PENZI LISILO SAHAULIKA 07---08

Kikohozi hicho wala hakikuweza kuwashtua Ben na Adera kutokana na story kufikia patamu bali kiliishia kujipenyeza kidogo tu masikioni mwao,Upande wa nyuma kumbe Mr Steve alikuwa akiwachungulia kimya kimya na ndiye aliyekohoa kama ishara ya kuwajulisha kwamba kuna mtu nyuma ya kibanda japokuwa wao walikipotezea.Sasa wakawa wanaendelea na story bila kujua chochote kile kilichokuwa kikiendelea...baada ya Steve kufanya mizengwe kadha wa kadha kule nyuma uvumilivu ulimshinda akaamua ajitokeze mzima mzima."Ahahahaa!! Ben naona upo na mrembo pembeni yako!" Alisema Steve kwa unafiki huku moyo wake ukichemka kwa hasira maana mapigo ya moyo huo yalikuwa yakienda mbio sana."Ndo hivyo,huyu ndo shemu wako aisee" Alisema Ben kwa utani hisia zikamshinda Adera mpaka akajikuta akimkumbatia Ben bila kutarajia....yaani ikawa kama Ben alichelewa vile kumtamkia anampenda ikiwa yeye tayari kashampenda zamani .Sasa Adera akiwa amemkumbatia Ben ,ile chuki ya Steve ikafikia pabaya akaona ni bora aondoke tu pale asije akafanya mambo kwa pupa akasababisha hasara isiyotarajiwa."Basi poa Adera,ah! Basi poa Ben ngoja mi niwaache kwanza".Aliwaaga akaondoka kichwa chini hadi nyumbani kwake."Ben kumbe Steve ni rafiki yako ?" Aliuliza Adera huku akimshika begani Ben."Ndio Steve ni rafiki yangu na urafiki wetu umetokea mbali sana maana kwa sasa tunaishi kama ndugu kabisa,tunaheshimiana na tunasaidizana kwa jambo lolote lile". Aliongea Ben."Waooo!!" Aliongea Adera huku akimkazia macho Ben ,macho yaliyokuwa yamebeba hisia kali.....binti huyo aliona afanye hivyo ili kumfikishia ujumbe Ben kwamba anampenda na anatamani awe wake maishani."Ben nikuulize kitu?" Aliongea Adera kwa sauti ya upole sana na iliyopambwa kwa unyororo wa hali ya juu."Kitu gani hicho Adera usiogope we niambie tu kwani nitakisikiliza".Alisema Ben ."Ben hivi una girlfriend?" Aliuliza Adera kwa kigugumizi kidogo."Hapana sina girlfriend Adera,kwa nini umeuliza hivyo?" Ben nae akaamua kumuuliza."Nimeuliza tu jamani kwani kuna ubaya gani". Aliongea Adera."Ben ukimpata binti mrembo atakayekupenda kwa dhati utajisikiaje". Aliongea Adera huku akiendelea kumlegezea macho Ben."Nitajisikia vizuri sana kwani natamani iwe hivyo cha msingi tu asiniumize". Aliongea."Sawa Ben".Baada ya kuongea hivyo,Adera alisimama kisha akamnyanyua na Ben wote wakawa wamesimama kwa pamoja.Adera akiwa amemshika mkono walitoka nje ya kibanda,binti huyo akawa anampiga picha Ben kwa Siri kisha kuzitunza bila ya yeye kujua."Adera naona muda unaenda nataka niwahi kwenda kupika haraka haraka". Aliongea Ben."Si tulikubaliana kwamba mimi nitakupikia hicho chakula? Ben acha mimi nikupikie chakula we baki tu hapa hapa maana Mimi nikiivisha tu nitakuletea ule Sawa Ben?" ....."Daah! Basi Sawa Adera mi nimekuelewa".Baada ya maongezi hayo kumalizika,Adera aliondoka pale akiwa na furaha ya ajabu sana akaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwao,alifika huko akamkuta house girl wao akijiandaa kuanza kufanya maakuli ya mchana."Dada Agnes naomba uniachie jiko kama masaa mawili hivi niandae chakula mimi mwenyewe". Aliongea Adera."Haaa! Unamaanisha leo hii chakula cha mchana utapika mwenyewe siyo?" House girl aliuliza."Yeah! Leo nimejisikia tu kupika".Walielewana vizuri na hapo hapo Adera akakaa jikoni kuandaa chakula cha mchana,kwa bahati nzuri mama yake kwa muda huo alikuwa kazini hivyo hilo wala lisingeweza kumta shida Adera.Alianza kwa kuandaa mboga nzuri sana na tamu akamaliza baadae akapika pilau ya kipekee mambo yote yakawa poa.Baada ya kumaliza kukiandaa chakula hicho,alichukua hotpot mbili.....moja kubwa kiasi na nyingine ndogo kiasi akaziwekea chakula haraka akamaliza.Kimya kimya alitwaa kikapu cha maana akatoka nacho hadi chumbani kwake baadae akakiweka humo kwa muda akatoka tena na kwenda kumjulisha Agnes kwamba chakula tayari anaweza kwenda kumwambia Jimmy wale kwani yeye atakuja kula baadae.Basi Agnes alimsikiliza vizuri mno boss wake huyo nae akafanya kama alivyoambiwa.Adera alipomaliza kumpa taarifa hiyo Agnes alirudi chumbani kwake akakichukua kile kikapu akatoka nacho nje haraka hadi kwenye gari yake,,,alipanda humo akaiwasha hivyo gari kisha akaondoka kwenda kibandani kwa Ben.

Akiwa anaelekea huko,mara simu yake ikapokea ujumbe .....Alipoufungua akakutana na maneno haya ."Adera kumbe mimi ulikuwa ukinichora tu ,ni mara ngapi nilikutamkia kwamba nakupenda na hukunielewa!! Yaani pamoja na kuwa na pesa na uhendsome wangu umeniona mi boya hadi ukaamua kumtunuku Ben penzi,kijana muuza mchele?? Ila poa tu".Aliusoma vizuri ujumbe huo ila akashindwa kuelewa ni nani huyo maana namba ile ilikuwa ni ngeni kwake .Ilimbidi apige simu ili kujua ni nani huyo ."Haloo,nimeona umenitumia ujumbe nani wewe?"......"Aaaah! Mrembo yaani kwa mara hii tayari umeshafuta hadi namba yangu?"....."Hayo mimi hayanihusu cha msingi nataka uniambie wewe ni nani?"....."Mimi ni Steve"....."Steve? Hivi we kijana unataka nikuambieje ili ulielewe ,nilishakutamkia wazi wazi kwamba sikutaki hivi mbona hunielewi?"......"Usiseme hivyo Adera mi nakupenda wewe na natamani uwe mke wangu"....."Funga domo lako mi sikupendi na sikutaki full stop".Adera alikata simu hapo hapo kisha akaendelea kukanyaga mafuta ya gari yake kuwahi kibandani kwa Ben.Steve alichanganyikiwa sana baada ya Adera kumkatia simu kiasi kwamba hasira ilimwaka mpaka akaitupa juu ya jiwe iPhone yake na kuifanya ipasuke."Adera,Adera,hivi unataka nikufanyie nini ili ujue kwamba nakupenda?? Ina maana Ben ndiye anayekutia kiburi siyo?? Ngoja nitajua cha kufanya maana Mimi katika maisha yangu sijawahi kukubali kushindwa kizembe".Alijiongelesha Steve huku akizunguka zunguka,,Haraka aliingia ndani na kwenda chumbani kwake kwenda kulala ili angarau akapunguze mawazo na aweze kujipanga vizuri ili ajue atafanya nini.

*********************

"Ben hiki ndicho chakula ambacho nilikuahidi kwamba nitakupikia naomba ukipokee". Yalikuwa ni maneno ya Adera baada ya kufika huko kibandani na kumkuta Ben akiendelea na biashara yake hiyo."Asante sana Adera" alisema Ben huku akikipokea chakula hicho kwa mikono miwili.Baada ya Ben kukipokea,Adera alizipiga hatua hadi kwenye gari yake na punde si punde akarudi na juice ya embe ambayo nayo aliiandaa akaja kumpatia Ben.Ben alianza kula muda huo Adera akimtazama kwa macho ya shauku huku akitamani kumtamkia anampenda japo hilo lilimpa wakati mgumu sana kutokana na kwamba alikuwa akiogopa kumtamkia hivyo.Yeye alikuwa amekaa tu huku akimkodolea macho Ben asijue hata cha kufanya."Adera mbona wewe huli?" Aliuliza Ben baada ya kumuona Adera akiwa amekaa tu."Usijali Ben nataka ule wewe ushibe maana Mimi nimeshiba". Aliongea Adera."Haya bwana ngoja mi niendelee kula".Ben alikula chakula hicho mpaka akakimaliza na kisha kuinywa ile juice."Asante Adera,nimeinjoy maana chakula kilikuwa ni kitamu sana ".Alishukuru."Asante pia kwa kukubali kukila chakula changu,,Ben nikuambie kitu?" Aliuliza Adera."Niambie tu". Alijibu Ben."Hivi macho yako yanaponitazama mimi yananionaje?" Aliuliza Adera."Yaani macho yangu yakutazamapo yanakuona wewe ni binti mpole sana na umejaliwa kuwa na uzuri usiokuwa na mfano na kwako wewe Mungu aliumba". Aliongea Ben na kuufanya moyo wa Adera ugubikwe na furaha kubwa isiyokuwa na mfano."Asante Ben". Aliongea Adera."Ila Adera mbona naona kama kuna kitu unatamani uniambie?" Aliuliza Ben."Mmmh! Niko poa tu Ben ila kama hutojali natamani leo Usiku tuchati".

ITAENDELEA....... 

SEHEMU YA 8.

ZANZIBAR
"Sawa Adera mimi nimekuelewa vizuri sana,cha msingi nataka nijue ni muda gani tutakao utumia wakati tunachati?" Aliuliza Ben huku akinyanyuka pale alipokuwa ameketi."Tuanze kwenye mida ya saa tano za Usiku maana kwa muda huo Kila kitu kitakuwa kimetulia sana na tutakuwa free sana". Aliongea Adera huku akivichukua vile vyombo vya chakula."Haina shida,kwa muda huo tutaanza kuchati ".Maongezi yao yalimalizika kwa mtindo huo baadae Adera akasimama akiwa na vile vyombo akawa anazipiga hatua kuiendea gari yake,,,tayari kwa muda huo ilikuwa imeshatimia mishale ya saa saba na nusu majira ya mchana.Adera baada ya kupanda ndani ya gari yake aliondoka na kurejea tena nyumbani kwao huku Ben nae akiendelea na shughuli zake za pale kibandani.Sasa baada ya binti huyo wa kizaramo kuondoka,muda mfupi baadae kama dakika tano tu hivi ,Steve alifika kibandani kwa Ben akiwa na vijana wake wawili aliokuwa akiwaita mabodigadi wake.Ben kwa vile alimfahamu Steve kuwa ni rafiki yake wa dhati wala hakuwa na wasiwasi nae kabisa....aliwakaribisha kwa busara sana nao wakaketi kwenye lile benchi alilokuwa amewaandalia nae pia akaketi pembeni yao."Ben vipi harakati zinaendaje aisee maana siku hizi kijana angu umekuwa kimya sana au Mzee wa Hali mpya,Kasi mpya na nguvu mpya amekumotiveti nini?" Aliuliza Steve huku akimkonyesha jicho la Siri kijana wake mmoja aliyekuwa amekaa kunako upande wa kulia wa huyo Steve mwenyewe ."Ndo hivyo rafiki yangu kama unavyojua ujio wa raisi wetu huyu Kikwete umekuwa chachu sana kwetu sisi vijana hasa katika suala zima la kimaendeleo ikiwemo kupambana kuutokomeza umaskini". Aliongea Ben."Kwa hapo sasa nimekupata vizuri ila jaribu na wewe angarau siku moja moja uwe unanitembelea maana ni kitambo sana hujaja kunitembelea kwangu tangia uanze maisha haya mapya uliyonayo kwa sasa ". Aliongea Steve huku akimkazia macho Ben ."Upo sawa kabisa rafiki yangu Steve ila sema tu majukumu ndiyo yanayonifanya niwe hivi ,ila nitapanga siku nije nikutembelee hususani kwenye krismasi maana nitakuwa free sana....harafu Steve nasikia sasa hivi umeshakuwa boss vipi ni kweli ndugu yangu?". Aliuliza Ben."Aaaah!! Hilo siyo la kuuliza Ben,na ndio maana nikaanza kwa kukusihi utenge muda uje nyumbani kwangu uyaone mazuri niliyokuandalia,waswahili wanasema kizuri kula na mwenzio usisuburi kibaya ndo umshirikishe.Harafu sikia Ben mi naona kwenye krismasi ni mbali sana tufanye juma mosi ya wiki hii uje kwangu tupige story na isitoshe kuna zawadi ya maana sana nimekuandalia zaidi ya ile ambayo nilikupatia,leo si ni alhamisi,,njoo juma mosi ndugu yangu itakuwa poa sana". Aliongea Steve mpaka akawa amefanikiwa kumshawishi Ben ambaye alimkubalia."Nimekuelewa na nitakuja wala usihofu Steve".Alisema Ben na kumfanya Steve awageukie vijana wake wawili huku akitabasamu,alimpa tano Ben nae akampa baadae Steve akasimama na vijana wake kisha wakamuaga Ben nao wakaondoka.Kwa sababu walikuwa na gari yao walipanda na kuelekea vichakani kwenda kupanga mambo yao ya siri zaidi kuhusiana na Ben.
Masaa yalizidi kuyoyoma hatimaye jioni nayo ikawa imewadia.....Jioni ile Adera alifanya kazi zake zote haraka haraka kisha akazimaliza akaingia chumbani kwake kimya kimya kama hayupo vile.Akiwa humo chumbani alilifungua faili lake la picha kisha akaanza kuzitazama zile picha ambazo alikuwa amempiga Ben bila ya yeye kujua huku akitabasamu.Aliizumu picha moja ya Ben aliyokuwa amempiga vizuri kisha akaichumu na muda huo huo akajisemea "Laiti kama kijana huyu nimpendaye nikifanikiwa kumpata katika maisha yangu haki ya nani simuachi maana sijawahi kuona kijana kama huyu,kwanza ni handsome pili ni mcheshi na anajiheshimu sana,tupilia mbali utajiri maana hata kama asingekuwa na senti hata moja bado angekuwa wangu....na katika yeye nitamuita baba watoto wangu nae ataniita mama watoto wake .Ben kijana nikupendae siwezi kukubali nikupoteze hata kama watu watanishangaa eti kwa nini niwe na wewe wakati mimi ni binti wa kitajiri na wewe ni muuza mchele,,,kamwe siwezi kukupoteza Ben wangu maana wewe ndiwe mwanaume harisi wa maisha yangu na moyo wangu umekuchagua wewe ".Alijisemesha Adera mpaka machozi yakawa yana mlenga lenga,Sasa ile picha alianza kuiediti vizuri kisha akaipamba na emoji za upendo kwa kuizungushia baadae akaiweka kwenye screen yake ya simu huku akiiandikia maneno ya "I LOVE YOU MY BEN".Kwa upande wa Ben baada ya kufika ghetoni kwake jioni ile alienda kujitupa kitandani moja kwa moja kisha akalala chali huku miguu yake akiwa ameiweka ukutani.....ilionekana na yeye mawazo yalikuwa yameshaanza kumuandama kichwani."Hivi huyu binti mbona ananitega hivi? Duuh sijui Usiku wa leo kupitia charting sijui nimfungukie tu maana nahisi kama nimeshaanza kumpenda japo kuwa sijui pa kuanzia....niki
mwambia nampenda sijui atanitukana?? Aaah!! Potelea mbali bwana mwanajeshi haogopi kufa acha nimfungukie tu hata kama atanikataa poa tu".Alijisemesha Ben,,,sasa wakati akijiuliza amuanze vipi Adera kumwambia anampenda upande wa Adera nae mambo yalikuwa hayo hayo ."Daah! Ben leo lazima nimwambie tu ukweli hata kama atanitukana sawa cha msingi lazima hisia zangu nizitendee haki,japo kwa mila zetu za kiafrika kumtongoza mvulana haikubaliki ,acha mimi nionekane tu mjinga maana siwezi kukubali kuutesa moyo wangu namna hii".Alijiongelesha Adera huku nae akiwa amejilaza kitandani.
*************
Saa nne za Usiku ilipofika,Steve aliwachagua vijana wawili wakakamavu sana kisha akawatuma hadi kibandani kwa Ben Usiku huo huo wakakiharibu kile kibanda baadae warudi tena pale ngomeni.Vijana wale baada ya kupewa maelezo hayo na boss wao waliondoka Usiku huo huo wakaenda hadi kibandani kwa Ben wakakivuruga kibanda chote kisha wakarudi na kumkuta boss wao akiwa na wale vijana wengine."Boss tayari kazi tumeshaimaliza vipi kuna jingine limebakia tukalifanye fasta?" Aliuliza kijana mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Db K."Kwa sasa hakuna jingine maana muda bado".Alisema Steve."Boss huyu fala anayekunyima furaha kwa nini usitutume tu tuende tukammalize mara Moja ili huyo demu awe wako milele?" Aliuliza Mr Mluto."Hapana sitaki tumuue kwa risasi au mapanga hapa tutamuua kwa kutumia akili". Aliongea Steve ."Sasa boss tutamuua kwa kutumia akili kivipi?" Aliuliza Db K."Si juma mosi amekubali kuja ,siku hiyo ndo itakuwa mwisho wa maisha yake......sikilizeni siku hiyo andaeni sumu kali sana ,hakikisheni kwa namna yoyote ile anainywa hiyo sumu iwe kwenye kinywaji kama juice au kupitia chakula .Mnatakiwa pia muwe na lugha ya ushawishi".Alizungumza Steve.
"Sawa boss ila endapo njia hiyo itashindikana basi tutakuwa na njia moja tu ya kumpasua ubongo,maana kivyovyote vile siku ya juma mosi lazima Ben afe". Aliongea kijana mwingine aliyekuwa ameshikilia bastora mkononi mwake ."Yap hapo umeongea kitu kijana wangu,Kwa kweli Ben si wa kumuacha aendelee kuishi maana dalili zote za yeye kuwa na yule binti zimeonekana dhahiri ....inawezekanaje kijana mshamba kama yule awe na demu mkali? Aisee hapana!!!". Aliongea Steve kwa sauti yenye ukakasi .
ITAENDELEA......................................? 

Post a Comment

Previous Post Next Post