MOYO WANGU 07----08----09

Mbali na yote mr Yusufu alimsikiliza sana Sheby kwani alimuona pia ni mtu mwenye busara…
“Sawa nimekuelewa mwanangu, unaweza kwenda”
“Sawa baba jioni njema,msalimie mama”
“Usijali zimefika, kuwa muangalifu”
“Okay bye” Sheby alimuaga bosi wake na kutoka nje kwakua muda wa kazi ulikua umeisha, alienda mpaka parking ya magari akaingia kwenye gari, akawasha gari lake na safari ya kuelekea nyumbani kwake ilianza…
******** ***** ********
Kutokana na foleni iliyokuwepo siku hiyo ya jumatatu, Sheby alifika nyumbani kwake mida ya saa moja na nusu, kama kawaida alitoa kirimoti kidogo katika mfuko wa suruali yake kasha akakibonyeza na geti lilifunguka, hapo alikanyaga mafuta taratibu na kuingiza gari lake aina ya prado, alibonyeza tena kirimoti na geti lilijifunga, alisogeza gari mpaka sehemu ya parking na kuliweka sehemu yake, na baada ya hapo alifunga vioo pamoja na milango ya gari na alipomaliza alielekea upande ambao ndiko ulipo mlango wa kuingilia ndani kwake, alifungua mlango na kuingia ndani lakini alishangazwa na ukimya uliokuwepo hapo ndani, alipita sebuleni na kukuta chakula kipo mezani lakini alipojaribu kumuita mpenzi wake Warda bado kuliendelea kuwa na hali ya utulivu, alitoka hapo sebuleni na kuelekea katika chumba chake, hapo alipigwa na butwaa baada ya kumuona Warda akiwa amelala na jinsi alivyoonekana ilionesha wazi kuwa hakutoka siku hiyo, sheby alipatwa na wasiwasi na kudhani huenda kuwa mpenzi wake anaumwa, Sheby alisogea mpaka karibu na kitanda alicho lala mpenzi wake na kumuamsha kwa ustaarabu, Warda aliamka kivivu, alikutana na tabasamu murua la Sheby na bila kutarajia alijikuta akimrukia na kumkumbatia kwa nguvu, baada ya muda wa kama dakika moja huku warda akiwa bado amemkumbatia sheby, warda alianza kudondosha machozi kuonesha kwamba kuna kitu kinamsumbua, sheby aligundua kuwa warda atakua analia baada ya kuhisi shati lake alilokuwa amelivaa limenza kupata hali ya ubichi, alijitoa katika kumbatio lile na hapo alikutana na uso wa warda ukiwa umependezeshwa na machozi, sheby alipagawa na asijue mpenzi wake amepatwa na nini,

#itaendelea 


Sheby aligundua kuwa suzan atakua analia baada ya kuhisi shati lake alilokuwa amelivaa limenza kupata hali ya ubichi, alijitoa katika kumbatio lile na hapo alikutana na uso wa warda ukiwa umependezeshwa na machozi, sheby alipagawa na asijue mpenzi wake amepatwa na nini, mambo mengi sana yalipita katika kichwa chake na kuhisi huenda tayari kuna vijidudu watu washaingia katika penzi lake na hapo tayari mpenzi wake ashapewa maneno ya uongo kuwa yeye kuna mtu anatembea nae, alitoka katika dimbwi hilo la mawazo baada ya warda kuanza kulia kilio cha kwikwi, sheby alimfuta machozo mpenzi wake na kumuuliza ni kitu gani kinamsibu, warda hakuongea bali alitoa simu yake aina ya iPhone 6+ na kufungua sehemu ya ujumbe mfupi (message) hapo alitafuta ujumbe aliotumiwa na bosi wake na baada ya hapo alimkabidhi sheby ile simu,sheby aliipokea ile simu na kuanza kuusoma ule ujumbe mfupi, na hapo macho yalimtoka pima baada ya kuona ujumbe ule…
“Kuanzia leo sitaki kukuona katika ofisi yangu, nimekufukuza kazi kwasababu zangu binafsi, na wala usijisumbue kuja katika ofisi yangu kama unajipenda maana unaweza ukaozea mahabusu, ila kama utakua tayari kunivulia nguo yako ya ndani na kunipanulia mapaja yako unaweza ukapata kazi, kwa kifupi nalihitaji penzi lako ili uokoe kazi yako”
Sheby alishusha pumzi ndefu baada ya kumaliza kusoma ujumbe huo, alimtazama mpenzi wake ambae alikua akilia taratibu huku akivuta kamasi jembamba ambalo lilikua likitaka kutoka, sheby alisikitika sana na alichukia kupita kiasi kwani hakupenda hata siku moja kumuona mpenzi wake akipata tatizo lolote kipindi ambcho yeye yu hai, alimpenda na alimthamini kuliko kitu chochote chini ya jua, licha ya warda kuwa mpenzi wake pia alikua akimchukulia kama ndugu, licha ya warda kuwa mpenzi alimchukulia kama mtu wa karibu kwake na pia alimchukulia kama mshauri wake mkubwa, alimtazama warda ambae bado alikua akilia na hapo alipatwa na uchungu mkubwa moyoni mwake, alifikiria ni jinsi gani atamsaidia mpenzi wake, alifahamu fika kwamba warda kwao ndio baba ndio mama,

#itaendelea 

Sheby ndipo alipogundua kuwa jukumu la kumsaidia warda ni la kwake yeye mwenyewe, alitambua kuwa yeye ndiye nguzo pekee ambayo warda anaitegemea, aliirudisha simu mahala pake na kisha alivua nguo zake na kupanda kitandani, alimvuta warda karibu yake na kumlaza katika kifua chake….
“Warda mpenzi wangu, yakupasa utambue kwamba katika maisha kuna changamoto nyingi sana ambazo binaadamu huwa tunakutana nazo, na ili ufanikiwe huna budi kupambana na changamoto hizo kwa nguvu zako zote ili ufanikishe malengo yako, kufukuzwa kazi wewe haimaanishi kwamba ndio mwisho wa maisha yako, yakupasa kukaa chini na kumshukuru mungu wako kwa kila jambo kwani huwezi jua mungu amekuepushia nini katika kampuni hiyo”
“Unayo yasema sheby ni sawa sijakataa ila kwanini litokeee kwangu, mbona kila siku mimi ndo nakuwa napatwa na matatizo, nimeishi maisha ya shida tokea Utøtoni nimesoma Kwa tabu nimeangaikaa wazazi wangu hohehae hawana juu wala chini mm ndio msingi wao wa kuwalea halafu leo mtu ananifukuza kazi kisa anataka afanye ngono na mimi, kwanini mimi? Eee mungu nimekukosea nini mpaka unanitenda haya, nibora uichukue roho yangu kuliko kuniacha hivi na kunipa mitihani kila siku”
“Paaaaa” ulisikika mlio wa kofi, naam ni kofi mwanana kabisa kutoka kwa sheby lililotua vyema katika shavu la warda, warda hakuamini, tangu wajuane na sheby na kukaa katika mahusiano kwa muda wa miaka mitatu hakuna hata siku moja ambayo Sheby aliwahi kumpiga hiyo ndo ilikua mara yake ya kwanza kupigwa na Sheby, alishika shavu lake na kukutana na sura ya sheby ikiwa na makunyanzi huku macho yake yakiwa mekundu utadhani ametoka kuvuta bangi, hii ilitosha kabisa kumjulisha warda kuwa sheby alikuwa ana hasira kupita kiasi, licha ya warda kupigwa kofi hilo hakuthubutu kuinua mdomo wake, alikaa kimya na kusubiri kusikia sheby ataongea nini na ni kwasababu gani sheby ampige kofi…

#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post