MOYO WANGU 04---05----06

siku zote Mr Yusufu alifurahishwa sana na utendaji kazi wa sheby na alitokea kumpenda sana, alimchukulia kama mwanae ukizingatia Alisha hadithiwa historia ya Sheby na pia alikuwa rafiki na baba ake walisoma na kuishi pamoja miaka ya nyuma, Sheby alimpenda na kumuheshimu mr yusufu kama baba yake mzazi ukizingatia mzee huyo hakubahatika kupata mtoto katika kipindi chote cha maisha yake,hivyo Sheby na mr Yusufu walikua ni kama baba na mtoto…
“Aaa karibu mzee, shikamoo”
“Marhaba mwanangu, vipi hali yako”
“Salama tu sijui wewe na mama huko nyumbani”
“Tunamshukuru Mungu tu wazima wote, vipi unafanya nini kwa sasa?”
“Nipo napitia form za watu waliotaifishiwa mali zao”
“Okay uzipitie kwa umakini na hakikisha unazisaini kabisa kabla ya kuzileta ofisini kwangu”
“Sawa boss” alijibu Sheby
“Hahahaha Sheby mwanangu mimi sipendi uniite boss, napenda ukiniita baba”
“Okay sawa baba nimekuelewa”
“Haya mwanangu kazi njema” alisema mr Yusufu na kuelelekea katika chumba cha ofisi yake.
**** **** *****
Wakati Warda alipofika kazini wakati anapaki gari ili aweze kuingia ofisini, alisikia mlio wa message katika simu yake, aliichukua simu yake na kuangalia ujumbe ulikua umetoka kwa nani, “Boss” ndio jina lililotokea katika screen ya simu yake aina ya Iphone 6+, alipofungua sms hiyo alijihisi kutaka kuzimia kutokana na message hiyo ilivyoandikwa, message ilisomeka hivi;
“Kuanzia leo sitaki kukuona katika ofisi yangu, nimekufukuza kazi kwasababu zangu binafsi, na wala usijisumbue kuja katika ofisi yangu kama unajipenda maana unaweza ukaozea mahabusu, ila kama utakua tayari kunivulia nguo yako ya ndani na kunipanulia mapaja yako unaweza ukapata kazi, kwa kifupi nalihitaji penzi lako ili uokoe kazi yako”
Warda aliipitia hiyo message mara mbilimbili na hakuamini kama boss wake anaweza kumuandikia message kama hiyo ukizingatia jinsi walivyokua wanaheshimiana, alilia sana lakini baadae alijifuta machozi, alichukua simu yake na kutafuta jina lililoseviwa boss na kuruhusu simu itoke(calling)…, simu upande wa pili iliita na hazikupita sekunde kadhaa simu ilipokelewa…
“Haloo warda natumai umepata message yangu, na……..” kabla hajamaliza kuongea warda alimkatisha….
#itaendelea 


Haloo Warda natumaini umepata message yangu, na……..” kabla hajamaliza kuongea Warda alimkatisha….
“Sikiliza wewe mpuuzi usiekuwa na haya wala adabu, mimi siyo mwanamke wa dizaini hiyo, kama umeshindwa kuvuliwa chupi na mke wako na akakupanulia mapaja nenda kwa Malaya wanaojiuza huko mtaani na siyo kwangu mimi mwanahizaya wewe, sikutegemea mtu mzima kama wewe unaweza kuniambia maneno machafu kama hayo mshenzi wewe, nenda nikome kama ulivyokoma ziwa la mama yako, tena unikome, sina dhiki kiasi cha kukuvulia wewe chupi kwaajili ya kazi, mpuuzi mkubwa wewe, tena unikome… na ufute namba yangu pindi nitakapo kata simu hii….”
“Warda una…”
“Msyuuuuuu” warda alimsonya na kukata simu.
Siku zote warda alikua ni mwanamke mwenye msimamo kweli katika mambo yake, na alishaapa hatokuja kumsaliti sheby katika maisha yake, ndio ilikua ni haki yake kuapia kutokuja kumsaliti sheby, sheby alimtimizia kila analolihitaji kwa wakati, alimtimizia hata mahitaji yake ya kimwili, kwa kifupi kwake yeye alikua ndiyo kila kitu….
Baaada ya kumaliza kuongea na boss wake aliwasha gari na kurudi nyumbani kulala akiwa na mawazo sana, baadae alikata shauri na kuendelea na kazi ndogondogo za nyumbani huku akimsubiri Sheby aje ili amueleze kilichomkuta….
**** **** ******
Siku zote katika maisha sio kila mtu atafurahi kuona mafanikio yako, wengine huchukia na kutamani ushuke na uwe masikini wa kutupwa, hivyo ndivyo ilivyokua kwa sheby, sio kila mtu pale anapofanyia kazi alifurahia mafanikio yake japo ni wachache ambao hawakufurahishwa na mafanikio yake, wengi walimpenda hasa kutokana na ucheshi wake pamoja na upole wake, mbali na hilo pia sheby alikua ni mshauri mzuri sana pale ofisini kwa wafanyakazi wenzake, endapo mfanyakazi yeyote alimfata na kumuomba ushauri, Sheby alimshauri vizuri na hata wakati mwingine kama mfanyakazi alikua anamatatizo, sheby alidiriki kutoa pesa katika mshahara wake na kumsaidia huyo mfanyakazi ili atatue matatizo yako, hivyo ndivyo jinsi sheby alivyoishi na wafanyakazi wenzake. Mbali na vyote hivyo vizuri ambavyo sheby alikua akiwafanyia wafanyakazi wenzake, hali ilikua tofauti kwa John ambae alikua ni muhasibu msaidizi, alimchukia sana sheby

#itaendelea 

hali ilikua tofauti kwa John ambae alikua ni muhasibu msaidizi, alimchukia sana sheby, tena alimchukia kupita kiasi, siku zote hakupenda mafanikio ya sheby, alitamani mafanikio yale yawe kwake, siku zote aliweka tabasamu feki alipokua na sheby, lakini moyoni mwake alimchukia kupita kiasi, uzuri ni kwamba sheby alilitambua hilo na siku zote alijifanya kama haelewi kinachoendelea, alimpenda john na alihuzunika pia kwanini john alimchukia vile.
Siku hiyo walipomaliza kazi alimsubiria boss wake mr Yusufu ili amwambie kinachoendelea kati yake yeye na john ili siku likija kutokea tatizo basi wajue pakuanzia. Alipomaliza maliza kupanga kazi zake alitoka na kwenda kwenye ofisi ya Mr Yusufu na kugonga mlango, aliruhusiwa kuingia….
“Ooo karibu mwanangu”
“Asante baba pole na kazi”
“Nashukuru pole na wewe”
“Aaaa baba nilikua na maongezi na wewe kidogo kama hutojali”
“Ebu keti kwanza hapo ngoja nimalizie hii kazi hapa halafu tuongee, kwani ni maongezi marefu sana?”
“Hapana ya kawaida tu na mafupi pia’
“Okay subiri kidogo”
Sheby alisubiri na baada ya dakika kumi mr Yusufu alimaliza kazi zake…
“Sasa mwanangu tunaweza tukaongea”
“Baba ni kuhusu john”…

“John yupi, yule muhasibu msaidizi?”
“Ndio baba”
“Enhe kafanyaje tena”
“Baba john amekuwa akinichukia sana tangu mlivyonizawadia nyumba , sasa nahofia siku ya siku anaweza akafanya jambo ambalo linaweza likaniweka mimi katika wakati mgumu au akaiweka ofisi katika wakati mgumu”
“Eeee kumbe kijana mbaya sana yule, kwanini akuchukie mwanangu, wewe umezawadiwa vile kutokana na utendaji wako mzuri wa kazi,sasa kwanini akuchukie, ngoja nitamfukuza kazi”
Hakika Mr Yusufu alichukia sana, hakupenda kuona mtu akimkwaza Sheby, kwani alimpenda kama mwanae…
“Hapana baba usimfukuze mwache tuu, jaribu kumuita na kumshauri itakua bora zaidi ya kumfukuza”
Mbali na yote mr Yusufu alimsikiliza sana Sheby kwani alimuona pia ni mtu mwenye busara…
#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post