtoka kabla hata hajanyanyuka vizuri mara akasikia milio ya risasi,,ile anayanyanyua tu macho yake sauti hii ikasikika."Upo chini ya ulinzi,simama hapo hapo".Mbele yake walionekana maaskari watano wakija huku mama Adera pamoja na Steve wakiwa ni miongoni wa walioambatana na maaskari hao.Ben baada ya kumuona Steve alichanganyikiw
a na hasira ikamuwaka akauweka chini mwili wa Adera na kisha kumkimbilia Steve ili akampige.....alichomoka mara Moja tu akaishia mikononi mwa wale maaskari."Niachieniiiii,, Niachieniiiii huyu ni shetani tena shetani wa kuzimuni,niachienii".Ben aliyaongea hayo huku akijitutumua kuwatoka wale maaskari asifanikiwe....Steve alisogea pembeni akawa anatabasamu tu wakati mwingine kumcheka Ben tena kwa dharau."Kijana yaani umeuwa harafu bado unajitia jeuri ya kuendelea kufanya fujo? Sasa wewe utafia jera". Aliongea Askari mmoja aliyekuwa ameshikilia simu ya kiaskari kwenye mkono wake wa kulia.Mama Adera nae baada ya kuuona mwili wa mwanae umelala aliukimbilia huku akilia akaufikia na kisha kuchuchumaa chini akawa anazidi kulia huku mkono wake wa kushoto akiupigiza juu ya ardhi."Adera .....Aderaaa...
.Aderaaaaa!! Mwanangu kumbe kuniaga kwako unaenda kupanga mipango ya kimaendeleo na mumeo,kumbe matokeo yake ndio haya?? Mwanangu.... Mwanangu,,amka basi Adera,,,Adera amkaaa!! Baba yako hayupo na wewe pia umeenda mwananguuu!! Adera amkaaa!!".Alilia sana mama Adera,Steve akajitoa ufahamu na kumsogelea mama huyo kisha na yeye akachuchumaa na kujifanya anamnyamazisha mama huyo kinafiki ili mradi tu Ben aonekane ndiye mwenye makosa maana hakukuwa na ushahidi mwingine,ushahidi wote alikuwa nao Adera ambaye ni marehemu sasa,,,,Ngoja tuone itakuaje,Sasa Steve akawa anamnyanyua mama Adera huku akimfuta machozi "Pole sana mama yangu,nadhani sasa ndo umeelewa kumbe hukupata mkwe wa ukweli bali ulipata mkwe mwenye tabia za nyoka tena aliye na sumu ya kutisha,pole sana ". Aliongea Steve akawa anazidi kumbembeleza mama Adera mpaka akatulia na kuyaamini maneno yote ya uwongo wa Steve kwamba Ben ndiye aliyemuua Adera."Niachieniiiii!! Steve.....Steveee hivi nilikukosea nini mimi,,,nilikukosea nini mimi?? Kwa nini unanifanyia unyama kama huu kwa niniii". Aliongea Ben lakini hakuna hata mmoja ambaye alimuelewa na kumuamini."Steve ndiye aliyemuua Adera,,,Steve ndiye aliyemuua". Aliongea Ben huku akilia kwa uchungu."Una uhakika gani,pumbavu simama hapo". Askari mmoja alimpiga Ben na kiwiko cha bunduki mgongoni mwake huku akiyasema maneno hayo."Vijana sijui bangi zimewachanganya yaani umekamatwa na ukiwa na ushahidi wote harafu bado unajitoa ufahamu eti Steve ndiye aliyehusika,,,Mkuu nadhani tusipoteze muda hapa,huyu kijana tuondoke nae tukamuweke mahabusu mara Moja na kesho yake ahukumiwe maana sidhani kama kuna ushahidi mwingine zaidi ya huu ". Aliongea Askari mwingine kisha Ben akapigwa mtama na kudondoka chini ,,Alipojitutumua ili asimame juu huku kizunguzungu kikimuandama alipigwa tena akandondoka chini na aliposimama tayari damu zilikuwa zimeshaanza kumtoka puani na mdomoni,,,Ben hakuwa na ujanja tena alinyamaza kimya yote hayo akamuachia Mungu tu,aliamini kama ridhiki yake ipo basi ipo tu na aliamini hata kama atahukumiwa kifungo cha maisha ipo siku Mungu atashuka mwenyewe kuja kumtetea.
Walimkamata kwa kumning'iniza kisha wakampiga pingu mikononi mwake na miguuni mwake baadae wakambeba juu juu na kumrusha ndani ya Defender yao mithili ya gunia la mzigo.Baada ya hapo walirudi hadi kwenye ule mwili wa Adera wakaupandisha ndani ya ile gari ya marehemu Adera mwenyewe,,wakampandisha na mamaye aliyekuwa ameishiwa nguvu,Steve nae akapanda ndani ya ile ile gari kisha wakajiandaa kuondoka.Maaskari wanne walibaki ndani ya ile Defender na askari mmoja akaambatana na kina mama Adera kisha safari ya kuondoka pale ikaanza.Mwili wa marehemu Adera ulisafirishwa moja kwa moja hadi hospitali ya taifa ya Mhimbili ukaenda kuhifadhiwa huko kwa ajili ya mazishi.Ben yeye alipelekwa moja kwa moja hadi mahabusu akaenda kutupwa huko huku asipewe hata dakika mbili za kujieleza zaidi ya kusibiria hukumu tu.Masaa yalisogea hatimaye Usiku ukawadia huku Ben akiwa ndani ya mahabusu,,,mpaka muda huo alikuwa hajatia chochote tumboni mwake na njaa ilikuwa ikimtesa sana.Mbu ambao kwa muda huo walionekana kama ndo marafiki zake nao walimgeuka na kuanza kumshambulia bila hata ya kumuonea huruma.Ben maskini wa Mungu alijikaza hivyo hivyo tu kusubiria mwisho wake,,,Macho yake kwa muda huo yalikuwa yameshavimba kwa machozi na mdomo wake ulikuwa umepauka vya kutosha."Baba,,,mama yangu mpo wapi wazazi wanguuu?? Kabla hamjafa mliniachia usia kwamba mimi ndiye mzaliwa wa kwanza mliyenizaa kwa taabu na uchungu mzito.....mkaniambia wadogo zangu pindi nyinyi mtakapotoweka duniani watanifanya mimi kuwa ndiye Baba na mama kwao,,,mkaniambia nisikate tamaa katika kujituma kufanya kazi japo sikuwa na elimu.Wazazi wangu kama mnaisikia sauti hii ya uchungu ya mtoto wenu tambueni kwa sasa walimwengu wameamua kunirejesha shimoni,,,Wazazi wangu mapenzi yamenifanya leo hii nionekane mimi ni mkosaji kwenye kosa lisilokuwa langu!! Kwa sasa sijui wadogo zangu wanaosoma wataishije maana Kaka yao hapa nilipo jera inaningoja na kifungo cha maisha kinanisubiri kwa kosa lisilokuwa langu". Alijiongelesha maneno hayo Ben huku akiwafukuza mbu waliokuwa wakimzunguka zunguka mbele ya uso wake."Mungu sijui hatima yangu leo hii ila kama wewe kweli upo najua utakuja kunitetea hata kama nitahukumiwa kifungo cha maisha". Aliongea Ben kisha akayafumba macho yake kuusaka usingizi.
**************
Kesho yake kulipopambazuka kabla Steve hajajiandaa kwenda kushuhudia hukumu ya Ben aliwatoa vijana wake wote ngomeni mwake akawa anawatangazia neema."Hahahahaha!! Ukiamua kupambana na mwenye pesa lazima uumie tu,mimi ndiye Steve billionea mtoto wa hili jiji.....Ben kwisha habari yake maana alikuwa akijiona kidume sana kwa kuwa na yule mrembo aliyekuwa akiutesa moyo wangu.Sasa nadhani muda huu ni wa sisi kula bata tu maana kazi tumeimaliza,,,vijana wangu leo nitaandaa sherehe kubwa sana ya kujipongeza maana tumefanya kazi kubwa ,unajua tusingemuua yule binti leo hii tungekuwa tunazungumza mengine,maana jera tungeenda sisi badala ya yule mbuzi anayejiita Ben". Aliongea Steve kwa lugha ya kejeli na dharau za hali ya juu huku akitembea tembea kwa maringo kuwazunguka vijana wake waliokuwa wamepanga mstari mmoja mrefu."Boss mimi kwa upande wangu nina duku duku moja tu". Aliongea kijana mmoja hivi aliyekuwa amejipanga mwishoni mwa mstari."Duku duku gani hilo ?" Aliuliza Steve."Inatosha sasa,sioni haja ya kuendelea kumtesa Ben ili hali kama Adera tayari ameshakufa,mi naona si busara kabisa ,kwa hapa haihitaji elimu ya chuo kikuu kumuachia huru Ben". Aliongea kijana huyo Steve akaishia kumcheka sana huku akimsogelea na kumshika begani."Nilidhani una duku duku la maana kumbe unaongea ujinga tu,wewe kwa akili yako ulidhani nani angestahili kuubeba ule mzigo wa lawama za mauaji? Unajua hapa nilipo mimi nina degree ya kitaa pia nina degree ya darasani najua kila kitu pamoja na ujanja wote,,,isitoshe nimefunzwa na wazazi pamoja na wazwaaji,sasa wewe shoga nadhani umechoka kuishi,ngoja nikushikishe adabu".Steve baada ya kuyaongea hayo aligeuka nyuma kidogo tu akachomoa bastora yake na kumshuti yule kijana muda huo huo akadondoka chini na kupoteza maisha hapo hapo.
ITAENDELEA.................. 

Post a Comment

Previous Post Next Post