PENZI LISILO SAHAULIKA 09---10

                    ZANZIBAR 

Mipango yao ilipomalizika.....kila mmoja aliondoka eneo lile kwenda kunako sehemu yake ya malazi maana hata Usiku ulikuwa umeenda sana japo kuwa ilikuwa ni mishale ya saa nne na dakika arobaini na tano.Wale waliokuwa wakihusika na masuala ya malindo kwa Usiku huo nao walielekea sehemu zao za kazi.Steve baada ya kufika chumbani kwake alikaa kwenye sofa moja kubwa lililokuwemo humo akawa anajishika shika kichwani na wakati mwingine kujikuna kuna kana kwamba kuna kitu kilikuwa kikimuwasha.Juu ya hilo sofa hakukaa sana alikaa kidogo tu kama dakika saba hivi baadae akasimama na kuanza kuelekea kitandani,,,alizipiga hatua za pole pole kukifuata kitanda chake kile lakini baada ya kubakiza hatua moja akifikie kitanda hicho alisimama na kuendelea kujikuna mpaka akakaa chini kabisa."No...Nooo!! Haiwezekani binti mrembo kama Adera nimkose wakati naona kabisa ndo chaguo langu...aisee hapa nitafanya kila linalowezekana ili nimpatee".Alijisemesha Steve kwa sauti ya juu kidogo muda huo huo akijipiga piga kifuani kwa hasira .Basi majira ya Usiku yakawa yanazidi kusogea hatimaye saa tano ikawadia....huo ndio uliokuwa muda maalumu wa kina Ben na Adera kuchati kama walivyoahidiana,,,kwa upande wa Ben baada ya muda huo kufika aliwasha data maana waliahidiana watachati kwa njia ya WhatsApp.Adera nae akiwa ndani ya chumba,aliwasha data akabaki anajing'ata ng'ata asijue hata pa kuanzia....alionekana akifanya hivyo kwa dakika takribani mbili baadae akajitutumua na kuamua kuanzisha charting."Mambo my?" Aliandika ujumbe huo Adera huku akijishika kifuani ,aliutazama mara mbili mbili baadae binti akafumba macho kwa hisia na kuutuma ujumbe huo huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio .Ujumbe huo ulimfikia Ben akawa anautazama huku akitetemeka mithili ya mtu aliyemwagiwa maji ya baridi.Kitu pekee ambacho kilimfanya autazame ujumbe huo mara tano tano ni lile neno la "MY" Moyo wake ukamtuma huyo binti tayari kashaanza kujileta mwenyewe kama samaki kwenye ndoano yenye chambo."Aaaah! Leo hapakuchi bila kumpata Adera,na leo ndio leo siogopi".Alijiongelesha Ben huku akicharaza ujumbe wa kumjibu Adera,,Ben aliandika ujumbe huu "Poa tu my love mzima wewe".Baada ya kuusoma moyo wake ulilipuka paaa!! Akatamani aufute kabla ya kuutuma ila akajikaza na kujisemea lolote na liwe,kama ambavyo alifanya Adera nae alifumba macho akautuma ujumbe huo moja kwa moja ukaenda kumfikia Adera.Adera alipoupata huo ujumbe mapigo ya moyo wake yaliongezeka kwenda Kasi kiasi kwamba ilifikia hatua kijasho kikawa kinamtoka maana hisia kali zilimuijia."Ben hivi mimi ni mrembo kweli?" Aliuandika huo ujumbe kwa mara hii akautuma moja kwa moja bila ya kuogopa,ulipomfikia Ben nae bila ajizi akaamua kuusoma na kumjibu."Ndio Adera wewe ni mrembo sana tena zaidi ya sana,Adera nikuambie kitu?" Aliandika Ben kisha akautuma ujumbe huo kwa Adera.Adera nae baada ya kuupata akajibu kwa maneno haya "Niambie my".Aliandika Adera.Ben baada ya kuupata akajibu kwa maneno haya"Adera usema ukweli nimetokea kukupenda natamani uwe wangu wa maisha,tuishi kama mume na mke na ikiwezekana tupendane kwa dhati hadi ulimwengu ushangae,tafadhari Adera naomba unikubalie maana nimechoka kuumia kwa ajili yako,japo mimi ni mtoto wa kimaskini naomba unielewe maana mapenzi hayachagua ".Aliandika ujumbe mrefu kidogo Ben na kabla hajautuma alifumba macho kwa hisia kisha akautuma ukamfikia Adera bila ajizi,,,Sasa Adera hapo alichanganyikiwa kwa furaha maana alijua lengo lake limeshafanikiwa amempata ampendae,,,haraka haraka alicharaza maneno haya kisha akayatuma akiambatanisha na picha yake nzuri aliyokuwa ameipiga full ikiyaonyesha maungo yake ya mwili pamoja na kwamba alikuwa amevaa nguo ."Ben hata Mimi Adera nakupenda sana tena nina weza sema kwa upendo nilio nao kwako ni zaidi ya vile unavyofikiria.Nahisi ndiye niliyekuwa wa kwanza kukupenda maana usema ukweli nilikuwa nikiumia sana hususani pale nilipokuwa nikikuona ukiongea na Wanawake kadha wa kadha pale kibandani,,,Ben kwa uwoga tu wa kike ndio maana nilikuwa nikisita kukutamkia wazi wazi kwamba nakupenda,ila ukweli ndio huo nakupenda zaidi ya mara elfu na mamia yake".Aliandika hivyo Adera kisha akautuma ujumbe huo kwa Ben.Sasa furaha baina ya wawili hao kwa Usiku huo japo walikuwa sehemu tofauti tofauti iliwafanya waanze kuuombea Usiku uende haraka ili wakutane angarau miili yao iweze kupashana joto,,,Adera kwa Usiku huo usingizi kwake uliyeyuka kabisa akawa anatamani atoroke Usiku huo huo kwenda nyumbani kwa Ben kuusindikiza Usiku huo akiwa amejilaza kifuani kwake.Ben nae kwa Usiku huo nae usingizi ulimgomea maana hata jogoo lake lilikuwa likichachamaa mara kwa mara na wakati mwingine kutoa ute ute mwingi kwa hamu aliyokuwa nayo,hii ilitokana na muonekano mzima wa Adera ulivyokuwa.Ile picha tu ambayo Adera aliituma kwa Ben kwa wale wapiga punyeto ingekuwa chakula tosha kabisa .

 Katika ile picha,Adera alikuwa amevaa kimini cheupe kilichokuwa kimemtaiti sana huku kikiyaachia wazi wazi mapaja yake yale meupe na yaliyonona.Katikati kililichora vizuri tunda la Adera lililokuwa limevimba kwa wastani.Juu alivaa kijiblauzi chekundu ambacho kilikiacha wazi wazi kitovu chake kilichokuwa kimezama ndani,,na kilikuwa kikiyaonyesha maziwa yake muonekano wa robo tatu ,mazima yaliyokuwa yakionekana kama embe dodo zilizonona vizuri.Na alipigwa picha hiyo akiwa amelala kitandani kwake tena chali,bila shaka aliyempiga picha hiyo alikuwa ni Agnes.Sasa jogoo la Ben likazidi kuchachamaa kila akiitazama picha ile ikabakia kidogo tu aipigie nyeto ila ikambidi ajikaze kiume ili asifanye hivyo kwa kuamini ule msemo usemao "Ndege ni wako ya nini umshikie manati".Akiwa amelala chali huku akijitahidi kuirudisha mashine yake katika hali ya kawaida aliandika ujumbe wa kumtakia Usiku mwema Adera nae akalala.Usiku wa manane Ben alianza kuota akiwa anafanya mapenzi na Adera tena juu ya kitanda kimoja cha kifahali na binti huyo alikuwa akipiga makelele ya utamu kupita maelezo,,,sasa ndoto ile ilimfanya Ben aanze kugugumia kana kwamba anaupata utamu halisi na bila kutarajia baada ya kukurupuka usingizini alikuja ameshaichafua nguo yake ya ndani.Alikaa juu ya kile kitanda akashusha pumzi kidogo kisha akalala huku akitamani pakuche haraka.Kwa upande wa Steve baada ya usingizi kumgomea aliona kubaki ndani ni kuzidi kujitesa zaidi.....alitoka humo akaenda hadi kwa vijana wake wale wa mawindoni akaenda kukaa huko huku akiwa amejishika tama."Boss,unaonekana una mawazo sana unaweza kutuambia ni kwa nini una mawazo kiasi hicho!!" Aliongea kijana mmoja."Unauliza kabisa hivyooo,hujui Adera ni kwa namna gani anavyoutesa moyo wangu ?" Aliuliza Steve huku machozi yakianza kumlenga lenga."Lakini boss mbona hilo tunalijua,harafu boss kama binti amezidisha nyodo mi naona temana nae tu,kwani kabeba moyo wako? Mpige chini tu !! Kwanza mabinti wapo wengi tu,usilazimishe kumpenda mtu asiyekupendaa".Alisema kijana yule na kumfanya Steve apandwe na hasira ya juu sana."Unasema nitemane nae siyo?" Aliuliza Steve huku akisimama juu."Ndio boss achana nae tu,utampendaje binti asiyekupenda? Temana nae tuu usije ukaugua ugonjwa wa moyo bure".Alijibu kijana huyo bila ya wasi wasi wowote ule."Sawa nitatemana nae ila kabla sijatemana nae lazima nikuteme wewe kwanza".Steve kwa hasira alichomoa bastora yake aliyokuwa ameichomeka ndani ya suruali kisha akampiga risasi ya kichwani kijana yule nae akaanguka na kufa pale pale.

****************

Hofu ilitanda kwa wale vijana wengine baada ya kushuhudia kwa macho yao mwenzao akipigwa risasi na boss wao Steve .....kimoyo moyo walijikuta wakianza kutetemeka sana."Sikieni nyie maboya,yeyote atakaye dhubutu kufungua bakuli lake kunipinga mimi kuhusiana na Adera nitamtoa ubongo kama nilivyomfanya huyu pimbi". Aliongea Steve kwa hasira."Huo mzoga uzoeni hapo kisha mkawatupie fisi ndani ya lile porii".Alisema Steve huku akianza kuondoka eneo hilo.Vijana wale walimsubiria boss wao mpaka alipoondoka ndipo wakaubeba ule mwili wa mwenzao wakaenda nao hadi kwenye lile pori wakaenda kuchimba kaburi Usiku huo huo wakauzika kimya kimya ule mwili bila ya Steve kujua chochote kile.

Masaa ya Usiku yalienda mbio sana hatimaye kukafanikiwa kupambazuka,,, Asubuhi na mapema Ben aliamka na kuanza kujiandaa kwenda kibandani kwake kuendelea na mihangaiko yake ya kila siku.Aliandaa mazingira ya nyumbani kwake vizuri na baada ya kuona kila kitu kimekaa Sawa aliondoka na kurejea huko haraka sana.Sasa baada tu ya kufika kibandani kwake huko,hakuyaamini macho yake baada ya kukuta kibanda hicho kikiwa kimeharibiwa vya kutosha.Ben aliiweka mikono yake kichwani akawa anasikitika kupita kawaida bila ya kujua ni nani aliyemfanyia hivyo,kila akijaribu kutafakari ni nani aliyekosana nae hakupata jibu kabisa,Maana pale mtaani alikuwa akiishi vizuri na watu."Ben pole.....pole Ben,,,Ben poleee".Hizo zilikuwa ni sauti za wapita njia baada ya kumuona Ben akiwa amechuchumaa mbele ya kibanda chake huku machozi yakimtoka.Akiwa hajui afanye nini mara upande wa nyuma yake akahisi kuna mtu amemgusa begani,ile anageuka tu kumbe ni Steve."Ben watu ni wabaya sana ndugu yangu,aisee wamekufanyia nini hiki ,pole sana acha kulia".Alisema Steve."Ben nadhani huu muda nitakusaidia kukisimamisha tena kibanda chako ila uniahidi jambo moja,sitaishia hapo tu bali nitakufanya uwe tajiri wa kuogopwa hapa mjini".

ITAENDELEA.........................................? 
.

                  SEHEMU YA 10.

             
"Sitaishia hapo tu Ben bali pia nitafanya kila linalowezekana ili wewe uwe mkubwa hapa mjini,nitakufanya uwe na pesa na ikiwezekana uwe bilionea kama nilivyo mimi kwani hakuna linaloshindikana".Alisema Steve huku akiunda maneno mengine matamu matamu ya kumhadaa Ben ili aingie ndani ya mtego wake."Steve wewe si tu rafiki yangu bali kwa sasa umekuwa kama ndugu yangu tena wa damu....sioni jambo lolote ambalo litakuwa kikwazo kwangu kuweza kukusaidia pale panapowezekana hata kama si kwa njia ya pesa,,unaweza kuniambia ni kitu gani hicho ambacho unataka mimi nikusaidie?" Aliuliza Ben huku akimtazama Steve aliyekuwa ameushikilia mti mmoja kwa mkono wake wa kulia.Steve alikaa kimya kidogo akawa anawaza huku akijishika shika kwenye pua yake na wakati mwingine kujikuna kuna kichwani,Alipotulia alimkazia macho Ben kisha akamwambia "Adera Ben,Adera". Aliongea Steve huku akijiinamia chini kana kwamba ameingiliwa na huzuni furani."Adera amefanyaje tena ? " Aliuliza Ben huku mapigo ya moyo wake yakianza kwenda mbio kidogo maana alijua labda kuna kitu kibaya kimempata."Adera nampenda sana naomba umfikishie hii taarifa kwani naumia sana kwa ajili yake,nadhani wewe atakuelewa maana Mimi nimejaribu kila liwezekanalo lakini nimeshindwa". Aliongea Steve huku akisimama wima ."Ati nini? Aaa...aaa!!...Lakini Steve kwa upande wangu hilo halitawezekana maana tayari Adera nimeshaanza nae mahusiano na ananipenda na mimi nampenda,kwa hiyo sidhani kama hilo litawezekana kwa kweli mimi nakushauri tu utafute binti mwingine rafiki yangu maana mabinti katika dunia hii wapo wengi sana,jikaze rafiki yangu japo inauma sana". Aliongea Ben na kumfanya Steve aanze kutokwa na machozi."Ben nimekuelewa rafiki yangu najua hiyo haikuwa ridhiki yangu ,kesho au kesho kutwa nitaja ipata tu iliyo ridhiki yangu,,,haya Ben ngoja nikuletee mafundi wakutengenezee kibanda chako". Aliongea Steve kisha akaondoka ndani ya lile eneo akiwa amejawa na masikitiko makubwa yasiyokuwa na mfano,,,Baada ya kufika kwake aliwapigia simu baadhi ya vijana wenye uweredi wa kutengeneza kibanda akawatuma waende hadi kwa Ben wakamtengenezee kibanda chake,,,,Vijana hao walimuelewa boss wao nao wakaenda na kuifanya kazi ile kwa umaridadi sana...na kibanda cha Ben kikawa kimekamirika siku hiyo hiyo.Kwa upande wa Adera baada ya mishale ya saa kumi kuwadia pale nyumbani kwao aliwaaga na kuwaambia hatorudi siku hiyo kutokana na kazi ngumu za kiofisi atakazokuwa nazo......aliwadanganya kuwa atasafiri nje ya Dar kikazi na hatorudi kwa siku hiyo.Kutokana na maneno yake hayo yaliyokuwa yakifanana na ukweli hakuna hata mmoja ambaye alimpinga kwani hata mama yake alimkubalia na kumsihi akawe makini tu huko aendako.Sasa baada ya kuondoka kwao huku akiwa ameiacha gari yake alielekea moja kwa moja hadi kibandani kwa Ben."Adera huyoooo!!" Ilikuwa ni sauti ya Ben ikimlaki binti huyo mrembo baada tu ya kufika huko,,,Ben alimkaribisha kwa kumkumbatia nao wakafurahi kwa pamoja kisha wakakaa na kuanza kupiga story.Walifanya hivyo hadi majira ya jioni yakawadia.Sasa kama kwenye saa kumi na moja na nusu hivi,alionekana Steve akija mbele yao huku kwa muda huo akiwa anaonyesha uso wenye tabasamu kuashiria kwamba hakuwa na kinyongo cha namna yoyote ile,alifika pale nae akakaa pembeni na kuungana na wependanao hao katika kupiga story."Steve umefuata nini hapa?" Aliuliza Adera baada ya kumuona Steve akikaa pale."My love Adera huyu Steve ni rafiki yangu wala hapa hakuja kwa ubaya wowote naomba usimchukie ,kama kuna ugomvi itakuwa ni vizuri sana kama mtasameheana".Alidakia Ben."Adera ni kweli kwa sasa unanichukia sana tena zaidi ya sana ila napenda tu nikuambie yafuatayo.....Kwanza tuyasahau yote yaliyopita na tugange yajayo,,kwa sasa mimi wala sina kinyongo na wewe Adera maana nimetambua kukulazimisha uwe mpenzi wangu wakati hunipendi ni kosa tena lisilostahili kusamehewa......Naomba kwa yote niliyokutendea unisamehe na tuanze upya kama mashemeji maana wewe ni kipenzi cha rafiki yangu Ben na Ben huyu unayemuona tumetoka nae mbali sana,Adera kama hutonisamehe unadhani siku nikifa utamsamehe nani,maana kovu la wewe kutonisamehe mimi litabaki pale pale ndani ya moyo wako ,Nisamehe Adera tuishi kwa amani ". Aliongea Steve na kumfanya Adera aanze kudondokwa na machozi,alimtazama Steve huku akigugumia kwa kwikwi baadae akasimama na kisha kumnyanyua Steve nao wakakumbatiana , kitendo hicho kilimfanya Ben aanze kutabasamu kwa kudhani sasa kila kitu kitaenda vizuri na wataishi kwa amani kumbe alikuwa akijidanganya tu.Si kwamba Steve huo msamaha aliouomba ulitoka moyoni mwake bali aliekti tu ili lengo lake litimie ."Steve mi nimekusamehe na ninadhani kwa sasa tutaishi kwa amani tena". Aliongea Adera kisha watatu hao wakasimama na kukumbatiana kwa pamoja.Baada ya kukaa waliendelea na story kama kawaida."Adera yaani kwa hapo umempata mume halisi wa maisha yako maana Ben ni kijana makini sana". Aliongea Steve."Aaaah! Shemu acha basi jamaniii" Aliongea Adera huku akimuegemea Ben."Unadhani nakudanganya shemu,Ben ni mwanaume wa kipekee sana na ipo siku utayaamini maneno yangu,,hapo umepata mumee". Aliongea Steve kisha akasimama na kuanza kuondoka pale akawaacha wawili hao waendelee na story zao."Jamani shemu ndo unaenda au?" Aliuliza Adera baada ya kumuona Steve akiondoka pale."Shemu kuna kazi kidogo naenda kuifanya lakini msijari nitakuja ten siku nyingine". Aliongea Steve."Haya shemeji haina shida".Baada ya Adera kuongea hayo ,Steve aliondoka moja kwa moja na kuelekea kwake.Huku nyuma Adera na Ben story zilinoga mpaka Adera akawa anamkumbatia Ben na wakati mwingine kumlalia mapajani huku akideka kama mtoto mdogo,Ben nae humo humo kibandani alikuwa akimchezea chezea mrembo huyo kitendo ambacho kilimfanya anogewe na kuanza kulainika kabisa."Benn!! Tuondokee my twende nyumbani maana umenifanya niwe na hamu ya mhogoo!!" Aliongea Adera na kuzidi kumtamanisha zaidi Ben.

 Ben alifungasha kila kitu kisha wakaondoka moja kwa moja hadi nyumbani kwa Ben.....walifika huko wakakaa kwenye kitanda na kisha kuanza kuchezeana chezeana na hazikupita hata dakika tano wote wakajikuta wakiwa watupu huku Adera akiwa chini ya kitanda na Ben akiwa juu yake wakifanya kile kinachofanywa na kila kiumbe wa kike na kiume.Walipomaliza kuzipata raha hizo zisizoelezeka walipongezana kisha wakaenda kuoga kwa pamoja na baada ya kuoga walirudi tena kitandani kuendelea na raha zao.Basi ndivyo ilivyokuwa.....siku ziliendelea kukatika moja baada ya nyingine huku mapenzi baina ya wawili hao yakizidi kuchanua kila uchao,kiukweli walipendana sana,,ilifikia hatua hata wanamtaa wakawa wanawaonea wivu kwa upendo ule waliokuwa nao.Hawakuweza kusikiliza maneno ya watu zaidi ya wao wenyewe huku wakipanga mikakati mingi mizuri ya maisha yao ya baadae hasa pale watakapooana na kuanzisha maisha yao."Unajua mpenzi wangu Adera tangu nikupeleke nyumbani kwetu kukutambulisha kwa wazazi wangu hadi leo hii nimekuwa na furaha sana moyoni mwangu ,furaha ambayo hata haielezeki".Maneno hayo aliyaongea Ben wakati wawili hao wakiwa pembezoni mwa ufukwe mmoja hivi wakipungwa upepo maana kwa muda huo hapakuwa na kitu chochote kile cha kuwabuguzi."Hata mimi,mwanzo sikudhani kama mama angeweza kukubali kuolewa na wewe kutokana na ile biashara uliyokuwa ukiifanya ila kwa Sasa nina furaha sana maana tangu nami nikutambulishe kwa mama yangu nimekuwa na furaha sana moyoni mwangu,na nakupenda sana Ben sitaki nikupoteze hata siku moja". Aliongea Adera."Natamani mapenzi yetu yadumu Adera".

*************************

BAADA YA MIAKA MIWILI .

Ben na Adera walioana na hapo sasa wakayaanza maisha yao kama mume na mke,,walifanikiwa kujenga nyumba yao nzuri na ya kifahali maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam na furaha baina yao ikawa inazidi kuongezeka,,,pia walifanikiwa kujitengenezea kampuni lao binafsi ambalo waliliita kwa jina la "BENADERA COMPANY LIMITED" Na wakawa wanazidi kupanga mipango mingine mingi ya maisha yao ya baadae.Ilikuwa ni siku ya juma mosi saa tisa za alasiri,Adera na Ben walitoana out kwa ajili ya kuianza wikiend yao vizuri......Baada ya kufika kwenye hotel moja waliyokuwa wameipanga walienda na kukaa nyuma kabisa mwa ile hotel."Mume wangu kwa sasa naona tuanze mikakati ya kupata watoto maana Mungu ametusaidia mpaka sasa". Aliongea Adera huku mkono wake wa kulia akiwa amemkumbatia mumewe Ben."Hata mimi nilitaka niseme hivyo sema umeniwahi tu". Aliongea Ben.Sasa wakati wakiwa wanaendelea na maongezi yao,Huku nyuma Steve akiwa na vijana wake watano walishuka ndani ya gari moja aina ya Tax kisha Steve akawageukia na kuwaambia.

"Sikieni,,huu ndo muda maalumu tuliokuwa tukiusubiria kwa hamu.....Sasa cha kufanya ni hiki!! Nyie mtabaki hapa hapa Mimi nitawafuata wale maboya wanaojiita wana ndoa,nitaenda kumshawishi mkewe na Ben kwa namna yoyote ile ili akubali kuondoka na mimi na baada ya hapo tunamaliza mchezo fasta,tumeelewana?"......"Ndio mkuu "......"Huu ndo muda wa Ben kuzilipa gharama zangu zote nilizozitoa tangu mwanzo hadi siku ile wanafunga ndoa". Aliongea Steve na baada ya hapo akajitengeneza vizuri na kisha akaanza kuzipiga hatua kuwafuata kina Ben walipokuwa wamekaa."Oooh!! Shemu nakuona upo na mumeo kipenzi!!". Aliongea Steve huku akisogeza kiti ili akae."Shemu karibuu". Aliongea Adera."Asante shemu ila sijaja kukaa sana hapa,nimekuja kwa jambo dogo tu". Aliongea Steve."Steve jambo gani tena hilo?" Aliuliza Ben."Mke wangu nimemuacha nyumbani ana matatizo makubwa sana,amesema kama shemu hana kazi muda huu niondoke nae akamsaidia mambo ya sirini". Aliongea Steve."Shemu pole sana,sasa ngoja nimuage mume wangu Ben ili tuondoke harakaa". Aliongea Adera na kumfanya Steve aanze kuchekelea kimoyo moyo.

ITAENDELEA.......................................... 

Post a Comment

Previous Post Next Post