IN'BOBO 08 lovestory

Ilipoishia.

"mmnhh!!!kwa hiyo hicho ndo kimeku.........."Mara nikakatisha kuongea baada ya kuhisi kuitwa tena.Nikapiga mahesabu sijui itakuwaje kama atakuwa marry ndiye mbisha hodi,nikajua hapa lazima varangati litakuwepo kivyovyote kwani kama mtu angemuona Sophie angejua moja kwa zote kwamba ni shori wangu kumbe akhaaa.

endelea.

sikukosea,mawazo yangu yalikuwa sahihi kwani baada ya kufungua mlango,nilimkuta marry akiwa wima sambamba na mlango.sikutaka kuonesha uoga mapema kwani marry angeanza kuhisi ndivyo sivyo.

"Oo kumbe ni wewe kipenzi,karibu ndani.nimekungoja kweli yani"niliongea kwa kujiamini pasipo kuonesha utofauti wowote.

"asante mwaya,nisamehe kwa kuchelewa hubby,bi mkubwa aliniagiza ndo maana nimekawia mno kuja" marry alinambia lakini akiwa ndo ameanza kupiga hatua kuingia ndani baada ya Mimi kumkaribisha.

"Mbona kama pamepoa......umepik......."marry alikata kuzungumza mara alipoingia na kumkuta Sophie akiwa amekaa kitandani.

"Tuuu.....uuun......ddaa,niiniii hiki mbele yangu?......yani wee....yaniii ndo ume.....oooh mungu wangu tunda we ndo wakunifanya hivi,ata siamini"marry aliongea kwa taharuki kubwa kivyovyote fikra za kuwa Sophie ni mwanamke wangu,zilimpata.hivyo sikutakiwa kuwa na haraka kuzungumza nae kwani nisingeweza kupunguza tatizo,bali lingeongezeka na kuwa kubwa zaidi.

"Marry ebu tulia bhasi malaika wangu mbona unakurupuka kuongea vitu visivyo na maana"

"eti ee,kwa hiyo ninavyoongea ni vya kijinga siyo?we sio wa kunitenda hivi tunda,kwanini ulinikubalia nije ilhali una appointment na mwanamke mwingine,why tunda.....why unanionea kiasi hiki,nimekukosea nini tunda?"marry aliendelea kulalama.

"tulia kwanza nikueleze,asa unavyopiga mikelele,itakusaidia nini?"

"nitulie?nitulieje kwa mfano akati nimekufumania uko na mwanamke mwingine,utaniambia nini wewe,nakuuliza utaniambia nini tunda......."bado marry aliendelea kufoka.

"nisikilize marry,kuwa mtulivu ili nikueleze sasaaa........huyu ni mdada anakaa nyumba kadhaa kutoka hapa,amekuja kwangu kwa sababu kuna ugomvi kati yake na bwana'ake.mumewe alitaka kumkata na panga ndo kakimbilia huku"nilijaribu kutengeneza uongo wa kuniepushia lile varangati lililokuwa linaniandama.lakini mistari yangu ilionekana kukosa ushawishi wa kumfanya marry aamini kile nilichokuwa nakiongea.

"Tunda.....tundaa.....tundaaa naona hunijui wewee si ndio,nakwambia nitakujazia watu asaivi,niambie huyu kinyago ni nani wako hadi awe ndani kwako muda huuuu.......hiyo ya kupigwa na mumewe sijui hawala wake mi sitaki kuisikia"mori ulikuwa umempanda marry si kitoto.hakuwa mrahisi kuelewa.unajua muda wote huo Sophie alikuwa kimyaa,akitazama namna tulivyokuwa tukijibizana mimi na marry.

"unataka nikwambiaje labda enhee,nikwambie uongo ili ufurahi au........,we ni mwanamke gani usiyeweza kuyasoma ata mazingira ya fumanizi huweje,matokeo yake unaingia na kuanza kubwata maneno yasiyo na maana,hivi kama huyu mdada angekuwa demu wangu ningekufungulia mlango?......mwanaume gani hupenda kufumaniwa kizembe kama hivi,yani Mimi na akili zangu nikufungulie mlango akati ndani Niko na demu mwingine, inakuingia akilini kisawasawa kweli?"

"sikia tunda mi sitaki maneno mengi ninachotaka uniambie ukweli tu bhasi,ata ukiongeaje sintokuelewa katu.huyu pimbi mbele yangu ni nani kwako?"

"ni jirani yangu tu,nimezoeana nae"nilijibu kwa ufupi.

"unafahamiana nae si ndio?,huku chumbani kwako kafuata nini......"bado marry aliendeleza ubishi wake tena alikuwa akiongea akiwa serious kuliko kawaida.

"marry nikueleze nini ili uelewe lakini......mi najua unahisi kuwa huyu ni mwanamke wangu,kitu ambacho sio cha kweli,naomba unielewe mpenzi wangu Tafadhali"

"siwezi kukuelewa kirahisi.......,we anti umefuata nini kwenye chumba cha bwana'angu usiku kama huu,umeshindwa kukaa na basha wako kazi kuparamia waume za watu siyo......."marry aliurusha mpira wa maneno kwa Sophie ambaye bado alikuwa mkimya.

"Nakuuliza we mshenzi usiye na haya wala soni......umeshindwa kukaa na bwana'ako hadi ukaja kwa bwana'angu?,kwanini wadada wa siku hizi hamjiheshimu jamaniii......."bado maneno ya marry kwenda kwa Sophie yaliendelea.

"bwana ako hajui kukukuna ama nini......,au hiyo sambusa yako mumeo ameshindwa kuila vizuri hadi ukatosheka mpaka ukaamua kutoka na tunda wangu,ivi unajua nilikotoka na huyu mwanaume,nakuuliza we malaya......"daaah hapo marry ndo aliharibu mchezo,kitendo cha kumuita mwenzie malaya aisee kilikuwa kibaya Atari,kwani Sophie aliamka kama mbogo na kuanza kutupiana maneno na marry.

"Naomba ujiheshimu we dada,hunijui sikujui.unaniitaje malaya kwani umenikuta najiuza........we mpumbavu nini tena ukome,nakwambia unikome.mi sio mwanamke wa kujirahisisha kwa mabwana,nikwambie sasa.na huyu unayemuita bwana'ako kwa bwana'angu hafiki ata kidogo.usihesabu kama una bwana apa mjini,upo nyonyo.na nikuonye tena ukome kuparamia watu ovyo utakuja kuparamia pabaya......."

"Heheheheeeeeiiiyaaa,ivi unajua ubora wa mwanaume wewe au unaongea ongea ovyo kuondoa nishai.........,huyo bwana ako kwa tunda wangu ni kama shog........"marry alinyamaza ghafla baada ya mimi kuingilia kati kwani niliona kwamba mambo yanazidi kuwa mabaya zaidi kutokana na hawa wanawake kuanza kurushiana maneno yaliyokuwa machafu.

"sikieni nyie mabinti,mikelele kwenye chumba changu sitaki manake mmejitanua kama kwenu apa,sasa nasema hivi ambaye Mimi sio bwana'ake naomba atoke nje chapu,nitaja mzabua mtu makofi"niliongea kwa hasira huku kiasi fulani maneno yangu yalimlenga Sophie.niliamua kumfukuza kijanja ili nikibaki na marry urahisi wa kumtuliza ungepatikanika.nashukuru Sophie aliondoka lakini huku akimuachia marry matusi ya nguoni kitendo ambacho marry hakukubaliana nacho,nae akaamua kumrudishia vile vile.

sasa baada ya Sophie kuondoka,kindumbwe ndumbwe kikabakia kwangu,manake marry alikuwa amefura hasira mpaka shida.kila nilipomuongelesha hakutaka kunijibu zaidi ya kuguna na kuishia kunitizama pasipo kuongea neno.

"Kwa nini naongea alafu hunijibu love,tuseme umeninunia kiasi cha kutotaka kuongea na mimi eeh"niliongea kwa huzuni kubwa baada ya kujaribu kumuongelesha marry pasipo kupatiwa ushirikiano.

"tunda kwa ulichonifanyia hivi ni haki kweli,kwa nini unanisaliti wakati uko na mimi,tunda......kukukubali uwe mwanaume wangu ni kwamba nilikuwa tayari kukutimizia ashki zako za mwili,iweje umchukue mwanamke mwingine?ina maana mi mapenzi yangu huwa huyafurahii,niambie tunda........sikuridhishi au huwa unaniomba penzi nakunyima?,sio siri umeniumiza sana,nimeumia mno na sijui nitayaondoa vipi haya maumivu niliyonayo........."marry aliongea kwa unyonge.kidume nikatulia kidogo kuandaa point zangu za msingi ili niweze kupambana na hoja ngumu kutoka kwa marry.

"marry mpenzi,kwa nini unakuwa na shaka na mimi,unataka kuniambia kuwa mi ni mwanaume mwenye tamaa za ngono si ndio?.........ni sawa pengine niko na tamaa ya ngono,lakini siwezi kutamani mwanamke mwingine isipokuwa wewe,huyu msichana uliyemkuta nakuapia kwa mungu,ata si mwanamke wangu.tena hilo wazo siko nalo kabisaa,kama unafikiria hivyo bhasi jua unanionea tu.mwanamke Wangu ni wewe marry,moyo wangu uko kwako,we ndo unanikosha kunako roho yangu.usifike hatua ya kudhani kuwa sina mapenzi na wewe,nakupenda marry,nakupenda na ndio maana Niko na wewe.sina ujinga wa kuyafanya macho yangu yaone mwanamke mwingine yeyote.ni wewe pekee unayeonwa na macho yangu........."nilirusha maneno yangu yaliyokuwa na hisia za huba ndani yake.siunajua kuwa mapenzi ni sayansi ya maneno eeh au ulikuwa hufahamu hilo?basi tangu sasa elewa kuwa ipo sayansi ya mapenzi ambayo hutumika ndani ya mapenzi yenyewe.

"Sina uhakika kama unanipenda tunda,siwezi jua labda ulinitamani tu,kwa ajili ya kunitumia kwa muda....,haiwezekani mimi kuamini kuwa huyu mdada niliyemkuta si mtu wako.pengine huna malengo na mimi ndio maana una badilisha wanawake kila siku.unakumbuka siku ile pale sokoni,nilikukuta na msichana mwingine,nikakuheshimu kwa sababu ulikuwa ofisini kwako.........haya na leo tena nimekufumania live uko ndani ya chumba chako na kademu kengine unataka kunidanganya danganya kama mtoto.....siwezi kukuelewa nimekwambia."marry alifunga kuongea.

"Sawa kama hutonielewa.ila we ndo nikupendaye sina mwingine,naaa......ili kukudhihirishia hilo kuna kitu nilikuwa nimekuandalia,ngoja nikuoneshe......"niliongea huku nikipiga hatua kusogea kwenye kona ya chumba changu,kuna kitu nilikuwa nakifuata.baada ya kukichukua nikarejea nacho pale alipokuwa ameketi marry.nikavuta stulu iliyokuwa mbele yake nikaisogeza jirani kabisa ya miguu ya huyu bibie,nikaweka kile nilichodai kuwa nilikuwa nimekiandaa kwa ajili yake mwanamke huyu.

"Nimekuandalia chakula kizuri leo,nataka ule ufurahie mapishi yangu"nilizungumza huku nikifungua mfuniko wa hotpot ambayo ndani yake kuliwako na chakula special kwa ajili ya bibie marry.

Nilikuwa nimeandaa wali samaki,ukiwa sambamba na ndizi pembeni.kwa utaalamu wangu katika mapishi,niliuandaa kiumakini zaidi kwa sababu tu nilikuwa na lengo la kuufanya kuwa chakula cha kum'supries marry.na kweli alistaajabu baada ya kuvuta harufu nzuri ya wali ambao ulikuwako katika hotpot.nilifahamu wazi kwamba marry angevutika na msosi mnono niliomuandalia.

"Kwa nini umeamua kunifanyia hivi tunda?......ili kunilainisha ama?"

"ni kwa sababu nakupenda marry,alafu uliwahi kuniambia siku moja kwamba huwa unapendelea sana kula wali samakil,leo uliponambia unakuja,nikaamua kukuandalia.karibu ufurahie chakula nilichokiandaa kwa mikono yangu"bhasi marry akatabasamu kiaina kuonesha kukubali kula.nilichofanya nilimnawisha kisha marry akaanza kula mdogo mdogo.alipofikia kwenye samaki,nilimuomba kumsaidia kumlisha.kwa mbwembwe nikatoa kipande cha steki kutoka ubavuni mwa samaki,nikakipeleka mdomoni kwangu kisha nikaking'ata halafu nikampelekea marry mdomoni ambaye nae alikipokea kwa bashasha.niliendelea hivyo hadi samaki alipomalizika.

"Asante tunda wangu nimeshiba"

"mnnh mbona hivyo umeshiba kweli?"

"Kabisa nimeshiba mume"

"Duu haya sawa mke"

Kilichofuata nikatoa vyombo kisha nikarejea kukaa tena pale pale nilipokuwa nimekaa mwanzo.nikachukua ndizi nikaimenya baadae nikaanza kukata kipande kidogo kidogo namlisha marry,lakini kipande cha mwisho nilifanya kama nilivyokuwa namlisha samaki muda ule.nilimsogezea mdomo marry ukiwa na kipande cha ndizi,marry akaudaka mdomo wangu mzima mzima.midomo yetu ikaanza kugombania ndizi ndani kwa ndani,ndizi ilipokwisha tukaendelea kunyonyana mate moja kwa moja.

Itaendelea. 

Post a Comment

Previous Post Next Post