MOYO WANGU 46---47---48

Sheby alimtilia wasiwasi, hivyo alishuka katika gari lake na alipo hakikisha milango ameifunga vizuri alianza kusogea eneo ambalo alikuwepo yule kijana, lakini wakati amekaribia kufika lile eneo, yule kijana alikurupuka na kuanza kukimbia, sheby kwa kasi ya ajabu alichomoka kama mshale na baada ya hatua kumi tuu alimkaribia yule kijana.. “Tiii!!” ndicho kishindo kilichotokea baada ya sheby kumpiga ngwala yule kijana, na kabla hajakaa sawa ngumi nzito ilitua katika shingo yake hali iliyomfanya apoteze fahamu, sheby aliangalia kushoto na kulia na kuona hakuna mtu ambae alikua akimfuatilia, hapo alimbeba yule kijana ambae alikua hana fahamu na kuelekea nae sehemu ambayo alikua amepaki gari lake, baada ya kufika sehemu ambayo alikua amepaki gari lake alienda mpaka sehemu ya nyuma ya gari ambapo alifungua buti na gari na kumuweka yule kijana na baada ya hapo alilifunga buti la gari na kuingia katika usukani na safari ya kuelekea kwake ilianza. Mida ya saa mbili kasoro usiku sheby alikua akipaki gari lake katika nyumba yake ya siri ambayo ilikua maeneo ya kigamboni, kutokana na uzio kuwa mkubwa hakuna aliyejua ni kitu gani kimejengwa ndani ya uzio huo, ni warda na sheby pekee ndie waliokuwa wanajua eneo hilo, sheby alimtoa jamaa yule na kumuingiza katika chumba kimoja ambacho kilionekana ni chumba cha mateso kutokana na vifaa vilivyo kuwa humo ndani, hapo sheby alimkalisha yule kijana katika kiti ambacho kilikua kimesimikwa humo ndani na kumfunga kwa vyuma maalum vilivyokua katika kiti hicho,baada ya hapo sheby alitoka na kufungua geti la jumba hilo la siri, alipotoka alielekea katika duka la karibu na kununua kiberiti cha gesi baada ya kununua alipita kwa street venders(machinga) na kununua taulo na baada ya hapo alirejea katika jumba lake na kuingia katika chumba ambacho alimfunga yule kijana, aliingia na kumkuta yule kijana bado amepoteza fahamu, alitabasamu kisha akachukua maji ya baridi ambayo aliyatoa katika fridge na kumwagia yule kijana, kijana yule alikurupuka na kutaka kukimbia lakini juhudi zake hazikufua dafu kutokana na vyuma ambavyo alikuwa amefungwa… 

#itaendelea 

Tulia usiwe na papara, kuwa mpole” alizungumza sheby kwa sauti ya kukoroma Almanusra yule kijana azimie, nah ii ni baada ya kumuangalia aliyekua akimsemesha na hapo alikutana na mtu ambae alikua kavaa kininja, hakika alipagawa na asielewe mtu huyo ni nani. “Kupona kwako wewe ni kunijibu maswali yangu kwa ufasaha” alizungumza sheby kwa sauti ya kukoroma na yenye kitetemeshi kikubwa

“U… uu..likuwa un…a…se….m…a.je” alizungumza yule kijana kwa sauti iliyojaa woga “Unaweza ukaniambia mwanamke mliyemteka maeneo ya Coco beach mmemteka kwasababu gani?” alizungumza sheby kwa sauti isiyokua na masihara “Aaah!! Mimi sijui, unazungumzia kuhusu nini?” alijibu yule kijana kwa sauti kavu “Okay hamna tatizo.” Alizungumza sheby kwa sauti ya kukwaruza huku akiwa katika vazi la kininja kumaanisha kwamba alikua tayari kwa vita ambayo ipo mbele yake kwaajili ya kumtafuta mpenzi wake, alifungua kibox kidogo ambacho kilikua mezani na hapo alichukua kile kiberiti cha gesi alichonunua, alimsogelea kijana yule na kukiwasha kile kiberiti, alikisogeza mpaka karibu kabisa na uso wa kijana yule na hapo alimuuliza tena.. “Una hakika haujui ninachozungumzia? Aliuliza Sheby kwa sauti ya ghadhabu.. “Ndio sijui unachozungumzia!!” alizungumza yule kijana kwa sauti ya kufoka, na hapo alicho kifanya sheby alikizima kile kiberiti, alichukua taulo alilokua amelinunua kwa machinga na kumfunga nalo yule kijana usoni na baada ya hapo alichukua maji ya baridi na kuanza kuyanyunyiza taratibu katika taulo lile, kadri muda ulivyokua ukienda ndivyo yule kijana alivyozidi kupata tabu katika upumuaji.
. “Koh koh koh..” alikohoa yule kijana baada ya kuona anaweza akapoteza maisha kizembe ingawa alikua hana hakika sana kama atatoka salama katika eneo hilo ambalo mpaka mda huo alikua hajafahamu eneo hilo liko wapi, sheby aliendelea na zoezi hilo na aliporidhika alilitoa lile taulo usoni mwa yule kijana “Koh koh koh” alikohoa yule kijana huku akitapika maji ambayo aliyanywa kipindi ambacho taulo lilikua usoni mwake “

#itaendelea 

Nafikiri sasa unaweza ukaniambia kwanini mlimteka yule binti kule maeneo ya Coco beach” alizungumza sheby katika hali ya utulivu “Tulimteka kwasababu tuliagizwa na boss wetu.” Alizungumza yule kijana huku akipumua juu juu “Huyo bosi wenu ni nani?” aliuliza sheby “Ni John, yule muhasibu msaidizi katika ofisi ya TRA tawi la Posta.” Alijibu yule kijana “Wewe unaitwa nani?” aliuliza tena sheby “Naitwa James, ni mdogo wake na John tafadhali usiniue!” alizungumza yule kijana aliyejitambulisha kwa jina la James katika hali ya uoga hasa alipomtazama mtu huyo aliyekua akimuhoji akiwa ndani ya vazi la watu hatari duniani, yani maninja.. sheby moyoni mwake alifurahi sana baada ya kuona kuwa alikuwa amemshikilia mdogo wa adui yake mkubwa John na aliapa kuwa kitu atakachomtendea John hatokuja kukisahau katika maisha yake.. “Mlivyomteka mlimpeleka wapi?” Sheby alimuuliza James.. “Wamempeleka katika pori la Bagamoyo na huku ndipo ilipo kambi ya siri ya kaka John kwaajili ya kufanyia mambo maovu” alizungumza James kwa kirefu “Okay sawa wasalimie kuzimu..” alizungumza sheby na hapo alichomoa jambia lake la kininja ambalo alikuwa ameliweka mgongoni kwake na hapo alitenganisha kichwa na kiwiliwili cha mdogo wake John, sheby alishaamua kurudi katika hali yake ya zamani hali ya kuwa na roho ya kikatili, na hapo hakuna kingine alichokua akiwaza zaidi ya kuua tuu, aliubeba mwili wa James ambao ulikua hauna kichwa na kwenda kuutupa katika bwawa la mamba ambao alikua akiwafuga humo ndani na baada ya sekunde kadhaa James alikua tayari ameshaliwa na mamba wale, Sheby baada ya kumaliza zoezi hilo alirudi mpaka katika kile chumba cha mateso na hapo alikichukua kichwa cha James na kukinyunyiza dwa flani hivi ambayo ilisababisha damu iliyokua ikitoka kuganda, baada ya hapo alikiweka kile kichwa katika mguko wa rambo na kukiingiza katika box na kulifunga box hilo vizuri, baada ya kulifunga vizuri box hilo, alilibeba na kwenda kulipakia katika buti ya gari, alirudi ndani na kuchukua silaha zake za kininja na kuingia kwenye gari ambapo safari ya kwenda katika pori la Bagamoyo kwenda kumuokoa mpenzi wake ilianza… 

#itaendelea 

Post a Comment

Previous Post Next Post