DADA MAMU 13

Dada Pammy akianza kunihadithi stori za shemeji zangu yaani hata sikujua kimesibu kwanini dada pammy aliamua kuongea yale. Aliendelea kuniambia huku akinitumbulia macho kama kuonesha msisitizo juu ya mambo yale huku vikifatiwa na vicheko kiukweli muda mfupi tu niliweza kubaini tabia ya dada pammy yule mdogo wake Aunty hakuwa ametulia kabisa yaani ni mapepe ile mbaya.

Tuliendelea kuzungumza kama nusu saa wakati tumejiziuka na mazungumzo mara dada mamu alifika eneo lile huku akinitumbulia jicho kali sana muonekano wake ule nilishaanza kuhisi kitu japo kuhisi si kitu kizuri. Maana dada mamu alionekana wazi wazi ndani ya fikra zangu hakufarisha hali ile na kama si maongezi basi ujio ule ulikuwa ukinyima raha vibaya.
Alitamani hata aseme kitu ila alibaki tu nacho ndani chake kinywa tuliendelea kuangalia tv huku muda ukiwa unaenda mbaya mpaka mida ya kula ilifika tukala huku tukiendelea na shughuli zingine kuna muda nilitamani niende kutembea ila mastori tulikuwa tukizungumza na da pammy haya kunifikirisha tena habari za kutembea niliendelea kubaki nyumbani huku nikiweka sawa nguo zangu za shule kwajili ya kesho.

Muda ulienda na hata pale ilipofika usiku niliendelea kuwa na da pammy tuliendelea kuongea tu huku dada Mamu akiwa anafanya shughuli zake hakutaka kabisa kuwa na sisi nilijuwa hilo wazi ila nilishindwa nifanyanye mpaka mida fulani nilipoona muda umeenda. Niliwaaga yeye na da pammy nikaingia zangu chumbani kulala si kutaka kuchelewa kwasababu kungenichelewesha kumka hivyo niliamua kulala mapema kwa maana kuchelewa shule maana kunawalimu hao niwatata sana pindi uchelewapo anakupa kipigo takatifu mpaka unakumbuka mizimu ya mababu Na mabibi zako kwahiyo ili kuepusha hilo Niliamua kulala zangu mapema tu.

#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post